Nakusalimu katika jina la YESU, Bwana YESU asifiwe!
Kuna vitu vinabeba roho ya kuzimu, lakini vipo kanisani au vinatumika katika kanisa, ingawa wanasingizia ni MUNGU, na kwakujua na kutokujua, watu wengi wamebeba roho za kuzimu japo wanampenda MUNGU.
1Yohana 4:1-2
“1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.”
Anasema zijaribuni hizi roho, kama zimetokana na MUNGU, kwasababu watatokea manabii wengi wa uongo; manabii wengi ni vinywa vya kusema neno la Mungu kwa uongo. Leo tukazijaribu roho zilizopo makanisani; ni za MUNGU au za kuzimu? Usipozijaribu, utaangamia kwa kujuaa na kutokujua. Wewe mwenyewe utaijaribu kwa mafundisho, na vile Roho mtakatifu atakavyokuongoza, ujue unakwenda wapi? Uko wapi? Na je uko salama?
1Yohana 4:3
“3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.”
Roho inayompinga Bwana YESU, haitaki kumkiri, haitokani na MUNGU! Kuna wakristo hawataki kumkiri Bwana YESU, ila wanang’ang’ania ni wa kristo; Hiyo roho inampinga Bwana YESU, haitoki Mbinguni, ni roho kutoka kuzimu, ni roho ina nguvu, ina uwezo wa kumpeleka mtu inapotaka, na shetani akatumia hapo hapo katika hiyo roho.
Kuna roho ya MUNGU kwa njia ya mdomo, neno la Mungu linasema; ‘watu hawa wananiabudu kwa mapokeo ya wanadamu lakini ndani ya mioyo yao sipo, nipo kwa mdomo tu.’ Ni vizuri kutoka katika ukristo wa midomo, lakini tuijaribu hii roho, MUNGU ameruhusu tuijaribu.
Matendo 1:8
“8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Anawaambia wanafunzi wake, subirini mpaka mtakapojazwa yule Roho mtakatifu, atawatia nguvu, hata ya kushuhudia yale yalio kweli, niliyofundisha na kuyafanya. Na kwanini wasubiri? Ina maana kabla ya hapo, wangeondoka hawajapata ile Roho ya MUNGU, hakika wangepotezwa. Napenda ujue habari ya huyu roho wa MUNGU, yawezekana una omba sana, na kuabudu, lakini huna roho wa Mbinguni! Kuabudu kwako, ukristo wako, tayari ni majivu, umeangamia pasipokujua na kujua.
Matendo 2:1- 4; Katika ile siku ya Pentekoste, walipokusanyika, wote wakajazwa Roho mtakatifu, ila watu wamefundishwa pentekoste ni kitu kitakatifu, ni wokovu, Hapana!
Maana ya ‘Pentekoste’; ni kanisa la Hamsini; lakini kanisa alilojenga YESU ni kanisa la kwanza, na kanisa la mwisho ambalo litakuwa na utukufu, ambao utukufu hautafanana na ule wa kwanza. Sasa pentekoste, kanisa la hamisini, limetoka wapi? Shetani ameweza wapiga upofu, akaweza kuangusha makanisa, kwa baadhi waliokoka kwasababu tu yakujiita kanisa la pentekoste.
Wengi mmepokea mafundisho haya kwa kutokujua hili neno la hamsini, baadhi ya makanisa yanachoka kwasababu yamejiita ya hamsini, wanasema hawajaokoka ila ni makanisa ya pentekoste au ya hamsini. Je, YESU amejenga kanisa la hamsini? mnajipa namba ya nyuma, ndio maana mnakuwa hamuendelei, mpo nyuma tu kwakujua na kutokujua mkijiita wapentekoste! Kataa ‘mimi sio kanisa la hamsini’ ni ‘kanisa la Roho mtakatifu.’ Mbinguni hakutakuwa na kanisa la dini flani, dhehebu flani au la hamisni, ni kanisa la wokovu, ambalo kuna kuwa na ile roho ya MUNGU.
Mathayo 3: 13-17; Tunaona mtumishi wa MUNGU Yohana, anajua YESU ni mkuu zaidi yake, hivyo alitaka kubadilisha, yeye ndiye abatizwe na YESU. Ila YESU alifahamu; ilivyopangwa, ikiwa tofauti, Roho ya MUNGU haitashuka pale, kwa sababu ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote, na Yohana alipokubali kumbatiza YESU, Roho wa MUNGU akashuka akamtambulisha YESU. Roho wa MUNGU alishuka kwa YESU, kwakuwa alibatizwa, ubatizo unaotoka Mbinguni, ambao ulipangwa.
Roho wa MUNGU anashuka katika vitu vya MUNGU vilivyopandwa kutoka Mbinguni, Ingawa kuna vitu vinavyobeba roho ya shetani ndani ya kanisa, katika kusema neno la MUNGU, kama kujifunika kofia lakini haibebi Roho ya MUNGU, hataitwa shetani ndani ya neno la MUNGU, ila atafundisha mafundisho ya uongo :
Neno la MUNGU linasema; usiongeze wala usipunguze, Yohana alipotaka abatizwe yeye, YESU mwenyewe alikataa, hakubadili neno la MUNGU ili asije akakosa ufalme wa Mbinguni, ametufundisha njia. Na wewe mwanadamu, wewe mataifa, kubali ilivyopangwa, ukibadili inakuwa siyo roho ya mbinguni itakayoshuka kwako.
Hata navyosema Bwana YESU asifiwe, kama sina ile roho ya mbinguni, basi katika ulimwengu wa roho haifanyi kazi, lakini ikiwa nina roho ya kuzimu, basi wale watu wakisema ‘Amen’ wataondoka na roho ya kuzimu. Shetani anaijua hii biblia lakini ana roho yake amewapa watu wake, na vile vile MUNGU anao wanaomskiliza kwa utukufu wake.
Umebatizwa kwenye kisima, baharini, au ukiwa mtoto mdogo; Roho wa MUNGU hawezi shuka katika ubatizo wa namna hizi, kwa sababu siyo ya kwake, bali atashuka yule roho wa kutoka kuzimu.
Usiseme Imani yako, yakupasa ubatizwe hivi, hata mashetani wana imani yao, ila neno la MUNGU halibadilishwi. Unapokea roho ya kuzimu ukiwa mdogo, ndio maana makusudi ya MUNGU juu ya mtoto alipaswa ayapate, hayapati, anaishi kwa neema ya MUNGU.
Watu wanaweka Imani kwenye misalaba; misalaba ni laana, alibeba msalaba YESU; dhambi na mateso yetu, Kwa nini ujitikwe tena? ile alama ya kujumlisha unayoweka kwako, tayari wewe umeweka alama ya mateso juu yako. Unaabudu sanamu unasema MUNGU nibariki, atakuja mungu mwingine kutoka kuzimu, kwa sababu MUNGU wetu siyo wa sanamu.
Mnaabudu wafu; mnapowakumbuka wafu kwa ibada, yeye siyo MUNGU wa wafu, hivyo roho mtakatifu wa mbinguni hawezi kushuka hapo. MUNGU anakutaka sasa hivi, ukishakufa, hata watu wakuombee, wanapoteza muda, MUNGU, yeye siyo wa wafu !
Nyumba za ibada zimekuwa za harambee au michango, wanaita kabisa sherehe ya mazao, wakiita roho mtakatifu, ila roho mtakatifu atayeshuka ni wa kuzimu siyo wa Mbinguni. YESU alikataa nyumba ya BABA yake kuwa soko, Madhabahu ni mahali patakatifu, msifanye minada au kamari mafungu ya kumi ya watu, waache wakauze na kuleta sadaka wenyewe.
Mathayo 6:3-4
“3 Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”
Naongelea habari ya sadaka zenye Roho ya MUNGU unapotoa ndani ya kanisa.
Ila ukikuta kuna bahasha maalumu ya kuchangia, unaandikwa jina ukitoa sadaka, unapewa risiti; yote haya huo msingi tayari roho wa MUNGU hayupo, itakuja ile roho kutoka kuzimu maana ilishaandikwa sadaka ni siri yako. Wachungaji, Manabii, Mitume, haya yote mnayatoa wapi? Mbona mnamsaliti MUNGU?
Tunaponywa kwa jina la YESU, kwa roho mtakatifu, kwa ushirika wa neno la MUNGU, sema sasa hivi watu wanaponywa kwa maji, udongo, wengine wanaponya kwa kuwapa dawa flani. Wote hawa wameona wanadamu ni wajinga, wamewateka, shetani akaona kuliko kuwalisha neno la MUNGU, lijae ndani yao, yeye atajaa ndani yenu.
YESU akirudi, wewe utakuwa na roho gani? zichunguzeni hizi roho, wachawi wanashamiri kwa sababu hamna roho ya MUNGU. Na hizi roho za kuzimu, zinajenga mpaka makanisa, lakini YESU hayuko ndani ya hayo majengo, kuzimu ndiyo inapokea sadaka zenu zote, kwa namna vile kanisa lilivyotekwa.
Wagalatia 1:6
“1 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi, yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.”
Kwa nini mnaifwata injili ya namna nyingine? zijaribuni izo roho zingine, Una uhuru wa dhambi! Yale mambo MUNGU amekataa yamekubalika makanisani? Toka huko ukatengwe nao, Ni wakati wa kufukuza hizi roho, kama unazo, umeziamini, umerithi au umezikubali. Neno la MUNGU linasema acha dhambi, okoka, msifu MUNGU.
Wengi mnampenda Bwana YESU lakini hamtaki kumkiri; kumkiri ni kuokoka, kuongozwa sala ya toba, Bwana awe mwokozi wa maisha yako, bila hivyo ukristo wako haukamiliki pasipokuokoka, akasema atakayenikiri nami nitamkiri mbele ya BABA yangu.
SALA YA TOBA:
Sema; Bwana YESU ninakubidhi maisha yangu, atoke yule roho mchafu aliyenishikilia, nilipigwa muhuri kwa njia ya ubatizo, kwa njia ya ubarikio, kwa njia mbali mbali, hata za maombezi ya sadaka, wakati wewe unaponya bure, hatanikatoa na mafungu yangu ya kumi. Ninaomba Bwana ukanitoe, uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima. Asante Bwana YESU, anishikilie Roho mtakatifu wako, unitie nguvu, unibadilishe siku kwa siku katika jina la YESU.
Amen.
PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.