Pages

Wednesday, February 26, 2025

JINSI HEKALU LA SULEMANI WA KUZIMU LILIVYO!

 BWANA YESU ASIFIWE!


Nitawafundisha kuhusu Hekalu la kuzimu lilivyo. Nini maana ya Hekalu? Nani alianzisha hekalu?  Ilikuwa ni ahadi ya mfalme Daudi mtoto wa MUNGU ila yeye hakuweza kulijenga alijenga mwanae aitwaye Sulemani. BWANA YESU ASIFIWE! Sulemani ni jina la Kiaarabu na maana ya jina hilo ni Shalom (Amani) na Sulemani alifanya mambo makubwa sana na alikuwa mtoto wa ajabu katika historia ya Ufalme wa MUNGU na utukufu umrudie MUNGU mwenyewe kwenye kiti chake cha enzi maana ni mapenzi ya MUNGU mwenyewe yalifanyika kupitia Sulemani.

Kama nilivyotangulia kusema nitafundisha kuhusu hekalu la kuzimu lilivyo ila nitafundisha juu ya Hekalu la Sulemani la kuzimu lilivyo? Nani anaishi ndani ya hilo hekalu huko kuzimu. Nilishawafundisha katika mafundisho mbali mbali kuwa kuna Yesu wa kuzimu sasa kama kuna Yesu wa kuzimu basi ujue kuwa kuna Sulemani wa kuzimu. Kama yupo roho mtakatifu wa Mbinguni basi ufahamu yupo roho mchafu ambaye ndiye roho mtakatifu wa kuzimu, usishangae ukisikia kuna BABA wa mbinguni na pia kuna Baba wa kuzimu, wanakaa wapi? Wanakaa katika Hekalu. Watu wengi wanampenda MUNGU ila kwa kujua au kutokujua wanakaa katika Hekalu la Sulemani la Kuzimu na kuna uwezekano wengine walishaunganishwa na Hekalu la Sulemani la kuzimu.


2 Wakorintho 6: 6-18

Biblia inasema pana ushirika gani kati ya nuru na giza? Na watu waliopo katika nuru wanamtaja MUNGU na waliopo katika giza wanamtaja MUNGU na watasema MUNGU ni mmoja lakini nachowaambia yuko MUNGU Mkuu aliyeumba mbingu na dunia lakini kule kuzimu katika Hekalu la Sulemani yuko aina ya Mungu anayeitwa naye Mungu mkuu yeye yupo katika hilo hekalu la shetani. Usione mtu anasema MUNGU MUNGU, je ni wa mbinguni au ni Mungu mkuu aliyopo katika hekalu la Sulemani? Wakati Sulemani anajenga Hekalu kipindi kile MUNGU mkuu wa Mbinguni alikuwepo mule ndani na kuzimu ndivyo ilivyo Mungu mkuu wa kuzimu yeye yupo ndani ya Hekalu la Sulemani wa kuzimu. BWANA YESU ASIFIWE!


2 Wakorintho 4:1

Mungu wa dunia hii ni mungu ambaye ana mambo ya kumpinga MUNGU wa mbinguni. Ukisikia mungu wa dunia hii hayo unayoyafanya mabaya ambayo siyo ya mbinguni au ukayaamini au ukayashiriki ndio ya mungu wa dunia hii lakini simaanishi kwamba wanadamu waondoke duniani, unajua kitu kinaitwa Ulokole kinanichanganya sana kama MUNGU ameweka dunia hii je dunia inakuaje mbaya, MUNGU hajaumba dunia kuwa mbaya ameiumba kuwa nzuri na ukisema ni mbaya unakuwa kama umeona kazi ya MUNGU si salama na akamtuma mwanae YESU KRISTO duniani ili nanyi mkaifurahie na wengi wanaifurahia dunia na kama huifurahii utakwenda kuifurahia; na wale wanaomfuata mungu wa dunia hii wale wanaomfuata anawapa kuifurahia hii dunia maana yeye atawakamata kwa muda mchache, atawatumikisha kwa muda mchache lakini baadae hao watu watakufa, watarudi chini ambapo yupo mungu mkuu wa kuzimu na watachomwa naye moto. Usione hii dunia haifai, inafaa na unatakiwa umiliki na kutawala ukiwa na huyu MUNGU mkuu wa mbinguni. Faida ya kuwa na MUNGU wa mbinguni unatawala, utafanikiwa, utaondoka, hutachomwa milele, utastarehe. IIa wa mungu mkuu huyu wa kuzimu atachomwa, wanaomwabudu watachomwa. MUNGU wa mbinguni anataka watu na mungu wa hekalu la Sulemani kuzimu naye anataka watu na huyu ni mungu aliyejificha sana. 


Anavyosema nuru na giza havina ushirika na nawaambia kuna injili za mungu wa kuzimu na watu wote watamtaja MUNGU ikiwapo ubatizo wa kikombe wanamtaja MUNGU wa mbinguni ila pale unakuwa unamtaja mungu wa kuzimu yuko kwenye ile hekalu. Umebarikiwa kama mtoto mkubwa; umebarikiwa na huyo mungu, unaabudu sanamu uko na huyu mungu. Huyu mungu ana mafungu ya kumi ana sadaka za shukurani, huyu mungu hekalu lake ndilo linafanyika soko, watu hawaokoki wako na mungu wa dunia hii lakini MUNGU wa mbinguni anataka tuokoke sasa hapana ushirika kati ya nuru ambaye ni MUNGU wa mbinguni na giza ambaye ni mungu mkuu wa kuzimu. Yamekuja mapokeo ambaye ni mafundisho ya wanadamu yanatoka huko chini. Kama neno la MUNGU la kweli limetoka juu basi ujue neno la uongo limetoka huko chini sasa kwa ajili ya wale ambao hawataki kusikiliza hawataki kuelewa hao wamepotea. Mmesoma habari za Eliya, Eliya yeye alikuwa hana mali nyingi ila Eliya alikuwa na MUNGU mkuu wa mbinguni japokuwa alikuwa mwenyewe na wale watumishi wa Baali walikuwa ni wengi na walikuwa na mungu mkuu wa kuzimu ambaye hupo katika hekalu la Sulemani kuzimu aliwapa mali sana aliwainua sana hata mfalme akaona hawa watumishi kwa sababu wa mali na ni maarufu basi hao ndo walikuwa karibu na Mungu lakini ilikuja kujulikana ni yupi alikuwa na MUNGU wa Eliya na sasa itakuja kujulikana MUNGU wa watumishi wa kweli na mungu wa watumishi wa uongo na wale wanaomwabudu mungu wa kuzimu ambaye ana waganga ana wachawi ana waaskofu, mitume, waalimu kila mahali na hata wale walioitwa na MUNGU mkuu wakamsaliti basi wanachukuliwa na mungu mkuu wa kuzimu na mtu anakuwa mchawi lakini bado anasoma biblia, ana miujiza, anasema ili upate kuombewa au huduma za kiroho utoe kiasi fulani na wakifanya hivyo mungu wa kuzimu anawatia nguvu hao watumishi wake.


Unawza ukajitoa kujenga kanisa kumbe unamjengea mungu mkuu wa kuzimu la hekalu la Sulemani. Ujenzi wake ni tofauti na ujenzi wa MUNGU wa mbinguni. Yeye anachangisha watu, yeye anakopa hela benki hana nguvu kama MUNGU wa mbinguni anayesema atafungua milango kaskazini na magharibi na mambo yatakwenda huyu ni MUNGU wa mbinguni, njia zake siyo njia za wanadamu wala akili yake na uwezo wake siyo za wanadamu. Inafika mahali wanaona wanaweza kukufanya chochote ila ukiwa na MUNGU wa mbinguni atafanya njia, ndiye aliyekuwa MUNGU wa Musa, walifika mahali kulikuwa na bahari, bahari ikafunguka. BWANA YESU ASIFIWE. Kumbuka Daniel alikuwa na MUNGU wake mkuu wa mbinguni, MUNGU wa miungu wengine walijikusanya ili wamuue ila Daniel alijiamini alifungua madirisha na alikuwa anaomba wala hakujificha baadae aibu aliwakuta wale wanaoabudu mungu mkuu wa kuzimu na kumpinga MUNGU mkuu na inawezekana na wewe unampinga MUNGU mkuu wa kuzimu kwa kujua na kutokujua basi ubadilike ili haya yasikukute asije ule mwisho akasema Hakujui. BWANA YESU ASIFIWE. MUNGU wa mbinguni anasema wanaume wasivae kofia kichwa ni utukufu wa MUNGU, angalie kule kuzimu niliwaambia jinsi lilivyo wanavaa kofia, sasa kwa nini huyu MUNGU wengine wanafanya mapenzi yake, wengine wanafanya kinyume na mapenzi yake na wanasema ni MUNGU mmoja, siyo MUNGU mmoja. MUNGU wa mbinguni amenyooka. MUNGU wa mbinguni yeye hana ushirka na wafu sasa wanapofanya ibada za wafu au kukumbuka wafu ujue hapo ni mungu wa hekalu la Sulemani wa kuzimu ndiye anayeshiriki. Huyu mugnu mkuu wa hekalu la Sulemani wa kuzimu unatakiwa uanze kumbomoa, kumwangamiza. Huyu mungu wa dunia hii anawapumbaza watu na kuwapofusha wasiokoke, mkifa mtaombewa. Mwombe MUNGU uonyeshwe au uone jinsi watu walivyo waliokufa na wapo huko chini. BWANA YESU ASIFIWE. Itafika mahali MUNGU ataipiga hii dunia.


Katika Hekalu la Sulemani kuzimu kuna vitengo vya kuvuruga amani ya watu duniani, kuna vitengo vya makufuru, hicho chumba kimejaa makonokono ukutani kila mahali na hayo ndo makufuru ya kutesa wanadamu na kuvuruga amani kwenye nchi za watu, sasa kama kwenye nchu hamna mtumishi wa MUNGU anayeomba kwa MUNGU wa mbinguni utashangaa watu wanaomba kwa Mungu lakini hali mbaya ina maana ya kwamba hakuna mtumishi wa MUNGU wa mbinguni aliyoko na MUNGU anayeomba.


1 Wafalme 5:1-4

Kwa nini linaitwa Hekalu la Sulemani. Ni kwa sababu lilijengwa na Sulemani na alivyolijenga hilo hekalu ni tofauti na baadhi ya mahekalu yanayojengwa dunia hii hata kama likitwa kwa majina gani, MUNGU aliamuru kusi na kila mahali na ikafanya na ndivyo ikawa na MUNGU akakaa mahali pale. BWANA YESU ASIFIWE. Sasa na Shetani akajenga na la kwake kuzimu na Joka Kuu kwa hiyo kuna hekalu la shetani na hilo hekalu  ndilo linashirikiana na wanadamu sasa na ukisoma neno la MUNGU linasema nyie mnalolichezea hekalu la MUNGU hamjui mnaliharibu? mtaharibiwa? Utaharibiwa kivipi? Unaliita la MUNGU lakini upo na Mungu wa kuzimu. Kazi ya Mungu wa kuzimu ni kuangamiza watu waliookoka, kuwaangamiza kiroho, kuwarudisha nyuma na majeshi yake, In the name of JESUS naamuru yamrudie mwenyewe ninayachoma moto mpaka kuzimu, nachoma maagano yake hata yale yalioko ndani ya watu, sema Amen! BWANA YESU ASIFIWE! 


Katika Hekalu la Sulemani Kuzimu kuna Eloi Sabachthani yale maneno ya Eloi Sabachthani yapo kuzimu. Yapo yale maneno ya koriambasaka saka (maneno ya kunena) sasa ujiulize mtu ana nena ni mhubiri lakini anachukua pesa kwa ajili ya huduma za kiroho hiyo imetoka katika hekalu la Sulemani la kuzimu, yule anayebeba na Hekalu la mbinguni hawezi beba sanamu (Kutoka 20:2-5). Unavyoabudu sanamu unakuwa umemchukia MUNGU bila kujua wakati wewe unampenda MUNGU kumbe MUNGU ameona unamchukia. Unapofuata mafundisho ya uongo unakua umemchukia MUNGU umetengenezewa sehemu ya kumchukia MUNGU pasipokujua lakini unampenda na mwisho unatumikishwa na unatekwa kwa hiyo mateka wengi ni wa shetani pasipokujua na siku mmoja utapotezwa ndio maana unasikia kuna wachungaji wa uongo, manabii wa uongo, mitume wa uongo, mwalimu wa uongo, maaskofu wa uongo na hawa ndo wapo kwenye hekalu la Sulemani wa kuzimu na ndio maana ukiwaambia watu waokoke watasema ni uongo, ukisema watu waombewe bure watasema ni uongo, ukisema msiabudu sanamu watasema wale ni wa uongo wamepotea. Kwa hiyo yale ya uongo kwao ni yale ambayo MUNGU wa mbinguni hayataki, yale ya MUNGU wa mbinguni ndio ya kweli lakini hawa wa huko chini wanakuita ni wa uongo. lakini nikuambie, uongo unavunaga chap, ukweli unaendaga taratibu na ukweli unabaki pale pale, ni mtego ambao umetumika kuwaandalia wanadamu mateso makubwa sana kwa kujua na kutokujua.


Katika Hekalu la Sulemani kuzimu wapo wazee 24, wapo kina Esther, Farao, Herode, wapo wale wafalme waliokuwa wanafanya mabaya wapo huko, ile nguvu walikuwa nayo kipindi wanatawala imetoka huko lakini siku kwa siku shetani anaongeza vitu kwenye hekalu la Sulemani maana shetani alikaa na MUNGU na alikuwa anaona alikuwa anachukua na anaweka copy. Wanakuambia unaabuduje kitu usichokiona, MUNGU ukimwona unakufa. Nashangaa makanisa baadhi wanaweka sura ya yule mwigizaji na mawigi kama YESU, huo ni uongo, sura ya YESU hakuna, sura ya YESU ukiiona wewe unabadilika sasa mbona wanakaa na sura ya YESU na hawabadiliki wako na mikuki na masanamu sasa jiulize huyu ni YESU yupi? ni Yesu wa hekalu la Sulemani kuzimu. Wamecopy vingi, mkiimba nyimbo za tenzi na wao wanaimba nyimbo za tenzi hivyo hivyo, mkisema Halleluyah nao wanasema Halleluyah hivyo hivyo nimewafundisha ili mjue, ulinde sana ulicho nacho ukristo siyo sababu ya wewe kwenda mbinguni, bali ni kuokoka. Kuna mapepo makristo hata chini kuna kristo na huyo Kristo ndo anamwaga roho wakristo wasiokoke. 

Kikubwa ni kuokoka na kumpokea BWANA YESU; SEMA BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZIFANYA KWA KUJUA NA KUTOKUJUA NINAMKATAA HUYU mungu mkuu WA HEKALU LASULEMANI NINAJITENGA NA MAMBO YAKE NA HATA SADAKA ZANGU NILIZOZITOA, MAKOFI YANGU NILIYOPIGA NIKIWA KWENYE MSINGI HUO NAJITENGA NAYO. AMEN! 


"NINAIVUNJA MITANDAO YAKE, NINALIBOMOA MILANGO YAKE, NILALILIPUA KWENYE ANGA. NALILIPUA, NALIVUNJA KILA TAIFA, NALIVUNJA KUZIMU, NALIVUNJA BAHARINI, NAVUNJA NJIA ZAO, NAVUNJA MAJESHI YOTE LEO KATIKA LILE HEKALU LINALOKUTESA NAZILIPUA. MAANA HATA UKIMWONA MCHAWI ANAKULOGA ANATOKA KWA mungu HUYO HUYO NAMVUNJA HUYO MCHAWI KWA DAMU YA YESU. HUYO mungu AIACHIE NAFSI YAKO, AACHIE NYOTA ZAKO, AACHIE JINA LAKO, NINAMKEMEA, NINAMPIGA, NINAMCHOMA MOTO, NINAMBOMOA KWA JINA LA YESU NA VITU VYAKE KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NA MWILI NINAPINDUA PINDUA KATIKA JINA LA YESU. AMEN"


NABII HEBRON WILSON KISAMO.