Pages

Wednesday, March 11, 2026

MAPIGO SABA YA VITASA, DHIKI KUU YA MIAKA TATU NA NUSU YA MWWISHO ( SIKU 420 ).



Bwana YESU asifiwe ! Katika kipindi hiki nitaelezea yale mapigo saba ya mwisho ya dhiki kuu, ni mapigo na mateso ya dhiki kuu ambayo yatakuwa katika miezi ile 14 ya mwisho, ambapo ni siku 420 za mwisho. Mapigo ya vitasa, ni mapigo MUNGU anamaliza ghadhabu yake juu ya ulimwengu na wanadamu waliokuwa wamebaki hapa duniani. Kumbuka:

· Nilianza mapigo ya kwanza nikaelezea yatakuwa ni ya mihuri.

· Nikaja mapigo ya pili ya baragumu.

· Na sasa mapigo ya tatu ni mapigo ya vitasa.


Yeremia 30: 7

“ 7 Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo. ” naongelea habari ya tabu kubwa sana aliyoandaliwa Yakobo. Yakobo anaweza kuwa mtu wa MUNGU, mwana wa Israel au Yakobo wa shetani. Ila hii itahusu Yakobo wote, lakini Yakobo yule ambaye atavumilia haya mapigo katika ile ghadhabu ya MUNGU ya mwisho, yeye ataokolewa.

Nimeshaongelea juu ya mapigo hayo, je utavumilia? Lakini kama utavumilia, ina maana una mkataa YESU sasa hivi ! MUNGU ana ahadi ya kukuokoa endapo utavumilia, kipindi hicho watu walishanyakuliwa katika unyakuo imebaki ni ile miaka mitatu ya mwisho.

Ufunuo16: 1-21 nitaelezea kwa hatua sawa na vile Roho Mtakatifu atavyoniongoza. Habari hizi ni kwaajili ya watu watakaobaki, wale ambao wanamkataa YESU sasa hivi, wale ambao wanachezea wokovu. Hayo yatakao wakuta ni vizuri uweze kuyajua maana yamefungwa na shetani ili watu wasieze fahamu, ili wakapata kuangamia.

Ufunuo 16: 1- 2

“ 1 Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, enendeni mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya MUNGU juu ya nchi. 2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”

Habari ya majipu kwa wale wenye chata ya huyo mnyama, na wenye kusujudia sanamu yake, na hata sasa hivi kuna wanadamu wanaabudu sanamu, hao teyari wameshajingiza kwenye hayo mapigo. Labda kwa neema ya MUNGU waache sasa waje katika njia za YESU watapona.

Ila kipindi hicho, wakati wa dhiki kuu, watakaokuwa wakiabudu hiyo sanamu na kupiga chapa, ni kimaana kukubaliana na mambo ya mpinga kristo, wakati huo kristo hayupo tena duniani. MUNGU atakuwa akiwaangalia, mkiwa mnatembea na hiyo chapa. Mtateseka na majipu yasiyo pona, watu wataoza, wataumwa magonjwa yasiyo na mfano.

Ufunuo 16: 3

“ 3 Na huyo wapili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote venye roho ya uhai katika bahari vikafa.” Pigo hili, mito kuwa damu, bahari kuwa damu.

Ufunuo 16:4- 7

“ 4 Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji zikawa damu. 5 Nami nikamsikia Malaika wa maji akisema, wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe nao wamestahili. 7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana MUNGU Mwenyezi, ni za kweli na za haki, hukumu zako.”

Wako watumishi wa MUNGU walioteswa, wakina Yohana walikatwa vichwa. Na wako wengine ambao ni watumishi wa MUNGU ( akisema manabii inamaaana ni wasemaji wa kweli wa injili) walinyanyaswa, waliotaka kuuwawa, waliologwa, waliopewa sumu, waliofunguliwa kesi, waliofanyiwa kila hila, wote watalipwa mapigo.

Kama wewe una vitu hivyo acha ! kwasababu yana kuhusu. Hakuna jambo lilofanyika MUNGU hajaandika rekodi yako, majani yataongea, miti itaoangea, ardhi itaongea, mwisho utakwenda wapi?

Ufunuo 16: 8 - 9

“ 8 Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 9Wanadamu wakaunguzwa,maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la MUNGU aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”

Jua kuwaunguza watu wote kama moto, wanadamu wengi, wanavyopitia katika matatizo hivi sasa, wanamtukana MUNGU, wanamdharau. Na kipindi hicho atawatesa na bado watamtukana MUNGU, lakini MUNGU ataendelea kuwatesa, ndiyo mapigo hayo.

Ufunuo 16: 10 -11

“ 10Na huyo watano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, 11 wakamtukana MUNGU wa mbingu kwasababu ya maumivu yao na kwa sababu ya majipu yao wala hawakuyatubia maneno yao.”

Mateso yatakuwa kila eneo, kila kitu kitauma, yule atakayebaki atateseka. Kumbuka watakuwa teyari na roho za shetani ndani yao, na shetani amewaekea ili waangamie hata wanapoteswa ni ili wapotee, wafungwe fahamu wasije wakabadilika wakamrejea MUNGU. Hivyo, shetani na zile namba, na ile chapa itawafanya wamkatae MUNGU maana ile roho ya huyu ambaye yuko chini haimtaki MUNGU, na wanadamu wataunganishwa hivyo hivyo isipokuwa wale ambao watang’ang’ania toka mwanzo kwenye mateso, iwe wamekatwa au wamechomwa moto.

Kutakuwa hakunaga amani tena, kwasababu amani nayoiongelea ya sasa hivi ni kwasababu kuna uwepo wa YESU na MUNGU. Uwepo wao utakapoondoka, amani itakuwa hakuna tena. Nilipoenda kuzimu, niliona kuzimu hakunaga amani, wao ni kupigana tu, ndiyo maana huku duniani wanataka wanadamu na mataifa ya fanane na huko kuzimu. Na wako wanadamu wanaenda huko kuzimu, wanapewa zile roho za kuja kuichafua dunia.

Ufunuo 16: 12- 16

“ 12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha lile joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya MUNGU Mwenyezi 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye na kuyatuza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”

Huo mto ‘ Frati ’ utakaushwa kabisaa, na badala ya maji pale kutembea itakuwa ni udongo ili nchi mbalimbali katika vita ziweze kupita kama barabara.‘ Har- Magedoni, ’ nilipata kufika kwa neema ya MUNGU, Ni eneo kubwa, mwanzo mpaka mwisho lisilo na makazi ya kudumu zaidi ya kilimo, wanaisraeli wakitambua kuna ahadi ya Mwenyezi MUNGU ya kupigania hapo, wasijenge watakuja pigiwa hapo. Napo wafalme wote na wanasiasa watakuja kubadilishwa katika ulimwengu wa roho, watakuwa katika ufalme wa mpinga kristo, watawenda kupigania pale, mataifa kwa mataifa, na ndipo MUNGU atawamalizia pale.


Ufunuo 16: 17 -18

“ 17Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu katika kile kiti cha enzi, ikisema imekwisha kuwa. 18 Pakawa na uememe na sauti na radi, na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyo kubwa tetemeko hilo. ”

Itatokea tetemeko ambalo neno la MUNGU linasema kabla ya kuumba ulimwengu halijawahi tokea. Itatokea radi, mitikisiko ya ajabu, kila kitu kitavunjika vunjika, unavyovijenga, unavyovianda, maviwanda, kila kitu.


Ufunuo 16: 19- 21

“ 19Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka, na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za MUNGU, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka Mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana MUNGU kwasababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”

Pigo la saba; mawe kutoka Mbinguni yatawapiga, kuwavunja, mvua ya ajabu, tetemeko, mateso ya ajabu, kwa wale watakaobaki. Je, mateso yote utaweza kuvumilia? Yamekwisha kuandaliwa, malaika wameanda ghadhabu, tazama milima mirefu yote itaondoka, mataifa yataondoka, visiwa vitasambaratishwa, itakuwa ni vunja vunja. Kinachovunja hujui kinatoka wapi, siyo nguvu za kibinadamu, ni kwa yeye mwenyewe ajuavyo. Hiyo yote ni hasira hamumtaki YESU mwokozi. Yeye hajaleta ukristo yeye ameleta wokovu kwa jina lake YESU.

Ili ukapate kuokolewa na haya, okoka mpe YESU maisha yako na ukapate kuishi katika utakatifu. mpinga kristo atakuambia usikoke, utakwenda Mbinguni, tutatakuzika. Napenda kukuambia eh mwana wa MUNGU haitakuwa hivyo.

Kumbuka katika haya mateso ya vitasa, bahari kuwa damu, jua kuunguza watu, kutakuwa kuna giza, mto Frati kukauka, haya yote yatatimia ili kuhakikisha ile ghadhabu ya Mwenyezi MUNGU inakwenda kutimia, lakini bado itakuwa siyo mwisho wa dunia !

Sasa haya maombi unayoambiwa tutakuombea, yatakusaidia, yatakufikisha Mbinguni; Hayatakufikisha Mbinguni! Nachokuambia YESU mwenyewe hata alivyokufa alijikabidhi maisha yake na roho yake mikononi mwa baba yake. Hata maombi yaliyofanyika na Maria, Magdalena na wanafunzi wake, haikusaidia kitu. Walipomzika, wengine walienda zao kuvuwa samaki, hata kazi za YESU alizowaachia, waliachana nazo. Na wewe kitakachoweza kukusaidia, unyakuliwe kama akishuka sasa au kama ukatangulia, ili uweze kunyakuliwa na kukosa haya mateso yote au mitihani utakayopitia katika nyakati hizo, ni kumpa YESU maisha yako kiukweli.

Hata maombi ambayo walimuombea Musa haijasaidai, alikuwa ameshatengeneza na MUNGU. Yeremia, Yoshua, Paulo, wote maombi haijawasaidia. Yohana mbatizaji alikatwa kichwa, kichwa kikapelekwa sehemu nyingine, maombi juu ya huo mwili haikusaidia, kilichosaidia ni yeye alikuwa na MUNGU, ana YESU moyoni mwake alishajikabidhi.

Hivyo, MUNGU ana agano na mtu aliyekwisha mpa maisha yake, kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, hawez kukusahau, hawez kukusaliti. Lakini leo hii, dunia hii kwa kiwango kikubwa wanaona ni mambo ya kawaida, kumbuka ulitoka huko juu, unatakiwa urudi huko juu, lakini shetani anataka uende naye chini, kule alikofukuziwa.

Hii ni ghadhabu ya Mwenyezi MUNGU, shetani alikosea kutoka Mbinguni, ni ghadhabu hiyo. MUNGU ana hasira miaka mingi , ghadhabu imekaa, akaja kwa viumbe wake, ilivihukumiwe kwa haki, akamtuma mwanaye YESU Kristo, akatuma manabii, akatuma watumishi wake na injili yake, lakini watu wameikataa.

Isaya 30: 1- 2

“ 1 Ole wa watoto waasi; asema Bwana, watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi, wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu, wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi. 2Waendao kutelemkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao , na kutamainia kivuli cah Misri.”

Nilikuwa naongea na Roho Mtakatifu siku moja, juu ya habari ya uzinzi unaofanyika hapa duniani, na ndoa zinazofungishwa lakini haziko Mbinguni, maana mmefungisha mahali hawamtaki YESU, na huwezi tumia kitu cha Mbinguni mahali ambapo hamna YESU. MUNGU wa Mbinguni hajaunganisha ndoa hizo kwasababu yeye hakai kwenye sanamu, na kwa namna hii wana ndoa wengi ni wazinzi kwa kuju na kutokujua, na haya ibilisi ameyaficha. Anasema kwa kifuniko lakini siyo cha roho yangu wajifunikao.

Sasa hamuokoki alafu mnafunga ndoa kwa jina la YESU na Roho Mtakatifu, na yeye amesema ameleta wokovu, hajaleta dini. Mnamtajaje mahali ambapo roho yake haifiki, haingunishi ! hata akisema muende kwa amani ile roho ya YESU haiendi na nyinyi, mnaitamka lakini siyo kwa roho yake mnaenda bali nyingine. Na hii husababishia watu kuwa na uzinzi sanaa mpaka wazee, hata wa miaka 80 hawajafunga ndoa kama apasavyo Roho Mtakatifu kwasababu huwezi kufunga ndoa kama hujaokoka.

Na hata kama umefunga ndoa siyo ya Roho Mtakatifu, inabidi ibarikiwe upya, ili uzinzi ukatolewe maana haya ulikuwa huyajui ni mambo yamefichika. Amesema kwa kutumia kifuniko wakijificha, wakijifanya ni roho yangu, huku kukiwa na sanamu, mtumishi anatumia uchawi, uzinzi mnamepelekea YESU akabariki. Wengine wana mimba wanajongea YESU akawabariki, msingi ambao siyo MUNGU anautaka.

Zinaa inaendelea kuhalalishwa na baadhi ya watumishi katika ulimwenguu huu, ikiwa mambo ya kiroho hawasemi ukweli, wanadamu wanatakiwa waambiwe ukweli, inawasaidia, wanawekwa huru. Neno linasema “ Ole wenu mnaowazuia watu wasiende wakati nyie hamuendi ” na hii ina hukumu kubwa, umefanyika kuwazuia maelfu na mamilioni, kuwakwamisha na habari za uongo, yako mapigo kwaajili ya watumishi.

Msiabudu wachungaji, manabii, mkaona ni Mungu. MUNGU yeye, hafananishwi na chochote. YESU, mwana pekee wa MUNGU alimwabudu baba yake, yeye mwenywe hakaubudu vitu kama hivyo. Imeandikwa usiabudu miungu wala chochote alichokiumba, mwabudu MUNGU, kumbuka YESU ni umoja wa nafsi ya Mungu na Roho mtakatifu, hao tu.

Anakuhitaji, amekupenda, akakuumba kwa mfano wake, sasa kwanini uje kuangamia kwa ghadhabu aliyoipanga kumuhukumia shetani ? Hamumtegemei MUNGU, mnamtegemea shetani, mnazini mpaka na wanyama, Ni makosa makubwa, nani dhambi, nani laana, sasa msipende kufanya madhaifu waliofanya wengine, Mwokozi anarudi, na haya mapigo yameandaliwa. kitakachokusaidia ni wokovu !

SALA YA TOBA:

SEMA; BWANA YESU NINAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZIFANYA, NINAKUPA MAISHA YANGU MWOKOZI UNISAIDE. JINA LANGU ULIANDIKE KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE, UNIOKOE MOYO, NAFSI NA ROHO YANGU NA VIUNGO VYANGU VYOTE, MPAKA MACHO YANGU NA AKILI YANGU. NISAIDIE NIKUPENDE, NA ROHO MTAKATIFU ANIONGOZE KWA UTUKUFU WAKO KATIKA JINA LA YESU.

‘ Najitenga kabisa nakukataa kurudi nyuma. Nasonga mbele, najua mbele ni pazuri, nyuma ni paya.’

Hiyo siku unaweza shangaa hata mchungaji wako akabaki, mtu uliyetegemea atakupeleka Mbinguni. Na neema ya mwisho ndiyo hayo mateso yote, itafika mahali, hata wale wanaosema wanampeda Bwana YESU utapigwa panga. Je utashinda hiyo?


AMEN!


PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.