JE! UNA MOYO WA AINA GANI?
BWANA YESU nakushukuru kwa muda huu tena, baba kwasababu wewe ndio mfalme na hakuna zaidi yako, wewe ndio mwana wa pekee wala hakuna spea nyingine Zaidi yako na MUNGU anakujua, asante BWANA YESU, nashukuru. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
1 WAFALME 3 – 10 - 15 - Neno hili likawa jema machoni pa BWANA, yakuwa Sulemani ameomba neno hili. MUNGU akamwambia, kwa kuwa umeomba neno hili, wala jukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho ya adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe. Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika Wafalme kama wewe siku zako zote. Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu na amri zangu kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi. Naye Suleimani akaamka na kumbe ni ndoto. Akaenda Yerusalemu akasimama mbele ya sanduku la agano la BWANA akatoa Sadaka, za kuteketezwa, akatoa na sadaka za Amani, akawafanyia karamu Watumishi wake wote.
Neno hili MUNGU alikuwa akisema na mimi, Ni moyo wa aina gani Selemani aliokuwanao na pia napenda nikufundishe na wewe ujue kuwa jinsi mtu alivyo ndivyo moyo wake ulivyo, kama ni mchawi na ndani yake ipo roho ya uchawi, au jinsi roho ambazo zinatenda kazi kwa mtu huyo na zingine zinaonekana katika matendo au mwonekano wa mwanadamu huyo kimwili ndivyo mtu huyo alivyo hata kiroho, na mtu huyo ameumbwa vizuri na Mwenyezi MUNGU na yamkini kwa kujua au kutokujua roho hizo zinapoingia au anapoziruhusu ndipo mtu huyo huanza kubadilia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Sulemani aliomba hekima kwa sababu hakuwa nayo na baada ya kuomba hiyo mwenyezi MUNGU akampa vingi, vingi mapaka leo hii ni historia tunaelewana! Lakini nitapita kwenye maombi, nilikuwa naombea baadhi ya vitu MUNGU akaniambia yule moyo wake umebadilishwa, uko hivi na yule moyo wake umebadilishwa uko hivi na kama Sulemani mwana wa MUNGU, Nabii wa MUNGU, Mungu aliubadilisha Moyo wake ulibadilishwa akawa tofauti kabisa yaani akapewa Hekima, Yamkini na wewe umebadilishwa kwa kujua na kutokujua, ukisoma katika Neno la MUNGU kuna mahali YESU anasema nipe moyo wako, kwa nini anasema hivyo? YESU anasema hivyo ili afanye jambo ndani ya moyo wako, zipo aina mbalimbali za moyo, Kuna moyo wa Utakatifu, MUNGU akikufanya kuwa mtakatifu utakuwa mtakatifu na kuna moyo wa wokovu utasikia mtu anataka wokovu, lakini kama moyo wake haujafanyika wokovu mtu huyo hawezi kuokoka, kuna moyo wa dhambi ndio maana mtu anatenda dhambi kuna moyo wa dini ndio maana mtu anapenda dini, kuna moyo wa umaskini utakuwa maskini, utajiri ndio maana unafanana na utajiri, MUNGU amempa mwanadamu vitu hivi lakini yuko adui huwaga anaiba mioyo ya watu na kuwapa watu wake, utakuta mtu anasema mimi sina furaha ina maana amewekewa moyo wa huzuni, mwingine ni madeni tu amewekewa moyo wa madeni, na moyo wake una madeni, unaweza ukawa huna moyo wa kuoa au kuolewa huwezi, kuoa au kuolewa unatakiwa kusoma hauna moyo wa kusoma, utasoma na utaacha ashukuriwe MUNGU ambaye anatufunulia hayo, huna moyo wa kwenda ibadani ndio maana huendi, huna moyo wa kumshukuru MUNGU ndio maana huwezi mshukuru MUNGU, huna moyo wa wa toba na rehema ndio maana huwezi kuomba toba na Rehema, hata mataifa mengi hayana Toba na Rehema na hata mataifa mengi hayana moyo huo wa kuomba toba na rehema ndio mana MUNGU ameagiza mataifa wafunge ili kuomba toba na Rehema hawakufanya hivyo kuhusu janga la mfumo wa upumuaji, kumbuka ahadi ya MUNGU ipo pale pale ili MUNGU aondoe ugonjwa huo wa changamoto za upumuaji, hawakusikia ila sasa sitazungumzia hilo tena. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Shetani ameiba moyo na kubadilisha mioyo ya wanadamu ili watu wasiwe na hofu ya MUNGU watu hawana hofu ya MUNGU, hawana hofu ya dhambi hawana hofu ya kumwogopa MUNGU, wanamwona MUNGU ni wa kawaida, yamkini ni wewe au ulishapita huko na Moyo wako unapobadilishwa ndio unafanana hivyo, ili ufe lazima moyo wako ufe, lazima ufe na wachawi wanauaga kwenye moyo ndio ufe na hata wachawi wanauaga kwenye moyo lakini kama BWAMNA YESU akiwa ameushika moyo wako wachawi, wala mapepo, wala majini, hawatauchezea, mizimu nao watakuchezea, kila mchawi moyo wake ni mchawi na kila mshirikina moyo wake ni mchawi ndio maana anaendagga kwa waganga, wachawi wenzake. Ukitaka kupona sikiliza Neno ninalokuelewesha. Usiwashangae hata wale ambao wanakushangaa unapookoka, wao moyo wao una pepo, wa kwako una wokovu ndio maana wao wanakushangaa ungelikwa na wokovu wasingelikushangaa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Pepo sio lazima lilie, mie hata siku moja sitataka au sitaki moyo wangu ufanane na wa mtu yeyote kila mmoja ameumbwa kama vile MUNGU alivyotaka sio kama yeye anavuyotaka, sasa kuna baadhi ya watu wakiona mtu amefanya matendo mazuri ndio wanataka wawe kama wao, mtu yule au ajifananishe na huyu hiyo sio sahihi penda MUNGU akutengeneze moyo wako, wewe kama wewe, kuna moyo wa wivu, fitina, ufisadi, mwizi mwizi unaibaiba tu ndio maana ulivyo unakuwa na ujasiri Fulani kuna moyo wa kutokumtolea MUNGU sadaka,Kumbuka kuwa nabii Sulemani, alipokuwa akiambiwa kitu alikuwa anakamilisha ibada yake na sadaka, na wewe jifuze maana ibada hukamilishw ana sadaka, na unapokuja kanisani au kufanya ibada yako Penda kumtolea MUNGU katika jambo lako ni ibada, ibada haikamiliki bila sadaka, jiulize ni mambo mangapi ambayo MUNGU amekutendeea na umeyapokea lakini haujayakamilisha kwa sadaka, angalia Selemani kakamilisha, MUNGU anaweza akukuita na akuonyesha jambo Fulani, ukashukuru kweli lakini hukulikamilisha kwa sadaka, Hapo je! umejifunza jambo? BWANA YESU asifiwe, sadaka ni Ibada, hata unapotoa sadaka ni ibada tofauti na kusifu na tofauti nakushuhudia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Kuna moyo wa kutangatanga ndio maana mtu anatangatanga hakai mahali pamoja anahamahama leo hapa kesho hapa, leo kanisa hili kesho lile, mwingine hataki kumsikiliza MUNGU wana hataki kutengenezwa na MUNGU hana moyo huo, huna moyo wa kunyenyekea, (kuna moyo wa kunyeyekea wengi ni wanyenyekevu mbele za watu ila mbele za MUNGU hakuna kitu, MUNGU haangalii ulivyo MUNGU huangalia moyo, Basi ni wapi umefika MUNGU anataka akufinyange akuinue lakini huna moyo wa kupokea kwa MUNGU, unakuwa na moyo wa kupokea kwa mizimu hutaweza kufinyangwa na MUNGU, hauna moyo wa kupokea kwa MUNGU, MUNGU anataka akubariki hauna moyo wa kubarikiwa na MUNGu unataka vya shetani hatima yake mi mikosi, shida na balaa. Jinsi mtu alivyo ndiyo moyo wake ulivyo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Utakuta mhubiri anamoyo wa uongo yeye hupinduapindua vya MUNGU sasa huwezi kusema mhubiri huyo ni wa MUNGU huyo ni wa shetani kwa sababu baba wa uongo ni shetani kwa sababu moyo wake umefanana na uongo na sio MUNGU, kwa sababu anawanyang’anya watu na kuwafundisha uongo, mfano. leta pesa kiasi Fulani nikuombee, leta sadaka ya ukombozi, na mambo kama hayo, na wakati huo anawadanganya watu kwa kutumia jina la YESU, ubatizo wenyewe unaobatiza ni wa kikombe, lakini anatumia jina la YESU, Kuna baadhi ya wakristo wana vichwa vigumu mkristo anakuambia namwamini MUNGU sana, namjua MUNGU sana, lakini haokoki ni kichwa kingumu hicho, hata mashetani pia wanajua MUNGU na YESU sana na hayaokoki, Bwana Yesu asifiwe, wewe okoka, unaweza ukabadilishiwa moyo wako wa kumwomba MUNGU ukawa huombi tena, moyo wa kuomba unaondelewa na unawekewa moyo wa mapooza, wanaiba moyo hata wakusoma Neno la MUNGU unakuwa husomi tena, kuna moyo wa kwenda Mbinguni wa kwenda Jehanam, mtu anayekwenda Mbinguni moyo wake unafanana na yeye kabisa, mwambie MUNGU azidi kukutengeneza na pia mtu wa Jehanam ana moyo huo na utamwona kabisa, matendo yake, sasa jiulize wewe, Je! una Moyo gani wewe? Sisimei moyo huu unaodunda tetete, unaosukuma damu, naongea katika Roho, una moyo wa aina gani? Wa kiherehere ndio maana unakuwa kiherehere? una moyo wa kiburi kama shetani ndio maana unakuwa kama shetani na mwisho wa kiburi ni kufa na mwisho wa kiburi kuangamia? kipindi cha Nuhu watu wengi walikufa? Mioyo ya wale watu ilikuwa na kiburi juu ya MUNGU na walikuwa hawataki mambo ya MUNGU na ndivyo ilivyo hata sasa watapona wale ambao mioyo yao itabadilika na ninachojua kuwa MUNGU ni mkuu kuliko miungu yoyote ile na yupo na mimi na yupo na wewe pia; kwa hiyo mambo yoyote ambayo ni kinyume na MUNGU hayatakuwa na nafasi hivyo basi usiwe mwoga kama MUNGU wako ni mkuu kwelikweli hapatakuwa na cha shetani ambacho kitakaa kwako. Lakini pia unaweza ukawa umeokoka na ukawa na MUNGU na bado pia ukawa unavurungwa vurungwa lakini pia Biblia inasema anitafutaye kwa bidii ataniona yamkini ulikuwa kondoo ulikuwa umepotea na siku nyingi unakuwa unazungukazunguka na hata mimi nilikuwa nimepotea nilikuwa nazunguka zunguka na katika kuzunguka zunguka zipo sehemu nilikuwa naona nipo na YESU na sehemu nyingine sikuwa nae lakini BWANA akaniokoa, kwanini biblia inasema jipe moyo mkuu, moyo wa ujasiri, moyo wa Imani, moyo wa kumtegemea MUNGU, huenda ikawa wewe unatamani kuwa na mali, lakini una moyo wa filisi, Bwana YESU asifiwe.. Kila mtu ajikague, usisubiri ile siku ya mwisho kwa sababu hakuna ajuae lini ataondoka, kifo cha mtu ni siri ambayo MUNGU mwenyewe ameificha, Moyo wako unafanana na wewe yawezekana nusu MUNGU nusu mapepo, pia inawezekana kuwa robo tu ya moyo wako ndio umempa MUNGU ni pale unaposhangaa kuwa mbona mtu yuko kanisani na kesho kwa waganga, kuna mtu anampenda MUNGU kwa sababu anapata kitu Fulani, YESU alimpa Baba yake Moyo wake, ndio maana alishinda, angalia alichokifanya na tunajifunza nini kupitia YESU ambaye ni mtoto wa mfalme ambaye alitoka akaja ili auwawe, na sisi tumepata uzima. Hivi leo au wiki nzima au mwezi mzima umetukana mara ngap?i umesema uongo mara ngapi? wewe umesengenya mara ngapi? lakini huna moyo wa kumshukuru YESU aliyekufa kwa ajili ya dhambi zako ili upate kusamehewa unaona ni kawaida, ni kawaida tu, na utabakia kawaida usipotaka kubadilika na hatimaye utapigwa kiberiti. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Unaakiwa uwe na moyo wa shukrani, kumdhukuru MUNGU, na YESU pia kwasababu kwa mapigo aliyopigwa YESU; kupitia yale mapigo tukakombolewa na leo hii tupo kama tulivyo, tumepata Neema ya ukombozi, tuko huru, tumeimarishwa na kupewa ujasiri na ukombozi kwa sababu ya damu yake na Hebu fikiria Je! kama damu yake YESU isingelimwagika? Hizi dhambi zote zingekwenda wapi? Na wengine ni sugu kila mara wanarudia dhambi, Anasamehewa anarudia, kila wakati unasamehewa, unarudia, YESU anakusamehe, Je! umemwambia asante, Moyo wa shukrani huna, sasa kubali mwombe MUNGU akutengeneze akuumbie moyo wa shukrani na kuthamini yale ambayo kwa Neema tunatendewa kila wakati. Tunaelewana watoto wa MUNGU? hebu mpe MUNGU moyo wako, kama ulikuwa unawapa majini, mapepo, mizimu wanadamu, sasa hebu mpe MUNGU Moyo wako aweke kitu chake ndani yako, hasa katika Imani ukapokee Zaidi, sijui mnanielewa? Kwanini MUNGU anasema amelaaniwa amtegemeage mwanadamu? Mwanadamu anakufa lakini MUNGU hafi, sasa usitegemee ulichonacho mali, elimu, cheo, watoto au chochote wewe mtegemee MUNGU tu, mwangalie MUNGU yeye ni MUNGU aliyekuwepo na atakaye kuwepo unatakiwa ujikane na uwe na Moyo wa kujikana ili ufanye yale yanayompendeza MUNGU, ukijikana hata kama watakutikisa na majaribu wewe hautatikisika, Wenginge wana mpenda YESU wanaangalia watoto, kwa sababu mioyo yao ipo kwa watoto, wanaona wao wameishiwa nguvu na watoto ndio watawasaidia, watoto ni wanadamu wanadamu hubadilika, sasa basi inafika wakati umeamua kuokoka, na watoto ukimwambia umekokoka wakikuambia kwa vile umeokoka sisi hatukuhudumii na wewe unamwacha YESU kwa kuangalia vitu, na matunzo ya dunia hii, bila kuionea huruma roho yako na bila kufikiri kuwa baada ya maisha haya ni wapi uneleke? Basi unaacha wokovu kwa sababu ya mwili na vitu vya kupita, kwa hiyo unakuwa na moyo wa kinafiki, nafiki, sema kweli, kama umeamua kuokoka basi okoka na YESU atakutetea, anayekwenda mbinguni sio mnafiki, Ukiwa unashiriki matambiko hutaenda Mbinguni. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Ukiwa na Moyo wa kusema kweli, kuchapa kazi, lazima utakuwa hivyo na mafaniko utayaona, kuna moyo wa uzalendo na nchi yako, moyo wa upendo, Moyo wa upendo haubagui, ukiwa unaangalia mtu na vitu alivyonavyo ndio umpende, huo sio upendo wa kweli, ni unafiki tu, YESU hakuangalia una nini alikupenda tu na MUNGU unapomruhusu ndio anaonekana Zaidi kwenye maisha yako na mpaka watu watabakia wakishanga kuwa Je! ni huyu? Kwa sababu ukiamua kumwachia MUNGU moyo wako yeye anakutengeneza na kukufinyanga apendavyo. Kuna baadhi ya watu wanaenda kwa waganga ili wapendwe unafikiria nini kinawafanya wapendane? Ni mashetani yanaingia kwenye moyo wa kila mmoja hivyo shetani A anakuwa meunganishwa na shetani B na kuunganisha na wanadamu kimwili lakini mashetani ndani ya watu ndio yanapendana sana, Wengine wanakuwa marafiki na wengine mke na mume kwa kuinganishi cha shetani ila mmoja wapo au wote wakipata neema ya wokovu hutengana na hatimaye mtu hushangaa ilikuwa nilipenda au kupendwa na mtu ambaye sikutarajia wala kumjua? Jibu! Waliunganishwa kishetani. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Kuna Moyo wa uaaminifu kwa MUNGU, na moyo wa uaminifu kwa shetani, sasa wewe huna hata moyo wa uaminifu wa fungu la kumi kwa MUNGU, kitu ambacho wewe mwenyewe unakishika, sasa pale shetani anapokupiga au unapokuwa umeachilia mlango kwa kukosa uaminifu wa kumtolea MUNGU fungu la kumi, utaanza kulia liaa, unalia lia, MUNGU mbona sionekaniwi? MUNGU mbona mambo yangu ni magumu? Wewe ndio sababu wanadamu wanatakaga MUNGU awe mwaminifu kwao, sana lakini wao hawapendi kuwa waaminifi kwa MUNGU, lakini wanampenda MUNGU lakini shetani ndio anawasababishia hayo, moyo wa hila ndio maana unamtendea mwenzako hila, anayekutendea hila lazima ndani ya moyo wake zina hila moyo wa hofu, Hebu tafakari, aliyoyapitia YESU, hebu fikiri mfano. YESU aondoke halafu uamchwe kwa hata siku mbili ujifunze halafu YESU akurudie; halafu Uone hii dunia ilivyo au itakavyokufanya ikiwa YESU ameondoka kwako na Neema yake imeondoka, Ni hatari sana ikiwa hii Neema ya YESU na YESU akiondoka ndani yako, Usitamani jambo hilo litokee kwako, mimi mwenyewe sikubali YESU aondoke kwangu, unatakiwa unang’ang’ania YESU na MUNGU, kama mtoto anyonyaye kwa mama yake wakati ana njaa hakubali kuondolea kwenye ziwa la mama yake basi sasa na wewe mng’ang’anie YESU hivyo hivyo utafika, kata una moyo wa kujiinua omba wa kunyenyekea, Moyo wa kuwa na vitu vingi, watu wengio hawapati vitu hivyo kwa sababu ya moyo wa kuziwazia makuu, moyo wa kujiona hufai mbele za MUNGU, lakini MUNGU anakujua na anajua kuwa unafaa, lakini adui ndio anasababisha hatimaye unakata tamaa na unapokata tamaa mapepo na majini ndio yanapoingia sasa hata kama watu watu wanakudharau, wewe linda sana Moyo wako kuliko chochote ulindacho, Ukisoma Neno linakaa kwenye moyo, kunaweza ukawekewa Moyo wa kutokuamini, moyo usiotaka kusoma Neno la Mungu, hukeshi, huombi hufungi, huwezi kushuhudia matendo ya MUNGU wala kuongeza watu kuja kanisani, huwezi kukaa katika utakatifu haya yote yanaanzia ndani ya moyo, sasa jichunguze. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
MUNGU huweka maisha yako katika moyo, na ukishakubali na kupokea yanatokea kimwili, ndio maana wanasema usicheze na MOYO ukishasikia kwenye ufahamu wako mambo yanaenda ndivyo sivyo, mawazo mabaya, hapo sasa ujue kuwa kuna ufalme mwingine umeshajengwa ndani yako na wameanza kudokoa moyo wako sasa amua usidokolew, usitikiswe na moyo wako usihangaishwe na ufalme wa Shetani, kwanini YESU alivyokuwa jangwani anaomba shetani akamfuata akaanza kumjaribu na endapo YESU angelikubali mambo ya shetani pale jangwani, YESU angelibadilika kuwa kama shetani lakini Moyo wa YESU ulikuwa strong, alisimama na Neno la MUNGU, imeandikwa mtu haishi kwa mkate tu na usimjaribu BWANA MUNGU wako, kwa hityo shetani anatakaga mtu afanane na yeye lakini kwa kujua na kutokujua, napenda nikufunulie kuwa kuna moyo mingi ya watu imefanana na shetani na wengine pia wamefana naye japo hawana mikia, meno marefu, na manywele kama yeye,. Unapokiri kuwa MUNGU ameshindwa hutashinda kwa sababu umeshakiri kwa kinywa chako kuwa MUNGU ameshindwa, unakuwa umeshajikiria na adui anaweka mambo yake sasa kataa moyo wa kushindwa, kukiri madhaifu kwa kila jambo ili MUNGU aweke ya uzima, Je unapenda kufanana na vitu vibaya? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Wengi pia huangamia kwenye maisha yao kwa sababu nafasi za mioyo yao wanawapa watu badala ya kumpa MUNGU, kuna magumu unayopitia kwa sababu masikio yako yanacontrol moyo wako, maana masikio husikia mambo mengi ndio maana nawaambia usipokee moyo wa uongo kwa sababu moyo wako pia utabadilika utakuwa unapokea ya uongo badala ya kupokea ya MUNGU aliye hai, Kila mtu ajiangalie, Je! Anafikiria mabaya mangapi? Na je unataka mwenzako apate mabaya na kumwombea au kumfikiria mabaya mangapi? Je! huo ni moyo wa MUNGU au wa pepo? kila baya au ovu unalofikiria au unafikiria kwa mwenzako ni Pepo linakuwa ndani yako hivyo basi utakuwa na mapepo kibao, unakula na Pepo, unalala na pepo unatembea nalo, unakaa na pepo unasali na pepo kila unachofanya unafanya na pepo maana Pepo ndio yuko ndani ya Moyo wako, sasa agalia usije kufa na pepo maana hata Mbinguni hutaenda. Tumepewa moyo wa kusamehe ila wengi hawasamehi, huwezi kumsamehe mtu, sasa usipomsamehe mtu unapata faida gani? Samehe songa mbele, usiposamehe huo ni Moyo wa kinyongo, kwanini watu wengi wanakufa na Presha kwa sababu moyo una shida na wengi wao ni vinyongo na kutokusamehe, lakini katika Moyo wako ukiwa amejaa YESU nakuambia hutakuwa na magonjwa wala mauti ila uzima, kwenda Mbinguni sio kwenda sokoni unajua hata kwenda Mbinguni lazima uwe na moyo wa kwenda mbinguni, hata mtu akitaka kukutapeli atakuwekea moyo wa kukutapeli ndio utaamini ndipo aweze kukutapeli. Na hata kwenye injili watakuwekea moyo wa kukudanganya, hivyo wakikuhubiria uongo utaamini, kwa vile wameshakuwekea moyo huo kiroho kwenye ulimwengu waroho, hivyo unakuwa umesha amini injili uongo hata ikija Injili ya kweli hutaikubali wala kuisikia kabisa. Tayari unakuwa mwana wa uongo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Soma Biblia, Nabii wa MUNGU Yohana zawadi ile, kutoka kwa MUNGU kuja duniani kuleta ubatizo wa maji mengi kama alivyoagizwa na MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia, akaja YESU nae akabatizwa hivyo hivyo ina maana hao wengine wanaoenda kubatizwa tofauti na alivyobatizwa YESU mioyo yao ni tofauti na Moyo wa YESU, wanakuwa wamebatizwa ubatizo wa uongo na wao watakuwa wafuasi wa uongo na mioyo yao ni ya uongo ila ili ufanane na YESU batizwa kama yeye abudu, mahali alipo YESU, kaa alipo, tunaelewana, mwamini MUNGU simama imara. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Zipo ahadi ambazo MUNGU ametupa amesema watashindana na wewe lakini hawatakushinda ila sasa kwenye moyo wako lazima kunakuwa na kitu ambacho MUNGU ameweka ili wakishindana na wewe wanaporomoka, sio unashindana na mtu kimwili, unamwangalia MUNGU, mioyo ya watu imeibiwa na wahubiri wa uongo, au wachawi wanapitaga usiku wanawanga, wanaiba mioyo ya watoto wa MUNGU na kuiunganisha kuwa kitu kimoja na yao, ndio maana watu ambao wapo kwenye nyumba za ibada ambazo zipo kinyume na MUNGU hata ukiwaambia kweli wao hung’ang’ana tu maana mioyo yao imeunganishwa nao, hivyo nao wanaona ni sawa, wako sehemu sahihi kumbe la. Neema ya MUNGU ndio inasaidia na kufanya moyo wako hautikiswi, nyakati hizi za hatari amua, kubali, umpe MUNGU moyo wako, na utaendelea kusonga mbele, Tafakari! Na ujiulize! Moyo wako ukoje? Umewekewa nini kwenye moyo wako? Ni kifo? majini au kitu Fulani?! Shetani hapendi mtu ambaye anatambua nafasi ya moyo wake, yaani mtu anayejitambua, anayelinda mkao wa moyo wake, (anamchukia sababu hawezi kuingia kwenye moyo wa namna hiyo, hakuna nafasi ya mambo ya shetani, ila ya MUNGU tu. Linda sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo) Na katika moyo wako anatakiwa akae MUNGU, YESU na Roho Mtakatifu. Ndani ya moyo wako mweke MUNGU tu na nawaombea mioyo yenu ikombolewa kwa jina la YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
“Baba Mungu katika jina la YESU asante kwa muda huu na wakati huu BABA, ninaikomboa mioyo yao katika jina la YESU, mioyo ambayo imeibiwa ambayo imebadilishwa imewekewa shida, kuasi na kukata matumaini iliyowekewa kuanguka, filisi, nguvu za giza, mali zimeporomoka, Nyota imerejea ila moyo unashida nami naamuru nyota yako na moyo wako ufanyiwe matengenezo sana kwa jina la YESU” www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Sema BWANA YESU ninakukabidhi moyo wangu, nainyang’anya miungu, majini, mapepo, mashetani mafundisho ya uongo, wanajimu ramli waganga, wachawi kila ambacho nilikikubali kikafanana na mimi na kikaharibu maisha yangu ikawa na mlango wa kunifuata mimi mpaka sasa, Mimi ninakataa katika jina la YESU na kwa damu ya YESU, ninaomba moyo wa wokovu wa toba, rehema, kukuamini kunyenyekea, kusikiliza wa kwenda Mbinguni wa kushinda ulimwengu na siku moja nifike Mbinguni katika jina la YESU Kristo wa Nazareti aliye hai. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mwenyezi MUNGU awabariki, awainue, nina hakika kuwa mioyo yenu imebadilika na hiyo ndio ishara kuwa maisha yako yamebadilika, kutembea kusimama, kuamini, kuomba, kufanikiwa na siku zako zimebadilika, ndoa yako imebadilika, miaka iliyokuwa imeibiwa imerejeshwa, moyo wa faraka na mahangaiko na kiburi kwa MUNGU utoke kwako, nakuombea moyo wa unyenyekevu hekima Selumani alipewa moyo wa hekima akapewa na wa utajiri nawaombea, Utakatifu na hekima na kuushinda ulimwengu, na wa utajiri wala usitoke katika maisha yako katika jina la YESU. Kuna watu waomba lakini hawapati nami naurejesha kwa jina la YESU ukapate sasa kwa jina la YESU Kristo wa nazareti nakuombea moyo wa kukesha, kumpenda MUNGU, ibada, kutokukosa Ibada, kumuheshimu MUNGU kuwa na hofu ya MUNGU na nakutenga na moyo wa mazoea na ukawaida. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org
Mwenyezi MUNGU awabariki, Mwenyezi MUNGU awe nanyi.
Imeandikwa na Nabii Hebron.