HII NDIYO IMANI KUU WANAYOPEWA WAHUBIRI WA UONGO NA SHETANI.
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote! Nimewaandikia ujumbe huu ili zaidi kuwasisitiza kuwakumbusha YESU karibu anarudia, ameniambia maandalizi ya BABA yake wa mbinguni yameshakamilika ili kuja kuwanyakua wale wote ambao wamempokea kama Bwana na mwokozi na kudumu katika utakatifu na kusimama imara. Msishangae mnavyozidi kuyaona machafuko katika ulimwengu wote na bado yataendelea zaidi maana ilishaandikwa katika kitabu cha Ufunuo hata katika kitabu cha Daniel na ndivyo ilivyo kila neno lake litatimia na hakuna atakayeweza kushindana na MUNGU, hata bakia salama na zaidi hataurithi mbingu. Dunia imechafuliwa na shetani na mawakili wake ila ilipasa yatimie. Nawasihi mataifa yote leo unaposoma ujumbe huu umpokee YESU maana hata ninayoyaandika siyo maneno yangu mimi Hebron Nabii wake.
Ukisoma kitabu cha Wagalatia 3: 7-11
"Fahamu basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba MUNGU atawahesabia haki mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, katika wewe mataifa yote watabarikiwa. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za MUNGU katika sheria; kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani."
Katika mistari unyoisoma niliyokuandikia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wa mbinguni. Baadhi ya watu wengi wameiacha imani njema ya YESU mwokozi wakafuata imani mbovu au za uongo na kuwapoteza waelfu wapo wanaojua; na wengine hawajui. Kuwa mkristo tu haikusaidii kuwa mfuasi wa YESU, maana yeye anataka umkiri na umwamini kwa imani na matendo kama alivyofundisha ulimwengu katika kipindi chake alivyokuja na sasa ni kipindi cha YESU kurudi. Muda na siku ni siri yake MUNGU peke yake na ameniambia nijue pia maana hawezi fanya jambo bila kumjulisha Nabii wake. Hata wale watumishi wa upande wa shetani ni ni midomo ya shetani; shetani huwajulisha mipango yao na kuwajulisha au kuwadanganya wanadamu ili waamini na mwishowe wachomwe moto milele.
Waebrania 10: 26, 37-39
YESU akirudi ataangalia mbegu ya imani uliyoipokea je itakuwa ni yake au ya mpinga kristo au ya mizimu; leo umkiri YESU; naomba sana usidharau au kuyapuuzia maneno haya; itakuwa kama kipindi cha Nuhu, wengi walimcheka Nuhu. Mafuriko yalipokuja ndipo wakakumbuka na muda ukawa umeisha.
Kama nilivyogusia aina ya imani ambayo kila aliye mpinga kristo au freemason ni lazima awe na hiyo imani ya ajabu sana, ni imani itendayo kazi kwa wahubiri wengi pasipokujua au kwa kujua; unajua ukweli lakini haufuati, unapindisha neno. Hiyo imani ni aina ya imani ambayo ipo kuzimu katika kitengo cha imani na utendaji wake ili kuwadanganya mataifa na kuwateka. japo wapo wanaojua wapo kikazi kabisa na shetani ana nguvu ya kuwafunika waonekane kuwa ni malaika wa nuru na kumbe siyo. Imani yenyewe nitaielezea kwa ufupi ili wakati mwingine ukifuatilia mafundisho ya Nabii Hebron utajua kwa undani na uendelee kuibomoa iyo imani katika ulimwengu wote.
IMANI YA NYANI:
Huyu mnyama Nyani siyo mgeni anajulikana japo yeye siyo mnyama mbaya bali kule kuzimu pia shetani ana nyani wake. Hii imani ya nyani ni imani ya uwizi bila uoga, aibu wala hofu ni imani ya kunyang'anya watu vitu kwa kutumia jina la YESU. Sawa sawa na nyani kama akiona mahindi au matunda anachukua bila uoga na kuiba na kukimbia na ataenda tena. Kwa hiyo wanapewa hiyo imani ya nyani inaishi ndani yake, anatumia kuibia watu vitu na kuwanyanganya. Atakachotaka kwako ile sauti ya mhubiri inakuja na nguvu ya imani ya kuchukua vitu vyako na ukatoa ukifikiri unamfanyia YESU. Alishasema watatumia jina langu ili kuwapoteza watu wengi. Imani ya nyani inaiba nyota, pesa na endapo imani hii ipo kwa mhubiri ni lazima akupangie kiasi cha kutoa bila aibu, wakati neno linasema sadaka ni siri yako. Sasa kwanza uoangiwe kiasi au ili upate huduma ya kiroho ni mpaka utoe pesa, wakati neno linasema ninakupa bure,toa bure. Soma (Mathayo 6: 2-4). Sasa ndugu msomaji hapa hauoni unafundishwa kuwa mnafiki mbele za MUNGU pasipo kujua au kujua ili hiyo misingi ya imani ya Nyani (Mathayo 10:8) hapa ndipo utaijua ni mhubiri mwenye imani ya nyani wa kuzimu ambaye amepewa na baba yake ili aifanye kazi ya shetani akiwatumia wanadamu.
Unapobadilisha neno au kuigeuza nataka uelewe kuwa unatenda dhambi na na una dhambi, mataifa yote kunayo dhambi ya makusudi. Hivi umeshajiuliza ya kuwa kuna maisha ya baadaye na baada ya haya utakuwa wapi? Jinsi ulivyo ndivyo na maisha yako ya baadaye yatakavyokua. Ni bora ubadilike leo YESU anakuhitaji kabla hajafunga mlango wake. Mbinguni hakuna kwenda kwa vyeo, umaarufu, elimu wala madaraka, nabii, mfalme, majini, mtu maarufu mchungaji, mtume au mhashamu askofu ni kwa "KUOKOKA" tu wala silipindishi neno kabisa.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE. UNIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE. MIMI NAJIKABIDHI KWAKO, NATUBU, SIMTAKI SHETANI TENA.
Damu ya YESU iwafunike.
NABII HEBRON WILSON KISAMO.