Pages

Thursday, June 17, 2021

  JINSI YA KUFANYA ILI MAPEPO YASIKUVAMIE - LUKA 8: 27–37

Baba nakushukuru, Nakubariki na kukuinua MUNGU wa Ibrahim, Isaack, na Yakobo, MUNGU uliyeniumba, uiliyeumba viumbe vyote, nakushukuru Nakubariki, naendelea kualika uwepo wako na Neema yako, upendo wako ukatamalaki, kusudi lako likaendelee kutimia na ukafanye upendavyo kwa watoto wako na ukamhudumie kila mmoja kwa utukufu wako, asiwepo ambaye hatapokea, tazama mioyo yao, tazama njia zao, tazama BWANA,  nakushukuru kwa ajili ya Roho Mtakatifi wako, kwa Jina lako, na kwa damu ya YESU kwa maana kama  sio YESU sijui ingelikuwaje, lakini MUNGU unatuwazia Mema na mazuri Nakushukuru BABA, Nakushukuru kwa Neno lako.  Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Neno la MUNGU ni takatifu latoka  Mbinguni twakushika siku zote,  Lakini napenda ujue kuwa liko Neno ambalo halijatoka Mbinguni na Neno hilo sio Takatifu na hata ukilishika  halitakusaidia chochote, Wengi wanataka Neno toka kwa MUNGU na wengi pia tulishapokea Neno ambalo halitoki kwa MUNGU, hata mimi nilikuwa  mmojawapo (Nilipokea kabla sijamjua MUNGU wa kweli) Na Neno ambalo halitoki kwa MUNGU sio Takatifu, Nilipokuwa najianda kuja kanisani leo,  Niliongea na MUNGU akawa ananiambia Hebron, unajua kazi yako ni kuwaleta watu Mbinguni akaniambia mwaka 1800, 1700, 1400, wale wanadamu ambao walikuwa wakiishi miaka ile Je! Kuna hata mmoja ambaye yupo hai leo? Akaniuliza! Na mimi nakuuliza Je! Waliokuwa wanaishi miaka hiyoi wapo? Je! Kama hawapo wamekwenda wapi? Miaka ya 1800, 1700 1400, wako wapi?  Waliokuwepo 1400 wako wapi? Na hata kizazi hiki kitapita, yako maisha yajayo walioyashika kama Hebron ninavyokuongoza hivi leo wamefika, hata mimi Hebron nimemsikiliza MUNGU name nimefika nilipo na wewe mwana wa MUNGU jiangalie na ujichunguze, ipo siku utaondoka unakwenda wapi? Akaniambia wapo wenye mali nyingi na waliziacha hapahapa  na sasa hivi watu wanang’ang’ana na mali na wataziacha hapa hapa, sasa badala ya watu kung’ang’ana na wokovu ambao utakupeleka  Mbinguni wao wanang’ang’ana na mali  na kumsahau MUNGU wakati mali hizo .zitabakia hapa hapa, lakini Mbinguni tuendako ziko mali nyingi Zaidi na za thamani  kuliko za duania hii. Napenda nikuambie kuwa kila kitu utakiacha hapa lakini YESU uliyemshika utaondoka nae, Lakini pia unatakiwa uwe na vitu hapa basi Moyo wako usipende vitu sana kuliko YESU maana yeye ndiye anayekupa, Selemani alikuwa na Vitu vingi sana lakini alimpenda MUNGU kuliko vitu na Daudi alikuwa na mali nyingi lakini alimpenda MUNGU sana, na wengineo wengi na hata Suleimani alipokufa hakuondoka na kitu sasa tafakari, Je! Itakufaa!  Napenda nikuulize kuwa Je! wale ambao walikuwepo vizazi vilivyotangulia wako wapi? Je! Kumbukumbu zao zipo?   Wapo walioenda kwa shetani na wapo walioenda kwa MUNGU na hata sisi tupo ambao tutaenda kwa MUNGU na wapo ambao wataenda kwa shetani. Ninakukumbusha watu kwasababu wanadamu wamejisahau watu wamejisahau, lakini tunamshukuru MUNGU kwa jambo hili. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Umekuwa au umewahi kujiuliza! Ufanyaje ili mapepo yasikuvamie na ufanyaje ili wachawi wasikuvamie, wakukimbie, ufanyaje  ili nguvu zao zisikuweze na ufanyaje ili giza  litoke mbele yako, ufanyaje ili mapepo yasikufunge? Maana watu wengi mapepo yako ndani yao na pepo sio lazima lilie au lipige kelele au aongee nitakwenda kukufundishawww.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Luka 8: 27–37 – Nae aliposhuka  Pwani, alikutana ma tu mmoja wa mji ule, mwenye Pepo, hakuvaa nguo siku nyingi,  wala hakukaa nyimbani, ila makaburini. Alipomwona YESU alipiga kelee, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, nina nini nawe, YESU, mwana wa MUNGU aliye juu? Nakusihi usinitese. Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa nae mara nyingi, na hata aliindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. YESU akamuuliza, jina lako nani? Akasema jina langu ni Jeshi; kwa kusababu pepo wengi wamemwingia.  Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; basi wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale, akawapa ruhusa. Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi liliteremka toka gengeni Kwa kasi, wakaingia ziwani wakafa maji, wachungaji walipoona yaliyotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka kwenda kuliona lililotokea, wakamwendea YESU, wakamwona mtu Yule aliyetokwa na Pepo ameketi miguu kwa YESU, amevaa nguo, ana akili zake; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza jinsi alivyoponywa yule ambaye amepagawa na Pepo. Na jamii ya watu Wagerasi iliyo kando kando walimuomba aondoke kwao; kwa kuwa walishikwa na hofu nyingi; wakapanda chomboni, wakarudi.

 

Haleluya!  Nataka ujifunze kuhusu pepo, Nataka umwelewe pepo, nataka ujifunze kuhusu pepo, nataka ujue kuwa ni kitu kibaya sana, Pepo anatoka wapi Pepo ni roho au nguvu ya  ya kumwongoza mtu kwenda kwenye mabaya,  au dhambi Pepo yuko kwa ajili ya kushuhudia mabaya kwenye maisha yako, Pepo  ni mtenda kazi wa Ibilisi aliye tumwa na shetani kuja kuwatesa wanadamu na viumbe vingine na kazi yake ni  kusimamia  wanadamu ili wapate taabu na mateso, kwa nini MUNGU kupitiia  mwanaye akasema Msiondoke hapa wanafunzi wangu mpaka niwatumie Roho Mtakatifu,  pepo na roho Mtakatifu wana kazi tofauti,  Roho Mtakatifu anatoka Mbinguni na Pepo ni roho Mchafu wa shetani, Na anawafuata wale wanaomkubali na wale ambao wanamkumbatia, wapo kwa majina yao, Pepo sio mpaka apige kelele au kugaragara na  ni aina ya  malaika wa shetani ambaye kazi yake ni kutenda mabaya kwa wanadamu, alipokuja YESU alikuwa na  na Roho natakatifu na alipokutana na huyo mgerasi,  mapepo yalilia msitutoe kwa hiyo mapepo yanajua kuwa kiboko chao ni Roho Mtakatifu,  sasa inashangaza sana unaweza ukasema una Roho Mtakatifu lakini kumbe una pepo, umeokoka lakini una Pepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Pepo linaingia kwa mtu likipata njia, yako aina nyingi za mapepo na kila pepo lina jina lake na ndio maana YESU aliwauliza kuwa nyie ni mapepo gani? Wakasema kuwa ni Jeshi na mimi nakuuliza je! Ndani yako yuko nani? huwezi ukawa na roho Mtakatifu halafu ukaenda kwa mganga, au kwenye dhami, Pepo litakuongoza kwenda huko, Pepo ndio litakuongoza kwenda  kuabudu mizumu, halafu mtu huyo atakuja kanisani na kusema haleluya! Haleluya!, Mtu huyo ni mwongo, anapepo, sio uone mpaka  pepo linabiringita, kuna mapepo ambayo yapo ndani ya watu yanafanya maisha ya mtu  yawe mabaya lakini mhusika anaweza asijue, inawezekana ni pepo la kutengenezwa,  Pepo la kutupiwa linaagizwa likushughulikie wewe, pepo ni nguvu mbaya ya kuharibu,  yawezekana ni Pepo la ugonjwa, uzinzi, wizi,   na mengineyo. Pepo hukua kwa viwango na jinsi ambavyo unayakumbatia  ndivyo yanavyoongezeka kama ulikuwa na Pepo la udokozi  ukaendelea na tabia hiyo baadae unakuwa jambazi,  na jangili. ili Mwanadamu atende mabaya lazima anapepo, na pepo linazunguka zunguka  kutafuta njia na yapo hata  mapepo ya makanisa  na yanatoka kuzimu yapo yanayosambaa  angani kuchafua hali ya hewa, lipo pepo likwamishalo maisha yako ila ukiwa na Roho Mtakatifu na Malaika wa MUNGU wakikutangulia Mbele utapita katikati yao ila watu wengi husema napita katikati yao wengi hawapiti kwa sababu wana pepo la hasira , Uongo, Roho Mbaya na mengineyo, www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Achene MUNGU awachunguze ili awajenge unapepo la uchoyo, una pepo mpaka kwenye jicho, jicho la kiburi, Pepo la kiburi mpaka kwenye Macho, Pepo la fitina, ulafi, chuki, kutakia wengine mabaya hilo ni pepo, utakuta  mtu ananena kwa Roho  wakati ni mwongo, huyo ana Roho Mtakatifu au Pepo? na kinachonena ndani yake ni Pepo au Roho Mtakatifu? Tafakari!  Na ujichunguze na wewe pia ndani yako yuko Roho Mtakatifu au Pepo. Pepo hapendi hata uvae vizuri,  Pepo akawa amekaa  hapa duniani na hata kipindi kile kwenye Bustani ya Eden, Shetani akamwaga Roho zake , Hata kaini nae Pepo lilimfuata na kaini alikuwa na wivu, wivu, Pepo likaingia likajikuza mpaka  akamuua ndugu yake. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Pepo linaangalia tabia ya mtu ilivyo ndivyo liingie,kuna watu wanatabia za kipepo  angalia Yuda alikuwa na tabia ya kupenda Pesa na Tamaa, Yuda kama Yuda alikuwa hapendi kumsaliti au kumuua YESU  lakini iliandikwa na kwa sababu  MUNGU alijua huyu anatabia hizo ndipo pepo likapata mlango na njia.  Pepo alipomvaa Yuda akamsaliti YESU na baada ya kumsaliti YESU, pepo lilipomaliza kazi yake, Pepo aliondoka na Yuda akatafakari kuwa sasa nimefanya nini hapa? ndipo alichukua maamuzi ya kujinyonga, Pepo la  kusaliti lilipoondoka, akamwachia Pepo wa majuto na hatimaye alijiiua, wangapi wananung’unika? Kama una manung’uniko nataka ujue kuwa una pepo,  unaweza ukakaribisha pepo kwenye familia yako  wewe ni  manung’unika tu,  Baraka zinaondoka  na yamkini upo kwenye biashara zako na umempokea YESU ila wewe ni kunung’unika tu, mbona MUNGU haleti wateja?  Wakati umeambiwa ushukuru katika kila jambo, jiamini. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Ibrahimu alivyoambiwa toka, nenda katika nchi ya ahadi yeye alisonga mbele, lakini ndugu zake walikuwa na mapepo ya kumzuia, lakini yeye alimsikiliza MUNGU na MUNGU hapendezwi na wenye roho ya kusitasita maana hatima yake ni kuporomoka, wanabakia hivyo, hivyo, mie nataka unyanyuke usonge mbele,  wanafunzi  wa YESU walizajwa roho Mtakatifu kwa sababu  YESU alijua kuwa bila Roho Mtakatifu,  Pepo atawapoteza. Jiulize! Kwanini mtu anapoa katika wokovu, hawezi kuomba au kufunga kwa sababu Pepo linakuwa limemvaa na sio mpaka uone Pepo anapiga kelele. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Amua kukataa nguvu za mapepo zinazokaa kwenye maisha yako, kukaa kwenye kazi, ziko za kutupiwa, mtu anayekuendea kwa mganga huwa anakutupia pepo ili ushindwe kufanya jambo, na litakupata endapo huna MUNGU lakini Roho Mtakatifu akiwa ndani yako Pepo Linaungua, na hata wakikukutumia Pepo ili ufe, utashanga wewe ndio unanona, usijenge ndio unajenga, usipate mtoto ndio unapata, pepo la uchumi, mtu anakuambia uchumi mgumu Je!  Kwa MUNGU kuna jambo linashindikana? Magumu yanawapata watu kutokana na kutokujua jinsi ya kukaa na Roho Mtakatifu na MUNGU pia, Watu wengi wana Roho Mtakatifu wa mazoea, wana roho Mtakatifu wa jina nakuambia ukweli, kwanini unaomba kitu halafu hukipati? au hakikufikii? wakati uko na Roho Mtakatifu? kumbuka mabaali walikuwa  wanaomba tena wanataja na Roho Mtakatifu kumbe wao walikuwa na mapepo na Elia yeye alikuwa na Roho Mtakatifu na akaomba na akajibiwa, MUNGU alimsikia Elia na Kumjibu, ilifika wakati Elia alifunga mvua,  ikafika wakati akaifungua, wenye pepo waliangamia, kuna Pepo wa dini na wa ukoo wenu pia. Na ndio maana wanakuita ukafanye matambiko na mambo ya ajabuajabu, basi kataa. Na ili ujue aina ya pepo ulilonalo, ni hivii,  tatizo ulilonalo ndio pepo, kukosa kazi, mwingine akipata hela haikai ana pepo chuma ulete, kuchukiwa tu na mengineyo ila  pia ukiwa na Roho Mtakatifu, mapepo hayatakupenda ila utapita katikati yao. Ukiwa na pepo utakuwa msindikizaji, utasoma mwanzo mpaka ufunuo lakini pepo halisikii maana pia mashetani wanajua kitabu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Tumesema Neno la MUNGU kuwa ni takatifu kwa sababu halina pepo na haitawezekana Neno ambalo lina pepo liende Mbinguni, Neno takatifu tu,  hakuna ushirika kati ya MUNGU na shetani, tunajua ubatizo ni mmoja mtakatifu toka Mbinguni, Je! Inawezekanikaje kuwa Roho Mtakatatifu abatize tofauti na MUNGU? huyo ni Pepo  huwezi kumchezea MUNGU hata mimi nilipokuwa mdogo nilishawekewa hilo pepo la ubatizo wa kikombe,  nasema peupe hilo ni pepo,  ila nilishapata Neema nikabatizwa kama YESU likanitoka,  Unasema unaenda Mbinguni, Je! Utaenda Mbinguni na pepo, YESU anaruddi kuna Pepo sadaka mtumishi anakuambia lete sadaka hapa, toa mpaka ikuume sio sadaka takatifu hizi hao ni wanafanya biashara, wanaocharge watu pesa za maombezi wote hao wana mapepo, Sema Amen. Hata kwenye Luninga utakuta kipindi cha mtumishi cha kanisa Fulani kinarushwa, mhubiri anahubiri, halafu anakuambia namba zinapita kwenye screen  toa sadaka kusapoti huduma ili ubarikiwe, na ufunguliwe, sadaka ni hiari ya mtumishi akikulazimisha ujue ni pepo na anamapepo huyo, YESU amenituma nikuambia na nitasema ninavyojua tumharibu shetani, lazima tumharibu pepo,  Pepo atoke kwenye maisha yako, pepo wa kukwamisha maisha yako atoke, yuko mtu mwenye pepo wa roho mbaya, roho mabaya tu, mtu anaroho mbaya sana, kumbuka  Roho Mtakatifu ni wa upendo, pepo huwa anazuia Baraka zako na Roho Mtakatifu hawezi kukuletea Baraka wakati una pepo, Pepo hakupendi anataka akumalize, na shetani akipumua tu anaacha roho mbaya. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Je! Unajua kwa nini watu wanajiua au kuuana pepo ndio husababisha, uongo ni pepo, Pepo la kuongea uongo kwenye simu, uko sehemu Arusha unasema uko Dar es salaam hilo ni pepo Biblia inasema usiwape watu vilevi angalia sasa, watu wangapi wanawapa wenzao vilevi, wengi wanakunywa kila mlevi anapepo ni ukweli haupingiki, Pepo haliwezi kubarikiwa, katika baadhi ya nyumba za Ibada wanabariki pombe, Je! Pepo linaweza kubarikiwa? Spirity! Roho ya shetani kweli unaweza bariki pombe kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu? Nani aliyetuloga? Unaweza ukaambiwa Nenda na amani ya Bwana lakini msingi wake ni mapepo, unawezaa ukawa na magonjwa tu hayaishi, ni pepo hao,  wachawi wakikushindwa watakuambia wewe u mchawi Zaidi, kwa sababu wamekushindwa, waambie una Roho Mtakatifu, na unayaweza yote katika yeye akutiaye nguvu.  Yapo mapepo ya kukukwamisha, kuna pepo la uoga hofu mashaka, kushindwa na unatembea nalo, kwanini unaomba kitu hupati? Bali wenzako wakiomba wanapata?  Wewe unakuwa umetanguliwa na pepo, na pepo likikutangulia watakuwekea kutatangatanga, kulialia, kukata tamaa na aliyekuwekea anaweza akawa amekutamkia pia kuwa utarudi kwa magoti, yaani kuomba msaada kwako ila sasa umeshatoka huko usirudie matapishi, waambie sasa ninaye YESU silii tena, sitangitangi wala sitarudi kwa magoti. Hata mimi maadui waliniambia kuwa sitaweza kuifanya kazi ya MUNGU, sitafika, Nitakufa lakini sasa napita katikatai yao, tena katika jambo ambalo wanataka  nisipite ndio napita katikati yao, kwa wepesi. Pia kuna pepo mkosi, huwewzi kuabudu mbao ukasema kwa jina  la YESU lazima una mapepo, Neno limesema usiabudu sanamu, wewe unaabudu una pepo, leo watu  wanakufa wanaangamia kwa pepo korona na mwanadamu mpaka atandikwe ndipo anamrudia MUNGU, Pepo ndio anakupeleka kwa waganga na unachanjwa na unavumilia,   kila uliyekubali  kuchanjwa una pepo, wengine huchinjiwa kuku kichwani, wanapanda paka, Pepo hilo usiku utasikia nyaunyau, Paka ni kiumbe cha MUNGU lakini kiumbe huyu wanadamu wanamtumia vibaya. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Pepo wakasema tupeleke kwa nguruwe na nguruwe wenyewe walikataa mapepo,   wakafa kwenye maji, wewe ni hekalu la MUNGU la Roho Mtakatifu Je! Yuko pepo katika fahamu zako? Mbona unawaza mabaya, Unawaza mipango mibaya? Kwanini?  Waza mema na uwaze ya Mbinguni, amua sasa utaona Roho Mtakatifu akikuvusha, akikubariki mpaka utashangaa. Kuna pepo anaitwa subira anakufanya usiwe na subira na ndio maana watu wanaingia kwenye tamaa, mpaka wanaua wazazi wao na wanatoa kafara na sababu kubwa ni huyo pepo akishakuingia aisee anakupeleka kule harakaharaka unawekewa na pepo wengine na huyo pepo akishajaa ndani yako hofu ya MUNGU inaondoka, yawezekana ni Askofu, Nabii, muimba kwaya, mchungaji na utakuwa unahubiri lakini bado unakuwa unatenda mambo mabaya, na mimi nakuuliza hofu ya MUNGU iko wapi? Huna!  Lakini una hofu ya ujasiri wa pepo ndio umejaa ndani yako na tena hata kumpinga MUNGU, angaliwa wana wa Israel wale ambao walikuwa na Roho Mtakatifu walimsikiliza Musa wakapona, lakini wale ambao hawakuna na Roho Mtakatifu walikuwa na pepo, pepo likawaua, wakati huo walikuwa wanakufa kimwili lakini sasa ni kiroho. Pepo mpaka kwenye miguu, kiuno, kifua, mifupa kila mahali unaumwa hospital hupati dawa jiulize Je! Pepo linasikia dawa?  Lakini Mkubali YESU leo apitishe operation, yupo pepo biashara, kazi, madini, kwakazi na mapepo kwa ania zake, au unapewa kitu na mganga hata hirizi ndani ni mapepo,  nakuna watu wengi mapepo yamewekwa kwao na kuna wengine wametoka kwa wababa wa kiroho sehemu mbalimbali wamewekewa Pepo liwatese, liwalinde lakini ukimkubali YESU ninakwenda kutengua katika jina la YESU Kristo wa Nazaret, Pepo la kufanya watoto wako wasikusikilize, Pepo la mabishano, Pepo la kula miaka, kufanya usiishe miaka mingi, la kuzuia magari Pepo la kuzuia mambo mazuri likaondoke na kuna watu wana mifugo  lakini  hawana  wala hawapati faida kwa sababu ya Mapepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Biblia inasema usimwibie MUNGU fungu la kumi na mapepo yanaangalia hapohapo na kwa njia hii unaweza ukawa umtoa fungu la kumi lakini ukawa unatoa kwa mapepo, Unashangaa! Sio makanisa yote ni ya MUNGU mengine ni ya mapepo, ikiwa mtumishi amejiita, amejiamkia, akajiamulia kwenda kufanya kazi ya MUNGU na hakuitwa na MUNGU, ana pepo au  kama aliitwa na MUNGU halafu akamwasi MUNGU hapo ndipo mapepo yanajaa ndani yake, anakuwa kitukokituko, ndio maana baadhi ya Makanisa wanakopa Benk, wanalipa riba wakati MUNGU alishakataza,  wanafanya harambee, minada, kunadi Baraka za watoto wa MUNGU, wanamatabaka kanisani na mambo kama hayo, hizo zote ni pepo ndio anayewaongoza. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Roho Mtajkatifu ni Nuru lakini pepo ni giza, utasikia shindwa pepo lakini wewe mwenyewe una pepo, pepo hawezi kumtoa pepo mwenzake,  angalia ulimi wako umejaa uongo, Roho ya hila ndani yako, ndio maana wengi hujichokea tu, uchovu tu,  kuna pepo wa uchovu pia,  pepo kisura anachosha sura hata upake  mafuta ngozi haisikii, kuna tabia za pepo, mama anaweza kuwa nazo, mkwe anaweza kuwa nazo, baba, shangazi, mtumishi anaweza kuwa nazo sasa hawa wakiwa na tabia za pepo kinachozaliwa nacho kinakuwa ni pepo, Kataa hizo tabia za pepo au pia unaweza ukatumiwa pepo akulinde, atembee na wewe,  sasa amua acha hizo tabia. Biblia inasema pepo akitoka, hutoka huko na huku akitafutafuta nafasi tena, sasa nakuuliza kwako ipo nafasi ya Pepo utasema hapana Je! Tabia yako haina pepo? Kukata tamaa, ubabe, nitakukomesha,  kurusha mipaka, mrushi, ukichukua pesa za watu hurudishi unanyamaza tu mbegu ya pepo,  itaendela kufunga maisha yako,   unaweza kujiuliza ni wapi nilipokukosea BWANA YESU kumbe msingi wako una Pepo ndio maana unakwamakwama, kuna pepo la kidomodomo , mdomo kutoa matusi vilevile  kama ilivyo  kuna pepo bubu, kiziwi, kipofu na mengine ni roho  na pia unaweza kupenda tu wake au waume za watu hilo ni pepo,  kufanya kazi na usipate mafanikio, unapokosa Baraka au mafanikio  ya kazi ya mikono yako ujue lipo pepo na unapoongeza manunguniko hatima yake hufanikiwi kabisa, maana unazidi kuongeza mapepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Nina Neema MUNGU amenipa ya kuona kiroho, wakati mwingine naona watu wanamwomba MUNGU, wanamnung’unikia MUNGU wanapiga mpaka ngumi au chini kwa hasira wanamalazimisha MUNGU, wanataka MUNGU awajibu, wanasema! MUNGU kwanini hunijibu? Kwanini! Sasa badala ya kuomba kwa unyenyekeevu unaomba kwa hasira, hebu nenda Ikulu Je! Unaweza mlazimisha Raisi akufungulie kwa lazima? Hapana! Na yamkini ukaishia kufukuzwa na maaskari, unapoomba omba, nenda kwa adabu na unyenyekevu mbele za MUNGU na MUNGU atakusikiliza na kukujibu sawasawa na mapenzi yake MUNGU.  Lakini pepo likikulinda utaanza kama ngonjera, MUNGU nakuja mbele zako, lakini una mawazo mabaya, ukiwa na pepo maombi yako ni bure. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 YESU ana roho nzuri Jiangalie na wewe Je! Unawapenda watu, unawasaidia, Je! Una Roho Mtakatifu, kwanini huokoki na mtu atakuambia   nimebatizwa kwa Roho Mtakatifu lakini umebatizwa kwa kikombe maji ya kudondoshewa, huo ni ubatizo batili. Sasa basi  ukitaka Pepo ang’olewe kwako kwanza mkiri BWANA YESU ndipo Roho Mtakatifu  akuingia na kukutawala lakini sasa wewe hutaki kuokoka na unapoomba unasema nakula chakula kwa  jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kama hujaokoka utakula kwa jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu wa kipepo, utakuwa unapoteza mda wako BWANA YESU asifiwe,  utalala kanisani kumbe unapigia makofi mapepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Kanisa letu hatuchangishi kwa sababu mimi sina Pepo,  Yuko Roho Mtakatifu na Malaika wake wanatangulia katika kazi ya MUNGU na biblia inasema MUNGU amtuma  Roho Mtakatifu ili akashuhudie Neno lake, Yawezekana wewe ni Mkristo lakini  Roho Mtakatifu hayupo wa kushuhudia kazi ya MUNGU, Neno lake kama ilivyo Kweli watu wanaombewa  kwa Pesa na kwa kipindi hiki kuna baadhi yaMakanisa ya shida eti yako na Roho Mtakatifu lakini Kanisa, kama kanisa linakopa hela Benki, sasa huyo Roho Mtakatifu ameishiwa ama?  Na wewe muumini unasumbuliwa mpaka nyumbali kulipa deni ambalo kanisa limekopa Benk? Usilipe madeni kama hayo, kama unataka kwenda Mbinguni huyo sio Roho Mtakatifu, wala usimkumbushe MUNGU kuhusu hilo maana MUNGU wetu sio wa michango na madeni, wengine wanajiuliza huyu Nabii Hebron anawakataza watu wasimjengee MUNGU,  Mimi sijawakataza  ila kama kanisa limekopa Benk Je! Hiyo ni fomula ya MUNGU au miungu? Mimi ninasema usiijengee Miungu hata kama inakuja kwa mwavuli wa kanisa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Tunasababu ya kupiga Mapepo, kumkanyaga shetani kwa sababu tunaye MUNGU na tunahubiri injili wa kweli kwa sababu tunaye Jeshi la MUNGU, simama na MUNGU,  usiyumbishwe maana huna pepo ila ukiwa na Pepo unatikiswa, ukiwa na Roho Mtatakatifu hautikiswi, YESU alitikiswa mpaka mwisho,  lakini alishinda kwa sababu Roho wa BWANA MUNGU alikuwa amejaa ndani yake na hakumwacha baba Yake, Mpaka alipokata Roho, na YESU apofufuka hata wenye mapepo walisema kweli alikuwa mwana wa MUNGU nakutia moyo na wewe, Nampinga shetani kwa kuwa YESU yupo, napinga majini kwa kuwa YESU yupo, Napinga nguvu za giza, Nahubiri ukweli, Ninaringa ringa, napinga mafundisho ya uongo, batizo za uongo, kwa Kuwa upo wa MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

YESU ni mzuri, baadhi ya watu wanahubiri injili kama vile YESU hayuko, umeokoka unaishi kwa hofu kama vile YESU hayupo? Unaishi kwa uoga kama vile YESU hayupo? Unaogopa wachawi Kama vile YESU hayupo?  Unakufa haraka kama vile MUNGU hayupo? ninapiga  vita  vya kiroho  kwa ujasiri kwa sababu niko na MUNGU, yupo ni MUNGU wa vita tupige vita tusonge mbele kwa sababu YESU yupo, usijali YESU yupo, kataa mapepo, mapepo yanakuburuza yanakupaka mavi, wengine wana  mapepo mpaka kwenye viuno,   baaadhi yenu mnashanga viunoni, hayo ni mapepo, upendo  haukai kwenye shanga au cheni au  vitu mvyofunga kiunoni kwenu ili mume akupende, hayo ni mapepo kwanza upendo haukai kiunoni, wengine watoto wakizaliwa huwafunga kaniki, si pepo hilo? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Madhabahu za pepo zipo, na zile sadaka au vile vitu ambavyo mtu hupeleka kwa mganga ndizo sadaka ambazo zinanena kwenye ulimwengu wa Roho, pepo akishika kitu chako anabakia na kumbukumbu za kitu hicho na kukuwekea au kukiwekea walinzi wa kipepo kukilinda, wala hutajua kuwa ameshikilia ni mpaka unapokutana na YESU wa Nazareti akuokoe, MUNGU ni wa haki sasa aaangalia umetoa sadaka  kwa  majini, imebakia ni ibada inaongea,  sasa ili uwe huru sema Ibada zote za mapepo zinyamaze kimya,  ili ubakie na Ibada ya Roho Mtakatifu kwenye maisha yako, sawasawa? Acha kuogopa midomo ya mapepo,  wao sio MUNGU, kama una Roho Mtakatifu na kama umemkamata YESU mimi nakuambia, malaika wa MUNGU wanaokutangulia mbele utavushwa tu hata kama  ni mashimo, wakitaka  kukuua utalindwa tu na utapita katikati yao. Na mapepo yatateketea. Siku moja nilikuwa katika mji Fulani nikawekewa sumu kwenye chai,  malaika walikuwa wananitangulia, mbele wakavunja kikombe na sikunywa ile chai. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

          BWANA YESU asifiwe, mifano ni mingi ila huwezi ukawa na Pepo halafu umwone MUNGU usishindane na mwenye haki wa MUNGU.  Mtu mwenye mapepo akiona mwingine amefanikiwa anachukia mpaka anauma / nang’ata kidole kwa hasira, Tafakari! wanadamu waliokuwa wakiishi hata kabla ya miaka 1800 hawapo, unajua wako wapi, wengine  walichukuliwa na  Roho Mtakatifu na wengine walichukuliwa na roho mchafu sasa sitaki uchukuliwe na Pepo nataka ukaurithi uzima wa milele, Samehe, achana na mambo ya ajabu, unaweza ukawa na pepo wa kuiba vitu vya wana wa MUNGU au vya MUNGU pepo anakutengenezea laana, ili usimwone MUNGU,  unaweza ukawa na Pepo  la kutokuheshimu wazazi wako wa kiroho, Baraka zimekataa / haziji tena kwako hujui sababu,  unabakia kufunga na kutumia akili kumbe una pepo. Nitawaombea. Kuna watu wamefungiwa mapepo kwenye ulimwengu wa Roho. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Niliona wenye pepo walioshindana na Daniel walibakia na aibu na wenye pepo walioshinda na YESU walibakia na aibu,  Walioshindana na Eliya walibakia na aibu  na hata kwako  watabakia na aibu kwa sababu zile nguvu zinakwenda kuondoka, kuna baadhi walikaa kwenye nyumba zenye mapepo nao wakaondoka nayo,  inaweza pepo likawa kwenye nguo tu, umevalishwa Maroho, BWANA YESU asifiwe, Unaeza ukawa na pepo akili, mawazo mabaya, mabaya, mbona unapoteza, muda hebu amua yamkni umebakiza miaka 10  ufe, hutaki kuacha mabaya  hutaenda Mbinguni maana MUNGU ni wa haki, usidanganywe kuwa utakapokufa utaombewa  wakati wako ni sasa tengeneza na MUNGU wako mda ni sasa huu ndio wakati wa Neema usiicheze Neema hii, mkatae pepo na    yeye atakukimbia,  ni mkristo  lakini unapigia waganga wakakuchekie kwenye ramli na hata kama unasoma zaburi au unanena unapepo na unakwenda kwa waganga una pepo, hata hao wanaosema nitakupigia Ramli, wote wana pepo kila mganga wa kienyeji nayeagua anapepo, Ramli ni Pepo na kama humwabudu MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia utakuwa na Pepo, Pepo wa kutupiwa hutumwa na wachawi ili kukukuharibia maisha yako, kama  kutokueolewa, Nuksi balaa na mikosi Ila ukiwa na   Roho Mtakatifu utaona Malaika wanakuzunguka, wakija kukufanyia jambo wanakuta malaika wamekuzunguka wanabakia wakishangaa kwa sababu kila jambo la ubaya wanalotaka kukufanyia wewe unakuwa unaulinzi wa MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Ndoto mbaya unazoota au unaota mabaya tu ujue ni pepo hao wanafanya kazi, maana adui anataka kuharibu maisha yako mimi nataka ushamiri, Wengi hupanga mipango haipangiki lipo pepo ambalo kila ukipanga linaharibu halifanikishi jambo lako, lakini nitawaombea na MUNGU wa Mbinguni atawafungua.  Unajua hata mwanadamu anaweza akawa anamapepo anaomba maombi hayajibuwi kwa sababu yeye ndani yake lipo pepo MUNGU hasikilizi Pepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

MUNGU yupo, kama MUNGU yupo nani atatushinda na kama YESU yupo nani atatushinda, Hakuna, Vunja hiyo Imani  ya kusema siwesiwezi, Nitapita kwenye maombi atakavyoniongoza Roho Mtakatifu kutoa mapepo, kuyasaka na  kuyaragaza mapepo, watu wamekauka wamekata tamaa  unakuta kijana badala aoe binti anaoa mama mtu mzima kwa sababu anakuwa amekata tamaa, anaona hapendwi, yule mama anamwambia  nikuoe anakubali, Hata binti mwenye pepo ndio anamwambia mwanamume nioe, kwa sababu yamkini binti amemtoa mwanamume out, amenunulia vitu, amefanya yote kwa kijana lakini kijana haonekani kuwa atamwoa Binti anaamua kumwambia kijana nioe. Huyo ni pepo, maana sio kawaida ya binti kumwambia kijana nataka unioe. Tulia kwa Bwana YESU utapata vyote.  Au pia Wazazi wanaweza wakawa wamekata tamaa kwa sababu Binti au kijana wao haoi au kuolewa, Mke/mume mtu hupewa na MUNGU ila sasa ukipewa na wanadamu au mganga sio kusudi la MUNGU ni la mapepo. Wanandoa na wachumba simameni katika nafasi zenu ili mapepo yawakimbie, mitandao nayo imeongeza na kuwafanya wanadamu kuwa waongo kijana anaweza kuwa na wachumba hata wanne, anawaita wote darling, lakini wao hawajuani, hapo anakuwa na pepo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Pepo akimtoka mtu, mtu huanza kubadilika, unaweza kukuta mtu ameokoka. Mapepo ni mabaya na yapo tu kila mahali, hata katika ibada utakuta mtu anaiba kitu cha muumini mwenzake, hata makanisani kumewekwa Camera, kwa sababu pepo likimvaa mtu, popote anaiba tu, usiamini mtu hata kama akikuambia nimeokoka sikiliza Roho Mtakatifu ndani yako, MUNGU amekuambia yeye hacharge Riba,  hayo ni mambo ya kaisari pia ipo miujiza ya kipepo, kutolewa mawe, miiba na vitu mwilini hayo ni mapepo vitu hutolewa katika Roho sio kimwili, Sadaka za kipepo kukabana mashati,  ndio maana baadhi ya makanisa huwalazimisha waumini kutoa sadaka za kulazimisha, Mfano. Wanakuuliza nyumbani kwako mpo wangapi ukijibu unambiwa ili kufanikisha jambo hili unatoa elfu kumi kwa kila mmoja yaani kwa idadi  ya wanafamilia wako kama ina watu sita utoe elfu sitini. Ndio namna watumishi wakipepo wanavyotafuta pesa hilo ni pepo unakuwa umetoa kwenye mapepo kwa sababu sadaka yako ni siri yao. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Kumkatisha mtu tamaa katika kufanya kazi ya MUNGU, anayekutatisha tamaa ana pepo, uumefika mwisho umekata tamaa, mwambie pepo toka. Yuko pepo wa uvivu na huwapenda au hukaa sana kwa watu waliokoka, kwa sababu shetani wanajua, mtu aliyeokoka akifanya kazi atabarikiwa, kwa hiyo wengi walokole wengi wamewawekea pepo uvivu, kuzubaa zubaa kujiona kawaidakawaida na kuridhika, na vile wanajua kuwa watakwenda Mbinguni wanaona mali ni za nini?  Lakini ukifika Mbinguni MUNGU atakuuliza kwanini hujajenga kiwanda? Au kwanini hukufanya jambo Fulani? Wewe usiyefanya kazi Unadhambi, Pepo wa njaa. Niliwaambia tuombe Rehema  kwa ajili ya dunia nzima, kwa sababu Pepo Korona limeingia, japo wapo wanaomdharau MUNGU, na hata baadhi yao waliwadharau Watanzania na kuwabeza kwa vile waliamua kumwomba MUNGU, ndio tumeomba MUNGU  na MUNGU ametusaidia.  Na Nchi nyinginezo endeleeni kutubu, shauri lenu. Hasa baadhi ya wasomi, msomi gani halafu humjui MUNGU, Ukiwa na elimu yako kama humjui MUNGU ni hasara tu, Tafakari ni wasomi wangapi wamekufa wangapi?  Wengi wamekuwa mafuvu, na wanasubiri kuchomwa moto, sasa angalia Pepo asikae na wewe mpaka saa yako ya mwisho maana ni Roho inaona asije akakuchukua yeye akakupakia kwenye basi la mapepo katika ulimwengu wa Roho na ukawekwa kwenye nyumba ya mapumziko ya mapepo. Hata kama pepo limekukatisha Tamaa, limekuharibu, Rejea kwa MUNGU Roho Mtakatifu atafanya Zaidi na Zaidi, tunaelewana? Ayubu aliachiwa mapepo yakaharibu vitu vyake vyote lakini yeye alikuwa na Roho Mtakatifu, hata kuna watu ambao vitu vyote vimeharibiwa vimeisha usije ukamtukana MUNGU, huenda MUNGU anataka kukunyanyua sana lakini wewe unakuwa ni sababu ya kuchelewesha na kufanya MUNGU asichukue utukufu kwenye Maisha yao.  Sema nataka MUNGU akachukue utukufu kwenye maisha yangu. Sema sitaki mapepo yafanye utukufu kwenye maisha yangu, sema natubu na kuomba rehema, imetosha.  BWANA YESU  naomba toba na rehema, naomba  uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, ulitoe jina langu kwenye, mapepo, miungu, nitoe kwenye nguvu zao, kwa majina yao unanijua mimi nasogea kwako Bwana  katika ulimwengu wa Roho na mwili yako mapepo yalinisumbua sasa nimejielewa  natakiwa kuwa Mtakatifu, kuna mapepo ya magonjwa manung’uniko na ya laana,  Sema, pepo maendeleo, pepo dhambi  toka kwenye maisha yangu, leo nafuta mkataba ambao nilifunga na wewe naubomoa na kuufuta na Roho Mtakatifu akanitawale siku zote na hata milele Roho Mtakatifu ashuhudie Neno la MUNGU ashuhudie wokovu wangu, na Neno lake  akapate kulishuhudia mapigo yote ya majini na mapepo yakaharibikiwe mda huu katika jina la YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Kila shida na Mahangaiko naiondoa ndani yenu, Njia zenu ziachiliwe na Mapepo kwa Jina la Yesu. Kila pepo kwa jina lake akuachilie na Pepo anayeishi na wewe aangamie, Pepo anyekaa nyumbani kwako aangamie Katika jina la YESU na aondoke moja kwa moja na asirudi tena, Sasa Roho Mtakatifu  ajae kwenu na Baraka za MUNGU zijae Baraka za mapepo ziondoke,  Nuksi na vifungo viwaachilie, Pepo wanaowalinda ili msifanikiwe lolote, waondoke kwa jina la YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Baba nawakabidhi mikononi mwako, BABA pigana na wanaopigana na watoto wako,  Pigana na anayepigana na Tanzania, Pigana na anayepigana na Imani za watoto wako hawa,  BWANA pigana na anayepigana na nyota za watoto wako, pigana na  wanaopigana na afya zao kuanzia sasa na hata milele,  na wewe ulioletwa kwenye machela katika ulimwenye waroho nimekufufua.  Mshangilie BWANA. BWANA  awabariki sana jina la MUNGU liwe nanyi, Amani yake  na furaha palipopungua pakajae, Muongezeke, muinuliwe, mbarikiwe Mbarikiwe Mpaka wenye Mapepo washangae, MUNGU akatukuzwe juu ya Baraka zako.  MUNGU awatunze MUNGU awaonekanie, sasa na hata Milele MUNGU BABA hili ni Jeshi lako Takatifu, Lijenge upya liinue upya, lifariji wewe ni mrejeshaji, mponyaji, unayehuisha, wewe unawezesha, wawezeshe BWANA na mambo yao nawatabiria yakawezekane. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

BWANA amekuinua, Bwana atembee na wewe ndoa zenu na familia zenu naziinua na ziombea na kazi zenu nazizungushia moto nazitamkia zipanuke na kuongezeka. Neema ya MUNGU ifungue mipaka kwenye kazi, biashara, kilomo, ufugaji, na  kwenye maisha yenu ya kiroho na kimwili naondoa mipaka ya ukomo wa shetani na mapepo walikuwa wamekuwekea sasa njia zenu na zifunguke. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 

IMEANDIKWA NA MTUME NA NABII HEBRON