Pages

Friday, April 19, 2024

 

KILA MWANADAMU ANAYE MUNGU!

 

1 WAFALME 18:15-40

Neno la MUNGU lina elezea Habari ya Mtumishi wa MUNGU Eliya.

Kila mwanadamu anaye MUNGU ndani  yake, awe ameokoka au hajaokoka ana MUNGU. Neno la MUNGU linaelezea kwamba yupo MUNGU,na yupo MUNGU wa aina moja tu amabaye ni MUNGU wa Mbinguni aliyeumba mbingu na nchi  aliye kuumba wewe na tunaye mwabudu. Mnaposema kila mtu ana MUNGU si jambo la kwanza kusikia, pia kuna miungu ya shetani, akajenga mfumo wake ambao mwanadamu atampenda ili afuate mambo ya shetani, akaona ngoja awapoteze watu wa MUNGU, kwa kuwavuta. Ni vizuri kujua MUNGU yupo mmoja, kwa nini MUNGU wawe wengi? Kwani dunia hii ilijengwa ili iwe na MUNGU wengi. Basi unakuwa na MUNGU aliyekuumba na anakupa na uhuru wa kumtaka MUNGU yupi?. Katika dunia hii kuna miungu ya mizimu, Kuna miungu ya Matambiko, Ng’ombe, miti, miungu ya kabila

Tunaona yaliyotokea wana waisrael, na kuwapata katika taifa la Israel na wakati huo alikuwepo Nabii wa MUNGU Eliya lakini walikuwepo manabii wanaitwa Baali, walikuwa wakitawala taifa lile mpaka wakimuongoza mfalme wao, walikuwa wanamwabudu huyo Baali, ikafika wakati mambo yakawa mabaya sana. Wakamwambia Eliya wewe Mtaabishaji unatutesa, unasababisha mambo hayatokei katika taifa letu. Taifa la leo ni wewe kuna mambo hayaendi vizuri ni kwa sababu hujamshika MUNGU. Si kila  mtu anasema nina MUNGU , nina MUNGU, kuwa makini sana.`` Miungu ni mfumo wa shetani.”

Tabia mmoja ya MUNGU anapenda kuabudiwa, kuheshimiwa na kunyenyekewa, ili MUNGU akupate anataka umsikilize, umwabudu na kumnyenyekea ,na moja ya tabia ya MUNGU neno lake ni kweli.

Tulifundishwa habari za ma YESU, na sasa tunafundishwa  za huyu MUNGU. Watu  hawamjui, taifa la Israel  likateketea na kuangamia mpaka mfalme wanaomba kitu ambacho sicho, kwa sababu Eliya alikuwa na madhabahu, na wao walikuwa wana madhabahu hivyo hivyo, wale wauongo walikataa hawa wa kweli mpaka wanawaua, mtumishi alikuwa Nabii Eliya wakabakia.

Ukisoma neno la MUNGU wengine walifichwa kwenye makorongo, leo hii wanataka kuwaua kiroho siyo kimwili. Naamini pia wewe uko Imara, mjue sana MUNGU mkamate na umuelewe usije ukawa unasema una  MUNGU kumbe unamiungu ya ukoo, miungu ya kiafrika. Miungu inatenda na inafanya miujiza, kile kipindi cha Musa na Farao, Musa yupo na MUNGU na Farao yeye yupo na Miungu yake, anatoa machura, Manyoka. Ila ya Musa ilikuwa tofaut zaidi, ndiye MUNGU tunaye mwomba ndiye aliye, atafanya jambo la ajabu kwako. Ukiwa na huyu MUNGU hautetemeki wala hautikisiki, Eliya pamoja na matisho yote lakini bado alifika kwa mfalme, huyu ndiye MUNGU, tukisoma zaidi ni MUNGU wa Daniel.

 

Unaweza kuambiwa nina MUNGU wa Eliya kumbe ni Miungu ya matambiko na aina za miungu ziko nyingi sana, kama aina za YESU, Hili Neno limetumiwa na Miungu ya kila namna, Kuna Miungu ya sanamu, lakini kuna YESU wa sanamu, pia kuna Ukristo wa sanamu, kuna ukristo wa wafu.

Wanatumia neno hili hili kuhakikisha wewe hapo unatawaliwa na Miungu mingine kwa kujua na Kutokujua kama walivyokuwa wana waisrael kipindi hicho, Mtumishi wa MUNGU Eliya akamalizia. Akaanza kuabudiwa MUNGU wa kweli.

Kuna Mungu wa Wachawi, Si unaabudu wachawi? Kuna Mungu wa Majini, na kuna Mungu wa Mali, Mungu pesa, Mungu wa Dini, Kuna Mungu wa kila Taifa na kuna Mungu wa Dunia hii ambaye si Mungu huyu mambo yake hayo , anataka yeye akukontroo wewe mwanadamu, anataka umuabudu yeye na umnyenyekee na kukuteka kwa maana haupatikani katika kila mahali. Lakini ameingia kwa eneo hili kwamba umpende, basi anataka umuabudu.

Kwa kuwa Israel walimpenda MUNGU, wakasema ajulikane MUNGU anaejibu kwa moto, ndiye MUNGU. Wale wote wakabadilika wakamfuata MUNGU wa Eliya. Lakini kabla ya hapo walikuwa wakiabudu mungu mwingine, “sasa Hivi ni Kiroho”; Watu wengi sasa hivi hawana MUNGU hata kama wanasema Baba yetu uliye mbinguni. Matokeo yake unateseka tu, na madhara yake hautaenda kwa MUNGU.

 

Tabia za MUNGU” Kujibu”. Moja ya Tabia ya MUNGU yeye aliyeumba Mbingu na Dunia atahukumu, lakini moja ya Tabia ya Miungu inakuhukumu, inakufanya wewe uwe kwao kwa kujua na kutokujua. MUNGU aliye hai habadiliki ni yeye jana leo hata milele.

 

 Mtu akisema anamwachia MUNGU, kumbe ni unamwachia Miungu inaweza kukufungisha ndoa bila ya kujijua. Hii Miungu ina Listi ya majina ya watu, na pia ni roho ambazo zimetengenezwa na Ibilisi au Shetani, zikawekwa ndani ya mwanadamu, ili kuwaharibu wanaokwenda mbinguni, MUNGU wa mbinguni yeye ni njia ya kukutana na wewe na tabia yake kubwa ni Kuokoka, Kupitia njia ya kumfikia yeye. Miungu mingine haina kuokoka inaenda moja kwa moja. Madhara yake siku miungu inahukumiwa na wewe unahukumiwa. Neno la MUNGU yeye si mungu wa wafu,umepoteza miaka Mingi  unapigia makofi Miungu, Lakini MUNGU aliyekuumba haumpigii makofi.

Ukoo pia una Miungu yake, haitaki MUNGU wa kweli, inafanya watu wasimwogope MUNGU, hawana hofu ya MUNGU, Pia imewafunga watu kiasi ambacho inasema kunyweni pombe. Wakati MUNGU yeye yule jana na hata milele, Ni Alfa na Omega. Neno lake halibadiliki linapobadilishwa in Miungu mingine inabadilisha, Mfano  kumtolea MUNGU risiti wakati nyumba za MUNGU hazihitaji michango. Mpaka Uguswe, unapofanywa hivyo, unakuwa haumtolei MUNGU bali Miungu, haifai kuahidi pia utatoa shilling ngapi ngapi.

Mafundisho ya neno la MUNGU yamekuwa mabaya siku hizi, Eliya alipoletwa Israel ndipo watu walimwamini MUNGU. Ni vizuri kujua unampenda MUNGU yupi, mafundisho yamekuwa mabaya  sana. Kama Mfalme alivyotekwa na Israel mpaka MUNGU akamtuma Nabii Eliya watu wakaanza kumjua MUNGU. Lakini kwa sasa Mambo yamerudi yaleyale, Wachungaji wa miungu na Kondoo nao ni wa Miungu , kama Neno la MUNGU linavyosema waliowake watamsikia, wa Miungu watasikia kwa Miungu, Simama Imara.

 

Ipo shida nyingine mtu akiwa upande wa MUNGU hataki matatizo , hata tukisoma Eliya angalia alikuwa na MUNGU lakini alipata matatizo alimwangalia MUNGU, Musa pia alipita kwenye magumu lakini alishikana na MUNGU, tazama Ayubu amepita kwenye matatizo yake mke wake aliyepewa na MUNGU na huyo huyo alimwambia aachane na MUNGU na akamwambia MUNGU hakupendi  lakini bado Ayubu alimwangalia MUNGU na akashinda.

Nataka nikufundishe jambo  mwingine anaweza kusema MUNGU amekuacha lakini MUNGU  hajakuacha, usije ukawa kama mke wa Ayubu, yawezekana ni mwaaamke au mwanaume uko hivyo hivyo, YESU mwenyewe alipita kwenye kipindi kigumu na ni mwana wa MUNGU wale wa Miungu walimcheka na alishinda. Na wewe unaweza kuharibu muujiza wako usipomsikiliza MUNGU, acha kuangalia vitu, usikie kwa MUNGU, uki tembea naye, atakuvusha na ahadi zake zitatimia kwako.

 

Moja ya tabia ya MUNGU hapendezwi na Uongo. Tabia za MUNGU amemtuma mwanae tubatizwe kwa maji mengi, angalia tabia uliyonayo ya ubatizo wa maji mengi? Ubatizo wa kikombe ni tabia ya Miungu, unapobatizwa na ubatizo wa kikombe huyo ni mungu yupi? Siku ya mwisho utahukumiwa. Na kwa mtu anayempenda MUNGU atakuwa makini, mtu anayemwabudu MUNGU na kumnyenyekea , Shetani hampendi kabisa, hampendi kwasababu ianajua hampati, YESU kipindi kile aliingia hekaluni akakuta  watu wanafanya biashara aliwafukuza.

Angalia sasa hivi michango mingi makanisani, mpaka watu wanaogopa kwenda makanisani ni kwasababu tu mambo yanayofanyika.

Unaweza kufanywa kondoo wa Miungu, kwanini hautaki kuokoka mpaka sasa hivi?! kubali ili utimizi haki yote, ili mbegu bora ipandwe ndani yako.

Bwana atakurejeshea vitu vyako vyote, vilivyochukuliwa nashetani na Miungu, na hautahukumiwa na utabaki kuwa huru.ili miungu isipate nafasi, mwangalie MUNGU.

YESU ni mwana wa MUNGU hofu na mashaka vinaweza kuyumbisha maisha yako. Wala usiende mbinguni ukaenda kwa miungu. Eliya aliwachinja mabaali, akaomba na moto kutoka mbinguni ukashuka, MUNGU alikuwepo na Eliya.

Wapo watumishi wachawi na wanaenda kuzimu na wanapewa nguvu na upako wa shetani. Lakini napenda nikutie moyo mwana wa MUNGU, unaweza kupita kwenye kipindi kigumu, ukaona kama MUNGU hayupo na wewe, usiogope atakuinua tu, we mwangalie yeye kama Eliya alivyomwangalia MUNGU mpaka akawauwa Baaali mia nne hamsini. Kuna mambo mengine MUNGU anaweza kukuangalia tu, ili kukuandaa uwe imara ili atakapo kuja atakunyankua ukawe kifaa chake kizuri.

 

Kumbuka aliamini neno moja tu,yupo na MUNGU ndio maana hamkumsiliza mke wake. MUNGU anakutaka wewe, anasema yeye ni MUNGU anayesamehe tena mtu akiwa hai sio amekufa ndio uombewe, mwanadamu shetani anamtaka na MUNGU hivyo hivyo anamtaka mwanadamu.

Mbingu ya MUNGU inakutaka wewe ili utubu umrejee, ukaishi maisha ya kumpendeza MUNGU. Kubali umpokee YESU sasa awe Bwana na mwokozi wa maisha yako ili miungu isikupate tena. Pia ufanyike kuwa mwana wa MUNGU, Uwe na MUNGU siku zote za maisha yako.

 

’Bwana YESU niko mbele zako ndani ya agano la Damu ya YESU ninaomba Rehema Toba na Msamaha, Futa jina Langu kwenye kitabu  cha hukumu, andika Jina langu kwenye kitabu cha Uzima wa Milele lisitoke huko mpaka YESU utakaporudi. Amen”

 

PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.