KUVUNJIWA AGANO LA DAMU.
Waebrania 9: 15-22, Zaburi 89:3-4, Mwanzo 25:24-33.
Waebrania 13:20 na Mathayo 26:26-30.
BABA ninakushukuru kwa neno lako na
mapenzi yako, ambalo umepanga kwa ajili ya viumbe vyako na kanisa lako ili
kulifundisha, kulijenga, kuliponya, na
kulivusha hatua nyingi zaidi mbele, nakushukuru kwa sababu unamjua kila mmoja na sisi tu viumbe vyako na
unafahamu kuwa ni jambo gani au kifungo gani au ugonjwa upi ambayo unawasumbua
watoto wako na unajua ni namna gani ambavyo utawafinyanga, wapo wanaolia, wapo
wanaonyanyaswa, wanaopingwa na vitu wasivyo vijua na wapo ambao adui hataki
waishi lakini wewe unataka waishi, BABA ninaomba injili yako na neno lako likafanye
mapenzi yako na kumwaibisha yule ibilisi, ninavunja kila kusudio la shetani kwa
watoto wako na ninaamuru mapenzi ya shetani yashushwe chini na utukufu wako
MUNGU ushuke juu ya watoto wako.
Agano la damu limekuwa likitesa watu sana, maisha ya wengi
yamekuwa ndivyo sivyo; na baadhi anachukulia kuwa ni hali ya kawaida, wakiona
ndio sahihi kumbe sivyo,
Agano – Kipindi cha MUSA vitu vyote
vilikuwa vikisafishwa kwa damu, yaani kulikuwa na sadaka za damu; kama
alivyofundishwa na MUNGU. MUNGU alifanya agano na wana wa Israel kupitia agano
la damu ya wanyama, lakini pia katika agano jipya MUNGU alifanya agano la damu
kupitia mwanaye Bwana wetu YESU Kristo, ndio tuko nalo hata sasa, hatuko katika
agano la damu za wanyama tena tupo katika agano la damu ya YESU. YESU alifanya
agano na wanafunzi wake la kunywa damu kupitia mzabibu, akasema hivi sitafanya
tena hapa dunia mpaka tena kwa BABA yangu kule mbinguni.
Agano ni mkataba na agano linakuwa
limegawanyika, kuna agano la kiapo ni agano ambalo ukilivunja mambo
yataharibika; mimi nafundisha mambo ya
kiroho na nikisema kuwa agano ni mkataba, ni mkataba kweli na ili mkataba
uvunjike kuna upande mmoja ambao utaumia, ila ukivumilia mpaka mwisho wa
mkataba basi unakuwa umemaliza mkataba wako kwa uaminfu na utapewa stahiki
zako. , Mfano. unaandika barua au kuomba
kazi, utapewa mktaba na lile ndio agano umeingia na mda wa mkataba husika, hata
wa mkataba wa kazi ukiisha mfanyakazi anakuwa huru, kuna maagano ambayo
yalifanywa kwa njia ya damu za wanyama
yanawatesa watu wa MUNGU na watu wanakuwa katika vifungo kwa kujua na kutokujua
kwa sababu ya kuvunja agano, ukisoma katika kitabu cha Walawi 17:11 na ule uhai
wa kiumbe chochote mfano wa mnyama uko katika damu na wa YESU upo katika damu yake
na ndio maana biblia inatuagiza kuwa tusile damu ya mnyama yeyote, utakapokunywa
damu ya mnyama MUNGU atakukatilia mbali, maana uhai wa kiumbe husika
ulichokunywa damu yake unakaa ndani yako, ndipo utakuta baadhi ya wanadamu
wanakuwa na tabia fulani fulani zingine kama za wanyama, kuna maisha ambayo
watu wanapitia na wanateseka kwa sababu ya uhai wa mnyama au kitu ulichokula au
agano ambalo umefanya.
Leo tunajifunza ili shetani apate
hasara na MUNGU apate faida, nitavunja agano lilalokusumbua na kuwalipa kwa
damu ya YESU nawe utakuwa huru. Jiulize! kwa nini kuna agano jipya na agano la kale?
MUNGU mwenyewe alifanya agano la damu
kule katika bustani ya Eden baada ya Adam na Hawa kufanya kosa, MUNGU alifanya
agano la damu akachinja mnyama na akawavalisha
ngozi, na agano la ile damu ndilo ambalo mpaka sasa linanena, tunajikuta tunaishi katika shida na mateso, (Mtakula kwa
jasho na pia kuzaa kwa uchungu). Lakini MUNGU
aliweka akiba ya mwanae ambaye ndiye YESU;
kwa sababu wachawi nao wanatoaga kafara, wanaua, ili zile damu zinene/
ziongee kwenye ufalme wa shetani (Damu za wanyama mbali mbali na zile damu
zinaongea) na watu wa MUNGU wakawa
wanaomba na wanatoa damu na MUNGU anawajibu, (damu za wanyama hao hao) wanadamu wakawa inawatatiza na wengi
wakapotea kwa sababu damu zote zilikuwa zinanena, ndipo basi MUNGU alipotoa
damu ya mwanawe wa pekee YESU Kristo, ambayo ni damu ya pekee haifananishwi na
chochote, na ni ili ikanene tofauti na ya wanyama tofauti na kiumbe chochote,
kwa ajili ya wale ambao watamfuata yeye .
Tunajua ya kuwa YESU alikufa akapaa
Mbinguni, lakini damu yake ipo katika ardhi ilidondoka na damu hiyo inanena
uzima juu kwa watu wote na haswa kwa wale ambao wamemkimbilia, inanena ondolea
la dhambi, msamaha, ukombozi juu ya wanadamu ambao wamemkimbilia, inawezekana
kuwa upo kwenye vifungo ambavyo huenda wazazi wako walifanya agano la damu, au
wewe mwenyewe ulifanya agano kwa kujua na kutokujua, kwa sababu damu inaongea:
Mfano: Mtu aliloga au alienda kwa mganga, au alikuendea kwa mganga, mganga
akamwagiza apeleke mnyama huenda ikawa ni kuku, njiwa, ng’ombe au mnyama yeyote
yule; mganga atamwekea mikono, ataanza kusema/ kunenea vile vitu ambavyo mteja
wake anataka vifanyike ili kufanikisha lengo lake, na baada ya hapo mganga yule
atamchinja yule mnyama, ule uhai utaondoka na yale maneno yalionenwa na mganga
yatafanikiwa kutokana na ile damu iliyodondoka ambayo ni sadaka kwa shetani kwa
agano ya damu ya mnyama husika, huenda mganga alitamkaga kuwa mtu huyu awe kichaa
na utakuwa tu maana damu itanane, unaweza kuhangaika na hata
ukadhani kuwa ni mapepo ila kuna damu inayoongea, YESU
anataka uwe huru, na mimi Hebron mtumishi wake nataka nivunje agano ambalo
linakusumbua; nakata uwe huru.
Jiulize kwa nini watu ambao pesa zao
sio za halali wakifa tu na mambo yao/utajiri wao unafifia na hatimaye nao unakufa,
watu wanasema wanaenda nazo, sasa watakuwa wanaenda nazo wapi? Ukweli ni kuwa
kama mhusika alikuwa na agano fulani na amekufa na hakuna wa kuendeleza lile
agano maana maangano mengi ni siri ya wahusika,
na endapo lilikuwa ni la kutoa damu kipindi kwa kipindi, yule mhusika
atakapokufa lile agano litaacha kuzungumza ndipo hata mali za uchawi zinapokufa
wanasema mtu kaenda na vitu vyake ila ukweli ni kuwa agano lake linakuwa limeshaisha
pale alipokuwa amekufa kwa sababu hakuna ambaye amemrithisha na yamkini hakuna
ambaye alikuwanajua kuwa mafanikio ya mhusika yalikuwa kwa agano lipi. Hizi pesa za waganga ni mbaya usizitamani na
wala usitishwe na pesa za kichawi/ waganga,
kumbuka kile kinachochinjwa sio ambacho mganga anachokihitaji ila
anahitaji ile damu ya mnyama ambayo inamwagika pale chini, mfano: ushindwe
kuomba, ukate tamaa, usifike, uishie njiani, usifanikiwe na mambo mengineyo
mabaya na hata kama ulikuwa unachinja chinja kwa ajili ya matambiko, kuombea
marehemu au mizimu acha na uombe toba kwa sababu tumeshatoka huko katika agano hilo, na hata
YESU alipokuwa wanamtesa na yote waliyomfanyia YESU alivumilia kwa sababu YESU
alikuwa na agano na BABA yake na damu ya YESU alikuwa ni ya ushindi na ya
thamani sana, alitaka kusudi la BABA yeke
litimie, kwa ujasiri na kwa upendo; YESU alivumilia akijua kuwa upo ushindi
katika damu na kila ambaye atakayefanya agano naye la wokovu, na la kumkimbilia
YESU hii damu itawatetea, na hata kama imekauka kwenye vumbi bado uhai wa YESU
unaongea, juu yako juu ya kila
mmoja, kwa maadui damu ya YESU
inawabomoa, inawazimisha, inawateketeza,
na kwa wale wa upande wake damu
inawatetea.
Wachawi wana mbinu zao za kiroho na bado
wanaendelea kumwaga damu za wanyama na ndege na hata wadudu ila inategemea ni
agano lipi au ni damu ya kiumbe gani umeagizwa. Wakati mwingine unaweza kuota
kuwa kuna mnyama ameletwa anachinjwa mbele yako, au unachinjwa au unalishwa
yote hayo ni maagano na huwa yana fanya kazi sawa sawa na vile ambavyo yameelekezwa
kwako.
Maombi ni silaha, ila pia uwe na
mbinu za kuomba kwa sababu unaweza ukawa
ni mwanajeshi mzuri lakini silaha zako huzitumii na matokeo yake unashambuliwa, sitaki ushambuliwe na usikubali kushambuliwa,
kuna mikataba ya kimwili ipo mfano; mikataba ya kazi, kupanga nyumba, nk. Kuna
agano takatifu na agano chafu na agano la MUNGU na agano la miungu. Yoshua
hakujiamulia mpaka akafanikiwa kuwafikisha wana wa Israel ila MUNGU alifanya
agano na Joshua yale maneno MUNGU aliyomwambia Joshua yaliwafikisha. (Yoshua
utawavusha watu hawa akawavusha) hilo lilikuwa agano kati ya Yoshua na MUNGU, sasa
basi endapo eti utajifanya Yoshua au useme sasa mimi nawavusha kama Yoshua au
nafanya kama Yoshua halafu uone kama utaweza, hawatavuka hata! Ila MUNGU akifanya
agano na wewe lazima utavuka, mimi Hebron MUNGU alifanya agano na mimi kuwa
utawavusha watu hawa kwa majira yake ambayo yeye alipanga na utawafikisha
mbinguni na kweli nitawavusha na mbinguni mtafika maana sio agano langu ila ni
agano la MUNGU na litatimia sasa iga kama utaweza; ila shetani huwa anataka mwanadamu
avunje agano lake na MUNGU; na shetani
hapendagi wana wa MUNGU wafuate agano la MUNGU na agano la MUNGU la kwanza
wokovu, ndio maana MUNGU alimleta YESU; ila
watu hawataki agano la wokovu, wengi wana agano la dini yangu, huo ni mkataba
mwingine, vunja mikataka mingine ubaki
na mkataba na BWANA YESU vunja mikataba mingine, na hata wakikucheka wewe mwangalie YESU; jipime hivi leo ikiletwa milioni 500 halafu ukaambia chagua wokovu au fedha
utachagua nini? wengi watachagua pesa halafu wokovu baadae, wakijipa matumaini kuwa
nitatubu, sio sahihi, mchague YESU utapata vyote.
Unaweza ukawa umeokoka na ukawa
umerithi maagano ya wazazi wako kwa sababu kuna baadhi ya makabila kila mwisho
wa mwaka wanaenda wote na mwanzo wa
mwaka wanaenda tena wote, ina maana mwaka ukiisha mnaenda kufanya agano na
mwaka ukianza wanaenda kufanya agano tena la kuanza mwaka, mbuzi zinachinjwa na
damu inamwagwa, mbege, pombe, maombi ya miungu, matambiko nk. Ili tu mhusika
anayefanya na kufanyiwa agano hilo awe salama, hilo si la MUNGU. Kuna baadhi ya
watu wanaishi kwa maagano, acha mimi niyavunje kwa sababu maagano hayo yanatesa
watu wengine, mfano. Mtu amemfanya ndugu yake taahira, au aumwe tu au
asifanikiwe au ni wa kulia tu, hapo kuna ambaye anateswa na ambaye anatesa,
sasa yule ambaye anatesa wengine, aliyefanya agano ndio anafanikiwa wanaohudumia
yule anayeteswa na anayeteswa mwenyewe wanaumia sana, sasa mimi Hebron sitakubali
mteseke, nataka kila mmoja aishi maisha ambayo MUNGU alikuandalia. Damu ya
maagano, inatesa, inaongea, inapiga, inaua, ila aliyeingia katika damu ya YESU
anafunikwa kwa damu ya YESU, lakini hizi biashara za damu za maagano zikivunjika
ndipo waganga watalala njaa, Je! umeshaelewa maana ya hizo damu, umechinjiwa
kichwani au kuna aliyefanya agano na wewe, ndipo unaona mambo hayaendi hufiki,
malengo hayafiki kumbe kuna agano la damu ulilifanya au kufanyiwa au wazazi
walifanyaga sasa unalirithi, Je! una
agano Je! ulishavunja agano? Agano ni mkataba, agano nia damu na inanena Je!
ulishalivunja? Wengine wameogeshwa kwa
waganga na hatimaye unakuwa na agano lenye uhai wa kitu fulani, vunja maagano
yanatesa sana; amua tuvunje uwe huru.
Agano jipya ni agano la damu ya YESU,
mbona baadhi na hata wewe mkristo unachinja chinja kwa waganga wakati lipo
agano la damu ya YESU? Wakati hata MUNGU
ambaye amekuumba aliona kwamba agano la damu ya YESU lifuatwe kwa sababu damu
iyo ni tofauti na maagano ya damu yeyote ile,
damu ya YESU ni ya thamani sana, very special, haipatikani popote, na
hata shetani anaiogopa, hivyo basi huna haja ya kuchinja na kutoa sadaka kwa
mashetani na usifanye hivyo tena, ukifanya hivyo utakuwa umeingia agano na
shetani na hata ambao bado wanaobeba hirizi kwenye begi au popote umeingia
kwenye mkataba na mashetani na hata unaweza kukuta mtu hawezi kusoma kumbe
anaingia agano na mashetani…….kuoa/kuolewa labla mababu walifanya hayo maagano
hivyo yataendelea kuongea tu, na maagano yapo pia ya kurithi ndio maana zipo familia ambazo magano hayo ndio yanafanya kazi mfano watu hufa kwa
presha, sukari, pumu, kensa nk. Miaka michache hayo ni maagano ambayo yameweka
awali na mababu na mabibi na kama hayajavunjwa na wewe yatakupata na hutaishi siku nyingi na itatesa uzao wako pia utaharibikiwa na hata kifo chako kitakuwa
kimefanywa na shetani, siri ipo kwenye hiyo damu ya agano; yawezekana ni chakula
au maneno mabaya ila kwa damu ya YESU utakuwa salama, watu wanapofunga ndoa
ndio wanafanya agano la kuwa mwili mmoja wanaapa wanakula kiapo, kile ni kiapo
kinapokelewa na MUNGU hiki hakivunjwi, na je utaendaje na BWANA YESU wakati
wewe hutaki awe BWANA na mwokozi wa maisha yako? Unabembelezwa njoo kwa YESU uokoke
unasema mimi bado bado, ukiwa humkubali YESU basi unakuwa na mkataba na
shetani.
Kuna tabia mbaya ambapo watu wanafanya uzinzi na wanasema ni mapenzi; hapana sema wanafanya uzinzi, ukweli ni kwamba kabla ya kuoa na kuolewa hayo sio mapenzi sema wanafanya au tunafanya uzinzi na ukiwa unamtambulisha mtu sema huyu ni mzinzi mwenzangu na sio mpenzi wangu hiyo ni lugha ya shetani ya kupamba uovu ila ukweli ni kuwa ninyi mfanyayo hayo ni wazinzi. Mdada au mkaka hawezi kusema naenda kuzini anasema naenda kufanya mapenzi kwa sababu neno uzinzi lina uhalisia wa kuwa naenda kufanya dhambi ila akisema naenda kufanya mapenzi lina jambo fulani kwa sababu mapenzi ni kwa wanandoa na wamehalalishwa na wana agano hilo, na wana ndoa wanapendana kwa hiyo kama unaishi maisha bila ndoa ujue kuwa yule ni mzinifu mwenzako; tuambiane ukweli watu fungeni ndoa kila ambaye hajafunga ndoa anazini hata kama una umri wa miaka 90 bado u mzinzi. Mimi nawaambia ukweli ili muache dhambi na pia siku ile ya mwisho nisidaiwe, na mimi nifurahi kuwa nimewavusha salama, nipewe taji yangu kuwa nimewafundisha ukweli na mmepona.
Kuna agano la damu, kila mtu ambaye
anazini; wazinzi, wahusika uzinzi;
anakuwa amefanya agano la damu katika miili hiyo, na katika kuzini utakuwa
umeungana na wale ambao ulizini nao; na hatimaye utakuwa na agano na mwenye
mkosi, mshirikina, mwenye vifungo, umeshare laana, nazinaendelea kunena juu
yenu, utajiri umeshapokonyolewa, umebakia dhiki, na mambo mengi mabaya unakuwa
umeyabeba, lakini kuanzia awali
tungeambiwa hayo ni mabaya ungefanya neno mapenzi lina thamani na linafuta neno
uzinifu ndio maana watu wanaendelea na uzinzi.
Kuna maisha unataka ila huwezi,
kuyafikia kwa sababu kila kitu kiliondoka, kazi, mavazi, chakula, masomo, furaha, amani, na
mema ambayo MUNGU alikujalia yameondoka kwa sababu ya uzinifu umeshajiunganisha
na kuwa mwili mmoja na mtu fulani, mnasema ndoa ndoano, vunja lile agano,
mikataba, kuna mikataba ya kiapo kuwa ni wewe tu, nitakuoa, sina mwingine
halafu wala hujawaoa au kuolewa na hao Je! Umeshavunja hilo agano? Zaidi
unaweza kuolewa kwenye nyumba na nyumba hizo zikawa na maagano au mila mara
unaingizwa kwenye kijumba, mara unashikilia chungu, mara unapewa jiko kwa mila
na desturi, mara unaingizwa ndani kinyumenyume mara mama mkwe au baba ndio
wanakuogesha, mara unafanyiwa jambo
fulani hapo ndoa hiyo itakuwa ya mizimu na mashetani sema nataka damu ya YESU
tu, kuna agano la ukoo na kila ukoo hautakiwi kwenda mbinguni na
ukitaka kuhakikisha unaenda kwa mzee wa ukoo, ila waambie wazee waukoo kuwa
nataka kuokoka hatakukubalia, watakuambia
kikwetu hayo hayako na kwetu ni haya (Matambiko) na siyo hayo ya MUNGU, (japo
midomoni hao wazee wanamtaja MUNGU ili kukupumbaza ila kumbuka MUNGU
hachangamani na uovu wala mila) na kuna agano la damu ya mtu, sadaka ya mtu, ukiua mtu itaongea sana juu
yako; maagano sio mazuri yana mateso,
unaweza ukafanyiwa jambo kwa kujua na kutokujua agano likakutesa maisha yako
yote, kuna watu ni walevi tu, wazinzi tu, shida, agano la
umaskini, agano la ufukara, agano la vifo vya kipepo. Pia kuna maagano ya mtu
na MUNGU, mtu na mashetani, mtu na majini, mwili kuchorwa ni mikataba lakini ni
mkataba unaofanya na ibilisi na mkataba
ambao unaufanya na ibilisi ni mbaya , na ibilisi huwakamata watu wa MUNGU ambao
ni vuguvugu na wamekosa ulinzi wa MUNGU na wanawaibia baraka zao na ndio maana
yule mfanya maagano kila wakati huambiwa aue au amwage damu baada ya mda anaua
mwingine na mwingine, kama umefanya
ukatubu, ila wengi mmefanyiwa vitu vya ajabu sana, na sio lazima mtu akujue, huwa
wanafanyaga, mtoto anazaliwa na anakuwa na tabia ya ajabu sana, na haifanani na
yeyote utakuta babu alizinigi siku nyingi,
mjukuu anazaliwa baada ya miaka
mingi baadae na tabia ile lakini mtoto wala wazazi wa mtoto hawajui ndipo
wazazi wanashangaa mtoto ametoa wapi hii tabia? Wanaanza kujiuliza, kumbe ni tabia
ya kurithi, agano linatembea kizazi kwa kizazi, kumbuka kipindi kile, kwa
wasomaji wa Neno la MUNGU, Ibrahimu
aliulizwa huyu ni nani? Akajibu ni dada yangu na kumbe alikuwa mke wake, miaka
ikaenda wakati wa Isaka naye aliulizwa kuwa huyu ni nani akasema ni dada yangu;
alirudia maneno ya baba yake yaani aliulizwa huyu ni nani akasema ni dada
yangu kumbe alikuwa ni mke wake (lakini Isaka hakujuaga kuwa Ibrahimu alisemaga
hivyo na yamkini Ibrahimu hakuwahi kumwadithia Isaka jambo hilo) uongo wa
baba mtoto naye akausema, mke wake
alikuwa mzuri sana, akasema ni dada yangu, agano na mtoto alirithi bila kufundishwa,
na baadae watu wale wakatambua kuwa ni mke wake, nao wakashangaa na kuhamaki! Kumbe
ni mke wako! Mbona hujatuambia ukweli? Je!
mabaya yangelitupata? Na kipindi cha Isaka aliambiwa hivyo; hilo agano. Nakupa huu mfano ukiendelea kutafakari, jinsi
agano linavyoweza kukaa na kuibuka baada ya miaka na katika kizazi hicho hicho.
Yako maagano ya kizazi cha kwanza hadi cha nne cha ukoo uliotoka, maisha
uliyotoka nataka niyavunje maana walitaka kukuteketeza kupitia maagano ila sasa
nayavunja ili uwe huru ila na wewe ukubali yavunjwe na uyakatae.
Kuna mtu anasema mimi ni wa hapa hapa
duniani, hilo ni agano hata YESU alisema hapa sipo petu tunapita tu, na wengi
wanaogopa kusema wao ni wa mbinguni, na ukisema watu wanakucheka hata mimi
awali niliwacheka wale ambao walikuwa wanasema ni wa mbinguni, kwa kipindi
hicho, mimi nilikuwa duniani, yaani mambo na starehe za dunia zilikuwa
zimenisonga, na sikuwa najua kuwa kwa YESU kuna raha hivi jamani, nilikuwa
nawashangaa ambao walikuwa wanasema wameokoka, sikujua kuwa mtu anaweza kuokoka
akiwa duniani, hili lilitokana na
mafundisho potofu ya mapokea ya dini, ila nilipopata neema ya wokovu, nikamfuata YESU na agano la uovu likavunjwa,
ndipo nikaweza kusema mimi ni wa mbinguni na sikuwacheka wala kuwashangaa tena
wale ambao wameokoka. Napenda kukufundisha na pia kukuambia ukweli kuwa kama
ulikuwa mshirikina au kiimani ulienenda au unaendelea kushikamana na mapokeo ya
wanadamu, ubatizo wa kikombe au batizo zozote zile ambazo zi kinyume na maagizo
na agano la MUNGU na uovu (Ubatizo sahihi ni ule aliobatizwa YESU wa maji mengi
tu) Ndugu yangu ni lazima dini uliyotoka uikatae na hata mimi niliikataa na ile Imani ya mapokeo ikatae na
hata mimi niliikataa, maovu yakiondoka na yale yanayoipinga kweli ya MUNGU
ukiyaondoa ndani yako ndipo YESU anaingia, unamruhusu YESU aingie, mbinguni
hakuna matabaka wako wa BWANA YESU na wokovu tu.
Maovu yakiondoka utayafurahia maisha
yako zaidi na zaidi, na hata kama umerithi mabaya yataondoka katika jina la YESU unaweza kuzaa mtoto; mtoto
atakuja na shida ile ile, Bwana YESU asifiwe, tunaelewana? kama agano
halijavunjika utabakia na vifungo, maagano ya kimwili lazima yaache kovu, na
wewe ulioingia agano la kuchanja lazima liache kovu na kama ulienda kwa mganga
lazima uache kovu, ndio maana una kovu,
huyu hataki hiki, hawezi hiki ni omba omba tu, kumbe damu ilishamwagwa; utazaa mtoto naye atanza kuomba omba tu, kuna
ambayo hawezi fanya kazi kabisa, kuna ambao ni kuchunga tu, ambao ni umalaya
tu, kuoa wake wengi tu, mmoja hamtoshi, kuna ambao wanafanya kazi sana wala
hawachoki, kuna ambao wanafanya kazi sana wala hawafanikiwi, matatizo tu, shuleni ni zero hafaulu, ni maagano na damu
ina nguvu na kuna ukoo wamemwaga damu kuna ukoo lazima waoane ukoo kwa ukoo au
kabila hilo hilo hawaoi au kuolewa pengine kwa sababu ya agano lililowekwa kuwa
endapo wakioa/kuolewa pengine mambo hayataenda, yataharibika, hayataenda ila
kwa nini sasa msikubali na damu ya YESU ikavunje hayo?? Utakuta mtu ana pesa na
mpaka anakufa hawezi kujenga au kuwa na maisha mazuri kwa sababu ya ukoo au
damu iliyomwaga, na inayonena juu ya yale maagano na hata ukijenga unajenga
kiasi kidogo. Je! Agano lako na MUNGU liko imara, Je uhusiano wako na agano
lako na BWANA YESU limesimama au ulishalivunja?
Upo imara au umeyumba?? Yawezekana kuwa unampenda sana MUNGU na unaomba
sana lakini wewe ulishavunja agano na MUNGU, kwa sababu MUNGU huweka agano na
mtu na havunjagi yeye ni mwaminifu; MUNGU havunji agano lake kwa mwanadamu ila
mwanadamu huvunja agano lake na MUNGU; usiogope wewe unayeogopa, usiwe na shaka
wewe mwenye shaka, amua kumrudia MUNGU,
omba neema ya kurejewa na MUNGU na usifanye tena uovu ila wewe uliyevunja
agano, maana MUNGU amesema usivisujudu wala kuviabudu chochote alichokiumba
MUNGU, usiabudu sanamu, usiibe fungu la kumi,
na mengineyo ambayo MUNGU aliyakataza na wewe ukafanya au bado unafanya
hapo unakuwa umevunja agano na MUNGU.
Agano langu na MUNGU (Mimi Hebron) ni kuwaombea bure, kusema ukweli na kuwafikisha mbinguni nami sivunji agano langu na MUNGU; usione mhubiri anahubiri na anachukua pesa yeye huwa ameambiwa hivyo na sio MUNGU amemwambia maana injili au nguvu ya MUNGU haiuzwi wala huwezi nunua ila anayefanya hivyo ni mtumishi wa shetani; ndio maana anafanya hivyo; ndipo shetani anampatia pesa.
Siwezi vunja agano langu na MUNGU, na hata agano la ubatizo
kuna baadhi ya wanadamu wamelivunja, sasa wanabatiza ubatizo kinyume na agano
la MUNGU unakuwa umevunja agano la MUNGU, acha kubali ubatizwe ubatizo wa YESU
uwe huru, utoke huko, Mimi Hebron nawafundisha maana ile siku ya mwisho nitatoa
hesabu kwa kazi ambayo nimeifanya; nitaulizwa na endapo nisingeliwafundisha
ningeliulizwa mbona hukuongea, mbona hukuwafundisha, mimi nimeshawafundisha,
sikiliza chukua hatua ya agano la wokovu.
Unapoamua kuokoka amua ndani yako na usifuate
mkumbo kumbuka unapookoka halafu ukavunja agano la wokovu unaweza ukapita
katika kipindi kigumu ambacho unaweza kukata tamaa ila shida au chanzo ni wewe
ambaye utakuwa umempa nafasi shetani na akapata mlango wa kukukandamiza kwa kuvunja
agano na MUNGU wako, pia unapovunja
agano la wokovu unaweza waza mabaya, utataka au ukatenda uovu, utatakata
kuyarudia maisha ya kale kabla ya wokovu na hata ukarudi nyuma, na hata ukamkufuru MUNGU yamkini ukawaza
moyoni mwako kuwa hakuna MUNGU, wokovu wenyewe ndio huu, hapo unakuwa
umeshavunja agano kwa kutaka tamaa na yamkini wakati unaomba ulishavunja agano
na MUNGU kwa namna nyingine kwa kujua na kutokujua na ndio maana wokovu wako
unaona unashida, ukiona hali hizo zinakupata basi chukua hatua, yakupasa kuomba
rehema, halafu omba neema ili MUNGU arejeshe agano lake kwako, nami nakuombea
nawe ukiendelea kuomba ili MUNGU akurejee na ahadi na agano lake kwako litimie.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU ninaomba unisamehe, dhambi
zangu zote, nilizozifanya kwa kuwaza na kwa kunena na kwa kutokutimiza wajibu
wangu, nimetenda dhambi, nimefanya maagano kwa njia ya ndoto, chakula, uzinzi,
uovu kwa kumwaga damu, kuwategemea
wanadamu na waganga ambao wanatumia miungu yao na sikukutegemea BWANA YESU,
nimeenenda katika njia za wasio haki, BWANA YESU kwa kinywa changu nalivunja
maagano yote niliyoyafanya, ninafuta maneno yote niliyonena na hata
niliyowanenea wengine na maagano maovu niliyoyafanya kwa kujua na kutokujua,
BWANA YESU, ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, naomba ufute jina langu
kwenye kitabu cha shetani na maagano yake, ninaomba uanandike jina langu kwenye
kitabu chako cha uzima wa milele. Ninakupenda BWANA YESU ninaomba neema ya
kukaa ndani yako na ndani ya agano lako, ninaomba ahadi zako zitime kwangu na
nisitoke katika mikono yako. Kwa jina la BABA, Mwana na la Roho Mtakatifu, Ee
BWANA YESU ninaomba unisaidie.
Mtume
na Nabii Hebron Wilson Kisamo.