Pages

Friday, February 27, 2026

KUVUNJIWA NA KUBOMOLEWA MADHABAHU ULIZOJENGEWA NA WACHAWI AU UKOO.

BWANA YESU ASIFIWE !

Madhabahu ni nini?

Madhabahu, ni mahali ambapo mtu anafanya sala au anatoa sadaka na kwenda kuongea na MUNGU au shetani; na ili MUNGU afanye kazi, anashirikiana na madhabahu, shetani pia hushirikiana na madhabahu ili afanye kazi. Wanadamu wengi wamekuwa waovu, wamekwenda kwenye madhabahu za shetani. Na hizi madhabahu za shetani zimekuwa zikiwatesa wao na ndugu zao, zikaenda kuwatesa hata watu wasiofahamiana nao, waki baki kuteseka na hii dunia. Hii ni kwasababu ibilisi amepita katika madhabahu na kuwatesa. Madhabahu ulizojengewa na wachawi, miungu au wanadamu ili wakupoteze, zinakwenda kuvunjika.

Yeremia 1: 10

10  Angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa na kubomoa, na kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda.”


Utukufu wa shetani ukapate kuteketea katika maisha yako, utukufu wa MUNGU ukapande. kuharibu na kuteketeza uovu wowote uliotokea au utakao tokea ili kupingana nawe MUNGU. Na kusihi Bwana uende ukavune na kujenga watoto wako, neno lako na uweza wako Katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti.


Malaki 4:3

3  nanyi mtawakanyaga waovu, maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu, katika siku ile niifanyayo, asema Bwana wa majeshi.”


FAHAMU, MADHABAHU GANI IKO JUU YAKO AU INAYOTEMBEA NA WEWE?

1. MADHABAHU ZA KIKANISA, AMBAZO NI KATIKA ROHO ZIMEJENGWA NA SHETANI;

Hizi lazima tuzibomoe kwasababu ndio chanzo kikubwa cha kutesa watoto wa MUNGU. Mchungaji anakuwa amepewa madhabahu na majini, miungu katika hali ya uchawi, atawachunga wale watu na kuwateketeza wasifike mbinguni. Hii madhabahu ya kipepo ni ya kuwatesa wanadamu. Viongozi wao; wainjilisti, manabii, wachungaji, wote ni wakipepo.

2. MADHABAHU YA KUTENGENEZEA, KUTUPIWA, KUJENGEWA;

Unajengewa usiwe na biashara, kufanywa ufunge duka au hoteli, kufanya bidhaa ziharibike ufilisike, hizi zote ni madhabahu zinatumwa na maelekezo. Unaweza kuta wamemwaga viwembe, viuzi katika eneo lako la kazi, hizi ni madhabahu za kukutesa.“Unapokuwa na Bwana YESU haijalishi wataziweka hizo madhabahu, hawatafanikiwa katika jina la YESU. Natangaza zianze kuondoka zikamrudie aiyekuwekea au kukutumia huo uharibifu.” Ukiona mtu ana mwaga mwaga vitu vya ajabu nyumbani kwako, ina maana ameshaiba kile kizuri, kwahiyo amekuja kuweka kibaya. Ama amekuja kufunga hapo kwako ili yeye akafanikiwe, akainuliwe, akapate vyeo, wengine wasipate. Anapodondosha kitu ni ili faraka itokee, roho ya mfilisi, unakuta wadudu wanatembea ndani au anakuwekea madhabahu katika mwili, unahisi vitu vinakutembelea usivyo viona.“ Katika jina la YESU alivyo vipanda vikamrudie yeye na vingine vipate kuteketea.” Ili mchawi akome, asirudie, mdhibiti!
Usiseme tu MUNGU nakuachia wewe, hapana! hapa tuko katika vita vya kiroho, haijalishi ni wazazi wako, au ni mfalme, ni boss wako au mume wako, MUNGU yeye anatandika, kwasababu uchawi ni kitu kibaya na ndicho kinaweka uadui kati ya wanadamu na MUNGU.

3. MADHABAHU ZA KIMAPOKEO;

Hii madhabahu hushirikiana na madhabahu ya kuzimu, ndomaana unasikia kuna injili ya namna nyingine. “Hii injili ya namna nyingine imetoka wapi?” Injili ya namna ya kishetani, kuabudu kishetani, kusali uchi, watu kubatizwa kwa kikombe, ni injili ya madhabahu ya namna ingine sio ya Mbinguni. Ubatizo wa kikombe; siyo wa madhabahu ya mbinguni. Eneo la kubatizwa linatakiwa liwe na ushirikiano na muumbaji Mwenyezi MUNGU. Ambayo ni mto utembeao, ndomaana unaskia kijito cha utakaso. Maji ya kikombe, kisima, beseni, vyote hivyo siyo kijito cha utakaso! Bali inashirikiana na kazi ya mwanadamu. MUNGU katika tendo la kubatiza anashirikiana na uumbaji wake mwenyewe. MUNGU utukufu wake umrudie yeye mwenyewe katika jina la YESU. Hivyo, watu wengi hawajabatizwa, wamedanganywa. Kuna wahubiri wengi unawaona wanatenda miujiza, ila utashangazwa ile siku ya mwisho, mambo mengi waliyofanya na Umaarufu ndipo YESU atakaposema huyu siyo mtumishi wangu! Zile kondoo siyo zangu, haijalishi mpo maelfu, piteni kushoto katika ziwa la moto.

4. MADHABAHU ZA KUPAA AU KUSAFIRI KWA UNGO;

Usione mtu anapaa, ni nguvu gani zinafanya mpaka anapaa? Hizi ni madhabahu zingine, hutumia fisi kama usafiri wao, zinakuwa zipo zinaishi ndani ya nyumba za watu. Hizi ni madhabahu za kichawi zinazotesa wana wa MUNGU, zingine hufanya kazi usiku tu. Unakuta wanyama mbalimbali; paka, mbwa, panya, ndege, mbu, wanapita mahali popote, kumbe ni mtu yumo ndani yake. Hizi zote ni madhabahu, “ Katika jina la YESU, hawa wanaokuja hivi ni wezi, wanaiba vitu. Wapate kuteketea, wavunjike katika jina la YESU.”


5. MADHABAHU ZA SIMBA AU CHUI;

Hizi madhabahu zinakuwa kwa watu, zinakuwa zinawatawala wengine, wana waogopesha, zikiwatisha. “ Ninazivunja, yuko simba wa Yuda atetemeshaye, angurumaye, akateketeze katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti.”


6. MADHABAHU ZINGINE NI NYOKA, WADUDU;

Zinaingia nyumba za watu, zinakaa kwako, zinaangalia riziki zote, na kufunga riziki na kupeleka kwa yule aliyeileta. Zinazunguka hata kwenye mifugo, vitu vinakufa unawaza vimekufaje kumbe walituma nyoka, paka, sisimizi, panya. “ Natamka, wakafe katika jina la YESU na kama kuna sehemu yeyote vitu vyako vimekufa vikafunguliwe wavunjika katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti.”


7. MADHABAHU YA POMBE;

Watu wanashindwa acha pombe, kwasababu wameshakufanya taira. Wamekuchukulia vitu vyako, nyota yako, lazima wakuachie matatizo. “ Zivunjike katika jina la YESU.” Unaweza kuta mtu anahitaji cheo flani; udirector, mkurugenzi au amiliki mali flani, awe maarufu, mwanamziki au mchezaji mpira. Ile madhabahu itaenda kuiba vitu vya watu, wanakuwa wadhulumaji, wana madhabahu juu yao. Hawa ni adui wa Bwana YESU na MUNGU, haijalishi unaheshimika ila kwa MUNGU wewe ni adui na utalaaniwa. Baadhi ya shule na vyuo unaona zinanyayuka na kuvuma, kumbe wanaibia watoto nyota, wanabaki boksi, wao wakisonga mbele. Ni rahisi sanaa mashule na vyuo kukuibia kwasababu tayari shule ina majina yako yote matatu na tarehe na mwaka wa kuzaliwa. “ Katika jina la YESU, MUNGU alikupa mtoto mwenye akili, kama alipita katika maeneo hayo, katika jina la YESU hizo madhabahu zenye shule za kipepo, sema zianguke, zitekete. Navunja kusudi hilo kwenye ulimwengu wa roho na mwili. ” Mwizi wa kichawi wa kiroho hana huruma, ataiba mpaka utumbo, mpaka pumzi, maana ndani yake, majini, mapepo yana vuta vitu vyako.“ Navunja kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti. ”


8. MADHABAHU YA KUZIKA BIBLIA;

Watu wanazika biblia kwenye nyumba zao wakati wanajenga, zile nyumba zinakuwa na madhabahu ya miungu ya kuuwa neno la MUNGU. Watakao kuwa hapo, hawatakuwa kiroho. “ Ninavunja kila mahali katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti.”


9. KUNA WATU WAMEJENGEWA MADHABAHU ZA MATESO;

Inakuwa wewe ni kuteseka, kila kitu tu ni kuteseka, ukiamka mateso, mahangaiko, hizo ni madhabahu, haziishi hata ukiomba na kuomba. Kitu kilichojengwa bila kubomolewa kinakuwa bado kiko pale pale! Maombi ya kuomba ni tofauti na maombi ya kubomoa, hayo yanatakiwa ya bomolewe katika jina la YESU maana walipanda katika roho, haijalishi walikutupia vitu, iko damu ya YESU na wako malaika wake wa kubomoa.

10. MADHABAHU ZA KIGANGA;

Hawa waganga wote wana madhabahu za shetani. Wapiga ramli, wasoma nyota, wote.

11. MADHABAHU ZA KIKABILA AU UKOO.

12. MADHABAHU ZA KITAIFA KWA TAIFA LAKO KWA JINA LAKE;

Kila taifa kwa jina lake linashirikiana na jina la taifa hilo lilopo kuzimu katika kutesa raia waliopo katika taifa hilo; kuwashikilia kila mwanadamu katika taifa lake. Hii inamaana kila mwanadamu ametoka katika taifa, na kila taifa kuna madhabahu ambayo iko kuzimu kwa jina la taifa hilo katika ulimwengu wa roho. “Wewe unayepata ujumbe huu, ukapate kutolewa leo, katika jina la YESU, ukapate kufunguliwa akili yako na ufahamu wako. ”Lazima ujivunie kuwa na madhabahu ya YESU, jivunie kuwa na YESU, hawata kuweza, watajipanga, watapanguliwa, watavunjwa, watabomolewa, na wewe utapita katikati yao, YESU atapita katikati yao.


13. MADHABAHU ZA KUIBA UNYAO;

Watu wanakanyaga tu chini, watu wanaiba unyao, zitavunjika na aliyefanya atavunjika!


14. MADHABAHU YA KUIBA SAUTI;

Hata ninapo zungumza hivi wako wanaotaka iba sauti kipepo ili akizungumza aonekane kama Nabii. Hiyo madhabahu ivunjike katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti.

15. MADHABAHU YA KUVAMIWA NA KUIBIWA;

Yamkini, kuna mtu anayefaidika kwenye nyota yako, ile bidii yako, inawezekana ni rafiki yako au mzazi au hamjui. Anakuwa hapendi mafanikio yako, lazima akutumie jini au mfilisi ili upate kukaa kituo kimoja, yeye afanikiwe. “ Nina ziharibu katika jina la YESU, nazivunja, nikizibomoa, wachinje mbuzi, wakarenew imekuaje biashara zake zinaendelea (wewe simama imara). Nazivunja hizo madhabahu, ziteketee. Nina amuru katika jina la YESU. YESU akasema pepo nenda kule wakaenda nguruwe nao walienda kwenye maji, na mimi naamuru rudi huko ukatende yalio kusudika kufanyika kwangu, yakamtese mpaka ajue mimi ni mwana wa MUNGU nime okoka.”

16. MADHABAHU ZA DHAMBI;

Kutenda dhambi imekuwa kama kawaida, imekuwa tabia bila hofu, ataenda kanisani bila hofu ya MUNGU. Hizo ni madhabahu, akija kanisani ataketi kiti cha mbele huku kiunoni ana irizi, ameua ndugu na marafiki, ametoa watu kafara, lakini anasema anakuja kanisani kutoa sadaka zake. Wengine wakipanda gari wanaendesha bila viatu, nyumbani wanalala chini, yote inakuwa ni maelekezo ya madhabahu. Mwingine, madhabahu inamwambia zini na watoto wachanga, zini na kichaa, ili akapate kuinuliwa lakini wanainuliwa kishetani. Nakusihi mpe YESU maisha yako, kwanini wakataa madhabahu ya wokovu? Ingawa wewe ni mkristo lakini hujaokoka, huna madhabahu ya Mbinguni! Taka Madhabahu ya Mbinguni katika Roho Mtakatifu, na ili uwe wa mbinguni cha kwanza okoka, Roho Mtakatifu atakusajili katika jina la YESU KRISTO atakuongoza na asipungue, aongezeke.


SALA YA TOBA :

SEMA; BWANA YESU NIMEKABIDHI MAISHA YANGU MIKONONI MWAKO, UANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA. NINA MKATAA SHETANI NA MAMBO YAKE YOTE KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI. AMEN.


PROPHET HEBRON WILSON KISAMO