Pages

Saturday, March 21, 2026

UWE MACHO NI SIKU YA KUJICHUNGUZA YESU ANARUDI.

BWANA YESU ASIFIWE, leo napenda ujue jambo fulani ambalo MUNGU anataka ujue, katika wokovu wako ili siku ya mwisho uwe na cha kumjibu MUNGU.


Mwanzo : 2:16-17;

“ 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana hakika siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”

Hapa MUNGU alikuwa akimpa maagizo Adamu, hata wewe kwenye maisha yako yote MUNGU anakupa maelekezo na maagizo kwasababu anakupenda hataki uangamie yakupasa uyafuate na kuyatii ili ufanikiwe hapa duniani na baadae ukarithi ufalme wa mbinguni, katika maisha ya mtu ili asife katika dhambi anatakiwa asimame mwenyewe katika Imani ya sheria na hukumu za MUNGU ili apae kushinda kwa kuwa katika hukumu mtu atasimama mwenyewe mbele za MUNGU.

Mwanzo 3:9-19
 mfano huu unakufundisha nini ni kwamba MUNGU hakumuuliza Hawa kwanini walikula matunda ya mti ambao Adamu aliambiwa asile japo Hawa ndiye aliyemshawishi Adamu ina maana MUNGU alikuwa hajui? Hapana hakumuuliza Hawa kwa sababu hakumpa maagizo ya mti yeye alimpa Adamu ndio maana alimuuliza Adamu? Haya sasa nikufungue macho na ujiulize.

Warumi 10:9;

9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”

Kwa maana ukimkiri hii ni mtu mmoja sio wengi akamkiri YESU kwa kinywa chake, siyo vinywa vyao yakuwa ni BWANA na kuamua moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu ataokoka, hapa anamzungumzia mtu mmoja sasa basi siku hiyo utaulizwa kwa nini hujamkiri YESU, au kwanini hujaokoka hauwezi kusema ooh nilikuwa na Mchungaji wangu lakini alinifundisha ya kwamba hakuna wokovu kwa mtu akiwa duniani, mwana wa MUNGU Bwana atakukataa ataseme ni kweli kabisa kutakuwa hakuna kisingizio.

Mfano mwingine yamkini umeona pombe ikibarikiwa na mchungaji wako kanisani au hata nyumbani na wewe utaulizwa kwanini ulikuwa unakunywa pombe huwezi kujitetea eti kwa kuwa Mchungaji alikuwa anabariki pombe alikuwa anakunywa nawe ukajihalalisha, hakuna utaulizwa neno langu linasemaje? Utaambiwa pita kule sikujui.

Utaulizwa wewe (fulani kwa jina lako kwanini umefunga ndoa na mimba tena kwa agano la shida na raha ukianza MUNGU mimi sikufundishwa; neno linasemaje? Utaulizwa habari ya Rebeka na Isaac, vile vile kwa wale mtu yule ambaye hataki ubatizo wa maji mengi ya mto unaotembea.

MUNGU akimuuliza fulani mbona hujabatizwa utasema mimi nilibatizwa na mchungaji kanisani kwa kutiwa maji kidogo utasema au kichwani, au pengine kwenye kisima ndani ya Kanisa na umesoma kuwa YESU alibatizwa mtoni wala hajawahi kujiuliza au umewahi kujiuliza, siku ya mwisho hutasema mchungaji wako alikwambia hivi na vile MUNGU amekupa wewe hautakuwa na nafasi mbela za BWANA YESU kunyosha kidole, kulaumu, wala kumshitaki, kwa hiyo ni bora uwe na tabia za kusoma neno kwa wingi ujue maelekezo MUNGU akupe neema na ujue jinsi ya kusimama mwenyewe kwa MUNGU hakuna kunyosheana kidole ni kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe naamini umejifunza.


SALA YA TOBA:

Kama hujaokoka kiri sala hii sema “BWANA YESU ninatoka kwa uovu wote niliotenda kwa kujua na kutokujua na kuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha mauti andika jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.

MUNGU akubariki sana kwa hatua uliochukua MUNGU akuponye akufungue akushike na kukusaidia……… Amen.

APOSTLE DORCAS SAMUEL MDEE.