DHAMBI
NI NINI? (Kwa nini inamfuatilia mwanadamu tu)
Zaburi
32:1-2 na 1 Yohana 5:17-18
Bwana YESU
ninakushukuru kwa mda huu tena, Nakushurkuru kwa Neno lako ambacho ni chakula
cha roho zetu ulichokiandaa kwa ajili ya kulisha kondoo zako ili wakapate nguvu
ya kufika mbinguni na pia nguvu ya kuishi hapa duniani kama upendavyo kwa
utukufu wako MUNGU. Nikiendelea kuharibu yale mabaya juu yao na kuendelea
kuondoa kila kilicho kinyume na mpango wako, MUNGU wewe ni mwenye nguvu na hakuna
aliye Zaidi yako, nimeuona mkono wako toka
kipindi cha akina Musa na manabii na hata ulipokuwepo YESU na bado
utaendelea. MUNGU ninakutukuza na ninakubariki.
Dhambi
ni nini, ni vizuri kujua dhambi ni nini
na ipo kwa ajili ya nini inamtaka nani na ila
lengo gani na kwanini dhambi isimfuate mbuzi, ng’ombe au samaki wa baharini? Kwa nini imchague mwanadamu?
Jiulize!
Neno
la MUNGU:
Biblia
inasema heri asiyehesabiwa dhambi na kusitiriwa makosa yake, na kwanini
haijasema jambo jingine?Unapokuja kanisani kabla ya ibada unaanza kutubu dhambi
kwanza au hata ukiwa unataka kumwomba MUNGU unaanza kwa toba ndipo unamwomba
MUNGU. Je! Kuna nini katika dhambi?
Bwana YESU
asifiwe, kabla ya kuanza ibada mlitubu dhambi, kwanini mlitubu? Au kwanini
tunatubu? Wanadamu wanaona kutenda dhambi au kufanya dhambi au kuwa na dhambi
ni kitu cha kawaida ila yatupasa akujiuliza kuwa hii dhambi inatoka wapi?
Chanzo chake ni nini? Dhambi ni uchafu ambao uliletwa na ibilisi ili kuwachafua
wanadamu ndio maana tunapomwomba MUNGU atusamehe, tunaomba utakaso
(kusafishwa). Tunapoomba kusamehewa dhambihuwa tunaposema tusafishwe dhambi
zetu, kwanini tusiseme tusafishwe jasho au kuogeshwa mwili,kwanini tunaomba
kusafishwa na hata YESU alikuja
kutusafisha dhambi, na MUNGU aliweka sheria zake na shetani alizivunjakwa
sababu yeye alimwasi MUNGU na anataka wafuasi wa kwenda nae motoni na ndio
maana hata mwanadamuwanapenda dhambi sana kuliko kuipenda sheria ya MUNGU, kwa
sababu wengi wao wametekwa na Shetani ila dhambi ina madhara makubwa sana.
Mtu akivunja sheria hapa dunia, ambayo imewekwa
na kaisari au taifa Fulani atapelekwa
mahakamani kwa sababu ya kuvunja au kukiuka kipengele fulani na atahukumiwa kwa
kifungo cha mda Fulani mfano mwaka, miezi sita au kutozwa faini na pia MUNGU
anaangalia sheria, na amri alizowawekea wanadamu ili wazifuate na Sheria hizi
zimewekwa ili wanadamu wasitende dhambi.Hivyo basi ikiwa kuna sheria za Kaisari
na za MUNGU basi ya MUNGU mpe MUNGU na ya kaisari mpe kaisari.MUNGU anangalia
sheria zake ili azitimize, hata hivyo baadhi ya wanadamu huvunja hata sheria za
nchi au kufanya kosa Fulani, na yamkini mwingine ni kweli amefanya kosa ila
atakana hata mbele ya mahakama kuwa hakutenda kosa hilo na hata anaweza kukuuliza/kuuliza
Je! wakati alipokuwa anatenda kosa hilo nani alikuwa shahidi? Na kama huna
shahidi mshitakiwa anakuwa huru, ila kwa MUNGU huwezi kukana kosa. Dhambi ni
kitu kibaya sana Kinakufanya unuke mbele
za MUNGU japo kimwilini umejipulizia
pafumu/Marashi,unanukia vizuri, hutaisikia harufu hiyo kimwili ila hata hapo
ulipoketi au kusimama hunuki lakini mbele za MUNGU unanuka sana, lakini watu
huona kuwa dhambi ni kitu cha kawaida, na Je!umeshawahi jiuliza mbona nikitaka
kumwomba MUNGUlazima kwanza niombe toba, rehema na utakaso, ili niwe safi, ndipo nimwombe MUNGU? Hivi nikwanini?
Je! Ni lazima uombe toba ndipo usogee kwake? Ndio ni lazima kwa sababu MUNGU
hasikilizi watu wachafu wenye dhambi kwa sababu mshitaki wa wanadamu yuko
karibu nae anakusikiliza kama hujatubu anakushitaki na anadai haki kuwa MUNGU
huyu anadhambi, hajatubu, utamjibuje? Lakini ukitubu unakuwa na haki ya kupata
majibu yako toka kwa MUNGU.
Zipo
aina tofautitofauti za dhambi, ziko za kimwili na kiroho pia naposema za
kiroho, dhambi unaweza kuitenda katika ulimwengu wa roho, na kimwili pia. Mfano. kunywa pombe, kuzini, kula vyakula
katika roho au ndoto, unakuwa unaota kuwa umezini, unakuwa umezini na jini
mwili wako unakuwa nusu mtu nusu jini na
endapo umezini na mfu unakuwa nusu hai nusu mfu katika ulimwengu waroho
kwasababu unapozini unakuwa umeunga na
yule mhusika kimwili na kiroho, kwa kujua na kutokujua. Pia kuna dhambi za kiinjili, dhambi hii imegawanyika
katika sehemu nyingi sana, na Neno la MUNGU linasema usilibadilishena
ukilibadilisha kwa namna yeyote ile ni dhambi, tayari unadhambi mbele za MUNGU
kwa kujua na kutokujua na ndio maana biblia inasema ile siku ya mwisho
watahukumiwa kwa kupunguza au kuongeza Neno lolote Zaidi ya kile ambacho
kimeandikwa au kwa kuvunja Sheria na amri za MUNGU, lakini kuna kipindi cha
neema sasa kwa kuwa ulikuwa hujui na MUNGU amewatuma watumishi wake ili
kuwaelekeza, kuwafundisha na kuwaambia ukweli ili wanaamu wafunguke akili,
fahamu zao na mioyo yao imwelekee MUNGU, wajitambue wapate kutubu na kumrudia
MUNGU ukiujua ukweli hofu ya MUNGU itakuwa ndani yako na kwa Neema ya MUNGU utakaa
kwenye msitari.
Dhambi
mnazijua sana lakini naongea dhambi ya kiinjili, na dhambi ya kiinjili ni pale
ambapo mtumishi anatoa huduma za kiroho kwa pesa, michango na kuuza injili hiyo
ni dhambi na biblia imesema nimekupa bure toa bure, anayetaka pesa ili akuombee
anadhambi na wewe pia ambaye unatoa pesa ili upate hilo hitaji toka kwa huyo
mtumishi nawe unadhambi,hata kumwona mtumishi wa MUNGU kwa pesa yeye na wewe pia wakosaji mbele za MUNGU
unajua sheria haipingwi? Ubatizo tofauti
na ule ambao YESU alibatizwa ni ubatizo wa dhambi, ubatizo ambao u kinyume na
ule wa mpango wa MUNGU ni dhambi nasisitiza ni dhambi, kubatiza kwa kikombe,
kwa kisima, na batizo zote ambazo hazikuagizwa na MUNGU ni dhambi, na wote na
hata watumishi ambao wanayafanya hayo watatoa hesabu ya maneno ya injili ya dhambi ambayo
wameifanya, ukimwambia mtu abatizwe,
ubatizo ambao YESU amebatizwa anakataa kwa sababu ndani yake umejaa ubatizo wa
dhambi, wa kikombe, wa mapokeo ya wanadamu, na MUNGU hautambui na shetani na
yeye amewafanya wanadamu waitetee dhambi na mimi nikiwaambia kuwa baadhi ya
makanisa yana dhambi wanadamu watanishangaa kuwa inakuwaje? Kanisa na
linalotaja jina la MUNGUlinakuwaje na dhambi? Kumbuka, Neno la MUNGU limeandika,
Kipindi YESU alipoingia Kanisani akakuta biashara zinafanyika hapo alipindua
meza zao, Na sasa hayo yapo katika baadhi ya makanisa, YESU alivyoingia
kanisani akakuta watu wanauza na wengine kuombewa kwa matabaka, yote hayo ni
dhambi tena dhambi mbaya, hata na wewe ambaye ulitoa mali zako kwa ajili ya kuombewa unadhambi,
utajiuliza Hebron anafundisha nini ila
ukweli ni kuwa kila ufanyacho kinyume na mpango wa MUNGU ni dhambi, kwasaa
unaweza usinielew ila naomba MUNGU uelewe ili ubadilike, ile siku ya hukumu
utakumbuka maneno haya, unaweza kuona
kuwa maneno haya hayafai kwa sababu wengi hawapendi ukweli ila ila ukweli yamkini unona kuwa hayakufai au
kuona kuwa nakueleza nini? Ila kwa MUNGU yanafaa na mimi ninafaa na pi hata
kwako nitafaa na mbele za MUNGU ninafaa kwa sababu nakufundisha ukweli, ndio
maana MUNGU aliona kuwa dunia imechafuka imekuwa chafu, si uchafu wa vumbi au
majalala ingekuja hivyo hata kwa moto au mvua au vyovyote ingesafishwa ila
alimtuma mwanaye aje atusafishe, kwa damu ya thamani, tena mwanaye wa pekee,
kwa sababu MUNGU ni MUNGU wa haki, na kwa sababu ni MUNGU wa haki alimtuma
mwanaye ili uturejeshee haki, haki yako na yangu ambayo yule mwovu aliiba tulipokuwa
tumechafuka na dhambi, kwa sababu mwanadamu alinyang’anywa haki yake, ya kujua
ukweli ili kwamba shetani nae apate wafuasi wa kumtete na kuacha kumtetea MUNGU
kwa kujua na kutokujua na ndio maana mpaka sasa watu wanapoambiwa waokoke, hawataki,
waache dhambi wanang’ang’ania dhambi, wampokee YESU hawataki.kwa nini unaambiwa
uokoke ili utoke kwenye dhambi na unakataa? Ina maana unapenda dhambi, humpendi
YESU, japo unamtaja na hupendi kwenda Mbinguni au huujui ukweli, au
haukufundishwa ukweli kwa sababu hata sasa kuna baadhi ya makanisa wanawaambia
watu wasiokoke, wanawakataza watu kuokoka, wanakuambia usiokoke, huwezi kuokoka
ukiwa duniani, kaa hivyo(inamaana ukae tu katika dhambi) na siku ya kufa,
kanisa husika litakufanyia ibada, ndugu
yangu MUNGU sio mpumbavu aliweka sheria zake ili zifuatweacha kudanganywa na
injili za uongo hatimaye utakufa na
dhambi, umepewa akili timamu umkiri YESU,kusema tu wewe u mkristo, bila wokovu, bila kumkiri
YESU haitakusaidia kwa lolote, mpaka uokoke kama alivyo agiza ndipo utakuwa
mkristo kamili.
Kwanini
unaogopa kuokoka, kwanini unaogopa kutolewa katika hali ya ukosaji? Endapo Ukikubali
na ukiamua na kuokokaMUNGU atakusaidia kusimama imara siku kwa siku na
kuishinda dhambi kwa sababu bado dhambi itakufuatilia nyuma ikuotee, tafakari
na utathmini mpaka sasa ni wandamu wangapi wameshakufa katika dunia hii wakiwa
bado hawajaokoka na pia waliambiwa kuwa watafanyiwa ibada na ni kweli
wamefanyiwa ibada ila ukifanyiwa ibada wakati umekufa, itakusaidia nini, maiti
inasikia? Marehemu anatubu? Je! wameenda wapi sasa? Tafakari. Sasa amua kuokoka
kabla ya kufa.
Dhambi
za kiinjili msiabudu sanamuna mnaabudu sanamu, unatubu hapo hapo kanisani
halafu hapo kuna sanamu inaabudiwa, ni dhambi, mnatenda dhambi acha kuabudu
sanamu. Na wewe ambaye umeokoka umetoka kwenye
dhambi ijapo kuwa unakuwia vigumu kuacha dhambi kwa haraka ila kwa vile
umeamua na MUNGU anakusaidia nami ninakutia moyo, simama imara utashinda, hii
dunia imekwisha kuchafuka na ondoleo la
dhambi huondolewa kwa kumkiri BWANA YESU
na kuachana na mambo mabaya. Sasa akija YESU Je! Atawachukuwa wangapi?
Tafakari ni makanisa mangapi ambayo hawaruhusu watu kuokoka, wanawapumbaza watu kwa jina la YESU ila wengine wanajua
kuwa wanadanganywa na wengine hawajui, ila Nuhu alipokuwa anatengeneza
safina, watu walimcheka, hatima yake wengi
waliangamia na sasa safina ni hii injili ninayokufundisha, kwenda kwa mganga ni
dhambi, mganga mwenyewe ana dhambi na kuna nyumba ambazo hata Baraka haziendi
kwa sababu kuna vitu vya dhambi ndani ya nyumba hizo, vitu vibaya vikiwa ndani
yako au ndani ya nyumba yako ni dhambi unajua ukiwa na dhambi au vitu vya
dhambi vinakuharibia mipango yako, unaweza ukawa mtu wa dhambi na kwa vile u
mtu wa dhambi na dhambi inakufuata tu, unaenda kanisani lakini mshirikina,
mwongo, mzinzi, na mambo kama hayo hizo zote ni dhambi, unajiita mkristo ila
unadhambi, jamani MUNGU anajua mioyo na
MUNGU anakuangalia jamani inakuja hukumu na itakuwa kipengele kwa kipengele,
watatengwa wakosaji na watakatifu, hawa watakaa huku na wale kule. Jitadhmini
dhambi zako maana unaweza kujipima kuanzia sasa, unatabia za dhambi,
msengenyaji, mwongo, mvivu, unachukia wenzako, unadhulumu, unajipima hapa hapa
utajijua kuwa wewe ni mkosaji au si mkosaji na kama unampenda MUNGU kataa kuwa
mkosaji, na hata kama huwezi yupo Roho Mtakatifu
atakuwezesha ila sasa wako baadhi ya watu wanasema tunakuja mbele zako
sisi ni wakosaji tu tusamehe, (kukiri kuwa
u mkosaji kila siku sio jambo jema, hebu jitahidi usiwe mkosaji, unapofanya
dhambi ya kukusudia, hautasamehewa kwa sababu unafanya kwa makusudi, dhambi ni
dhambi tu, ziko za ana nyingi, Paulo alikuwa ni mwenye dhambi naye alitete sheria za shetani kwa
kumpinga BWANA YESU ila MUNGU alimbadilisha Paulo, akawa anamtetea MUNGU na
kumpinga shetani, akanza kutetea za MUNGU na akawa mtumishi wa MUNGU aliye hai.
Mpinge shetani na umtete MUNGU, wengi hawataki kumtetea MUNGU.
Unapookoa uwe mstaarabu, sio unapigapiga
kelele tu, kupiga kelele ni kupoteza muda, unapotaka kumtoa mtu kwenye dhambi,
mweleze kwa upole mvute na sio umkaripie na kumwambia kuwa unadhambi wewe! Utakufa wewe!hapo utakuwa umehukumu, na unapohukumu kumbuka
kuwa utatoa hesabu ya maneno na hukumu ulizohukumu watu siku ile ya
mwisho, utatoa hesabu siku ile, kuna vyakula vya dhambi, watu wanapenda
kufanya dhambi, wanapenda dhambi na pia baadhi hufanya dhambi ya kumwibia MUNGU
hata sadaka na zaka zake ni dhambi, kumtakia mwezako hila, kumwonea mwenzako
wivu ni dhambi, mtu anajifanya rafiki yako ukitoka anakusema, dhambi za kutoa
maneno yako ambayo unayazungumza ambayo sio ya staha, dhambi ya kushuhudia uongo, dhambi ya kumkufuru
MUNGU, na Roho Mtakatifu na zinginezo nyingi.
Kuna
aina ya mungu anayeitwa mungu dhambi kwa kuwa dhambi inaondolewa kwa utakatifu
basi ukitenda dhambi mungu dhambi ndio anakuwa mungu wako, mawazo yako yanakuwa
ni dhambi, njia zako dhambi, unawaza dhambi, nitammaliza, nitamkomesha, nitamfanyia hila hayo uwazayo
kinyume na MUNGU ni dhambi, hukuitiwa hayo umeitiwa mema, acha dhambi ikikomaa
inazaa mauti, hivyo dhambi huzaa mauti, na ndio maana shetania anang’ang’ana
watu watende dhambi na wasimkiri BWANA YESU maana mungu dhambi ndio anayetenda
kazi na roho zake zinasambazwa kwa wanadamu. Utakuta kanisa linaenda vizuri ila
panatokea tu mmoja kati ya watumishi analigawa kanisa, na kuacha mhimili ambao
ndio mbeba maono na kufungua matawi, inafikia hata kanisa linakuwa
limegawanyika mara mbili au mara tatu, yule ambaye ni mtumishi wa MUNGU
atabakia akimtumikia MUNGU ila yale matawi sasa yatakuwa sio ya mpango wa MUNGU
ila watakuwa wakiwapumbaza watu kwa kulitaja jina la YESU, ila roho itendayo kazi sio ile ya mpakwa mafuta aliyeitwa na YESU
hivyo mungu dhambi ndio atakayeongoza tawi lile.
Dhambi
ni mbaya, dhambi ya miili, ya mikono, miguu ina dhambi, hutaona viungo
vimeandikwa imeandikwa ila inakuwa na dhambi; tunakuja ibadani lakini tunakuwa
na dhambi na dhambi inakufuatilia nyuma;wewe ikataena ukiwa mtakatifu tu hata
wachawi na shetani hakuwezi, sio kwamba ukiwa umeokoka hutapata majaribu,
majaribu yapo,lakini katika kujaribiwa kwako inakuwa ni kwasababu Fulani hata
YESU alikuwa mtakatifu; lakini alijaribiwa na majaribu ambayo unayapata
yanakuza Imani yako pia. Na pia ni kipimo chako na MUNGU kuwa je unampenda
MUNGU na MUNGU pia anakuangalia, kama je! Unampenda? na ndio maana majaribu
hayafanani, Bwana YESU asifiwe, utakuta
wengine wanaomba hata kwa kiburi mfano
mtu anaomba kwa kumwambia MUNGU, MUNGU endapo hutanijibu nitajua kuwa wewe
haupo, au nimesimama na Neno lako Baba, leo nitajua kwamba wewe ni mwongo au ni mkweli hicho ni kiburi kwa sababu sio mapenzi ya
MUNGU unamlazimisha MUNGU kufanya mapenzi yako, Sio sahihi kuomba kwa
kumlazimisha MUNGU, kuomba ni unyenyekevu, ndio maana baadhi ya watu hawapati
majibu yao ya maombi kumbe hukuomba kwa
adabu ila pia wako wahubiri ambao wanaomba kwa kupindua sheria za MUNGU, wako
baadhi ya watumishi wenye dhambi na pia wako waumini wenye dhambi sasa jilinde
na dhambi na usimame imara maana kuna kulipwa ile siku ya mwisho,lakini napenda
kukuambia kuwa kuna watu ambao wataingia mbinguni na hawatalipwa hata mia, kuna
mema mbinguni, yapo malipo kila mwisho wa mwezi, mataji pia hayatafanana, hivyo ujue kuwa ukaribu wako na MUNGU duniani ndio
huo huo utakuwa ukaribu wako na MUNGU mbinguni, unaweza ukawa umefika Mbinguni
ila yamkini umbali wa mahali MUNGU alipo ni Tanzania na wewe upo South Africa,
hivyo kila kitu kitatadhmini unafanya nini, au umefanya nini, unaweza ukawa kila siku asubuhi unaende
kuripoti kwa wenzako lakini wapo ambao watakuwa na vyeo vikubwa, maana Mbinguni
wanaenda kazini, MUNGU anakaa ofisini, kwa mfano wa hata sasa ilivyo katika
serikali ziko nafasi mbalimbali katika utendaji kazi ili kukamilisha au
kufanikisha kazi na mbinguni pia ni hivyo hivyo, usujiangalie jinsi ulivyochoka
hapa duniani yamkini unanafasi kubwa Zaidi ya wafalme wa duniani, umepewa mdomo
wa kumwimbia MUNGU lakini hutaki, mwili wa kumchezea MUNGU hutaki ila
ukipelekwa kwenye baa unacheza miziki ya duniani kwa nguvu zote, kupiga makofi
ya kanisani taabu ila kwenye siasa, unaipenda sana, na utashangilia sana.
Lakini kanisani huwi mshabiki namna hiyo, dunia na mambo yake yatapita, moyo
wako umpoikee BWANA YESU na sio akae na kutoka ila akae na aishi. YESU akiishi
kila utakaloomba linatokea na linafanyika na unafanikiwa kiroho na kimwili na
unakuwa na ulinzi na pia ukimpokea yesu wa uongo ataishi na utapata taabu ila
YESU wa Mbinguni akiishi mambo yako
yatakuwa salama, hakuna shida wala mchawi wala tabu ambayo itaishi kwako.
Watoto wa MUNGU msijidharau, hakuna ambaye anaweza muua YESU, hawawezi
msambaratisha YESU hata kama wanakutisha kwenye ndoto na mambo mabaya, unaweza
ukawa umelala na likaja jambo baya au hata ndoto mbaya na ukashindwa hata
kuinuka kwa maana hayo majitu huweka uzitona magandamizo ila ndani ya moyo wako
ukiweza kumtaja YESU kweli utavushwa, na hawatakufanya jambo lolote, ila kama
YESU hayuko ndani yako utaishia kupata hofu na kupiga kelelel. Ukiwaza mambo
mabaya YESU anaondoka, ukifanya mabaya anaondoka. Mengine MUNGU anayaachilia
yaje, lakini hayatakushinda walau tu moyo wako unauwezo wa kusema kwa jina la YESU
ni vita vya kiroho, yakitokea hivyo
ukashinda amaka usilale mfuatilie kwa maombi ukiwa na Malaika.
Mwanadamu
anakuwa amezaliwa mapema, ila tu inakuwa
siku yako haijafika ya kuingia hapa duniani na hata ile nyota ambayo
ulipewa kuna kazi ambayo ulipewa au ulikuwa unafanya huko bado hujaikamilisha,
kwanini YESU akafa na akaenda kuzimu, miaka yote kabla hajafa aliwahubiria
habari za ufalme wa MUNGU juu ya habari ya toba na msamaha, wako waliookokaga,
wako walioachanga, MUNGU ni wa haki wote walichukuliwa na Bwana YESU, sasa wewe
Je! unasubiri YESU akufuate tena
makaburini, wale waliokolewa kwa neema, siku alizokuwa ameshuka huko
chini kwa Siku tatu zilikuwa za kumpiga shetani na kuwatoa watoto wa MUNGU
kwenye umateka maana wengine walikuwa hawakusikiaga injili ila sasa wewe ambaye unasikia injili unataka YESU akufuate makaburini? Jielewe,
dhambi ni mbaya uone kuwa dhambi ni mbaya, wengine hudhani au kuona kuwa
kufanya dhambi ndio Mtindo wa maisha, (life style yao) uongo wa mtu aliyeokoka ni
wa hatari sana kuliko wa ambaye hajaokoka kwa sababu pepo limtokapo mtu
likakuja na wengine saba, kiburi, faraka katika ndoa au familia, Ndoa zinashida kwa sababu ya dharau na
viburi, endapo mwanandoa wanakiburi
kweli ni taabu tupu, hakikisheni dhambi haiingii kwenye ndoa, dhambi za
watoto wadogo walizopokea kupitia ubatizo, bila kuiondoa dhambi hakuna
chochote, Ukikuta umesimama vizuri shetani atakusingizia au atakuingiza kwenye
kambi mbaya ya uovu dhambi mbaya chukia dhambi mambo yanapoharibika unaanza
kusema wokovu huu mbaya, nimechoka,
kumbe tatizo ni dhambi, ukiiba sadaka ni dhambi, chochote unachoiba ni dhambi,
usiibe chochote MUNGU anaangalia sheria yako, usiibe hata siku moja. MUNGU
atakufanyia favour yakena wakati mwingine anakufanyia favour yake unakataa,
MUNGU anaweza kukutendea jambo Fulani ukakataa wakati ni favour kwako toka
kwake. Mshukuru MUNGU kwa Neema zake
kwako nakwa favour ambazo amekupa.MUNGU ataamuru hata waovu wakuletee Baraka, hivi
pesa au vitu unavyopokeaga vyote ni vitakatifu?
Je! Vinatoka kwa watakatifu tu? Au vingine vinatoka kwamchawi,washirikina
nk. Mtu akikupa hela au chochote unakataa au unapokea au hata yule bosi ambaye
anakupa hela unajua kuwa anatoa wapi hizo hela na maagano yake ni nini? Hauweki mfukoni? Gari unalopanda unajua lina
nini? Unajua vina maagano gani? Hujui! Ila
Neema ya MUNGU tu inatulinda. Hata shule tunazopeleka watoto wetu je tunajua
zina maangano gani? Wenye nazo wana maagano gani? Ila tu usimpeleke mtoto shule
ile ya kumwomba yule mungu mwingine, hata wangu simpeleki. Na pia ujue kuwa
wakati unapokuwepo duniani na unatamani
kufanya jambo, kazi au mradi Fulani, na
usipolifanya ni dhambi, usipolitimiza ni dhambi na ukilifanya kwa ulegevu ni
dhambi, unapochelewa tu ni dhambi,
lazima jambo litumie, mwanafunzi hataki kusoma ni dhambi, ni dhambi hata
mwanamume kutokujali familia yake ni dhambi, mwanamke kutokumpenda mume au
familia yake, ni dhambi kumdharau mwanadamu ni dhambi, ziko dhambi za aina
nyingi, kama kuna faraka ni dhambi, kubeba kinyongo, watakao lipwa ni
watakatifu na utakatiifu sio kuoga ni kuacha dhambi, utatoa hesabu siku ya
mwisho, kuwa na uchungu ni dhambi, moyoni mwako mweke BWANA YESU. Kufunga ndoa
na majini ni dhambi, Watu wengi wamevaa pete,
wamefunga ndoa na majini, wanawapa mali, vyeo nk wamekuwa mwili mmoja
namajini ni dhambi, ni dhambi kufanya ibada mahali ambapo hayuko MUNGU, MUNGU
anakusafisha, anakutengeneza halafu
unarudi huko ni dhambi, kwani hata sasa si kuna baadhi ya viongozi wa dini na ni wachawi kabisa ni dhambi hiyo
sasa msingi wote huo ni Dhambi, usiipende na usihukumu na kila ukitenda dhamnbi
ujue kabisa kuwa wewe utahukumiwa, hauna ndoa ni dhambi.
SALA YA
TOBA:
Bwana
YESU ninaomba unisamehe dhambi zangu
zote, nilizotenda kwa kujua na kutokujua, nimekaa na mistari ya biblia kumbe
nina dhambi nyingi ziliniwekea ukuta na
kunitenga na wewe nataka uwe karibu name, ninaomba uwe karibu nami, umeniumba
na hali nzuri nikachafukia hapa duniani nikaridhi dhambi za ajabu, tabia za
ajabu, ninaomba unitengeneze na uyatengeneze
na mataifa maana ulikuja kuwaokoa wenye dhambi na sio kuwasafisha wenye jasho
au waliochafuka na vumbi bali ulikuja kuokoa wenye dhambi, ili watu wazijue sheria
zako na ukaweka pingamizi la msamaha kwa damu yako. BWANA YESU ninaomba
nitembee katika njia zako na kukaa katika njia zako, na nimesimama na mistari
ya Neno lako na haikutimia kumbe nilikuwa mwenye dhambi kiroho na kimwili,
nimeacha dhambi na kujitenga nayo, naomba unijaze nguvu zako na za Roho Mtakatifu
na YESU ulie ndani yangu usiingie na kutoka, naomba ukaishi naomba ukafanye
makao asante BWANA YESU.
MUNGU
ninakushukuru, wabariki, walinde, watakase katika jina la YESU, Baba MUNGU
ninaomba ukafanye marekebisho kwa watoto wako maana kila mmoja unamjua na
unamwelewa, wawajua vema, wawajua vema, ninaomba uwafungue, wawe huru.
Nawaombea nguvu ya kusonga mbele, kushinda dhambi, nguvu ya utakatifu, katika
ulimwengu waroho na mwili na ninaomba uwatenge na mungu dhambi nawaombea
utakatifu maana unapendezwa na watakatifu walioko duniani maana wanaupendeza moyo
wako BABA ninakuomba ukahusike na ninawakabidhi katika mikono yako na Mbingu
iendelee kufungukakatika maisha yao, mwanga ukaendelele kuwepo kwao na watoto
wako hawa wakazidi kuwa karibu na mboni ya MUNGU, na jicho la MUNGU likiwalinda na hata mkono ambao
utajaribu kuwagusa ukagusane na mkono wa MUNGU, Baba MUNGU naomba watoto wako
wakaone faraja yako na furaha ya wokovu. Amen.
Mtume
na Nabii Hebron Wilson Kisamo.