KUTENGWA NA ROHO YA ASILI YA UKOO
NA FAMILIA.
WAGALATIA
3:12-14 & 1WAKORINTO 15: 42-49.
Roho
ya asili ya ukoo ni nini?
Ukitafakari
watu wote tuna ukoo (mfano: Massawe, Mwanga, Mbise) katika ukoo kuna nguvu
ya asili ya ukoo na kuna roho ya asili ya ukoo. Mara
nyingi tunaongelea kabila flani lina tabia flani hizi ni roho za asili za
koo, unakuta asili yao ipo inatembea nao kizazi kwa kizazi imerithishwa
kutokana na maagano.
Mfano
katika koo flani kuna asili ya kufa haraka, kila mwaka familia inazika au kuna
ugonjwa wa kurithi, kisukari kinatembea kwenye familia uzao baada ya uzao na
mnawekewa roho ya kuikubali na kuona hali ya kawaida “kwetu
wanasumbuliwaga na kisukari ni ugonjwa wa familia tu.”
Hapo
ni kujiuliza kuna agano gani koo yako imeweka inayotembea juu ya familia yenu? Unatakiwa
kuvunja hilo agano nakumpa YESU maisha yako akusafishe kiroho na kimwili.
Roho
za asili za koo ni maagano walioingia mababu wa miaka elfu iliopita ambao ni
mizimu (watu waliokufa na hawajaenda mbinguni). Kuna kuwa kuna mila wameziweka
na kuzifwata na kurithisha kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha nne. Na
baadhi ya mila au tabia mbaya za asili ni:
•
•
Uzinzi - unakuta babu alikuwa na wanawake wengi, hiyo roho inatembea kwenye
familia huwezi tulia na mwanamke mmoja ndani au nje ya ndoa.
•
•
Kuchinja wanyama kwa ajili ya Ibada - Ni mila na desturi zimekuwa zikifanywa
toka miaka ya nyuma na imebaki kuendelezwa na familia wakimwaga damu na pombe
katika makaburi ya wazee waliokufa.
•
•
Uchawi - wakiamini mizimu ya ukoo inawasaidia, kuwashirikisha, kuwaomba ruhusa
kabla ya jambo lolote na kurithisha hiyo roho katika familia.
•
•
Hakuna kuokoka - Watu wamekuwa wakikiri “mimi ni wa dini ya baba yangu na
mama yangu, sihitaji kuokoka.” Kwa kujua na kutokujua wanajifunga katika
roho za asili za koo.
Wagalatia
3:13 KRISTO alitukomboa katika laana ya torati. KRISTO alikufa kutuokoa
na hii laana ya roho za asili lakini bado kuna watu hawataki ziachilia/
kutengwa nazo.
•
•
Kiburi cha ajabu kikiambatana na hasira kali sio mtu wakuambiwa na kutii kuna jeuri
isio ya kawaida.
Lazima
utengwe na hizi Roho uwe wa ukoo wa YESU, kwa kukataa asili ya ukoo na iondoke.
Jambo
lingine, unakuta mtu kuna tabia unakuwa huzipendi; tambua kila kabila zina
tabia zake na kuna roho za koo zinakulinda ili ubaki kuwa wa kwao na usiende mbinguni.
Unatakiwa utengwe na mizimu ya koo na mizimu ya jina lako kwani majina
yakurithi yanakuja na tabia na roho yake.
Mwambie:
MUNGU
ninakupenda lakini kuna vitu vinanisumbua ila wewe ni mfinyanzi, Naomba
unifinyange.
Njia
ingine ambayo roho za asili zimetumia kushikilia watu ni kupitia zinaha. Mtu
mmoja anakuwa na roho za asili za koo mbali mbali kutokana na aliozini nao,
umezini na watu wa kabila tofauti wenye tabia tofauti nguvu na roho iliojuu yao
ina ambatana nawe. Unakuwa ni mtu mwenye tabia za ajabu kwa kujua na kutokujua.
Baadhi
ya dalili umeshikiliwa na roho za Ukoo:
•
•
Kwa aliyeokoka unakuta kabla hujaokoka mambo yako yalikuwa yanaenda vizuri
lakini baada ya kuokoka kuna kuwa na ugumu na kazi haziendi vizuri. Hapo kuna
kuwa na nguvu ya ukoo inapinga wokovu na kufunga maisha yako wanakuwa
wanakulinda wakidai wewe ni wa ukoo wao na siyo wa wokovu.
•
•
Mfano mwingine: Unapokuwa umeoa kabila lingine tofauti na mila na desturi zenu,
vita vinainuka kuna kuwa hakuna maelewano kutokana na roho ya asili ya koo
inakuwa ina nguvu juu ya hiyo ndoa.
•
•
Pia unapokuwa unaota waliokufa (Mizimu) zile roho zinakuwa zinakushikilia
usiende mbinguni “Unatakiwa kuvunja uhalali walio nao juu yako.”
Ukitafakari
kabla ya elimu, mila na desturi zilikuwa zimetawala kwenye kila kabila na vitu
vingi vya ajabu vilikuwa vinafanyika wakiamini ni mizimu yao inawasaidia.
Lakini MUNGU alitumia elimu kutufungua na tabia na mila za koo.
Na
sasa mwambie:
MUNGU
nina rejesha vyote vilivyochukuliwa na roho ya asili ya ukoo nikawe huru.
Na uzidi kukataa roho ya asili kwenye kila kitu
chako; elimu, ndoa, mtoto, kazi.
MTUME NA NABII HEBRON.