Pages

Tuesday, May 19, 2026

KUTOLEWA KATIKA MASHIMO YA MAGEREZA YA KIROHO.

 Bwana YESU asifiwe! Yako mambo ambayo MUNGU amekupangia ila huyaoni, yako wapi ?


Isaya 42: 22

22Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.”

Mashimo yanayozungumziwa ni katika ulimwengu wa roho, siyo mashimo haya unayo yaona. Magereza ninayozungumzia siyo haya wanayofungwa wahalifu hapa duniani, yako magereza katika ulimwengu wa roho ambayo shetani kazi yake ni kuwafunga watoto wa MUNGU wateseke.

Kuna mahali unakuwa hufanikiwi, kumbe uko gerezani; “yakavunjike katika jina la YESU” Wengine wamefukiwa kwenye mashimo hawaonekani; “utakwenda kutoka wewe na vitu vyako, na vitu vyako vikarudi hatakama viko ndani ya mnyama akavitapike, popote vilipo virudi.”

Watu wameibiwa na kutekwa na wachawi, kitu kinachotekwa ni nafsi, nafsi ndiyo mtu; Natamka "wachawi wanaokuchezea wafekwe, wachawi wa Tanzania wafekwe, wa bara la Afrika wafekwe wote na malango yote, hata salia hata mmoja." Na wewe unayetaka mambo ya irizi; Acha!

Katika dunia mambo yameharibika sana; Kwanini vifo vinazidi? MUNGU alileta watumishi kuzuia vifo, ila vifo vingi siyo mpango wa MUNGU, shetani anauwa watu kila siku. Kazi ya watumishi imekuwa ni kuzika tu, kusema Bwana amefanya; “nakataa hizo vifo katika jina la YESU.” Imefika hatua watu wanasimamia Imani na kuweka vyama vya kufa na kuzikana, hilo ni pepo! Hujaumbwa kwa ajili ya kwenda kuteseka kwenye chama cha kufa na kuzikana.

Unapokuwa kwenye chama cha kufa na kuzikana, unakuwa na matatizo yasiyoisha ya mauti. Katika chama cha kufa na kuzikana, mkiwa mnatoa ile fedha ya mchango kwa mwezi au mwaka kama ni 5,000/= au dollar 100; kile kitendo cha kutoa fedha, inakuwa ni sadaka katika ulimwengu wa roho, pasipokujua unakuwa umejiingiza katika agano la chama cha kufa, hivyo utatembea na roho ya mauti, hatakama hutakufa, vitu vyako vitakufa, akili itakufa, unakuwa unatembea na mauti.

Makanisa na familia mnakuwa na chama cha kuzikana; mnafikiria kufa tu, tayari MUNGU wako amekuwa ni MUNGU mfu siyo MUNGU aliye hai. Ukifa hata ukawa hapo barabarani watu watakuzika tu, kuna watu wameliwa na mamba na kutupwa sehemu mbali mbali, watafufuka tu ile siku ya mwisho. Hata ukifa ukaachwa hapo hospitalini, utazikwa na serikali yako. Kuna watu wanawaza hata wakiondoka kanisani atazikwa na nani, akija YESU utabaki hapa hapa kwasababu wewe matumaini yako ni kufa na kuzikana tu, mambo mengine siyo uchawi bali unajimaliza mwenyewe kwa kujua na kutokujua. Utoke katika hilo lango la kufa na kuzikana katika jina la YESU.


SHETANI AMELIPIGA KANISA ASILIMIA KUBWA:


Nyota:- Ni neema ya baraka za maisha yako. Baraka zako ziko wapi ? Umekuwa na maisha magumu, hutakiwi kuwa na maisha magumu wewe uliye ndani ya YESU. “Haki yako ambayo huioni ukaipate, maisha magumu yakavunjike.” Usione YESU hayupo, yupo ila wako mayesu wauongo, wanateka nafsi za watoto wa MUNGU, wanakuwa misukule, wanawekwa kwenye madhabahu, dukani au katika biashara. “Malaika wa shetani ambao ni majini na mapepo wakangamie katika jina la YESU.”

Watu wanampenda Bwana YESU, ni wakati wa kusimama imara YESU anarudi. Hata akirudi watu bado mko kwenye vibuyu “vipasuke katika jina la YESU uachiwe huru.”

Sadaka ya mavuno:-
hakuna sadaka ya mavuno, kuna fungu la kumi, mavuno uliyopanda kama ni gunia kumi, unatoa gunia moja hilo ndiyo fungu la kumi, unauza hilo gunia moja kisha unapeleka fedha au sadaka kanisani. Lakini sasa unaambiwa hilo gunia moja upeleke kanisani linapigwa mnada; “ 100,000/= , 150,000/=.” inamaana fungu lako la kumi limepigwa mnada, umetupa! na mahali kama hapo, YESU hayupo, imekuwa ni soko.

Fungu la kumi ni lako mwenyewe usipangiwe na mtu, ni sadaka ambayo ni mpango wa MUNGU kamili ila ukilitoa kwa mapepo halikemei bali lina filisi, mambo ya sadaka ya mavuno siyo mpango wa MUNGU ni wa shetani.

Katika biblia MUNGU ambaye yupo ni MUNGU wa Isaka na Yakobo tu! Kuna watu wanaomba sana MUNGU lakini sasa hawajui wanamuomba MUNGU yupi? Kuna madhabahu zinafanya kazi ya shetani, na mtumishi amepewa agano lake lazima waseme “Mungu wanabii flani” sasa yupo Mungu wa nabii flani au ni MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo?

Na wewe muumini unapokiri Mungu wa nabii flani, unakuwa umeunganishwa katika agano la shetani, “Usikae ukasema Mungu wa mtumishi flani ” sema MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Mnapotezwa mnakuwa na mapepo, alisema “watatumia jina langu kuwapoteza wengi.”

YESU anakuitaji, uko wapi? umeshikwa wapi? Ni wakati wa kukata minyororo yote na kutolewa katika ukibarua wa shetani, nafsi nyingi zimetekwa, “baraka za nafsi zilizotekwa zikarudi katika jina la YESU.” Hata wewe ukiona baraka zako huzioni, ujue zimetekwa katika ulimwengu wa roho. Pale MUNGU anaposema utakuwa hivi, yanatakiwa yakatimie.

Ubatizo wa kisima:-
wako watu wamezika nafsi zao kupitia ubatizo wa kisima, ambao haupo! hilo ni kaburi. Unajiita mkristo unakwenda Mbinguni, mbingu gani unaenda wakati nafsi yako imebaki kwenye kisima? Kibinadamu kisima siyo kisafi, atakuja mtu hajaoga, mchafu kimwili na kiroho, anachafua maji, atatumbukizwa na mwingine kwenye kisima! kabatizwe katika kijito cha utakaso, kinachotembea, kabatizwe upya! Na ubatizwe kwa jina la MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo na siyo jina la mchungaji au nabii.

Kupeleka udongo kwenye maombi:- unapokuja kwenye maombi, unaleta vyombo vyako au mifugo yako viombewe au unakuja wewe? ‘unapaswa kwenda wewe.’ sasa unaposikia mahali leta udongo uombewe, kwanini unapeleka? Fahamu mahali unapokaa kuna baraka zako, sasa unapopeleka udongo, baraka zako zinachukuliwa katika ulimwengu wa roho, baraka zako zinaenda kwa mtumishi, yeye anafanikiwa, wewe unabaki mweupe na matatizo. Hata dukani kwako au katika biashara, hutaona pakinyanyuka. YESU hakututuma tuombee udongo, tunakuombea wewe, kupitia wewe vitu au mali zako zitatakasika.

Liko jini linaitwa muhubiri au nabii, linakaa juu ya mtumishi, mnaona mtumishi anahubiri kweli, kumbe ni pepo, na wanatumia mapepo kuwangusha na kupiga kelele mkidhani mnafunguliwa kumbe ni pepo. Ndiyo maana watu wanaenda kwenye maombi miaka na miaka ila tatizo bado liko pale pale. Unakuta madhabahu ni ya kuzimu, siri anaijua mchungaji au mwinjilisti, wachungaji wanaenda kwa waganga, wanachanjwa wakisema waweze pata waumini wengi. Nchi inaendelea kutobadilika, maendelo hayaji, kumbe ni uchawi; uchawi Januari mpaka Disemba uchawi. Wachungaji wengine wanajipulizia manukato ya kipepo, mkiwasogelea mnaanguka na mapepo mnabaki kusema ni nguvu za MUNGU kumbe ni mapepo. Nyota yako, baraka zako za kiroho na kimwili viliibiwa kwasababu haikuwa na ulinzi, tubu ureje kwake, kusudi la MUNGU likatimie.


SALA YA TOBA:

Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, namkataa shetani na mambo yake yote. Eeh Bwana YESU naomba ukanitoe kwenye magereza, ukanitoe kwenye mashimo, ukanifungue, ukanishikilie kwa utukufu wako. Eeh MUNGU BABA, MWANA na roho mtakatifu uliye mbinguni. Amen!

PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.