YESU ALISEMA
NA HAO ADUI ZANGU WASIOTAKA NIWATAWALE WATACHINJIWA MBALI.
LUKA 19:27
BWANA YESU ASIFIWE, YESU mfalme mwana wa MUNGU wa pekee
aliye bora kuliko viumbe vyote vya mwenyezi MUNGU aliyeumba mbingu na nchi. Hiki
ni kipindi cha hatari ambacho tunatarajia YESU aje kulinyakua kanisa lake au
wale watu wake ambao wamekubali kutawaliwa na YESU na kuokoka kwa kumkiri yeye
sawa sawa na neno lake katika kitabu cha Warumi 10:9. Napenda mlijue hili kwa
wale wanaofikiria YESU atabakia kukaa kimya tu atakaporejea katika ile siku ya
hukumu ambayo yeye mwenyewe atakaa kwenye kiti akihukumu kila aliyemkataa na
yeye atamkataa kama MUNGU alivyomkataa shetani na ndivyo YESU atakavyowakataa
waliokataa asiwatawale walivyokuwa hapa duniani na hata wakifa.
Roho ya kukataa kutawaliwa na MUNGU ilianza kwa shetani na
ndivyo akatengwa na mbingu mpaka sasa na milele akafuatana na waasi wake ambao
walikataa kutawaliwa na MUNGU wakamtii shetani akawatawala na baada ya kumtii
shetani wakatupwa kuzimu mpaka leo, wakabakia mbinguni wale waliokubali kutawaliwa
na MUNGU aliyeumba mbingu na nchi na viumbe vyote. Baada ya hilo anguko shetani
akawapoteza wanadamu wamkosee MUNGU kama alivyomkosea yeye ili mwanadamu apate
kutawaliwa na shetani badala ya MUNGU. MUNGU akamtuma YESU kutoka mbinguni aje
afanyike upatanisho kwa njia ya kumkiri YESU ili YESU akutawale usiwe adui ya
MUNGU bali uwe adui wa shetani, lakini cha ajabu kumetokea wapotoshaji wenye
roho za shetani, ambao baadhi yao wameshatawaliwa na shetani baadhi wakijua na
wengine pasipokujua wakitumia jina la YESU na neno lake lakini hawawaruhusu
watu wamkiri YESU kabisa, wajiite wakristo tu, waende kanisani linaloitwa kwa
jina la kristo ila wasijaribu kuokoka.
Cha kujiuliza mataifa yote na kama unayo akili timamu kabisa
je MUNGU alimtuma YESU kwa nini? Je dunia ingekuwa sawa angekuja kufanya nini? Angebakia
mbinguni wala asingesumbuka wala kuja
kuteseka katika dunia hii yenye dhiki na taabu tele. Shetani akawatawala baadhi
ya watumishi na akaanzisha makanisa anayoyatawala yeye pasipo watu kujua au kwa
kujua kwa kujificha sana, akaweka mapokeo yake ya kuchanganywa na neno la MUNGU
kwa mtego wa kutega watu wasije kwenda mbinguni. Bila kuokoka ina maana utakuwa
adui wa YESU au umeshakuwa adui bila kujua au kwa kujua.
Ni kwa jinsi gani unaweza ukawa adui wa YESU bila kujua?! Iko
hivi hutaki kuokoka, YESU alikuja kuokoa kilichipotea au kupotoshwa na shetani.
Akatumwa YESU ili ile siku ya mwisho asiwepo mtu atakayekuwa na cha kujitetea
yeye ni MUNGU wa haki na anatenda haki kumtuma mtoto wake atuletee habari njema
ya wokovu lakini cha ajabu wapo wenye miguu ya mabaya wanaopeleka habari mbaya
yaani kuhubiria watu wasome neno tu, waende ibadani na hamna kuokoka. Sasa niwaulize
mataifa je wokovu unaupataje? Jibu ni kwa kumkiri YESU au kwa kuongozwa sala ya
toba na mtumishi ambaye tayari amekubali kutawaliwa na YESU mtakatifu wa
mbinguni. Ukiwa hujaokoka hata maombi unayoomba kwake ni kazi bure maana
utamwombaje yeye usiyekubali akutawale? Hatua ya kukutawala ni pale unapokiri
sala ya toba, hapo ndio mwanzo wa kuondoa utawala wa giza katika maisha yako
ukifanyika kuwa mwana wa MUNGU. Usikubali kukaa kanisani bila kuokoka utakuwa
bado ni adui wa YESU, na adui wa YESU wote katika ile siku ya mwisho
atawahukumu ajuavyo yeye akiwa kwenye kiti chake cha enzi yake, atakuja
kuwafyekea mbali au chinjia mbali kwenda jehenamu kama alivyofukuziwa mbali
shetani na malaika zake. Sasa unangoja nini? Unajitia moyo kuitwa mkristo tu
ndio utaenda mbinguni. Napenda kuwakumbusha YESU alisema watatokea makristo
wengi na watawapotosha wengi kupitia jina lake, hata sasa imeshatimia.
Dini baadhi wanajiita wakristo lakini hawataki kukiri wokovu
au kwa lugha nyingine hawatawaliwi na YESU wa mbinguni bali wametawaliwa na
Yesu mpinga (mpinga kristo). Na kama hawatawaliwi na mpinga kristo sasa kwa
nini wanakataa kumkiri YES? Hapo mwenye skio na asikie na mwenye macho apate
kuona na mwenye ufahamu akapate kufunguka. Auelewe ukweli na ukweli ukamweke
huru aepuke kuwa adui wa YESU kuanzia sasa na hata katika maisha ya baadaye.
YESU atakuja mara ya pili na kila kilichoandikwa lazima
kitatimia tu. Nimewaandikia watu wa mataifa yote mpate kujua siri hii ya
kutawaliwa na YESU itakufanya usiwe adui yake na pia utakuwa rafiki yake na
hata katika ule mwisho akija YESU katika unyakuo atawanyakua marafiki zake tu
waliomkubali na kumkiri tu hata mnaykua adui yake. Neno linasema itakuwa siku
ya kilio maana watu watapotea au jamaa hutawaona tena watapaa na mawingu wameshinda
kuokoka.
1.
AINA ZA MAKANISA ANAZOTAWALA YESU.
2.
AINA ZA KANISA ANAYOTAWALA SHETANI (MPINGA
KRISTO).
AINA ANALOTAWALA
YESU:
Yafuatayo
yanafanyika;
Ø Watu wote
wanamkiri YESU (Sala ya Toba).
Ø Ubatizo- wa maji
mengi ya mto yanayotembea.
Ø Mtumishi ameitwa
na YESU.
Ø Maombezi ni bure
hamna kudaiwa malipo.
Ø Sadaka haziandikwi
majina wala kupeana risiti.
Ø Barikia watoto tu
na batiza watu wazima.
Ø Zipo aina ya
huduma tano alizozileta YESU.
Ø Neno la kweli.
AINA YA MAKANISA
ANAYOTAWALA SHETANI (MPINGA KRISTO).
Ø Hakuna kuokoka
wala sala ya toba.
Ø Ubatizo wa
kumwagiwa maji kichwani, ubatizo wa baharini, ubatizo wa drum, kisima, kubatizwa
kwa jina la mchungaji.
Ø Mtumishi anajiita
au aliasi kwa YESU.
Ø Maombezi ni pesa
lazima ulipie.
Ø Sadaka unaandika
jina, unapewa risiti, au cheti cha hongera mtoaji.
Ø Wanabatiza watoto
wadogo kwa maji kumiminiza kichwani siyo kama alivyobatizwa YESU. Neno batizwa
ni kuzamishwa sasa hicho kikombe ni UONGO
mkubwa mbele ya macho ya watu na MUNGU
ni tendo la uongo, haja utawala YESU bali ni shetani ndio katawala. Mfunguke macho.
Siyo kila roho ni za kuamini; zijaribuni kama ni roho za MUNGU halafu zipinge maagizo
yake.
Ø Zina huduma sita.
Ø Neno limechanganywa
na uongo. (Ufunuo 22: 18-22).
Ø Kanisa lake
linakopa benki ili liweze kujenga kanisa yaani Mungu wake ni maskini ni lazima
aombe mahali achajiwe riba.
Ø Kuna sanamu, wanaomba
wafu.
Ø Jina la YESU
linatumika kama ni nembo ya biashara ule uhalisia wa YESU haupo.
Ø Uchawi, miujiza
ya kishetani..
Ø Ule mwisho wao
watapelekwa kwenye mbingu ya shetani alipo kwa sasa na watakuwa watu wote ni
adui wa MUNGU pasipokujua.
ANGALIZO:
Ni
bora uujue huu ukweli utakusaidia kumrejea YESU na kumng’ang’ania kabisa hata
kuzikimbia hizo nyumba za ibada zinazokufanya uwe adui wa YESU au madhabahu za
kukufanya uwe adui wa YESU pasipokujua au kujua. Leo kwa neema yake amenituma
Nabii Hebron Kisamo ninawafudisha nchi zote kuhusu ujanja huu wa shetani, isije
ikatimia kwako katika siku ile ya mwisho ukijitetea mbele ya YESU na
ukajishangaa kwa nini anakuambia sikujua wewe hata kama ulinitumikia. Ondoka zako
ukatupwe huko, ulivyokuwa duniani hukutaka nikutawale.
TUBU:
BWANA
YESU naomba unisamehe natubu dhambi zangu naomba unandike jina langu kwenye
kitabu chako cha uzima wa milele ninamkataa shetani na mambo yake yote. Naomba usiwe
adui yangu nimekukubali wewe ndiye bwana na mwokozi wangu milele, unitawale
wewe, mimi siyo mali ya shetani katika jina la YESU Kristo wa Nazareti
aliyekufa na kufufuka na kupaa mbinguni.
Ujumbe
huu watumie na wengine na kwa njia hiyo utazidi kuwa rafiki mzuri wa YESU.
NABII HEBRON
WILSON KISAMO.