KUNYANG’ANYA MADHABAHU MBALIMBALI ZILIZOSHIKILIA MAISHA YAKO
Asante Baba kwa mda huu na wakati huu, wewe ni MUNGU mwenye uweza na mamlaka, ni MUNGU usiyefananishwa, ni MUNGU mwenye madhabahu yako kuu, yenye uwezo mkubwa kuliko madhabahu zote, ninakushukuru kwa siku ya Leo naendelea kusafisha anga na kuondoa kila aina ya vizuizi kwa jina la YESU, BABA ninaomba ukawatendee watoto wako mambo makubwa, uaendelee kuwaponya na kuwainua, ukaendelee kuwarejesha na kuwatia faraja na pale ambapo yupo adui asiendelee kuwagandamiza watoto wako, na adui wa watoto wako hawa wateketezwe, BABA kama neno lako linavyosema kuwa hao waamori hamtawaona tena, naomba uondoe shida, mikosi magonjwa, laani kwa watoto hawa na zisionekane tena katika jina la YESU. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Haleluya atakuja kwa mawingu alioyewambwa mtini, atakuja, na atakuja kweli, sasa anaonekana kiroho lakini ile siku ya mwisho akaonekana kimwili, BWANA YESU asifiwe. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Somo: Isaya 19:19-22 - BWANA YESU asifiwe, leo ninafundisha na kufanya maombezi ya kuwanyang’anya wale wote ambao wameshikilia maisha yako, maisha ambayo wameshikiliwa katika madhababu mbalimbali, za ukoo, majini, kabila, nk. Maana biblia inasema pale unaposali ndipo mahali ambapo maisha yako yanakuwepo, umesali kwa majini, kwa waganga, mizimu na kuiabudu sasa si maisha yako yamebaki kwao? Umelala makaburini, mpaka unafika wakati unaona maisha hayaendi hayasongi yamekwama, yamkini unajua au hujui sababu ambayo inasababisha yakwame, lakini ashukuriwe MUNGU kwa kuleta madhabahu yake hii itawanyang’anya, hapa ni haki. “Katika siku hiyo itakuwepo madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, Na nguzo mpakani mwake kwa BWANA, nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri kwa maana watamlilia BWANA kwasababau ya watu wawaoneao, naye atawapelekea MWOKOZI mwenyewe kuwatetea, nae atawaokoa, na BWANA atajulikana na Misri na Wamisri watamjua BWANA siku hiyo nao watamtumikia kwa dhabihu na matoleo nao watamwekea BWANA nadhiri na kuzitekeleza nae BWANA atapiga Misri na akipiga na kuponya nao wakirudi kwa BWANA atakubali maombi yao na kuwaponya”Sina maana ya Misri ile, ila hapa duniani, Duniani kuna dhiki kubwa, naifananisha na Misri lakini MUNGU anasema atashusha madhabahu yake katika Misri ambayo ni dunia hii tuliopo, na kwa wale wanaomkimbilia ataenda kuwaponya na kuwarejea lakini ninachokifundisha hapa ni madhabahu; nina Imani wote mnaelewa kuwa hakuna jambo lolote ambalo linafanyaka bila Madhabahu, kwasababu MUNGU mwenyewe ana madhabahu na shetani ana yakwake, mambo ya kiroho yanahitaji madhababu, usifikiri kila kitu ni roho Mtakatifu, hata kiroho pia kuna mambo ya giza na jinsi unavyoishi wewe kuna nguvu inayofanya kazi na wewe, nguvu inayokusaidia, yawezekana ya MUNGU, majini, mapepo au ukoo uliotokea, au nguvu nyinginezo, mnanielewa? Ukisikia Neno madhabahu sio zote za MUNGU maana hata kipindi cha Elia, Elia alikuwa na madhabahu ya MUNGU, majibu waliyapata; lakini Baali alikuwa akiomba pia kwenye madhabahu yake ambayo haikuwa na MUNGU na hawakujibiwa maombi yao, BWANA YESU asifiwe, amini majibu yako yapo hapa kama vile Eliya alivyoomba mambo ambayo hakuyatazamia aliyapata, Ni haki yako na haja yako kupata majibu. Yamkini katika maisha yawezekana umezurura umekwenda huku na huku, saa nyingine umeingia kwenye madhabahu za MUNGU, zingine za mpinga Kristo zingine za miungu hivyo lazima na maisha yako yataguswa, na madhabahu husika, lakini sasa umefika kwa MUNGU na madhabahu yake lazima itagusa maisha yako yawe mema nay a Amani na furaha na mafanikio, maadui zako wataangamizwa, afya yako itaimarika , Baraka za kimwili na kiroho utaziona, lakini endapo uliabudu mahali ambapo kuna madhabahu ya shatani nazo pia zitagusa, ila kwa uharibifu, zitaharibu afya, uchumi na maisha yako maana gusa yake ni tofauti naya MUNGU, shetani atakuwekea magonjwa, nuksi, balaa na mikosi, wanaiba, wanafunga, wanachukua, vitu vyako, unabakia huna chochote wala huna thamani, tazama wale ambao walikuwa upande wa baali mdhabahu zao ziliua uchumi mpaka Imani zao wakawa wanalia mpaka kujikatakata na maumivu lakini hawakujibiwa ila Elia alikuwa katika madhabahu ya MUNGU alijibiwa kwa kiurahisi, unajua hata shetani hutoa majibu lakini hajibu kama MUNGU, ni mbaya sana kuabudu katika madhabahu ambayo haina MUNGU, kiumwili haitaitwa kuwa haina MUNGU, wataiita ya MUNGU na kwa jina la YESU ila Matendo yao hayafanani na matendo na maagizo ya MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mtumishi wa madhabahu lazima awe na conection na MUNGU, na huyo mtumishi awe ameitwa na MUNGU, sio wa kusomea au kupigiwa kura au kuteuliwa na wanadamu, na MUNGU anapoishusha madhabahu yake anashusha kwa ajili anakupenda wewe, ili maisha yako yaongezwe na pia yaongezewe nguvu na ulinzi wa MUNGU, madhabahu ndio inayokulinda wewe, ndio inayokufikisha Mbinguni, Biblia inasema unaposali ndipo maisha yako na jina lako lilipo na hata Baraka zako ndipo zinapotokea, yamkini umezunguka sehemu mbalimbali, kwa MUNGU, wachawi, waganga, mapepo, au madhabahu za aina tofauti, na umekwenda mwenyewe na unakuwa unajipeleka mwenyewe, na ulipotoa sadaka zako ndipo adui alipokukamata, adui humkamata mtu pindi anapokuwa ametoa sadaka, (Sadaka ambazo adui hutumia kama silaha ya kukupigia ni zile ambazo umetoa kwenye nyumba za ibada ambapo MUNGU haabudini katika roho ila kimwili wanasema MUNGU na pia kwa washirikina, waganga, mila vile vitu ambavyo unatoa au kupeleka ndio sadaka hizo), Watu wengi huamini kuwa, au kwa mawazo au fikra zako kila ambapo yamkini unasikia jina la YESU linatajwa wakati wa ibada au MUNGU anatajwa unadhani ni YESU au MUNGU wa Mbinguni ndio wanaabudiwa, nawe umetoa sadaka kumbe la!, hivyo sadaka hizo zinaweza kunena kwa MUNGU kama umetoa kwa MUNGU na kwa shetani kama umetoa kwa shetani kwa kujua na kutokujua, umepiga makofi, umeabudu, kumbukumbu yako inabaki au ilishabakia katika madhabahu hizo, Na umepata Neema ya kumjua YESU na umekuja kwa YESU na baada ya kuja kwa YESU kuna mambo huyaoni kumbe yako kwenye madhabahu nyingine, umeshikiliwa, maana madhabahu zile za awali bado zimebeba kumbukumbu zako, na wanaozishikilia au kutuma kutafuta kumbukumbu hizo hata kama zilikuwa zimefishwa ni majini mapepo, mizimu, waganga, unakuta hupati kazi kwa sababu ulishakwendaga na ukatoka sadaka, kutoa fedha au damu kwa mganga, umechanjwa uhai wako ukabakia kwa waganga, yawezekana hata nyota yako uliibiwa sasa ukija katika madhabahu hii ambayo MUNGU yupo inamrejeshea, inapiga adui anayeshikilia, inamnyang’anya, inakurejeshea, inampiga hata shetani na unapata Baraka na kazi.
Adui akiona amepambana na wewe na amekushindwa, anatakaga akutoe mahali ambapo MUNGU yupo, madhabahu ambayo jina na ahadi zako zipo na Baraka zako alizokupangia mwenyezi MUNGU, ili tu apate njia ya kukuteka tena ila pia utakuzungusha huko na huko ambapo jina lako haliko na hutaweza kupata Baraka, maana jina lako huko halipo huwezi kubarikiwa, (Napenda nikufundishe kuwa watu wengi huangaika na makanisa huku na huku na kule na kule, ila unajua kwa nini hawafanikiwi wala hawajibiwi? Kwa sababu wanatangatanga huku na huko na huko na huku ambapo majina yao hayapo, ndio maana huponywi, hubarikiwi huinuliwi, hatima yake wanaishia kukata tamaa na kuona kuwa MUNGU hayuko lakini kuyumbishwa huku ni mpango wa adui ili usipate vitu vyako, Mimi Hebron nakuambia MUNGU yupo hapa, kaa tulia msikilize MUNGU upate Baraka za MUNGU) Mimi hapa jina langu liko kwenye madhabahu ya YESU ni BWANA na Mwokozi wa Mataifa yote, Baraka, ulinzi na kila kitu napata hapa, sasa siwezi toka hapa nikaenda madhabahu nyingine nikaanza kuomba MUNGU na biblia inasema pale unaposali na jina lako ndipo lilipo, miaka, Neema, maisha, watoto, magari, nguo, uzima, uhai, siku zako shule, chakula, furaha yako, Amani yako, usafi wako, biashara, ufugaji, kazi, kilimo na mengineo yamkini kabla hujafika mahali hapa ulipitapita pengi kwenye madhabahu tofautitofauti, tayari umejiunganisha na huko hivyo kila ufanyacho kinakufa, unabakia kujiuliza kwa nini mbona sifanikiwi, kumbe kule wana kumbukumbu zako inakuwa hivi madhabahu fulani wakishapata conection ya chochote ambacho kitawafikishia au kuwaunganisha na wewe hichohicho watatumia kukupata au kujua ulipio hata kama upo kwa MUNGU, lakini uzuri au ukweli ni kuwa ukiwa kwa MUNGU wa kweli mambo yako na vitu vyako vinakuwa kwenye usalama ndio maana nasema madhabahu ya YESU ni BWANA leo inakwenda kuwanyang’ang’anya kila kitu, na inakuletea na inakukabidhi lakini sasa usirudi nyuma, utakuta mtu ameokoka lakini yeye akipata shida, anarudi kuangalia bao kwa mganga, mtu huyo anakuwa ameibiwa, kuna mdhabahu mbalimbali hata za chakula, hata chakula cha kwenye ndoto hutoka huko kwenye hizo madhabahu na zinapika chakula na wewe utaona kuwa unakunywa maziwa kumbe unakunywa damu, kwenye ndoto unakunywa maji kumbe ni damu, sasa kwenye ulimwengu waroho wanauwezo ya kubadilisha ukaona tofauti, nyama ya mtu ukaona unakula kuku, au nyama choma ya mbuzi, maji au maziwa ua juice, bia, pombe, kumbe kihalisia unakunywa damu ya mtu na ile damu unayokunywa kiroho au chakula cha kiroho ni madhabahu ambayo inajengwa ndani yako ambayo ni kinyume na ya MUNGU, kuna madhabahui za picha na sura, zinaweza kuchukua sura yako kiroho, kuna madhabahu ambayo inamficha adui yako anayekushambulia ndio maana mchawi halisi humwoni wanavaaga sura za watu, maana katika fomula ya kiroho ukishamwona mchawi kazi yake inakuwa imekwisha, hivyo ulimwengu wa roho humficha nae huvaa sura ya mtu mwingine ambayo sio ya yule anayekuloga, lakini ukisha mwona yule halisi anayekuloga mabaya aliyopanga kwako hayatafanikiwa, hivyo huwa wanakupumbaza uone mwingine ndio mbaya kumbe la, mtu wa karibu au mwingine kabisa ndio adui yako sasa unakuta mtu anahangaika, analaumu na kuona wengine wabaya kumbe mchawi yuko kando tena atajidai rafiki yako wa karibu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mimi nimepata Neema ya kuyatambua na kujua hata ambaye anajibadilisha, ila yamkini wewe neema hiyo huna au hata ungelikuwa nayo usingelikuwa na subira ungeenda kugombana na mtu wakati vita vyetu si katika damu na nyama. Vingine acha MUNGU asikuonyeshe maana roho yako haiwezi kubeba, ziko madhabahu mbalimbali uliomba yamkini upate mke/mme sasa umeomba kila mahali na ukatoa na sadaka na kumbukumbu zako zipo pengine sasa umekuja kwa MUNGU na shetani naye anakutafuta na setilite zake ni zile sadaka ambazo umetoa kule, hupati aliyesahihi wa MUNGU na ukikaribia au ukipata ni matatizo mpaka unaona ndoa ni mbaya. Sasa umefika kwa MUNGU umepata mke/mume na Neno linasema ndoa na isheshimiwe na watu wote sasa hata na ninyi ambao mpo kwenye ndoa mnyenyekeane, msaidiane, mpendane, upendo ni lazima kuna baadhi ya wanandoa ambao akipingwa busu ma mwenzake anashangaa, Watu wengi huwaita wake zao Mama (mother) au Baba (father) huyo mke/ mume alikutana na wazazi wako akakuzaa? Je amekuzaa? Na kwa nini usimwite mume wangu au mke wangu? Kwa nini usimwite my wife au husbad, my fiancé kwa nini mchumba wako unamwita demu? Mwambie mke wako akuite mume na mwambie mume wako akuite mke wangu.. Hivi mke unamwita mama ulinyonya kwake? Ila hata hivyo sio ajabu wako wanaonyonya, MUNGU atusaidie, aturehemu, ndio maana inafika mahali unamwombea mke wako sasa badala ya kusema MUNGU mbariki, mbadilishe mke wangu unasema mbariki mbadilishe mama yangu, MUNGU atambadilisha na kumbariki mama yako mzazi sio mke wako kwa sababu mke wako sio mama yako, na kwa mume vile vile unapenda mume wako abarikiwe unamwombea, sasa badala ya kusema MUNGU naomba umbariki mume wangu wewe unasema mbariki na umbadilishe baba yangu hivyo Baraka hizo zitaenda kwa baba yako mzazi nasio mume wako, ni bora muitane kwa majina yenu, MUNGU ni wa haki shetani anakuwa anakushitaki hivyo baraka hizo zitaenda kwa yule ambaye kinywa chako kinamtaja, Katika ulimwengu waroho unachokiomba ndicho hichihicho kitakuwa chako, unachokitamka ndicho kinakuwa hicho, kila unachokiomba katika ulimwengu waroho wanakisiakia, Malaika na MUNGU na Roho mtakatifu wanakisikia ila huyu mmbea shetani anakaa hapo kando kukusikiliza na ukiomba kinyume au ukikosea anakushtaki anamwambia MUNGU amesema baba na sio mume amesema mama na sio mke hivyo Baraka hutaziona zitachelewa au zitaenda kwa wazazi na sio mume wala mke. Mwombe MUNGU ambariki mke au mume wako, ndio maana hata wanandoa baadhi hawawezi kushirikiana katika ndio, au kutembea pamoja na mambo mengineyo yanashindika katika ndoa, utasikia tangua huko maana mtu ameshamfanya mwenzake mama au baba kwa maneno ya kinywa hivyo hatadhubutu kumshika mkono, au kumkumbatia maana kichwa kimeumbwa na katika ulimwengu waroho mke ulimfanya mama na mume baba, sasa kuna mambo ambayo hutakaa uweze kuyafanya katika ndoa maana ni mambo ambayo ukifanya unakuwa umemfanyia baba au mama mzazi, maana uliyaumba wewe kwa kinywa chako, na usiseme MUNGU mguse demu wangu, ni maombi mabaya; ukitaka MUNGU akubariki mwite mume au mke. Kuwaombea wazazi wetu ni vyema na yatupasa kuwaombea sana, ila hapa nilikuwa nawafundisha jinsiambavyo shetani amewateka wanadamu hasa katika ndoa na akachukua Baraka, uthamani maisha ya wanandoa kwa kujua na kutokujua, unamwita mke mama mume baba kweli ni sahihi? Ndio maagizo ya MUNGU hayo? Funguka! Madhabahu ya YESU inarejesha fahamu na akili kwa yale yote ambayo yalikuwa yamepote, Baba wa kiroho unamwita baba ni sawa, Jiulize! Je! Kwa nini YESU alivyozaliwa alipelekwa madhabahuni? Ni ili ile madhabahu imbariki, imlinde, imkuze na imfunike, mnaelewa? Lakini sasa zimekuja madhabahu za aina nyingine unabarikiwa ukiwa mtu mzima na unajua mema na mabaya, unafanyiwa na sherehe na mziki ya kidunia, na pombe hivyo basi unakuwa unapokelewa na madhabahu za pombe na sio za utakatifu.
Hata mchumba akitaka kukuoa au ukitaka kuoa ukimwita mama au baba hatakuoa maana kiroho anakuwa baba au mama yako na hata mkiona mtachukuliana kama baba na mama na sio mume na mke. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Penda sana kukaa katika madhabahu ya MUNGU na kumpenda MUNGU unaweza ukawa unampenda MUNGU lakini madhabahu hizo haziko kwa MUNGU na wala hawampendi MUNGU na wakikushinda watakazana na watakutoa kwa YESU ukitoka wanakuchana na kukutesa sana, angalia Elia yeye alikuwa anampenda MUNGU na MUNGU alikuwa na Elia na hata wale mabaali walikuwa wanampenda MUNGU na walijua wako na MUNGU, wanaompenda, kumbe walikuwa kwenye madhabahu ambayo haikuwa na MUNGU kilichowapata ni kifo, kuna madhabahu za hirizi, za ndoa mke/mme kwa mganga, umekuja kwa MUNGU sawa ila bado hujafunguliwa ili utolewe kule ambapo ulikuwa umefungwa au kujipeleka ukafungwa kama uko huku na kule wote wanauhalali, ukiwa vuguvugu shetani atachua nafasi hiyo kukupata, mimi nashangaa sana wanawa Israel waliteswa na madhabahu ya farao MUNGU akashusha madhabahu kupitia mtumishi wake Musa, Musa akawaambia twendeni, hawakuacha hata kitu kimoja, wewe kiroho umeacha vingapi? Kiroho huwezi kujua ni MUNGU na Roho Mtakatifu ndio anajua na mangapi yameibiwa na ni mangapi umeyaacha, SEMA: BWANA YESU kaniguse, iwe ni madhabahu ya maagano ya kila namna sitakI! Sitaki! nataka kuwa huruuu, unaweza kujikuta huwezi kabisa utakatifu kwa sababu ulipita kwenye madhabahu ambazo sio takatifu, Mbinguni kinachokupeleka ni Utakatifu, Ni kwa neema tu, Mbinguni kinacho kupeleka ni madhabahu na madhabahu inayokupeleka ni ile ambayo MUNGU ameiweka ndani ya watumishi wake ambao anawajua, aliowaita, nakuwatuma hapa duniani, na kama mtumishi amemwacha MUNGU ile madhabahu inaondokaga na mtumishi anabakia mtumishi jina, umenielewa madhabahu ya MUNGU inaponya bure, haichangishi, madhabahu zote ambazo zinadai pesa hata awe mtumishi wa cheo gani, huyo hatambuliwi na MUNGU na madhabahu hiyo haina MUNGU, asilimia kubwa ya watu wanaonena kwa lugha ni waongo japo kuna kunena ya MUNGU, biblia inasema usilielie, kanisani watu wanalialia tu utafikiri wamejazwa nguvu za MUNGU kumbe wana uchungu, ametelekezwa, ameachwa, hawana kazi, chakula na mambo kama hayo, badala ya kujaa upako wa furaha wa MUNGU umejaa uchungu na majonzi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Atakuja na mawingu, madhabahu ndio itamshusha, hata Elia alivyopaa ni madhabahu ya MUNGU ilimpandisha, kule Mbinguni wanasali, wanainama, wanainuka, wanasema MUNGU wastahili, wastahili, mdhabahu inaumba, vitu vyote vimeubwa kutokana na madhabahu ya Mbinguni, umepata Neema ya kumtumikia MUNGU unakuwa umepewa Neema kidogo na watumishi hawafanani hata kutenda kazi kwao, kama wewe ulivyo hata nywele zako zikipimwa hazifanani idadi yake na za mwingine, Madhabahu hii, ya YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, imekuja kwa ajili ya dunia nzima na hakuna madhabahu ambayo inaweza kushindana na madhahabu hii ya YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Madhabahu hii ni ya dunia nzima, wale ambao waliamua kumtumikia shetani au wenye madhabahu za shetani wamebakia na wivu sisi tunasongambele tunaenda Mbinguni tunamwinua MUNGU na mahali aliposhuka mtumishi wa MUNGU na madhabahu ya MUNGU ipo pale, Je! umepita makanisa mangapi? Mikutano mingapi? Leo Umepata Neema ya MUNGU kubali sasa ufanyiwe operation, lakini inastaajabisha kwa wewe ambaye umekubali kumpokea YESU na kwenda Mbinguni halafu unaka kanisani, baadae kwa mganga na unarudi tena kwenye dhambi, ukifanya hivyo ujue umeshafutwa jina lako latika kitabu cha cha uzima wa milele, tubu sasa, acha dhambi, watu wengi hawamtaki MUNGU, unajua kama uko kanisani na hujaokoka ina maana humtaki MUNGU na hutaenda Mbinguni na wewe unapookoka unakuwa umemwasi shetani ila watu wengi hawapendi kumwasi shetani, wanapenda kumwasi MUNGU sasa kwa cheo chako omba rehema, rejea, okoka, mrejee MUNGU umuasi shetani, usipinge, acha ubishi, okoka uende mtoni ukabatizwe, watu wengi wamedanganywa na madhabahu nyingi huwaongezea wanadamu upako wakulewa, uongo na kufanya dhambi Zaidi, upako wa kuwa na mioyo migumu, hata aliyewaumba hawamsikilizi lakini shetani ambaye wanaenda kuchomwa nae moto wanamsikiliza hata wewe ni kwa Neema umeokolewa linda sana /ulichonacho na angalia ni wapi unaenda kuabudu, maana kama mtunishi ni mchafu na mwenye dhambi akikuwekea mkono nawe utanajisika na kumbuka kuwa madhabahu ya shetani ni kuzimu na hapa duniani lakini madhabahu ya MUNGU inafanya kazi Mbinguni, duniani na kuzimu na madhabahu ya MUNGU invunjavunja ya shetani, nay a shetani haipandi Mbinguni. Jina lako lipo wapi? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org Anayekupenda hukuambia ukweli, YESU alisema ukweli, mambo ya MUNGU ni ya kweli. Ubatizo wa kikombe ni batili hautoki Mbinguni ukibatizwa hivyo utachomwa moto, hata wanzilishi wa ubatizo wa kikombe hawakutoka Mbinguni, ndio maana waliweza kubadilisha Neno la MUNGU wangelikuwa wametumwa na MUNGU asingelibadilisha Neno la MUNGU ndio maana watu wanaendelea kumwasi na baadhi yao hawaqamini kuwa MUNGU yupo, wako ambao wanakwenda kukuombea ili uharibikiwe na usifikie kusudi la MUNGU, hata mimi huwa wananitolea sadaka kwa miunge na kunishitaki kwa shetani ili nishindwe, ninuke, nisifanye kazi ya MUNGU lakini hazijajiju na hawataweza kwasababu nimemkubali YESU, nimepata Neema na nina ulinzi wa MUNGU hivyo basi hata wewe ukimkubali YESU hawatakuweza. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Ukiwa umeokoka na Wachawi wakishindwa kukuloga hawasemi una MUNGU ila watasema ni wachawi zaidi yao, yasikubabaishe hata YESU walimuita mchawi ni maneno ya aliyeshindwa, ukitaka ushindi jambo ni lile lile kuomba, usichoke katika kuomba, Ila usiombe vibaya, kuomba vibaya ni kuomba mapenzi yako yatimie na sio ya MUNGU, omba mapenzi ya MUNGU yatimie kwako kama vile ambavyo MUNGU alitaka uwe na ukiwa katika madhabahu ya giza hutajibiwa, Neno linasema tokeni katikati yao mkatengwe nao na MUNGU atawarejeshea vitu vyenu mnavyovijua na msivyovijua, unaweza ukabadilishiwa miaka ndio maana watu wengi wanakufa kabla ya kuona Baraka za MUNGU madhabahu zinajua kuwa unaishi mda gani ila haijui siku ambayo unakata roho maana zina mwongozo wa maisha yako kuwa umeletwa kwa kusudi fulani na baaada ya hapo unarejea kwa baba ila wanakuchukua, wanakubadilishia vitu vyako kwa kujua na kutokujua hutakaa ufanikiwe unaishia kwenye taabu tu hadi siku ya kufa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
MUNGU naweza akawa na mpango mzuri na wewe lakini huenda ukawa unampinga MUNGU, na MUNGU hapendi kubishiwa tazama ameumba mlima Kilimanjaro mlima umetulia tu, amekuumba wewe, kutoka katika hali ya majimaji mpaka ukawa mtu mzima, akakupa na akili ila unampinga MUNGU, ila pia shetani anawekana roho ambazo ni mlango ili uendeleekumbishia MUNGU na kukaidi kusudi la MUNGU unatoa kafara mbaya kwa shetani, rejea sasa, Ni kipindi cha Neema, na kwa YESU kuna Neema, usimpinge MUNGU. Kuna madhabahu za kutoa vyeo na yamkini kuna wafuasi wa shetani ambao walishapata vyeo ili ombi lao lijibu kwa kabisa yawapasa wakuuwe ndio maana wanatoa kafara za wanadamu, lakini ukiwa na ulinzi wa madhabahu ya YESU hutakufa, ukiona unapata shida kimbilia kwenye madhabahau ya MUNGU utakombolewa, na wakati ukiwa umeokolewa na YESU utasikia watesi wako wako hoi, wamefilisika, wameshindwa, hawana kitu, sasa cha kufanya wewe kazana na ng’ang’ana na MUNGU ili upate ulinzi na mafanikio Zaidi ili adui avune aibu. Hata akitukanwa Mchungaji wako ambaye amekutoa kwa miungu,maneno mabaya, machafu na hata kama unasikia wewe usisikilize hayo kwa vile unajua ni wapi MUNGU amekutoa na unatukanwa kwa ajili ya ukombozi wako na wa wengine na kwa ajili ya Neema ambayo MUNGU amekupa kupitia mtumishi wake huyo wewe ng’ang’ana tu na MUNGU isisikilize hayo, Kuna madhabahu za kuogeshwa, yamkini unashuka kwenye gari ya dhamani halafu unaambiwa kaa chini yamkini ni chini ya mti, au porini kwenye jiwe, unatandikwa na mkia wa mnyama na umetulia tuli, unasikilizia maumivu na unaambiwa usilie, nab ado utachanjwa unavumilia tu, hiyo ni madhabahu ambayo imejengwa ndani yako na ni mbaya sana, kuna madhabahu ya ajali, kuna mahali nilipita wao walikuwa wametegesha ajali ili waibe vitu vya watu yaani gari ikipinduka, lakini watu wasife, ila tu lipinduke wao wachukue vitu na kuondoka navyo, na kweli kwa sababu ni madhabahu huwa magari yanapinduka, zipo madhabahu za chakula, vyakula vingi sivyo, kuna madhabahu zinapumua makufuru, unakuwa na ufahamu wako lakini unaona kuwa hauko sawa upo upo tu, kwa nini mtu anaenda kwa mganga anamwambia nataka kufanikiwa sana, mganga hana akili za kumpa mwanadamu ila anachofanya anaenda kwenye madhabahu wanaangalia ni nani ana akili na mahali gani kumekaa vibaya anaangalia je! Kuna ulinzi wa MUNGU? Kama hakuna ulinzi wa MUNGU wanaiba chap wanamletea yule ambaye ameenda kumwomba mganga na yule aliyeibiwa akili unakuwa hana akili, unawekewa ya kitu kingine ndio sasa unaona baadae mbona Fulani mtu amebadilika hakuwa hivi, mtoto huyu hakuwa amekuwa mjinga, mume huyu amebadilika, mke amekuwa kituko, Wachawi ni wabaya sana, uchawi unafanya maendeleo yasiwepo kwa wachawi hakunaga maendeleo, wachawi wameharibu, unataka kufanya biashara unaambiwa nenda kawaone wazee wa mji, Napenda nikupe ushuhuda, wakati nilipoanza kufungua kanisa la Arusha, baadhi ya wahubiri wakubwa wakaniambia kuwa nenda kawaone wazee wa Mji, sasa mimi Hebroni nilipewa maagizo na MUNGU halafu ningeendaje kuwaona wazee wa mji, sikufanya hivyi nilikataa, kabisa na sikwenda. Nikawaza nafsini mwangu, mzee wa mji ni mchawi na mzee wa mji ni mpinzani wa MUNGU sasa mzee wa mji anaweza kuniongoza mambo ya MUNGU ilihali na yeye ni mpinzani wa MUNGU? Nakatafakari, Je! Shetani na MUNGU wanaweza kuketi meza moja? Hapana! Kwa vile niliitwa na MUNGU sikwenda kwa hao wazee na nikaanza kazi ya MUNGU na mpaka sasa naendelea kwa sababu kanisa hili ni la MUNGU na ni kwa ajili ya Mataifa yote nami nitakwenda hata pasipofikika na nitafika kwa sababu ni kazi ya MUNGU mwenyewe, Haleluya! Na wengine wanasema huyu Hebroni aishie, aende Ulaya huko, na hata nikienda nina watoto wa kiroho ambao pia wameitwa na MUNGU na hata Iweje nitakuwa nakaa mda mfupi na kurejea Tanzania, Wafuasi wa shetani wanaogopa madhabahu ya moto wa Mbinguni kwa sababu wakija na moto wao unazimika. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Shetani aachie watoto wa MUNGU waachie watoto wa MUNGU, Kwa mamlaka ya Jina la YESU madhabahu zote ambazo ni kinyume na mpango wa MUNGU zibomoke, kwa jina la YESU, Je! ulisha fika mahali ukasema nimekata tamaa, siwezi? Yamkini unaona aibu kusema kweli ya jambo ambalo ulifanya ili ufunguliwe lakini hata ukifundishwa usipende kuona aibu jiachilie kwa MUNGU fungua moyo wako, Mficha ugonjwa kifo humfichua, watu huwaza mioyoni mwao nikiwa muwazi watanionaje au itakuaje, kila mtu ana changamoto na majaribu yake jiachie kwa MUNGU na MUNGU atafanya, Usiionee aibu injili na usione aibu kwa ajili eti mwingine anakuona katika kusema na kutangaza kweli ya MUNGU, Mwambie MUNGU ninakushukuru umeniona, unajua kwa nini watu wengi hawanyanyuliwi na MUNGU? kwa sababu hawapendi kuona kuwa wana shida mwambie MUNGU akuchunguze na hata kama sadaka zako unaziona kuwa ziko sawa mwambie MUNGU nakuomba uzipokee, na mapenzi yako yatimie usijihesabie haki, mwingine anasema MUNGU mimi sikosi kanisani mwaka mzima, nafanya kazi yako kwa bidii , unamwomba MUNGU kwa Matambo? Unasogea mbele za MUNGU kwa matambo ya madhabahu ya sifa na kujiinua ya shetani? yamkini ulikuwa unamatambo ya kutoka mbele na kwa vile una pesa nyingi unataka wengi wakujue kuwa una pesa hivyo unataka uambiwe toa ahadi mbele za watu, napenda nikufundishe kuwa kila anayefanya hivyo thawabu yake imebakia kwa wanadamu, na hapa kwa vile ni kwa MUNGU hiyo tabia au huo mfumo wa kutoa sadaka kwa namna hiyo haupo. Sadaka za kutajwa kiasi, kuandikwa majina, harambee zinapelekwa kwa shetani kwa sababu ni matangazo, thawabu zimebakia kwa wanadamu na MUNGU hakuagiza hivyo basi mnakuwa mmemkufuru MUNGU, Kumpenda mwenzako, kuamka kuomba, kufunga, kuhubiri, upendo, mama bora mke bora mama bora zote hizo ni sadaka, kutenda wema, zote hizo ni sadaka, kusaidia wajane na yatima, kutazama wagonjwa, kusaidia watu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Biblia inasema mkatengwe nao, kataa madhabahu ambayo inakataa watu kuokoka, huwezi kusema unaenda Mbinguni na ukakaa mahali ambapo sipo kwa MUNGU, jina lako lipo Mbinguni na maisha yako yapo mahali ambapo MUNGU yupo, usikubali kutolewa hapo ambapo MUNGU yupo, wengine hutaka kukutoa kwenye madhabahu ambayo mchungaji ana MUNGU na kukupeleka kwenye mahali ambapo mchungaji hana MUNGU, usitoke kwenye MUNGU. Ni bora ukiwa upo kwa shetani utoke ukimbilie kwa MUNGU lakini sio umeshaujua ukweli na ukaamua kumfuata shetani na kumwacha MUNGU, utaharibikiwa. Nyumba ambayo hujaizoea huwezi kaa na huwezi imba nyimbo za BWANA ukiwa huko, kimwili utaimba lakini kiroho hutaweza. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Popote ulipo madhabahu ndio inakulinda. Baadhi ya wachungaji husema tunakula madhabahuni ni sawa, lakini cha kustaajabisha baadhi yao hawawezi kuwa hata na Bustani ya Mboga yaani kazi ya mikono yao maana Madhabahu ni kazi ya mikono ya MUNGU, sasa kama huna kazi yako MUNGU atashusha Baraka wapi? Haleluya! Ulokole! Ulokele ni Roho ambayo umefanya watu wazidi kuwa wavivu, kusudi la MUNGU ni ubarikiwe ukiwa hapa duniani na Mbinguni. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
MUNGU anakuangali wewe Je! Ni madhabahu gani imekutesa? Wewe hujui ila MUNGU anajua zipo za Mizimu, miungu, shetani za uasi, uganga, ushirikina maagano, dhambi, kila ambaye hajaokoka amemwasi MUNGU nini kinakufanya usiokoke? Kama hujaokoka ina maana shetani ndio rafiki yako? Kwanini usimpokee MWOKOZI YESU? MWOKOZI YESU anarudi, anakupenda njoo akuokoe uwe huru, ukiona vita ujue ziko madhabahu ambazo zimejengwa juu ya nchi hizo. Unajua kuna madhabahu zilizopo ndani ya Nchi, ndizo zinalinda Nchi ikiwa MUNGU yupo MUNGU anailinda ila kama Nchi imekabidhiwa kwa miungu basi miungu ndio inailinda na ndio maana watu wengi katika baadhi ya Nchi wanakufa sana kwa vita na mambo mengineyo sababu ni madhabahu. Nchini kwetu Tanzania Madhabahu ya MUNGU ya kutetea ipo ndio maana miaka ya nyuma niliwaambia Tanzania sio Masikini na itabadilika ndege zitakuwepo na mtaona maendeleo, hayo yote ni MUNGU alinieleza nami niliwaeleza kwa sababu ni Madhabau ya MUNGU basi yametimia.Tanzania ni Edeni, MUNGU anaisuka Tanzania, sasa Mtanzania awaye yote akienda kutafuta uongozi kwa waganga hatapata hata, Kwa sababu MUNGU hachangamani na hayo na Nchi hii MUNGU ndio anayeiongoza. Baadhi ya watu wamezini makaburini ili wapate watoto, sasa hao watoto wanakuwa wa madhabahu ya mizimu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Wakati nimeenda kuzimu, nilienda kiroho na sio katika mwili, YESU mwenyewe ni madhabahu, sasa yeye ni mbabe anatoa taarifa nakuja, YESU ni Zaidi, akanionyesha mpaka kiti cha shetani, akaniongoza na kunielekeza jinsi ya kufanya kazi yake na kuharibu ufalme wa shetani, aliponionyesha kuzimu alinionyesha sector mbalimbali sehemu ambazo wanatolea kafara, YESU akaniambia, “nakuonyesha sio kukufundisha tu ila ili nami nikutume ukaiharibu hizo kazi za shetani” kwasababu ili YESU afanye kazi anamtumia mwanadamu na ili shetani afanye kazi anamtumia mwanadamu. YESU akaniambia, “Hata mimi nilivyokufa Mwili wangu ilibakia pale kaburini kimwili na kiroho nilikwenda, lakini nikarudishwa nikafufufuka, akaniambia, Hebron, wewe hujafa uko mzima hivyo nakufundisha kiroho” YESU akanionyesha, angalia wachawi wanavyofanya kazi zao, angalia ule ndio uchawi wa baharini, uchawi wa ndani ya bahari, uchawi wa maji, uchawi wa anaotumia biblia, uchawi wa madhabahu ya kuwapa maaskofu vyeo, uchawi wanaopewa viongozi wa dini mbalimbali, uchawi wa kupata vyeo mbalimbali vya dini au serikali, uchawi wa kutoa kafara, kuna sehemu za kuiba maisha ya watu, kuiba nyota, kuweka madhabahu ya marais watoa kafara kubwakubwa ili kupata vyeo, nk. Baadhi ya nyumba za ibada hazina nguvu kabisa, hazina nguuvu za MUNGU zinayumbishwa, yumbishwa watu wanaenda kudanganywa, baadhi ya viongozi wa dini wakitafuta Pesa, wanawafundisha mafundisho ya wanadamu sio ya MUNGU, wanadamu wakiambiwa namtuma Mikael, Gabriel, kwa jina la YESU, wengi wanadhani ni wale wa Mbinguni ila napenda nikufundishe na kukufunulia kuwa pia yupo Michael, Gabriel, Makerubi, YESU wa kuzimu, hivyo ili kuwe na uthihirisho wa MUNGU ni lazima ujue kuwa ni madhabahu gani inayotenda kazi hapo, ya MUNGU au ya shetani, duniani kuna dhiki nyingi, lakini kaa katika haki, mpende MUNGU na utavuka kwa wepesi, unayepita pagumu na uliyevunjiaka moyo hebu simama, mwangalie MUNGU na umtegemee MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Pia madhahabu za pepo wa utambuzi unashaanga mhubiri anakuambia mambo yako A-Z, mpaka unaamini na kumbe ni pepo wa utambuzi, na Zaidi mtumishi wa madhabahu ya shetani atakuambia leta sadaka ya ukombozi au tatizo hilo ni kubwa sana bila kiasi Fulani cha fedha huwezi kupona, lakini Neno la MUNGU limesema mtumishi wangu asijiulize ulize, nami napenda ni wafundishe, hata inawezeka na kuwa unataka umtumikie MUNGU, wengine hupenda utumishi kwa ajili ya tumbo, kwa ajili ya tumbo na sio kwamba wana uchungu na kazi ya MUNGU watu kama hao MUNGU hawataki kwa sababu umekuwa umetegemea kupewa kitu na Zaidi wanakuwa kama wamenunuliwa, unampenda MUNGU ili ilipwe, ili upone, ili uwe na maisha mazuri au ili usilogwe? Ina maana huna upendo wa dhati na MUNGU, ina manaa umenunuliwa, upendo hauangalii vitu, umpende MUNGU kama alivyo nae atakupenda Zaidi. Unafikiri kazi ya MUNGU ni sehemu ya kutokea maisha? Ni sehemu ya kutajirikia Kwa kunyanyasa kondoo? Kwanini watumishi wawaegemee kondoo? Wawafanye watoto wa MUNGU ATM mashine zao? kwanini watu wasiwe kama akina Sulemain na Daudi, walimpenda MUNGU sana, na MUNGU akawabariki, wamebarikiwa sana, hata mimi na wewe tutabarikiwa mpaka tutashangaa, endapo tutampenda MUNGU. Usipende kuokoka kwa sababu wachawi wanakushambulia au magonjwa au kitu Fulani mpende MUNGU kwa kumpenda sio kwa sababu ya kitu Fulani, umeona mtu anampenda mke au mume kwa sababu ya pesa na mafanikio, siku zikiisha upendo unaisha, huo ni unafiki sio upendo. Tazama Ayubu, Ayubu alimpenda MUNGU mke wake alimdhihaki lakini Ayubu hakumsaliti MUNGU, Mke wa Lutu aligeuka kuwa chumvi, kwa sababu ya tamaa, hakuwa na thamani tena, Ibrahimu alimpenda MUNGU kweli, kweli, sio kwa unafiki na amekuwa baba wa Mataifa MUNGU anawajua walio wake anawaelewa, Kipindi cha Musa ilifika mahali wengine walikuwa hawamtaki Musa, wakajitenga nae, waliokuwa upande wa Musa yaani waliomkubali Musa walipona na wale ambao walimkataa walikuwa maana MUSA alikuwa na madhabahu ya MUNGU na ule upande mwingine hawakuwa na MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Ukiokoka, Unakuwa umemwasi shetani na umemkubali MUNGU, na hapo ndipo shetani anaanza kukufuatilia ili ukate tamaa, maana anajua ukitoka kwake na kwenda kwa MUNGU wa kweli yeye hata kupata tena, na endapo hujaokoka hatakufuatilia maana wewe ni wake hujamuasi, na shetani anajua mko njia moja mtachomwa moto pamoja, na akitaka kukuchoma nyama, kukufanya lunch yake mda wowote anaweza, hivyo ndio maana hakusumbuisumbui, maana wewe u wake. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Ukiwa umeokoka una mamlaka hata shetani akukufuata mwambie ashindwe, ateguke na avunjikevunjike, hata mimi nilipoitwa na MUNGU, nilipata vita kwenye madhabahu za ukoo, kwenye familia niliyotoka hawakutaka mtu awe mtumishi wa MUNGU wa kweli, ila ukiwa mshirikina mchawi wanakupenda, na hawatakupiga vita, Ukiwa unampenda MUNGU watakutukana na ukiokaoka utatukana, mara wanasema huyu anahubiri atauwawa huyu, lakini sikutikisika wala sikuuwawa maana niko na MUNGU, hivyo amua na MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Madhabahu za masharti, achana nazo unaweza kumwasi MUNGU hata kwa matendo yako endapo huna msimamo basi unakuwa unarandaranda. Wako ambao wana ahadi na wahubiri wa kichawi au waganga na umewekewa hofu utauwawa usipowapelekea nadhiri na ahadi zako, sasa umekuja kwa MUNGU achana nao, usiwe na hofu usiwapelekee, ng’ang’ana kwa YESU. Penda hela lakini isikutawale, mwombe MUNGU akupe Zaidi lakini uweze kuzitawala, zisikutawale, maana ukiomba kidogo hazitakutosha utazidi kuwa mhitaji, ni bora uombe za kutosha na uweze kuzitawala, na zisikutoe kwa MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Natuma damu ya YESU ikabomoe madhabahu za ukoo familia, maserafi wa mashetani na wawaachilie, mashetani wa makanisa nawaamuru wawaachie kwa damu ya YESU, naitanguliza damu ya YESU na nalipa damu ya YESU na sadaka za miunganiko yao yote, zote navunja kwa jina la YESU, madhabahu za kifo zikuachie, Baraka zao za kichawi zikuachie, nateketeza madhabahu za ukoo na family kizazi cha kwanza mapaka cha Nne Iliyoshikilia mali zenu, mpaka maisha yamekuwa machungu, naamuru kwa jina la YESE uachiliwe, mababu, mabibi, mahari, mateso magonjwa, na madhabahu zingenezo zote za shetani na majenti wake zikuachilie, MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo atakuponya na atakwenda kukuweka uwe huru katika jina la YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Baba katika jina la YESU ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, namkataa shetani na mambo yake yote na kazi zake zote, BWANA YESU, nakataa madhabahu zote za mpinga Kristo, madhabahu za mapokeo za dini, uchawi, miungu, za kumwasi MUNGU, za kutataa wokovu, na nyinginezo zote ninazojua na nisizozijua, ziniachilie kwa jina la YESU, BWANA YESU Naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, kuanzia sasa, Sitembei mimi na madhabahu za mapepo, natembea na madhabahu ya MUNGU wa MBINGUNI, Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Naamuru, Madhabahu ya kabila lako ikuachie, mume / mke ikuachie. Kwa jina la YESU, Mikosi, kuibiwa nyota, misukule, mapepo, majini, na zile zinayokusumbua, iliyoshitaki watoto wako, faraka, kwa jina lake zinaziharibu, nazibomoa ,zinazoondoa kwa jina la YESU, furaha, Amani, kicheko, Baraka za kiroho na kimwili nay ale mema yote unayostahili kutoka kwa MUNGU wa Mbinguni uyapokee sasa. Madhabahu ya COVId haitakuweza, maisha mabaya yawe mazuri, narusha moto wa Madhabahu ya YESU ni BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE utateketeze hizo madhabahu, madhabahu za miungu ziteketezwe, kuta za Yeriko na Babeli, zimeanguka, wanaoshindana na wewe madhabahu imewamaliza, tazama wanaokuja kimwili, BWANA YESU, shindana nao maan awanashindana na wewe, Elia ilijibu kwa moto itajibu na kwenu, msafishwe kwa damu ya YESU MWENYEZI MUNGU awalinde, awasafishe kwa damu ya YESU, isiwepo madhabahu yeyote inayonena juu yenu na MUNGU wa Mbinguni awalinde. Sadaka zinazonena juu yenu wanyang’anye. WAAMBIE: mizimu, majini ukoo nimewakana peupe kumbe mambo yeni ndio ya giza, nimewakana peupe mbele ya MADHABAHU YA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Madhabahu hii iwabonde, iwateketeze, kwa jina la YESU, iambie madhabahu YA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE unanijua, unanitambua, na kila mahali nitakapoenda madhabahu inaniona inanimulika, YESU nakupenda, MUNGU kupenda. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
MUNGU AWABARIKI SANA.
Imeandikwa na Nabii Hebron Wilson Kisamo.