KILA MKRISTO
ANAYE YESU NDANI YAKE
BABA ninakushukuru kwa muda huu tena na ni siku nyingine ya uumbaji, tumekutana na watoto
wako kama sheria yako na sisi tumeyatii maagizo yako, nawaombea wote wanaosoma na
hata wanaosikiliza you tube naomba ukutane nao wote, injili yako ikatende
ukamguse kila mmoja ukampe amani, ukawatie nguvu na ukawape furaha ya mwaka wa
2024. Bwana YESU asifiwe, Haleluya, jiandae kupokea kila ambacho YESU
amekuandalia siku ya leo.
Mathayo
24:3-10, 22-26
Kila mkristo anaye YESU ndani yake, Je! Ni YESU yupi yuko ndani yako maana kuna YESU mwana wa MUNGU na yesu ambaye ufalme wa shetani humtaja. Chanzo cha Mkristo ni Bwana YESU, alipokuja hapa ulimwenguni, tukaamini na tulipomwamini tukawa wakristo, kila mkristo anaye YESU ndani yake kwa sababu anamwamini YESU na ndio maana ameitwa Mkristo; lakini YESU anasema watakuja makristo wa uongo, watawaambia mwende huko, yuko huko, akasema kupitia neno lake msiende, mnajua ni kwa nini anawambia hivyo? Kwa sababu makristo wanatafuta mtu aliye na Bwana YESU wa kweli ili waweze kumteka, kwa kumyumbisha yumbisha katika nyumba za ibada ambazo zinamtaja YESU ili hali zingine sio, (maana kuna YESU mwana wa MUNGU na yesu ambaye ni wa aina nyinginezo nyingi nasema hivyo maana kuna yesu wa sanamu, mapokeo, ubatizo wa watoto, ubarikio wa wakubwa, ubatizo ambao ni tofauti na ule ambao YESU alibatizwa, yesu wa upako, wa maji, udongo nk. yaani yesu anayetajwa ili kuwapumbaza watu wajue au kuamini au kudhani kuwa ni YESU mwana wa MUNGU kumbe la! Wanataja yesu wa maagano ya mtumishi husika au kwa lugha nyepesi wanawadanganya watu/ wanadamu watoto wa MUNGU kwa kutumia jina la YESU) na wengi wametekwa kwa namna hiyo kwa kujua na kutokujua.
Mfano, hata
mimi nilikuwa mkristo lakini mkristo wa upande mwingine kwa sababu habari za
YESU wa kweli zilikuwa hazifundishwi ila nilijiona ni mkristo kwa kujua na
kutokujua, na nilipokuwa huko walikuwa na wao wanatuambia, ukiambiwa yuko huko,
usiende, yuko kule usiende (Hapa nazungumzia ukristo wa mapokea, ubatizo wa
watoto, kubariki wakubwa /vijana, kufanya harambe kanisani, kufanya minada
kanisani, ndoa za jinsia moja na mambo kama hayo) kwa kujua na kutokujua
nilikuwa mpinga kristo. Nilijiita mkristo ila kumbe nilikuwa na vifungo na
nilikuwa namwabudu yesu mwingine, na walikuwa wananizuia ili nisimpate YESU wa
kweli, mpaka pale nilipopata neema tena ya kufundishwa, kuokoka, na kumkubali
YESU mwana wa MUNGU na nikawa huru, na sasa nawaletea habari za YESU wa kweli,
ili mumkubali yeye na awaweke huru, na hata YESU alisema watatumia jina lake na
watawapoteza wengi sana.
YESU alisema
watakuja makristo, inamaana ni majitu mabaya, yenye roho mbaya kweli na
yamewapoteza wengi, naomba niulize swali; wewe una YESU yupi ndani yako? Kwa
sababu ukiendelea kusoma, katika kitabu cha Mathayo anasema nitakuchoma,
utachomwa moto hata kama ni mkristo kwasababu hukuwa na YESU mwana wa MUNGU ila
ulikuwa na yesu mwingine ambaye alitengenezwa au ni shetani anatumia jina la
YESU kupoteza watu, wengine watamwambia tulikuwa kanisani tulikesha, na yeye
atawaambia kuwa sikujui, sikujui unapokuwa mkristo ndani ya moyo wako yuko YESU
lakini ujikague na kujipima kuwa ni YESU gani yuko ndani yako na ndani ya
maisha yako ili usiwe katika msururu wa yesu mbovu, kuna aina mbili za yesu
kuna YESU ambaye ni mwana wa pekee wa MUNGU, ambaye alitabiriwa, akaja, akapaa
mbinguni na sasa tunamsubiri, kuna yesu, yesu mpinga neno la MUNGU asiyeokoa,
asiyetaka watu waokoke, kuna yesu anayetaka watu wakate shauri tu wasiokoke, kuna
yesu wa uchawi, mizimu, mwanadamu anajiita yesu, ni mhubiri anajiita yesu, hapo
pamewachanganya baadhi ya wakristo kwa kujua na kutokujua, kweli unampenda
YESU; ila kunakuwa na mitego ili usimfikie YESU wa kweli, leo napenda
nikufundishe ili ujue kama una YESU mwingine umfukuze huyo yesu na umkaribishe
YESU wa Nazareti, YESU mwana wa MUNGU, alitabiriwa, aliyekufa na kufufuka
akapaa, Mbinguni na sasa tunamsubiria.
Hiki ni kipindi cha hatari sana shetani nae anakazana ili apate watu wa kwenda naye kwenye moto, napenda nikufundishe na kukuombea pia, ili ujue kuwa ndani ya moyo wako yuko YESU wa aina ipi, ila pia unaweza kujitathmini ukajua nani yuko ndani yako ni aina ipi ya YESU iliyoko au uliyoiamini na inayoishi ndani yako maana siku ya mwisho itakuwa ni kilio nakusaga meno, maana yamkini una yesu mwingine. Unaweza ukawa unampenda YESU wa kweli ila kwa kujua na kutokujua yesu mwingine ndio yuko ndani yako kama kivuli, anajidai anakupenda na atakubariki ila baraka zake sio za YESU wa mbinguni, anakupumbaza ili usimpate YESU wa kweli. YESU aliwambia wanafunzi wake kuwa wakiwaambia yuko huku msiende yuko kule msisadiki, unajua kwanini aliwaambia wanafunzi wake? Napenda nikufundishe alitabiri na kufundisha mambo yajayo na ndio yaliyoko sasa, basi ninakusihi kama una yesu wengine basi wafukuze ukae na YESU wa kweli. maisha yako yakabidhi kwa YESU mwana wa MUNGU aliye hai, wangapi mnampenda YESU? Wote tunampenda YESU, Hivi YESU anabadilika?
Amesema anakuja kuokoa, lakini yuko yesu ambaye anakataza watu kuokoka, ukisoma neno la MUNGU; YESU anaponya bure, lakini kuna yesu anaweza kuwa ndani ya mhubiri, ndani ya kanisa ndani ya madhabahu yeye anaponya kwa pesa, huyo sio yesu wa mbinguni huyo ni yesu mwingine, unaweza ukawa unampenda YESU sana lakini kumbe wewe uko na yesu mwingine sio wa Mbinguni. Mimi nilizaliwa katika ukristo lakini nilizaliwa katika yesu mwingine kwasababu mfano halisi YESU MWANA WA MUNGU alibatizwa akiwa mtu mzima na alibarikiwa akiwa mtoto mdogo, lakini mimi nilibatizwaga nilipokuwa mdogo, nikabarikiwa mkubwa, neno la MUNGU limepingwa. Ni mfano hai kuwa nilizaliwa katika Ukristo ila ndani ya yesu mwingine, mpaka nilipookoka nikampata YESU wa kweli. Ukweli ni kuwa na yesu ambaye anabatiza watoto wadogo huyo sie, yesu anayebariki watu wazima/vijana huyo sie, ni yesu mwingine akikuambia njoo huku, njoo huku, usiende, sasa hivi injili imebadilishwa kuwa biashara, YESU ninamjua nyumba zake sio za minada, sio za harambe, YESU ninayemjua nyumba zake ni za sala, ibada na kumsifu MUNGU, ukikuta mahali ambapo panaitwa kwa jina la MUNGU na wanafanya minada, huko hayuko, huko usiende huko yuko yesu mwingine mkatae maana na huyo yesu feki anamiujiza yake, (YESU mwana wa MUNGU hafanyi minada kanisani, alishawapinduliaga meza kipindi kile walipokuta wanafanya biashara kanisani).
MUNGU ana
ufalme wake na shetani nae ameweka ufalme wake, pia kuna yesu wa mizimu,
mapepo, majini lakini katika falme zote anayetafutwa ni mwanadamu; MUNGU anamtafuta
mwanadamu ili amrejee yeye na shetani anamtafuta mwanadamu ili amwasi MUNGU;
ila ile siku ya mwisho wengi watalia, yuko yesu ambaye anabariki pombe, unasema
wewe ni mkristo lakini unabariki pombe / unakunywa pombe huo sio ukristo, acha,
napenda nikufundishe na ufahamu kuwa mahali wanapokuambia au wanalitaja jina la
YESU na wanaendelea na mambo ya dunia (mambo ambayo MUNGU aliyakataza) mfano
kunywa pombe, kutambika, ubatizo wa watoto wadogo; hapo wanalitaja tu au
kulitumia tu jina la YESU lakini wanawateka na kuwaelekeza wanadamu kwa
shetani, na baadhi ya wanadamu wanapenda mahali pa vuguvugu yaani MUNGU kidogo
na mambo mengine kidogo; hapo utaona wengi wanamiminika kweli napenda
nikukumbushe kuwa siku ya mwisho ni kindumbwe ndumbwe, kilio na kusaga meno.
YESU amesema usiabudu sanamu, mnapoingia nyumba za ibada na zina sanamu huyo ni
yesu mwingine usiende, namna yawa kuteka ni kwa kile ambacho mtu unakiamini,
kuna yesu anayewabagua watu kanisani, wenye pesa wakae huku wataitwa majina
mazuri, gold, almasi, silva, lakini usiye na pesa ataambiwa kaa kule, YESU
hanaga ubaguzi wala habagui, anawapenda watu wote, kanisa lenye matabaka hilo
silo la YESU.
Mimi mwenye kabla ya kumjua YESU wa kweli nilikaa na yesu feki, mpaka nilipoamua kuokoka nikampata YESU wa kweli akazaliwa ndani yangu, Je! kwako amezaliwa yupi? Miaka ya nyuma alizaliwa yesu wa kikombe, aliibuka anayeponya kwa jina la YESU na kwa mia 500 watu wakaenda kunywa kikombe wakijua ni YESU kumbe La! (walitajiwa jina la yesu lakini ni yesu feki) maana hata YESU original amesema anatoa bure, anaokoa bure, anaponya bure sasa yesu wa sh. 500, ya kikombe alitokea wapi? Taifa lilitekwa kwa yesu mwingine, dunia imetekwa imeshikiliwa, imedanganywa wakiwa wanalitumia jina la YESU, unayesoma upone, YESU anajua wengi mnampenda, anawapenda sana, nanyi mnataka YESU awaongoze ila inashindikana kutokana na mafundisho na mapokeo potofu ambayo uliyapokea na yakakaa ndani yako sana unaposikia habari za YESU wa kweli unaona ni ushamba, ni uongo ila napenda nikufundishe kuwa yale aliyoyaandika YESU yasiongezwe wala yasipunguzwe ndivyo yalivyo ole wake aongezae au apunguzae.
Amua umfuate YESU wa kweli. YESU asiyebadilika anasema yeye ni
yule jana leo na hata milele na neno lake ni lile lile, MUNGU anasema usiabudu
wafu, baadhi ya wakristo wanaabudu wafu [yaani mtu amekufa ameshazikwa baada ya
mda fulani mnamfanyia ibada ya kumbukumbu au kumwombea YESU hakuyaagiza hayo],
na kuna yesu mwingine anakuja kwa njia ya wokovu utaongozwa sala ya toba na
mtumishi asiye na YESU wa mbinguni, unabatizwa kwenye kisima sio YESU,
unabatizwa kwa jina la mchungaji sio YESU wa mbinguni, utasema umeokoka (kwa
kuaminishwa na kufanyiwa mambo kama YESU ila kumbe ni mambo ya wakala wa yesu
mwingine (wamecopy maagizo ya YESU mwana wa MUNGU sasa wanawadanganyia watu)
kama vile ni ya kweli ila kwa yesu mwingine.
Nakuletea hii habari njema uijue usipoteze mda wako, usimame imara, unaweza kusikia mchungaji, mwalimu, mwinjilisti, mtume, nabii, kiongozi wa dini Fulani kwa cheo chake; ukajua wote ni watumishi wa MUNGU; ukweli ni kwamba wako wa YESU wa kweli na wako wa Shetani ni kama vile mtu ambaye anaenda kwa mganga na kupewa pesa unachopewa ni jini pesa na unapata pesa; wako wenye pesa za halali ambazo wamemwomba MUNGU na kufanya kazi na kubarikiwa wakapata pesa, hata kwa watumishi; unaweza kupewa utumishi na mganga, jina mtumishi kwa cheo chako, mhubiri, kiongozi wa imani kwa dhehebu lako, mwimbaji mzuri ila umepewa na majini na hao hao wanalitaja jina la YESU ila utawatambua kwa matendo yao, ila hawa wanawaonea watoto wa MUNGU; nataka nikawashughulikie kwa kwa njia ya maombi ili muwekwe huru pasiwe na jini au pepo, na sihitaji upotee, na hitaji umpokee Bwana YESU ili akuokoe nae afanye njia pasipo na njia, afanye njia ya kukuokoa uwe huru yaliyoshindikana akatende, ili hao watesi wakikuambia kwenye ulimwengu wa roho njoo huku wasiweze na wasikuone. MUNGU kupitia wana wake amesema usitoe kwa riba, leo makanisa yanadaiwa, hilo haliwi tena kanisa la MUNGU linakuwa kanisa lenye mashtaka ya kutoa riba na shetani anapata nafasi na yesu mwingine analitawala, tunaamini kila mtu ana YESU ila inategemea ni YESU yupi ni kama vile tunaamini MUNGU yuko ni kweli yupo na ni MUNGU ila swali ni aina ipi ya MUNGU AU NI MUNGU yupi ambayo upo nae, MUNGU aliye hai, mungu sanamu, miungu, mungu mzimu, mungu wa familia, mungu wa dunia, mungu wa wafu, mungu mwanadamu, mungu mnyama, kuna aina nyingi sasa ni wewe kuamua MUNGU yupi ambaye umemchagua, ila miungu lazima watoke katika maisha yako, inawezekana unamiungu ya kikabila, kidini, kiwilaya nk. Hii haisikii; Lakini MUNGU aliyeziumba mbingu na dunia ukimwita anakusikia, anakupenda, anakujibu, anakupigania anakuweka huru, ila kinachosikitisha kuna baadhi ya wahubiri ambao wao wanaogopa kusema kweli ya MUNGU na wakihofia kulogwa na wahubiri wengine, kuchafuliwa majina, maslahi kupotea na mambo kama hayo, ila mimi nitaihubiri kweli ya MUNGU ili muwe huru na MUNGU wa mbinguni atukuzwe, nakuombea uwe huru kwa jina la YESU. Kuna mambo ambayo yatakamilika kwako, yale ambayo unadhani kuwa hayakamiliki yatakamilika, MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia kwa siku sita na siku ya saba akapumzika atayakamilisha.
Nitakuombea MUNGU yale ambayo hayakukamilika yakakamilike. Nitakuombea upako wa MUNGU wa kuyakamilisha; ila pia kuna upako wa MUNGU na upako wa shetani upako wa majini, nk. watu wengi wanaombewa na mayesu, na kwa pesa na hawajui kuwa wana majini ya upako au wanaponywa kwa majini (yanapooza ugonjwa baadae unarudi au unaambiwa toa hela au kitu fulani au yesu amesema anataka kitu Fulani ndipo akuponye ) maombezi yanayofanyika hivyo yanafanana na upako wa kiganga na upako ambao sio wa MUNGU; leo ukaondoke kwenye maisha, yako majini yamewekewa kwa watoto wa MUNGU ambao wanakimbilia miujiza na upako na kupewa maji, maji yenye upako wa majini hatimaye watu wanakuwa watumwa kwa mhubiri na kukimbilia huko; kumbe wana kimbilia mahala ambapo sipo, unakuta mhubiri ana maagano ya maji ya majini ambayo akiwapa mnakuwa wa shetani na mnamilikiwa na yesu mwingine hakuna upako zaidi ya neno la MUNGU; simama imara, usikatishwe tamaa katika kumfuata YESU, hizi ni nyakati mbaya sana ni wakati ambao shetani wameliteka kanisa na unafarijika kusema wewe ni mkristo lakini matendo yako hayaendani na mkristo, Imani yako haiendani na mkristo kwanini unaogopa kumkiri Bwana YESU kwa vile unaogopa watakusema, amua kumfuata Bwana Yesu na waambie kweli kuwa mimi sijapotea nimeokoka na nimemua kuifuata njia ya uzima wa kweli; usirudi nyuma, YESU anakupenda anakuhitaji na anasema umtafutae kwa bidii atamuona, na hata sasa unaposoma ndio namna ya kumwona, anakupenda na wewe mkubali YESU wa kweli mfungulie moyo wako apate kuingia afanya makao kwako.
HAKUNA JAMBO LA KUMSHINDA MUNGU na atalifanya lolote lile ambalo unaona yamkini lilishindikana yeye atakuweka huru, mwambie YESU nilipoteza mda mwingi kwa yesu feki; kumbe kuna yesu alikuwaga amezaliwa ndani yangu ambaye sio YESU wa mbinguni na kila mmoja anaijua nafsi yake, itatmini upo kwa yupi?, kwa YESU wa kweli au yesu feki, na nafsi yako inakushuhudia ndani yako; endapo YESU wa mbinguni ambaye ni Mwana wa MUNGU alieye hai angelikuja mda huu kwa unyakuo ndani yako unashuhudiwa kuwa ungelibaki au ungelienda baadhi ya watu wanaenda kanisani lakini pasipo kujua au kwa kujua aina ya YESU iliyo ndani yao; asilimia kubwa wamepotezwa, kama kipindi kile cha MUSA na farao, kila mmoja alikuwa na upako wake mmoja wa MUNGU na mwingine wa shetani na shetani amewateka kwa kusema upako, upako na watu wakisikia neno upako wanakimbilia, ila MUNGU alisema iwe usiku ikawa, iwe mchana ikawa, simama wakasimama, pona wakapona, sasa upako wa sasa ni upi ambao mnautafuta? Fuateni neno la MUNGU muwe salama. Haleluya! Baadhi ya wahubiri hutafuta pesa za waumini kwa njia tofauti, tofauti na kwa ujanja wa hali ya juu na unaweza ukasema wanamtumikia MUNGU kumbe wana upako wa majini, upako wa shetani na baadhi yao husema ninamtumikia MUNGU, wameitwa na MUNGU kumbe anamtumikia shetani, na wamejiita hivyo MUNGU hawajui, kumbuka kuwa MUNGU ili afanye kazi yake anamtumia mwanadamu na shetani vile vile anamtumia mwanadamu, unaweza ukamtumainia baba wa kiroho sana, yamkini nae ana upako wa majini au shetani, na unakuwa mateka, mtumaini MUNGU. Endapo upo ufalme wa giza ambao unakushikilia au kuna pesa za makampuni ya majini au chochote ambacho kinakushikilia kinyume na mpango wa MUNGU kikuachie ili MUNGU wa mbinguni akurejeshee maisha, kazi, biashara, nyota yako, malengo yako, neema yako na majini ya wizi, maupako ya shetani yatateketea, na mambo ambayo sio ya ufalme wa MUNGU yatateketea, YESU anasema usiogope heri wewe ambaye hukutoa hela ya maombezi kwa sababu nguvu ya MUNGU hainunuliwi, kununua nguvu za MUNGU ni dhambi. (Mhubiri anakuambia toa kiasi Fulani uponywe usidhubutu kutoa) yapo majini yanayofuatilia karama za watu, yakishafunga kwako kunakuwa kugumu, unakata tamaa ili yakuvute kwa shetani na ili uone kuwa kwa shetani ni kwepesi, unapata miujiza au mafanikio kwa haraka ndugu unapotezwa, jikane kwa MUNGU, amua mpokee BWANA YESU, kumbuka kabla ya kumjua YESU, tulikatazwa tusimkiri BWANA YESU, tukadhani na kuaminishwa kuwa dini itatupeleka Mbinguni, kumbe matendo yako ndio yatakupeleka sio dini ya baba wala ya mama yako, kubali YESU azaliwe ndani yako, kwanini mnafundishwa kuogopa kumkiri YESU? Unaogopa au kuona haya au aibu kusema mimi nimeokoka, kwasababu tu wanadamu watakucheka, usikate tamaa kwa vile watu watakuchukia au kukutenga kwa sababu YESU amezalliwa ndani yako au kwa sababu umeamua kumkiri YESU, maana YESU alishasema na iliandikwa kuwa watawachukia ni roho ya shetani itendayo kazi ndani ya watu ili kukukatisha tamaa usifike kwa MUNGU, achana na hayo mwangalie YESU mfuate YESU, kwanini baadhi ya wakristo wanadhani kuwa watu waliookoka wamepotea wakati wao ndio wako sawa na mkristo ambayo hajaokoka ukristo wake bado haujawa kamili kwa sasababu YESU alileta wokovu hakuleta dini, Je! YESU anaubaguzi? Hawataki kweli?
Baadhi ya
wahubiri wanaenda kwa waganga anawawekea mikono, anawawekea majini ya
biringita, mnasema MUNGU anatenda, lakini sio MUNGU , bali wanaenda kwenye
upako wa kipepo na unatumika kuwateka watu wa MUNGU ili wamwache YESU na
wamfuate shetani, habari hizi sio njema sana kwa baadhi ya watu ila ukisema
kweli unachukiwa na ukisema uongo wao wanaona ndio sawa kwa sababu wako kwa
kazi maalum ya kumtukuza shetani na wamemwasi MUNGU ukisema kweli utachekwa, ni
bora usema kweli kwa sababu atoae uzima, pumzi, na hewa ni YESU na sio
mwingine, hivyo kila cha yesu feki kitoke ndani yako na cha YESU mwana wa MUNGU
kingie ndani yako kuna yesu wa kurithi, kuna yesu mpaka anawadanganya wanadamu
msile mkae mpaka mfe ili mwende mbinguni ni yesu feki huyo, acha mambo yakuwatumainia
wanadamu maana kuna majini ya kuabudu, kusifu, kuhubiri, jini mkristo, nk. Jini
ambalo lipo na linazuia ya mpango wa MUNGU kwako usitimie, namwomba MUNGU
litoke ili ya MUNGU yatimie kwako.
MUNGU
anawatenda kazi ambao ni malaika ambao hushuhudia na kusimamia kazi ya MUNGU
itendeke sawasawa na shetani nae ana malaika wake wa kuharibu mipango ya MUNGU
juu ya maisha yako, miaka yote ungekuwa na YESU malaika wa MUNGU wanakuwa wako
wakikulinda, MUNGU anaangali neno lake alitimize ila kwa bahati mbaya ukitekwa
na shetani malaika wa MUNGU hawakai nawe mpaka pale ambapo utamrejea MUNGU, Je!
umemkubali YESU mwana wa MUNGU? Je! Umemkana shetani? Basi mkubali YESU MWANA WA
MUNGU maisha yako yaongozwe nae na sio miungu. Napenda nikufundishe kuwa kuna
maji ya upako, na asili yake ni maji ya chemchemi inayotoka kuzimu, unaponunua
unakuwa umenunua uchawi na tumekuwa tunawaombea watu wengi wanakuwa na mapepo
unapokuwa umekunywa yale maji, nguvu nyingine inaingia ndani yako na sio nguvu
ya MUNGU, maji yale ni ya ufalme wa giza. Kwenye biblia kuna mafuta ya upako ya
mzeituni ambayo hata YESU alipaka watu kwa kuwaweka wakfu na wafalme pia,
wafalme wote walikuwa wakiwekwa wakfu kupitia mafuta ya mzeituni na ile
mizeituni iliota pale Israel kwa wingi sana maana MUNGU alikuwa na kusudi na mwanadamu
ili akatakase vitu vyake na watu wake, na shetani nae huchuku mafuta na kuweka nguvu
zake, mti wa Mzeituni ulikuwa na kusudi La MUNGU, wakati mti unaota shetani
hawezi kuutamkia jambo lolote la kishetani, ila ukisha kuwa mafuta anatia nguvu
zake ndio maana utakuta mafuta dukani yanauzwa sh. 10,000 lakini kanisani
100,000 yanapokuwa yanauzwa hivyo ujue ina nguvu nyingine ya majini na maji
pia, nakufundisha na iko siku utakumbuka haya ninayokuambia, maji
yanawawamaliza, kwanini usilikubali neno la MUNGU na neno hilo likufungue?
Unajua maana ya manabii wa uongo ni kila mtumishi ambaye anafundisha neno la MUNGU
kinyume na kile ambacho kimeandikwa au anachopasa kifundisha, anahubiri uongo, kinywa
cha uongo, usitishwe na mtu ambaye anakuambia mpaka mambo yako ya ndani ukajua ya
kuwa huyu ndie mtumishi, la hasha! Hata majini yanaona na usipende sana
kutabiriwa tabiriwa maana watu wengi hupenda haya, mfano mtumishi anakuambia
Utakuwa hivi, utakuwa vile, mwishowe huwi na unakata tamaa utaona kuwa
ulichoambiwa kanisani hakikutimia ni uongo na utaona MUNGU hajibu kupe
ulitabiriwa uongo, na hakuwa MUNGU ila mwanadamu na majini yaliyo ndani ya huyo
mhubiri ili uridhishwe na hatimaye upotenzwe toka kwenye mikono ya YESU uwekwe
kwa yesu feki au kwa miungu.
MUNGU
anakupenda, YESU anakupenda na dini zingine wanamwita Nabii Issa na ndie aliyeandaliwa
katika ujio wa kuwanyakuwa watoto wa Ibrahimu ambao amemwamini ambao wamemkubali
akae ndani yao, wakati wa unyakuo atakutia nguvu upae nae na atakutia nguvu yamkini
utafufuka au atakukuta hai, watu wote watafufuka, wakristo na hata ambao sio wakristo
ndio maana MUNGU akamwambia YESU, ukifika wakati utakufa na utasulubiwa na utafufuka,
na YESU alipokuwa anawaambia wanafunzi wake ambao alikuwa pamoja nao, walikuwa
wakishaangaa kwa kipindi kile mda ule ulikuwa hajawadia ila muda ulipofika
ikatimia. Napenda nikufundishe kuwa kipindi ambacho ulikuwa bado hujampokea
Bwana YESU kuna mambo ambayo hukuyapata maana yesu feki alikuwa akikugandamiza
ila sas unapompokea YESU KRISTO AMBAYE NI MWANA WA MUNGU mambo ambayo ulikuwa unayaona
magumu yatakuwa mepesi na utakuwa mshindi, utafufuka, mbegu yoyote hufa na hufufuka
na wewe utafika mahali utafufuka, kila mkristo ana kristo ila je! Ni Kristo
yupi? Mara nyingi tunaambiana siku moja tutakutana wote kwa YESU, Mbinguni ni
kuzuri na mzigo wake mwepesi, Je! Endapo mtu ana hili jini la kikristo, na pepo
la kikristo au kiongozi wake kwa jina lake ndani yeke ndio huyo yesu mwingine
yupo tutafika wote pamoja? Tutakutana kweli huko mbinguni? Jibu ni Hapana,
maana wengine wataenda kwa YESU mwana wa MUNGU na wengine wataenda kwa yesu
mwingine ambaye ni kwa shetani, na ujue kuwa jini linakaa kwa mhubiri na pepo
linakaa kwa kondoo ambaye yeye anaongozwa na mchungaji kwenye jini kwa maana
pepo haliwezi kumshinda jini. Bwana YESU asifiwe! Hivi YESU akija utakuwa wapi?
Yuko YESU wa uongo, wa kutengenezwa, mwanadamu hujiita YESU, nk Je! Wao
walitabiriwa, walizaliwa na Maria?
Mchungaji
anaingia kanisani unasikia MUNGU, MUNGU, au YESU, YESU yule ni mwanadamu, unamuitaje
majina ya MUNGU? Ni kumchezea MUNGU wivu wa kumpenda YESU au MUNGU uko wapi?
Mbona mnaacha jina la MUNGU linatumika kinyume na mpango wa MUNGU? Na hao wote
Wanatoa fungu la kumi, wanaimba, hapo kuna baadhi wenye MUNGU, na wasio na MUNGU
usipoteze mda wako, kwa kuendelea kufanya ibada sehemu ambazo wamemwacha au kumwasi
MUNGU, rejea maana miaka yako imeliwa na madumadu, rejea mapepo yamekula, rejea
kwake, MUNGU anakupenda na anakuhitaji usibadilike, kwanini kufuata injili ya
namna nyingine, Injili isiyo na MUNGU wa kweli, nawaeleza kuwa haitafika June
2024 kuna mambo ambayo MUNGU atayafanya kwa ajili ya kutengeneza kazi yake na
kuokoa zaidi maana waumini wameshikiliwa na watumishi ambao sio wa MUNGU na hao
wameshikiliwa kama ATM mashine (yaana watumishi wanawafanya vijakazi vyao)
kanisani huitwi kondoo unaitwa pesa ukifikiri unapendwa kumbe wanapenda pesa
zako, Imeandikwa sadaka ni siri lakini mbona unaandika jina unapewa receipt na
usipotoa mzee wa kanisa anaulizia, atakuambia unadaiwa fungu la kumi kwa miezi
kadhaa Je! Hayo ni maagizo ya YESU kudai sadaka? Huyo yesu mdai sadaka ni YESU
yupi? Sadaka yapasa kuwa siri ya mtu na MUNGU hayo ni mafundisho ya yesu feki
au YESU mwana wa MUNGU? Baadhi ya viongozi wa dini wanasomea kazi ya MUNGU kama
uinjinia au udaktari lakini roho itendayo kazi sio ya MUNGU.
Tafakari njia zako na injili ambayo unaifuata ni ya Kristo Mwana wa MUNGU au ile iliyobadilishwa ya kristo Yule mwingine, namna ya kuelewa chunguza injili unayoisema / kufundishwa, Je! Unaabudu sanamu, unaibeba shingoni, unaruhusiwa kuibusu sanamu unaisujudia unaruhusiwa kufanya matambiko, unaambiwa kanisani katambikie kwenu namhubiri anakuambia katambikie, unabatiza watoto wadogo? Unabariki vijana au watu wazima, haipaswi kuwa hivyo, mheshimuni MUNGU, heshimuni na kutii maagizo yake, MUNGU ni MUNGU ambaye anapaswa aheshimiwe kuliko chochote, kuliko hata mfalme yeyote. Endapo unampenda MUNGU lakini ukawa unaendelea kufanya mambo ambayo ameyakataza ujue kuwa umetekwa kwa kujua na kutokujua na kwa kutotii ya MUNGU unakuta umefanya kazi za shetani, umejengea shetani kanisa, unapiga makofi kwa shetani. MUNGU ni wakuheshimiwa kuliko chochote, MUNGU na upako wake haufananishwi na wanadamu, ninatakuombea MUNGU akulinde na mwambie BWANA YESU azaliwe ndani yako, sema, YESU naomba uzaliwe ndani yangu na utasema endapo alizaliwa yesu yule mwingine afe, sema simtaki yesu feki, maana huyo yesu wa kutengeneza amekuwekea vifungo, laana, mikosi, MUNGU anasema yeye sio MUNGU wa wafu, wewe ni mara ngapi umeenda makaburini na kuwaombea waliokufa, unaenda kuwalilia wakusaidie unadhani kama hawajatubu wakiwa hai utawasaidia? Au mtu alieyekufa na yuko kaburini anaweza kukusaidia? La hasha!
SALA YA TOBA:
Sema; Bwana
YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozitenda kwa kujua na kutokujua,
Bwana YESU nakushukuru kwa sababu nakupenda na nakuomba mwana wa MUNGU wa pekee
uliye kwenye kiti cha enzi, na nilitamani uzaliwe ndani yangu na nakupenda
lakini kabla yako alizaliwaga mwingine, naomba uingie ndani yangu vunja vya
huyo mwingine ambaye alizaliwaga ndani yangu, vunja na unyang’anye vyote
vilivyo vyangu, mnyang’anye hatima yangu maana sina urafiki nae na neno lako
linasema katika Wakorintho 2:6-17 Tokeni kati yao mkatengwe nao ninaomba
nikatengwe nao, najua ninaishi na watu na siwezi kukimbia kuishi nao ila
nikatengwe na mambo mabaya katika ulimwengu wa roho na mwili na sishiriki tena ibada
za kupinga maagizo ya MUNGU kwa jina la YESU, nimekuudhi sana naomba nisamehe, nilidanganywa
sana, nililipa mikopo ambayo kanisa ndio lilikopa na kanisa linamwakilisha MUNGU,
na MUNGU hakopi anafanya kazi yake kwa kutumia wanadamu pasipo kukopa, nilikuwa
mzee wa kanisa na kufanya mnada kanisani nilikuwa nadhani ninakupendeza kwa kufanya
mnada kumbe nalichafua kanisa lako, YESU ulisema nyumba ya baba yangu haipaswi kufanywa
soko, na mimi ninajua ni helaku lako na nilifanya soko, naomba unisamehe,
nafuta maagano hayo na mashitaka hayo kwa damu ya YESU, ninajitenga nao kiroho
na kimwili, rohoni, kwenye damu na kwenye nafsi, BWANA YESU naomba unisafishe
na naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, Bwana
YESU ninakushukuru, ninakupenda sana.
BABA ninakushukuru, ninaiona damu ya Mwanao YESU Kristo ikipita, ikiwasafisha, YESU akakuponya,
akufungue, akuweke huru katika jina la YESU, nguvu ya mapepo itoke, majini yakuachilie,
majini upako yatoke katika jina la YESU, maji ya upako yatoke ndani yako,
uponywe kwa JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI, ukawe huru kwa jina la YESU pokea
uponyaji. Chochote ambacho kinakusumbua kiondoke, napiga majini yote ya
madhabahu ya upako wa shetani, malaika wa MUNGU wakakufungue, majeshi ya
wapiganaji toka mbinguni wakakupiganie wewe ambaye YESU amezaliwa ndani yako,
majini yanayokugandaniza usiku yasikurudie tena nakuombea kibali chako MUNGU
akifungue, kwa jina la YESU. Nguvu za uchawi, za majini, za mapepo ya level
tofauti tofauti yatoke kwa jina la YESU, jini ulililowekwa na mhubiri wa
kipepo, jini la dini kwa jina lake likutoke kwa jina la YESU na ukawe huru,
mikono yako irejeshwe, aliyefunga nyota yako ifunguliwe kwa jina la YESU
maagano yeyote ya damu au chochote yanayonena juu yako nayanyamazisha kwa jina
la YESU na ninaomba kwa ajili ya Baraka zako za mwilini na rohoni zifunguliwe
kwa jina la YESU na kilichokutangulia kinyume na mpango wa MUNGU kiondoke kwa
jina la YESU pepo la kumchukia MUNGU likutoke na pepo la kumchukia BWANA YESU
likutoke kwa jina la YESU. Pepo la kuchukua kweli ya MUNGU likutoke kwa jina la
YESU. Kinachoshilikia kichwa chako kikutoke kwa jina la YESU. Nakuombea upako
na miguu yako kila utakapokanyaga ufanikiwe, ukikanyaga mitego ya shetani
isikudhuru kwa jina la YESU MUNGU akurejeshee miguu yako kwa jina la YESU, kwa
ambaye amefungwa kwa agano laardhi kuwa hautafanikiwa, ardhi mtumishi wa MUNGU
nakuamuru fungua Baraka juu ya mtoto wa MUNGU anayesoma somo hili mda huu kwa
jina la YESU KRISTO wa Nazareth aliye hai.
Mabaya yaondoke kwako na anayetumia kiungo chako chochote akafanikiwa hata kama amekufa akuachilie na vitu vyako virejee kwa jina la YESU naomba sasa kwa ajili ya karama zako, yesu wa aina nyingine namkatilia mbali, namtenga na wewe kwenye ulimwengu waroho na damu na nyama, namtenga na mali zako na vitu vyako na YESU KRIST0 WA NAZARETI akutawale siku zote za maisha yako yote. Majini ya kuzubaa yakutoke, na damu ya YESU iendelee kukusafisha na majini yaliyotumwa kukuangamiza na yachoma, hakuna uganga wala uchawi juu yako, kwa jina la YESU, yapo mafuta yenye nguvu za MUNGU na yapo ya shetani pia, maji, vitambaa, udongo wa upako ukuachie kwa jina la YESU vitu hivyi vimewafanya baadhi wa wakristo kuviamini na kuvitunza bila kujua ni hirizi ambazo umepewa na baadhi ya hao wahubiri ambao wanatumia vitu hivi kwa maagano waliopewa na shetani ili wakuteke wewe na wakutenge na MUNGU, kataa na hayo majini yakuachie na vitu hivi navitenga nawe kwa jina la YESU ukawe huru na umtumaini YESU KRISTO WA NAZARETI. Kila jini linalofuatilia PESA au company yako likauwawe Kwa jina la YESU BWANA YESU akuweka huru, akakupe amani, ukamilifu wa BWANA YESU, leo ukapate yale yote ambayo yalichelewa, ni wakati wa BWANA YESU ambapo waamori na wafilisti waliokutesa wakuachilie BWANA YESU anawamaliza wote; ni wakati wa wanaoshindana na wewe; wanakwenda kurudi nyuma na uliyefunika maisha yako ufunuliwe, uonekane sasa, ubarikiwe, uinuliwe uwe na kibali, BWANA YESU akufungue katika jina la YESU. Ninawapenda msimame imara hakuna kutumikishwa na ni maombi yangu nakuombea mkono wa BWANA YESU uwe na wewe sasa hivi na mambo yako mwaka huu yawe safi MUNGU aendelee kukubarki na kukutunza.
Nakutenga na
upako na wa shetani na majini ambayo yalikufanya uteseke na ukawa hivyo manaa
kila aaminiaye hupokea na wewe uliamini ikawa hivyo, sema kama nilipokega vichafu
sivitaki tena na moyo wangu nakukabidhi BWANA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU.
MUNGU
AWABARIKI.
MTUME NA NABII HEBRON WILSON KISAMO