UJUMBE KWA MARAIS WA AFRIKA KUTOKA KWA MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA DUNIA NA VIUMBE VYOTE.
BWANA YESU ASIFIWE. Nawasalimu marais, wafalme wote wa bara
la Afrika kwa jina la YESU mwana wa MUNGU wa pekee aliyeko mbinguni kwenye kiti
cha enzi ambaye pia ndiye mkombozi wa ulimwengu huu aliyeteuliwa na MUNGU wa
Ibrahim, Isaka na Yakobo, ambaye ndiye Alfa na Omega wala hakuna anayefanana na
yeye. Yeye alikuwepo hana mwanzo wala mwisho, na ndiye aliyetuumba sisi wanadamu.
Mnamo mwaka jana mwezi wa Septemba alisema na mimi kuhusu
bara la Afrika, akaniambia wewe nimekuita Nabii wa mataifa na nitasema kupitia
wewe katika kila taifa, kila bara kwa wakati wake ili niukomboe hii dunia
kutoka kwa huyo mwovu. Nitakutumia kuponya nchi, mataifa, mabara kama chombo
changu, nyakati hizi ni za hatari sana na adui anajua kuwa wakati wowote
mwanangu YESU atarudi katika unyakuo ila hajui siku wala muda hiyo ni siri
yangu hata mbingu yangu haijui ni lini. Useme
na bara hili la Afrika, uwaeleze yafuatayo maraisi wote wa kila taifa yafuatayo
yaliyotoka kwangu mimi MUNGU, atakaesikia atapona ila atakayekaza shingo yake
MUNGU atapambana na yeye. Mimi sijui ni kivipi nina nukuu kama ilivyo siwezi
wala kupunguza neno la MUNGU au agizo lake.
Mimi ndiye niliyeumba mataifa yote na kila bara ninakusudi
lake nililoliweka kwa utukufu wangu. Nayapenda mabara yote. Anza Afrika kwa
nini ni maskini wakati niliwawekea utajiri mkubwa? Watoto wake wengi katika
nchi la Afrika wamekuwa wakimlilia MUNGU wakiuliza ni kwa nini wamezaliwa
Afrika? Wakiona au kufikiria MUNGU haipendi Afrika au anaupendeleo na mabara
mengine ndio sababu yanaendelea. Akaniambia anza sasa uwaeleze yafuatayo ila
mengineyo ni yako mwenyewe niliyokuambia katika bara hili.
·
Waeleze baadhi yao wanirudie mimi MUNGU ili
kupitia wao niziponye nchi zao ikiwa kama watakubali na kutii.
·
Wawe na uchungu na uzalendo maana baadhi yao ni
waizi wanauza nchi kwa mataifa mengine wakijua na wengine hawajui.
·
Afrika hapo mwanzoni ilitawaliwa na wakoloni na
wakoloni hao walitajirika kupitia Afrika wakazijenga nchi zao, sasa baadhi ya
wao kuondoka nchi zikapata uhuru, wakaja na mtindo mwingine ya kutawala
kiuchumi.
·
Wakazizuia nchi za Afrika zisiendelee na
kujiendeleza kiuchumi kama kuwa na viwanda vingi, kuzalisha mafuta (kuchimba
petrol) na natural resources.
·
Wakawawekea vikwazo wakikopa wanawapa masharti
ambayo yatawafanya wawe watumwa wa kile chochote watakachokitaka kwenye hiyo
nchi lazima watii agizo lao na wasipotii basi watakuzima.
·
Baadhi ya nchi Afrika zimenunuliwa kupitia
misaada. Ipo ya aina mbali mbali ikiwemo ya kisiasa kusaidia vyama vya siasa ili
ukiingia madarakani hicho chama kutii maagizo ya mfadhili, nikisema vyama siyo
vyote ila wapo wengi tu.
·
MUNGU hapendezwi na hiyo roho na tabia ya kuomba
omba kila siku misaada, mikopo ya ajabu ya
hizo nchi. Kila rais ajue anayo dhambi juu yake. Kiongozi lazima awe na
hekima ya kuongozwa kutoka kwa MUNGU na siyo hekima ya kimungu.
·
Baadhi ya wakoloni kwa sasa wamelitawala bara la
Afrika kiuchumi bara hilo linyanyuke sababu
wanajua kabisa Afrika ndiko wanapopatia raw materials na viwanda vyao,
walivyovijenga huko kwao sasa ikiwa Afrika itatumia raw material zake ikaweka
viwanda vikatengeneza mali hafi wao hawatauza maana soko lao litakufa sasa ili
lisife ni lazima tumlinde Afrika kwa vikwazo na mikataba ya kujifunga miaka
nenda miaka rudi. Sasa anayeshikiliwa ni rais au mfalme au mkuu wa nchi hiyo
wakishamfanikisha au wakampa pesa au kumnunua wafanyayo hayo ndipo taifa
linakuwa chini ya vikwazo vya kutoendelea kiasi kwamba utashangaa taifa lina petrol
lakini ili lichimbe mpaka lipewe kibali na nchi za nje. Huu ni ujinga na
kupungukiwa na akili. Petrol ipo nchini mwako ukichimba wanakukalia vikao ulaya
eti unaharibu mazingira. Hivi mbona huko kwao wanachimba na hawapingui? Utaona mfano
mafuta yaliyochimbwa Uganda nchi za Afrika hazipingi ila utaona baadhi za Ulaya
zinapinga na kuweka vikwazo. Je hii ni halali nyie viongozi wa Afrika? Imefika pabaya
mpaka MUNGU anaamua kusema nanyi je hii ni akili kweli? Lini Afrika itaendelea?
Kwani Waafrika mnafikiri hamwezi kufanya? Mnaweza tena zaidi. Mlikaa kutegemea
wazungu tuu. Wao walijituma na wanafanya kazi na sisi tunakubali kabisa
kuzuiliwa kufanya maendeleo yetu.
Kama rais Yoweri Museveni asingesimama imara mafuta yasingechimbwa
hapo Uganda ila amefanya vizuri sana.
Congo ni nchi ambayo utajiri wake ni mkubwa sana unazidi
bara la Amerika lakini angalia maisha ya Wakongo (Zaire). Watawala hao wa
kikoloni walibeba mali wakapeleka kwao. Sasa wanachokifanya wanajua Congo
ikaendelea ikajenga mfano viwanda vya simu, wao wanaochukua raw material watafunga
viwanda vyao siri ya vita ni vita vya uchumi. Utashangaa hapa majeshi nani
anyesaidia kupigana na nchi hiyo? Pesa, silaha nani anawapa? Mjiulize lakini
mnajua ukweli marais baadhi yenu mmekataa kusema kweli mmeshirikiana
kuziangamiza nchi zenu kwa kujua na kutokujua.
Mfano:
Kwa nini Congo vita haziishi? Na vinafadhiliwa na nani? Vita
hivi ni kwa ajili ya kuwavuruga Wakongo wasiwe na amani wakatulia. Wakijenga viwanda
kwa raw material zao hao wanaochukua hizo raw materials hawatapata tena na
watafunga viwanda vyao, sasa ni lazima wafanye mjue zote kulishirikisha nchi inavurugu kila wakati japo siyo nchi
zote za nje zinakusudi baya na Congo.
Afrika Magharibi hivyo hivyo Libya waliomua Gadafi ni hao
hao sababu walifadhili vita. Afrika amkeni. Siyo kila ufadhili unayokuja
au kupewa kwa lengo jema lina kusudi baya, wakishamaliza kusudi lao kuwavuruga wenyewe
kwa wenyewe, wao wana starehe kwao nyie
mnabakia na matatizo na umaskini japo nchi yako inautajiri ya asili
aliouweka katika nchi hiyo na hiyo ni mifano michache tu. Kwa kweli kila rais
atafakari aone ni wapi pa kujirekebisha tena na kutubu kwa MUNGU. Usione unatembea
na msafara na heshima unazopewa zitakupa kiburi usimtii MUNGU.
Niulize swali hao waliotangulia marais miaka yote, wengine
wamekufa kumbu kumbu lao hamna wala heshima waliyoipata haipo tena, bali ni
kusubiria hukumu. Na msidanganyike mtaombewa na nchi nzima ukifa utapokelewa siyo hivyo tubu sasa yeye siyo MUNGU wa wafu.
Kwenda kuomba omba msaada muone ni aibu na wanajua mnapenda
misaada dada ili mvipate msaini masharti yao kuna mfano yapo sana ikiwa MUNGU amekataza akasema ole wao
wafiraji wanaofanya hayo hawatauona ufalme wa MUNGU (1 Kor 6:6-9) usome. Yaani mnalazimishwa
kukubali hayo machafu kuwaangamiza wananchi wenu waanze kuyafanya. Kuyakubali ili
mpewe pesa za mikopo au bure mje kuangamiza wananchi. Utakaye saini hiyo dhambi
inatembea na wewe.
Mkicheza iko siku watabadilisha sheria hakuna kufanya tendo
la ndoa kama asili yake bali mwanamke afanye tendo la ndoa kwa mdomo wake tu.
Afrika haya mambo hayawaumi nyie baaadhi yenu marais?
Fanyeni kazi, uvivu ni laana, Afrika imebarikiwa sana na
MUNGU. Najua ikiwa rais atasimama imara na taifa lake atapingwa na Ulaya na
kupingwa kwake ni ili waje waibe.
Umoja wa Afrika msimame imara nyie ni wabarikiwa mna nguvu. Msifikirie
mnapendwa na wote, wanapenda raw materials zenu. Fungueni viwanda, acheni vita,
fungueni soko la Afrika.
Mwakwepe vibaraka ambao ni mawakala wa vita Afrika-
wakalisheni waache. Wale wanaoiba waache maana hawatakubalika na MUNGU kama ni
viongozi na wamekuwa wakitembea na laana ya MUNGU nchi na wana nchi.
Mtende haki, msiue wananchi bila sababu. Msitumia madaraka
na nguvu kutafuta kutawala, mkumbuke mtawala mkuu ni MUNGU.
Napenda ujue yapo baadhi yenu mnajua kuwa vita ni RAW
MATERIAL.
Fungueni viwanda sababu mnaweza na siyo kwamba hamwezi.
Msikubaliane na masharti na mikataba mibovu itakuwa ni laana
kwako na hata kukuzuia kufika mbinguni.
Mtoke kwenye group la omba omba, wenye shida, umaskini. Mpambane.
Ulaya wanashirikiana, why not Afrika yote?!
Mjielewe nyie ni wabarikiwa ila mmefanywa wenye uhitaji
sababu wametengeneza mfumo wa vita ya kiuchumi na hawatakubali nyie kuwa juu
ila mkikubali na kutii itakuwa.
Nawapenda sana marais wote wa Afrika. Nawaombea. Amen.
MTUME
NA NABII HEBRON.