Pages

Sunday, December 24, 2023

 

MERRY CHRISTMAS 2023 AND A HAPPY NEW YEAR 2024.

 

BWANA YESU ASIFIWE!

Nawatakia heri ya Krismasi na mwaka mpya wa ushindi mkubwa wa wokovu.

UJUMBE KUTOKA KWA YESU:

Mumpokee yeye ili mrithi ufalme wa mbinguni, mrithi neno lake la kweli, ubatizo wake wa kweli na ubarikio wake wa kweli. Msidanganyike na mafundisho ya uongo, yatawarithisha kwa yule mwovu.

“ Ubatizo niliourithi mimi YESU ni ule wa uliyotoka mbinguni kwa nini baadhi yenu hamtaki kuurithi ubatizo huo? mnarithi batizo siyo za BABA yangu, haijalishi mnatumia jina langu, mmerithi ubatizo wa yule mwovu na huo ubatizo ni kiapo cha yule mwovu, mbadilike mrejee mkafuate ubatizo wangu, mrejee ndipo mtaurithi ufalme wangu, tofauti na hapo utaurithi ufalme wa shetani kwa kujua au kwa kutokujua. Nimewajulisha habari hizi kupitia mtumishi wangu awaeleze ulimwengu wote; ninakaribia kurudi kwa mara ya pili kama neno lilivyoandikwa. Lakini nikiiangalia ulimwengu wengi wamerithi viapo vya shetani ambavyo siyo vyangu ni vya shetani kwa hiyo sina uhalali nanyi bali shetani ana uhalali nanyi; na MUNGU ni MUNGU wa haki kiroho na hata kimwili. BABA yangu akiangalia, wanadamu wengi wananipenda lakini wameshikwa na viapo vya ibilisi. Nimemtuma mtumishi wangu, atakayesikia asikie na asiyesikia asisikie.

Mimi YESU nilibatizwa katika maji yanayotembea na alitumwa Yohana anitengenezee njia na niliirithi hiyo. Wanafunzi wangu waliirithi na watu wengine wakaendelea kuurithi. Lakini baadhi ya watu wengine wameendelea kurithi ubatizo wa kikombe, wa kisima, wa vumbi, kwa jina la mchungaji na nyinginezo nyingi tofauti na huu kutoka kwa BABA yangu mbinguni, na vyote ni viapi ambavyo siyo vya BABA yangu; mnarithishwa vingine na kupigwa upofu. Nilikuja duniani ili muurithi wokovu, lakini baadhi hamuitaki mnahangaika tu kujiita mfuasi wangu kama vile yule mpinga kristo anavyojiita.

Riithini ubarikio wa kwangu; watoto wadogo ndo wabarikiwe na siyo watu wazima. Wengi wameurithi ubarikio ambao siyo wa kwangu kwa hiyo sina uhalali nao mpaka uvunjwe na wanirejee mimi.”

 

SALA YA TOBA:

BWANA YESU ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, na pale niliporithi mambo ya shetani na siyo ya kwako ninaomba unisamehe. Ninaomba uniondolee viapo vyote vya shetani nilivyoapishwa kwa kujua na kutokujua na kunitoa katika uhalali wa shetani. Ninaomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima na ufute jina langu katika kitabu cha hukumu. Asante BWANA YESU.

 

PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.