Pages

Wednesday, February 5, 2025

TOFAUTI KATI YA MASADUKAYO, MAFARISAYO NA WACHUNGAJI!

 BWANA YESU ASIFIWE!


Nitawafundisha tofauti kati ya Mafarisayo, Masadukayo na Wachungaji, nikisema Wachungaji namaanisha Nabii, Mitume, Wainjilisti na hata Waalimu. Nitafundisha tofauti lakini pia jambo la kujiuliza ni kwa nini zamani hapakuwa Wachungaji? Hawaluwepo watu wanaitwa Mitume, Wainjilist wala waalimu kwa ajili ya neno la MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE, neno la MUNGU lina mpango wake na mipango yake aliloiandaa MUNGU, na kwa kujua na kutokujua dunia sasa hivi kwa kiwango kikubwa kinaongozwa na Mafarisayo na Masadukayo kwa kivuli cha kujiita Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti na Mwalimu.


Mathayo 23:22-23

Wahubiri wa kipindi kile walitafuta namna ya kumtega BWANA YESU ila jambo la kuuliza wangekuwa na MUNGU huyo huyo mmoja, je wangemtega?? Japokuwa walijaribu walishindwa kumtega BWANA YESU.


Marko 8:14-15

Kwenye hili neno anatajwa Herode. Herode alikuwa ni mfalme, yamkini hata sasa kuna wafamle wanaoshirikiana na Mafarisayo na Masadukayo kwa kupinga injili ya kweli, lakini nawaambia Herode hakufanikiwa chochote kusudi la MUNGU ni YESU liliendelea pale pale, Mafarisayo hawakufanikiwa YESU alipita pale pale. BWANA YESU ASIFIWE! Ninaposema Mafarisayo na Masadukayo hawa ni watumishi wa dini waliokuwa wanajishirikisha na mambo ya siasa, ni watu ambao wapo kwenye kivuli cha injili ambao wanapenda madaraka, wanapenda kunyenyekewa, wanapenta utukufu, na sasa hii roho ya Mafarisayo na Masadukayo ndo imesambaa dunia nzima na imeingia katika zile huduma tano alizozileta BWANA YESU, YESU hakuagiza Mafarisayo wala Masadukayo wawapeleke watu mbinguni na shetani ni mjanja sana akapita hapo hapo; hao wanampenda MUNGU na yamkini hawajui akawaingizia roho ya Mafarisayo na Masadukayo kwa hiyo Mafarisayo na Masadukayo wamejaa tele katika dunia hii kama kipindi kile walivyokuwa wanaongoza mahekalu na sasa wametapakaa na wana waumini wa Kifarisayo na Sadukayo kwa kujua na kutokujua na sipo hapa kwa ajili ya kumsema mtu bali nipo hapa kwa ajili ya kusema kweli ya neno la MUNGU. YESU alichukiwa na Mafarisayo na Masadukayo kwa sababu YESU alisema kile ambacho BABA yake alimfundisha akawafundishe wanadamu; na wale waliokuwa na yale mambo walimchukia YESU ila hawakumchukia YESU bali walimchukia MUNGU, kumtega YESU walimtega MUNGU, MUNGU hategeki! Yamkini wewe unampenda MUNGU sana lakini wewe ni Sadukayo au ni Farisayo.


Luka 4:16-21

Mafarisayo na Masadukayo walimpinga YESU kuanzia pale hekaluni, wakamfukuza pale madhabahuni na leo hii kweli yake inafukuzwa madhabahuni, haitakiwi na hao wasioitaka wanajiita Maaskofu, Mitume, Wainjilisti, Waalimu, Wachungaji na Manabii saa kama ni Manabii alioanzisha YESU, ni Mitume alioanzisha YESU kwa nini wamkatae YESU? Kukataa haya mambo ni kumkataa BWANA YESU. Kipindi kile walimfukuza YESU madhabahuni na leo hii kuna wanaomfukuza YESU madhabahuni, neno lake la kweli halitakiwi madhabahuni na leo hii kuna roho ambayo ipo inayokataa mambo ya YESU sawa sawa na kipindi kile alipokuwa hapa duniani na hiyo roho inatenda kazi ndani ya watumishi ambao ndani yao kuna roho ya Mafarisayo na Masadukayo maana Mafarisayo na Masadukayo wapo kiroho ila wanatenda kazi ndani ya wanadamu; wachungaji, wainjilisti, mitume, manabii, wachungaji humo humo ndani yao na wasiseme Mafarisayo na Masadukayo walikuwa wabaya wakamuua YESU wakati wapo baadhi leo hii wanaomuua YESU pia. Kumuua YESU ni kubadilisha neno la MUNGU, kuombea watu kwa kudai pesa hao hawanatofauti na Masadukayo na Mafarisayo tena wana roho mbaya juu ya wanadamu. Tabia ya Mafarisayo na Masadukayo ni kufanya yao kazi ya MUNGU ni kwa michango, kuchafua nyumba ya MUNGU kwa kufanya Harambee, YESU alikuta wakifanya hivyo hekaluni akawafukuza lakini leo hii yamerudishwa; anatajwa lakini matendo ni yale yale ya Mafarisayo na Masadukayo.


BWANA YESU ASIFIWE!

Mafarisayo na Masadukayo wanaamini katika wafu, hawaamini ufufuo YESU aliofufuka. Hawaamini habari ya wokovu wanajikita zaidi katika siasa na madaraka, hawaamini habari ya kunena, wanasema miujiza hakuna lakini YESU aliyaleta! Ndo maana mahali pengine walisema YESU ni pepo na pengine walisema yeye siyo Malaika. Leo hii kuna makanisa hawaamini kuwa watu wanaombewa na kuponywa hao ndio Mafarisayo na Masadukayo na msifikiri waliisha kule Israeli, bado wapo katika kila bara, kila mtaa, kila nchi, na kwa lugha nyingine hawampeleki mwanadamu yeyote mbinguni, kwa lugha nyingine hawafanyi kazi na MUNGU na kwa lugha nyingine hawapo katika ufalme wa MUNGU ni ufalme mwingine. Hata kifo cha YESU kilisimamiwa na Mafarisayo na Masadukayo; alifufuka bado maaskari walipewa pesa kwenda kusema uongo mkubwa sana; walisema hajafufuka ameibiwa, ili anza kwa Mafarisayo na Masadukayo, walifikiri kazi walioifanya walifanikiwa lakini ilikuwa mpango wa MUNGU YESU afe na afufuke.


Katika utendaji kazi ya Mafarisayo na Masadukayo wao wanachukua utukufu wa MUNGU, mfano wanaposamehe dhambi za wanadamu; mchungaji anasema nakusamehe dhambi zako, mwinjilisti anasema nakusamehe dhambi zako, Nabii anasema nakusamehe dhambi zako. BWANA YESU ASIFIWE! Hakuna tofauti na wakati ule watumishi wengi baadhi yao wanapenda sifa, sifa ni za MUNGU, Utufuku niwa MUNGU. Hawa hawawezi mrudishia MUNGU utukufu maana mungu wao ni mungu wa Mafarisayo na Masadukayo ila wamejificha katika kifuniko ya kujiita Mchungaji, Mwinjilisti, Mwalimu, Mtume, Nabii. YESU aliwakuta Masadukayo na Mafarisayo lakini YESU alileta nini sasa? YESU alijua kuwa Mafarisayo na Masadukayo siyo kusudi la MUNGU, BABA yake alimpa maagizo kutoka mbinguni na mimi leo naziletesha upya kama anayonifundisha kwa ajili ya mataifa yote kwa sababu Mafarisayo na Masadukayo wakaua ile injili ya kwanza, ndo maana leo hii watu wengi ni wakristo lakini hawataki kuokoka, wanaamini kuwa mkristo inatosha kwenda mbinguni, unakuaje mkristo bila kuokoka kwanza? Utakuaje mkristo bila kumpokea Kristo kwanza? Utakuaje Mkristo bila kuandikwa katika kile kitabu cha ukoo wa YESU mbinguni hapa Mafarisayo na Masadukayo hawataki na hawataki kwa sababu wapo walioshikwa na wapo ambao hawajui, na Mafarisayo na Masadukayo kutenda kwao kazi ni kwa mapokeo ya wanadamu biblia inasema watu hawa wananipenda kwa midomo lakini wanafundisha mapokeo ya wanadamu. YESU alikataa mapokeo yao alifuata ya BABA yake na sisi tunatakiwa kuyafuata ya BABA yake mwenyezi MUNGU. Sasa nikuulize unamtaka mwanadamu ambaye siku zake ni miaka 40, 60 anakufa hakupeleki popote, ameumbwa na huyo anayemuua, anayeongea na uhai wa MUNGU huyo. Shetani ameleta naye kufundisha, YESU alisema watakuja waongo wakitumia jina lake na kipindi hiki waongo ni wengi wakijipenyeza kwenye biblia, napenda nikuambie shetani ana biblia, anajua kila mstari, ndo maana alimwambia YESU jitupe, YESU akamjibu imeandikwa usimjaribu BWANA MUNGU wako, YESU alijua neno la BABA yake lakini shetani hapo hapo anataka achomeke ya kwake ili kuwateka watu. BWANA YESU ASIFIWE!


Utendaji kazi ya Mafarisayo na Masadukayo wanatumia uchawi kwa hiyo usishangae siku hizi kuna watu wanamiujiza wa kipepo. Wanaombea watu kwa kudai pesa ndo hao. Imeadikwa utoapo sadaka yako kulia wala kushoto isione, leo hii unaambiwa uandike jina na kiasi hawa ndio Mafarisayo na Masadukayo katika ulimwengu wa roho, si Nabii, si Mtume, si Mchungaji, si Mwinjisliti, si Mwaalimu shetani anajua vikoba vyake kama ulikuwa haujui uelewe sasa Nabii Hebron ametumika hapa kunieleza ili ukweli niujue. Ila wanadamu wana shida mmoja ya watanionaje, watanielewaje, kumbuka ukifa utazika mwenyewe saa unachomwa utakuwa mwenyewe hakuna watanionaje, badilika mrejee BWANA YESU uokoke. Mafarisayo na Masadukayo hawaendi mbinguni ila pia hawawezi kujiita kwa majina hayo kuna namna nyingi ya kujificha na nakufunulia. BWANA YESU ASIFIWE!


Waefeso 4:10-11, 14-16

YESU alileta huduma zake tano ili kukamilisha mwili wa Kristo. Alileta huduma tano akizifundisha zifuate mambo yake, hizo huduma ni viungo kwa ajili ya kukamilisha mwili wa Kristo, mwili kuwa imara. Lakini kuna jambo nataka nikufundihse hapo, hawa Mafarisayo na Masadukayo wakaingilia hizo huduma wakaleta huduma inaitwa Askofu (Bishop), YESU hakuleta hilo jambo, Askofu ni huduma ya 6 na kama ni 6 ina maana namba 666, sasa hao ni nani kumsahisha YESU? Tukija kwa Mafarisayo sasa, wanakwenda kwa mapokeo ya wanadamu, hizi huduma 5 ziliachiliwa roho mtakatifu (Matendo 1: 6); Biblia inasema mtajazwa nguvu ambaye ni Roho mtakatifu haikusema mtajazwa Askofu, ila hizi huduma tano kwa asilimia kubwa kwa baadhi ya watumishi zinaendeshwa na roho ya Askofu na siyo roho mtakatifu na ndio maana utaona hizi huduma tano kwa asilimia kubwa zimekuwa na uchawi, zimekuwa na unyang'anyi zimekuwa na kubadilisha neno la MUNGU na ni kwa sababu chanzo chake ni kuweka neno Askofu. Roho mtakatifu akawekwa pembeni akawekwa Askofu. Kama ni Askofu YESU angekuwa ni Askofu, kama ni Askofu angekuwa ni Petro; hakuna mtumishi aliyekuta kiwango cha Petro, hakuna aliyepita kiwango cha Mathayo mpaka sasa lakini si Askofu. Kiongozi ni roho mtakatifu, na alipokuja walijazwa nguvu, wakaendelea na wakaendeleza kazi sasa baada ya YESU kuondoka na wanafunzi wake kuuwawa wakaongeza hiyo huduma ya Askofu, hiyo ni roho ya Mafarisayo na Masadukayo, kupenda madaraka, kujikuza na hata leo hii watu hutafuta Uaskofu kwa kulogana, kwa kupigiana kura kwa kuuana ili tu mtu aheshimiwe; uheshimiwe na wanadamu wakati MUNGU anakuona wewe ni takataka, kama ulikuwa haujui nakujulisha sasa!!


Kwa neno Askofu hata kama anahuduma nyingine tayari analaaniwa na utapokea maroho na Roho Mtakatifu hana nafasi kwako hata kama unampenda MUNGU, ijue kweli sasa ili kweli ikuweke huru. Mmoja ya tabia ya Mafarisayo na Masadukayo ni wanapenda kusali sala ndefu wakifikiri wanasikilizwa na MUNGU lakini wengine hawajui. Tabia zingine ni kujiona wao ni Mungu, Nabii anajiona yeye ni Mungu, mwingine anaona anauwezo wa kusamehe watu sasa ukiona hivyo kwa MUNGU wao siyo wachungaji bali ni Mafarisayo na Masadukayo na shetani anasema hawa ni watu wangu. Kuna Masadukayo wa aina mbili; kuna wa kimwili na kuna wa kiroho; kimwili kuna wahubiri wamesimama na biblia ila wanasema hakuna kuokoka, wanabatiza tofauti na Ubatizo wa YESU wa maji mengi, wanabariki watoto wakubwa badala ya watoto wadogo tofauti na neno, huu ndo Ufarisayo na Usadukayo. 


Mafarisayo na Masadukayo wa kiroho sasa ni Nabii, Mtume, Mchungaji Mwinjilisti, Mwalimu wanajiita kwa hizo huduma kimwili ila kiroho ni Freemason, ni mwizi wa pesa, anafanya kazi ya kanisa kwa kukopa benki wakati MUNGU yeye anasema niulizeni, niiteni tena anasema yeye siyo MUNGU wa kuchajiwa riba hayo ni mambo ya wanadamu kwa hiyo wanadamu kwa hiyo wanadamu mnapotoa sadaka hapo hambarikiwi maana hamtolei MUNGU bali mnamtolea miungu na kwenye hayo majengo MUNGU hata kaa aingie maana ni kichafu cha shetani na kitu kichafu cha shetani hakitakasiki. Unaweza uaksikia Nabii anaitwa mungu anaitwa yesu au Mtume anaitwa mungu anaitwa yesu hao ndo Mafarisayo na Masadukayo wameingia kwenye kanisa, na hizo roho zina nguvu na hizo roho zinatawala na hizo roho zinatiisha zikitumia jina la YESU, mnajikuta mkoo kule kule kwenye mambo yaliyotendeka Israel wakati upo nchini mwako, roho zinatembea.


Mafarisayo na Masadukayo asili yao ni dini na dini kazi yake ni kumpinga YESU, iweje YESU alijitambulisha "mimi Ndiye" ila wakamtaka kumtupa na ndivyo ilivyo siku hizi, wanatoa vya YESU wanakufundisha cha mwanadamu. Unaweza ukakuta mwimbaji anasema ameokoka lakini kiroho yeye anaimba kwa kutumia uchawi au maagano tayari huyo ni mwimbaji wa kidasukayo na anazidi kupoteza watu kupitia kuimba kwake, ndipo ule mwisho atasema Bwana nilikuimbia nakupenda sana na ataambiwa Sikkukujua. Sala za Mafarisayo hazisikiki kwa MUNGU wala hazipokelewi na ndipo waling'ang'ana kumng'oa BWANA YESU ila ilishaandikwa kuwa atakufa na kufufuka. Kama umewekewa mkono na Mfarisayo au Sadukayo na kupakwa mafuta umepokea mafuta ya Mafarisayo na Masadukayo na siyo ya YESU.


Kazi ya wachungaji ni kukemea mabaya kwa kila taifa, kila eneo, siyo kuwa mwana siasa na kujiunga na chama kimoja. Ukijiunga kwenye siasa tayari unakuwa na ubaguzi na kugawanya watu wakati mchungaji yeye ni kwa ajili ya watu wote. Unaposhiriki siasa unaharibika hata kama ni mtumishi wa MUNGU unaharibika, kile kitu ambacho MUNGU aliweka ndani yako kwa ajili ya kuongoza watu na kuwapeleka mahali pengine kinatumika na shetani. Wewe waombee wana siasa washauri na siyo kujiunga kwenye siasa, hauwezi tumikia mabwana wawili. Kwenye siasa utasema uongo, kwenye siasa utatukanwa, ni YESU anatukanwa si unajua siasa ni mchezo mchafu ina watu wake, ni karama pia MUNGU amewekea watu ili mambo ya mataifa yaende ila siyo Wachungaji mnaingia huko. BWANA YESU ASIFIWE! Ukiwa kiongozi ongoza watu kwenda mbinguni, kama ni siasa wewe washauri siyo una kadi, YESU ana kadi ya chama chochote?! Ukiwa na chama tayari hilo ni doa mbele ya Mwenyezi MUNGU. Siyo uchukie vyama; vyama vipo na vitakuwepo lakini wewe kama mchungaji hupaswi kuwa na chama maana kwanza utaonekana mbaguzi katika watu unaowaongoza, hutakiwi kuwa na upande mmoja, hutakiwi kuonea, unatakiwa kusimama kwenye haki. BWANA YESU ASIFIWE!


YESU alileta hizi huduma tano akaacha maelekezo yafuatwe, sasa walipoua wale mitume walijua wamemaliza ila MUNGU ana akiba zake wapo watumishi wa MUNGU wa kweli na wataendelea kusema kweli na watavunja vunja kazi za shetani ikiwamo mimi nikiwa mmoja wapo nitaendelea kuvunja tu misingi ya Mafarisayo na Masadukayo ili wanadamu wapate kupona, mimi nimejitoa sadaka kwa BWANA YESU kwa MUNGU kwa dunia kwa ajili ya injili Neno lake, ninajua nina ahadi ya neno la BWANA. Na wako waliojitoa sadaka kwa shetani kuhakikisha mapokeo ya wanadamu yanatapakaa kila mataifa; kwani Herode si aliungana na Mafarisayo. Inawezekana hata kuna Mafarisayo kwenye nchi mbali mbali wameungana na Herode ndo watawala kuhakikisha wanaizima injili, injili haizimiki utajizima mwenye, unaweza ukadhani unashindana na mtu kumbe unashindana na MUNGU na atakuzimisha hapo hapo halafu utapokelewa na mateso ambayo hayataisha milele. badilika! Furaha yangu ni uokoke. Musa alikuwa na uchungu na watu alitaka waokoke, alikuwa anawaombea rehema kila siku na mimi nakuambia Okoka!!


Leo hii kuna makanisa hawaamini mapepo, hawapigi mapepo, hawaamini miujiza. Hiyo roho ililetwa kutoka Rumi, mmoja wa watawala wa Israel ni Warumi na ndio waliomuua YESU walikuwa watu wa fedha nyingi sana, si vibaya watumishi kuwa na fedha mbona Sulemani alikuwa nayo lakini leo hii kuna watumishi wenye fedha za madawa ya kulevya, kuuza bangi, kuua watu, ujambazi, ujangili, uwizi wa kura. Hujasikia mhubiri anajiita Nabii au Mtume anaungana na mtu anawaambia nataka mkamuue fulani huyo ni Sadukayo na Farisayo; mimba za wamama wote ziharibike hapa kanisani hayo ni mapepo hayo niekufichulia kimwili japokuwa roho yako haijui; roho yako ikajue, roho yako ikasimame! Utaweza ukakuta mahali kuna miujiza na watu wamejaa kanisani lakini wote ni mapepo itakuuma sana na mimi siwezi kunyamaza, ikifika wakati wake nitakufikia popote ulipo. Injili lazima iende mbele! Nilizaliwa mimi nilikuwa Mkristo wa Mafarisayo na Masadukayo sitaki kuokoka mimi lakini najiita Mkristo. Najiitaje Mkristo wakati nilikuwa namkataa yeye ambaye alikuja ili nipate kuokoka. BWANA YESU ASIFIWE. 


Yawezekana wewe umeitwa na MUNGU lakini una vinyago, unajiita Mkristo lakini bado una mambo ya Mafarisayo, una vinyago, unataka kwenda mbinguni na vinyago. Raheli mke wa Yakobo alikufa kwa sababu hakutaka kuacha vinyago, ila sasa haufi kimwili bali unakufa kiroho, ukaache vinyagi hivyo ukampokee BWANA YESU, tatizo ni unaangalia hawa watu watanionaje?! Na napenda nikuambie, adui wa mtu aliyeokoka ni watu wa nyumbani kwake wale ambao wapo karibu sana naye. Angalia Ayubu; mke wake ndo alitumika kumrudisha nyuma lakini Ayubu hakukubali yeye aliangalia mbele tu, angalia mke wa Lutu ni mtu karibu na Lutu, yeye aliangalia nyuma lakini Lutu alisonga mbele. Ibrahim alitoka kwao ila watu wa karibu ndo walikuwa wanamkatalia asiende na kusudi la MUNGU. Mimi ilifika wakati MUNGU alinitenga na familia  mpaka wazazi; siyo kwa sababu nachukia ndugu ila wangetumika kunitoa katika kusudi la MUNGU, na nikakaa mbali mpaka nikasimama ndipo wakasogea karibu maana sasa siyumbi. Siyo kwamba MUNGU anachukia ndugu, hapana, ila sometimes MUNGU anahitaji muda na wewe akufundishe. Mrejee MUNGU, Mrejee BWANA YESU. YESU anarudi na atakaporudi atarudi na gari la moto, hatapanda kwenye gari la mtu hapa duniani na atakuwa na msafara la moto kutoka mbinguni, asije akakuambia mtu kuwa YESU atakuja kupanda gari lake, mwambie mwongo wewe! Pepo! MUNGU anakupenda, okoka sasa.


SALA YA TOBA:

BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZIFANYA KWA KUJUA NA KUTOKUJUA. NAMKATAA SHETANI NA MAMBO YAKE YOTE, NA MAFARISAYO NA MASADUKAYO NAJITENGA NAO ROHONI NA MWILINI NIMEJUA KWELI BWANA YESU NIMEKUPOKEA.


NABII HEBRON WILSON KISAMO