Nawasalimia katika jina la YESU
Tuombe Baba katika Jina la YESU nawaombea watoto wako nguvu ya kupokea neno na kulitendea kazi Naangusha falme zote na mamlaka zote za giza katika Jina la YESU, Bwana YESU anawapenda na anataka kuwafundisha kuhusu kibali.
Neno la MUNGU linatoka katika kitabu cha Matendo 10:35-36, Napenda ujue mwana wa MUNGU utendaji kazi wako utapimwa , maisha hayatafanana na mbinguni, itapimwa jinsi ulivyofan nv d ya kazi ya MUNGU huku duniani mfano unaomba kwa dakika tatu kwa wiki itapimwa, alivyokupa MUNGU siku ya mwisho yatapimwa, utowaji wako utapimwa, unavyohudhuria vipindi utapimwa maneno haya ninayoyasema ya sikilize hata siku ya mwisho yatakuwepo wako malaika wanaoangalia rekodi yako kila siku MUNGU amekuwa akisema na mimi sana kuhusu kibali, tunaona yakwamba kaini uso wake ulikunjamana kwa sababu habili ndugu yake alipata kibali kwa MUNGU kwa sadaka yake, lakini kaini hakupata kibali jambo hilo likamchukiza sana Kaini,kuna aina mbalimbali za kibali,kuna kibali umepewa na MUNGU, kibali umepewa na miungu, kibali umepewa na majini, kibali cha mizimu, pia kuna kibali umepewa na wanadamu mfano, kibali cha kuendesha gari ambacho kinahakikishwa kwamba wewe unafaa, watu wengi leo hii hawana kibali kama kaini,kwa kujua na kutokujua, Habili alikuwa na kibali mbele za MUNGU ndio maana sadaka zake zikapokelewa,sadaka zake zikafika, kaini hakuwa na kibali mbele za MUNGU kwa sababu alitenda mabaya, hata leo hii kuna watu hawapokelewa sadaka zao mbele za MUNGU kwa kujua na kutokujua lakini nataka nikufundishe ili ujue ukapate kibali mbele za MUNGU kwa jua na kutokujua lakini nataka nikufundishw ili ujue ukipata kibali mbele za MUNGU, Tunaona alisema hakika MUNGU hana upendeleo ukitenda haki mbele za MUNGU utapata kibali, kuna watu leo hii wanasema MUNGU ana upendeleo, MUNGU hana upendeleo jiangalie wewe kwanza tenda mema kwake utaona kibali, lakini dunia hii unaweza ukawa unakubalika na watu wenye nguvu za giza siyo kibali cha MUNGU, watu wengi hawana kibali mbele za MUNGU,wewe kama huna kibali mbele za MUNGU ni sawa kama umekufa huwezi kuwa na chochote katika dunia hii.
Kibali ni Roho ambayo MUNGU anawapa wanadamu, leo hii watu wanataka kibali mbele ya wafalme, mbele ya mtajiri badala ya kutaka kibali mbele za MUNGU, ukipata kibali mbele za MUNGU, MUNGU anafanya kibali katika mambo yote kwenye dunia hii, kiko kikabli cha wokovu ndicho kibali kitakachokupeleka mbinguni lakini watu siku hizi wanakatazwa kuokoka nausipookoka hauwezi kufika mbinguni lazima uokoke, kuna kibali na Neema watu wengine kwa sababu ya kutenda mabaya neema inapungua mpaka kibali kinakwisha, Bwana YESU asifiwe! Nitasoma kitabucha Esta sura 5:2, Esta alizaliwa na neema ya kibali cha MUNGU, laikini kuna wakati mambo yalikuwa magumu waliamua kuomba kibali kwa MUNGU kwa MUNGU hawakuomba kwa mfalme, mfalme akageuza kila kibali kwa mfalme, mfalme akamnyenyekea Esta kwa sababu MUNGU alimpa Esta Kibali, Bwana YESU asifiwe! Sana kuna mtu atakuwa anaomba kibali kwa kiongozi wa kanisa badala ya kuomba kibali kwa MUNGU watu hawataki kutafuta uso wa Bwana wapate kibali, wakristo wengi hawana kibali cha kwenda mbinguni, hawana kibali cha kuwa karibu na Bwana Yesu mbinguni wanakwenda wenye kibali na Biblia inasema lazima ulinde neema ulinde kibali hicho,hutakilinda kwa Rungu utakilinda kwa maombi.
Yawezekana kibali chako wewe ni cha kukataliwa,kuchukukiwa, kudharauliwa na hapo ndipo utaona dunia ni chungu kwasababu ya mateso kwa sababu huna kibali cha MUNGU, Nyakati zile za mwisho kitaondoka kibali cha kutubu,kitaondoka kibali cha kulielewa neno hata ukisoma hutaelewa, Biblia ndivyo itakavyokuwa, bali wale wenye neema na kibali cha MUNGU ndio watakaoelewa hata sasa watu hawaelewi neno la MUNGU bali wanaelewa uongo.
Bwana YESU asifiwe! Ukiwa na kibali cha MUNGU hakuna kitakachokuweza angalia mfano wa Esta alikuwa na kibali kwani walimuweza? Hapana Soma Mwanzo 39:21 Yusuphu alizaliwa na neema ya kuwa waziri mkuu na yeye alielewa namna ya kutafuta kibali za Bwana, angalia mfano wa Yusufu alivyopata kibali mbele ya mkuu wa magereza, Mkuu wa magereza alikuwa hamjui yusufu lakini kibali cha MUNGU ndani ya Yusufu kilimfanya Mkuu wa magereza ampe Yusufu kibali. Na hata wewe shetani anajua kabisa wewe utakuwa nani kwa Kibali cha MUNGU alichokuwekea Ndani yako lazima atakuwekea usiku, inabidi uombe kibali mbele za MUNGU.
Inawezekana umeolewa lakini kibali na Neema ya ndoa imechoka unakosa kibali kwa mume wako, umekosa kibali kwa mke wako, yawezekana ni mtumishi, Mchungaji yakupasa uombe kibali machoni pa Bwana, yawezekana ni muimbaji yakubidi kuomba kibali mbele za MUNGU lakini shida iliyoko watu hawataki kuomba kibali mbele za MUNGU, yawezekana unafunga sana na kuomba lakini huna kibali mbele za MUNGU mambo yatakuwa Magumu, mkiwa na kibali mbele za MUNGU hata wachawi wanakuloga vipi.
Mambo yako yatakuwa shwari hawatakuweza, kama yaliyomtokea Yusufu alitaka akalinda neema yake kwa kutafuta uso wa MUNGU. Sasa kuna watu ambao MUNGU anawatoa kwenye ulevi anawapa uwezo wa kushuhudia lakini kama huna kibali cha MUNGU watu bado watabaki na mafaili ya ulevi wako wa zamani, kwa hiyo chochea hiyo neema hata mimi sasa hivi nina hubiri lakini watu bado wako na mafaili ya zamani, lakini nimechochea kibali ambacho MUNGU amenipa ndio maana leo mmejazana, Haleluya!
Inawezekana ni mfanya biashara, MUNGU amekupa kibali hicho, au karama ya ukulima inyenyekee kumuomba MUNGU kibali ili akuongezee Ekari za kulima, watu wmechoka kwa sababu neema aliyokupa pengine ni Uinjilisti au amekupa Udaktari, au fundi, amekupa kumpigia makofi, amekupa neema ya kumtumikia na mali zako unatakiwa uombee kibali ndipo mambo yatafunguka lakini ukikaa na kusema mimi ni mtoto wa mfalme ‘’my friend’’ mambo yatakua magumu unaweza ukabadilishiwa neema yako ukawekewa neema ya kishamba tu ukawekewa Uwoga, kinachotakiwa kuomba neema ya kuvaa vizuri, neema ya ujasiri, unaweza ukawekewa neema ya kuvuta bangi tu, kuvuta sigara tu inakubidi uombe kibali cha kuokoka, na ukishaokoka ombea wokovu wako kibali ili wasikuweze kama walivyotaka kufanya kwa Esta ikashindikana, walivyotaka kufanya kwa Ayubu ikashindikana – Bwana Yesu asifiwe!
Sasa unapoitunza neema sana ndipo unaenda kupata kibali sana, soma kitabu cha Samueli 1;2:26, leo watoto wengi wanazaliwa kwa neema lakini hawana vibali kwa Bwana lazima umuombe kibali kwa Bwana, Sunday School humpeleki, unmpeleka Baa tu, mtoto atajifunza vitu vya Baa tu atajifunza mambo ya MUNGU saa ngapi, Hata YESU mwenyewe alipoulizwa na wazazi wake pale walipokua wakimtafuta aliwajibu inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu alikua na kibali cha kwenda nyumbani ka Bwana, Sasa kama huna kibali cha kuhudhuria Ibada, huna kibali cha kuhudhuria mikesha itakuwaje inabidi uombe kibali.
Inawezekana na wewe hapo MUNGU ameweka kitu ndani yako lakini unakikalia tu, kwa sababu huna kibali mbele za MUNGU na mbele za madhabahu, inakubidi uombe kibali ili uwee kuvifanyia kazi na MUNGU atakuinua – Soma Waebrania 12:15 kwa hiyo kila mtu ana neema ya MUNGU ikikupungukia hutaenda mbinguni, ikikupungukia hutaweza Vita, hata malaika walikua na neema ya MUNGU lakini ilipowapungukia waliitwa wana wa shetani angalia na wewe neema ya MUNGU isikupungukie usije ukaitwa mwana wa shetani. Bwana YESU asifiwe! Angalia Daniel alikua na kibali mbele ya macho ya MUNGU kwa hiyo walipomuweka kwenye tundu la simba hawakumdhuru kwa kuwa alikua na kibali mbele za Baba yake hata wakati amechoka alirudi kwa Baba yake kuomba kibali ndipo aliposhuka Elia na Musa kumtia nguvu hicho kilikua kibali cha MUNGU ndani yake kibali ni Roho lazima uombe, ngoja nikwambie hakuna maisha magumu katika Dunia hii kama kukosa kibali mbele za MUNGU. Inawezekana wewe unayo neema ya kua mtu fulani lakini kwa kua hunyenyekei ujue hilo jambo halitatokea itabaki historia nilikuaga,Shetani hapendi watu kupata kibali toka kwa MUNGU ili mambo yao yanyooke shetani amewafunga Shetani amewafunga kabisa, hivi MUNGU akiweka kibali mbele zako hata majaribu yanapokuja utayaona takataka.
Mnaweza mkawekwa Magerezani, mnaweza mkasingiziwa lakini mnapaswa kushikamana Shetani akikukosa kwenye Uchawi kwenye nini anakutafuta neema iondoke lakini mkishikamana hamtawezwa. Unashikamana kiroho mnashikamana kimwili, mfano wa yule mwanafunzi mmoja alimkata sikio mlinzi mmoja wao kwa sababu walikuwa wameshikamana na Bwana YESU.
Haleluya! Leo hii ukiona mwenzako ameanguka kwenye wokovu mnawatema mate, Bwana YESU alikuja kwa ajili ya wenye dhambi na ndipo ataokoka, sio wewe uwe na kazi ya kumhukumu mwingine, jichunguze wewe umetenda mangapi, jifunze kuteteana kama Bwana YESU alivyokuja duniani kufanya kazi ya wokovu, kuwaokowa watu usimseme mtu mwenye kibali cha Bwana utaharibikiwa, Mtumishi akiwa na kibali cha Bwana atahubiri kweli, Ukiwa na kibali cha Bwana huwezi kuabudu sanamu kama MUNGU ukiwa na kibali cha Bwana huwezi kuombea mtu kwa kutoza pesa, hivyo ni vibali vya shetani hawana huruma, ni afadhali ukienda Hospitali watakutibu ili usikate roho watakwambia ulipe pesa baadae lakini kwa mtumishi mwenye kibali cha shetani atataka pesa kabla kumuombea mtu ata kama anakata roho ni mpaka atoe pesa, Nabii Hebron nina kibali cha kupeleka watu mbinguni nina kibali cha kuponya bure, sina kibali cha mapooza, sina kibali cha kigeugeu, nina kibali chako nina kibali cha mataifa cha kukuongoza ufike mbinguni. Haleluya! MUNGU amewaletea kibli cha ubatizo wa maji mengi nyie mnataka ubatizo wa kisima, wa kikombe alafu unaenda mbele za MUNGU atakwambia kwenda wewe, inawezekana una kibali cha kwenye masanamu YESU hakanyagi huko hata kama unalitaja jina la YESU, ninakuambia uombe kibali cha kwenda mbinguni ukiwa hai hautapata kibali cha kwenda mbinguni ukishakufa eti unaombewa na watu ukiwa kaburini hutaenda mbinguni ukisha kufa ndio uende mbinguni ni uongo. MUNGU wetu sio wa wafu MUNGU wetu yu hai anaongea na walio hai, bali wanaombea wafu wanamuomba MUNGU mfu.
Mtu asiye na kibali cha MUNGU ni mtu anayesahaulika ni mtu hata hakumbukwi unaweza ukakosa hata kibali cha pesa, unaweza ukakosa kibali cha chakula, unaweza ukakosa kibali cha mavazi, unaweza ukakosa kibali cha kusalimiwa hata kukumbukwa, MUNGU anasema amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, mtegemee yeye lakini watu wamebadilika wanamtegemea mwanadamu kwa akili zao za kinafki kwa mfano mtu anakukumbuka siku mtot amelazwa Hospitali ili umpe pesa ya kumtoa mtoto, kuna mtu anakukumbuka saa anafukuzwa kwenye nyumba, hivi ni vibali vya shetani.
Kibali kinalindwa kwa maombi mfano Esta aliangalia ahadi ya MUNGU akaomba kibali tazama walikua waangamizwe lakini kibali kiliondoa, angalia Sara alikuwa na neema akatembelewa na malaika kupewa habari za kupata mtoto uzeeni Sara alicheka alijidharau kwa umri alio nao, yawezekana hata wewe unaambiwa utapata Gari unajidharau ukiangalia hali uliyonayo, Ibrahimu kabla ya kuzaliwa alikuwa na neema ya kuwa Baba wa mataifa na ikawa, kwa hiyo wewe ndiye utakayesababisha alichokupa MUNGU kitokee. Sulemani alikua na kibali cha kumjengea MUNGU lakini Baba yake Daudi hakua na hicho kibali ila angeomba angelipewa.
Kibali kinaweza kuibiwa ili kisiibiwe unakitolea sadaka ya ulinzi, familia inaweza kukunenea hutapata mtoto na kweli hutapata mfano hutaishi na mke na kweli hutaishi na mke, lakini ukiomba kibali hayo hayatatokea, kuna kibali cha kukaa na mke wako, kuna kibali cha kuja madhabahuni kama vile Samueli, kama kikichukuliwa huji,kun ahata kibali cha kumshangilia MUNGU.
Kibali chako kikichukuliwa unakuwa mtu wa kukata tamaa unaona hupendwi, unaanza kua mtu wa hasira unaanza kuwa mtu asie na maisha mazuri, ukiona hivyo omba kibali kwa MUNGU, ukipata kibali utaona mambo ya ajabu, kama wewe ni mwan ndoa kibali la sivyo mtaishi maisha kama ya mbuzi na kondoo, kama sio watu, ni mchungaji omba kibali ni muimbaji omba, unaweza kuwa na kibali cha kukata tamaa tu, unaweza ukawa na kibali cha kwenda kuzimu na unakwenda kuzimu, kama una mtoto muombee kibali cha MUNGU asitumikishwe na wachawi, mwombee kibali cha kuja hemani mwa Bwana, watoto wana vibali vya pombe, vibali vya Bangi kwa sababu mama yake alivyokua mjamzito alikuwa akitumia vitu hivyo, Omba kibali cha utajiri omba kibali cha cheo, omba kibali cha kusoma, omba kibali cha kuheshimika, kibali cha kupenda watu, kibali cha kuheshimu watu, Vibali vya watu wengi vinashikiliwa na ukoo, kuna watu hawana ata kibali cha kwenda Nchi za nje kuna watu hawana kibali cha kuambatana na wenzi wao, wengine hawana hata neema ya kucheka na wake zao, neema ya kufunga ndoa omba kibali.
Kibali kinaendana na Nyota, kuna kibali cha kung’ang’ana na Bwana YESU, kibali kinaweza kuisha muda, ukikosa ibada mara nyingi kibali kinaisha au kupungua kuna kibali cha Roho Mtakatifiu, ukiwa na kibali mambo yako yanakua rahisi, kuna kibali cha miaka yako, kuna kibali cha kumsujudia MUNGU, kuna kibali cha kupiga magoti, kibali cha kunyenyekea MUNGU, kibali cha ulinzi omba kibali cha kazi ya mikono yako, kibali cha kusogea madhabahuni pa Bwana. Vibali vyako vitarudi kwa njia ya maombi.
Sema Bwana YESU asante kwa neno lako niko mbele zako ndani ya agano la Damu ya YESU naomba toba rehema na msamaha kwa yote niliyokosa kwa mawazo, kwa maneno, na vitendo vyote vya uovu- nakukubali wewe kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, namkataa shetani na mambo yake yote futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele – Bwana YESU nakuomba unirejeshee vibali vyangu vyote vilivyochukuliwa na adui kama upendavyo Amen!
Prophet hebron Wilson kisamo.