MAOMBI YA
KUINULIWA KIUCHUMI WAKO.
KUMBUKUMBU
LA TORATI 1: 27-28.
KUMBUKUMBU LA TORATI : 15-20
BWANA YESU ASIFIWE!
Mambo yote MUNGU ameandika kwenye biblia ni unabii na hakuna
neno ambalo halitatimia kwa hivyo basu ni lazima kutembea katika nyakati za
kinabii ili lipate kutimia katika maisha yako, lakini wanadamu sasa hivi
wanataka kuona kitu kabla ya wakati wa MUNGU. Yawezekana unataka itokee mwezi
ujao, miezi miwili hapana, YESU alitabiriwa ujio wake miaka mingi sana lakini
si yametimia, na kwako pia yatatimia kwa wakati apendao MUNGU mwenyewe.
Unabii ni kinywa cha MUNGU kwa hivyo basi lazima utimie
kwako. Uko unabii wa kwenda mbinguni na itatokea, uko unabuu kuwa BWANA YESU
atarudi mara ya pili na itatimia, lakini kuna wanadamu wanaosema hatarudi tena
achana na hao, kwako wewe kama kuna jambo unalihitaji kutoka kwa MUNGU na
halijatimia subiria, wakati wa BWANA litatitimia; Ikiwa ni uchumi au maendeleo
yako nitakutamkia leo na litatokea. Neno uchumi una mapana sana, kuna
maendeleo, utajiri, pesa, mali, uchumi wa elimu, uchumi wa ujenzi, uchumi
kwenye ufugaji, kilimo; uchumi ni mafanikio kwenye eneo fulani la maisha yako.
MUNGU toka mwanzo alimpa Adam na Hawa kumiliki na kutawala uchumi, baada ya
anguko shetani akapata kuiba hiyo nguvu ya kumili akawe anaiba vitu vya watoto
wa MUNGU na kuwamilikisha watu wake. Leo nitamwamuru shetani aachilie kila kitu
cha uchumi ambacho amewaibia watoto wa MUNGU ambapo MUNGU aliwapa kumiliki na
kutawala na ni haki yao isipokuwa pale ambapo mtu atakapokataa kumtii MUNGU na
kumsikiliza ndipo hataweza kumiliki uchumi wake atabakia kwenye malalamiko kwa
MUNGU kumbe kosa ni la mtu mwenyewe.
KUMBUKUMBU
LA TORATI 28: 1-14
Huu ni unabii toka kwa MUNGU lakini watu wengi wanataka
kuinuliwa katika uchumi lakini hawataki kuisikia sauti ya MUNGU hii haiwezekani
utahangaika sana, uchumi ni roho ina nguvu yake ndo maana leo hizi nchi maskini
kiuchumi wanaangalia nchi tajiri kiuchumi na kutawaliwa nao; wakiambiwa kushoto
ni kushoto hawakahoi. Usiogope, yawezekana kuna vitu kwako vilikuwa havionekani
vita kwenda kuachiliwa utaviona. Hivyo basi ukitaka kufanikiwa kiuchumi ni
lazima usikilize sauti ya MUNGU na kutii ndipo hapo MUNGU anakwenda kukuinua.
KUMBUKUMBU
LA TORATI 28: 13-15
MUNGU anataka akikuinua usimuache lakini watu wengi wanaona
mafanikio ndio MUNGU, MUNGU hapendezwi na huko jambo kabisa. BWANA YESU
ASIFIWE!
3 YOHANA
1:2; MUNGU anatuita wapenzi. Anataka ufanikiwe kwa hiyo mafanikio
ni uchumi. Mafanikio ni baraka lakini huyu Ibilisi aliiba uchumi akaushikilia
dunia nzima leo hii mimi Nabii Hebron nasema walioiba uchumi wa watu wa MUNGU
au wa mataifa mengine nakwenda kubadilisha kwa jina la YESU. Uchumi ni kama
nyota inaweza ikaibiwa inaweza ikabadilishwa, kuna vitu vitatu vinafanya uchumi
unanyuke, kwanza ni mwanadamu mwenyewe, pili ni MUNGU na tatu ni shetani. Uchumi
maana yake ni maendeleo, kubarikiwa, kuinuliwa, huyo ni MUNGU afanikishaye njia
zako, ainuaye njia zako kuweka vitu vya uthamani ndani ya watu ndio uchumi,
BWANA YESU ASIFIWE! Aliyegusa uchumi wako MUNGU akamshughulikie katika jina la
YESU. Mafanikio MUNGU aliyopanga juu yako wewe na uchumi aliyopanga juu yako
wewe ukafanikiwe lakini hazipo, jipe moyo zitaenda kurudi kama unategemea
uchumi kutoka kwa MUNGU maana kuna wanaotegemea uchumi kutoka kwa shetani ambao
ni wengi na hawa ndio wezi wa uchumi wa wana wa MUNGU na wao hawafanikiwi kwa
kuwa wamechukuliwa uchumi wao.
Ufanye nini basi ili MUNGU ainue uchumi wako kwanza ni lazima
uokoke na kufanya kazi kwa bidii yako hata kama ni kidogo. Mtolee MUNGU fungu
la kumi hata na sadaka lakini kuna mtu mwingine anakwambua mimi nimeshatoa
fungu la kumi basi na kosa ambalo watu wengi hufanya ni pale MUNGU anapowapa
zaidi lakini badala ya kumpa MUNGU kidogo cha haki yake mtu anang’angania na
chote, basi ndipo utakapoporomoka. Ili kufanikiwa zaidi katika uchumi wako
uongezeke, unatakiwa pia kutolea uchumi wako sadala na kuiombea ulinzi. Shetani
anapoiba uchumi au kuua uchumi wengi hulia badala ya kufuata maelekezo. Wengi wanaweza
kuwa na nyota na ndoto kubwa za ajabu lakini ibilisi amefunga uchumi wako. Kinachotakiwa
kufanya ili uchumi wako ufunguliwe mambo mengine ni katika kufunga na kuomba
biblia inatuongoza hivyo. MUNGU anataka ukamilike katika uchumi na ushike mamia
kwa mamia kukua katika uchumi na vita inategemea bidii yako japo ninakuombea.
Watu wengi waliokoka ni wavivu hawajitumi hawataki kufanya
kazi, kufanyia kazi neno la MUNGU lenye linasema asiyefanya kazi na asile. Umeshawahi
kufanya maombi ya kuinuliwa uchumi wako kwa njia ya sadaka? Hawa jamaa wa
shetani wanafanya sana ibada ya sadaka ya kuinuliwa kiuchumi unasikia
wanaangusha mameli, unaskia wanachinja na kutoa sadka ili wainuliwe kiuchumi,
kuna makabila mengi ikifika mwezi wa kumi na mbili wanaenda kwa wazee kutambika
na kutoa makafara kwa ajili ya uchumi.
Kuna aina mbali mbali za uchumi ikiwemo za kiroho na
kimwili. Kama kwenye ulimwengu wa roho uchumi wako umechafuliwa na kimwili
utachafuliwa. Mfano mtu anaota yupo sehemu fulani anafanya kazi lakini kimwili
hafanikiwi, ina maana uchumi wake umechukuliwa na mtu mwingine ni mpaka
urejeshewe na hapo ndipo penye furaha kubwa ya mtu lakini afanikio makubwa ni
kwa BWANA YESU ukiokoka. Nawaombea uchumi wenu ukarejeshwe kama umefichwa, kama
umefunikiwa ukaachiliwe leo katika jina la YESU na hata kuna baadhi ya makanisa
uchumi wao hauko na wakaenda kukopa benki badala ya kujibidiisha badala yake
yanakuwa na laana. Shetani ameingia kwenye uchumi na kuwataka mawakala wake
wauwe ili wapate makafara ya damu shetani anawaongezea uchumi wake. Kuna uchumi
wa kuvalishwa ukichukuliwa unaogopa hata kuendesha magari, hata kuvaa vitu vya
thamani kama dhahabu. Ulichonacho kinatakiwa kiongezeke lakini usipofanya bidii
hakiongezeki na siku ya mwisho utaulizwa.
Liko jini la uchumi ni jini kubwa sana linalopambana na
uchumi wa watu waliookoka ndio maana utaona watu waliookoka wanapambana sana
katika uchumi ulipokuwa kwa shetani anaachilia lakini ukija kwa YESU mtu
anapambana sana ni kwa sababu hili jini linataka kumkatisha tamaa ili amuache
YESU. Utakuta kuna baadhi ya mataifa wanaomba dola kwenye nchi nyingine
hawapati, wanaomba visa kwenye nchi nyingine hawapati ni kwa sababu hizo nchi
zina uchumi mkubwa hazitikisiki hata ziambiwe nini hazitikisiki kwa sababu nchi
hizi zinajibidiisha hazitikisiki. Kuna uchumi uko magereza na kuna uliyofukiwa
cha kufanya ni kufanya bidii utaulizwa amekupa ukamilike. Kuna majini yanaitwa
kwa jina linalotawala uchumi wako unachotakiwa kufanya ni kulipiga hilo jini,
libomoe, liangamize.
Huyu jini uchumi, pepo uchumi, Mungu uchumi akitawala eneo
fulani anatawala na uchumi wa wana wa MUNGU inabidi kuwashughulikia ndipo
utafanikiwa, kwa sababu kazi yao hawa ni kuangalia nani anauchumi mzuri wanaiba
wanawapelekea watu wao sasa usipofanya ibada ya sadaka kwa ajili ya ulinzi wa
uchumi wako ili usiseme utahama ni kwa sababu mambo hayaendi ujue ndio hayo
majini ukiyapiga uyapige kwa jina la mji ulioko na sehemu ulioko wa wilaya,
jiji, nchi, kitongoji chako.
Kuzimu wanataka waiunue marais wao na MUNGU anataka ainue
marais wake hizo nchi waliokata wa MUNGU sasa mambo ni mabaya sana.
Unaweza ukaona pesa hazikai ni hawa wanga wanaoenda baharini
wakiwa uchi ili kuharibu uchumi. Kuna jini linaitwa mkia linakufunga wewe
unakuwa mkia badala ya kuwa kichwa utajikuta haufanikiwi utajikuta unaingia
kwenye umaskini, pia kuna jini linaitwa mashambulizi ya uchumi piga hilo jini,
ukifanya hivyo utafanikiwa wachawi wataona wamekushindwa. BWANA YESU ASIFIWE!
Ukiwa na jini la umaskini litakuwa maskini. Unaweza ukafanya biashara na mtu
kumbe ana majini unakuta anachukua pesa zote anakuachia filisi. MUNGU ni mchumi
mzuri sana hata mvua ananyeshea kwa bajeti hata nchi pia zina bajeti kwa nini
unakuta nchi zikitumia bajeti vibaya zinaenda kwenye nchi zenye uchumi nzuri
kukopa kwao halafu wanapewa masharti magumu hata ya kuuza sehemu ya nchi kwa
sababu ya uchumi mgumu inabidi wakubali ili kupata mkopo kwa hiyo kila mtu
anatakiwa awe na bajeti asiende kwa wachawi kwa ajili ya uchumi mbaya, pesa za
uchawi zina teas, zina masharti magumu walizo nazo hawana raha.
Unapokiri udhaifu mchawi anaiba uchumi wako na kuwauzia
wengine; mfano unakiri kuwa mwaka huu ni wa shida kweli utakuwa wa shida. Ukisema
ndoa hii haifai itakuwa hivyo. Chochote ulichokiri vibaya kwenye maisha yako
itakuwa hivyo inabidi ufute kwa maombi ili usikatishe baraka fulani ficha
usiongelee ili itimie. Kuna mtu anapata kitu anatangaza mpaka mtandaoni
umenunua gari unapost, umejenga nyumba unapost haifai, fanya mambo yako kimya
kimya watu waone wenyewe. Itakupunguzia vita, nimekufundisha ili ujue uamue cha
kufanya utamwona MUNGU.
SALA YA
TOBA:
BWANA
YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZIFNYA KWA KUJUA AU KUTOKUJUA.
NAKUKUBALI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU NAMKATAA SHETANI NA MAMBO
YAKE YOTE NA TABIA ZAKE ZOTE. NAKUOMBA BWANA YESU FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU
CHA HUKUMU NA MATESO UNIANIDKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA
MILELE. AMEN.
NABII
HEBRON WILSON KISAMO