Pages

Sunday, September 19, 2021

 

MUNGU AMEISAMEHE DUNIA NA CORONA (COVID-19) IMEONDOLEWA

Haleluya!

Bwana YESU asifiwe,  Nazungumza lile ambalo MUNGU ananiambia sasa na pia mnamo tarehe 14.09.2021 alinipa ujumbe wake kuwa niiambie dunia imesamehewa. Ameniambia kuwa dunia hii  inaishi  kiunabii, kuishi maisha yako wewe ni kinabii, mwanangu alivyokuja hapa duniani ni unabii, ninaposema  mwanadamu atakufa ni unabii na hakuna mtu ambaye anaweza kupinga,  Neno la MUNGU tunalolisoma ni unabii, Je! Kuna mtu ambaye hatakufa? Kinywa cha MUNGU kilishasema, na Je! unaweza kupinga kuwa si unabii? na shetani hapendi  kusikia unabii wa MUNGU na ni wakati wa  nabii za kishetani kuisha, wale ambao wanang’ang’ania  na MUNGU Mpaka mwisho, MUNGU ataweka kitu chake kwao na watashinda, kuzaliwa ni unabii, mwanamke na mwanaume wataoana na watakuwa mwili mmoja ni unabii, au ni mipango ya wanadamu? Hapana! YESU kuja kwake ikatokea ni unabii, Yohana Mbatizaji akatangulia ni unabii, alisema nasafisha njia kwa ajili ya yule ajaye ni unabii, leo tunasoma  neno la MUNGU na kumsifu YESU chanzo chake ni unabii na maisha yako penda yawepo  katika  unabii wa MUNGU na kama yalikuwa kwa shetani yatoke huko.  Iliandikwa katika vitabu vitakatifu kuwa nyakati za mwisho kutakuja magonjwa na mapigo na yamekuja ni unabii, utasema dunia haiishi katika unabii? Lazima iishi katika unabii maana yeye aliye Nabii mkuu ambaye ni MUNGU ndiye aliyeiumba dunia, MUNGU  yeye ndie anayeyafanya hayo yote.

Basi yako aliyoniambia MUNGU aliyekuumba wewe,  akaniambia waambie na mataifa yote na ndio maana hata leo  matawi yote ya  Kanisa letu yanasikiliza mubashara (online) MUNGU ana njia nyingi za kufikisha ujumbe wake.  Niliwaambia tuombe toba na rehema kwa ajili ya dunia, mmeomba, BWANA YESU asifiwe, sasa  kama alishasema kuwa katika nyakati za mwisho kutakuwa na mabaya na mimi Nabii wake ninapoenda kumwomba MUNGU  na MUNGU ananipa malelekezo  kuwa kaombe hivi na kutokana na maagizo ambayo MUNGU amenipa nami natii na kuyafanyia kazi, Napenda kuwatangazia wale ambao mnanisikiliza kuwa  lile pigo lililokuwa limeipiga dunia ambalo ni shetani alikuwa ameipiga  dunia kisawasawa, ikapelekea watu kupoteza maisha, watu wamepoteza ndugu, watu wamepoteza kazi, maisha na wengine wanateseka sana na sio MUNGU aliyelifanya ila ni shetani ndiye alikuwa  akiitandika dunia na akitandika mataifa  kwa sababu dunia ilijaa dhambi, watu wote walitenda dhambi, Matajiri kwa Maskini, wafalme, maraisi, maspika, watumishi mbalimbali  wanaojiita wa Mungu, maaskofu, wachungaji, mitume, manabii, walimu na wengineo kwa vyeo vyao inamaana wote walifanya dhambi, MUNGU akaondoka na MUNGU anapoondoka shetani anapata nafasi,  MUNGU  ni amani, MUNGU ni  uzima, MUNGU ni  ushindi wetu,  MUNGU ndiye uzima wa milele, MUNGU ni uponyaji, basi ndipo shetani ambaye ndiye ugonjwa akaingia,  shetani yeye ambaye siyo amani akaingia, shetani yeye auaye na kuteketeza akapata nafasi   ndipo ikawepo kazi ya kumwondoa,   na kazi ya kumwondoa  ilikuwa ni kuomba toba na rehema na dhambi sasa imeondoka katika dunia nzima,  na MUNGU ameisamehe dunia nzima,  amesamehe  na kufuta wala hakumbuki maovu ya wanadamu.

MUNGU akaniambia Hebron nenda   kawaeleze kuwa nimewasamehe na hata kanisa limesamehewa, MUNGU anaposamehe anaanza upya na wewe maana shetani ameng’olewa sasa msikubali tena kutenda dhambi. Mmefunga, mmelia, lakini zaidi ninachowaeleza endelee kumnyenyekea MUNGU, atawanyanyua sana, acheni  kujikuza, nyenyekeeni sana, mnyenyekeeni MUNGU  yeye MUNGU akapate kuwanyanyua, ndiyo kazi iliyobakia kumyenyekea MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia.

BWANA YESU asifiwe, kati ya wiki  mbili au tatu zilizopita niliwaambia kwamba  MUNGU ameondoa Korona katika Nchi ya Tanzania na sasa si mnaona imeisha na ni kwa Maombi tuliyoyaomba, Tanzania ndiyo Eden  na kupitia Maombi hayo COVID imeondolewa duniani kote, na haitarudi  tena, itabakia  mkiisikia kama historia. MUNGU ameiondoa; na muda mfupi ujao  mtasikia imeisha kabisa na itakuwa ni historia. MUNGU ndiye aliyefanya hayo maana katika Neno  la MUNGU anasema mnaponirudia,  wanangu, MIMI MUNGU nitawasamehe na sasa ameiponya Nchi.  Nilieleza mengi kwenye clip ya Tarehe 15.09.2021. Muwe mnapenda kusoma  na kufuatilia blog zangu ili mjue ni nini kinachoendelea; na mipaka ya Nchi mbalimbali itafunguliwa na safari za Ndege zimeshafunguliwa, mtaziona.  Maana kupitia pigo hilo wengi walikosa ajira,  wengi walifukuzwa kazi, sasa kazi zinarudi na watalii watakuwa wengi sana, mliofunga makampuni yanafunguliwa. Mshangilieni MUNGU si jambo dogo, ni siku ambayo shetani  analia sana. Viongozi wengi  walikuwa wafe sasa hawatakufa tena,  masikini  hawatakufa, matajiri hawatakufa, waumini hawatakufa, watoto wa MUNGU hawatakufa tena kwa ugonjwa kwa pigo hilo, umasikini unaondoka, tumshangilie BWANA YESU, wengi mmepoteza watu na uchumi umeharibika, BWANA YESU anaujenga upya, nimesema niwajulishe ili msibakie kituo kimoja cha kuendelea kuomba rehema wakati kwa neema ya MUNGU tumeshasamehewa  dhambi.

Dhambi  imeshang’ooka ni kazi kubwa mmefanya, Mbingu imetuombea na  MUNGU ametusikiliza, maana wanadamu walijitahidi kwa kila namna, ila ilishindikana,  hapo ndipo  dunia ijue kuwa MUNGU yupo, MUNGU ni zaidi ya sayansi na wanadamu na  sayansi na akili za wanadamu  kwa MUNGU si kitu, MUNGU ndio mwana sayansi mkubwa.  Bwana YESU asifiwe.

Nimekuwa nikitafakari,  wewe ambaye unayepata kusikia kitu cha kweli  toka kwa MUNGU, Mshukuru MUNGU, wapo wanaoambiwa vitu lakini havitimii kwa sababu havitoki kwa MUNGU. Msamaha huu ni kwa mataifa yote na Nchi zote Rehema imepita. MUNGU wetu anajibu maana MUNGU wetu si baali; niliwaambia kuwa sitakufa na Corona na  sijafa bado nadunda na naendelea kumshukuru MUNGU,  maana kila eneo umesamehewa, endelea kumshukuru MUNGU maana umesamehewa, usikumbuke mambo yaliyopita machafu.

 MUNGU  ni amani na BWANA ameanza na wewe,  njia ulizokuwa umeona zimefunga, zimefunguka na  BWANA akiwa na wewe kila mlango utakuwa wazi  akiwa na wewe anakulinda hakuna ambaye atakupiga, basi amenieleza kuwa epukeni dhambi, ila ameniambia kuwa wale ambao wanatumia jina lake kwa   uchawi, nguvu za giza,  kuwanyang’anyia watu pesa,  kufanya  miujiza ya kipepo,  bishara, na wale ambao wamejiita hao sio watumishi wake MUNGU  aliyeumba Mbingu na Dunia. MUNGU ambaye anafanya jua litembee, amesema hivi “Hasira yake itakuwa juu yao milele na hao hawajasamehewawatakufa sana, wataporomoka sana, si mimi  nimesema, ila ni  MUNGU kaniambia hivyo; kwa sababu wao ndio walikuwa chanzo cha watu kufanya dhambi  na shetani akawa hawagusi ila sasa MUNGU ndio ameanza kazi yake, na mimi siwezi  kupinga kazi ya MUNGU” na amenionya kuwa "peleka ujumbe wangu hivi ninavyotaka."  Mwanaye anarudi  kuchukua kanisa. Japo wanadamu wanaonaga kuwa MUNGU ni mpole tu.

Nilikuwa naomba na kuna mambo ambayo  nilikuwa nakutana nayo mpaka mimi mwenyewe nikamwonea MUNGU huruma, mpaka nikamwambia MUNGU pole yaani kwa vile nampenda mpaka imefikia mahali namwambia MUNGU pole;  ni kwa sababu kile ambacho nimekiona kilikuwa si cha kawaida, kwa sababu MUNGU amemuumba mwanadamu, akamweka duniani, Mwanadamu  akampa MUNGU kisogo,  na ni kama vile ambavyo wewe unampa MUNGU kisogo,  MUNGU akaipa dunia kisogo na akawa anawaangalia wale ambao  walikuwa wanamwangalia MUNGU aliwaponya; na wale wengine wakapata mapigo, lakini sasa amewasamehe wote.

 MUNGU amemuumba mwanadamu kwa gharama kubwa, nguvu zake  amezileta kwa gharama kubwa sana  lakini   huyu huyu mwanadamu anashika biblia na anaenda kuhubiri na kuchezea jina la MUNGU na anatumia nguvu za giza. Yaani nilitafakari, nikaumia,  mpaka nikamwambia BABA pole,  hivi kama ni wewe  utafanyaje? MUNGU atukuzwe maana ni MUNGU wa rehema,  MUNGU atabakia kuwa ni MUNGU wa rehema tu ila ndio hali ilivyo  katika dunia mambo sio mazuri hasa katika baadhi ya makanisa na asilimia kubwa  kanisa limetekwa na shetani hivyo limekuwa liovu na hapo ndipo shetani atakapokamatia watu.

Bwana YESU asifiwe, ndio maana  unatakiwa kuishi kinabii na ninaishi kufuatana na Roho Mtakatifu anavyoniongoza na ninaishi kinabii,  na sio kwa kalenda. Ninaishi vile ambavyo MUNGU anataka,  mnatakiwa mumpende MUNGU mnaimba MUNGU ni pendo   anapenda watu lakini baadhi wa watu hawampendi MUNGU,  wanapendaa 'boy and girls friends' Kuliko MUNGU watu wanapenda Pesa; napenda  niwaambie MUNGU ni pesa, jina lake ni mali,  MUNGU ni dhahabu, hebu mpende yeye  mali na pesa utazipata, MUNGU jina lake ni  mali, ana majina mazuri; majina mazuri yote ni yake. Mpende MUNGU. Wengi wanakimbilia kwenye mali, huko  ndipo wanasombwa na mwovu, mpende MUNGU kama Ibrahimu, Sulemani, na  Daudi, hizi ni nyakati za Mwisho mumpende MUNGU zaidi,  wengi wanakuja kwake ili kupata baraka za MUNGU lakini hawampendi MUNGU.

Unampenda MUNGU, unampenda  YESU kama hivyo basi toa maovu yote ya moyoni kwako halafu moyo wako umwachie YESU; nikisema utoe vyote ni vile vibaya, maana dhambi ilifanya watu wakiomba hawajibiwi, watu wakitoa sadaka hazipokelewi, machozi mengi yakawa unafiki mbele za MUNGU maana hayakuwa maombi yenye majibu,  na badhi wa watumishi wakawadanganya hata wakuu wa Nchi kuwa tunaombea Mataifa yenye dhambi; ila maombi yao hayakufika maana  wangewaombeaje wakati wao wenyewe waliokuwa wanaomba walikuwa na dhambi; lakini MUNGU  ni wa rehema. Tumeomba, akasikia na ameyarehemu mataifa yote, akaniambia "wewe nimekuita ni nabii wa Mataifa, waambie watasikia na wale ambao  watanitafuta  waendelee kunitafuta kwa bidii na wataniona."

  MUNGU awabariki, MUNGU awainue.

 

Imeandikwa na Mtume na Nabii Hebron.