MAOMBI YA MWENYE HAKI HUJIBIWA
Tunamwomba MUNGU Mtakatifu, tunamwomba
MUNGU mwenye haki BWANA YESU asifiwe, kuna watu wanamwomba MUNGU na hawatendi
haki ya MUNGU na MUNGU hawezi kuwatendea haki, kwa sababu yeye MUNGU ni MUNGU
mwenye haki.
Mimi sijui wewe una haki ipi? Wewe mwenyewe yakupasa ujielewe kwa maana
kuna watu wanaomba sana, yamkini wako kanisani au sehemu nyingine lakini hana
haki, Lakini Biblia inasema maombi ya mwenye haki, MUNGU ndiye huyajibu, Kila
mmoja ajitafakari. Lakini nakufundisha ili ujue kuwa MUNGU anapendezwa na haki
yake, sitakiupoteze muda, unaopoomba omba kama una haki mbele za MUNGU na sio
kama msindikizaji, Je! Unajua maana ya kuomba? Kuombani kutafuta ushirika na MUNGU
sasa wewe hutaki kuwa mwenye haki wa MUNGU, halafu hutaki kuwa na ushirika na
MUNGU utapataje haki hiyo au maombi hayo yatajibiwaje? Unaweza ukawa unasoma sana,
unatoa sadaka sana, unaimba sana, lakini hutapata mafanikio kwa sababu sio
mwenye haki wa MUNGU.
Rumi
1:16-17 -
Kwa maana siionei haya injili; kwa sababu ni uweza wa MUNGU uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza
na kwa Myunani pia.
Yakobo
5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi
na kuombeana mpate kuponywa, kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa
bidii, Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia
moja na sisi, akaomba kwa bidii Mvua isinye na mvua haikunya kwa juu ya
Nchi muda wa Miaka mitatu na miezi sita akaomba tena Mbingu zikatoa Mvua nayo
Nchi ikazaa matunda yake.
Zaburui
34-15-22 –Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
naMasikio yakehukielekea kilio chao, Uso wa BWANA u juu. ni juu ya watenda
mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye BWANA akasikia, akawaponya
na taabu zao zote, BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho
huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANAhumponya nayoyote,
Huihifahi mifupa yake yote, haukuvunjika hata mmoja. Uovu utamwua asiye haki. Nao
wamchukiao mwenye haki watahukumiwa. BWANA na huzikomboa nafsi za watumishi
wake. Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
BWANA YESU Asifiwe,
Macho ya Bwana huwaeleke wenye haki,
na haki ninayoongolea ni katika ufalme wake, maana haki nyingine ni za
kishetani na ambazo asilimia kubwa ya watu ndizo wanazozitaka, maana kuna
familia nyingine zina haki ya kuabudu mbuzi, hiyo MUNGU hakuangalii maana hiyo
ni haki ya shetanipamoja na mambo mengine yanayoabudiwa nje na mpango wa MUNGU
au kinyume na ya mpango wa MUNGU.
Walilia BWANA akawasikia, akawaponya
na taabu zao, yawezekana wewe unaomba
sana lakini wewe si mwenye haki mbele za MUNGU na taabu zinabakia pale pale,
shida zinabakia pale pale utazunguka
kwenye maombi huku na huku bila majibu Nyumba za ibada nazo zinatakiwa ziwe
nyumba za haki ambazo MUNGU ameziweka kwa haki yake sio ambazo zimejiita au
kujiamkia (Yaani mtumishi anayefungua kanisa kwa kujiamulia yeye, ambayo hiyo
sio haki na haki ni MUNGU na MUNGU hataonekana, watu wengi hujiamulia na husema
ngoja sasa nifungue kanisa ili apate hela, Yaani anaona atakusanya sadaka
kiurahis kama hujaitwa na MUNGU unakuwa unajipandikizia laana, wengine hupewa
nguvu na mizimu, miungu lakini sio watumishi walioitwa na YESU wamejiita hatima
yake waumini hata muombeje hamfanikiwi wala hawapati hiyo haki ya MUNGU) 19
Mateso ya mwenye haki ni mengi,
lakini yeye BWANA humponya na hayo yote, ili MUNGU akuponye anaangalia haki
yake aliyokuahidi, huhifadhi mifupa yako yote hatautavunjika hata mmoja, uovu
utamuua asiye haki, jicho lake
linamwangalia mwenye haki wake na asiye
hali ule uovu utamuua, unaelewa? Biblia
inatufundisha kuwa MUNGU anatembea na wenye haki. 22Bwana huzikomboa
nafsi za mtumishi wake wala hazitangamia, Unaweza ukawa unamkimbilia MUNGU
lakini kumbe kwa kujua au kutokujua unakuwa huna haki ya MUNGU.
Tumesoma Warumi; Kwa maana siionei
haya Injili kwa sababu ni uweza wa MUNGU
uletao Wokovu kwa kila aaminie kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia kwa maana
haki ya MUNGU inadhihirishwa ndani yake
toka Imani hadi Imani kama ilivyoandikwa mwenye haki ataishi kwa Imani.
MUNGU anasema kuhusu haki lakini watu
wengi wameacha kuifuata haki ya MUNGU na
wanaona kuwa wao ndio wenye haki mbele za MUNGU badala ya kufuata haki ya MUNGU
kwanza ndio wawe wenye haki wao hufuata haki zingine ambazo sio za MUNGU na
kudai haki ya MUNGU.Ni haki ya MUNGU yeye kuumba dunia na kutuumba kama sisi
tulivyo, wanadamu kwa kujua au kutokujua
wengi wetu tunadai haki kwa MUNGU
wakati sisi hatutaki kufanya haki kwa MUNGU, Biblia inasema utakufa na uovu
utaangamia, MUNGU ni mwenye haki na Neno lake
ni lenye haki, MUNGU anasema usiabudu wafu, lakini wakristo kwa kujua na kutokujua wanaabudu wafu na sio haki ya MUNGU kuabudu
sanamu ni haki ya shetani,inakuwa ni haki ya shetani na mtu anakuwa mwenye haki
wa shetani na ile haki itawaua na hiyo haki ya shetani inaendelea kuwauwa kwa
kuwadanganya kuwa wakiwa hai wasiokoke mpaka wakifa BWANA YESU asifiwe, ni
haki yako wewe kuishi ni haki yako wewe
kuombewa bila kuchajiwa Pesa, lakini utakuta
mtumishi anakuambia leta Pesa hiyo sio haki yake, wala sio haki ya MUNGU
ni haki ya shetani, usifikiri anayeshinda mahakamani kwa kumdhulumu mwingine
haki yake, akafanya kona zake akashindahalafu akasema ni MUNGU amemsaidia, huyo
sio MUNGU ni shetani MUNGU ni wa haki, hapa ni shetani amemsaidia, nataka tuelewe, tumekuja kwenye maombi, mimi
ninaomba umwone MUNGU kama vile ambavyo mimi ninaomba lakini maombi pasipo haki
haikusaidii kitu haki ya kwanza.
Ukitaka kwenda kwa MUNGU ni lazima
uokoke, lakini unadanganywa usiokoke halafu unaomba na unasoma kitabu chake, unajisumbua
maana shetani anajua ukisha ijua haki ya MUNGU hakika mema au uzima mtauona, mambo
mazuri mtayaona, ni haki yako wewe kuwa Tajiri, kuponywa kufufuliwa ni haki
yako kufika pale MUNGU apotaka lakini shetani na yeye ana haki yake maana wako
wanadamu ambao na wao wakikuona umefanikiwa kitu, Roho inawauma inamaana
hawataki haki yako isimame.
Shetani huwa hataki mtu apate haki
yake toka kwa MUNGU na ndio maana anapotosha watu kwa mafundisho ya uongo, na
roho hiyo ya shetani imeingia kwa wanadamu ambapo utakuta mtu umeolewa, wanapita barabarani yamkini mume
wake ameshika mkono baadhi yaowananuna,
kwa sababu wanandoa hao wanapendana na wakiachana wanadamu watacheka, ina maana
hawataki haki yao isimame, umenyanyuliwa roho inawauma ina maana hawataki ile haki
uliyopewa na MUNGU isimame, ninawaambia katika jina la YESU mateso ya wenye
haki ni mengi lakini utakwenda kusimama, Nataka
uelewe haki, ni haki yako kuomba
na kumpigia makofi MUNGU ni haki yako kumpenda MUNGU, mimi nawafundisha haki ya Neno la MUNGU na ukitaka niibadilishe,
mimi sitabadilisha, sitapunguza wala sitaongeza chochote, nitasema na
nitafundisha kweli ile ya haki ya MUNGU, aliyoileta MUNGU yanipasa niwahubirie watu ukweli, wala nisichanganye changanye na mengineyo
ambayo sio ya haki ya MUNGU.
Ubatizo wa Yohana ni haki yaMUNGU
aliileta toka Mbinguni, Hivi YESU alibatizwa kwa maji mengi? Jibu ni Ndio! Hiyo ni haki ya MUNGU kwa
sababu yatoka kwa MUNGU, haki ya ubatizo wa kikombe imetoka wapi?na haki ya ubatizo
wa kisima imetoka wapi?Haki ya ubatizo ya mchanga imetoka wapi?Hizo zote ni
haki za shetani, au unaushahidi kuwa ni haki za MUNGU? kama ndio sema basi! Usiwe mnafiki mbele za
MUNGU ni haki yangu kusema ukweli na jicho lake linaniangalia ni haki yake
MUNGU, mimi nakuambia simama na haki yake MUNGU na wanaosimama mbele yako
kinyume na haki ya MUNGU, MUNGU atawaondoa,
nataka nikufundishe ili uijue
haki yako, haki imekosekana katika dunia
hii sio makanisani au hata kwenye nchi mbalimbali haki hafanyiki, nina waambia
haki lazima irudi, haki ya kuokoka ya kumwabudu MUNGU, haki ya kusimamisha Neno
la MUNGU, haki ya mapenzi ya MUNGU, lakini kwa sasa matendo ambayo wanadamu
wanayotendewa hasa au hata kutenda mengi
sana yamekuwa si haki ya mapenzi ya MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia.
Ni haki ya MUNGU wewe uitete Injilina
ukinyamaza mawe yatamshangilia, unajua mawe ni nini?Ni watu walio na mioyo
migumu na wasio haki watamshangilia na hata punda watamshangilia MUNGU,
usimletee MUNGU maringo ni haki ya MUNGU uzaliwe, amekupangia ukafanikiwe
katika njia zako MUNGU ndiye aliyekupangia, ila wapo baadfhi ya watu wakiona njia
zako zimenyooka kukunyang’anya haki yako.
Na Kama uliabudu kwenye madhabahau
ambazo sio ya haki ya MUNGU hata miujiza ikiwepo hapa sio ya haki, Mfano: Mtu
anaenda kwa mganga Je! ni haki ya MUNGU au ya Shetani, chale, tunguri, ramli.
Ramli - hilo ni jichola mapepo na mashetani.Ramli nipepo utambuzi,acha kwenda
na kufanya hayo, toka kati yao ukatengwe nao, simama kwenye haki utamwona MUNGU,
achana na hizo haki za kishetani, wanaweza kukuzingua zingua simama na haki ya
MUNGU na adui anaponyanyuka MUNGU atamtuliza Je! Utashindana na MUNGU? Ambaye ameumba
dunia nzima akaiwekea misingi minne na ina nguzo zake, ambazo yamkini ile siku
ya mwisho atavunja mbili tu dunia inakuwa imeharibika, Je! Maombi yako ni ya
mwenye haki? Au unakuja kujaza kanisa, unapoteza muda wako au msindikizaji hata
mpiga debe stand, utasikia anatangaza Moshi, Dar lakini haendi, saa ya gari
kuondoka anateremka, isiwe tunaenda Mbinguni wengine wanashuka, nataka nikipiga
debe saa ya kuondoka ikifika tuondoke pamoja, ukitaka kutoka nitakuzuia au mara
nyingi makondakta wanajazana kwenye basi na wanakuambia bado seat chache kumbe
wao hawaendi walikuwa wamejaza seat tu ili abiria wapande waone gari limejaa,
hata sasa wako wahubiri ambao hawawapeleki watu Mbinguni ni sawa na wapiga debe
hao, wanazuia watoto wa MUNGU kwenda Mbinguni wakati wao pia hawaendi wanazuia
Haki yao, watu wanakufa mapema kwa sababu haki ya kuishi hawana wamejikatia
tamaa, wanaona kifo, nani kakuambia unakufa?Wengine husema nimefika mwisho,
hapo anaiona kuwa hana haki ya kuishi, una haki nyingi inakupasa uzijue.
Unaweza ukawa mwombaji ukawa hauna haki kwa MUNGU unayemwomba.
Tafuta haki na MUNGU kwanza, haki ya
kwanza okoka, si kwa mdomo kwa matendo, na si unaokoka nje lakini ndani ya moyo
ni Paka au Mbwa Mwitu. Mimi Hebron endapo MUNGU atazidi kuninyanyua kwa viwango
vya juu Zaidi na Zaidi sitabadilika kimwili au kiroho au hata kimatendo
nitaendelea kunyenyekea na kumsikiliza MUNGU.
Maombi ya mwenye haki hujibiwa, watu
wengi husimama na Mistari ya biblia Yakobo, Yohana, Zaburi na mingineyo katika maombi,
ni sawa yamkini hana haki, hivyo maombi hayajibiwi haki yako unaipata wapi?
Okoka, unaweza ukawa unasali kwenye madhabahu isiyo nahaki ya MUNGU, ina haki
ya mizimu Mapepo, au miungu MUNGU anasema usibudu sanamu lakini watu wanafuatahaki
ile ambayo si haki ya MUNGU, na ndio watu wanayoipenda. Kabila niliyozaliwakila
mwezi wa 12 wanaenda kuchinja Mbuzi, badala ya wao kumshukuru MUNGU kanisani,
huwa wanaenda makaburini kushukuru, wanaenda kushukuru kwa kuchinja na kumwaga
damu ya mbuzi makaburini, Je! kwa kabila wanafanyaje? Je! Mnajua?Hata baadhi ya watu
huja kanisani kumshukuru MUNGU lakini wanarudi tena kwenye matambiko, MUNGU hashukuriwi hivyo ndio maana hamwongezeki,
kwenye mataifa mabalimbali mambo sio swari kwa sababu MUNGU akishaondoka, Taifa
linaanza kugombana, na wananchi watakosa haki yao, mtapiga makofi na kumwimbia
MUNGU na kumtafuta MUNGU, na kujiuliza kuwa MUNGU yuko wapi? Kama hakuna MUNGU
hutamwona. utaona Elia yeye alikuwa
anatenda haki na anamwamini MUNGU,
akiomba majibu hata kwa moto yanajibiwa, wale wengine walikuwa wanaomba kwa baali hakukuwa na majibu, Eliya akafunga mvua miaka
3 na miezi sita, mwenye haki wa MUNGU
baadae akatulia na akaomba mvua
ikanyesha, na leo upo kwa mwenye haki wa MUNGU, nitakuombea maana sibahatishi nataka upate haki yako haraka, haraka ila wengine wamejikatia tamaa
wanaangalia mke au mume wake,wanaangalia majaribu na vituko vya nyumbani kwao,
mwingine anangalia ada ya shule,
uliyakosa hayo kwa sababu hukuwa mwenye haki wa MUNGU, maana ni haki yako usome, ni haki yako urejeshewe
hata yale ambayo umenyang’wanywa, wachawi au washirikina wao huiba haki za wana
wa MUNGU na kukuachia haki mbaya,
unaweza kukuta mtu ni tajiri sana lakini yamkini ameiba haki za watu kama mia
mbili, halafu wanakuwa wamewaachia haki
mbaya, mbaya kwa shetani hakuna kitu,
MUNGU ni wa haki Shetani alivyokuwa mbinguni aliambiwa atende haki na MUNGU
lakini alipoacha kutenda haki MUNGU akamporomosha, umenielewa, yamkini MUNGU alimwambia utakuwa
malaika wa sifa milele lakini kutokana na yeye kutokufuata haki ya MUNGU, MUNGU alimporomosha na malaika
zakewaliporomoshwa. Yamkini umtumishi au umeokoka MUNGU ana haki ambayo
alikupangia katika maisha yako auahadi ilawewe kwa kutokufuata haki au
maelekezo anayoyataka, unayapinga basi anakuporomosha, anaachana na wewe halafu
anasonga mbele, lazima muelewa, Nikupa Neno likusaidie.
Lakini kwanini watu hawataki kuokoka
mpaka sasa hivi? Watu hao wanakuwa na haki ya kwenda Jehaman na siku ya mwisho
MUNGU ni MUNGU wa haki na ataangalia Je! Uliokoka hapa duniani? Kama
uliokoka na kufa katika haki utakaa na
wenye haki wa kwenda mbinguni na kama hutaki kuokoka utakufa na utakaa na wenye
haki wa shetani ambao wanasubiri kuchomwa ile siku ya Mwisho, linda sana
ulichonacho asije mwizi kukunyang’anya, sijaona mwenye haki ambaye aliachwa na MUNGU,
lakini yakupasa wewe uikubali haki, kuna ahadi nyingi kuwa watashindana na wewe
lakini hawatakuweza kwanini? Hawatakuweza kama utakuwa mwenye haki wa MUNG,
BWANA YESU asifiwe, Mtu anaomba anamwambia MUNGU kumbuka yale ambayo
nimekufanyia, ukijifananisha na Kornelio akina Dorkas, hawa walikuwawenye haki
katika MUNGU na haki ikawafufua, tunaelewana, Hebu wewe jitafakari! MUNGU
angalia niwapi umetoka? Unapoabudu? Angalia ni wapi umetoa sadaka zako? Je
matendo yako ni ya haki? Sasa kama
ulikuwa hujui napenda ujue, hata katika maombi ambayo unamwomba MUNGU, MUNGU
huwa anangalia haki ndipo akujibu. MUNGU
anaangalia, Je! umeshikamana na haki yake? Amesema usiabudu nyani au viumbe
vyovyote, pia usiabudu miungu, Je! Wewe unaabudu nini? MUNGU anasema usiabudu
viumbe vyovyote ila MUNGU tu, mara unaabudu watu, sanamu au mti, MUNGU si
sanamu wala hapondwipondwi, wala hafananishwi na chochote atakuwepo, alikuwepo
na atazidi kuwepo.
Wengine mioyoni mwao wanasema, huyu
Hebron anasema au anafundisha nini! Mimi nitasema kweli katika jina la YESU, vitu
vingine si kuomba,unajua kwa nini watu wanashambuliwa na majini na Mapepo? Kwa sababu wanapata nafasi ya haki shetani
(Yaani ipo milango ambayo shetani anapata na anakuvamia kwa urahisi) wanapata
mlango lakini pepo au jini likikuta kuna Moto, Yaani YESU, linaondoka,
ukikuta mtu ana mapepo mengi ndivyo alivyo na milango mingi ambayo
inamruhusu shetani awe na haki katika mwili au mtu husika,, sio milango ya bawaba
ni katika roho, Je!Umekaaje wewe, unawazaia nini wenzako? Unawaza mema au
mabaya? Na hata unaweza kuimba wimbo,
ukasema YESU tembea nasi,YESU tembea nasi, twakuomba, wakati huna haki ya kutembea na yeye, YESU hatatembea na wewe, Haki
lazima uipokee, uikubali na uiamini halafu utaona akikutendea, kuna wakati
nilisafiri wakataka kuniangusha lakini
malaika wakaenda wakazima ndege ile na mizigo ikiwa imeshawekwa ndani, lakini
MUNGU aliniambia ndege hii hautapanda, begi lemewekwa mapailoti wameshaendaa, ndani yangu nasikia
hutapanda ndege hii, nikajua ni akili za
kibinadamu, kumbe jamaa walitaka nikadondokee mahali, hawakuweza, usishindane
na mwenye haki, nilienda na nilirudi
salama.
Jicho la MUNGU hupenda kuangalia
mwenye haki wake, haki kwenye Neno haki kwenye kweli, haki ya kumpenda, haki ya
kutokutikisika, haki ya kumtete MUNGU, haki ya kupenda kweli na kupenda kazi
yake, lakini ukiwa mnafki, mnafki sukuma twende, Jicho la MUNGU halitakuangalia,
Mzimu wa babu itaingia itakutandika, tandika, wachawi wanakunyoa nywele, mambo yatakuwa
hayaendi, hata kama umepakwa mafuta ya utumishi na wewee yamkinikumbe mnafki
mambo hayataenda, Maombi ya mwenye haki MUNGU huyasikia.
Napenda nikufundishe kwanza ili
nitakapokuombea kama ulikuwa huna haki upate na kama kulikuwa kuna mambo
mengine ya kuacha uache ili upate haki zako. Kwenye wokovu kuna milima na tambarare
Rumi 1:17 – Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, sasa sijui wewe ni mwenye haki wa Shetani au majini au miungu na
kanisani upo, watu kama hao MUNGU hawapendi nakuambia ukweli, injili ya
kukupaka mafuta ili ujae kanisani sina, nakuambia ukweli ili upone. Je! una
haki, yamkini unaweza kusema kuwa MUNGU
habaguagi mashetani wala watakatifu, maana huwanyeshea mvua wote, hiyo ya mvua
ni Neema tu, ila kaa ukijua kuwa Kila
mmoja anavuta kwake MUNGU anavuta kwake na shetani nae anavuta kwake, Je! Unamtendea MUNGU haki yake au unamtendea
shetani haki yake?Unajua hata wachawi wanamtendea shetani haki yake? Akiambiwa
saa saba usiku atoke nje anatoka kwa muda
muafaka wala hachelewi, akiambiwa
tukuwekee kuku kichwani anatulia kuku anachinjiwa hapo, chochote ambacho mganga
atataka kukufanyia anakufanyia umetulia hapo, unakuwa mwaminifu sana kwa
shetani badilika sasa yatupasa tuwe waaminifu kwa MUNGU, usipotenda haki
inaondoa Baraka, usipoangalia familia
haki MUNGU anaondoka anampa yule ambaye anaitunza familia, unacho hauna MUNGU anajua, MUNGU
anapokushushia Baraka na weewe ukajiona
ni wewe ataviondoa vyote mkose wote.
Utakumbuka kipindi cha Suleiman, akaletewa wamama
wawili, wakiwa wanagombania mtoto mmoja, na kila mmoja akisema ni wakwake, Basi Suleiman
akasema namchinja mkose wote, mama halali wa mtoto akasema kuliko achinjwe ni
bora apewe mwenzake amlee na yule ambaye mtoto hakuwa wakwake akasema ni bora
aachinjwe ili wakose wote. Suleimani akatambua kuwa mtoto yule alikuwa wa mama
ambaye alisema bora asichinjwe, hivyo Haki ikatendeka, lakini mama yule alikuwa
anaibiwa haki yake, wewe umeibiwa haki ngapi? (katika maisha yako mpaka
ulipofikia umeibiwa na wengi yamkini ni
kibabu au kibiki, kimzimu au wachawiyamkini chenyewe kilivaa majani kinataka na
wewe uvae majani kama yeye, wewe ukivaa koti koti inakuwasha au haki yako ya
usafi imechukuliwaga na mjomba miaka mingi wewe hutaki kuoga) unaweza kuibiwa haki
ya kuwa mtoto wa mfalme hata ukipelekwa mahali ukanunuliwe chakula cha 10,000
unasema uwiii ungenipa tu nikale cha mia
500 haki imeibiwa, shetani hana kitu na
anabahati mbaya mimi naijua siri yake nataka ukaipokee na aliyenayo mimi namnyang’anya
na kukukabidhi, Biblia inasema haki inapoondoka
hata kwenye Taifa, Taifa linaangamia, kuna Nchi mambo yameharibika ni vita na pia katika Nchi
nyingine mambo pia yameharibiak haki haipo,
MUNGU nachukia kunyanyasana, MUNGU hapendi yako mambo mengine nawaambiaga yanatokea
mabaya msifikiri ni MUNGU anafanya, mengine nimewaambia na mnasema Nabii
alisema ni kweli nawaambia na ndivyo MUNGU anavyotaka, lakini endapo yamekiukwa, na haki wa MUNGU
kuachwa na pia kwa mambo ya kunyanyasa watu MUNGU hapendi, Tunaelewana?
Si mpango wa MUNGU unadaiwa, unachukua
hii unalipa hapa mara pale unakopa tena, mashine ambayo ni wewe ni madeni full,
sasa endapo umejaa madeni Je! Una haki? Kila unapobarikiwa kiasi Fulani na
MUNGU unashukuru, halafu unalipa hapa kesho unakopa hapa ni haki hiyo kweli? Au
ni Madeni? Haki yako ya kuwa naPesa na kukaa nazo na kuzimiliki ipo wapi? Na unasema Bwana ananisaidia, Madeni yanatakiwa
yaishe, yakatike, Bwana YESU asifiwe, una roho mbaya, wakati MUNGU anaroho
nzuri, angalia ndani yako ipo Roho gani? Unataka huyu asifanikiwe, asifike
utakuwa umebeba mzoga utanuka, ujue kuwa unamapepo, mwingine anakukwamisha
mwambie pigeni Sanamimi sikwami. Wakienda kwa wachawi waambie kuwa wakaloge
sana kwa sababu hawatakuweza.
Pia katika baadhi ya makanisa kuna
Mungu asiye haki ndio maana huduma hutolewa kwa pesa, pesa tu, MUNGU anaponya bure, siku ile haki itatendeka na hujui kuwa ni
haki ipi, MUNGU wa haki yeye ndiye
aliyeanzisha haki, ukitaka kuziona Baraka za
MUNGU penda kutenda haki ila hapo ni pagumu. Unaweza kufunga na ukatoka
kwenye mfungo ukajikuta sio mwenye haki, Penda kupata mume/ Mke toka kwa MUNGU, Baraka kutoka kwa MUNGU
mwenye haki utaona hizo haki zikisimama milele na wengine wanapewa na MUNGU
haki zao lakini hawazipati au kuzipenda, wanataka zingine, MUNGU amekupa utajiri
wa haki yake lakini hupendi unataka ule
wa kuua na kutoa kafara na kuua ndugu au wazazi wake, wanawaua na wao wanaiba
haki yao, ikaibiwa haki ya watu kuokoka, ukawa mkristo wa bila
kuokoka, Mkristo wa bila kuokoka huna haki ya kwenda Mbinguni, amua unasuka au
unanyoa, kata mambo ya kutiwa moyo kwa uongo,
Wokovu umetoka wapi? Umetoka kwa MUNGU, Ubatizo wa Yohana umetoka kwa
MUNGU, Jiulize! Batizo za kikombe zimetoka wapi? Mbinguni? Hapana! Watu wengi
ukisema kweli wanadai kuwa usiseme maana watu hawatakusikiliza, ninachiamini
mimi na kujua ni kuwa endapo wewe hutasikiliza na kuamua kubadilika wengine
watapona na hatimaye uliyekataa utaenda Jehanamu shauri lako, baadhi ya
Madhababu hawataki kuhubiriwe kweli ya MUNGU kwa sababu waumini wataondoka,
sasa mwambie nahubiri ukweli wa kubaki watabakia na wakuondoka wataondoka,
lakini haki ya MUNGU lazima ihubiriwe tunataka haki, haki utakatifu, upendo na
kupokea Baraka za MUNGU.Ukiwa Mfungwa, umefungwanauko gereza lazima umalize
kifungo ndipo upate haki ya kutoka nje, la sivyo hutatoka labda tu msamaha
upitendipo utoke.
Mkamate MUNGU mwenye haki na maneno ya
wanadamu yasiyohaki hayatakupata, maneno hayo ni kama, atafika wapi, tuone
mwisho wake, ataishia njiani, hutaweza,
Maneno haya hayawezi kufanya jambo kwa mwenye haki wa MUNGU, Mwangalie MUNGU mwenye haki jicho lake litakuponya na
shida na mateso, na hawataonekana milele
katika jina la YESU wakijipanga wataangamia wakisimama wanaporomoka, kaa kwenye
haki adui zako watakuwa mwehu, kama una
haki hata Korona haitakupata, maana kuhusu ugonjwa huu akili ya mwanadamu
imefika mwisho na hata Korona ikija
haitakupata, ila kumbuka kuwa hizi ni nyakati za mwisho na wanadamu lazima
wapitiechangamoto nyingi kama vile ilivyoandikwa ili pia wanadamu wamgeukie MUNGU, Unaweza kujiuliza yaani Nabii anasema dunia
ipigwe, ya MUNGU siwezi kuyapinga ni
haki yake MUNGU yalishaandikwa, hivi jiulize kama ungekuwa hujapingwa,
hujalogwa, ungekuwepo kanisani kweli?Ungekuwa unasoma habari za YESU kweli?
Endapo wachawi hawakufuati fuati
tuseme ukweli, ingelikuwa hakuna misukosuko tofauti tofauti ungekuja kanisani
kweli? Kipindi kimeharibika baada ya shetani kuingia pale Eden, wakati ule wa
Adam na Eva, na ndipo MUNGU akamtuma
mwanaye wa pekee ambaye ndio haki yote atakaye mkubali na atakaye mpokea
atafanyika haki na kuurithi uzima wa milele, shetani hampendi mwenye haki
utakumbuka Ayubu, MUNGU akajua huyu ni mwenye haki wangu, akamwambia usiguse roho
yake, akaguswa kote lakini Ayubu hakumwacha MUNGU, kuna watu ambao wako na MUNGU wameshasimama, lakini akitukwanwa
tu au akakwazwa tu kwenye wokovu ataacha
na wokovu kama mke wa Ayubu, yamkini ni muimba kwaya au mchungaji wakakusema,
au wakatafutia skendo, ukasema huyu MUNGU namtumikia halafu mambo ndio haya?
MUNGU yuko wapi mbona asiwaambie wanyamaze? Hapo unakuwa kama mke wa Ayubu, basi
mshukuru MUNGU kwa kila jambo ili upate kuwa mwenye haki wa MUNGU. Lutu
aliambiwa na MUNGU nenda mbele, mwenye haki, yeye akatii mkewe hakutii akawa
jiwe la Chumvi. Kupitia mwenye haki mmoja familia inapona, mnanielewa, Musa
mwenye haki ya MUNGU anaongoza kupita bahari ya shamu wale waliomkubali
akawaongoza wakavuka na wale walomkataa waliangamia, wale waliomkataa na wale
wana wa Farao waliku hawana haki ndio maana waliangamia walikuwa wanambishia
Musa, walimkosoa,hawkumsikiliza, walifanya mazoea pia. Musa akawaambia walio
upande wangu waje upande huu, wale waliompinga Musa, ardhi ikawameza, na wale ambao walikuwa wana wa MUNGU, wenyehaki
ya MUNGU na wana haki ya MUNGU walipona na wakavuka, mimi nakujenga, usonge
mbele maana shetani anatafuta mahali pa kuporomosha watoto wa MUNGU, ukikaza
shingo unaporomoka, MUNGU anamwangalia
mwenye haki, anaangalia Kondoo, Taifa na Kanisa.
Taifa linaweza kupona kwa sababu ya
mhubiri mmoja au wawili wenye haki tu, ambao wamesimama naMUNGU, lakini yule
mwenye haki akiondoka au wakimchezea Taifa linaangamia, ila Taifa wakimwomba
MUNGU na kumrudia MUNGU mambo yanakuwa shwari. Mwenye haki wa MUNGU hutafutwa
na MUNGU mwenyewe, watu wana viburi sana, unajua usiwe na viburi kama baadhi ya
maraisi na wafalme waliopo dunian,i wao wakiwa na vyeo wanaona ndio wamekuwa kama
MUNGU. Wanadamu wote wako chini ya
MUNGU, na baadhi ya watu wanajiita YESU na waumini wanawaita wahubiri MUNGU,
MUNGU au YESU kumbe ni mwadamu si haki mwanadamu aitwe MUNGU, MUNGU
hafananishwi wala kulinganishwa, utukufu wa MUNGU usichukuliwe na shetani.
Tunaelewana kuwa waoga hawaendi
Mbinguni unapokuwa mwoga maombi yako hayapokelewi, mapepo yanaangalia mwenye
hofu na muoga, ukiwa na hofu hutaweza fanya jambo wala kufanikiwa, unapoteza
matumaini, unapomtegemea mwanadamu haki yako imepotea, hivyo mtegemee MUNGU
upate ujasiri na haki yako kwa urahisi, watu wengi hudai haki za mafao ya uzee
na haki za mali pale ambapo wana ndoa wameachana, huwa wanasema tumechuma wote,
tumezaa watoto, nk. Mwanamke anadai haki
yakekwa mumewe, sasa mbona mume akiachwa hadai haki yake? Mbona alikaa namke
vizuri na kuchuma mali pamoja? Na mke akili ikatulia mambo ikanyooka? Sasa
iweje mzazi mmoja anadai kuwa mtoto ni haki yake na mzazi mwingine je! Haki yake I wapi?, mtoto ni haki ya wazazi
wote. Hata sisi wazazi yatupasa kutenda haki, YESU peke yake ndio alikuwa haki
ya MUNGU maana ilikuwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ila mwanadamu ana wazazi wawili
baba na mama. Mambo ya MUNGU ni ya haki. Ni haki ya wanandoa kushikana mikono
wakati wanatembea, sasa ukiambiwa mshike mkeo mkono hata hapa kanisani utaona
haya, kwanza unaingia hofu na pili utawaza watu watanionaje? tatu uwiii, hata
kumshika mkono hawezi, atamwambia tangulia mbele naja, mshike mkono mke wako.
Fananisha kipindi au watu wakiwa wazinzi, utamshika mwenzako mkono, unaambiwa
ni wewe tu kijana anafura kichwa kama ubwabwa na binti unafura kichwa kama
pilau ambayo imefunikiwa juu, unajipa matumaini ni mimi tu nimefika umefika
wapi? Tulia uolewe au uoe acha uzinzi, Tunaelewana?
MUNGU anatakaga kufanya jambo kwako
lakini wewe ndio kwazo, yamkini ulikuwa ameolewa na ndoa ameshafungushwa ila
bado unachukua simu kisirisiri anampigia
aliyekuwa girl friend au mume ambaye mlishaachana, unamwambia nipigie Fulani,
maana baba Fulani ndio atakuwepo yupo kazini, unamwambia jamani nakukumbukaga?Sikusahau
aisee!! Wewe uliyeoa au kuolewa acha
unafiki, unamwambia mke wa mtu a,u
yamkini u mume au mke wa mtu, unamwambia
usinipigie mpaka nikubip ndio atakuwa hayupo bado unataka haki ya zamani? Acha
hizo tabia, mwingine ana wachumba wanne, kijana ndio anawaambiawale wachumba,
usinipigie simu, mpaka mimi nikupigie,jicho la mwenye haki linakuangalia
unavyowadanganya, badilikeni basi watoto wa kizazi hiki, MUNGU anaangalia haki
anaangalia msimamo wako, hapendezwi na
mtu anayeyumba yumba, mimi Hebron, baba yenu kiroho, ningekuwa nayumba yumba
msingelikuta makanisa yanaendelea si kwamba na mimi sipitii kwenye vipindi
vigumu napita lakini mimi sijali maana
uhai wangu upo hata kama sina hela namwangalia MUNGU, ndio maana makanisa
yanaendelea na injili itakwenda tu, kazi yangu itaenda tu, maana ni mwenye haki
wa MUNGU, wahubiri wengi sio wenye haki wa MUNGU, ndio maana wanachangisha na
kugandamiza waumini. MUNGU ameagiza mwenye haki wake amuulize naye atafanya,
sasa wengi wa wahubiri sio wenye haki wa MUNGU lazima wawaulize waumini, kuwa
watapata wapi pesa za kuendeleza kazi ya MUNGU, badala ya kumuuliza MUNGU, na
ni lazima wawaulize ninyi maana awanakuwa wenye haki wa wengine, sio wa MUNGU,
tunaelewana; hata sadaka zako unazotoa, mafungu yako ya kumi yamkini hujatoa
mahali ambapo ni pa MUNGU, sadaka hizo hazitaongea, hazitanena, utasota mpaka
utashangaa, hebu badilika na kila mmoja abadilike.
Haki ya MUNGU! Wengi huapa! na kuapa kwa Neno hilo wengi wameapa na husema
na kuapa hata kwa uongo, hata mimi nilishalisema sana zamani na Biblia inasema
usilitaje jina la MUNGU Bure na wanatumia kidole kuapa, haki wa MUNGU!Tena unasema hata nife! Hapa!
Hapa! na umesemea uongo, unathibitisha kutumia jina la MUNGU kwa uongo, bila kukumbuka kuwa Mbinguni kuna
kila kitu na kumbukumbu hazifutiki,hivyo yote uliyofayanya yapo, hapa duniani
unaweza ukafa na ukazikwa na hata kaburi
likapotea lakini kamera ya Mbinguni inajua
popote ulipo,ulipozikwa na kuna
spika inayorecord sauti yako masa 24, uliloga lini, tarehe, mwezi mwaka, mara
ngapi, unawaza nini? Ulifanya nini? Zote zipo Mbinguni, umeua ipo, ila unapokuja
kutubu na kuomba Rehema mambo yanafutwa unaanza upya, mambo mengine ndio maana
nawaambiaga kwa uchungu sio kwamba nakuambia au kukuonya ili ufunguliwe na
uinuliwe ila yanipasa nikueleze ili ufunguliwe na kuacha uache, ili siku moja
ufike Mbinguni na umfurahie MUNGU. Je! Itanifaidishanini endapo ninakuona hapa duniani, na nina uwezo
wa kukuonya na sikuambii ukweli halafu ukachomwe moto Mbinguni, ni bora nikuambie, acha, ili uponywe na
uninunie na ukifika Mbinguni utamshangilia na kumtukuza MUNGU, tunaelewana
watoto wa MUNGU? Lakini nikikueleza na ukashupaza shingo ukiangamia sitadaiwa
na MUNGU.
MUNGU hapendezwi na mwenye haki
anayesitasita, tena usije leta haki za
shetani katika kanisa hili, na kama zipo basi zing’ooke, haki za shetani na miungu zing’ooke na hata
kumwabudu wanadamu haitakiwi, wanadamu
wote wamwabudu MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia, umeomba maombi mangapi? na
umelia mara ngapi? Jiangalie una haki? Jichunguze,
hata mimi baba yako wa kiroho yanipasa
nikufundishe katika kweli na haki na nikueleze ukweli maana ni haki yako, nikuombee ni haki yako nikulinde kiroho kwa
maombi, nikeshe na nikulinde na nikuongoze ili uende Mbinguni. Biblia inasema
waheshimu wanaokuombea, ili yale yote ambayo yalikuwa mema yaje kwako, na
endapo utawabeza watumishi wa MUNGU wanaokuombea na kukesha kwa ajili yako
yatakata, yatakauka, hutapata baraka, hivyo waheshimuni wanaowaongoza kiroho,
wapendeni, unawezaukawa unateseka kwa sababu unadharau wengine, Roho wa MUNGU
anajua pale ambapo mtumishi wa MUNGU anakesha na kuomba kwa ajili yako halafu
wewe unamfanyia mabaya, fitina anamfitini, MUNGU anazuia yale maombi halafu
anakutandika,
SEMA: BWANA YESU ninaomba toba na Rehema, nilikataa
haki ya Wokovu kwa mda mrefu kwa kujua na kutokujuana nikataka haki ya shetani,
ikiwa ni pamoja na kuishi bila kuokoka, nikawa Mkristo ambaye amekataa wokovu, ninaomba toba na
Rehema, ninakataa haki zashetani, imani za kishetani, kwenda kwa waganga
mengineyo niliyofanya kwa kujua na kutokujua na ninatubu dhambi zote nilizofanya, madeni ambayo shetani anaidai ninawalipa damu
ya YESU katika ulimwengu wa Roho ninabomoa na kuvunja mikataba niliyoingia kwa jina la YESU, najitenga na haki ya Ibilisi ya
miungu, mapepo, haki za mizimu, haki za kuabudu mizimu na ile nguvu ambayo
inanisukuma kwenda kwa wanganga na
wachawi nina ikataa, maana sio roho ya
MUNGU ni roho ya Shetani, naikataa haki za shetani katika jina la YESU. BABA
MUNGU ninaomba haki ambayo inatoka katika kiti chako cha enzi, ndani ya
madhabahu yako ambayo umeweka haki yako, ukanitendee haki, ukanipone na
shetani, ukaponye amani yangu, ukaponye viungo vyangu, ukaponye wokovu wangu,
navua haki zote za ibilisi kizazi cha kwanza mpaka cha nne cha mizimu, mapepo
Miungu, nazivua maana zimenikosesha Baraka, zimeniwekea vifungo nazikataa kwa
jina la YESU, na kwa damu ya YESU,
ninaomba haki katika miaka yangu, haki iliyoibiwa naomba uirejeshe, utajiri
wangu uurejeshe, afya, nguvu, Amani nay ale ya haki yangu ninayoyajua na
nisiyoyajua yarejeshwe kwa jina la YESU.Nyota yangu irejeshwe. Naomba uandike
jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele na Naomba jina langu
lisitoke huko. Amen.
Mwenyezi MUNGU awabariki, awainue na
Muwe na Baraka tele. Amen.
NABII
HEBRON WILSON KISAMO.