Pages

Saturday, May 8, 2021

 

KUMTENGENEZEA MUNGU NJIA (Wapo Wakandarasi wa MUNGU na wakandarasi wa Shetani)

Baba wa Mbinguni, MUNGU uketie mahali pa juu, MUNGU wa miungu, MUNGU ambaye ni alfa na omega, MUNGU mkuu, uzidi kuinuliwa juu sana, naendelea kuomba toba na rehema  kwa ajili ya ulimwengu huu na kwa ajili ya mataifa yote, ukapate kuwaponya, na ukapate kuwabadilisha, naomba mda huu tena ukawafundishe watoto wako kwa maana unawapenda na nawaombea moyo wa kufundishika,  moyo wa kukuelewa, moyo wa kukufuata, moyo wa kukupenda na moyo wa kufika Mbinguni, najua hata mimi ni mmoja wa wale ambao umewatuma  kukutengenezea njia, lakini pia shetani nae anao wa kwake ambao amewatuma na kazi yao ni kutengeneza njia  za kuwapeleka watoto wako jehanamu wale ambao watamtii shetani, naomba ukaziteketeze na kuzibomoa njia hizo za shetani  na wale ambao wako katika njia ya shetani nakuomba uwaokoe ili wakafuate njia yako katika jina la YESU  kwa utukufu wako, Amen,  Bwana YESU asifiwe:

Somo: Mathayo 3:1-3 Luka 7:27-35

MUNGU anapenda mkumbuke kwamba kila mtu duniani ni msafiri, achana na usafiri wa duniani, msafiri wa duniani utakwenda na utarudi, msafiri wa kwenda Mbinguni unakwenda na hutarudi, MUNGU akamtuma Yohana akamtengenezee njia BWANA YESU, BWANA YESU akaja, akafuata njia zilezile na hata akaja akabatizwa na Yohana Mbatizaji,  hilo mwalijua, baadae na YESU akafuata njia, Ukisoma utaona kuwa Yohana alikuwa hanywi divai, wala  mkate, wakasema huyu ana Pepo, lakini akaja YESU yeye akawa anakula na kunywa pamoja na watu wenye dhambi wakamwita mlafi na tena waliokuwa wamamwita hivyo ni watumishi tena wanaojiita kuwa ni wa MUNGU, lakini ndani yao hawakuwa wa MUNGU kwa sababu wangelikuwa wa MUNGU wasingelimkana YESU na wangelikuwa wa MUNGU wasingelipinga na kubadilisha maagizo na Neno la MUNGU, sasa nataka nikutie MOYO, najua unasafiri na hata mimi  mwenyewe nasafari naelekea Mbinguni lakini ziko njia ambazo unatakiwa uzifuate na pia ipo ramani ya kuelekea, na  aijuae njia ya kwenda Mbinguni ni MUNGU, na anayeijua ni BWANA YESU na anayeijua ni Roho Mtakatifu. Na kuna njia iendayo Jehanam anayoijua ni Shetani, Roho mchafu  na na mapepo njia zote mbili amewekewa mwanadamu, Je! Ni njia ipi unataka uelekee na njia zote zi katika Roho,  na kuna hatari kubwa sana ya wanadamu kutokufika Mbinguni, acha nikufundishe  huwezi kutoka hapa;  Mfano: Piloti anatoka hapa anaenda Canada, lakini yeye akachukua  Ramani ya Madagasca, Je! anaweza kufika Canada?  Ndivyo na kanisa lilivyo kwa asilimia kubwa  watu wanaona kuwa ni njia ya kwenda Mbinguni lakini ni njia ya peponi, ni njia ya kwenda kwenye mashimo, BWANA YESU asifiwe, Unajua kiroho kuna makandarasi  wa barabara  ya kuelekea Mbinguni na hata mimi Hebron ni kandarasi wa kutengeneza njia yako kiroho,  Kama kuna miiba au mashimo lazima nisawazishe ndipo utaweza kupita baada ya njia kutengenezwa,  hata kipindi cha MUSA, alipokuwa Jangwani  alipewa njia,  ikifika usiku wingu linawaka moto, linatangulia, ikafika mahali walikuwa  hawawezi kupita  maana mbele kulikuwa na bahari lakini Njia ikatokea na wana wa Israel wakapita katikati ya Bahari wale ambao walikuwa hawaendi Mbinguni, na hawakuwa na Musa na walifikiria kuwa watamataliza safari ya kuvuka  kama wana wa Israel waliuwawa pale pale,  hii inamaana kuwa watu ambao wako katika ufalme wa shetani hawatakanyaga Mbinguni.

 Bwana YESU asifiwe, nasikia nikukumbushe njia; watu wanaona kuwa Neno hili ni dogo sana, unasafriri Je! Unakwenda wapi hata kama ni Kigoma lazima unakuwa na akili na nauli, ukiwa unajua kuwa utashuka vituo vingapi au utapanda magari mangapi au utauliza uliza, kwa asilimia kubwa baadhi ya makanisa hawajui njia ya kwenda Mbinguni wamebakia kuuliza uliza kuwa ni wapi? Ni wapi? Ataambiwa ni kwenye sanamu, harambee, toa sadaka kubwa mpaka ikuume, utabakia kwenye sanamu, na mapangoni, na dhawabu zako kubakia kwa wanadamu na si kwa MUNGU, na usije ukadanganywa kuwa ukifa utaenda Mbinguni wakati unaabudu sanamu, unapinga ya MUNGU, ukikata roho unaondoka kwa hiyo njia uliyonayo sasa hivi ndio direction ya kwako, ikiwa kwa waganga, mizimu, dhambi ndio njia yako halafu unataka ufike na ukakae kwa BWANA YESU? Hakunaga njia Mbili za kwenda Mbinguni njia ni moja mkandarasi wake nakueleza, BWANA YESU asifiwe, Tunaelewana? Ni mbaya sana unatamani ufike, halafu usifike,  njia hii ni katika roho, ufahamu na akaili na mafundisho unayoyafuata,  unaamini mafundisho ya miungu basi uko kwenye njia ya kuchimwa moto,  na hutaki kuokoka  halafu unataka kwenda Mbinguni? tiketi ya kwanza ya kufika Mbinguni ni wokovu lakini  utashangaa mpaka sasa unamwambia mtu okoka yeye atakuambia  mimi siokoki, kama hutaki kuokoka  na unaenda kanisani unapoteza mda wako, mimi sijali hata YESU aliitwa mlafi kwa sababu alitengeneza njia ya kweli, Yohana aliitwa anapepo kwa sababu  alitengeneza njia ya kweli sio kama walikuwa wanapendwa hata mimi sipendwi lakini nitakueleza ukweli, haikuanza kwangu, mimi nakufundisha ili shetani avune mambo yake mwenyewe, na sio akuvune wewe, tunaelewana? ni mbaya sana MUNGU  amekutuma na pia amewatuma watumishi wakutengenezee njia ya kufika Mbinguni, halafu wanakuja wengine wanakutengenezea njia ya uongo, maelekezo ya njia ya mbinguni  ni ukitoa  sadaka ni siri yako, njia ya shetani mtu akitoa sadaka mpe riziti  ujulikane ametoa ngapi,  na lazima mchungaji ajue kiwango ambacho umetoa hiyo sio njia ya Mbinguni ni kupotezwa njia, acha nikufundishe  na nibomea hizo njia za uongo ili uende Mbinguni na kuliko sadaka yako ionekane ni bora uile, uvae upendeze kuliko kuitoa halafu ikawa tanzi, mwingine anajiuliza anasema huyu Hebroni anafundisha nini? Mimi ni mkandarasi bwana ninango’a na kubomoa vya shetani ili usonge mbele,  na wengine wameingia kwa YESU na  wameshaishika njia  wako na Musa lakini  wanarudi kwenye  Kora watakufa, Dunia imeharibika YESU anarudi, YESU ananjia yake ndipo utakutana nae katika njia yake, shetani pia anamakandarasi wake Mitume,  nabii na wachungaji na watumishi wanaojiita kwa jina la MUNGU lakini sio wa MUNGU (wanajifunika mwavuli kwa kutumia jina la MUNGU) na MUNGU pia ana wakandarasi wake , Nabii, Mtume, Mwalimu, Mchungaji na Mwinjilisti.

Njia ni Mbili ya Nuru na ya Giza, Njia ya uzima imenyooka ila makadarasi wa shetani wanaweka vipingamizi (Zebra Cross, bamsi), kwenye ulimwengu waroho ili watu wasimwone MUNGU, wameongeza ongeza  mambo mengi, ubatizo wa Yohana umenyooka,  lakini shetani ameweka vipingamizi  watu wanabatizwa kwa matone kikombe, kwenye madram, watu wanatumbukizwa kwenye mapipa ya maji,  na baadhi ya watumishi wanampenda MUNGU lakini wameshaingizwa katika njia hizo za wakandarasi wa shetani kwa kujua na kutokujua, na hatima yake,  maombi yao  hayana majibu kwa MUNGU, wanaomba BABA MUNGU awakumbuke, lakini  MUNGU atawakumbukaje wakati ni makandarasi wa shetani? YESU anasema nifuate mimi, Usiabudu mizimu,  usiabudu sanamu sasa unapumbazwa unakuwa kwenye mafundisho ambayo yanakuelekeza kuwa sanamu ni kitu cha kawaida na kuwa kuna YESU kwenye sanamu, usidanganyike! Ndugu katika Kristo shetani na YESU hawachangamani, hawakaagi meza moja, siku ya leo au hata ulipomtafuta YESU wa kweli na kumpata, umemtafuta ili kuongezewa njia ya kusonga Mbele, yamkini huelewi labda umeshatembea 100,000 KM, ukimtafuta YESU au njia kamili ya kwenda Mbinguni, na ujue kuwa  kila unapokuja kanisani unaongezewa njia, Roho Mtakatifu anakufundisha na kukufunulia ni njia hizo lakini watu wengi wana shida hawapendi kufuata  hizo njia wanataka mapenzi yao, waabudu na kuamua na kutaka yale wanaohisi kuwa kwao ni sawa, wanataka wafundishwe kama watakavyo, sasa hapo tayari umeshapotea, kwa sababu hata mafarisayo walitaka YESU afundishe kama wanavyotaka  wao  na  hawakutaka yale ambayo yalitoka Mbinguni ambayo ni maagizo ya MUNGU, Yohana na YESU alikataa, waliwafundisha yale yaliokuwa maagizo ya MUNGU, na mafarisayo walimkataa Yohana na YESU ila MUNGU aliwapenda Yohana na YESU kwa sababu walimsikiliza MUNGU na sio Mafarisayo,  na mimi Hebroni sitawasikiliza Mafarisayo na Masadukayo, ninakufundisha yatokayo kwa MUNGU na wewe ambaye unanisikiliza amua twende mbele  ili tufike Mbinguni, usije ukafika  wakati wa uzee, (Wakati unatamani Neema hiyo na huipati tena)  ukachomwa moto, na hata kama unalala kanisani na kushinda kanisani na matendo yako hayaendani nay a MUNGU hutafika Mbinguni, amua sasa badilika.

 Njia ninazokufundisha na  misingi ninayokufundisha ni ili ikufikishe Mbinguni mtu atakuambia nimeshika dini ya mama yangu na baba yangu, ambayo yamkini ni ile  ya kubariki pombe, kuabudu sanamu, miungu, matambiko mizimu, mababu na mabibi, uko kwenye njia ya kuambiwa jisaidie na MUNGU atakusaidia, yamkini sasa unaenda kwa waganga na miungu kwa tiketi ya kujisaidia ili MUNGU akusaidie Mh! Umepotea na kupotezwa,  Utukufu wa MUNGU haushirikiani na mashetani, Amua! Mfuate MUNGU ana vyote, BWANA YESU asifiwe,  miili ya wanadamu  ina chale kama wanyama waliowekwa alama ili wasipotee, wanadamu wanapaa kama pepo, BWANA YESU asifiwe, kwa YESU kuna kila kitu tatizo ni njia, na njia inatakiwa ikae kwenye akili na ufahamu hakika utamwona MUNGU, na mambo yako yatakuwa safi safi,  Je njia gani unapita? Unakinyongo au Roho mbaya? unajua shetani na mapepo yanakuwa yanakufuata maana hizo sio product za Mbinguni tumepewa upendo, kusamehe, kushikamana na kuwa na tabia za MUNGU, ila kubaguana baguana, hata hapa kuna watu wanabaguanabaguana, kwa kuona wengine wana dhambi sana, na hawafai kuchangamana nao, sasa jiulize,   wewe mwenywe ulikuwa una dhambi, ukapata neema ya mtumishi au yeyote kukaa karibu nawe yaani kukuombea na ambapo ulihitaji msaada ulisaidiwa na kujibiwa maswali yako na hatimaye ukasimama katika njia ya MUNGU kama ulivyo sasa,  kama ulikuwa haujatengenezewa njia  na mtu, akakaa  karibu na wewe vizuri Je! Ungenyooka? Ungelisimama? Sasa mbona wewe ulitengenezewa njia ukaa vizuri, Leo hii unaona wengine kinyesi? Ngoja niwaambie ukweli, na hayo yapo sasa badala ya wewe kutumika kuwavusha wengine mbele unakuwa uzio (gate) la kuwakatalia wengine wasiende Mbinguni, huo ni uchoyo na ubinafsi, wakati unatengenezwa kumbuka pia ulikuwa na dhambi sasa kubali kuchukuliana na wengine ili nao waweze kufika Mbinguni, hata YESU alikaa na wenye dhambi ili wabadilike wafike Mbinguni. Kumbuka  shetani halali usingizi yuko kazini  akikuwinda na akiwinda watoto wa MUNGU na MUNGU hapendi mambo ya kuoneana, anatenda haki, Neno la MUNGU ni haki hivyo sipendi mtu amwekee au awe kwazo kwa mwingine, hivyo badilika umebadilishwa kwa Neema badilisha na wengine kwa kuwa kielele na mtetezi wa YESU ili wengi tufike Mbinguni..

 Njia ya Mbinguni imenyooka ila watu wanataka mahali ambapo mtu anaruhusiwa kuona  wake 5 ndipo aabudu mahali hapo, ni kizuizi hicho hufiki Mbinguni, Neno linasema mke mmoja ni mmoja tu njia sahihi ndio hiyo, ukimwambia mtu akabatizwe mtoni hataki ni tuta la barabara yako hilo,  Mkandarasi nakuambia ni hivi,  fuata hivi, maana  hata mimi Hebroni,  YESU ndio  ananielekeza huko mbele kuko hivi, kuko hivi, ndio maana nawaambia twendeni, ni bora  hata kama uko mbali na  yamkini kanisa lina mambo ambayo sio ya MUNGU na unajua kabisa MUNGU hayuko hapo, yaani yanayofundishwa au kuelekezwa kanisani hayafanani na ya MUNGU, ni bora ukae nyumbani ufanye ibada zako, umwombe MUNGU maana anakusikia kuliko ukasali mahali ambapo wanamkufuru MUNGU, ukisali ambapo wanamkufuru au wanampinga MUNGU kwa maana nyingine mahali ambapo Neno la MUNGU limegeuzwa njia hiyo ni ya Shetani na hutamwona MUNGU, unajinajisi,  sasa ni bora  usali na kumwabudu MUNGU wako ukiwa nyumbani ili usinajisike, wakati ukiendelea kumwomba Roho Mtakatifu akuelekeze mahali ambapo MUNGU anaabudiwa, katika Roho na kweli. Unanielewa?

Hata wakandarasi wa shetani wana barabara zao, maana wengi wana njia zao, baadhi ya makanisa yana bendera, ubatizo wa kisima, kutolewa vitu kwenye mwili (mazingaumbwe) Napenda nikufundishe jambo! Unapoombewa yamkini umefungwa mahali Fulani au kuna jambo umefanyiwa la nguvu za Giza, jambo lile hufanyika kiroho na sio kimwili, na hutolewa kiroho na sio kimwili, sasa baadhi ya makanisa hutoa watu vitu mafano: hirizi, wadudu, uchafu kwenye mwili, kweli! Inawezekana mfano: Mende akawa hai tumboni mwa mwanadamu au kipande cha nguo kwenye mwili wa mwanadamu bila mwili kuoza au mende kufa? Hayo ni mazingaumbwe, huo ni uongo! Kuweni makini! maana unachokiamini na kukifuata  kinakuchukua katika ulimwengu waroho, watasema ni elimu gani hii huyu Hebroni anatufundisha, ni elimu ya Mbinguni, ipokee na uifanyie kazi! MUNGU ndiye anayeongoza watu wake na hata watu ambao wameamua kuwa upande wa Shetani,  shetani huwaongozwa na kwa shetani mwenyewe  kuna njia  zake,  na hatima ya njia za shetani ni shida.

  Kuna njia kuu mbili ya giza na Nuru. Fahamu za watu wengi zilikuwa zimefungwa na wakakaririshwaa kuwa dhambi kuu ni uzinzi na pombe, kweli ni dhambi lakini ipo dhambi kubwa  sana ambayo ni kumkataa YESU,  kama hujaokoka unadhambi kubwa sana, kwanza unakuwa umemkufuru MUNGU kwa kujua na kutokujua, kwasababu MUNGU aliupenda ulimwengu, akamtuma  mtoto wake ili akukomboe, lakini bado hutaki na wapo makandarasi wa  shetani sasa wanakuambia hakuna kuokoka hapa duniani, na hao wakandarasi wanaosema kuwa hakuna kuokoka ni  wa mashetani il wanatumia biblia ili muone kuwa ni wa MUNGU,  ila wanafundisha kinyume na Biblia, sasa si bora watumie vitabu vingine ambavyo sio biblia? ( Ila wanatumia biblia ili wawafunge na msiujue ukweli ila ndani ya moyo wake na nafsi yake mtumishi wa namna hiyo anajijua kuwa sio wa MUNGU, ni wakala na mkandarasi wa kuiba watoto wa MUNGU na kuwapeleka kwa shetani) ukiokoka tu watu wanakuambia umechanganyikiwa, waambie  sijachanganyikiwa niko katika barabara sahihi,  wengine wanatishia utazikwa na nani na baadhi hata ukiokoka, ukadumu katika wokovu na ukafika ukomo wa kuishi hapa duniani yaani ukifa cha ajabu  watu wa dini wanang’ang’ania mwili wa marehemu, ila ni bora wang’ang’ane na mwili wakati roho yangu imeshaenda Mbinguni, maana mwili huo umekuwa gogo tu  sasa basi ni bora utengeneze na MUNGU ukiwa hai, hata waking’ang’ania mwili wako roho yako ipo salama. Wanasema wakulaze katika nyumba ya milele, Je! Kaburi ni nyumba ya milele, hata ukisoma biblia inasema baadae watafufuka  na watatoka huko, sasa anayekuambia kuwa kaburi ni nyumba yako ya milele ametoa wapi Neno hilo! Milele ya kwako itategemea mi njia ipi uliamua kuichagua tokea awali, ni jehanamu au Mbinguni? na katika njia ya Mbinguni acha kuangalia vizuizi (Vikwazo)   maana ukiokoka majaribu, makwazo, vikwazo, matusi,  utaona wanadamu, wananicheka, wananiangalia, malango ya shetani yanaongea sana  jua ni vizuizi sema  nabomoa, napita mbele, watu hawapiti kwa sababu kuna vizuizi, kwenye Injili vizuizi, kwenye sadaka vizuizi, sanamu, harambee, michango michango, kuoneana, tabaka, hivyo vyote ni vizuizi ila MUNGU  anaahadi juu ya watumishi na kazi yake na MUNGU ameagiza kuwa watumishi wake wamuulize yeye atafanya au ila sasa imekuwa ni kusumbuana hizo zimekuwa ni njia za shetani, acha niwafundishe mpone, kuna njia  yakupata utajiri kuinuliwa, upo kwenye njia ya kuinuliwa, kupata mke / mume, wewe umekaa katika kumlazimisha MUNGU ‘kaa katika njia ya kusubiri majibu ya MUNGU yawezekana ni promosheni, kaa katika kusubiri majibu ya MUNGU, lakini kama  hutaki kusubiri majibu  ya MUNGU maana unakuwa umeshaanza kutumia akili zako, na ukianza kutumia akili zako MUNGU anakaa pembeni anakuangalia, sasa kama ni kazi  utaenda  kuhonga wizarani ili upewe cheo, watu wengi hawakutani na miuzija yao kwa sababu  hofu inatangulia mbele wanawaza itakuwaje! Hawajiamini, hawajielewi hebu jielewe kuwa uko na YESU, ila pia unaweza ukakuta mtu anajua kuwa anatembea na YESU na kumbe alishamwacha YESU, YESU amebakia jina,  anapita kwenye mapito miba, uchumi unapingwa, dhiki, adha, taabu, magonjwa, umaskini na mambo kama hayo,  sasa rudi katika njia na utakuwa huru. Siku za karibuni nilikuwa napita katika barabara Fulani, nikakutana na jambo la uonevu na nikatakiwa kutoa tozo kwa kosa ambalo halikuwa langu, hivyo nikasimama katika nafasi yangu, nikamwambia mhusika kuwa ni wapi nimezidisha mwendo? Akaniambia twende nikakubali, kufika pale picha ya tukio haikuwa ya kwangu na  kwa vile sikuwa tayari kutoa fedha hizo ambazo hazikuwa halali na walivyoona nimekuwa jasiri basi wakaniachia, Bwana YESU asifiwe, nikamuuliza MUNGU ni  nini akaniambia jipe moyo ulimwenguni kunayo dhiki,  ulimwenguni mnayo taabu kweli, penda kujua  haki yako, mimi siogopi kwa sababu naijua haki yangu, na wewe ijue haki yako kwa MUNGU, lakini unaweza ukawa unatafuta haki yako lakini upo katika njia tofauti, Penda MUNGU akufanyie jambo usipende  kujitakia mwenyewe, tunaelewana?

Angalia hata kibinadamu kuna sheria ya kutengeneza barabara, na kiroho hivyo hivyo kwa hiyo hakilisha kuwa mkandarasi wako wa kiroho asiwe wa kujiita, alieachwa na MUNGU au wa kujitengeneza,  sio wa uchawi, au madawa, pia ujue kuwa  kuna miujiza ya ajabu, ajabu; miuziza  ya MUNGU ni katika roho lakini ya wakandarasi wa shetani ndio ile ya kutolewa, wembe, mawe na vitu kama hivyo kwenye mwili! Hebu tafakari! Wembe! Mawe! Mambo mengine yanasikitisha jamani, Hao ni wachawi na watu wengi ndio wanapenda miujiza ya aina hiyo ila hayo yameruhusiwa MUNGU anapambana na shetani anapambani.

Sema mimi ni msafiri, na ujue kuwa wewe ni msafiri, kuna wakati wakufa unakuwa umesafiri kivingine, wamesafiri wangapi? Wengi wamesafiri wameenda wapi? Waliokufa wameenda wapi?  Hiyo ni siri ya msafiri, angalia usije katiwa tiketi feki… ambayo sio ya Mbinguni, angalia usije ukaambiwa mwizi wewe, angalia  usidanganywe kuwa kuna tiketi za kimwili za kwenda Mbinguni, hiyo ni feki,   tiketi ya Mbinguni ni katika Roho. Watumishi hawapendi kuambiwa ukweli hasa wale wa kipepo, na ilianza toka awali kwa YESU na akina Yohana, kulikuwa na mahojiano kati ya YESU na Mafarisayo! YESU aliwauliza kuwa ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Wakasemezana wao kwa wao, walikuwa wanajua ukweli wakatakaa kusema ukweli kwa sababu walikuwa wanampinga MUNGU, japo ukweli waliujua, wakasemazana wao kwa wao, Wakasema hatujui na YESU akasema na mimi siwaambii.

 Kuna Baraka kukifuata yale ambayo MUNGU amekupangia na utayapata, simama wewe kama wewe unaweza ukadhani kuwa mwenzako yuko na wewe kumbe la. Ulizaliwa mwenyewe utakufa mwenyewe na utanyakuliwa mwenyewe, hamtakumbatiwa wawili  au  watatu, usiangalie maisha haya tunayo taabu  lakini usikate tamaa.

Unajua hata kanisani kuna wazuri na wabaya na katika uongozi wowote kuna wazuri na wabaya. Hata nilipoanza huduma walisema atakufa, ila mimi niko katika njia ya MUNGU kuna trafiki na kamanda, ukiwa na MUNGU hata ukitajwa jina kwenye ramli haikuwezi, nataka wanaokuloga wasiweze, biblia inasema watapigana nawe lakini hawatakuweza, ila kama umekaa nje ya barabara ya YESU watakuweza, mafano: natakiwa uende Msumbiji, ndege ina ramani ya kwenda Msumbiji unaenda Siria, Je! utapata wenyeji wa kukupokea?  Siku ya Mwisho pia unaeza jikuta uko kwenye mikono ya shetani unakutana na jitu la ajabu ila wale wa Mbinguni watakutana na YESU wanakuwa katika mikono salama, wanakumbatiwa, wanapigwa busu takatifu, cha kustaajabisha huku duniani hata sasa mtu akikupiga Busu unahisi au kudhani kuwa ni uzinzi hapana, hivi watoto wanavyobusu ni wazinzi? Wengine hata mke au mume hawawezi kuwabusu, Busu takatifu unapokelewa unafika wanakukumbatia, wanakuhug, ukienda kwa Waebrania unakuwa kama wao,   lakini yale mabaya usiyafuate, sisi ni wasafiri kiroho wengine wanapanda na wengine washuka na wengine wakishagundua kuwa  wanakaribia kushuka wanarudi tena kutafuta njia, sasa wewe usishuke tena,  maana ukishuka utakutana na majaribu mengi, tozo nyingi na mambo mabaya kama hayo ya shetani,  nuksi, balaa na mikosi, ujinga, magonjwa, na hatimaye Jehanamu.

Jinsi ulivyo ni kipimo chako cha kuwa unapita njia ipi, kila kitu shetani alinakili) (copy na paste) wengine wataanza  kuchimba njia chini,  ila mimi nataka uone njia  yako na ndoto zako uzifikie,  ndoto haziwezi kutimia wakati unakuwa kwenye ufalme wa shetani,  matambiko, uchawi na mambo kama hayo, wengi wanakutoa katika ufalme wa MUNGU, vibaka wanakupiga tero, maana wanaona vitu vyako kwenye ulimwengu wa Roho na vyote ulivyonavyo wanavichukua kwa sababu havina ulinzi,  linda sana ulivyonavyo,  kaa kwa YESU ilivitu vyako visiibiwe, watu wengi wanapotea, anajiona wana akili, unabusu mbao?  Hebu fuata njia sahihi, ambayo YESU  amenituma nikuongoze na Zaidi nimtengenezee njia, yeye amenituma sio kwamagreda na makatapila ni kiroho twende mbele, twende, twende tutafika, unaweza kukuta  bamsi / jaribu la kiroho mambo yako yakaharibika, unaweza ukawa unapoteza kumbukumbu,  tembea kwa YESU, Biblia inasema hata mtumishi wangu akiangua nitanyanyua.

 YESU anarudi eti, wako malaika wanajua njia zako, wanajua kila jambo ambalo shetani na mawakala wake wameliandaa, wameliandaa jema au baya, hivyo ukiona mabaya warudishie wao (Shetani na mawakala wake)   waambie kuwa unapita katika njia yako. Shetani anafanya vitu vya ajabu sana, sasa lazima muwe na mbinu na ujue kuwa nani amekaa kwenye njia yako, ubatizo wa watoto wadogo ni kubadilishiwwa njia, Masomo ya kandarasi wa Mbinguni ni tofauti na masomo ya kandarasi wa Kuzimu,   Ubatizo wa Mkandarasi wa Mbinguni ni mpaka mtu amkubali YESU lakini ubatizo wa mkandarasi wa Shetani ni kubatiza watoto wadogo. Kisicho na fomula hubomolewa hivyo tunawabomoa wakandarasi wa shetani ni kipindi cha Neema hichi, watu aje kwa YESU tusonge mbele, mwenye kuelewa na aelewwe pendeni kujua mambo ya rohoni sana, Sio kwa kunena, eti mtumishi anakuambia sema YESU, YESU YESU YESU, Harakaharaka mpaka mwisho utanena sasa ukisema hivyo mwishowe utaishia kusema  maneno ambayo siyo ua kugandamizwa macho eti uone maono au unawashwa kibao,  ili unene au ushukiwe na Roho mtakatifu nani ameleta hayo?,  hapo umeliwa, umepotezwa njia ya Roho Mtakatifu unafunga na kuomba na kuutafuta uso wa MUNGU yeye atakushukia mwenyewe. Biblia zingine zina vitabu kibao. Neno la MUNGU haliongezwi wala halipunguzwi, shetani huwawekea wanadamu mioyo ili wasiende Mbinguni, huwahubiria kuwa wasiokoke na Zaidi kuwaambia hakuna wokivu duniani, hivyo mtu hujivuta sana anafikiria sana, anawaza jinsi ya kuacha dhambi hawezi, lakini MUNGU akikutaka utaacha dunia na utaenda kwenye njia ya MUNGU.

Sala ya toba: Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua na kwa kutokujua,  naomba uandike jina langu katika kitabu cha uzima wa milele, ambapo kuna njia  yako ile ya uzima naomba utoe jina langu na vitu vyangu vyote ambavyo viliiibiwa kwa kujua na kutikujua pale ambapo nilipokuwa nimetembea katika njia ya wakandarasi wa ibilisi nikachomwa na miiba nikafilisikia huko nikapaukia huko, kikakata tamaa na  nimekuwa nikiendele katika kutaa katika njia hizo na siku kuona YESU nimetambua kupitia mjumbe wako Hebroni,  Nabii wako sasa ninatembea kwenye njia unayoitaka wewe, akinitangulia  kama Musa, hakika sitachomwa na miiba nitakula mema ya Nchi siku zote za maisha yangu, nikiwa hai na hata nikifa na wale malaika watanijua kuwa mimi na wakwako YESU, ninaomba BABA  MUNGU na tunawaombea watu wengine, wafunguke wafuate njia yako waachane na vizuizi ambavyo vimeongezwa ili kumpindua MUNGU, kumfananisha MUNGU  na sanamu ikiwa ni kumkufuru kwa kujua na kutiokujua BABA MUNGU nakuomba uwafungue, maana hakika wamepotea lakini kwa mawazo yao wanaona hawajapotea, akili zao zimepumbazwa na wanaona kwamba kwenda mbinguni ni kupotea na wao wanaona kwenda kwa shetani na kuchomwa moto ndio  wako sahihi BABA MUNGU  ninaomba uwafungue wapate kujua ukweli na ninaharibu  mipango yote ya shetani kwa  jina la YESU.

Ninaharibu njia za giza, za ibilisi, mpinga kristo, katika jina la YESU wako wanaoongozwa na watumishi wa kipepo, watumishi wanadamu ambao wanajiita MUNGU au YESU wakati wao ni wanadamu, BABA katika jina la YESU nawatenanga na laana na mikosi na mizimu na njia za matambiko na wale ambao wanaenda kwa waganga na wachawi ili wakupate waambie hamtanipata, ninajifunika kwa damu ya YESU,  naninajikabidhi mikononi mwako BWANA YESU  siku zote za maisha yangu. Amen.

MUNGU AWABARIKI, MUNGU awainue, MUNGU awafanyie wepesi katika njia zake zote sasa na hata milele. Amen.