Pages

Thursday, April 15, 2021

KUKOMBOLEWA NA YESU VS KUKOMBOLEWA NA SHETANI

 Baba ninakushukuru asante kwa mda na wakati huu ambao unaenda kuwakomboa watoto wako kiroho na kimwili, pia asante kwa Neno lako, asante kwa Yote ambayo yatatoka katika meza yako ya ufalme wako, Mbinguni, nami Nabii wako nayapokea na kuyapeleka kwa Mataifa yote na kwa watoto wako wote, ukawatendee sawasawa na  upendavyo,  nikiendelea kuharibu kila kilicho kinyume na  mpango wa  MUNGU na mpango wako MUNGU ukasimame kwa dunia hii na kwa viumbe vyote ukasimame kwa wanadamu na ufalme wa shetani uporomoke wote, usiku na mchana na siku kwa siku  milele na milele. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Bwana YESU asifiwe, Penda kufunga jitahidi uwe unafunga katika kufunga kuna majibu na wewe uwe sababu ya kufunga, mambo mengine haya wezekani pasipo kufunga na kuomba. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Isaya 42:18-22 – Sikilizeni enyi viziwi; tazameni enyi vipofu, mpate kuona. Nina aliye kipofu ila Mtumishi wangu? Au ni nani aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu Kama yeye aliye na Amani? Naam, kipofu Kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi lakini hasikii, BWANA akapendezwa Kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sharia na kuiadhimisha. Lakini watu wangu ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo; wamefichwa katika magereza wamekuwa mawindo wala hapana aokoae; wamekuwa mateka wala hakuna asemaye rudisha.

Sio wale viziwi au vipofu wasioona kabisa ni wewe au yule ambaye hulisikilizi neno la MUNGU ndio unaitwa kiziwi, maana linahubiriwa lakini unalipuuza ina maana hukulisikia, ungelisikia ungelitendea kazi, Bwana YESU asifiwe, na wewe usiyotaka kuona kweli ya MUNGU ndio unaitwa kipofu unapenda au kutaka kuona vitu vingine tu ambavyo sio vya kweli ya MUNGU au vya utukufu wa MUNGU na vile vya MUNGU hutaki kuviona walakuviamini. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Usipende kusema kiziwi yule hasikii na kipofu yule haoni, la hasha! Na mimi naongea katika habari za Ufalme wa MUNGU, Bwana YESU asifiwe,  basi kama wewe ni kiziwi au kipofu ufunguliwe macho yako ili uweze kupata kuiona NURU, Kiziwi haelewi  kweli au hutaki kuisikia na kuiamini, na  kama na wewe uko hivyo basi  wewe ni kiziwi, lakini  pia shetani ana mambo yake anayoyafanya ili watu wasisikie neno la MUNGU  na kulielewa, unakuta hata si kiziwi lakini kimwili lakini unafundishwa  habari ya wokovu au utakatifu husikii, huoni ya MUNGU au hata huamini,  basi wewe unakuwa ni kiziwi na hiyo pia ndio dalili moja wapo, na sasa kama hata MUNGU humsikii u kiziwi basi na kwasabu pia hata YESU hutamwona.

 Kukombelowa kirihi; kuna watu wapo katika magereza mbalimbali na ni wafungwa kabisa japo  wanatembea, lakini ndoto unazoziota zinakuonyesha uko eneo fulani na zingine zinarudia na umeshindwa kutoka na unajua kwamba kila kitu kinaanza  katika ulimwengu wa roho, kama uko vibaya katika ulimwengu wa roho au kuna jambo katika ulimwengu wa roho au adui amekufunga katika ulimwengu wa roho,  pasipo kutoka hapo hakika hayatatimia mazuri katika mwili wako, unaweza ukaota mfano. Sasa hivi u mtu mzima lakini unaota upo shule ya msingi uelewe kuwa kiroho elimu yako ilifungwa sasa ni lazima utoke kule, hiyo ni taarifa ambayo  unapewa na roho Mtakatifu, endapo uko upande wa MUNGU unajulishwa kuwa umefungwa  mahali Fulani unatakiwa kutoka. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Unaota uko na watu waliokufa kila wakati ila maana uko nao inatakiwa utengwe nao na yamkini umeokoka na bado unaota ndoto hizo unatakiwa kuendelea kuomba kwa kwasababu shetani na jeshi lake hawalalagi, si kwamba eti  ukishaokoka ndio unalala miguu juu  na kukoroma hapana ni wakati wa kazi na ni wakati wa kupambana  maana kumbuka kuwa umetoka gerezani na watakutafuatilia ili wajue kuwa umekwenda wapi? Au ni wapi upo? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Kuna vifungo  aina tofautitofauti vya kiroho, vya mizimu, mapepo, majini nk Bwana YESU asifiwe,  Kuna vifungo vya mapokea ya wanadamu na endapo una hicho kifungo kwenye ulimwengu waroho unakuwa umefungwa na  wanadamu  na hautakaa uweze  kumwona MUNGU au kumwelewa kwa sababu una mapokeo ya wanadamu. Kuna baadhi ya watu wanajiita MUNGU na wanabadilisha neno la MUNGU na unapopokea mapokea hayo ya wanadamu unakuwa huwezi kumwona MUNGU na wala kumwelewa, kuna watu wanateseka pasipo kujua kwa sababu ya kupokea vitu ambavyo vinamfunga kwa kujua na kutokuja japo wanampenda YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Umewahi kujiuliza kuwa, Kwanini hapo mwanzo dunia ilikuwa haikombolewi? Kwasababu kulikuwa hakuna agano, ndipo MUNGU akamleta mwanaye YESU Kristo ambaye ni agano lake,  damu yake ikamwagika ili wanadamu wapate kukombolewa lakini cha ajabu wanadamu hawataki kulifuata hili agano la BWANA YESU wanataka kuyafuata maagano mengine. Matokeo yake unaharibikiwa, Maana yake ni hii MUNGU alileta mkataba wake kati yake na wanadamu ili aweze kumkomboa mwanadamu, Mkataba ambao MUNGU ameingia na wanadamu ni kuwa kila ambaye ambaye anataka kwenda Mbinguni lazima akutane na BWANA YESU kwanza, lakini baadhi ya wanadamu tena utakuta ni Mkristo ukiwaambia waingine mkataba na Bwana YESU hawataki lakini mtu huyo huyo anajifariji na anakuambia kuwa ataenda Mbinguni, anajipa matumaini lakini yuko katika mkataba feki kwa sababu hakumkubali YESU, hivyo basi wanadamu wengi wako katika mkataba feki,  lazima kwanza uingie mkataba  na BWANA YESU, umkiri yeye, ili uvunje mkataba na shetani maana kabla ya kuokoka unakuwa  una agano la shetani, agano la  la dunia hii, sasa lazima ukubali kuvunja agano ambalo ni la shetani na la dunia hii ndipo umpokee Bwana YESU,  Lakini wengine watakucheka kwa kuwa umeokoka amechanganyikiwa  lakini waambie kuwa hujachanganyikiwa maana wewe umeshika agano na unakwenda Mbinguni kwa MUNGU wao ndio wamechanganyikiwa, hao ambao hawajaokoka shauri yao, kumbuka kipindi cha Nuhu alipokuwa anatengeneza safina, alishika agano la MUNGU, na kulifanya na alifanya kazi ya MUNGU ya  kuwaambia watu wamrudie MUNGU ila watu walimcheka sana, na wengi waliangamia, na ndivyo itakavyokuwa ile siku ya unyakuo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Watu wengi hawana mikataba ya Kwenda Mbinguni kwa sababu wanaogopa watatengwa na familia, watachukiwa, wasikutishe hao hata YESU walimfanyia hivyo na walikuwepo toka zamani, ni bora utenge na wanadamu lakini upendwe na MUNGU, unajua hata mwenye nyumba anatoaga mikataba kwa mpangaji wake lakini endapo unamkataba feki   hata mwenye nyumba hawezi kuukubali ndivyo ambavyo hata watu watakataliwa siku ile kwa sababu ya Mikataba feki. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mimi alichonituma Bwana YESU kwa watu wote, ameniagiza nikavunje mkataba na shetani ili watu waokoke na kila ambaye anamtaka YESU ni lazima afute mkataba na shetani kwa kumkiri Bwana YESU, amwambie shetani mimi sikutaki lakini endapo unawaza moyoni mwako nikimfuata BWANA YESU haya mambo yangu nitayaachaje  mfano.  Pombe, uzinzi, ulevi, tabia mbaya, ufisadi, kiburi, wizi na mambo kama hayo huko ni kushikilia mkataba wa Jehanamu shauri lako, utachomwa Moto huo ndio ukweli na kama unang’ang’ania shauri lako. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

YESU alileta mkataba wa  kweli  na hata wa injili na hata baadhi wa wahubiri ambao walikuwa na mikataba ya uongo walimkataa  lakini alibakia kuwa BWANA  mpaka leo wale waliomkaa walikufa wote na YESU yupo, na ni BWANA mpaka leo sasa kwa nini usiingie mkataba na BWANA YESU?  Ametuma wahubiri sehemu mbalimbali wakuambie okoka kaka, baba, mama, au kijana lakini hutaki?  Wewe ndio unaendelea na mkataba wako wa makaburini, kuabudu miungu, kutoa makafara kwa shetani, kwa waganga, kufuga majini na mambo kama hayo. Unatakiwa uiache na uingie mkataba na Bwana YESU lakini wewe bado unafanya au umeshikilia maagano na mikataba na shetani. Utaangamia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mfano Ubatizo   - MUNGU ameleta ubatizo agano lake na wewe ili kila atakae ingia akafanyike kuwa mwana wa MUNGU, akamtuma Yohana na Yohana akamtengenezea YESU njia na YESU nae akatumika aingie kwenye maji mengi nae akabatizwa, mimi sikusikia au kuwa imeandikwa kuwa YESU alibatizwa kwa jina la Mchungaji, ila  baadfhi ya watu wamebatizwa kwa jina la mchungaji huo ni ubatizo feki jamani haifurahishi kwa  sababu kwa kufanya hivyo watu watachomwa moto  Mkristo tu bila matendo haifai, lazima uingie mkataba na Bwana YESU, najua haya hayakufurahishi kwa kuwa  ni ya kweli ila kama wewe haufurahi wala hupendi kuambiwa ukweli acha MUNGU afurahi kwa sababu  nimesema kweli na shetani anune tu, na wenye  mikataba ya shetani hawapendi habari za kweli, zizungumzwe lakini MUNGU atabakia kuwa MUNGU tu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

  Bwana YESU asifiwe,  yawezekana unateseka sana  kumbe ni agano ambalo umeingia umebatizwa kwa maji ya kikombe ukiwa mototo mdogo huo sio mkataba wa YESU na  mkataba wa YESU ni kubatizwa kwa maji mengi,  Neno likibadilishwa huo unakuwa ni mkataba mwingine kabisa,  sasa MUNGU hautambui huo ubatizo  hivyo lazima tu uwe na maisha yenye mateso. Mungu ili afanye  kazi anatumia mwanadamu na ili shetani afanye kazi nae anatumia mwanadamu na wengi wamepotea sana , mkataba wa MUNGU  ni kuwaombea watu bure lakini mkataba wa shetani mhubiri anauliza una shilingi ngapi ndipo akuombee  hii mikataba batili  iacheni na ikimbieni maana hata unapoikubali na wewe unakuwa umeingia mkataba wa shida. Matokeo yake unamalizwa unakuwa kwenye maagano pasipokupenda na solution yake ni kuifuta. Tunajua dhahiri kuwa MUNGU akiingia mkataba na wewe utaishi na si wa shida ila unaweza ukajiona kuwa umeingia mkataba na maagano na MUNGU lakini yamkini ya shetani bado umeshikilia au hujayafuta matokeo yake utaendelea kuteseka www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Bwana YESU asifiwe, kwa MUNGU kuna kila kitu tatizo ni maagano / viapo kuna maagano ya Imani, Imani yako imeumbwa umwamini MUNGU aliyeumba Mbingu na Nchi ila Imani yako ikatekwa na mapokeo ya wanadamu, ikabadilishwa unaenda kuwaombea wafu Imani yako inakuwa na maagano nao wala hutamwona MUNGU, kuna watu wanahiji kwenye makaburi, mfano. Nimekufa na watu wanaenda kuhiji kwenye kaburi langu, sasa mwanadamu nimekufa nitakusaidia nini tena? Jiulize, hata kwenye kaburi la YESU pale Yerusalemu hakuna upako wala lolote, katalii tu kama mtalii usiabudu wala kusujudia maana YESU hayuko pale, kuna baadhi ya watu na baadhi yao walikuwa wachungaji na walishakufa miaka mingi sasa watu wanaenda kuomba kwenye makaburi yao wao wamejifanya YESU, hivi wao watakusaidia nini? Wamekufa na hawajafufuka kama YESU na wao sio YESU, mmeelewa na kuna watu ambao wao wamejifanya YESU katika hii dunia, eleweni jamani ngoja niwaambie ukweli mwanadamu gani amepaa Zaidi ya Elia, ya Enoko,  na  pia Bwana YESU?. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Napenda niwambie kuwa hata sasa mchezo huo upo,  mtu anakufa wanaedit na wanasingizia amepaa huo ni uongo na ulaghai jamani  kuweni wajanja jamani. Eti  mtu mwanadamu amekufa na akafufuka na amepaa hayuko kaburini wanajifananisha na Bwana YESU,  YESU ni mwana wa MUNGU wa pekee , Mtete YESU. Na hata sasa kuna maagano ya mavazi mekundu, meupe, yanjano, yablue nk. Hilo agano la mavazi halikupeleki Mbinguni aiseee, Utakatifu ndio agano lako wewe na Bwana YESU na sio mavazi, maana kuna baadhi ya wahubiri wamedanganya watu kuwa kuna baadhi ya mavazi uklifaa unakuwa mtakatifu mfano. Meusi, meupe njano kijani nk. Jiangalie hapo ulipo kwa vazi ulilolivaa jitadhmini je! Huna dhambi?  Wewe kama wewe Hununi, hukasiriki, hugombani, huna wivu, hutukani hujampinga MUNGU nk.  Je! Ndio kuwa Mtakatifu kupitia vazi? Enyi watumishi mnaojiita  wa MUNGU kumbe sio hebu acheni kucheza na akili na wanadamu. Kataa kumwita mwanadamu MUNGU kataa, tubu acha, na kama unaendaga kwa wanganga na una vitu vyao hebu kataeni  hayao maagano na kama una vitu vya waganga hebu chomeni maana unavyoendelea kuvishikilia vitu hivyo, hivyo hivyo ndivyo ambavyo majini na mapepo yataendelea kuingia na kutoka na kufanya mkao kwako na kuharibu vitu vyako . www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Na leo kubali hayo maagano yabomolewe na tunabomoa katika Roho,  utoke maana utakuwa ni mtu wa kulia,  huharibikiwa na hatimaye jehanamu, wengine mlikuwa mkifanya ibada za wafu (ibada ya wafu ni kumwomba mtu aliyekufa akusaidie au mtu alishakuwa kila mwaka mnafanya kumbukizi ya ile siku aliyokufa)  Je! maagano yale umeyavunja? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Ukiwa mfungwa huwezi kujifungua lazima liye huru ndiye akufungue. Bwana YESU asifiwe, hata mchawi akikuloga anakufanyia maagano yake lazima akufunge na ndio maana hata mchawi akikuloga akakushindwa au akaporomoka huwa ameshindwa masharti na anapigika na hata hapa baadhi yenu mlikuwa washirika wa waganga na wachawi na mambo kama hayo mkapigwa, na mkashindwa na mkapigika, si kweli! Sema ukweli na msema ukweli ni mpenzi wa MUNGU. na wanadamu wengi waliingia mikataba ya wachawi / waganga ili apate mke/ mume/ pesa watoto, wengi wameshindwa wakaporomoka na wenye Neema walimrudia MUNGU.  Mchawi anaweza kuingia agano na wewe kwa kujua au kutokujua akawa anatumia vitu vyako wewe ukawa huna chochote kwa sababu ya maagano yake yeye akafaidika na kunufaika kupitia wewe. www.prophethebron.or.tz

 MUNGU ana agano na wewe la maisha mema, mazuri yenye Baraka za kiroho na kimwili sasa wako wapi wa kusababisha upate hayo?  Utabakia na ukristo wako na unalia machozi ni vifungo, vifungo, vifungo na baadae unabakia kusema MUNGU hanijibu mimi, hufanikiwi na hatima yake huna chochote kwa sababu ya maagano ambayo umeingia wewe,  na wengine si uchawi ni dhambi na ukitenda dhambi vitu vinafutika,  vinabomoka, vinaharibika, kumbe mengine ni dhambi!  Acha dhambi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Kuna Maagano ya kula kwenye ndoto, na ukila hutajua kuwa ni maagano gani ambayo umekula kwenye ndoto, chakula au chochote ulichokula kwenye ndoto kimekuathiri katika maisha yako au hujui kuwa kimetamkiwa nini? Yaweza ukaona kuwa unakula chakula kizuri kumbe ni nyama za watu na unaweza ukaota unakunywa kumbe ni damu za watu lakini kimwili huwezi kukubali kuwa ulishawahi kula nyama au damu za watu,   Chakula cha ndotoni ni kibaya sana na mambo hayo ya wachawi ni mabaya sana lakini nitapita kwenye maombi ya kuvunja maagano, agano ni kiapo yamkini umekaa mda mrefu sana lakini una maagano ya ubatizo wa kikombe hutafanikiwa, hebu fikiria mfano umeandika mkataba halafu mtu mwingine akaubadilisha kinyume na kile ambacho kilikuwepo awali je utausaini? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Angalia duniani  mkataba wa ubatizo baina ya MUNGU na mwanadamu hakuna, na hili somo la ubatizo halifundishwi kabisa na ukiliangalia watu hawafundishwi  kabisa na wanaliogopa na wengi hawajui ukweli,   Hebu tafakari kwenye ubatizo halafu tulinganishe na mkataba ambao aliuleta MUNGU (YESU alibatizwa kwa maji mengi ndio mkataba wa MUNGU kuwa kila mwanadamu abatizwe hivyo, tena mtoni, tena maji yanayotembea,) sasa wanadamu wengi  wameshapokea mkataba mwingine na ile siku ya mwisho MUNGU atakuambia sikujui! Sikujui!  Unakuwa mbuzi lakini hupendi kuwa mbuzi lakini unaweza ukafanywa kuwa mbuzi Mbuzi anaenda mbinguni? Kondoo Je? Wewe ni kondoo au mbuzi?? Amua kuwa kondoo wa Bwana YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Mikataba aliyowekea watoto wadogo ni kubarikiwa na sio kubatizwa, na kama umebatizwa ukiwa mtoto huo ni mkataba batili ya wanadamu na ukiwa umefaniwa hivyo basi utatoa fungu la kumi, utasali sana sala ya baba Yetu aliye Mbinguni,  utapiga makofi, utatoa sadaka, lakini  unakuwa umewatolea majini, mapepo lakini  laiti kama mtu alipozaliwa tu, angelikuta njia yake ni njema imeandaliwa kiroho  kungekuwa hakuna shida kwa wanadamu maana mambo yangelikuwa  yananyooka, ungeliomba baba MUNGU unajibiwa bila shida, tena haraka, pasingelikuwa na mateso  Bwana YESU asifiwe. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mfano: Mwisho wa mwaka Watu wa makabila mbalimbali huweka watu wao kwenye maagano mbalimbali ili wasifanikiwe na wasimwone MUNGU, wakudhibiti nk. ila watakupata endapo hukuwa na agano na YESU unakuwa zero zero zero eee,  lakini ambaye uliingia agano na BWANA YESU kwa sababu unamkataba wa kulindwa, kupendwa, kuitwa mwana wa MUNGU aliye hai na mkataba ambao siku moja  utafika Mbinguni hawatakuweza wao ndio wataporomoka. www.prophethebron.or.tz/

 Imeandikwa usiabudu sanamu  moyo wako na Imani yako ndio umeamua  na kuling’ang’ania sanamu au nyumba ya ibada yenye sanamu agano hilo linakutesa ila  MUNGU wa mbinguni yeye hanaga  vitu hivyo unajua hata mahakani kipengele vya sheria vinasema 1,2,3 na mwingine akisoma ni 1,2,3 vyote vinafanana, siku ile  ya mwisho itafunguliwa Biblia na ndio kitabu ambacho kitakachokuhukumu  ulifanya nini na kitabu kinasemaje?  Usiabudu sanamu haya utasikia mpeleke kule huyo amekuwa mbuzi (mtenda dhambi) usipende maombi ya Baraka, baraka ujue kweli,  penda kwanza kuupata ufalme wa MUNGU na mengine yote mtazidishiwa  unaweza kuvutwa  na mtu na ukaenda, kumbe kakuvuta kichawi na sio kwamba eti ukiwa mtumishi hulongwi hata YESU alikuwa analongwa lakini alikuwa anapigana vita kiroho ila kuna baadhi wakiwa watumishi au anaimba kwaya wanasema ndio basi silogwi tena, my friend unalongwa, na kwa vile umeacha kuomba unalala tu hali yako inakuwa mbaya ila kumbuka kuwa hakuna kitu kibaya kama kujisahau au mazoea ila ni wakati wa kupambana na kuomba Zaidi. Kumbuka safari yako ya Mbinguni unakwenda kiroho na baraka zako zinakufuata kiroho ndio maana mwili unabakia hapa, tembea katika njia yake na agano lake na patano na kila ambacho kitakugusa kitaporomoka. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Acha kwenda kuingia agano na wachawi na kuogeshwa na waganga, ambao wanakuambia vua nguo, chini ya mti, makaburini, nyumbani kwao au mahali pa wazi hadharahi uchi!  Huoni aibu? Amua leo ukavunje maagano maagano ya kiroho ya kifamilia ya kuridhishwa ndio maana unasikia baadhi ya watu wanasema kwetu tuko hivi, hatuoi, hatuolewi, kuna mila, unaoa au umeolewa unafanya mila?  Mambo ya mila achana nayo, waambie kwetu Mbinguni sinaga hayo maagano, wengine hutemewa mate, sasa mfano huyo anayemtemea mate mtoto ili ambariki kama je anaugonjwa? Mate yanabariki? Mwanadamu atatamka tu, abarikiwe na  ainuliwe ila  anayebariki ni MUNGU katika roho na hatimaye kimwili, na  endapo mwanadamu huyo anayembarikia mtoto ana mwabudu MUNGU aliye hai ila kama huyo mwanadamu hana MUNGU matokeo yake  atabarikiwa na miungu au mizimu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mikataba ya kabla ya kuoa kupromise wanaume au wanaume wengi au hata wale ambao ulikuwa na mahusioano nao kimapenzi, Je! umeivunja? Kutoa Mimba je? Wanaume wengi wanajidanganya kuwa wao hawatoi mimba ila kumbuka kuwa alishiriki kuiweka na hata ikatolewa alishiriki kwa namna moja au, nyingine na lipo agano la kukataa au kutataliwa wababa wengi hukataa watoto wao wanalia tu huko waliko wana taabu utadaiwa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

                Unaota unaandika una hujui ukiandikacho unaweza kukuta ni saini, ni mikataba ya shetani, ni kufilisika, ni kukubali mambo mabaya, unaota unanunua kumbe kimwili hutakaa ununue vitu. Angalizo. Ziko ndoto za MUNGU na shetani na pia ziko ndoto za wachawi kuvaa sura Fulani unaweza mwona mtu kama mtu Fulani ambaye unamjua kumbe laaaaa ni nguvu nyingine.  www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

                Watu wengi huwa wanaota ndoto ambazo sio za MUNGU kwa sababu wenyewe hawana MUNGU sasa utaotaje ndoto za MUNGU aliyeziumba Mbingu na dunia wakati wewe una maagano mengine? Ndio maana wengi wanaota na mabaya yanawapata kwa sababu hawana MUNGU. Unaweza kuoteshwa ndoto na shetani kuwa utakuwa hivi utakuwa hivi unabakia kusubiri tu hufanikiwi hata, angalia  mfano wa maisha ya watu ambao wanapendaga kusema nimeonyeshwa, nimeonyweshwa nimeona kwenye ndoto au maono fuatilia maisha yao, wengi maisha yao ni mabaya yenye vifungo kwa sababu sio MUNGU awaonyeshaye ila shetani kwa sababu hawana mkataba na MUNGU wa Mbinguni. Ingia agano na YESU kiri sala  ya toba,  okoka, batizwa  mfuate YESU mahali alipo maana hata madhabahu kama haina YESU inakuwa mahali pa shetani unakuwa unaendelea kupoteza tu, maana kila ukienda mahali alipo MUNGU unajazwa nguvu za MUNGU na kila ukienda mahali ambapo MUNGU hayupo unajazwa nguvu za shetani, mizimu, miungu, mapepo na majini. Wanaendelea kukufunga na kukushikilia sana, kama huna MUNGU lazima miungu Ikushikilie. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Karafa lolote ambalo wanadamu miungu shetani analokushikilia MUNGU ataliondoa, wanataka uwe ovyoovyo, ufe, wao ndio watakuwa hivyo. Ila amua kaa kwenye agano lake na Neno lake mabaya hayatakupata lakini sio unaka kwenye neno lake lakini linauwongo, mhubiri anayekutoza fedha ni wa shetani,  na endapo umetoa sadaka kwenye chombo cha sadaka mahali ambapo hakuna MUNGU  na wewe utafilisika maana itanena mabaya sio mema maana hukutoa kwa MUNGU maana ukiitoa kwa MUNGU inakuwa manukato mbele za MUNGU na endapo ukiitoa kwa Miungu inakuja harufu Mbaya  sana kwako uliyetoa, Nuksi, balaa mikosi pia watoto wa maagano wanatafutwa kwa waganga na wachawi, maagano ya chale mwili umeuchanja, tatooo, nk. Ni hatari Sana kumbuka mwili wako ni hekalui la MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Rejeeni kwa YESU, ili muingie mkataba naye, msajiliwe Mbinguni, mkabatizwe, ili MUNGU awajue lakini baadhi ya watu hawataki mnasema badobado, nakula raha, ndugu moto unakuja, wengi husema jamani dini ya baba yangu na mama yangu, ujue kuwa dini haikusaidii hata YESU alizikuta akasema ndugu zangu ni hawa wanaomwamini MUNGU. Ingieni mkataba wa kuwa na MUNGU usisumbukie upendo wa kinafki ambao unaishia hapa hapa duniani na mbaya Zaidi mtu au mwanadamu humpenda mtu akiwa nacho, vikiisha ndio basi tena, na upendo wao mwingi ni wa kukuunganisha na miungu na sherehe ambazo zinakujumlisha kwenye agano la miungu / shetani. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

                 Baadhi wa tatumishi wamekuwa  kama wameparalize / kupooza  akili zao wao hawafanyi kazi yeyote wanabakia kuomba, hawafanyi kazi na ni tegemezi kuomba si kubaya ila kama huna kazi ya mikono  yako MUNGU atakubarikia wapi?  na hatima yake wamekuwa mzigo kwa waumini wao kabisa, kuwagongea nyumbani kuwaomba hela za matumizi yao binafsi, kuwafanya ATM machine, wanawachosha na endapo muumini atamwambia mtumishi sina fedha au hicho ambacho amemwomba, mtumishi anamlaani na kumchukia muumini. Tazama akina Daudi, Sulemani na watumishi waliotangulia walikuwa na mali zao jamani. Ni wakati wa mwisho unakuja kataa hayo maagano jamani. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

                                 MUNGU ameleta agano lake umpokee kwa kinywa baada ya hapo uende mtoni ubatizwe hutaki, lakini ungejua ukweli usingepotezwa ila heri yako wewe unayenyenyekea mbele za MUNGU.

Sala ta Toba. Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele nakuomba BWANA YESU uniondolee maagano yote na mikataba niliyoingia kwa  shetani na jeshi lake kwa kujua nakutokujua, mikataba  ya dini, ya majini, ya mila, ya makabila, ya mapokeo ya wanadamu, kiimani na kimwili niliyoyapokea na hata ubatizo wa uongo naomba Bwana YESU niondolee  sasa ili niwe tayari kuingia agano lako kiroho na  kimwili na kuukubali  ubatizo wa maji mengi. Nakushukuru Bwana YESU kwa kuniokoa. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Damu ya YESU ivunje maagano yoyote uliyoingia kwa kujua na kutokujua, ya waganga wachawi, mizimu miungu, kutokuolewa, kutokuoa, hampati watoto, kutokufanikiwa, kutokuwa na Imani, kutokuwa na baraka za kiroho na kimwili, magonjwa, nuksi balaa na mikosi, agano la kutokuwa na Amani na mengineyo yote, ninayavunja kwa jina la YESU. Baba katika jina la YESU nawafungua na nawaombea wavuke salama katika jina la YESU, kuna watu wako nusu nusu, nusu mti, jini, mti, sanamu kwa mamlaka ya jina la YESU mrejeshwe kwa jina la YESU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 

Tunza agano lako na BWANA YESU mtu asikutoe tena. Amen.

 

Imeandikwa na Mtume na Nabii Hebron