Pages

Friday, April 23, 2021

 KUHARIBU MALANGO YA SADAKA ZA MALAIKA WA SHETANI

Baba Nakushukuru kwa  muda huu, asante kwa yote asante kwa Neno lako, asante kwa majeshi yako  ambao ni malaika wako wanaokutii na kunyenyekea, Eee MUNGU nakushukuru, ninasema asante, asante, nakushukuru sana mfalme, nakushukuru roho Mtakatifu, nakushukuru BWANA YESU, naendelea kusogeza ibada hii  mikononi mwako katika jina la YESU Kristo wa Nazareti.

          Twende juu Sayuni, tulitoka Sayuni tukaja hapa dunianiani, na siku moja tutarudi Sayuni, BWANA YESU asifiwe,  maana huko ndiko nyumbani kwetu lakini kuna ambao hawataki kurudi Sayuni na wanataka kwenda Jehanamu, hebu badilika, BWANA YESU asifiwe.

Soma: DANIEL: 10-11-14; - 12:1-3, UFUNUO 5:11-13; UFUNUO 12:7-10

Tunaenda kujifunza jambo kubwa, kwa maana imekupasa kujua, mnakwenda level nyingine na kila wakati unapofundishwa mambo mengine unakuwa Kiroho na unapanda toka hatua moja kwenda nyingine kiimani,  unazaidi kukua  katika habari ya ufalme wa MUNGU na jinsi unavyozidi kukua ndivyo ambavyo unazidi kusonga mbele zaidi, maana imekupasa kujua hata wale ambao wako upande wa shetani wanazijua sana habari za shetani na zinawasaidia sana kwa upande wao  kwenye  ufalme wa shetani na sisi tuna njia zetu za kumfuata MUNGU ambazo zinatusaidia,  ambazo zina nguvu zaidi  ya njia za shetani na kila mmoja anajua.

Sio jambo geni sana najua kila mmoja anajua habari za Malaika, Nataka niwafundishe habari za malaika wa Shetani na sio kuwa kila wakati ukisikia malaika sio wote ni wa MUNGU wapo pia malaika wa Shetani, utakumbuka shetani alivyofukuzwa Mbinguni aliondoka na jeshi la malaika ambao walimuasi MUNGU ambao ndio amewafanya kuwa malaika wake na jeshi hilo au malaika hao wapo duniani na lipo kuzimu linafanya kazi. Ukisoma neno la MUNGU linasema Malaika ni watenda kazi wa  wa MUNGU na wako Malaika wa Shetani ambao ni watenda kazi wa Shetani, BWANA YESU asifiwe, tunasoma habari  ya Daniel, juu ya maombi yake na MUNGU aliyasikiliza na kuna mambo ambayo yamkini na wewe uliyaomba kwa MUNGU na MUNGU  ameshaachia majibu na MUNGU akishaachia MUNGU anatuma Malaika na mimi sijui kama wewe unaweza ukaomba kama Daniel, Kiwango cha Subira alichopitia Daniel ili kupata majibu yake kilikuwa ni kikubwa sana, malaika wa shetani walizuia maombi yake juu, akaja Malaika wa MUNGU Michael akafanya vita ndipo Malaika Gabriel akapenya akamletea Daniel, majibu ya maombi aliyokuwa amemwomba MUNGU, Yamkini na wewe kuna kikwazo mbele yako, wako Malaika wa Shetani, watapigika, watapigwa utapata jibu lako utapata mpenyo.

Watu wengi huwa wanasema MUNGU anampango na mimi, ni kweli ila napenda nikufundishwe jambo ambalo litakusaidia katika maisha yako, MUNGU akiwa na mpango na wewe, wewe usipende au sitake  kufanya la kwako,  yaani usimpangie MUNGU ila fuata lile ambalo MUNGU amekupangia au kukuelekeza, YESU alivyoitwa  angetaka mpango wake kusudi la MUNGU lisingelitokea la yeye kufufuka na kupaa  na kwenda Mbinguni, kuna watu ambao MUNGU amesha waonyesha kuwa utakuwa mtu Fulani, utafika level Fulani utakuwa mtu Fulani, au utakuwa kiongozi, lakini haitokei, kwanini? Lakini utabakia kusema MUNGU ulishaniambia, ila napenda nikuambie jambo moja wewe  mwenyewe unaweza ukawa kikwazo cha kusababisha kusudi la MUNGVU lisitokee, unapopewa kusudi la MUNGU wewe shukuru, lipokee, usiwe kigeugeu, litatimia, lakini ukiwa na kugeugeu utabakia kusema  MUNGU uliniambia hivi, lakini yamkini wewe unataka hivi, ambavyo ni kinyume cha kila ambacho kilikuwa kusudi la MUNGU kwako, ukiwa hivyo MUNGU anakuachaga hivyo  na kusudi lake halitatiamia na wewe utakuwa unabakia na ahadi tu, watu wengi hubakia kulalamika na kumuuliza MUNGU kuwa MUNGU uliniambia hivi na hivi  na mbona havijatimia? Sasa jiulize Je Ulifuata kusudi la MUNGU au la kwako? Hata mimi MUNGU alivyoniita amenieleza mambo mengi sana na hata sasa nafuata yale ya MUNGU na MUNGU anachukia kupingwa  MUNGU anachukia  pale ambapo mwanadamu anazungusha akili yake vile ambavyo anataka, na si kama vile ambavyo MUNGU anataka, ina maana umempuuzia, kwa kujua na kutokujua, hakuna kazi ngumu  hapa dunia kama kazi ya kuhubiri ni kazi ya kuhakikisha kuwa  unarudisha mwanadamu alipotoka Sayuni, na shetani naye kazi  yake anahakikisha na yeye atakuchukua na kukupeleka kuzimu na hutaenda Mbinguni na kila mara muombee kwa MUNGU yule anayesababisha wewe  kwenda Mbinguni na wana wa Israel wangevuka bahari ya Shamu bila Musa? Haingeliwezekana, kwa sababu Musa ndiye aliyekuwa amepewa maagizo, wana wa Israel walimsikiliza Musa, walikuwa wakisikiliza maelekezo, sasa na wewe sikiliza maelekezo utafika, mimi hapa mwenyewe namsikiliza MUNGU kwa kila hatua, ukitaka kugombana na mimi wewe leta mambo ya  ajabu, ajabu kuhusu injili, nitakuangalia tu, na kukuacha, namsikiliza MUNGU,  hata katika mafundisho namsikiliza MUNGU, sisikilizi yeyote ambaye ni kinyume cha MUNGU, na wewe ukitaka kuvuka msikilize MUNGU,  unaweza ukawa unasikiliza malango ya Shetani maana yanakaaga ndani ya  Wanadamu roho za kupingapinga mambo ya MUNGU, ni malango ya shetani yasikutishetishe hayo.

Biblia inasema Malaika ni watenda kazi wa MUNGU, kama ilivyo MUNGU ana malaika wake na MUNGU anamfumo wake na shetani nae ana Malaika wake, nae amenakili (Copy) Mfumo wa MUNGU, Napenda nikufundishe kuwa Biblia inasema Maika Mikaeli ndiye Malaika mkuu, na tunasoma kuwa Malaika Gabriel alizuiliwa siku 21,  akashuka malaika  wa vita Michaeli akapigana na mkuu wa uajemi walipigana  Malaika Mikaeli akalipiga jeshi la shetani, ( Mkuu wa uajemi). Malaika wa MUNGU ana nguvu  kuliko malaika wa Shetani na kama alivyo malaika mkuu Michaeli pia kuzimu yupo malaika Michael wa kuzimu, Gabriel wa kuzimu, Raphaeli  wa kuzimu napenda ujue hivyo lakini leo nataka malaika wa MUNGU afanye kazi kwenye maisha yako, na kama wako malaika wa shetani wamekushikilia mahali wakavunjwevunjwe na ukisoma Biblia utaona malaika wa habari njema, anakwenda kumwambia Maria utabeba mtoto na akaenda kwa Elizabeti, akaenda kwa Daniel akamwambia habari za mambo ya mwisho, na Je! Si mmeyaona?  Nampenda sana Michaeli, BWANA YESU asifiwe, Michael wa Mbinguni ninamjua, yeye ni Rafiki yangu na hata habari ya kufundisha ananileta yeye, ananifundisha, ananiambia twende hivi. Je! Wewe unampenda Malaika Michaeli wa Mbinguni?  Napenda nikuambia jambo,  Mnaombaga sana kuwa nawatuma Malaika, ni sawa ila napenda nikuambia kuwa, Malaika ni watakatifu,  wanaenda na watakatifu hata katika ufalme wa shetani  kuana malaika wa Mizimu na malaika wa mapepo, na malaika wa mizuka ukisoma biblia  inasema wako malaika ambao watasimama kuhukumu siku ile ya mwisho,  wako katika ufalme wa MUNGU na pia katika ufalme wa Shetani.

Kuna malaika wa Wokovu, wa Mbinguni, kuna malaika wa vita wa mbinguni wa kuzimu kuna malaika wa uimbaji wa Mbinguni na Malaika wa uimbaji wa kuzimu. Malaika wa MUNGU wako kwa ajili ya kukulinda wewe na Malaika wa shetani wako kuwalisha wale ambao wamemkubali na kuiharibu kazi ya MUNGU.  Malaika wa MUNGU wanafanya kazi, na wanaendana na mtu ambaye amemkubali MUNGU, Utakumbuka Paul na Sila walipokuwa gerezani walikuwa wakiimba, nani aliyewafunga pale? Je ulishawahi kujiuliza ni nani aliyewapeleka pale na kuwafunga na ni nani aliyewafungua?  Na wewe kamsifu MUNGU yawezekana wako malaika wa shetani ambao wamekufunga, msifu MUNGU na ukimsifu MUNGU Malaika wa MUNGU watakufungua katika vifungo hivyo vyote, haleluya!

Mtumishi wa MUNGU Daniel,  alitupwa kwenye  shimo, kuna wakati alitupwa kwenye moto na kuna wakati alitupwa kwenye simba, unataka kujua  ni nini kilinyamazisha wale Simba ni malaika wa MUNGU,  ambao walikamata meno na kinywa cha simba nao hawakumdhuru Daniel, nae Daniel alitoka salama, hata katika bahari wako Malaika wa wanaoilinda Bahari, wako malaika wa mvua na ndio maana hata wachawi wanaweza wakaifunga mvua, wakatuma malaika wao wakaizuia mvua ila hapa Tanzania kwa sasa hawataweza kwa sababu MUNGU yupo na Nabii wake nipo, kuna nchi utakuta kuna  vita watu wanauliwa, Nchi invurungwa na kuvuruga wanadamu, hapo huwezi ukasema kuwa ni malaika wa MUNGU, hao ni malaika wa shetani,  kazi yao ni kuharibu wanadamu ila hapa Tanzania wapo Malaika wa MUNGU, mimi ninavyowaambia  kuna amani, ni kweli ipo,  kwa sababu naelewa kuwa malaika wa MUNGU wapo wanailinda Nchi na hata shetani akipanga mipango yao mibaya naelewa maana wanajisumbua  maana wako malaika wa MUNGU  na yupo Nabii wake na Malaika wa MUNGU wanatembea na mimi popote niendapo wapo nami; “Kuna wakati nilikuwa nilisafari Nchi fulani, ndege ilipokuwa inshuka Malaika walikuwa wameshika tairi na kuiweka ile ndege chini taratibu, yawezekana kulikuwa kuna  malaika wa shetani ambao walipangwa kufanya uharibifu yamkini ilikuwa nisifike au ili Nchi ile isipate uponyaji na Injili ya kweli na lile ambalo MUNGU amenituma kwao lisifanikiwe lakini nilifika na nikafanya kazi ya MUNGU, Haleluya! Nilienda na kufika salama na kufanya kazi ya MUNGU na nirudi salama”.

Kuna Malaika wa biashara  toka kwa MUNGU, kwanini  biashara au kazi zako zinaharibika, haribika, ni malaika wa shetani, nuksi na balaa, mikosi, kuua wokovu, kuharibu, kazi zako ndio wapo wanafanya hayo, na kama malaika hao wa shertani walivyomuasi MUNGU ndivyo hivyo hivyo walivyo kuharibu wanadamu, wokovu na wanashirikiana pamoja na Shetani. Naenda kuwafekelea chini hao Malaika wa Shetani wote na itakuwa historia katika maisha yako na maanisha utaona upenyo, kama Paulo alivyokuwa amekaa gerezani malaika wakamfungua na hata wewe utakuwa huru, hata Petro alipotolewa gerezani unajua ni nani aliyemtoa? Ni malaika wa MUNGU ndio aliyemtoa,  wakati  mfalme alipokuwa anataka kumuua Petro, Petro alishatolewa na Malaika, na kama wachawi wanataka kukuua, au maisha yako yameharibiwa na Malaika wa shetani, ninakwenda kuliita jeshii la MUNGU linakwenda kukutoa,  hata kama unashida  gani? MUNGU atakutoa na kukuponya,  yupo Malaika anayeitwa Rapha ni uponyaji, yupo hapa, Rapha ni uponyaji pokea uponyaji. Yupo malaika wa madhabahu ya MUNGU na yupo Malaika wa Madhabahu ya shetani  na ndio maana huoni hapa madhabahuni tukichoma ubani maana tuinatumia damu ya YESU, kuna malaika wa sifa,  wanakaa na waimbaji na kuna malaika wa kishetani  pia wanakaa na waimbaji wa upande wa shetani na kuna malaika wa kilimo, elimu, karama, ufundi na pia kuna malaika wa kuharibu, na hata ukisoma biblia inasema kwa Malaika wa Kanisa Fulani na hata sasa kuna Malaika wa Kanisa la YESU ni BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Kuna malaika wa ubatizo ule ubatizo wa YOHANA na sio ubatizo wa kikombe, kumwagiwa maji au ubatizo zote ambazo ni kinyume cha ule ambao alibatizwa YESU, inastaajabisha baadhi ya watumishi walivyobadilisha kweli ya MUNGU, malaika  wa MUNGU unaweza kuwapeleka kwenye ubatizo wa kikombe?  Mambo haya yanakwenda katika roho,  kuna malaika wa kitengo cha sadaka, na sisi hatuandiki sadaka kwa sababu kuna malaika wa kitengo cha sadaka hao wanajua kiasi ulichomtolea MUNGU na wako malaika wa kulinda sadaka zako, na hata anayekula sadaka zako wako malaika ambao wanamshughulikia kwa sababu kula sadaka sio sahihi, Lakini pia wapo malaika wa wachawi, hawa wanatenda kazi na wachawi, hupita kuharibu, huwanga katika nyumba za wanadamu, hata utasikia sauti mbalimbali juu ya bati, kwenye paa la nyumba, naenda kuwateketeza na hutasikia hizo sauti tena na Malaika wa MUNGU watatenda  kazi  wakae  nyumbani kwako sasa.

 Malaika wa MUNGU wananisikiliza na wananielewa na MUNGU akishakuwekea mkono wake na akakuambia kafanye kazi yake, Malaika wa MUNGU huenda na wewe, na  Malaika wanamsikiliza MUNGU na wananisikiliza Hebron maana wanajua kuwa mimi ni rafiki yao,  wanaelewa kuwa huyu ni kamanda wetu, wanasikiliza maelekezo toka kwa  kamanda, kuwa ninasema nini,  na wao  wanatii na kusikiliza,  nami ninawaambia na kuwaagiza fanyeni kazi hapa, pale, kule, twendeni hivi nao hufanya, hivyo  waheshimuni malaika na ndio maana nawaambia kila mara waombeeni malaika wa MUNGU maana ni marafiki zako na hata ile siku ya mwisho unapokuwa unaelekea kwa Baba yako watakusindikiza, kuna vitengo mbalimbali, Haleluya! Ukisika Gabrieli sio wote ni wa Mbinguni, tunaelewana?  Rudi katika biblia kila walipotumwa Malaika wa MUNGU, yale ambayo wameagizwa. walifikisha ujumbe, ulitimia na katika ufalme wa MUNGU pia kuna malaika wa Vita na kiongozi wao ni Mikaeli huyu anapita maeneo yote, na  hata MUNGU ana idara mbalimbali naye anapanga ukipata Neema MUNGU atakuonyesha Malaika wake,  Mtu mmoja akasema Hebron, ameendaje Mbinguni na  anaishi na ameendaje kuzimu na anaishi? ujue ufahamu wa mtu huyo bado haujaweza kuchanganua mambo, Wamesahau kuwa tunaenda katika roho, Je! Hakuna ambao wapo hapa nanimewatoa kuzimu? Unaendaje? Unaenda  kiroho akuongoze MUNGU, nakumbuka hata siku ambayo nilikuwa nimekwenda Michael alikuwa Mbele,  YESU alitaka kunionyesha kuwa kila mahali anapoenda YESU anatangulia kwanza Michael,  wewe unaona Misafara ya viongozi, ufahamu huo wamepewa na MUNGU tena wamepewa  kidogo tu Mbinguni ni zaidi,  na Malaika wana mavazi yao na kiroho na wewe unamavazi na ndio maana unaambiwa ukifika Mbinguni utavalishwa mwili mwingine,  huu mwili umezoea, uchafu, chale, uzinzi, malango ya wanawake au wanaume, unasikia  kijana anasema huyu msichana lazima awe wangu hapa anakuwa na wanawake wengi na utasikia binti anasema huyu mwanaume lazima awe wangu hapa anawanaume wengi watu hao ni lango ya shetani la wanawake au mwamnke, sio kila lango ni la MUNGU.

Wako malaika wa injili wasimamiao kweli ya Neno la MUNGU wanawajua waliookoka wanajua kinachofundishwa hapa na nini kinachotakiwa kifundishwe hapa kwa ajili yako na wako malaika waletao riziki nyumbani mwako, wako malaika waletao mahitaji, ujenzi wako, na pia kuujenga ufalme wa MUNGU na hilo jeshi niko nalo na kupitia hilo tutahakikisha ulimwengu mzima unamrudia MUNGU na wanadamu wengi waende Mbinguni, na kila nitaposimama na kufundisha au kuelekeza au hata kwenda katika kazi Fulani  sio kwamba Hebron anakwenda mwenyewe niko na jeshi la MUNGU na kama unataka  kuniua uliue hilo jeshi kwanza, Je! Unaweza kumuua MUNGU? Huwezi hivyo basi huwezi kuniua.   Malaika wanakuleta kanisani, wanakuandalia chakula chako, wanaondoa makufuru ili ule japo hutawaona, gari linaanguka unatoka mzima, umefundishwa usifurahie adui wako akipata mabaya, kwa sababu MUNGU anafurahia wewe ukipata mazuri toka kwa MUNGU, Na unapowaombea wenzako MUNGU anazidi kuachilia mema kwako.

Nasikia malaika wanasema  watu hawa bado hawajatuelewa,  Malaika ni watumishi wa MUNGU  Mbinguni, Maserafi, makerubi pia ni aina ya Malaika wa MUNGU Mbinguni, BWANA YESU asifiwe, wako malaika wanaolinda Jua tu, wako malaika wanaolinda ardhi ili shetani asitoke na ikifika zile nyakati za mwisho malaika hao wataondoka  ndipo shteani atatoka moja kwa moja, wako Malaika wanaolinda madini, Malaika wa MUNGU na wako Malaika wa Shetani ambao wanalinda madin,i wako Malaika wa Amani,  wako wa uchumi,  wako malaika hapa, wako wa uchumi, wako wa ulinzi. Mnajua Tanzania sio kila mtu anawapenda, hebu fikiria tulipata Msiba katika Nchi, ila cha kustaajabisha wako baadhi ya wahubiri wanafurahia kuwa tuliona, tulionyeshwa, achaneni nao hao, wanatafuta umaarufu, Tanzania nisikilizeni achaneni na hao tusonge mbele, hao ni wapuuzi, hata wao kufa nao watakufa tu. Hata wewe uliyeokoka saa unakata roho yuko malaika ambaye anakuchukua na anakupelea mahali pa kupumzika na wewe ambaye unakataa  kuokoka kufa utakufa tu na saaa unakata roho kwa sababu MUNGU yeye ni wa haki wako malaika wa shetani atakuja Gabriel wa Kuzimi na kukuchukua na kukupeleka huko, Tafakari Je! Maisha yako sasa umeamua kumpa Nani? MUNGU au Shetani au Bado unasema badobado Rafiki yangu hebu rejea sasa Malaika wanakupenda wanakutamani wanakutamani kuna mambo wanataka wanyafanye kwako, kuna mambo ambayo wameagizwa kuyafanya kwako ila watafanyaje kwako wakati wewe hutaki? Wewe ndio sababu ya kuwakwamisha,  na wanashindwa kukuhudumia kwa sababu ya ugumu wa maamuzi yako, tabia za asili, moyo mgumu, kichwa ngumu, tabia za asili,  hata YESU alipokuwa Jangwa ni Malaika walikuwa wakimhudumia,  Umesoma na kuelewa habari ya wana wa Israel, unafikiri vyakula  walivyokuwa wanakula ni MUNGU  alikuwa anawapikia? ni Malaika tena vilikuwa vyakula vizuri vya afya, vyenye ladha njema, nzuri. Malaika ndio walikuwa wanatengeneza? Hapana!  MUNGU nae anaandaliwaga, Tukifika Mbinguni sio kuopiga makofi tu, jamani Maisha yako Mbinguni hapa duniani hakuna kitu ulitoka Mbinguni na utarudi Mbinguni nahuko ni Raha tele, amenituma Nabii Hebron nikurudishe kulekule, Je! unafikiri kuwa shetani ananipenda? Shetani anajua kuwa nimeaga, na anajua kabisa kuwa nimeaga kwa MUNGU, na Nikapata Neema na kibali cha kumtumikia MUNGU, anajua kabisa Hebron ameandaliwa, anaelewa niko na Michael anaelewa hata Michaeli kuna saa anaendelea na majukumu yake pia, lakini huyo shetani haniwezi.

          Uwezo wa wachawi kupaa au kuwanga, kutembea uchi, ujue kuwa wapo malaika wa shetani ambao wanawawezesha kufanya hivyo, wanapaa, anaenda na wanatimiza kazi waliyotumwa na shetani,  kwa masharti ya kuvua nguo, na kupaa uchi,  wanafanya hivyo free bila tiketi, bila booking,  kubook kwako  ni kupaa uchi na kwenda kugonga nyumba za watu kinyumenyume?  Kuna Malaika ambao wanaangalia rada ya MUNGU na wako wa shetani ni wale ambao pia wanaangalia rada za shetani ikiwamo ramli, kuna malaika wa shetani wa malipizi na mapatilizi na kazi yao ni kukushambulia ni watendakazi wa shetani na pia yapo makanisa ambayo pia watu wanayakimbilia japo hayana MUNGU wapo malaika ambao wanaitwa misukule, Kazi yao ni kukamata fahamu za watu, wanaofanya nao kazi, mtafikiri mnaenda kwa MUNGU kumbe mnaenda kwa shetani na pia napenda nikufundishe kuwa mahali alipo malaika wa shetani kuna utaratibu wao wa kishetani ikiwapo kutoa fedha kwa ajili ya maombezi na mahali alipo MUNGU utaratibu huo haupo huduma za kiroho ni bure hapo yupo malaika wa MUNGU, Malaika wa shetani  humpa mtumishi kibali cha kuweza kumfungua au kumpa ujumbe wa kishetani mtu au muumini kwa pesa, mara atakaopotoa hela, inakuwa kama hospitali, unalipa ndipo utibiwe ila mahali ambapo wapo malaika wa MUNGU, MUNGU huto ahuduma zake Bure. Mtu anayetaka kukuuwa huwa anawatuma malaika wa shetani, unaumwa hata dawa ukipewa huponi, ila ukifika kwa MUNGU unapona.

          Ukiwa mkaidi malaika wa MUNGU wanaweza kukutakaa, Usipende malaika wa MUNGU wakukatae, acha ubishi, kuwa mnyenyekevu, pendo utakatifu, kuna mambo mengine unayapata kwa sababu ya ubishi wako na kuna wakati MUNGU anaruhusu shetani akushughulikie na kwasababu MUNGU anakupenda, anaruhusu ili ukubali na uwe wake. BWANA YESU asifiwe.

Unapookoka kuna Malaika wanakuwa na wewe mpaka unamkubali MUNGU, kubali umshike YESU sana. Je! Watenda kazi wako ambao ni malaika unawatumia? Hata mimi,  situmii  akili yangu kwenye kazi ya MUNGU kwa sababu kuna ambao wameandaliwa kufanya kazi na mimi,  MUNGU alishapanga kuwa kuna mahali kanisa litakuwepo basi  anakuwa ameniandalia watenda kazi ambao watatenda kazi na mimi,  wako waliaondaliwa kuwaleta watu waokoke, wako waliaandaliwa kupigana na kuwateketeza wale ambao wanashindana na mimi pamoja na watoto wangu, ikiwa pamoja na wewe;  wewe u familia ya Mbinguni hebu pata picha ni mambo mangapi yanakupata, Petro, Sila na Paul walijielewa,  kuwa lipo gereza ambalo lilikuwa linawasumbua, ila walikuwa na Neema maana walimjua MUNGU wakavushwa hata Daniel alijiulewa, na akajua kuwa  MUNGU umenipa ulinzi basi akaomba ulinzi wa MUNGU umlinde na Meno ya Simba  akalindwa, kuna malaika wa ushindi, ushindi wako uko wapi?

Namna ya kuwadhibiti na ujue pia jinsi ambavyo malaika wa shetani wanafanya kazi, Malaika wa shetani hawafanyi kazi bila ya kutanguliza sadaka, ndio maana ukienda kwa waganga au kwa watumishi wa kipepo lazima utoe fedha au kitu Fulani ndipo usaidiwe, na sadaka kwa ajili ya kukushughulika na kile ambacho amependa kikatendeke kwa mwanadamu,   anaweza kutumwa malaika wa Mizimu wa wafu kwa mwanadamu anapewa sadaka kuua, kubomoa au kukuharibu na kama hujakaa vizuri na MUNGU wanapata nafasi. Tunajifunza kwa akina Daniael Paul na Sila wengine si kwamba wametenda dhambi zilikuwa hila za shetani lakini kumbuka kumwita MUNGU wako aliyekuumba katika kila jambo na malaika watajua kuwa huyu ni wa familia ya YESU nao watakuokoa na kukusikiliza na kukuvusha, watakuchomoa toka kwenye mikono ya shetani. Haleluya!

Malaika wanaangalia Neno la MUNGU mfano ukiwa mwizi wa fungu la kumi la MUNGU, malaika wa MUNGU wanaondoka nawe unakuwa huna ulinzi kwenye jambo lako ndipo sa wanakuja malaika wa shetani wanaoteketeza, hatima yake ni Nuksi, balaa na mikosi lakini aliyesababisha kuondoa ulinzi ni wewe.  Kuna malaika wa shukrani wa MUNGU na wa shetani, watu wengi wanaona kuwa hakuna sababu ya kumshukuru  MUNGU, ni haki yako kulindwa na kupewa mahitaji na maana ndio amekulinda,  sio sahihi kama unafikiri hivyo, lazima kumshukuru MUNGU kwa kila jambo.

Malaika wa shetani hushirikiana na Mizimu, nao wakiungana na wakitaka kukua unakufa kama huna MUNGU, pia nafsi nyingi zipo zinazurura tu hazijaenda  Mbinguni, ndio maana kuna mahali ukipita unasikia kama mwili au nywele zinasisimuka, unakuwa unakutana  na hizo nafsi ila hutakuwa unaziona kwa sababu hujapewa neema hiyo ila wenye neema hiyo huziona. Huzioni kwa sababu yamkini kiwango chako cha Imani kakijafikia hapo, waizi wa nyota ni malaika wa shetani, ukisikia vita ni malaika wa shetani huisababisha vita hivyo, ziko Nchi ambazo nikifika na nikikanyaga vita vitakimbia, sio mimi ila ni MUNGU anavyotaka, ukimkubali Nabii thawabu inaingia, kuna Nchi nimefika au nikifika tu inafunguliwa sio mimi ni MUNGU anataka nifike ili jambo lake litimie, ndipo nami ninanda. Biblia inasema wako malaika ambao umepewa ukikanyaga mahali unakuwa umepamiliki ila sio pa uovu au pa shetani ni penye kusudi la MUNGU tu, Maana kuna baadhi ya watu wanaolitumia Neno la MUNGU vibaya kuwa hata wakikanyaga kwa mganga wa kienyeji (Agent wa shetani), bar au sehemu za anasa ni kwangu, Je! ni sawa? Sio sawa. Kuna watu ambao hata malaika walikuwa hawawahudumii lakini sasa wanakwenda kuwahudumia, hata  ndoto zako anayekamilisha ni malaika wa MUNGU  ni kazi waliopewa wakulinde,  lakini kukulinda wewe kunategemea uhusiano wako wewe na MUNGU, unaweza kukuta mtu ni mkristo  lakini ana malaika wa shetani, ingekuwa kweli malaika wa injili anasema watu waokoke, dunia nzima ingekubali wokovu lakini  katika baadhi ya makanisa waumini wakiokoka wanatengwa na kanisa, huo ni mvurugano,  Bwana YESU asifiwe,  unadhani Eliya alivyopaa kimwili ni gari lilikuja tu likanyanyua?  Walikuwepo malaika wakamyanyua na wakamfikisha kwa MUNGU,  kuna malaika wa ndoa, ila wengi  wanamalaika wa kipepo ndio maana wanakosea kuoa au kuolewa.. kuna malaika ambao wanaangalia kusudi la MUNGU lililopangwa kwako, lakini wewe unalipinga, lakini MUNGU anakuambia ni hivi  ila wewe baada ya miaka mitatu unapinga lile kusudi halitatokea.

  Biblia inasema Malaika ni watiifu kwa MUNGU sana, wewe mwenyewe unashindwa kutii! kwa MUNGU utaweza? Kumbuka Yusuph alivyofanywa mtumwa, malaika wa MUNGU  walimnyanyua hadi akawa waziri mkuu lakini pia kuna wanadamu wanatafuta vyeo  Fulani kupitia wachawi, waganga, au malaika wa shetani na wanapata, wanachokifanya  wanaiba vitu vyako kiroho halafu wanakutoa wewe au yule ambaye amepangiwa na MUNGU (kwa sababu na yeye hakukaa sawa na MUNGU) wao ndio wanakaa, mimi nambomoa, kuna malaika wa  Fedha na dhahabu, za kwako zi wapi,  kubalini kubadilika mkamwone MUNGU na mkaone makubwa  zaidi, malaika watakaaje na wewe, wakati wewe hupendi kukaa na MUNGU?, roho yako mbaya, jicho lako unangalia wenzako vibaya kwa kiburi na dharau, wewe mwenyewe na vitu vyako hamumpendi MUNGU. Je! Malaika watakaaje kwako? Tunajua kabisa kila kitu tulichonacho ni cha MUNGU, tumepewa Neema ya kuvimiliki na kuvitunza kimwili lakini kuna baadhi ya watu ukimwambia mwachie MUNGU iwe mke, Mume, watoto na vyote ulivyonavyo ni vya MUNGU yaani umpe MUNGU nafasi ya kwanza kuvimiliki atakuambia ni vya kwangu, sio vya MUNGU zitafakari fahamu zako, Je! Wayajua ya mbele? Je! Unajua saa au siku ambazo utafika mbinguni utakuwa umelipwaje?  Umepewa karama na talanta hauvitumii unazibania bania siku ile ya mwisho kuna malipo utalipwa sawasawa na ulivyovifanya, umefunga, umepiga makofi, kila unachofanya utalipwa, ukifika huko hulipwi mapesa ni maisha ya kifalme, naona malaika wakiwa wanapita wanaandika record yako yote kwenye ufahamu na moyo wako wote. Mwambie malaika wa kishetani potea kwenye maisha yangu na hauna nafasi wanakuonea wivu maana wao walifukuzwa huko na sisi tunawafukuza, tunaelewana? Malaika, unaweza ukawa unaenda kwenye nyumba za watu unasikia mlango unagongwa, ukiangalia hakuna kitu, ujue kuna malaika wa shetani, wakati mwingine hutenda kimwili lakini hutawaona, mpaka wapende.

   Unaweza ukawa unatamani kuwaone malaika  wewe kama wewe lakini hutawaona mpaka wao wenyewe waamue ndipo uwaone yaani uwe unafaa kuwaona, (Imani yako na kiwango cha Imani ulichofikia) kuna malaika wa kulinda mwili wako kaburini ili usiliwe nyama,  wakati mtu amekufa wachawi hufika na kuangalia mtu yule na kuiba vitu vyake kiroho hata kama ni marehemu na usiku wanaenda kuliwa nyama, sasa nakuambia maiti  ya muumini wa kanisa hili  hailiwi nyama au mahali mtoto wangu amezikwa hata mchawi hakanyagi, mwili utakaa vema japo yeye yuko sehemu ya kupumzika, unajua wachawi hula nyama za watu na mbavu za watu hufanya  kama toothpick.

Nakufundisha mambo ya ufalme wa MUNGU sijui kuwa ni watu wangapi wamevuruga maisha yako na ni wangapi wametumwa kwako kuvuruga maisha au wokovu wako.  Biblia inasema Malaika wa MUNGU ni wengi kama mchanga wa baharini, Kuna malaika wa udereva, Pailot, na wa vitengo mbalimbali unapopanda ndege / gari au kufanya jambo Fulani,  wapo Malaika  wa ulinzi, wanaoonda mahali popote,  ukiwa ni mtumishi wa MUNGU au mwana wa MUNGU ambaye anamtii MUNGU,  Malaika  wanaenda nae  ili wahakikishe amefika salama, hutamwona Malaika ila atakaa pale kwenye nafasi yake akiongoza  na kukulinda,  anajua mtumishi wa MUNGU anakwenda mahali Fulani wanahakikisha umefika. Wakati Fulani nilikuwa natoka Autralia naenda Hongkong na mizigo ilishaingizwa kwenye ndege na nilikuwa nimeshaagana na watoto wangu wa kiroho ambao walikuwa wamenisindikiza, nao walishaelekea mahali pao pa kazi,  ilikuwa inapita Hongkong kuelekea Nchi nyingine ili niweze kurudi Tanzania na lengo lilikuwa natafutwa Hebron niuawe  hivyo  malaika  wa shetani walikuwa wameweka vitu vyao ndani ya ndege ila wanadamu walikuwa hawajui,  malaika wa shetani walishaweka mtego kuwa itaangukia sehemu Fulani  na walipokuwa wamepanga  wakajua Nabii Hebron ndio anapanda ndege hiyo na wakati tunasubiri kupanda , MUNGU akaniambia  hupandi ndege hii, kibinadamu Pilot na wahudumuu wote walishaingia,  nami nilikuwa nimekaa pa kuingilia ili kuanza safari, ila  malaika wa MUNGU wakaingia na kuizima kabisa ile ndege, haikuwaka tena, mara nikasikia tangazo kuwa ndege hii haitaondoka, abiria wote mtapelekwa hotelini na mizigo mtaikuta ilipoachwa  kibinadamu ni ngumu lakini nilipofika hotelini nilitubu na kumshukuru MUNGU nikamwomba MUNGU kwa ajili ya ndege na malaika wa MUNGU wakaandaa nyingine ambayo  malaika wa shetani hawakuijua nami nikapanda na  nikafika salama.

Uzuri wa malaika wa MUNGU hukulinda kila mahali, lakini kumbuka ili mganga akutese huwa anatuma malaika wake wa kishetani ndiye anayekutesa. Malaika wa MUNGU hukupigia salute kama unamweshimu MUNGU, Malaika huzunguka nyumba za wana wa MUNGU kama moto, endapo unamweshimu MUNGU, na unalindwa kuliko wafalme wa duniani, ukimpa YESU maisha malaika wanatembea na wewe,   Katika ufalme wa MUNGU ukimtii MUNGU unainuliwa Zaidi maana hata hao malaika wa shetani hunyanyuliwa kwa level zao katika ufalme wa shetani, lakini ufalme wa Shetani hauwezi kumshinda na kupinga kusudi la MUNGU. Sio kila mahali Michaeli anakwenda, hapana kuna vikosi mbalimbali hata kimwili sio kila mahali kamanda wa jeshi anakwenda, kuna meja, komando, kuna malaika wa kila kitengo mbalimbali. “Sema MUNGU kuna mahali nimeshikwa na malaika wa shetani, nami nitaita malaika wa MUNGU akutoe kama Petro”. Ataenda kukutoa, mapigo ni makali lakini unaenda kutolewa sasa watu wengi wanawaogopa mpaka wahubiri wa kishetani, usiogope tunaye BWANA YESU, usiogope!  Rejea kwa MUNGU.

Wakati mtu napooa au kuolewa, koo (yaani ndugu na majamaa, mashemeji au mawifi) husema mume au mke wetu, maana kuna malaika wa mila, na baadhi ya watu, (au hata wewe yamkini umeitwa), watu husema mke wetu au mume wetu, hebu tafakari umeolewa au kuoa wengi au mmoja?  Kwa sababu wameshasema na kukiri na wewe umeitikia na kulipokea malaika wa shetani wa kuharibu huingia na kila mmoja huanza kukugombania ni wangu, ni wangu na hatimaye ndoa inaharibika maana kiroho unakuwa na waume au wake wengi. Mke au mume ni wa mmoja. Kila mtu anataka mume na  mke mmoja, hata watoto wadogo wanapataga shida inapofikia umri wa kuona na kuolewa, maana ukiwa mtoto uliambiwa mke  wangu  akiwa wa kike (Babu, ndugu, jamaa, marafiki kama utani utani) au mume wangu (na bibi, ndugu, jamaa, marafiki kama utani, utani)  sasa ikifika wakati wa kuoa au kuolewa hapati mtu sahihi. Muwe mnafuta hayo maneno. Kuna baadhi ya watu wanataka nafsi zao tu ndio ziokoke, lakini taka Baraka, nautajiri wako na nafsi yako iokoke, ndugu jamaa, taifa na vitu vyao na vyako pia viokoke, maana wako pia malaika wa utajiri wa Mbinguni na wa Shetani na kazi ya malaika wa shetani ni kuiba utajiri wa watu wa MUNGU  na kuwaletea watu wao  ambao wanamsikiliza shetani. 

Sema: BWANA YESU  Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizofanya kwa kujua na kutokujua, BWANA YESU najua  wako malaika wanaonilinda wa Mbinguni naomba wanilinde kuanzia sasa, waokoe na mwili na familia na mataifa, BWANA BWANA,  najikabidhi mkononi mwako katika ulimwengu waroho na mwili,  Naomba jina langu liwepo katika  kitabu cha uzima wa milele na mimi niwe mmojawapo wa tunda la wokovu ulilolitoa,  BWANA YESU nimejitoa kwako, siku zote za maisha yangu, naomba nisimame imara na Roho Mtakatifu wako  akinitia nguvu nisitikishwe na malaika wa shetani na malango  ya Ibilisi iwe mwisho, nami niwe huru, katika jina la YESU Amen. 

Mtoto mdogo anawekwa wakfu habatizwi na anapowekwa wakfu ndipo malaika wa MUNGU humlinda kiroho na kimwili pia. Malaika wa shetani hawapendi watoto wadogo waanze na MUNGU hivyo wakabadilisha, wakaamua kuwa mtoto amwagiwe maji (ubatizio wa kikombe) hii ni ili asiwe wa MUNGU bali awe wa shetani, jambo hili ni chukizo mbele za MUNGU kwani ni mafundisho ya uongo (Mapokeo ya wanadamu) ndio maana umepita kwenye mateso kwa sababu haukuwa umekabidhiwa kwa malaika wa MUNGU kuanzia ulipokuwa mdogo, sasa basi usirudi nyuma na usibatize watoto wadogo.

 

Imeandikwa na Nabii Hebron.