Pages

Monday, October 3, 2022

 

TOBA NI NINI NA REHEMA NI NINI?

 

Luka 24:47; 2 Wakorintho7:10; Petro 2:9; Luka 13:5; Zaburi 145:8-9


Bwana YESU ninakushukuru wa Neno lako ambalo ni chakula cha roho cha watoto wako

hawa cha kuwanyanyua viwango vingine na kumshinda yule muovu na Neno lako likakae ndani ya

mioyo yao ambalo ndio wewe ambaye ni mkate wa uzima. Nakushukuru, naendelea kuharibu kila

nguvu za upinzani na moto ukitangulia kila eneo kwa ajili ya kuteketeza hila yeyote na nguzo za

ibilisi nazisambaratisha kwenye ulimwengu wa roho, baharini kuzimu na kila eneo katika jina la YESU

na kwenye maisha ya waoto wako.


Nini maana ya toba na maana ya rehema? Hivi vitu vina maana kubwa sana, ila baadhi ya

watu hawajui maana ya toba na rehema na pia hawajui kuwa toba inatumika wakati upi na ehema

inatumika wakati upi na sababu za kuletwa toba na sababu za kuletwa Rehema na toba inamhusu

nani na rehema inamhusu nani?

Na kwa jina la YESU watu watahubiriwa habari ya toba kwa mataifa yote kuanzia

Yerusalemu, Yerusalemu ni Pale alipozaliwa YESU na Je! Kwanini kuliletwa toba na toba ina maana

gani?


Huwezi kuingika kwenye toba kama huna hofu ya MUNGU lazima uwe na hofu ya MUNGU

ndipo utahisi ndani yako huzuni Fulani, (huzuni ya kuona umemkosea MUNGU, huzuni ya kuona

hapa sijafanya sahihi, huzuni ya kuona umemwacha MUNGU) ni moyo wa unyenyekevu, ukiwa na

unyenyekevu ndipo utagundua au utahisi ndani yako kuwa unatakiwa kufanya toba, lakini pia mtu

anaweza kutataa toba kwa sababu hana hofu ya MUNGU. Hofu ya MUNGU ikiwa haimo ndani yako

unakuwa na moyo wa kuipenda dunia na ndani ya moyo wako unahuzuni ya kuipenda dunia hii

(hivyo uovu na uasi utaona ni sawa na furaha kwako na kutubu kwa MUNGU ili kuiacha dunia moyo

wako unahuzunika kuwa nitayaachaje mambo mazuri ya dunia hii; unakuwa hutaki utakatifu ila

unaipenda dunia na mambo yake; hivyo hutataka kuomba toba au utaona kuwa haikupasi kuomba

toba, nawaaasa Wateule mtoke katika giza, ili muingie katika nuru ya ajabu, nazungumzia kuhusu

toba na toba inawatoa watu kwenye giza na inawaleta kwenye nuru.


Toba inatumika kwa jina la YESU ili imtoe mtu katika giza na imlete katika Nuru hivyo Toba

ni kitendo cha kuachana na miungu, majini, na mambo ambayo sio ya MUNGU na kumkiri BWANA

YESU wako watu ambao mpaka sasa hawataki toba kuanzia Yerusalemu mpaka Taifa lako na ukitaka

toba unaambiwa umechanganyikiwa, Toba ni kumpokea YESU kuanchana na mambo maovu

ambayo ulikuwa nayo; wengine wanasema kwa jina la YESU na unakuta mtu yuko kanisani lakini

hawezi kuachana na mambo maovu ya dunia hii. Toba ni kuachana na mambo ya dunia hii na

kumpokea BWANA YESU pale ndipo unapata toba ya kusamehewa na kupokelewa na Bwana YESU

ila endapo hutaki toba inamaana hutaki kupokelewa na BWANA YESU. Huenda ikawa wazazi wako

na familia yako hawataki au hawajawahi kufanya toba sasa wewe ukipokea toba wanaona

umechanganyikiwa hata wengineo wanakucheka, na kuna baadhi ya makanisa hayataki toba,

yanashangaza sana, yanatumia jina la YESU lakini hawataki toba na YESU mwenyewe ameagiza kuwa

watu waache dhambi na wapate toba kwa jina la YESU na ukiangalia dunia hii watu wengi wapo

gizani na hawataki toba, hawataki kumkiri YESU, ndani ya mtu wa aina hiyo roho yake inakuwa na

huzuni na dunia hii; hataki kuiacha dunia hii na kwenda katika Nuru na hataki kuokoka, hata wewe

ulipopata toba ndipo uliokoka na huo ndio mpango ambao MUNGU aliupanga kama fomula yake

kwa ajili ya kukomboa watu wake wa Mataifa yote ila ni kwa yule anayetaka kwa sababu hakuna

mtu ambaye analazimishwa kupokea toba ila ni uamuzi wako kwa upendo, ila kwa wale ambao

hawataki toba yapo maangamio.

 

Unapopata toba MUNGU anakutambua na kabla ya kupata toba Shetani anaona kuwa wewe

umali yake, na ni mali yake kabisa lakini ukishamkiri BWANA YESU na kumpokea unaomba toba na 

ili toba ikubalike lazima uokoke, hakuna sala au maombi yanayokubaliwa pasipo toba, msidanganyike,

na ibada pasipo na toba mtakuwa mnaomba miugu kwa kujua na kutokujua.

Msipotubu ninyi nyote mtaangamia, ndiyo maana yatupasa kukiri sala ya toba na tunaikiri au

untakiwa kuikiri ukiwa hai maana biblia inasema kuwa MUNGU wetu si wa maiti Bwana YESU

asifiwe, Toba ni kitu cha kuheshimu sana, ni kitu cha maana sana, ukitubu unakuwa umetolewa

kutoka katika ufalme wa giza na kuingia katika ufamle wa MUNGU.

Rehema: 


Zaburi 145:8-9

Rehema ni maombi ambayo yanaenda kuondoa mabaya ambayo yanakutesa, yaliyokupata

au yanayotarajiwa kukupata au yaliyopangwa au yanayotarajiwa kukupata ambayo yanatumwa na

ufalme wa giza; baada ya kupata sala ya toba unaendelea na kukazana katika utakaso na utakatifu,

na endapo utaacha njia ya MUNGU au kutenda maovu, unakuwa umemfungulia adui mlango, adui

naye halali usingizi, maana anajua umeshamwacha, naye anatafuta njia ya kukupiga kwa namna

yeyote huenda ikawa ni ugonjwa au taabu, anakupiga katika ulimwengu wa roho na ndipo mabaya

yanakupata, ili kuyashinda haya unatakiwa kuomba Rehema ili kuondolewa mabaya ambayo adui

ameyapanga yakupate, na ukiomba rehema hayatakupata.


Rehema huombwa majira yote, Asubuhi, Mchana na jioni, Shetani yuko kwa ajili ya

kukushitaki ili mabaya yakupate, ila penda kuomba rehema kila wakati, omba rehema kwa ajili ya

ufahamu wako, moyo, kukosa uaminifu na yale ambayo roho mtakatifu atakuongoza ndipo utakuwa

unasafishwa na Roho Mtakatifu na yale Mabaya ambayo shetani alikuwa amepanga juu yako

hayatatokea kwa sababu unapoomba rehema unasafishwa na MUNGU anakupigania, maana u safi.

Kuna rehema ya kipepo; na katika ufame wa giza kuna mambo mengi nilipata neema ambayo

nilifunuliwa na YESU, wale ambao wapo katika ufalme wa shetani wakivunja maagano yao au sheria

za shetani huwa wanaomba rehema kwa shetani, na pia huwa wanaombeana rehema kwa shetani

yawezekana ni waganga, mizimu yawezekana ni wachungaji au yeyote ambaye yupo katika ufame

wa shetani na anaposhindwa kufanya kazi basi ataadhibiwa, mfano. Alipewa kazi ya kuangusha gari

akashindwa atapewa kipigo na atapata mapigo, na endapo atashindwa basi hatima yake

atapandikizwa ugonjwa au jambo baya litampa na hatima yake anakufa au kutumikia adhabu

ambayo wamepewa. Au wengine wanakuwa wanaumwa ugonjwa Fulani, unakuta ni pigo kapigwa na

shetani kwa sababu ameshindwa kufanikisha jambo Fulani aliloambiwa afanye.

Unapoomba rehema unapata utakaso, na unakuwa ameachana na miungu na Shetani na

mambo ya giza na umeamua kumfuata BWANA YESU na katika safari yako hiyo endapo kuna

mabaya yanakufuata au yamepangwa kukufuata hayatakupata kwasababu unakuwa umeomba

Rehema na mshtaki shetani atakuwa mbali nawe, maana hatakuwa na la kukushtaki, hivyo mwaka

mzima utakuwa unapita katikati yao bila hofu wala shaka. 


ANGALIZO: 

Usifanye dhambi kwa makusudi halafu useme nitaomba rehema, kumbuka wana wa Israel walikuwa

wamekoka na ule uovu ambao walikuwa wakiufanya uliwafanya wapatwe na mabaya (MUNGU 

alikuwa anawaona) ila Musa alirudi kwa MUNGU na alipoomba rehema mabaya yakawa hayawapati, 

angalia sana ni wapi ambapo ulikuwa umekaa vibaya na ukawa unamchezea MUNGU huenda ikawa 

mabaya yanayokupata sio uchawi ila ni mkao wako ambao sio wa utakatifu na shetani yupo hapo kwa 

ajili ya kukutandika maana shetani ni mbea ni mshitaki wetu, macho yanahitaji rehema, umefanya hila

unahitaji rehema, ubaya wowote ambao umeufanya unahitaji rehema, usiikosoe kazi au uumbaji

wa MUNGU, maombi ya kuomba rehema ni maombi ambayo hutakiwi kuyakosa. Kila wakati omba

rehema kwa familia yako.


Kuna mambo mabaya ambayo yanayoweza kupata nchi au Taifa Fulani, mfano majanga

mbalimbali, ila endapo waombaji wataomba na kusimama katika nafasi zao baya lililotazamiwa

litaondoka, tuliomba rehema kipindi cha Covid, maana lilikuwa ni pigo ambalo liliipiga dunia kwa

sababu dunia ilifanya vibaya ila watu wa MUNGU walipo omba Rehema MUNGU akaisamehe dunia

na Covid ikaisha. Na wewe ukiomba rehema vitu vibaya vinandoka. Huwezi kuomba rehema kama

hujamkiri Bwana YESU kwa sababu hatakusikiliza. Mfano: Je! Unaeza mpigia simu mtu ambaye huna

mawasiliano yake, leo ukiuliza watu kuwa wa ngapi wameomba rehema, ni wachache, lazima

uombe au uongozwe sala ya toba ndipo upate kupata kibali cha kuomba Rehema mbele za MUNGU.

Watu wengi wanapata shida katika maisha ya Wokovu, katika safari ya wokovu kuna

majaribu mwingine anaanguka, mwingine anakata tamaa na mwingine anaweza akavamiwa ila

Biblia inasema kama ni wa kwangu nitamnyanyua na hata mtumishi anapoanguka kuna rehema, na

hakuna ambaye anapinga Rehema, Ukiona mtu amesamehewa na MUNGU na mwingine anapinga

ule msamaha ujue mtu huyo si wa MUNGU, kama mambo hayaendi vizuri kumbuka kuna kutubu na

kuna msamaha. Msamaha unaombwa pale ambapo mtu na mtu wamekosana hapo mnaombana

msamaha, sio eti mimi nimekukosea halafu unaniambia nikatubu, sasa nitatubuje wakati mimi

inanipasa nitengeneze na huyu ninayemwona ambaye nilimkosea kwanza.


Toba tunaomba kwa MUNGU tu, kuna mpango na fomula ya kwenda mbele za MUNGU, kwa

unyenyekevu, ukiona mambo hayaendi ingia kwenye Rehema, unaweza ukawa umeitwa na

MUNGU na umepakwa mafuta ya utumishi wa MUNGU ukaona ndio umefika unaona kuwa ndio upo

karibu na MUNGU, sio sahihi, Jiulize watumishi ambao wametangulia akina Daudi, Samson na

wengineo wote walikuwa wakiomba Rehema kwa MUNGU, Rehema ni msingi, lakini pia unaweza

pia ukawa unaomba rehema kwenye madhabahu ambayo MUNGU hayupo unakuwa unaomba

rehema kwa shetani kwa miungu, majini, mizimu, maana shetani yeye alicopy kwa MUNGU; hivi

kama mnaomba Rehema na toba na hamkuokoka mnamwomba nani? Yaani ina maana

mnamwomba shetani maana majina ya ambaye hajaokoka yako kwa shetani na sio kwa MUNGU

sasa ukiwa haujaokoka na unaomba rehema ina maana mnamwomba shetani ili awasamehe watu

wake na asiwapige, ila ukiokoka umetoka kwa shetani na unaenda kwa MUNGU cha kukusaidia,

simama katika nafasi yako ya utakatifu, na uwe unapendelea kuomba rehema kila wakati.

Omba rehema juu ya Malango yanayozungumza mabaya juu yako, utaona kila wakati

mambo yanaenda sawa. Rehema ina watu wake, nguvu yake, fadhili zake kwa watu wake, ndio

maana biblia inasema; Muanze kuhubiri toba kuanzia Yerusalemu mpaka kwa mataifa, Kama

hujatubu ina maana huna mawasiliano na MUNGU, sasa endapo huna mawasiliano na MUNGU

hutapata majibu ya maombi yako na hatimaye ndipo utaona watu wanaanza kwenda kwa waganga,

maana mtu ambaye hana mawasiliano au mahusioano mzuri na MUNGU maombi yake

hayatajibiwa, sasa ukikosa mawasiliano na MUNGU unatafuta mbadala (alternative) ndipo mtu

anaona ni bora aende kwa mganga yamkini anaweza pata majibu na hatima yake unaangamia.

Shetani ametuburuza na sasa sio wakati wa kuburuzwa tena, nitahakikisha tunafika, na

kama ulikuwa huombi Rehema sasa omba Rehema, siku isipite bila kuomba rehema, kuwaza

mabaya ni kujifungulia mikosi, sasa kuna Rehema nyingine inaweza ikachukua muda na nyingine

utaweza omba kwa mda mrefu lakini usijibiwe kama shetani, unafikiria shetani hakumwomba

MUNGU rehema? Aliomba ila ya kwake haikubaliki, unafikiri shetani nae hatamani kusamehewa ila

hana tena Neema hiyo Mengine yamefichwa, Shetani hawezi rudi Mbinguni. Fadhili za MUNGU ni za

milele na za shetani ni za milele, moto wa jehanamu ni mbaya sana ila toba ni kitu cha muhimu sana. 


Unaweza ukapokea sala ya toba, mahali ambapo msingi yake yenyewe hakuna Toba wala

hawaongozwi kuomba toba na wao wala hawaombi rehema, katika baadhi ya makanisa watu

hawaokoki na wanaruhusiwa kufanya matambiko, na wakimaliza mila wanaruhusiwa kutoa sadaka

za shukrani kanisani, hapo wanakuwa unajisumbua tu. Siku ile utaambiwa toka, toka sikujui kwa

sababu ya mambo kama hayo, (Mambo mabaya yatakufanya usifike Mbinguni) kumbuka siku ile ya

mwisho utajaribu kujitetea kuwa nilikuwa mtunza kanisa, nilikuwa mtumishi, mchungaji nk.

Atakuambia sikujui. Atakuambia hukuwa na toba yangu, atakuambia sikujui maana hukunipokea,

umefanya mabaya mangapi si ajabu hata sadaka unaiba, utayumba na hii dunia na baraka hutakaa

uzione, mapito mapito ndio utakuwa wimbo katika kinywa chako maana utaona kuwa maisha ni

mabaya, Omba rehema ulipokiri kuwa maisha ni magumu kweli yatakuwa magumu omba rehema ili

yasiwe magumi na utaweza tu. MUNGU atafanya; MUNGU akiamua kukubariki atakubariki tu, hata

kazi unayopata ina mkono wa MUNGU, imeruhusiwa ili uamue ni njia ipi ya kufuatilia, uruhusu moyo

wako kuomba toba, omba moyo wa toba, unakuwa na huzuni na unyenyekevu ndani yako ndio

maana unaamua kumpokea YESU kwa upendo na unyenyekevu .


Mara nyingi watu hujikuta wameingia katika ufalme wa MUNGU au wapo katika ufalme wa

MUNGU, na wanaweza wakatoka na kuiingia kwenye ufalme wa shetani, na shetani anawachezea na

wanarudi duniani, napenda nikuambie kuwa unapokiri sala ya toba malaika wanaandika jina lako

kwa thamani ya hali ya juu, hakikisha jina lako lisitoke katika kitabu cha MUNGU kuna watu

wanamsingizia MUNGU kuwa MUNGU akaniambia, kasema nami, ndugu yangu ukifikia unahitaji

rehema, MUNGU sio wa kuchezea Roho Mtakatifu sio wa kuchezea mimi nikikuambia nasikia

malaika wanasema au kutoa maagizo, ni lazima kitimie, na endapo nitaenda kinyume nitapokea

mapigo.


Unahitaji rehema, rehema ikipita MUNGU anamjenga mtu anamwinua na na kumbadilisha

yule mtu, hifadhi rehema, penda maombi ya Rehema, yanaondoa mapigo ambayo ulikuwa

unapigwa na sheatani au na MUNGU mwenyewe na rehema sio ya unafIki na unapoomba rehema

maombi yawe yanatoka katika moyo wako. Je! hujawahi kutenda dhambi? Katika rehema utaona

wokovu wako mwepesi tena hauna upinzani, hata wale wa shetani wanaomba Rehema endapo

ameshindwa kufanya jambo fulani, shetani anampiga anaomba rehena na anafunga na ana toa

sadaka katika ufame wa shetani, shetani anapokea sadaka hiyon au maombi yao mabaya hayampati

mfuasi wake. Kwa MUNGU ni Zaidi, penda kuomba rehema kwa MUNGU. Mengine ni kwa ajili ya

kujifunza, omba rehema kwenye mafugu yako ya kumi, Rehema uliposingizia uongo, wizi, rehema

kwa ajili ya maisha yako, unadhambi ambayo hata hukumbuki, hata kula kupita kiasi unahitaji

kuomba rehema, ndio maana ukivimbiwa tumbo linajaa, unacheua huna amani ni kichapo

kuvimbiwa ni dhambi.

Kitu kikikaa kwenye fridge mda mrefu hakitakuwa na virutubisho tena, hakina nguvu, Jiulize

je! Umekunywa damu ya wanyama ikiwa ingali mbichi marangapi? Au hata kama imekaangwa damu

ni damu tu, umekunywa damu mara ngapi? Neno linasema nitaidai damu ya mnyama ndani yako,

BWANA ataidai; kunywa damu kuna madhara makubwa sana, kiroho na hata kimwili, usinywe

damu, umekula chakula gani kiovu? mdomo wako umezungumza maneno gani? pale unapoomba

Rehema unakuwa umekubali kuwa umefanya makosa, na mabaya yanaondoka mema yanaingina

na YESU atakujua, na kama jina lako litakuwepo mbinguni Baraka na mema na Neema yake

inakufuatilia, usije ukasema naomba Bwana atembee na mimi wakati huna alama zake, na ya

kwanza iwe sala ya toba, omba rehema.

MUNGU atusaidie, yamkini hata wanadamu wenzako umewasemea mabaya, umewaahidi

wangapi kuwa utawaoa au utaolewa na au utawaona utafanya biashara nao, ukiwasifia na

kuwaambia hakuna kama wewe, umewadanganya wangapi? Ukimwahidi mtu kitu ambacho sio ni

kiapo, Usifanye jambo makusudi halafu useme naenda akuomba rehema, usishindane na watumishi

wa MUNGU usishindane nao maana unaposhindana nao unafungulia mambo, iheshimu

madhabahu, waheshimu watumishi wa MUNGU, na kama hutataka kuiheshimu kazi ya MUNGU

utakuwa umefungulia mabaya

 

SALA YA TOBA:

Sema;

BWANA YESU ninaomba toba na rehema nimeelewa kumbe bila toba nitakuwa sijatoka katika

ufalme wa giza iwe ni mkristo au si mkristo mkristo bila toba ni bure maana wewe uliona hii dunia

imeharibika ukaja kuleta toba na toba ni kwa wanadamu na viumbe vyote, naomba unibadilishe

unitoe katoka ufalme wa giza name ninaikiri sala ya toba, YESU naomba unisamehe dhambi zangu

zote nilizozifanya kwa kujua na na kutokujua naomba uandike Bwana jina langu kwenye kitabu

chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na mambo yake yote; nimepokea huzubi ya roho

mtakatifu na hofu ya MUNGU, na sio vinginevyo. Nakuomba Roho mtakatifu unisaidie nisirudi

nyuma tena naomba rehema katika wokovu wangu pale nilipokosea nilipofanya lolote wanijua

naomba unisamehe, naomba rehema kwenye maisha yangu kwenye kazi zangu ata kwenye vipawa

na karama ulivyonipa Rehema kwenye mali zangu kwa watoto kwenye kazi rehema na hata yale

ambayo nimeyasahau naomba rehema sitaki mambo mabaya tena, Hata Nabii wa MUNGU aliomba

rehema ukaghairi mabaya hayakuwapata, nasi tunaomba rehema tukiwa na nabii ya wako, siyataki

tena nafunga milango ya mabaya kabisa na hii nguvu ya rehema na nguvu hii inisaidie kila wakati

niweze kuomba.


MUNGU awabariki awainue awahifadhi kwa sababu kuna mambo ambayo yataondoka

kwako endapo umepokea rehema kwa moyo mmoja mambo yataenda mipango itanyooka na

wengine watapata watoto kwa sababu wameomba reheam ila kuna wale ambao wao ameamuna

kuwa na kichwa kigumu basi wao wataendelea kuona mabaya. Rehema uishike kwelikweli ikusaidie

sana penda kuomba rehema kila wakati, MUNGU ni wa rehema kama ulianguka utasimama rehema

inaponya kama kuna vitu vinakusumbua omba rehema vitoke.

 

Imeandikwa na Mtume na Nabii,

HEBRON WILSON KISAMO