SALA YA BABA YETU
Mathayo 6:7-15 - Sala ya Baba Yetu aliye Mbinguni, Je! unajua ni kwanini YESU alisema BABA yetu uliye Mbinguni? na kwanini hakusema baba yetu uliye Kuzimu? Na je! BABA yako yuko Mbinguni kweli? Au baba yako yuko dunia? Au yuko Kuzimu?
Nanyi mkiwa katika kusali msipayukepayuke kama watu wa Mataifa, maana wao wanadhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi, basi msifanane na hao, kwa maana Baba yenu anayajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba, Basi salini hivi Baba yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe, mapenzi yako yatimizwe duniani, kama Mbinguni, utupe leo riziki yetu, utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe wadeni wetu na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele, amen. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na BABA yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala baba yenu hata wasamehe ninyi makosa yenu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
BWANA YESU asifiwe, sala hii kila mmoja anaijua na kama kuna ambao hawaijui watakuwa wachache sana, lakini nataka sala hii ikafanye kazi kwako, maana hapo awali, kabla ya kupata Neema ya Wokovu, niliomba sana lakini haikuwa inafanya kazi, kiroho, ili MUNGU awe BABA yako, lazima uokoke, na mimi niliitajaga sana sala hii wakati nilipokuwa bado sijaokoka, na niliwacheka wale ambao walikuwa wameokoka, na hata sasa wengi wanaing’ang’ania sala hii na kuitaja pasipo kuokoka, MUNGU hawezi kuwa Baba yao, hivyo basi baadhi ya wanadamu kwa kujua au kutokujua baba yao sio wa Mbinguni, kwa sababu tu hawajaokoka, hizi riziki haziwezi kutokea, wala msamaha hauwezi kutokea kwa sababu katika ulimwengu wa Roho kuna baba wa kiroho wa aina Mbili, MUNGU ambaye ndie BABA wa Mbinguni na yuko baba wa uongo ambaye ni shetani, kumbuka kuwa ni kipindi cha hatari sana maana shetani yupo kila mahali lakini YESU amenituma nikufunulie siri hizi, Nina Imani kuwa watu wote wanapenda MUNGU awe baba yao. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Kuna mambo ambayo yamefichika na leo naenda kuyaweka bayana ili uweze kujielew kuwa upo upande wa MUNGU au wa shetani maana shetani naye anaweza akawa baba yako kwa kujua na kutokujua, na kumbuka kuwa shetani hajakuumba ila ni mjanja anakuteka, unajua kwanini YESU alisema BABA yetu aliye Mbinguni? Kwasababu YESU alitumwa na BABA yake akatufanya na sisi tufanyike kuwa watoto wa BABA wa Mbinguni, kwa kuokoka na kukubali kumtii yeye, na ukiisha kutii anakuandika kwenye kitabu chake cha uzima wa milele, kuwa huyu ni mtoto wangu na unapomwomba anakujua, anakupa riziki, anakusamehe, anakuinua, BWANA YESU asifiwe, sala hii inamaliza kila kitu, MUNGU anasema mapenzi ya MUNGU yatimie, Baba yetu uliye Mbinguni mapenzi yako yatimie, Je! MUNGU anatuwazia mabaya? Hapana! Ninaposema mapenzi ya MUNGU naomba mnielewe kwa sababu wanadamu wengi wamekolea kwenye uzinzi sio haya ila ni mapenzi ya MUNGU. Mapenzi ni kile ambacho MUNGU anakitamania kwako, yaani anakupenda, ukiangalia mambo ya MUNGU yanastaajabisha sana, angalia nyota kukaa angani ni mapenzi ya MUNGU, na imetulia pale, Jua kukaa angania ni mapenzi ya MUNGU, sayari nazo zinavyoning’inia ni mapenzi ya MUNGU, BWANA YESU asifiwe, amemuumba mwanadamu ni mapenzi yake MUNGU, yaani mapenzi ya MUNGU ni makusudio mazuri yake MUNGU. Lakini mwanadamu huyu huyu ndio kabadilika na hataki mapenzi ya MUNGU hamtaki BABA yake aliyemuumba, amemkana kwa kujua na kwa kutokujua, unaweza ukawa umemkana Baba yako, Baba yako ni Baba yako tu, hata kimwili watu huwakana wazazi wao na pia inawezekana kuwa na wewe upo hivyo kwa MUNGU, unatakiwa uokoke ili BABA wa mbingungi awe baba yako na kama huokoki baba yako anakuwa ni shetani japo wewe hutasema kuwa shetani ndio baba yako kimwili, kiroho ndivyo ilivyo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Lakini MUNGU ni wa haki na amemtuma mwana wake wa pekee atutengenezee njia na amenituma niwaeleze, amesema Mataifa yote yamrejee MUNGU ili MUNGU awe ndio BABA yao, maana wengine baba yao ni sanamu, majini, waganga, nyoka, au shetani na ndio wanaowaabudu na kuwatolea sadaka, hilo niangamizo, hii sala imefanywa kama ngonjera, napenda nikufundishe ili kila kipengele kikafanye kazi kwako, utusamehe, utusaheme, usamehewe kweli, BWANA YESU asifiwe, yawezekana umeokoka lakini yamkini bado shetani ni baba yako na shetani anafuatilia hapo, shetani hapendi wanadamu wawe wa MUNGU na pale unapookoka shetani huchukia na kuzidisha vita maana umeshamkana kuwa sio baba yako tena, lakini hilo lisikutishe, YESU mwenyewe alivyofuatwa na shetani kule jangwani, alimtaka YESU afanye mapenzi ya shetani ila YESU alikataa, sasa kama YESU alikataa kwa nini wewe usikatae? Unapokataa mapenzi ya shetani MUNGU anakufurahia na kukupenda na ahadi zake zinakwenda kwako na atakukumbatia naye atazidi kukulinda zaidi na MUNGU anapofanyika kuwa baba yako na kule Mbinguni hufurahia kuwa mwanangu anakuja. Na unapodanganywa kuwa usiokoke, ukakataa kuokoka, baada ya maisha haya utachomwa moto, unaweza kuwa mkristo na ukadanganywa kuwa usiokoke ukiwa hai mpaka utakapokufa, usikubali kudanganywa, MUNGU sio wa maiti MUNGU hasikilizi mzoga, ukifa hutaweza kutubu, (Sio mpaka uwe mzoga, ndio upelekwe Mbinguni yaani hujaokoka, hujampoka YESU hujatubu kabla ya kufa au ukiwa na nguvu zako). Okoka ili MUNGU ajivunie mbele ya shetani kuwa wewe ni mwenye haki wake, MUNGU alijivunia mbele ya Shetani kipindi cha Ayubu kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki wa MUNGU na alifanya mapenzi ya MUNGU tu, mimi sijui kuwa wewe u mtoto mpendwa wa MUNGU au wa shetani, Huwezi kusema baba yetu wa Mbinguni wakati unaabudu sanamu, maana MUNGU wa mbinguni hana sanamu, BWANA YESU asifiwe, MUNGU ndiye aabudiwaye na sio sanamu, mapenzi yake aabudiwe yeye, mapenzi yake tuokoke, mapenzi yake tubatizwe ubatizo wa Yohana, tena mtoni na sio kwa kikombe, wala kisima, wala wa vumbi, au mchanga, au wa bwawa la kuogelea (Swimming Pool) hayo hayaletwa wala hayakuandikwa katika kitabu kitakatifu sio mapenzi yake MUNGU. YESU ndio njia na alikuja kuonyesha njia na ni lazima tuifuate, YESU ndio njia ambayo ni mapenzi yake MUNGU na ni lazima tubatizwe kama YESU naye akatujue kuwa sisi ni watoto wake, Baba yetu aliye Mbinguni, hebu jikague mbona unakwenda kwa waganga kwenye matambiko, mbona hutaki kuokoka? Mara unaokoka unatoka tena? Humtaki MUNGU? Unapotoka kwenye wokovu au ukiokoka na kuacha baba yako anakuwa shetani na sio wa MUNGU wa Mbinguni, Ngoja nikuambie jambo, Shetani anaijua Biblia, na wanaomwabudu YESU au shetani hawata nyoosha mikono yako chini wote watanyoosha Mbinguni na watamwita baba, kwenye ulimwengu wa roho ndipo wa YESU, YESU atapokea maombi yao na wa Shetani, shetani ndiye atakayepokea maombi yao. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Napenda nikufundishe, Je! Umeshawahi kujiuliza kwanini wakati wa maombi tunabomoaga wafalme wa anga? Ni kwa sababu ipo Mbingu ya shetani mahali Fulani huko juu na hata ukisoma biblia, kipindi cha Daniel wakuu wa anga walizuia maombi ya Daniel, lakini hao wakuu wa anga hawana makao huko juu, wao wanajitanda tu. Unaposema sala ya baba yetu uliye Mbinguni wakati hujaokoka na unapoomba Mbingu ya shetani ndio inakusikiliza na unapoendelea kukiri ndipo inakujengea moyo mgumu wa kuukataa wokovu, na kama ulishasema sala hii na ikawa ni ya upande wa mashetani, sema; nakukataa shetani narudi kwako BWANA YESU, BWANA YESU naomba uipokee sala yangu, maana ndiwe BABA yangu na ukishamkiri YESU ukimwita ataonekana, watu wanaweza wakawa wanaomba mapenzi ya MUNGU yatimie hatima yake ni shida na mikosi, BWANA YESU asifiwe, Hata mimi Hebron aliponiambia nikamtumikie, kwa sababu ni mapenzi yake na mapenzi ya MUNGU hayazuiliki ndio maana hata sasa kazi yake inaenda, akisema utazunguka dunia ni mapenzi yake na ni lazima yatimie lakini ya shetani hayawezi kutimia ni lazima yavunjike maana shetani nae anapambana ili kuzuia mapenzi ya MUNGU, tutamchoma shetani moto awe majivu na tutaendelea kuondoa kumbukumbu zake zote; Unaweza ukawa umebanwa na mungu madhabahu, na anapata nafasi pale ambapo ulisali kwenye madhabahu ambayo MUNGU wa Mbinguni hakuwa anaabudiwa na kumbuka unachikikiri ndicho kinachokufunga, hivi baba wa Mbinguni anaruhusu sanamu? Baba yangu wa Mbinguni ana nguvu na uweza, na endapo ukiona mtu mwogamwoga ujue kuwa baba yao ni shetani na wanaogopa moto, na anafuatwa na zile roho zake na jina la kila ambaye hajaokoka limeandikwa kwa shetani ambaye ni baba wa uongo, sasa amua wewe mwenyewe ni mapenzi yako kumpenda MUNGU au shetani. Kila kiumbe kinatakiwa kimpende MUNGU maana ni mapenzi yake, BWANA YESU asifiwe lakini shetani pia nataka apendwe, mwambie shetani sikupendi, Unampendaje shetani? Kwani shetani amekuumba? Kwani unafanana naye? Unamkia una vichwa 20 una mkono Kama kontena? Sasa kwanini unampenda yeye, sadaka zako umetoa kwa shetani halafu unamwambia BABA wa Mbinguni naomba mafungu yangu ya kumi yanene kumbe yameenda kwa baba wa uongo. Mapenzi ya MUNGU watu waombewe bure, utakuta mtumishi anawaita wenye mahitaji anawaambia njoo mbele na anawauliza mna sh.nganpi? na anakutajia na kiasi, sala za toba na maombi ambayo mnaomba yote ni ya shetani acha nikuambia ukweli upone, usije ukalia siku ya mwisho pale utakapoona wenzako wanaondoka, napenda nikufundishe jambo, Elia Baba yake alikuwa wa Mbinguni na baali baba yake alikuwa ni wa kuzimu, kwa Elia MUNGU alioneka na hata wakati wa kuondoka MUNGU alimpaisha na akapaa,BABA yetu wa Mbinguni anakupenda na anamipango mizuri ambayo alipanga juu yako, ila shetani ana mapenzi mabaya juu yako na anakutakia mabaya tu, ila ukikaa na BWANA YESU mabaya na mapenzi ya shetani hayatakupata, na hayo mabaya yatarudi kwa adui, mwanadamu ambaye anakuendea kwa mganga huyo anakutakia mabaya, nayekuloga yatamrudia yeye, maana hizi ahadi ambazo wanasema atashindana nawe lakini hawatakuweza ni za BABA wa Mbinguni na sio za shetani, sio baba wa mapepo, majini au mapokea ya wanadamu na jambo lingine, kuna watu wanaomba kwa mapenzi yao na sio kwa mapenzi ya MUNGU Mtu analazimisha kuomba kitu Fulani na kitu hicho hakitokei, hiyo ni mbegu chafu, sema chafu, mwanadamu acha nikuambie kila unapoomba MUNGU anamapenzi mema nawe, utakumbuka hata YESU alitamani kuwa asife lakini aliomba mapenzi ya MUNGU yatimie, na sasa YESU ni mfalme wa wafalme. Kuna baadhi ya watu ambao huomba na kufunga na hawapati majibu kwa sababu wametaka mapenzi yao na sio ya MUNGU na ndio maana MUNGU hawajibu kwa sababu MUNGU anataka mapenzi yake sio yako. Acha kumpa MUNGU mipaka hivi unajua kesho ikoje? Shetani ndie anawafunga watu ufahamu ili waombe mapenzi yao, yale ambayo wanayoyataka wao, ila sasa yabidi mapenzi ya MUNGU ndio yatimie katika kila nyanja, ujana, wokovu, utumishi, ndoa, utajiri, maisha, na meningeyo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Ulipokuwa unaomba sala ya Baba yetu kabla ya kuokoka ulikuwa unamwomba shetani na sio MUNGU, shetani alipata nafasi ya kukupumbaza, kukuharibu, kukuibia haki yako, na ndipo alipoendelea kukuibia maana shetani anajua kuwa kila mwanadamu anavitu vyake na anajua kuwa vipo na jinsi ya kuiba, ndiposa yeye anaanza kuiba kwa maana yamkini ulitakiwa kuwa Rais, mbunge au mtu Fulani, shetani akakuibia, yeye huchelewesha mapenzi ya MUNGU kwa maana akiiba anagawia walio upande wake, lakini endapo utamrejea MUNGU, kumbuka kwamba penzi la MUNGU lipo pale pale, Baraka zake zipo pale pale, ila tatizo ni baadhi ya watu wanakuwa wameshashikiliwa sana na roho za shetani, na wao hawataki ziwaachilie hivyo wanabakia na matamanio kama wachawi, mchawi huwa na wivu na kuharibu vya wengine, lakini leo kubali, kumkataa shetani na kumvunja na kumharibu na kufuta sala zote ambazo ulizokuwa umemwomba, tumeomba ili tuweze kuona mapenzi ya MUNGU na sio kuona mikosi, balaa, magonjwa, machafuko na mambo kama hayo. Na Ili uwe mtoto wa MUNGU lazima uokoke na kwenye biblia imeandikwa kuwa tusiwe kama hao wanaopayuka, payuka, na hao ni wale ambao wanamwita MUNGU lakini hawataki mapenzi ya MUNGU hivyo MUNGU hawezi kuwajibu, na ukiona hakuna majibu ujue ni shetani ndiye uliyemwomba ambaye hana majibu. Hivyo mgeukie MUNGU aliye hai ambaye atakulinda, atakuvusha na atakuinua, BWANA YESU asifiwe, Je! Unamtaka baba yako wa Mbinguni? Unapoomba bila majibu unakuwa kama wale ambao waliokuwa wanamwomba baali, hatima yake hakuna majibu, na usifikirie kuwa MUNGU atakudondoshea Pesa hapana, atakupa akili ya kupata Pesa. Watu wengi huomba kwa baba zao, wakiliita jina la YESU au kwa sala ya Baba yetu kimwili lakini katika ulimwengu wa Roho wana baba zao tofauti na BABA wa Mbinguni hivyo wanabakia kulia na kulaalmika na kulaumu kuwa baba hunioni, hunisikii, kwani MUNGU huoni? Husikii? yaani unaomba maombi ya malamiko, Biblia inasema kabla hujaomba nalijua kuwa unataka nini,(MUNGU hujua kuwa ni kitu gani tunahitaji kabla ya sisi kumwomba) Biblia inasema kabla ya hujaomba nalikujibu sasa kwanini hujibiwi? Watu wengi huchanganya MUNGU na shetani, mtu hana msimamo mara anaenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta msaada, mara kwa mizimu, umekuwa wa vuguvugu sasa nani akujibu? MUNGU au shetani? Laiti ungelikuwa unaona, na una macho ya Rohoni na ukafunuliwa jinsi ufalme wa giza unavyofanya kazi ungeliogopa, bora tu usione, na pia inategemea na imani yako na kiwango chako, ila ikifika wakati, MUNGU akipenda atakuonyesha, sasa amua kumfuata MUNGU na mapenzi yake. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Na wahubiri pia, wapo baadhi ambao Baba yao ni MUNGU wa Mbinguni na pia wapo ambao shetani ndio baba yao wa kuzimu, YESU alipingwa na mafarisayo, maana baba wa mafarisayo sio baba wa YESU, mafarisayo walikuwa wa Kuzimu na YESU alikuwa wa Mbinguni na ndio maana alipokuwa anawafundisha walimpinga, mfano farisayo alishazoea kunywa na kulewa madhabahuni na BABA wa Mbinguni anasema msinywe pombe, baba wa Kuzimu anasema Kunywa usiogope, ukiokoka utengwe, ila BABA wa Mbinguni anasema okoka ili ufike mbinguni ili upate haki na mapenzi ya MUNGU, Jitadhmini wewe, kabla ya kuokoka ulikuwa unawachukuliaje au kuwaonaje watu waliokuwa wameokoka? Si ulikuwa unamcheka? Unaona kuwa wamechanganyikiwa? Hata mimi pia ilikuwa hivyo, lakini ni kwa sababu ndani yetu kulikuwa na baba wa uongo ambaye ni shetani akatufundisha na kutulisha ya kwake tukawa wapinzani wa BABA wa Mbuinguni kwa kujua na kutokujua, MUNGU atusamehe, napenda ujue kuwa mara tu ukifanyika kuwa mwana wa MUNGU shetani na wafuasi wake huwa wanakufanyia kikao kuwa utafika wapi? maana ufalme wa shetani ndio wenye kuombea watoto wa MUNGU maombi mabaya lakini usiogope tunanguvu, tunasonga mbele, BABA yako wa Mbinguni anakuhitaji, kwake kuna kila kitu na yeye amekuandalia makao, lakini hao ambao wanafuata sanamu ila wanasema BABA yetu wa Mbinguni hao makao yao ni Jehamu kwa sababu hata baba yao atachomwa na wanayemwita baba utachomwa acha kuomba mapenzi yako yatimie, omba mapenzi ya MUNGU yatimie kila wakati, kuna vitu ambavyo vimechelewa kwa sababu ya sala ambayo hukuwa unamwomba MUNGU pia ameita baba ambaye sio wa Mbinguni, yamkini, uliita miungu, majini, mapokea ya wanadamu baba na ulipowaita vitu vyako vikaharibika au wakaviharibu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Je! Unajua asili ya huyo anayebatiza Kwa kisima au kikombe? Unajua anaenda kinyume na Neno la MUNGU? Hao ndio wameifanya injili kuonekana kitukituko au kama mchezo wa kuigiza ila kama ukikaa na MUNGU wa Mbinguni hutakuwa kituko na kama ulikuwa kituko MUNGU atakubadilisha, BWANA YESU alisema jina hili litatumika sana na hata sasa wanalitumia ndio maana utakuwata hata watoto wanaitumia sala ya Baba yetu uliyembinguni na wanaipenda wakijua wanamwomba MUNGU na hata baadhi yao wanabandika mpaka kwenye ukuta chumbani wanakaririshwa ila yamkini mtoto huyo alibatizwa akiwa mdogo, hivyo sala yake hupokelewa na baba mwingine ndiposa unakuta maisha ya watoto yanaharibiwa na kuibiwa Baraka zao ambazo MUNGU wa Mbinguni aliwapa, maana iweje una alama ya ubatizo ya baba mwingine ambaye sio MUNGU halafu anasali sala hiyo au kumwomba MUNGU ambaye humwabudu halafu akujibu? Ataweza kukujibu wakati una lebel / alama ya mungu mwingine, sio rahisi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mapenzi ya MUNGU mtoto awekwe wakfu yaani abarikiwe na akikuwa mkubwa na kuweza kumkiri MUNGU ndipo abatizwe. Mapenzi ya baba wa uongo mtoto abatizwe akiwa mkubwa abarikiwe, maana ya kubatizwa hata kwenye kamusi ni kuzamishwa, lakini mapokeo ya wanadamu yamebadilisha kweli ya MUNGU, kumwagiwa maji kichwani halafu unasema ni kiimani yako; sasa wewe unaimani gani? Imani ya kubadilisha Neno la MUNGU? Unaakili kweli? Utasema huna dhambi ya kumkufuru MUNGU wakati umegeuza Neno lake, hiyo ni dhambi, YESU atakuja na mawingu na waliomkubali atawachukua na alisema anakuja, na hata sasa ndio maana kuna majangwa kama korona na bado yatakuja mengi ila amesema yule ambaye ni wa kwake utapita katikati yao hayo hayatampata. Mapenzi ya MUNGU yakatimie kwako, majini, magonjwa, mapepo na mengineyo yakatoke kwako, Yaliyowekwa kwa agano la sadaka yakatoke ndani yako, yakatoke kwenye riziki za kila mmoja mapenzi ya shetani yakatoke ndani yako na yabakie ya MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mapenzi ya MUNGU umpende MUNGU, mapenzi ya MUNGU ni upendo, wokovu, ila usiwe mchoyo kwa MUNGU, kuna watu wanampenda YESU na wanakuja kanisani kama vile watu wanaokwenda kwa maganga ili wafanikiwe tu, sio wanakuja kwa sababu ya kumpenda YESU la hasha! Wanapenda vitu ambavyo vinapaikana kwa YESU lakini YESU hawampendi, na utamkuta mtu huyo bado wanateka waume za watu, wanaenda kwa waganga, kutoa watu kwa YESU na kuwapeleka kwa shetani, kumbuka kuwa upo moto unaowaka juu yako acha, MUNGU atakupiga na piga ya MUNGU ni tofauti naweza kupiga kitu kimoja, uliza hata akina Daudi, kuna wakati watoto walikuwa wanakufa tu, anaweza kukupiga hutakubalika tena, hupendwi, hupati pesa wala kibali, unaumwa tu, na mengineyo na hayo huruhusiwa ili umrejee MUNGU, na ni ili MUNGU andelee kutimiza mapenzi yake kwako; unanielewa? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Sio wote wanalogwa au kufungwa? Je! Ukiumwa mahali kwani ni kila mahali unaumwa? Hivyo hutaona fimbo kama fimbo ya MUNGU ila anamruhusu shetani anamwambia piga pale. Tusipende kuishi maisha ya kutandikwa unatandikwa kabisa na wakati mwingine anakuuwa, Kumbuka kipindi cha mfalme Nebukadreza, alikuwa anamkufuru MUNGU na kujifanya kuwa yeye ni MUNGU hatima yake aliuwawa alikufa, Unajua hata wadudu, ndege, Malaika na kila kitu kitu kinamjua kuwa MUNGU ni baba yao, lakini wewe mwanadamu shida ni nini hasa mbona unahirizi, akili yako inafikiria kufanya matambiko ili ufanikiwe, mara hekalu la MUNGU linachanjwanjwa, haijalishi kuwa unaita, Bwana wa Mabwana uinuliwe, Nivute kwako Bwana YESU, kama hauna MUNGU wa kweli atainuliwa bwana shetani! www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Shetani anawapenda watoto wake sana, amua ni yupi unamshikilia. Kukitokea msiba ndipo utaona watu wanashika kitabu cha BABA wa Mbinguni, wanaimba, wanasali, wanafarijiana, ila yamkini mbele kuna sanamu, usifarijiwe na baba wa kuzimu, usitishwe na aina za mavazi ya baadi ya watumishi, yenye nakshi za alama za jumlisha, biblia, kubwa, goldi mikuki, mwana kondoo, na sanamu mbalimbali hizo zisikutishwe maana hata hazikupeleki Mbinguni, linayokupeleka Mbinguni ni neno la MUNGU lililo hai na Injili unayoipokea hapa unapata connection yako na MUNGU moja kwa moja . Kuna baadhi ya watumishi ambao wanaojiita, au wamepata utumishi wao kwa kupitia kwa waganga au wachawi hao ni waongo na Injili wanayoihubiri ni ya uongo, na MUNGU wanayemtaja sio wa Mbinguni, MUNGU hashirikiani meza moja na wachawi wala wakandarasi wa barabara ya Mbinguni waliojiita, yeye MUNGU anajua wale wa kwake. Bwana YESU asifiwe. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mafarisayo walijiona wanafaa lakini hawakuwa na kibali ila mtoza ushuru alikuwa na kibali mbele za MUNGU na hata sasa baadhi wa wahubiri hawana kibali mbele za MUNGU mwenye dhambi ukija kwa MUNGU, MUNGU anakukubali, MUNGU anakuhitaji cheo chako hakikupeleki Mbinguni, wala kwa kugandamizana, ni kwa Neno la MUNGU, iko wapi haki ya MUNGU ya kweli ya Neno la MUNGU la kweli? Je! watu wanavyochajiwa pesa za maombi ni haki? na pesa za maombi Je! ni haki? Na sala ya baba yetu inayotajwa ya haki? Je utajibiwa? Kuna nyimbo yamkini umeimba sana ila ni za huko kwa shetani, kiapo cha kuwa mtoto wa Mbinguni ni ubatizo wa maji mengi, umepotezewa muda wako na ubatizo ambao u kinyume ma ule wa MUNGU, amua ukabatizwe na mtumishi ambaye anajulikana na MUNGU na ni BABA yake ni BABA wa Mbinguni, lakini wengine wanaenda mtoni lakini wanaomba baba wa kuzimu na wengine humwita mwanadamu MUNGU na utasikia wanasali kwa jina la YESU na Biblia inasomwa Je! MUNGU ni mwanadamu? Inastaajabisha, Mwanadamu anajiita MUNGU au YESU, na kanisani watu wanakubali kuongozwa na mhubiri mwanadamu anayejiita MUNGU au YESU, tafakari! na ufikirie Je! MUNGU, Anakula kama wewe? Naumwa? Anaende hospitali? Anakaa duniani kimwili kweli? Nani kawaloga enyi wanadamu? Mwenyezi MUNGU halinganishwi wala hafananishi na chochote. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Lazima muelewe kuwa kipindi hiki ni kipindi cha mavuno shetani anavuna na MUNGU anavuna, ambaye ulishavunwa na MUNGU kaa tulia tumwangalie MUNGU usikubali kuvunwa na shetani na usikubali kurudishwa nyuma, Unatamani MUNGU akupe vitu, atakupaje wakati wewe sio mtoto wake na yamkini wengi wenu mmeomba na kumwita BABA MUNGU, lakini hakuwajibu kwa sababu hakuwa baba yenu nae hakuwajibu, ila kupitia somo hili mmejua sababu za kutokujibiwa, endapo utakubali kumkiri na kuokoka, ukiomba mapenzi ya Baba wa Mbinguni yatatimia kwako, Tokeni kati yao mkatenge nao, injili imekuwa ni vita, baina ya makandarasi (Watumishi) wa MUNGU na wa shetani, MUNGU anakutafuta wewe, Ndio maana mnaomba na kufunga lakini hakuna kitu, badilika BABA yako wa Mbinguni awe baba yako, kataa sanamu, baadhi ya wahubiri ambao sio wa MUNGU husema Hebron anawapoteza, sasa mimi ndio niliwapoteza ua mlipotezwa? Wakasema kipindi hichi cha mwisho watatokea manabii wa uongo kweli wapo, hivyo Hebron anavyohubiri na kuwaambia ukweli Je! Ni nabii wa uongo? au nawafundisha kweli! “Mimi nawafundisha kweli”. Hivyo mimi ninavyowaambia kuwa kama hujaokoka ukisema baba yangu uliye Mbinguni hatakujibu ninakupotosha? Na Kama hujaokoka hutaenda Mbinguni ninakupotosha? Wewe yapime yachunguze, utaendaje Kwa MUNGU wakati ulishamkana na hivyo MUNGU hakujui? Ni sawa na mfano huu. Ukoo wako na A na watu wa ukoo wako wanakujua kuwa ni A na utapata urithi wa upande wa ukoo A , itakuwa vugumu sana ukajitangazia au kutaka haki za ukoo wa B, na hutapata kwa sababu wewe ni wa upande wa A, hivyo basi ndivyo ambavyo pia ufalme wa MUNGU na wa shetani unavyotenda kazi, ukiamua kwa MUNGU utakuwa wa MUNGU na ukiamua kwa shetani utakuwa wa shetani. Baadhi ya ndugu, jamaa, na marafiki wanakuzuia na kukukatisha tamaa katika wokovu ili urudi nyuma usikubali, ujue kuna vikao vya kuzimu na vikao vya watumishi wakipepo, wanasaidiana sana na sio wa watmishi wanaotambuliwa na MUNGU, huwa wanapanga mbinu za kuharibu hii dunia, wanakaa vikao kwa kanda zao, kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, vikao hivyo hukaliwa katika ulimwengu waroho na wengine kimwili, wanapanga mbinu za kuiharibu hii dunia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Unasali sala ya Baba yetu uliye mbinguni, unalogwa, huna hata ada za watoto, mtoto anaenda shule hana hela, mtoto akifika anauza kila kitu kwa sababu hana hela ya matumizi, sasa tafakari! Ahadi kwa BABA yetu wa Mbinguni ipo wapi? Usitutie majaribuni, majaribu ni shida, dhiki, adha, ulevi, ugumba na mambo kama hayo, uongo, magonjwa. Usitutie majaribuni neno hilo linaepusha vita adha, dhiki na mengineyo, anza kuomba toba na Rehema maana shetani ameweka kumbukumbu zako kwenye ulimwengu waroho kuwa ulimwabudu yeye, ukipewa riziki na MUNGU itunze maana watu wengi wanataka kuona kitu kikubwa na kizuri kabisa, yamkini mtu anataka mke au mume na mwingine anataka aliye tajiri elewa kuwa hata ambaye unamwona kuwa ni tajiri, mpaka amefikia kiwango cha kuitwa tajiri alianza na riziki ndogondogo, watu wengi walioanzia chini na ndio matajiri wazuri, iwe kwenye ndoa na kwenye kila kitu, lakini siku hizi kijana au binti humchambua mwenzake mpaka hatari, mpaka ikifika wakati wa kuoa au kuolewa hapati hata wa kumwoa au kuolewa nae, na ukiona umri umepita unajipeleka na kulazimishia kuoa au kuolewa nae. Je! ni mapenzi ya MUNGU eti mwanadamu kuichambua kazi ya MUNGU? Acha mapenzi ya MUNGU yatimie, unatakiwa uwe mtu fulani ndio unatakiwa uwe hivyo na ni mapenzi ya MUNGU, na sio mwenzako amefanikiwa unaanza chuki, ukiwa na chuki wewe ni pepo, mapenzi ya MUNGU ni uishi maisha mema, kung’aa, kuinuliwa, kumtukuza MUNGU, kupata Baraka, mapenzi ya shetani ni uteswe, kulogwalogwa, nuksi, balaa, kilio na mikosi, sema siyataki hao, sema siyataki mapenzi yote ambayo ni kinyume na mapenzi ya MUNGU na uombe mapenzi ya MUNGU wa Mbinguni yatimie kwako. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Muombee mke wako au mume wako, mapenzi ya MUNGU yawe juu yake, lakini hayatimii, ulishawahi kujiuliza kwanini? Jiulize sasa! Je! Yatatimiaje kama unamwita mume wako baba au mke wako mama? wamekuzaa wewe? Je! mtu anaoa mama au anaolewa na baba yake? Ndio jambo hili limesababisha ndoa nyingi hazieleweki au mke anakuwa yupo yupo hajielewi wala haelewi nafasi yake na mume yupo yupo nae hivyo hivyo haielewe nafasi yake, utatafuta mchawi hutamwona, maneno yako ndio yamekufunga, na hata wengine mke wake au mume wake akitaka kumtembelea kazini utasikia usije, usije, sasa unamwonea mwenzako aibu basi ninyi sio ubavu mmoja tena, wengine huita mke bibi au mume babu, ndio maana maisha ya baadhi ya wanandoa ni wadogo kiumri lakini kimatendo ni kama babu na bibi, mmezeeshwa na ndio maana mnakufa haraka, mke ni mke na mume ni mume. MUNGU alisema mume au mke. Mungu anaangalia ulichotamka, mke au mume au kwa mchumba mwite vile ambavyo MUNGU ameongoza kupitia Neno lake, ili MUNGU atimize mapenzi yake kwako, watu wengi huogopa kusema mke wangu na wanawake wanaona vigumu kusema mme wangu. Hebu sema kwa kinywa chako. Wanaume wengine ni wabahili kwa sababu tu ya jina ambalo unamwita, udhaifu huo shetani huuchukulia faida ya kukugandamiza, mfano: unamwita mume baby kimwili utaona sawa lakini kiroho anamtengeneza kuwa baby (mtoto) nae katika uhalisia hupunguza majukumu kama mume na huanza kufanya mambo ambayo hayaeleweki eleweki, anapunguza hata majukumu ya wanandoa, hebu muite wako “mume wangu, mbele za watu halafu ufike nyumbani uombe hela ya matumizi, utapewa tu” kwa sababu kwa kutaja Neno mke au mme wangu ni kiboko cha kumpiga na kumpinga shetani, kwa sababu umempa mtu nafasi yake sahihi, unapomwita baby au honey kwenye ulimwengu waroho unamshusha hadhi, na wachumba hawaitani hivyo, mtu hamwiti mchumba wangu, humwita demu wangu, chali wangu, best, sweetie, sasa kwanini umwite hivyo na kwa nini asikuite mchumba wangu? Zamani wazazi wetu walikuwa wanapendana kiukweli na kuheshimia na kwa sababu hakukuwa na mizaha hiyo, ni bora umwite mume wako baba watoto na mke wako mama watoto, pia mkiwa wachumba, mchumba wako akikuita mchumba wangu unajiasikia vizuri. Kuweni waaminifu na kuchukuliana baadhi ya watu huwa wanapenda pesa hasa wachumba na wanaume wengi wao huwa wanajitahidi na kutoa pesa mpaka kukopa mpaka ile ya mwisho hata kama hana, ila sasa wanaume nanyi jifunzeni kuwa huru, wakati unayo unayo kweli na wakati huna ni huna kweli ili mwenzako ajue hali halisi. Upendo wa MUNGU, upendo wa kweli hauangalii kitu wala mali, jinsi mhusika alivyo ndio upendo halisi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Sala ya baba yetu itimie kwako, na sio ya mashetani, Riziki ni kuwa na maisha mazuri, kuwa na akili, na ufahamu, kuwa na nguvu za MUNGU, Uzima na kama huna uzima utadondoka chini, jielewe kuwa wewe ni nani? unakwenda wapi na unatakiwa kuwa nani, Bwana Yesu asifiwe, Kuweni na moyo wa Kunyeyekea kwa MUNGU na omba mapenzi yake yatimie. Pasipo Mapenzi ya MUNGU unaweza kung’ang’ania kitu kikaweza kukutesa, elimu, kazi, au riziki, endapo haina mapenzi ya MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mimi Hebron MUNGU alinipangia niwe daktari bingwa,mimi nikakataa kabisa na nilibishana na baba yangu sana kuwa mimi siwezi na wala sitaki kuwa daktari, nakumbe nilipoikataa kimwili kwenye ulimwengu waroho walishaiiba, wakaidaka, shetani akawapa wengineo, wakachukuaga kipawa hicho na mimi nikabakia nagombana na baba yangu maana yeye anataka, niende kusoma udaktari lakini mimi sikuwa nataka nikawa sielewani nae, na kumbe maadui walikuwa wameshanigeuzia wakaiba mapenzi ya MUNGU na kuniachia mapenzi yao. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mapenzi ya MUNGU yatakwenda kurejea na wakati huu katika ulimwengu wa Roho naona Mbingu zikiwa wazi na watu wakiwa wanapita katika njia nyembamba ya kwenda Mbinguni, Mbinguni unakwenda kwanza katika Roho kuna watu mmewapa hela wakaenda kuwafunga kupitia fedha zenu, nami ninaomba na mtafunguliwa kila eneo kwa jina la YESU. Kuna mikono ina shida tu imebadilishwa, itarejeshwa, usipende riziki ya mwenzio penda ya kwako, hebu anza kujikubali kuwa wewe ni wa thamani, kuwa u wathamani mbele za MUNGU na vyote ulivyonavyo ni vya MUNGU Je! Kuna jambo la kumshinda MUNGU? Hakuna! www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Sema Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, naomba unisamehe na unifutie mashtaka yote pale ambapo nilimwona huyu baba wa uongo kuwa ndio baba yangu, ninamkataa kiroho na kimwili katika jina la YESU na kwa damu ya YESU, BABA yangu yale yote ambayo niliomba nikiwa upande wake, halafu shetani akaniachia mabaya na kuharibikiwa naomba unitakase, ninaomba unisafishe mimi ni mtoto wako, Kumbuka mwana mpotevu alivyorejea, ulimpokea na kumsafisha na katika wale kondoo mia, yule mmoja ambaye alipotea ndio mimi nimerejea, nina kiu ninatamani MUNGU uwe baba yangu, ninakukiri katika jina la YESU sasa na hata milele, najitenga na sala zote za baba wa uongo kwa majina na level yake na namkataa, BWANA YESU ninakuomba unipokee na kunibariki na mapenzi wa MUNGU yarejee kwangu, jina langu likae kwako BABA MUNGU na najiweka mikononi mwako na sala hii ambayo ni agizo aliloliagiza kupitia YESU ambaye ni mwana wa MUNGU wa pekee, nami naikubali, naikubali, najitenga na sala mbalimbali za wapinga kristo na waliojiita ambapo nilipita nikaunganishwa huko na madhabahu zao sizitaki tena, nimetoka huko na nimejua sasa kwa BABA yangu kuna kila kitu na nimerejea sasa. Katika jina la baba, mwana na la Robo Mtakatifu. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Imeandikwa na Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo.