KUTOLEWA SADAKA - WEBRANIA 9:23-28
“Kuna watu wametolewa sadaka na sio sadaka zote hutolewa kwa MUNGU na
sadaka zinazungumza basi na leo umetoa sadaka yako lipo jambo ambalo MUNGU ataenda
kulitenda”.
BABA ninakushukuru, kwa neema yako, maana nimeona wasioweza kupumua
wanapumua. Ninaendele kuwakomba watoto wako mahali popote walipo, najua MUNGU
wewe ni mwema, ninaomba wema wako kwa watoto wako wote, MUNGU naomba
ukakutane nao, ukiwalinda, ukiwatunza, ukiwainua, ukiwaganga mioyo yao na kuwalisha
waliokauka ukawastawishe, waliojeruhika MUNGU ukawatengeneze na waliofungwa kwa
nguvu za giza za aina yeyote, naomba ukawafungue, maana najua wewe ni MUNGU
unayeweza na wewe ni MUNGU ambaye hujawahi kushindwa, wewe ni MUNGU wa Eliya
Ibrahimu, Isaka na Yakobo. BABA ninakushukuru kwa siku hii ya leo naendelea kufungua
anga na kumwaga damu ya YESU katika ulimwengu wote, na mabara yote, majini na
mapepo yawe vichaa, yaharibikiwe kwa jina la YESU, na kila nguvu za giza za aina yeyeote
ambazo zipo kwa watoto wa MUNGU ambazo zinawafanya wasielewe, naziteketeza,
ziungue kwa jina la YESU, kwa damu ya YESU na aliyesimama mbele ya watoto wako
ninamuunguza, maana najua liko jambo ambalo MUNGU anakwenda kulitenda, majeshi ya
shetani, mapepo, miungu, na mizimu, naiunguza, yote ikawe viziwi kwa damu ya YESU na
rekoda zote za kipepo zidondoke na kuteketea katika ulimwengu wa Roho na mwili na
Vizuizi vilivyokuwa mbele yako vinaondolewa kwa damu ya YESU ninaona ukisafishwa na
ukitiwa nguvu ninaona wewe unayeshindwa kupumua ukipumua na wewe ambaye umekata
tamaa ukitiwa nguvu usiyeweza kupokea neno utalipokea maana nguvu ya MUNGU ipo juu
sana, juu ya vyote, Haleluya! Amen.
BWANA YESU ambaye ni mwana wa pekee wa MUNGU, MUNGU anayetupenda
hata akatuumba na akatufananisha na yeye na akaleta Neno lake kwa ajili yetu. Bwana YESU
asifiwe, pokea nguvu ya kutiwa moyo na kila wakati uzidi kutiwa nguvu na usisinyae tena.
Kama kulikuwepo na adui ambaye alikuweza jana, sasa hatakuweza au kukutesa tena
utashangaa unakuwa nguvu mpya, mpya, kila siku na upokee katika jina la YESU.
Kuna watu wametolewa sadaka; sio sadaka zote hutolewa kwa MUNGU zipo ambazo
hutolewa kwa shetani na mawakala wake na sadaka zinazungumza kama umetoa kwenye
madhabahu ya MUNGU itazungumza kwa MUNGU aliyeumba mbingu na dunia na leo
umetoa sadaka yako lipo jambo ambalo MUNGU ataenda kulitenda na kama ulishawahi
kutoa sadaka za kwa miungu / wachawi au shetani mwenyewe sadaka hizo zinazungumza
kwake lakini kwa vile umeamua kurejea kwa MUNGU basi sadaka uliyotoa itafuta sadaka
hizo ulizotoa au kutolewa kwa mashetani. Jiulize nimetolewaje sadaka?
Haleluya, Katika kutolewa sadaka kuna mambo mawili; kutolewa Sadaka ni
kufanyiwa ibada ya sadaka, sadaka inapotolewa au mtu anapodhamiria kutoa au kufanya
ibada yake kwa njia ya sadaka; jambo hilo ni la hiari ambalo mtu huamuna yeye na nafsi
yake kumtolea MUNGU wake, Bwana YESU asifiwe, Hata shetani naye anafanya ibada ya
sadaka. Shetani alitupwa toka Mbinguni na alijua mambo ya Mbinguni maana hata
Mbinguni nao hutoa sadaka, lakini kama wanatoa sadaka hata MUNGU mwenyewe hutoa
sadaka kwenye madhabahu yake na shetani naye alipokuja kutengeneza ufalme wake hata
naye pia hutoa sadaka.
Ibada ya sadaka; ibada hii inakuunganisha kiroho (conection) na madhabahu ambapo
unatoaga sadaka zako ila baada ya mambo kuharibka MUNGU akamtoa YESU KRISTO wa
Nazareti ili sisi wanadamu tupate kibali mbele za MUNGU, kila mmoja anajua kuwa YESU
alifanywa sadaka kwa ajili yetu, MUNGU alitoa sadaka ambayo ni YESU MUNGU ili tupate
kibali, na YESU aliteswa na akafa na akafufuka , naye tena atarudi kuja kulichukua kanisa,
Njia iliyofanyika hapa ya ukombozi ni sadaka.
Somo la sadaka au namna na jinsi ya kumtolea MUNGU sadaka, limekuwa gumu
sana kwa watoto wa MUNGU, ila wachawi na watu wa ufalme wa giza wanalijua sana.Watu
wengi wanaangamia kwa kutokujua Mbinu, Kwa sababu katika baadhi ya makanisa au
nyumba za Ibada, hii Ibada ya sadaka imekuwa ya unyang’ganyi imekuwa ya kushauriana,
sadaka zimekuwa za maumivu, mfano wa Abel na Kaini, walitoa sadaka ila MUNGU alipokea
sadaka ya Abel kwa sababu ilikuwa haina mawaa na ya kaini ilikataa kwa sababu Kaini
alishakuwa na Roho mbaya kwa hiyo sadaka yake illikuwa inanena kwa mashetani. Kaini
akashikwa na wivu kwa sababu ibada ya mwenzake ilifika.
Mimi Hebron nilipokuwa nilianza kazi ya MUNGU kuna wakati nilichukuliwa kwa
kipindi cha kama Miezi mitatu, nilisali Mbinguni na nilitoa na sadaka Mbinguni lakini
nilikuwa sikumbuki kuwa hela nilikuwa natolea wapi, nafunuliwa kidogo, nakumbushwa,
vile atakavyo MUNGU, Bwana YESU asifiwe, niliona Maserafi wakitoa sadaka, wananijua, ni
kwa Neema na sio kwamba nilitaka nijipeleke Mwenyewe ila mimi ni kiumbe chake MUNGU
na MUNGU mwenyewe alipenda nifike huko. (Ni kwa Neema tu) Na ukitaka dunia hii
ikuchukie wafundishe watoto wa MUNGU kweli kuhusu sadaka, (utachukiwa mpaka na
shetani) kwa sababu asilimia kubwa dunianai wamefanya sadaka kuwa ni biashara na Zaidi
imekuwa ni kunyang’anya watoto wa MUNGU; nataka umtolee MUNGU sadaka vile
ambavyo ni kwa mpango wa MUNGU, nasio kama apendavyo mwanadamu, nakata sadaka
yako ifanye kazi Zaidi ya sadaka za mashetani, somo hili kulifundi nimepata vita sana, toka
nilipokuwa napewa maelekezo kuhusu somo hili na napenda nikujulishe kuwa ukilishika hili
somo; itakuwa mwisho wa matatizo yako.
MUNGU alimto YESU kuwa sadaka, na sadaka ile inaongea kwenye madhabahu ya
Mbinguni mpaka leo, anaitwa Mwokozi, Mkombozi, BWANA YESU asifiwe, na wewe ukiwa
unamtolea yeye inafika kwake Mbinguni, kweli tuna Neema ya ajabu, Tumefanya ibada ya
sifa, shuhuda, sadaka Neno na sadaka hizo zinaongea na kuna watu ambao wametolewa
sadaka kwa shetani/miungu au majini , na sadaka hizo zinanena ili wateseke, Mtu
anayeenda kwa mganga anaenda ili akupige akuharibu na akubomoe, unaweza kutolewa
sadaka ili usipae mtoto, cheo, Kazi, mafanikio, utumishi uharibike, sadaka inapiga na wengi
wamepigwa na sadaka za mashetani na wengi wao sadaka hizi zimewapiga sana lakini nina
habari njema nawatia moyo juu ya sadaka za mapepo ambazo ulitolewa na zinanena juu
yako ili usifanikiwe au usifike popote; zinazonena mabaya juu yako, nami nimetoa sadaka
kama kuhani wa MUNGU, na ninaamuru sadaka hizo zikanyamaje zote, wengi mtainuliwa
maana sadaka ambazo zinatolewa na miungu na mapepo na shetani ni za aina mbalimbali
ambazo hazina utukufu wa MUNGU, mfano, huogi, hilali, mchafu,mlezi, mzinzi, kahaba na
mengineyo mengi,magojwa, mateso, mauti na nyinginezo nyingi sana na sadaka hizo
zinaongea kama zilivyonenewaa na inapiga kila jambo ambalo unataka kulifanya, ndio
maana haukufanikiwa au haufanikiwi. Napenda nikufundishe kila jambo lako liombee, litolee
sadaka na kwa kila jambo ambalo utakuwa umetanguliza sadaka litakuwa linapiga aduni na
wewe utapata mafanikio.
Wengi wanaanza na wanaporomokwa kwa sabahu wengi si waminifu kwa MUNGU
na shetani anapata mlango ila kwa wale wa upande wa Shetani wao huwa waaminfu sana
na ndio maana wanafanikishwa na shetani kwa sababu hutoa sadaka kwa kutii na kwa
uaminifu wa hali ya juu, hufanya maagano, maagano, Baadhi ya watu kila mwisho wa
mwaka hufanya ibada ya sadaka kwa wafu, sadaka za maagano na mizimu, huchinja na
kumwaga damu na baada ya kufanya hivyo mwaka unapoanza wao huwa wanaanza na
nguvu mpya kwa sababu walishatoa sadaka kwa mizimu, miungu na majini, Umeshawahi
jiuliza je!wanafanikiwaje? Unaweza jiuliza kuwa inakuwaje? Shetani wala mizimu haina
chochote kitu wanachofanya ni kuchukua / huiba mafanikio ya wengine na kuwapa wale
ambao wanawatii wa ufalme wa shetani. Wengi mmeshatoa sadaka, mbalimbali za damu,
kuchinjiwa na sadaka za kukaa kuogeshwa na mganga, na sadaka zote ambazo ni kinyume
na mapenzi wa MUNGU huongea, kuna ndoa zimetolewa sadaka zimeharibiwa na
mashetani mfano mtu anakuambia nione kuwa utafika WAPI? Mimi inakuambia utafika, na
kuanzia siku ya leo sadaka ulizotolewa kwa mashetani hazitofanya kazi tena kwa jina la
MUNGU wa Ibrahi, Isaack na Jacob. Unaweza kutolewa sadaka ukaacha kazi baada ya muda
mfupi tu, na pia unaweza ukatolewa sadaka ukajikuta unamfuata mwanamume /
mwanamke hadi unaoa au kuolewa naye kipepo, ila leo nitahakikisha kuwa nawapasua
kweye ulimwengu wa Roho na sadaka hizo za kipepo hazitafanya kazi tena, Sadaka uliyoitoa
kwenye madhabahu hii, ikakuponye, kakuinue, ikakukumbuke, ikakufunikishe.
Nataka sadaka ya YESU peke yake ndiyo ikafanye kazi kwenye maisha yako, wengi
mmekuwa wateja wa kwa waganga na ndoa nyingi zinapata shida kwa sababu ndoa nyingi
Mume haitwi mume mpendwa / wala mke, Mume huitwa mume tu na mke huita mke tu
na wanandoa wengi huishi kama wanyama tu, MUNGU mwenyewe ni upendo na ili ujue
kuwa ziko sadaka ambazo zinena za kipepo ndio maana maisha ya baadhi ya ndoa ni
magumu na wala hayaeleweki, MUNGU ni upendo na ndoa ni upendo na anayetengeneza
ndoa ni MUNGU unamchukia au humpendi mke/mume ujue roho ya chuki ndio itawatawala
na ikiingia basi, mlango unakuwa wazi na hatimaye majini na mapepo yanaingia kuwavuruga
kabisa, ndio maana wanandoa mnachoka na kuchokana, kila ambaye ana mke / mme wake
ampende, wengi hujua kuwa upendo ni kupigana mabusu na kushikana mikono ni sawa ila
kuna maisha mazuri ambayo MUNGU amewaandalia wanandoa, siku hizi ndoa ni pesa na sio
mapenzi au upendo, Kuna koo ambazo zimewatolea sadaka mwanake au mwamume ili
wawe na tabia za ukoo (za kimizimu) hivyo ukimwambia jambo hatolitilia maanani kwa
sababu ya sadaka ambazo wazee walishatanguliza awali, na sadaka hizi zinanena, na ndio
maana wanawake wanadharauliwa, MUNGU hapendi, ni tabia chafu na ni laana,
ukimdharau mke/mume wako umejidharau mwenyewe, wanaume wengi ni wakorofi.
Sadaka! MUNGU akamtoa mwanae YESU kuwa sadaka, sadaka hutolewa katika madhabahu
na madhabahu hupokea na madhabahu inayopokea hukaa katika ulimweng wa Roho.
Kama nilivyotangulia kuandika hapo awali kuwa sio sadaka zote zatoka kwa MUNGU, Wapo
baadhi ya watumishi wanaojiita wa MUNGU lakini MUNGU hawajui wala hawatambui, watumishi
hao wanawatoza watu pesa, na wanawafundisha jinsi ya kutoa sadaka, ila namna ya kutoa sadaka
hizo inapingana na vile ambavyo MUNGU aliagiza; hivyo nao hupokea sadaka kimwili na kwa vile
wao wako kinyume na mpango wa MUNGU basi kwenye ulimwengu waroho shetani ndio
anayezipokea. Walienda nao kwa baba yao ambaye ni shetani nae akawafundisha jinsi ya kufanya;
kama ambavyo hata sasa wanafanya michango, Harambee, kupewa vyeti vya hongera unapotoa
sadaka, kuandika sadaka yako jina , kutangaza kiasi ambacho utatoa, hizi si sadaka bora ungekula
chips ila kwa MUNGU wa mbinguni sadaka zao huwa ni siri kwa sababu ni ibada ya sadaka ni ibada
ya siri kati ya mwanadamu na MUNGU. Hii ni elimu toka Mbinguni na ndio Nabii Hebron nimesema
hivyo, MIMI baba yenu, na aliyekuwa baba yangu wa kiroho alikuwa Moses Kulola basi na sitakuwa
na mwingine wa kiroho wa kibinadamu milele ni MUNGU tu na MUNGU mwenyewe ndiye
aliyeniambia hivyo.
Niliyowaambia miaka mingi iliyopita sasa yanaenda kuonekana kimwili, niliyowambia kuwa
kuna kipindi kitafika nitaanza kufufua watu na kimeshaanza sasa na nitaanza kufufua sasa kwa hiyo
msishangae pale ambapo nitaanza kufunua watu kwenye majeneza mda umefika, umefika MUNGU
ameniambia tufanye kazi sasa, unajua MUNGU naenda kwa nyakati; kipindi cha zamani YESU watu
walijua ndio nyakati za mwisho na wanafunzi wa YESU akina Petro walijua nyakati zile ndio mwisho
ila nazo zilipita kabisa lakini mwisho ulikuwa bado, na akina Musa walijua kuwa mwisho ndio
ulikuwa umefika lakini mwisho ulikuwa bado, wakaja akina Elia, Yeremeia, Ezekia, Malaki, Yohana na
wengineo wakasema ndio mwisho umetimia lakini ulikuwa bado. Nina habari njema ninayopenda
kukueleza kuwa kipindi kile hakikuwa mwisho ila kipindi hiki na nabii wake nikiwepo ndio mwisho
atakuja YESU; MUNGU anaenda kwa majira na nyakati na sasa ndio wakati wa kuja YESU, sasa sio
uache kufanya kazi na maendeleo, mimi mwenyewe sijui ni lini ila YESU anarudi na ni kipindi chake
ila siku imefichwa, nimewaeleza kuwa hata Mbinguni nimekaa na hata sadaka nilikuwa natoa ila
sikuwa najua hela nilikuwa nazitolea wapi, Ibada nilikuwa naingia pia lakini nakumbushwa kidogo,
vile ambavyo MUNGUU mwenyewe anapenda, ananikumbusha kidogo sana, anavyopenda yeye
mwenyewe, sasa inatakaiwa tumtolee MUNGU kama vile mbinguni wanavyomtolea, neno lake
tufundishe na kulitendea kazi kama vile Mbinguni wanavyofundisha, tumuimbie kama vile Mbinguni
wanavyomuimbia, Ubatizo wake kama wa Mbinguni ila ukipokea kinyume na vya MUNGU utakuwa
umeenda kuzimu.
Sadaka za kutolewa yaani ambazo watu hukutolea au hukutoa wewe pia sadaka kwa
shetani, miungu na mizimu, (Ni zile ambazo watu huenda kwa waganga, miungu, mizimu, mababu,
wachawi kwa jambo Fulani, ibada hizi huwa zinamadhara makubwa kwa sasabu mwisho wa siku hata
yule aliyemtolea mwenzake na wewe ulietoa wote mnakuwa mali ya shetan, hakuna cha bure kwa
shetani) Sadaka hizo zinakuwa na jambo la kukupiga, kukudhoofisha, umasikini, kuwa mtumwa au
magonjwa wako ambao walitolewa sadaka kwenye mali zao hawafanikiwi, kwenye Elimu
hawafanikiwi na wako waliotolewa sadaka ni wazito tu wawe wazito tu kwa kila jambo; ila
nakufundisha kuwa kila jambo penda kulitolea sadaka ili kila wakilisogelea wao ndio wanapingwa tu;
toa sadaka yako kweny madhabahu ya MUNGU iliyo hai, sadaka hunena, hulinda, sadaka ni ibada
ambayo inazungumza Mbinguni na inatenda kazi, shetani alitaka dunia isisamehewe kabisa ila
angalia sadaka ya MUNGU ilivyo, YESU akafa, tukasamehewa wote, mtukuze MUNGU kwa hilo; pia
sadaka ya shetani haikubaliki kwa MUNGU ila wengi waliomkubali MUNGU watapita katikatai yao;
hawatapata madhara penda kumtolea MUNGU sadaka, Ikiwa ni elimu, kazi, biashara, maisha ya kila siku,
itolee sadaka, toa sadaka yako, nenea ikutoe mahali popote uliposhikiliwa na yawezekana
kuwa umeshikiliwa mahali kwa sadaka; kimwili unaishi lakini kuko mahali ambapo umeshikiliwa na
wanawakeau wanaume au sehemu uliyokuwa ukifanya kazi, unaona huendelei mbele upo kituo
kimoja, maisha magumu, toa sadaka ya kujitoa huko utaona unatoka na kwa jina la YESU na
unakuwa huru, toa sadaka yako kwa jambo ambalo unlipitia, ili upone, kwa sababu kuna wengine
wametolewa sadaka ili wasipone sasa wewe toa sadaka kwa BWANA YESU, mwambie naomba
nipone na utapona, utakuta baadhi ya watu wanateseka miili yao inakonda, imechoka na hawawezi,
unakuta na mikono pia imetolewa sadaka haufanikiwi, chuma ulete, unajikuna kuna tu mkono eti
utapata hela kumbe ni chuma ulete, nimekufundisha siri kubwa sana; hata wale wachawi ambao
wanakushughulikiaga, wanakusumbua nao wanatumia sadaka, lakini wewe ukiwa mahali ambapo
MUNGU yupo; wachawi hawana guvu nao wanafyekwa kirahisi sana.
Kuna sadaka uinaweza kuwa maji ya chooni, au mkojo, damu ya kunguni, kinyesi, damu ya
mbu, kwanini Ibrahimu kawa baba wa mataifa mpaka leo? MUNGU alimjaribu kuwa akamtolee
sadaka na alimpima Je! ni sadaka ya upendo na Je! Inatoka moyoni? Sasa watu wana danganywa toa
sadaka inyouma, wakichukulia au kudhani kuwa sadaka aliyoitoa Ibrahimu ilimuuma, alipoambiwa
kuwa amtoe mtoto wake, hapana! Ibrahimu hakuumia au kuumwa moyo; MUNGU alipomwambia
nitolee mtoto wako awe sadaka, na kwa sababu Ibrahimu alimpenda MUNGU sana na alitoa sadaka
ile ya mtoto kwa upendo. Alifurahi tu kwa kumsikiliza MUNGU japo MUNGU alikuwa akimpima na
alipokuwa anataka kumchinja tu, alipogeuka nyuma akaona mwana kondoo akamchinja, kondoo
ikawa sadaka, akamwambia Isaka twende. MUNGU alikuwa nampima Ibrahimu lakini habari ya
kutolewa damu tena haipo katika ufalme wa MUNGU kwa hiyo kwa sasa wanaotoa damu ya
mwanadamu kama sadaka hao ni wachawi, wachawi ni watu ambao wanashirikiana na shetani ila
madhabahu ambayo ipo Mbinguni haishirikiani na shetani kwa sababu damu ya YESU ilimwagika
mara moja kwa ondoleo la dhambi na YESU alifanyika kafara ili damu isimwage tena, na hata sasa
kuna baadhi ya makanisa huchinja kama sadaka na endapo wanachinja, chinja hiyo madhabahu sio
ya MUNGU ni ya shetani, yapo baadhi ya makabila ambayo yanachinja chinja sadaka za mizimu
sasa unaona vile ambavyo watu wamekuwa na muunganko (connection) wa shetani? na mapepo na
majini na wengine wako makaburini kwa sababu walitolewa sadaka za makaburini.
Kila mara penda kukomboa watu, wateja na vitu vyako na wewe mwenyewe na ujifunike
kwa damu ya YESU, vitu vyako vikiwa wazi bila ulinzi, na ukiacha kuvitolea sadaka za ulinzi, watu wa
shetani hupitishwa na kukuibaia, ila ukivitolea sadaka, na kumkabidhi MUNGU wachawi
hawataviona, sadaka ina nguvu sana, najua wengi mmeshaambiwa kuwa tumeshakuendea kwa
mganga, hesabu siku tu kwa sababu wanakuwa amekuendea kwa mganga na wakutolea sadaka
wanapokuambia hesabu siku tu ujue wameshakunene mabaya yaje yakupate lakini ukiwa kwa
BWANA YESU; sadaka za waganga hazitofanya kazi kwako, kwanza madhabahu inakulinda na
wakijaribu tu; madhabahu inawapiga hao maadui.
Napenda nikufundishe ujanja wa shetani, endapo upo katika madhabahu sahihi shetani
atajitahidi kwa gharama yeyote akutoke ili akupate, akutoke kwenye mikono sahihi ya MUNGU,
akutoe kwenye madhabahu sahihi wewe utajisikia kuwa upo upo tu, husikii tena kuomba, kuja
kanisani, kusoma neno au kufanya kazi ya MUNGU ukiona hivyo chukua angalizo mapema, ujue
kuwa shetani anataka kukuchomoa hapo. Ukiona hali hiyo wewe ikatae kimbilia kanisani, omba
MUNGU akuvushe nae atakuvusha, wachawi ni waaminifu kumtolea shetani hata kama amepewa
masharti magumu kiasi gani, mhusika atamtii shetani/ mganga, lakini wakristo wengi unasahau
mpaka kumtolea MUNGU wetu sadaka, unajua jinsi ambavyo unatoa kila wakati ndivyo ambavyo na
MUNGU anakupa Zaidi, unaweza ukawa umetolewa sadaka mwezi wa fulani usishike kitu ukaona
mwaka au maisha ni mabaya ila napenda nikufundishe kuwa mwaka sio mbaya wala maisha sio
mabaya, wala hakuna siku au mwezi mbaya ila sadaka za wachawi na mabaya ndizo zinazonena juu
yako.
Toa sadaka kwa MUNGU inene iombee inene kama ya Abel , sadaka ina nguvu, nataka
nguvu ya sadaka ikafanye kazi leo kwako, nguvu ya sadaka ya MUNGU wa Mbinguni; toa sadaka
yako hata kama mfano unakwenda mahali fulani utaenda na utarudi salama; unapitia jambo Fulani
gumu litakuwa jepesi, huna Amani utapata Amani. Bwana YESU asifiwe, sadaka ya ushindi, tolea
mwili wako sadaka, unaumwa kila saa tolea sadaka, sadaka ya Mbinguni huambiwi leta au
kulazimishwa kutoa, sadaka hii tu mwenyewe hutoa kwa hiayi yako maana wewe mwenywe ndie
unayejua kuwa unataka MUNGU akufanyie nini, wewe mwenyewe ndio unajua, yamkini ulitolewa
sadaka ili uwe na mdomo wa matusi, utapeli, kufungwa gerezani, kukosa kazi, mateso, maumivu,
sadaka hizo hunena pasipo Neema ya MUNGU zitafanya kazi ambazo zimenenewa huko kwenye
malango ya giza.
Unahitaji jambo fulani, nyumba, kiwanja, maendeleo fulani, Je! Umeyatolea sadaka?
MUNGU atajua mchumba au mume wako kuwa kuwa ni fulani, au jambo lako limecheleweshwa na
kitu fulani, toa sadaka. Mtu anaweza kukuambia niombee niopate mke au mume, unamwambia
sawa unamwombea na anapata kitu anachotaka , ila watu wengi wanajua kuwa ukipata mume au
mke hata kama ni wa maombi hakutakuwa na mchangamoto, jua kuwa mume au mke kuna siku
atakasirika, atanuna, sasa akianza kununa mhusika nae ataanza kununa, na kumlalamikia na
kumkasirika MUNGU kuwa kwanini MUNGU umenipa huyu….halooo… majaribu hayakwepeki yapo
tu kukuweka imara ila ukiwa umemtolea sadaka neema na ulinzi wa MUNGU upo nae na tabia
ambazo huzipendi zitabadilika.
Toa sadaka yako kwa ajili ya watoto wako sadaka ya kulindwa, ya kupata ada mpaka
wamalize shule, mafanikio ya kimwili na kiroho, ulinzi wa MUNGU, dunia imeharibika, hata YESU
alipelekwa kanisani ile sadaka ikamlinda YESU ila kwa sasa imebadilika, unabatiza motto kwanza
hapo ulinzi unakuwa umeondoka na wakati sahihi ambao alitakiwa kubatizwa ndipo anabarikiwa
(Mtu anatakiwa abarikiwe, ( wakfu) ndipo abatizwe) unaletwa kanisa ukiwa mtu mzima
hukubarikiwa ukiwa mtoto, sasa hapo katikati mabaya mangapi umeshapitia na sadaka ngapi za
mabaya zimeshanena juu yako maana hukuwa na ulinzi wa MUNGU, unakuwa unatembea lakini
umekufa,. Unaweza ukawa unaombewa sana mambo yanatoka yanarudi na wewe yatolee sadaka
kama madhabahu unayoabudu ni ya YESU, utaona maadui wanafekwa. Mtu anaweza kukuambia
kuwa mimi siolewi au kuoa ninamwambia anza kumtolea MUNGU sadaka na uinene mwenyewe
kwa ajili ya mume/mke na baada ya muda anaona mambo yamenyooka lakini ukienda mbele za
MUNGU kutoa sadaka usiende na majibu yako yaani mfano MUNGU naomba niolewe na bwana au
nimwoe binti yule hiyo ni batili unakuwa umeenda kwa MUNGU na majibu yako; Nenda kwa
MUNGU na ombi kuwa naomba mke / mume, kazi au jambo Fulani na MUNGU atakupa zuri na la
mapenzi ya MUNGU sio ya mapenzi yako. Hata mimi nimeshatolewa sadaka nyingi na siku moja
nikaona wamenitolea sadaka ya nyangumi ili niache kazi ya MUNGU na mimi nikawarudishia ya kwao
na wametoa nyingine nyingi ili nirudi nyuma, nisihubiri, nisiwafundishe, nisifundishe kweli ya
MUNGU na mambo kama hayo, lakini kwavile niko kwa MUNGU basi sadaka zao hazikunena na mimi
namtolea MUNGU sadaka pia.
Unaweza kutolewa sadaka ya kushangaa shangaa, usifaulu, usifike kwenye madhabahu ya
MUNGU ya kweli, utakuta mtu anapata vikwazo ila ninazipindua hizo sadaka kwa jina la YESU,
sadaka za miungu, za majini, Eliya alitoa sadaka zake ndio maana alipaa Mbinguni, sadaka inaleta
rehema, heri, inaondoa matatizo, mikosi na kuchoka vibaya na utapiamlo, na mambo mengi ambayo
adui amekutengenezea ila sasa endapo wewe upo upo tu huko kwa MUNGU au kwa shetani, wala
sadaka zako humtolei MUNGU ila unazitoa kwa shetani hatima yake hufanikiwi Ssa ukiona wenzako
wanafanikiwa utaishia kwenye wivu pale ambapo wenzanko wanabarikiwa, unabakia na roho yako
mbaya tunaelewana? Mtoleee MUNGU sadaka ya Rehema kwa sababu umefanya dhambi kwa
kujua na kutokujua na kuna watu wanakaa kwenye nyumba za kupanga hawanunui hata bakuli au
waume wao au wake wanalewa, watoto wanaumwa tukumbe wametolewa sadaka, mtu akipita
ananuka sigara tu au pombe tu, mtu anachukua nyota yako anakuachia matatizo ili azidi kufanikiwa yeye,
chanzo ni sadaka alizotoa zinanena mabaya juu ya mtu husika.
Inaumiza ila lazima umtie moyo, tumetumwa kuwaokoa wote wamrudie MUNGU, toa sadaka kwa
MUNGU mambo yataenda tu, kazi huipati utaipata tu, utaona mambo yanaenda, ibada ya sadaka ya
kweli inajibu sana ila shetani kawafunga watu wa MUNGU kawawekea ubahili na uchoyo ili
wasifanikiwe na sadaka zingine ni zile za mtu kulala na mbwa, kurudi kinyumemnyume uchi,
watenda kazi wa shetani ni waaminifu kweli kweli pata picha mtu anavua nguo zote halafu anakuja
kinyumenyume ndio sadaka, ipo ya kuishi na majini hawaondoki na walipewa damu, sadaka ya
kuolewa na majini ambayo yamkini ulitolewa au majini walikutolewa na wakakuoa, Ila sadaka zote
hizo kwa MUNGU hubatilika, Mtegemee MUNGU, mpende MUNGU kwa akili zako, mali zako na kwa
kila kitu chako, kumbuka kumtolea MUNGU sadaka mara kwa mara zipo sadaka za aina nyingi sana,
Roho Mtakatifu akuongoze.
SALA YA TOBA: Bwana YESU nakuja mbele zako mimi mwenye dhambi; ninaomba
unisamehe; ufute jina langu, kwenye kitabu cha mateso cha ibilisi na naomba uandike jina langu
kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, BWANA YESU, nakuomba na ninajua kuwa wewe ni
sadaka ya MUNGU ambayo alikutoa ili mimi nikombolewe, nami nasogea kabisa kwako BWANA
YESU uniokoe kwa damu yako na kwa neno lako nimekusogelea BWANA YESU, ninatubu nimeshiriki
kwa kujua na kwa kutokujua na nilitoa sadaka kwa mashetani na mizimu na miungu na mapepo
wakaniunganisha na mambo yao na ufalme wao nakuomba BWANA YESU kwa sadaka niliyotoa leo
ikanitoe kwenye ufalme huo wa giza na ikanitenge na huo ufalme kwa jina la YESU, AMEN.
Kwa jina la YESU KRISTO wanazareth ninatuma damu ya YESU kwenye ulimwengu wa Roho ,
na nianamuru sadaka zote za shetani zitoke, kwa jina la YESU, mliotolewa sadaka kwa mapepo na
majini yanaishi kwenye miili ya watu na kwa sadaka ambayo kuhani wa MUNGU, mimi Nabii Hebron,
nimetoa leo hayo yote yaondoke kwa jina la YESU mabaya yote yaondoke, sadaka za kulindwa na
mapepo ziondoke kwa jina la YESU sadaka za damu za aina zote zinazonena ziondoke zote kwa jina la
YESU. Damu ya YESU ikanene mema juu yako na vitu vyako vyote ninavifunika kwa damu ya YESU
Kristo wa Nazaretha aliyehai, na Madhabahu zote za kipepo ninaziamuru zikuachiwe na ufunguliwe
kwa jina la YESU.
MUNGU awabariki, MUNGU awainue, Amani ya MUNGU iwe nanyi na damu ya YESU izidi
kunena mema juu ya maisha yenu. Amen.
Mtume na Nabii Hebron.