BWANA YESU ASIFIWE. Nawasalimu mataifa yote katika jina la BABA, la MWANA, la Roho Mtakatifu. Amen.
BABA ninakushukuru kwa neema yako na wakati huu nikiendelea kumharibu aliye mbele nyoka ibilisi shetani na nguvu zake zilizoko ndani ya watu. Nikiamuru nyoka yule wa Musa katika ulimwengu wa roho akawameze nyoka wote wa Farao walioko ndani ya wanadamu nje wakitobolewa wakiharibu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Mbingu zikiendelea kuwa wazi kwa jina la YESU kwa damu ya YESU KRISTO Nazareti. Amen.
BWANA YESU ASIFIWE,
Kama nilivyokwisha kuonyesha hapo picha hayo ni mafuta ya upako kwa jina lingine sema mafuta ya olive oil au kwa kiingereza Anointing oil. Lakini haya mafuta hapo yalipo hayana upako wa aina yoyote. Kwa hiyo ni mafuta kama yalivyo mafuta ya mizeituni.
BWANA YESU ASIFIWE,
Mwenyezi MUNGU aliumba mmea huu kwa kusudi lake kama wanadamu watumie kwa chakula na mambo mengineyo.Kwa namna alivyowaamuru Manabii kipindi cha nyuma kwa ajili ya kufanyia kazi yake.
Katika kitabu cha Kutoka 40: 10 -11 neno la MUNGU linasema hivi
“ 10 Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana. 11 Kisha utalitia mafuta birika na tako lake, na kuliweka liwe takatifu.”
Ninapoongea habari ya mafuta, haya si kwamba ni kitu kigeni katika dunia hii na siyo kigeni katika nyakati zile za kale. Lakini kipindi hiki cha sasa ni tofauti na cha kale. Maana hiki ni kipindi cha uovu wa hali ya juu sana. Ambapo huyu muovu anatafuta kila namna aweze kuwateka wanadamu na kulipindua neno la MUNGU kwa namna mbalimbali. Lakini kwa namna yoyote atakayojaribu hakika hataweza katika jina la YESU. Ndio maana Mungu mojawapo ya huduma zake akawa amechagua huduma ya Nabii katika zile tano kwa ajili ya kupeleka ujumbe na hatari inayokuja kujulisha wanadamu katika mataifa na katika dunia kama alivyoniita kwa ajili ya dunia.Ujumbe huu ni kwa ajili ya dunia nzima kama alivyokwisha kunielekeza BWANA YESU kuhusu haya mafuta ya upako. Mafuta yanayoitwa ya upako siyo salama siyo salama tena kwa sababu yameingiliwa na yule muovu wanayawekea uchawi wanawekea majini wanayapeleka kuzimu wanayaweka makaburini halafu anasingiziwa ndiye amekuponya unapoyatumia nami nakuja kwako utakayesikia usikie waeleze mataifa yote kuanzia sasa wasitumie mafuta yanaitwa upako mtaponywa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu na jina lake basi nitasoma katika kitabu kile cha Wakorintho.
2 Wakorintho 11: 14-15.
“ 14 Hivi wala si ajabu. Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakajigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
BWANA YESU ASIFIWE!
Neno la MUNGU linasema hivi; Shetani hujibadilisha hujifanya kama Malaika wa nuru. Na hivyo hivyo katika watumishi wapo ambao wanajifanya ni malaika wa nuru kumbe wameshajibadilisha ni wa shetani. Sasa wanavyokuwa kwa shetani pia wanatumia haya mafuta MUNGU ambayo alikuwa ameyaagiza yatumike katika agano la kale. Hata mimi nilikuwa nayatumia. Akaniambia “kuanzia sasa Hebron Nabii wangu usitumie tena mafuta haya. Nguvu zangu hata ukiyaombea sitazishusha hapo kwa sababu mafuta haya yamechafuka na kuteka dunia kwa kiwango kikubwa sana. Kwa sababu baadhi ya watumishi si wa nuru ni wa giza. Sasa nakueleza wewe kama Nabii wangu, hatari ni hiyo.” Kwa hiyo mafuta yote ya upako kuanzia sasa hivi hayafai kutumika tena. Atakayetumia anatembea na majini na uchawi. Kwa sababu mafuta haya nitakueleza mambo yanayofanya. Kama vile walibadilisha ubatizo wa kweli na kuweka wa kikombe usishangae na katika mafuta wamebadilisha.
BWANA YESU ASIFIWE,
Kama vile ulivyobadilisha neno la MUNGU sawa sawa na Wagalatia 1:6 kwa kufuata injili ya namna ile nyingine, ile nyingine ni ya giza. Kwa hiyo na katika mafuta haya wametamkia maneno ya giza na nguvu za giza na zaidi wameweka na mafuta ya nyama za watu walizokufa wanachukua kaburini pamoja na mifupa wanayasagia humu kwenye hayo mafuta alafu wanaweka na mengine na maji ya maiti katika mochwari mbalimbali kutokea moja ya nchi ya Afrika Magharibi kuna shimo kule wanayatoa kabisa halafu matokeo yake wanasema wanahubiri katika jina la YESU kwa sababu yameandikwa ni mafuta ya kutiwa ya kuponywa sawa sawa neno la MUNGU lilivyo lakini wao wameweka vitu vingine.
Sasa kuweka vingine madhara yake wanadamu wanatutumia haya mafuta wanasema YESU ameniponya, MUNGU ameniponya kumbe ni majini kumbe ni mapepo, na yanakuwa na maagano ya kuua kila anayetumia haya mafuta kwa wale ambao walikuwa wamekutana na bahati mbaya kukutana na watumishi wa kipepo wote wameibiwa nyota wote wamewekewa mauti siku zao za kuishi hapa hapa duniani zimekatizwa na hata YESU akija kupitia haya ya mafuta yanaitwa ya upako lakini kumbe si ya upako ni ya upako wa kishetani si ya upako wa KIMUNGU yatakufanya usiende mbinguni kwa kujua na kutokujua. Sasa ndio maana kama Nabii wake YESU amenituma nikuambie habari hii.
Hata mimi mwenyewe ameniambia nisiyatumie tena katika kanisa maana naye ananiambia najua wewe una nguvu za MUNGU anayekuwepo huko kwenye hizo nguvu za MUNGU. Sasa na wengine wanaendelea hivyo lakini wanaweka nguvu za shetani. Sasa uyaondoe, utatumia Hebron jina langu niko Roho Mtakatifu na mimi na wewe na nguvu zangu ziko juu yako nguvu zangu ni roho. Sasa jambo hili MUNGU ameliona ni hatari kubwa sana kwa sababu hawa watumishi wa kipepo wamezaliwa wengi sana na ndio wanatembea nayo. Wanayatumia kwa namna ya ajabu kuwatesa wanadamu na kuwafunga wasije wakaenda mbinguni, mwanaye anarudi. Unaona shetani alivyowateka watu na haya mafuta. Kwa sababu watumishi wengi zaidi wamejibadilisha ni wa shetani si wa Mwenyezi Mungu. Na ndio wanayatumia hayo kuwateka. Bwana Yesu asifiwe.Wanapojipaka yanakuwa yanawapeleka kuzimu.
Kutoka 25:6 anasema hivi.
“ 6 Na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri.”
BWANA YESU ASIFIWE,
Naelezea mafuta haya ambayo MUNGU alikwisha kuyaandaa kwa ajili ya wanadamu kwa ajili ya kazi zake ambapo haya mafuta mimi ninapoyachukua huaga ninayaombea natamkia nguvu za MUNGU uweza wa MUNGU. Sasa na akiona ule uchawi anatamkia majini yake yanaingia vile vile mapepo yake yanaingia vile watakaoitumia wewe wajinga pesa zote walete hapa. Nikisema kila jambo waniamini wanisikilize watakapoyatumia mafuta haya inakuwa majini yanaekwa kule ndani akiyatamkia yakafungue kazi zako yakakuite lakini yakakufunge hayo hayo yanatumika kwa uchawi. BWANA YESU ASIFIWE! Lakini na MUNGU hayo anayatumia. Sasa MUNGU ananiambia Nabii wangu Hebron usiyatumie tena na uwajulishe dunia nzima kwa sababu yamechafuka ila kama ni kwa kula chakula tumia.
Kutoka 32:33 inasema hivii.
" 33 Bwana akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi, ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu."
Sasa na katika haya mafuta hao watumishi wameweka uchawi. BWANA YESU ASIFIWE! Uchawi, halafu wanasingizia jina la MUNGU wanaitaja jina la YESU wanaitaja Roho Mtakatifu. BWANA YESU ASIFIWE! na wanasoma neno la MUNGU sasa kama yeye amefutwa kwenye kitabu cha MUNGU na wewe unapoyatumia unakuwa ni sawa sawa na mtu aliyejipaka maji ya maiti ni mtu ambaye amejipaka mapepo na majini kwa kujua na kutokujua.
Isaya 10:27
“ 27 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwasababu yakutiwa mafuta.”
Anasema utapaka mafuta ya kukata nira shingoni na mzigo wako utaondoka. Kwa hiyo MUNGU alikuwa ameandaa kitu kizuri kabisa kwa ajili ya kanisa lakini kimetumika vibaya kimebadilishwa. Na kama kimebadilishwa MUNGU ameniambia niwaeleze na YESU ameniambia niwaeleze.
BWANA YESU ASIFIWE!
Anasema “Hebron unakwenda katika roho siyo tena katika mafuta. Sasa mafuta yamewateka wengi sana kwa kujua na kutokujua. Na shetani huyu anajibadilisha kama alivyojibadilisha, amebadilisha kweli na nataka ujue kwamba pamoja na hayo mpaka sasa shetani ana uwezo wa kuiga nguvu za MUNGU zinavyotenda kazi za kuiga mipango ya MUNGU inavyofanyika.”
Nitasoma katika kitabu cha Kutoka 7:11 uone jinsi ambavyo shetani alivyokuwa akiiga namna ya nguvu za MUNGU. Lakini nguvu za MUNGU zinakuwa ni tofauti na mafuta ambayo alikuwa anatumia mtumishi wa MUNGU wa kweli yatakuwa ni tofauti lakini ameniambia never. Kwahiyo hata kama kuna watumishi wa MUNGU watakiombea nguvu za MUNGU hazitakwenda niwe na kujua iwe Mhindi iwe Mjapani iwe Mmarekani iwe Mwafrika uwe popote katika jambo katika bara lolote nguvu za MUNGU hazitashuka tena hapo wala roho mtakatifu hatashuka tena yatabaki hayo ambayo yamejazwa majini na mapepo na MUNGU ameliona hili akaniambia.
Kutoka 7:11 - 12
" 11 Ndipo Farao na yeye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. 12 Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; Lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.”
BWANA YESU ASIFIWE!
Unaona sasa hapa uchawi wa shetani anaiga nguvu za MUNGU waganga na wachawi. Na katika mafuta haya shetani na yeye akaiga kwa nguvu zake kwenye mafuta haya haya akaweka huko. BWANA YESU ASIFIWE. Lakini inasema nguvu za MUNGU tofauti unaona fimbo ya Haruni ikabadilika kwa hawa nyoka ikawameza. Kwa hiyo nguvu za MUNGU zinateketeza hata mafuta yote ambayo yalikuwa na nguvu za shetani napozungumza muda huu katika dunia nzima hazitafanya kazi katika jina la YESU. Na hilo agano nalivunja kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti aliye hai ninavyosema shetani ana uwezo wa kubadilisha kuiga. Sasa iko silaha ambayo ni jina la YESU. Nitasoma katika kitabu cha Mathayo 24 maana watu wengi wakaacha kumfikiria YESU wanaweka imani yao kwenye mafuta na waganga na wachawi. Pasipo kujua na kujua kwa sababu yale mafuta pia yana roho ambazo za kukuporomosha wewe na zinapokuporomosha unapotea.
Mathayo 24:4
“ 4 Yesu akajibu, akawaambia, angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.”
Na ndio hawa sasa YESU anasema kwa jina la YESU mafuta haya nimeyaombea lakini kuna majini kuna mapepo utawajuaje kwa matendo yao wamebadilisha hasa haya mafuta na mbingu sasa hivi ninavyozungumza iko wazi inasikiliza.
Mafuta haya yanawekwa mafuta ya wanadamu waliokufa makaburini mifupa mafuta mengine yanabusiwa na shetani alafu wanachanganya kwenye madumu. Wanaweka kwenye vikopo vyao.Wakishaweka kwenye vikopo vyao mnapewa. Kwa hiyo unaona una nguvu. Kumbe ni nguvu za majini zinakuangusha, zinachukua vitu vyako. Inakuwa ni sawasawa. Umeenda kwa mganga huyu na mganga huyu. Na haya mafuta yanakuwa na upako wa nguvu fulani sawasawa na huyo mchungaji kwa maagano aliyofanya. Kama ameua sana au amezini sana shetani ndio anaongezewa nguvu sana. Katika hayo mafuta na mnapoyatumia ndivyo mnapozidi kuporomoka sana. Kwanza unakuwa wewe katika ulimwengu wa roho ni mbumbumbu wa kiroho katika ufalme wa YESU pasipo kujua au kujua. Lakini ukisoma neno la MUNGU pia katika kitabu cha Yeremia mambo haya MUNGU aliyaona mbali sana.
Yeremia 50:6. Neno la MUNGU linasema
“ 6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; Wachungaji wao wamewapoteza; Wamewapotosha milimani; Wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzikia.”
MUNGU anasema wachungaji, wahubiri, mitume, wainjilisti, waalimu kuanzia sasa atakayetumia mafuta haya, Bwana MUNGU wa majeshi ameniambia yana mashetani hayakomboleki, hayasafishiki yabaki kwa kula tu. Kwa sababu kupitia mafuta haya kondoo wengi wamepotezwa na wachungaji na wainjilisti na manabii maana wao wanajua wanachokipata kupitia mafuta haya lakini si Mwenyezi MUNGU. Ukisoma katika kitabu cha Injili ya Mathayo 28 asema habari ya YESU Hakusema twende na mafuta. Baada ya kuja yeye alituongezea silaha nyingine ambayo ni jina lake Roho Mtakatifu. Sasa hivi watu waende na silaha hii. Maana kupitia silaha hii shetani amekuwa akitumia mafuta alafu anaweka uchawi alafu anakuja kutumia jina la YESU na Roho Mtakatifu mnaona ndio lakini kumbe siyo.
Mathayo 28:18
“ 18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”
YESU anasema amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani mpaka kuzimu. Basi nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la BABA na MWANA na ROHO MTAKATIFU na kuwafundisha kuyashika yote niliyoamuru ninyi. Natazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari. Hii ndio silaha uombewe kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa adui akawa anachukua hayo mafuta anakuja kudanganyia wanadamu japo wako watumishi wa MUNGU wale ambao wana MUNGU walikuwa wanatumia mafuta haya lakini wao hawako hivyo. Kwa hiyo sasa mimi mwenyewe wameniambia Hebron usiyatumie tena kwenye jina langu wala kwa roho mtakatifu wala kwa kazi ninayokutuma. Haya mafuta yameharibika, yanatumika vibaya na shetani yanawateka wengi yamewapotoza wengi na wengi watakwenda kufunguka na hata sasa shetani analia maana hii ni moja ya silaha ya shetani ambayo alijisingizia mafuta ya upako. Ndiyo ni ya upako kweli lakini upako wa shetani nguvu za shetani.
Sasa haya mafuta yanapowekewa nguvu za giza yanaitwa mafuta ya uchawi. Lakini wewe huwezi kujua kama ni ya uchawi. Haya ni mambo MUNGU ameyaona. Sasa angalia MUNGU alikuwa akimtuma Nabii wake Yeremia. Anamtuma Nabii wake Yeremia. Anamtuma nabii wake Musa. Sikilizeni habari hizi. Anayesikiliza atakwenda kuponya.anayekataa shauri yake. Ndio maana shetani hapendi Nabii kwa sababu anajua Nabii ni kinywa cha MUNGU. Itafika mahali MUNGU atataka kusema na wanadamu wakae njia gani wakaaje hivi ili wakapate kuponywa ili wakapate kuvuka, na manabii wako kwa level tofauti. Kuna wa kijiji, kuna wa wilaya, kuna wa mkoa, na mimi ni wa mataifa yote. Kwa hiyo ananipa kwa ajili ya wote kueleza mambo haya. anayesikia asikie akaponywe. Kwa hiyo kama unayo uyatupe tupa kabisa wala usinunue tena unanunua uchawi pasipokujua na kujua hata kama ulikuwa unakanyaga ni uchawi ni uchawi ni majini ni mapepo. Unaponywa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa jinsi ya kujua haya mafuta ya upako ya wa uchawi yalivyo; Hayataitwa uchawi lakini nakuambia jinsi ya kuyajua kwanza kabisa yanawekwa picha za mchungaji au jina la mchungaji. Sasa inavyokuwa hivi maana kwamba si YESU ni huyo mwanadamu na jina la hayo mafuta ni jina la huyo mchungaji siyo YESU. Hilo ni moja ya agano. Kwa hiyo mafuta mengi yameandikwa majina ya wachungaji hapo ni uchawi. Anasema utukufu wake ashirikiane na mwanadamu.
BWANA YESU ASIFIWE!
Jambo lingine jinsi ya kuyajua yanauzwa bei ghali sana kwa sababu ni agano ambalo anaambiwa uwauzie wanadamu labda laki 5 au 4 yaani yanakuwa ni very expensive yaani analangua wakati huyu MUNGU yeye hawezi kulangua hata kama yaani inapitiliza. Hayo mafuta ya upako wa kichawi yanakufanya pia usikuwe kiroho katika ufalme wa MUNGU. Unazidi kudumaa imani. Kudumaa unazidi kuporomoka, kuporomoka, kuporomoka.Unakuwa wewe ni mtu tu wa kutaka vitu vya MUNGU. Sasa kwasababu wengi wametaka miujiza, wamekuwa wakikimbilia kwenye mafuta wanaona wanafanikiwa wanarudi wanakimbilia lakini wameua nafsi zao, wamenyanganywa nyota zao na unaweza ukafanikiwa lakini mafuta yale yale yanakufunga pesa zote ulete kwa huyo mchungaji yeye anakuwa tajiri kwa sababu yeye ni kimbola tayari shetani na wewe anakufanya pepo lake na msukule wake.
BWANA YESU ASIFIWE. Haya mafuta kuna mambo yamefichika wanajua wengine nikizungumza siyo jambo jipya. Yanachanganywa na mafuta ya nyama za watu. Wale waliokufa makaburini wachawi wanakwenda kuiba usiku. Na maagano yake na mifupa. Mengine yanaekewa hata kope za macho ya wanadamu, yanawekwa mengine na nywele na vitu vya ajabu ajabu ambavyo vinapenda kumgandamiza mwanadamu pasipo yeye kujua na kujua. Sasa na wengi sana yamewatesa na katika kuwatesa yanawaharibu. Jambo lingine yanawekewa majini.Wewe huwezi kuyajua ni roho. Sasa akisema na roho mtakatifu anasema kwa jina la YESU nitatamka hivi utakuwa. Au namna nyingine yanakuwa na nguvu fulani ya kuangusha. Unaweza kuta watu wanajipaka wanaanguka tu. Ila ukianguka kweli nguvu za MUNGU zikikushukia unaweza ukaanguka.Lakini hizi wewe huwezi kujua mimi nakuambia kama Nabii wa MUNGU.
Unapoanguka kwenye ardhi chini maisha yako, vitu vyako, future yako inachukuliwa na kuzimu. Alafu yule mchungaji yeye anapewa kiasi alafu katika ufalme wa Freemason wao wanaendelea. Wanakupumbaza, wanakushikilia, nyie mkiona ni kitabu cha Mathayo kimesomwa imesomwa Zaburi alisema watawapoteza wengi kwa jina langu naongea habari leo ya mafuta yanaitwa upako. YESU alipokuja agano jipya yeye aliwaachia Roho Mtakatifu na jina lake. Sasa ninapoelezea habari hizi wengi watanishangaa na wengine watanielewa. Hizi ni nyakati mbaya sana. Nyakati za YESU kurejea.
Sasa Yesu ameniambia waeleze dunia nzima na wewe ukiupata ujumbe huu mtumie mwingine na mwingine. Mafuta ya upako Yote yana uchawi. Uchawi unasambazwa unauzwa. Yaani imekuwa kama irizi. Na nitamalizia bado kuna mambo mengine ambayo na yenyewe ameniambia waeleze dunia.Watu wananipenda lakini kupitia hiki kinawateka yale mafuta tu unajipaka ni namba 666.Sasa wengine ndio upako waliopewa na mbinu ya kufanya kazi hizo za kishetani. Na kupitia mafuta haya wametokea wachungaji wamezaliwa wengi sana kupitia haya mafuta. Mtu anaenda tu kwenye haya mafuta anapakwa anaonekana mchungaji,muinjilisti, mtume, ni nabii lakini si wa MUNGU. Haya haya mafuta ndio wewe unakuta unashangaa mhubiri anauza madawa ya kulevya lakini watu wanapona, watu wanafanikiwa anatenda dhambi si mtakatifu mambo yanakwenda tu hata afanyaje hata uue watu hata waangamie kanisani hata wachomeke. Yeye anaendelea tu. Lazima kujiuliza kama mwanadamu wenye akili huyu MUNGU si MUNGU wa mbingni ni Mungu mwingine wa Yesu mwingine. Sasa haya mafuta yanateka fikra yanafunga fahamu.Na kwa namna nyingine unapokonywa na shetani maisha yako kujipaka. Si umejipaka shetani mwenyewe. Sasa kwa mganga ukienda unaogeshwa unayatumia kanisani utafundishwa uyatumie hivi hivi. Kama yalikuwa na majini umekwenda na ndio maana watu wengi wamekuwa mbumbumbu. Pasipo kujua na kujua.
Sasa na madhara yake watu wengi watakuja kuchomwa moto siku ile ya mwisho watakaoendelea kuyatumia. Mimi sitalaumiwa nimewaeleza vivyo hivyo nawaambia tena kwa mara nyingine hili ni tamko kutoka mbinguni. Maji yote yanayotumika kuombea watu kumwagiwa msitumie yana mashetani yana majini yana miungu msitumie kuponywa kwa udongo msitumie chumvi, vitambaa vyote ni mapepo na majini msiombee kwa mishumaa au kupuliziwa maiki kwa oxygen mnaanguka hayo ni mashetani au kwa stika watu wanatembea na stika stika labda mkono wa mchungaji, mguu wa mchungaji ndio upone? Hapana tayari mnaabudu sanamu.
Amenituma habari hii niwaeleze. Mkapate kupona. Habari ya mafuta ni unajimaliza.Unayedharau shauri yako. Mimi nasema na nafsi yako, nasema na fahamu yako, nasema na viumbe vyote vinasikia na sauti hii na maneno haya hayatarudi bure kwa sababu ya hao wachawi lakini hawataitwa wachawi ataitwa ni askofu lakini mchawi ni mchungaji mchawi. Sasa basi hii nguvu napozungumza hivi haya mafuta yote dunia yanakwenda kuharibika. Hayatafanya kazi tena.Na kila atakayeyapaka kuyatumia ambayo yana uchawi atakutana na jambo ambalo litamwaibisha ajue kabisa na yeye amekuwa mchawi pasipo kujua au kujua. Sasa mimi ni mchungaji ninaongea na MUNGU. Yuko mchungaji mwenye anaongea na MUNGU. Yuko mchungaji m anaongea na shetani lakini anasema ni MUNGU au anaongea na miungu na kwa njia hiyo anawapoteza wengi. Kuanzia sasa watu wanaombewa kwa jina la BABA, la MWANA na ROHO MTAKATIFU basi wataponywa, Watafunguliwa, liko neno la MUNGU nguvu zake ziko. Tumesema tunaenda katika roho tutamaliza katika roho.
Bwana Yesu asifiwe!
Kila kitu kimepinduliwa. Shetani amefika kila mahali. Watu wanaponywa mpaka kwa matunda. Kwa maepo, kula maepo. Nimekula epo, epo la YESU likaniponya.Chungwa la YESU likaniponya. Buga la YESU likaniponya. Wewe umebadilishiwa injili unaponywa kwa jina la YESU. Amesema nimekupa bure toa bure. Unaombewa bure unatoa bure. Sasa imekuja nataka niguswe na mtumishi na mafuta anakuambia wakiwango fulani ndio napita na mafuta nawagusa ni majini hayo ni mapepo kwa sababu nguvu za MUNGU hakuna anayeweza kuzinunua. Hakuna! ila uchawi unanunuliwa. Yeye MUNGU humpenda ampae. Na hata MUNGU akimpa nguvu mtumishi anampa kwa level yake haziwezi kufanana hata na shetani hivyo hivyo kwa sababu anaangalia jinsi yeye mwenyewe alivyokubaliana na MUNGU kwa neema yake. Sasa hivi sasa imekuwepo makanisa ya mitume mengi katika dunia hii. Kila nchi mafuta. Wachungaji mafuta. Manabii mafuta. Waimbaji mafuta. Kondoo mafuta. Marais wana mafuta, mawaziri wakuu mafuta, wabunge wafalme mafuta. Sio YESU tena. Matokeo yake wamekuwa na wao wachawi pasipokujua kwa sababu kiongozi kipofu amewateka. Na madhara yake kama haya mara laleni kwenye mafuta mara binuka kwenye mafuta.
Nilikwenda mpaka Israel. Nimeyakuta ndugu msomaji mafuta haya yanamwagwa na kila dini watu wanapita na majini na mapepo unaangalia mbona jina la YESU linaondolewa uthamani wake. Kupitia roho mtakatifu nendeni mkaihubiri injili yangu sasa hili jambo MUNGU aliwapa wanadamu limebadilishwa sasa linampa shetani utukufu kupitia hapa watu wanatekwa unasikia leo ni mafuta watu wanaenda kwenye maombi kutafuta mafuta wanaenda kununua uchawi ni washiriki na MUNGU anaona katika ulimwengu wa roho na mwili lakini wewe ndugu hujui nyumbani kwako umeweka uchawi umeweka mapepo kumbe ni kamba ya kukufunga hata usiende mbinguni. Nimekwisha kukufundisha kuna wokovu wa kuzimu. Kuna wokovu wa kipepo. Kuna wokovu wa watumishi ambao wameitwa na shetani lakini wanasema wameitwa na MUNGU. Hawezi kusema ni shetani maana majini mapepo yote yanamwita shetani ni MUNGU ni BABA. Sasa ndio mambo haya wameitwa na baba yao wanaambiwa haya mafuta wekeni kitu hiki wekeni kitu hiki kitu hiki wanenee BWANA YESU wekeni na majini alafu kazi itakuwa nyepesi. Hata MUNGU alikuwa akimfundisha Musa jinsi ya kufanya kazi. Eliya nenda hivi Haya utarudi kwa Farao hivi MUNGU alikuwa anamwelekeza Nabii wake.
Sasa hata hapa mimi MUNGU ananielekeza ni hivi sasa waambie hivi unayosikiliza ni kwa faida yako. Mimi si kwa faida yangu. Mimi ni chombo tu kama mjumbe wake kukuletea habari hii njema. Mafuta yoyote yanayotumiwa kwa njia ya maombi ni mapepo. Ameniambia hii ni wiki ya pili sasa nilikuwa nayafanyia kazi. Kwa muda wake na wakati ikifika ananiambia haya peleka habari hizi. Kwa hiyo yote yana mapepo hayo mafuta sasa na wengine wanafanya sasa ndio kama uganga ndio kama uchawi. Na sasa hivi hiyo jambo walikuwa wanatumia la kuwashika wanadamu. Nguvu zao zimekwisha uwezo wao umekwisha. Sasa watumie jina la YESU. Watumie Roho Mtakatifu utaona hamna kitu tena. Hakuna wamewashika watu watabaki watumishi ambao wana MUNGU wa kweli katika jina la YESU mtu anakupa stika ya mkono shika hii nitakuinua shika wewe tumeambiwa hivi tusijifananishe na chochote kilichoko duniani na mbinguni tayari kwenye wokovu watu wanahusika na masanamu utabaki hapa ni habari njema hii nakuambia hakikisha unayakataa haijalishi umeokoka unaweza kuwa umeokoka lakini umetekwa na mafuta hata mimi nimetumia sana katika sehemu mbalimbali kwa kujua na kutokujua mara kuna MUNGU mara hakuna. Kwa hiyo wote tumepigika na mimi nilipigika lakini kwa neema ya MUNGU nilichomolewa huko katika jina la YESU.
BWANA YESU ASIFIWE!
Najua yaliyowasaidia wengi nilikuwa nayaombea watu wameparalyze sehemu fulani wapi wanakwenda kutumia wanaona mambo yanakwenda. Sasa kuja kuwafundisha kwamba hata shetani na yeye anabadilikaga kama ameweza kubadilisha neno la MUNGU na ana nguvu za kujifanya kwa kuwapofusha wanadamu. Sasa MUNGU ameliona hili na ameniambia niwaambie. Kwa hiyo mimi na mafuta ya upako bye bye katika jina la YESU. Na wewe unayetaka kwenda mbinguni yaache kwa sababu yana uchawi, yana majini yana mapepo. Tena Roho Mtakatifu ananiambia kuna mwingine yanawekwa mpaka damu za mbwa kama agano. Mwingine alikuwa sio mzinzi anapojipaka tu anakuwa mzinzi mwingine, anapojipaka tu ili kutumia tu ndio anaanza kuwa mlevi au ana akili zinaondoka, siku zake zinakwisha, mali zake zinaondoka. Yeye anaweza akaona anafanikiwa kumbe hata kile kiwango sicho ameshagawanywa nafsi amewekwa kwenye gereza kwa sababu wewe unatembea na irizi. Sasa MUNGU akisema wachawi hawataurithi ufalme wa mbinguni. Tazama kupitia mafuta unajipaka na wewe tayari ni mchawi. Utajitetea utasema kwamba sikujua. MUNGU amekwisha kusema wachungaji wanawapoteza na wengine ni vipofu na mimi nakuambia habari hii ikakusaidie ikakuweke huru.
BWANA YESU ASIFIWE!
Watu wanakuja na maji kwa jina la YESU anakumwagia ni uchawi ninawaambia sijui udongo unakuponya ni uchawi ni jina la YESU sijui vitambaa shika hii kitambaa utapona unachukua ni uchawi, ilifika mahali wakati ule sasa mtu akamgusa YESU, YESU akasema najisikia kama nguvu zimeniisha. Amegusa tu upindo. Maana nguvu za YESU zilikuwa mpaka kwenye upindo kwenye kila kitu. Sasa na wao shetani hapa wakaanza kuchukua binadamu sisi sasa hivi vitambaa vingine tunanunua hivi vitamba mnajua vimetoka wapi? Maana unasikia kanisani kila mmoja ashike vitambaa vingine vimewekwa majini vimenyewa vimechezewa mambo ya kila namna. Unakuja kushika na wewe umeshika majini umekwenda nunua kitambaa hiki bei fulani, ndio maana usishangae katika dunia hii sasa utakuta pasta ni mwanaume amevaa viatu vile vya kike virefu moka za kike zile ambazo zina kakisigino kama msumari na sketi kabisa kafunga na blauzi anasema haleluya god bless you watu wanaanguka watu wanabiringita mafuta haya mafuta ya kishetani yamezaa mitume, maaskofu, manabii, wainjilisti, kondoo wa kila namna za kishetani. Na watu wakamkimbia BWANA YESU. Lakini habari yao imefika, wewe unayenunua maji ni mashetani ili yakuponye udongo ni mashetani. Nakuambia popote najua shetani amekasirika lakini ana bahati mbaya. atakaa aniweze mimi hata mawakala wake hawatakawa niweze mimi wataporomoka watahangaika na kufika na kuteketea hilo ndio ninalokuambia shetani mwenyewe haniwezi wasaidizi wake hawaniwezi sembuse wewe rejea kwenye njia ya YESU kama unashindana na huyu mungu umekwisha. MUNGU anamchunga mtu maana amemuumba yeye kwa gharama kubwa.
Shetani anawaingiza kuzimu mnaambiwa mtaponywa kwa chapati kula tu na watu wanakula chapati nimekula chapati mambo yangu yakaenda vizuri unaona unawanyang’anya utukufu kwa kutumia jina la YESU kwenda katika roho unawekea kwenye chakula sasa hawa wamekukosa katika ndoto wakakulisha vyakula vile vya mtu anaota kwenye ndoto amekula amekunywa unajua vile unaweza umekunywa soda umekunywa maji ya maiti umekula nyama kumbe amekula mizoga hii ni kwa neema ya MUNGU katika dunia hii ukisema watu ambao watu wanasema sijawahi kula nyama ya watu nyama ya damu lakini ndoto ngapi umeota unakula nyama unajua ni nyama ya nini wale wanaweza kuibadilisha hata nyama ya mtu ukaona ni kuku ukaona ni roast ukaona ni chipsi unakula umekula hivo basi MUNGU akakutapishe katika jina la YESU basi nakusihi umkabidhi BWANA YESU maisha yako kwa sababu anarudi na jina lako liweze kuandikwa katika kitabu kile cha uzima wa milele. Sasa wengine yameandikwa katika kitabu cha shetani na mafuta yake kuzimu. Mioyo ya watu imejaa mafuta. Inaamini mafuta. Sio YESU tena.
MUNGU anaweza akatoa kitu lakini shetani anapita hapo ametupa ubatizo wa maji mengi kama YESU. Sasa umetolewa umekuja wa kikombe umekuja wa kisima. Sikiliza wengine wanakuja kwa jina la mchungaji alafu na jina la YESU. Halafu hapo hapo kubariki watu wazima badala ya watoto wadogo hivyo wamepindua na mafuta ni hivi hivi. Msishangae mnaojua hii sawa mafuta ni yana uchawi mbona hampigi kelele watu wabatizwe kama anavyotaka MUNGU kama mnapiga kelele kwa nini hamtaki watu wabarikiwe wakiwa watoto wadogo mnawafanya watu wazima wote hao mnajitakia kufutwa katika kitabu kile cha MUNGU. Anasema katika kitabu cha Ufunuo.
Ufunuo 22:18
“ 18 Nashuhudia kila mtu ayasikie maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.”
Sasa tazama mafuta wameweka majini wameweka mapepo tayari wameongezewa mapigo. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki MUNGU ataondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Sasa hapa utaona wameondoa ubatizo haya mafuta wameweka ushetani wameondoa ubarikio.Wameweka watu wazima badala ya watoto wadogo. Sasa ni nini mnafanya? Unajua unaweza ukawa unafanya kazi za kujaza tuseme neti ya mbu maji utajaza hayataka yajae. Yanadondoka siku zote hayatajaa. Ni kazi ya kujaza vitu ambavyo MUNGU havitaki. YESU havitaki. Anasema, "Niliwatuma baadhi ya watumishi miaka mingi wengine wakakataa. Wengine wakarudi nyuma. Wengine wakanikimbia wakakimbilia hayo mafuta.Wakaonekana wako na MUNGU, wako na mimi kumbe mimi siko nao. Napenda niwajulishe habari hizi kwa sababu mwanaye anarudi. Kwa utukufu wake katika jina la YESU ili ikakuweke huru.
1 Yohana 2: 26 - 27.
“ 26 Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanayowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha kaeni ndani yake.”
BWANA YESU ASIFIWE!
Hasa naeleza maana mafuta ya Roho Mtakatifu unavyookoka tu unapata mafuta ya Roho Mtakatifu yanakaa ndani yako. Sasa kuna mafuta ya ndani ya YESU na kulikuwa kuna mafuta haya ya nje. Sasa haya mafuta ya ndani jinsi unavyojiconnect na MUNGU na kumnyenyekea ndivyo yanaongezeka siku kwa siku na yakishuhudia ukweli na ndipo utamkuta mtu mwingine anakuambia anamtaja Roho Mtakatifu lakini mafuta aliyo nayo yaliyoko ndani yake yanataka ubatizo wa kikombe. Yanataka ubatizo wa kisima. Yanataka kubariki watu wazima. Sasa hayo mafuta ni ya uongo. Sasa na mafuta ya kweli yanafuata kama vile YESU yalivyofanyika kwake. Akasema hivi, watu hawa wanaombewa vitu kwa kifuniko cha jina langu. Kumbe sio roho yangu iko juu ya vitu hivyo. Haya mafuta yanawekwa majini mapepo. Sio roho ya MUNGU inakaa huko. Ni maji hatuponyi kwa maji si roho ya MUNGU. Kwa udongo, si roho ya MUNGU kwa vitambaa, si roho ya MUNGU kwa stika sijui za mikono miguu. Si roho za MUNGU kuna watu wengine wanauziwa shati na mchungaji analolivaa. Analipanga kiasi cha bei. Watu wanalinunua kwa kugombania. Siyo roho ya MUNGU. Ni mashetani ni mapepo.
Unakumbuka kipindi cha Farao? Waganga wa Farao walijaribu kubadilisha Nyoka. Sasa fimbo ya Musa ikawameza wote. Ndivyo ilivyo. Kama sasa hivi usicheke kipindi kile cha Farao na sasa hivi kimekuja kwa namna nyingine ambayo imefichika. Sasa kwa kujua na kutokujua Roho Mtakatifu akikaa ndani yako si atakuambia muokoke? mwingine anasema na Roho Mtakatifu amekaa ndani yake ndiye anamuongoza, tuabudu sanamu, tuabudu wafu, mshumaa utusaidie. Hapana. Katika jina la YESU imo nguvu. Damu ya YESU. Neno la YESU. Hicho tu. Lakini katika roho mtakatifu na usafi na weupe sasa unalitaja jina la YESU unairidhi hata kama hutumii uchawi humo huko huko ni vibranchi vingi vingi ubatizo kwa kikombe humo humo kwa sababu watakapochomwa wachawi ndipo watakapochomwa wenye majini ndipo watakapochomwa wanaobabudu miungu moto ni ule ule. Walevi, wazinzi, wachungaji waliomwasi MUNGU, wanaoamwagia maji.Watu wanakuja kanisani kumtafuta MUNGU.Wanaondoka na mapepo wanarushiwa maji wanaanguka alafu unasema kwa jina la YESU, kwa jina la YESU watu chini hakuna, siyo hivyo, MUNGU hayuko hivyo, haponyi kwa maji. Mwanaye YESU kuwa akimweleza akafundisha watumishi wake wakaendelea. Na hiki ni kipindi cha kwenda katika roho. Na kwa namna hii wengi wametekwa sana.
Mafuta ni mazuri MUNGU kayatoa lakini mwanadamu kayapitia hapo ametoa ubatizo tazama wa mwanaye tu umebadilishwa neno la MUNGU linabadilishwa watu waombewe bure ni pesa kumuona mchungaji hawa ni wachawi hawa ni waganga hawa ni wezi hawa ni wanyang'anyi wamejaa hawana uchungu na kazi ya MUNGU hawana uchungu na wewe wanataka kukumaliza na wakijua hawakupeleki mbinguni wakuchune haraka haraka wakumalize unabaki kusema nimepoteza muda wangu kwa MUNGU kanisani kumbe umeenda kwa wachawi aliyekutana na YESU hajapoteza muda wake aliyekutana na roho mtakatifu hajapoteza muda wake anayo faida hapa duniani na mbinguni akiandaa kujenga maisha yake yajayo. Maana umekuja hapa duniani utarudi mbinguni na umekuja hapa duniani usipoyasikiliza haya ya MUNGU utaenda kuzimu. Mshahara wa dhambi ni mauti.
Mauti ile ya milele, mauti ile ya mateso ambayo yatakuwa ni ya milele kama nilivyokwisha kusema katika habari ya dhiki kuu sasa uyakatae mafuta haya ukatae mahubiri yote ya maji yanaitwa sijui ya upako, soda ya upako, juisi ya upako, ugali wa upako, chipsi za upako, vitu kama hivvo vyote ni uchawi tena unavyokula ndio umevaliwa umemalizwa yeye atapita amini katika jina la YESU, YESU anatenda. Unasema nilikuwa hivi natafuta jambo fulani, baada ya kunywa maji baada ya kushika kile kitambaa tu nini kikakutokea? Naulizwa mambo yao yakaenda nani amekutendea? YESU muongo. Muongo nimeshaja maji yana uchawi na fimbo. Kuna wengine nilikuwa naonyeshwa wana fimbo. Wengine wanatumia majiini.Na wengine unakuta mhubiri wakati anahubiri analitaulo. Ameshika mkononi ni mchawi. Anajifuta ni uongo na wengine wanaficha mfukoni. Kwa sababu na wewe unajifanya kwa namna ile ile na kuwapoteza wengi.
Basi tumalize kwa muda huo nikikuambia mambo haya na neno hili likakusaidie ukapate kuwa salama. Usitekwe tena na haya mafuta ni ndugu yako ni rafiki yako mtumie rekodi hii akapate kujua hata wachungaji mkasikilize wa kila mahali maana wengine hamjui wengine mlienda mkatafuta upako kwa shetani mkapewa na wachungaji ukaanza kuwa mchungaji Akakutuma haya akafanye kazi ya MUNGU kumbe yeye alivyo na wewe amekuingiza huko huko sasa ndio itajulikana MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo aliyeumba mbingu na dunia. MUNGU wa Eliya atajulikana. MUNGU wa mtumishi wa MUNGU wa kweli atajulikana na mungu atakayeshindwa huyo ndiye ateketee. Ndio mungu wa wale mabahali. Hata sasa amekwisha shindwa katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti yamewaharibu ni uchawi maji yanarushwa watu wa kianguka.
Mauti ile ya milele, mauti ile ya mateso ambayo yatakuwa ni ya milele kama nilivyokwisha kusema katika habari ya dhiki kuu sasa uyakatae mafuta haya ukatae mahubiri yote ya maji yanaitwa sijui ya upako, soda ya upako, juisi ya upako, ugali wa upako, chipsi za upako, vitu kama hivvo vyote ni uchawi tena unavyokula ndio umevaliwa umemalizwa yeye atapita amini katika jina la YESU, YESU anatenda. Unasema nilikuwa hivi natafuta jambo fulani, baada ya kunywa maji baada ya kushika kile kitambaa tu nini kikakutokea? Naulizwa mambo yao yakaenda nani amekutendea? YESU muongo. Muongo nimeshaja maji yana uchawi na fimbo. Kuna wengine nilikuwa naonyeshwa wana fimbo. Wengine wanatumia majiini.Na wengine unakuta mhubiri wakati anahubiri analitaulo. Ameshika mkononi ni mchawi. Anajifuta ni uongo na wengine wanaficha mfukoni. Kwa sababu na wewe unajifanya kwa namna ile ile na kuwapoteza wengi.
Basi tumalize kwa muda huo nikikuambia mambo haya na neno hili likakusaidie ukapate kuwa salama. Usitekwe tena na haya mafuta ni ndugu yako ni rafiki yako mtumie rekodi hii akapate kujua hata wachungaji mkasikilize wa kila mahali maana wengine hamjui wengine mlienda mkatafuta upako kwa shetani mkapewa na wachungaji ukaanza kuwa mchungaji Akakutuma haya akafanye kazi ya MUNGU kumbe yeye alivyo na wewe amekuingiza huko huko sasa ndio itajulikana MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo aliyeumba mbingu na dunia. MUNGU wa Eliya atajulikana. MUNGU wa mtumishi wa MUNGU wa kweli atajulikana na mungu atakayeshindwa huyo ndiye ateketee. Ndio mungu wa wale mabahali. Hata sasa amekwisha shindwa katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti yamewaharibu ni uchawi maji yanarushwa watu wa kianguka.
Sababu watumishi kutamani nguvu, hawataki kuomba, hawataki kunyenyekea, hawataki kufunga, hawataki kushuka, hawataki kunyenyekea, wanataka tu vitu vya haraka. Unajua niwaambie wachungaji ambao mmekuwa wajinga wajinga hakuna kitu ambacho kinasimama bila gharama. Hata shamba lazima ufyeke visiki ung'oe kwa gharama. YESU mwenyewe alifanya. Mimi nataka tu wepesi. Matokeo yake umeingia kwenye shimo la moto. Na wengine wameshasaini mikataba hayafutiki tena wanasubiri kutekwa kuchomwa moto wa milele.Amewateka viongozi mbalimbali amewateka, wabunge mbalimbali amewateka wafanyabiashara, amewateka maskini, amewateka wanafunzi kutumia mafuta. Shetani anawaambia chukua hasa mchungaji unaitwa nani? Unaitwa fulani chukua, haya mafuta bwana ukafanye kazi ya kuwaleta wengi wakawe wanafunzi wangu lakini wasijue mimi ni baba wa uongo na wewe uwe muongo sana ninakupa upako na usemi wa uongo ukisema tu watu wa kukubali wa kuamini nimekupa huo upako. Unajua wanadamu wanapenda vitu sana ninawafunga mwenyewe na kuwateketeza mwenyewe maisha yao halafu ninaweka tena hiyo nguvu hapa kwenye mafuta, wakija wakiyagusa tu mambo yanafunguka wanaona YESU amefanya kumbe nimewateka kekundu. Sasa habari imekwisha damu ya YESU ikusafishe kwa neema yake. Amen.
SALA YA TOBA:
MPOKEE YESU SASA. SEMA BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA UNISAMEHE PALE NILIPOTUMAINIA MAFUTA AU STIKA AU VYAKULA AU UPAKO WA AINA YEYOTE ILIYOTOKA KWA SHETANI NIKIDHANIA IMETOKA KWAKO, PALE NILIPOACHA KULIAMINI JINA LAKO, PALE NILIPOPENDA VITU VYAKO BADALA YA KUKUPENDA WEWE, NINAOMBA UNISAMEHE. NAOMBA UANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NA KULIFUTA KATIKA KITABU CHA HUKUMU KATIKA JINA LA YESU AMEN.
PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.
SALA YA TOBA:
MPOKEE YESU SASA. SEMA BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA UNISAMEHE PALE NILIPOTUMAINIA MAFUTA AU STIKA AU VYAKULA AU UPAKO WA AINA YEYOTE ILIYOTOKA KWA SHETANI NIKIDHANIA IMETOKA KWAKO, PALE NILIPOACHA KULIAMINI JINA LAKO, PALE NILIPOPENDA VITU VYAKO BADALA YA KUKUPENDA WEWE, NINAOMBA UNISAMEHE. NAOMBA UANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NA KULIFUTA KATIKA KITABU CHA HUKUMU KATIKA JINA LA YESU AMEN.
PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.