Pages

Thursday, April 15, 2021

KWANINI WACHAWI WANAKUTOLEA SADAKA KWA SHETANI?

BABA ninakushukuru nalibariki jina lako na kulitukuza mfalme, nazidi kuliinua Neno lako juu sana mfalme wa wafalme, na Neema yako, na malaika wako, naendelea kuomba toba na rehema na naendelea kualika Jeshi lako na malaika wako na utukufu wako ukaendelee kukurudia MUNGU.

 BWANA Yesu asifiwe, Mkono wa MUNGU unakwenda kutenda jambo, kwa kila mtu, maana MUNGU alifanya kwa mkono wake, akaumba na vingine alitamka na kwa Mkono wake utafanya jambo kwako. Napenda tujifunze jambo moja ambalo pia nitapita katika maombezi, BWANA YESU asifiwe, anza kujiuliza ni kwanini wachawi wanakutolea sadaka?  Kwanini mizimu wanakutolea sadaka?  Kwanini wanadamu wanakwenda kukutolea sadaka kwa mizimu au majini au mapepo kuna nini? Bwana YESU asifiwe, umewahi kujiuliza sababu ya wao kufanya hivyo au wanapata nini au wanafaidika nini wakitoa au kukutolea sadaka kwa mawakala wa shetani na hatimaye shetani huzipoke? (Mwakala wa shetani mizimu, mapepo, majini, waganga, wachawi, miungu nk)   Wengine wanatoa sadaka kwa ajili ya kuchinja, Kuna nini? na wanakutaja jina kabisa au kuitaja familia yako, Je! kuna nini?  Bwana YESU asifiwe.

Somo: 1Wakorintho10:14-22 – Kwa ajili ya hayo, wapenzi, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi nilinenalo. Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja, Waangalieni hao waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, Je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilicholotewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile watoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani. Hawawezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani, Hamwezi kushirikiana meza ya Bwana na meza ya mashetani, Au twamtia Bwan wivu? Je! Tuna nguvu Zaidi ya yeye?

Bwana YESU asifiwe, Neno la MUNGU linasema habari ya mkate na mkate ni mmoja, siongelei habari ya mkate wa dukani, naongea habari ya Neno la MUNGU, ndio mkate amabo Roho zetu zinaula, Neno hili tunapolila la kweli tunakuwa mwili mmoja na BWANA YESU, lakini mkate huo huo ambao ni Neno  la MUNGU likifundishwa tofauti tu na likiwa tofauti tayari huwezi kuwa mwili mmjo na Kristo kwa sababu mkate huo umeshakuwa tofauti na YESU unakuwa au unageuza neno hilo kuwa la ufalme wa shetani, maana ni tofauti na amagizo ya MUNGU.

Neno la YESU linasema, Je! Mwatoa sadaka kwa MUNGU na kwa mashetani? Je! MUNGU anashiriki na shetani katika meza moja na shetani hapohapo? Mwataka kula meza moja na MUNGU na shetani Je! Yawezekana?  Ni habari ya neno la MUNGU,  mfano wewe ni mshirikina  unakuwa unakula meza moja na mashetani  mfano, kama unafanya matambiko unakuwa unakula meza moja na mashetani, ukiabudu mizimu unakula meza moja na mashetani unapotoa sadaka ya kumloga mtu unakuwa unakula meza moja na shetani, lakini ukiwa unamtolea MUNGU katika roho na kweli na katika madhabahu ya MUNGU ya kweli unakuwa unakula meza moja na MUNGU na kushirikiana na MUNGU, watu wengi wanamchukia shetani lakini wengi wanakula meza moja na shetani kwa kujua na kutokujua, unapoabudu sanamu unakula meza moja na shetani, na kila baya unalolitenda au kumtendea mtu  kwa hila na kumtolea sadaka kwa wachawi, waganga,wala meza moja na shetani, kwa sababu huo mkate sio wa BWANA YESU, BWANA YESU haukugawanyika, hivyo mkate huo ambao ni Bwana YESU haushirikiani na mashetani, Bwana YESU asifiwe. (Kumtolea mtu sadaka ni pale unapopeleka jambo, hoja, mtu, ombi kwa mganga au hata wewe unapoenda kwa mganga mganga anakuagiza leta kitu Fulani hiyo ni sadaka, hapo unakuwa unamega na kula katika meza moja na shetani)

Hapo awali kulikuwa na asili ya kutoa sadaka na hata mababu na mababu walikuwa wanatoa sadaka mbalimbali, kwenye ukoo, mila, kwa mizimu, Jiulize je! Walikuwa wanamtolea MUNGU? Jibu ni hapana watu wale walikuwa wanakula Meza moja na  mashetani, wanakaa meza moja na mashetani na hata kama umeolewa au kuoa au mtoto kuzaliwa au umeoata mali halafu ukafanyiwa matambiko ujue umekaa meza moja na mashetani na Zaidi  unapokuwa umeenda kwa mganga unakuwa umeenda kutoa dhabihu yako kwa mashetani.

Ukisoma biblia Kaini na Abela wakati walipokuwa wakimtolea MUNGU sadaka, sadaka ilikuwa inanena, kwasababu MUNGU anataka sadaka na shetani anataka sadaka, napenda nikufundishe jambo moja na sitaki uhangaike kwenye maisha yako na leo nataka nikufundishe  jambo ambalo tutakapoenda kuomba hutakaa usikie mchawi anasimama kwenye maisha yako  kabisa, kwa sababu wachawi hawana hata pesa, shetani ni masikini lakini shetani aliwafundisha watoto wake, wafuasi wake, wa ufalme wake watoe sadaka, zile sadaka wanapozitoa, wanazozitoa kwa ajili ya maombi yao kwa shetani, yamkini anataka gari, nyumba, mke, au mali, umaarufu, cheo nk. Na itategemea ameagizwa sadaka ip;I na mganga,  anaweza kuambiwa atoe sadaka za damu au hata za kuua mtu, akishatoa sadaka, shetani anazipokea na maombi yake na sadaka zile alizotoa zinapokelewa na shetani na kuambatanishwa na mapepo na majini toka katika ufalme wa shetani, kwa sababu zimepokelea kwa shetani zinapotumwa zinaenda kunena mabaya juu ya maisha yako, yaani zinaiba vya MUNGU ambavyo amekuwekea na kukuachia mabaya, maana shetani hana chochote, Baraka anazobariki watu huiba kwa wabadamu wengine kwa agano la sadaka/ makarafa mbalimbali na shetani hutumia namna ya  kuwaelekeza  wanadamu wakatoe sadaka kwake , nae shetani hutuma jeshi lake kwenda kuiba vitu vya wanadamu wengine au vya yule ambaye mwanadamu husika amekusudia kumloga. Hivyo kila anayekwenda kwa mganga mchawi, mshirikina kutafuta vitu huyo ni majangili, lakini nataka hao majangili wakamatwe sasa, (Huwa Wanaiba kiroho na yanatimia kimwili).

Yesu akafanyika sadaka kwetu sisi tukakombolewa na tukapata wokovu ili mimi na wewe tuokolewe,  MUNGU aliiingia  gharama na baada ya hapo tulizaliwa na Baraka zetu, lakini mchezo anaoufanya shetani huwatumia wanadamu na kuziiba kwa kutaka kupelekewa sadaka na wanadamu hivyo hutafuta hila  hufanya hila  ya kuiba mfano. una watoto wazuri wanakusaidia, watakuwa  na mnafanikio, wanajua watakuwa hivi, wamesoma, wanamaisha mazuri  wana Baraka njema,  maana  mashetani nao wanaona katika ulimwengu wao, hivyo yule ambaye anataka kuharibu au kuiba Baraka za walengwa, akienda kwa mganga,  huambiwa na mganga (wakala wa Shetani) leta kuku, au mbuzi au kitu Fulani ili watoto wako wawe kama wale, hivyo huiba Baraka za wale kichawi, kipepo, kishetani, kwenye ulimwengu waroho na kuwapa wale ambao wamemtolea sadaka (agano la damu, agano la sadaka) na wale ambao Baraka zao au maisha yao yameibwa kwa njia hiyo wao huharibikiwa,  ndio maana ndoa, familia, vyeo, mipango mingi ya watu imeharibuka pasipo wao kujua, wanashangaa mambo hayaendi, vitu vimekuwa ndivyo sivyo, wanateseka, kumbe wameshawahiwa na sadaka ambazo zimetolewa kwa mashetani na zinanena mabaya kwao.

Nataka nipite kwenye maombi ili kuharibu hii biashara ambayo imefanyika miaka na miaka ya kuibia vitu vyako na vya watoto wqa MUNGU kupitia sadaka, nataka tumalize yaani waizi hao waishe na vitu vyako, Baraka za kiroho na kimwili zirejeshwe, uwezo upo, mamlaka yako, Je! Unajua kuwa unaweza ukaa nyumbani kwa mtu na pale kwa mtu yule kama ni mchawi au kuna mizimu, ile mizimu inaiba vitu vyako, kutokana na sadaka walizokuwa wametoa au wanazotoaga? Wao wataiba vitu vyako vyote, wewe unabakia huna kitu wakati MUNGU amekupa Baraka zako.

Lakini pia kunakuwa na fungu la kumi ambalo tumeagizwa kuto kwa MUNGU, ambalo wanadamu wengi wamekuwa waizi hawapendi kumtolea MUNGU usipotoa fungu la kumi shetani anapata nafasi ya kukuibia maana Fungu la kumi ni agizo kutoka kwa MUNGU ni sadaka ya MUNGU na fungu la kumi unatakiwa utoe mahali ambapo MUNGU na injili ya kweli inahubiriwa na jina lako limeandikwa na MUNGU sio kila mahali. Watu wengine hutoa fungu la kumi kwa yatima, wajane, wahitaji, ndugu, jamaa na marafiki kama msaada, Je! Hayo ni maagizo ambayo yameandikwa kwenye biblia? Je! MUNGU ameagiza hivyo! Jibu ni Hapana. BWANA YESU asifiwe, ukitoa fungu la kumi mahali ambapo husali au mahali ambapo ni madhabahu ya kinyume na MUNGU je! Utabarikiwa hapo? Je ndipo maisha yako yalipo? na jina lako?

Unaweza kutolewa sadaka kwa mashetani, utajitahidi sana kufanya jambo hutakaa ufanikiwe, unaweza kujiuliza mbona nashindwa, kwanini, nimekosea nini na wapi, ni kwa sababu mashetani yanakuwa yameshaenda kule  ili jambo lile lisitimie,  inakuwa hivi shetani anakuwa ameshatangulia au kutanguzliza jeshi lake kwenye jambo lako hilo  kwa njia ya wizi na hutakaa ufanikiwe. Unaweza kushangaa mabasi, ndege zinaangushwa, ajali inatokea wewe utaona kuwa watu au mtu Fulani amefa au amekuwa kilema au jambo baya limempata, kimwili hutaelewa sana utaona ni ajali ila kama ni sadaka, shetani hutuma watu wake haraka na kuiba au kuviiba vitu vya watu wale na kuwapa wale ambao wamemtolea sadaka, basi mhusika aliyetoa sadaka kwa shetani hufanikiwa Zaidi ndipo utasikia au kuona ameongeza kiuchumi nk.  Lakini wewe au yule ambaye vitu vyake vimeibiwa na shetani hali yake inakuwa mbaya maana wameshaiba vitu vyako wewe unafilisika, kuna wanaua ndugu, au watu wanakufa sana, au wafanyakazi wanakufa sana ile ni sadaka ambayo mtu hutoa ili yeye afaidike hivyo basi  napenda nikufundishe  jambo ili hata wakifanya inakuwa ni zerozero na waporomoke kabisa haleluya!. Unaweza  sadaka ikatolewa kwa ajili ya watoto wako, kazi, maendeleao,  vikawa vituko tu mpaka ukajuta kwanini nimezaa, unabakia kulaumi, ukoo ukawa tu haueleweki, mkawa hamtaki wokovu na mashetani hufuatilia  hamtakaa muokoke wala kumtafuta MUNGU wa kweli na hata mkiokoka hamtasimama kwenye wokovu sadabu ya sadaka mlizotolewaga kwa mashetani, pesa yako yenyewe inaweza ikatolewa sadaka  hupati pesa au ukapata ila zinapita tu kama njia hufanyi wala hutafanya kitu kamwe, nataka tuwakomeshe uwezo upo. Unaweza kutolewa sadaka usiwe hata na kiwanja, mwizi tu yule aliyekuibia ndio atakuwa na kiwanja na kujenga hivyo sasa hata nyumba nyingi  pia ni za dhuluma za kuwaibia watu vitu vyao kiroho yamkini huna hata nyumba moja ila yupo jamaa ambaye anamajumba na mali nyingi anazomiliki ambazo ni za kwako pasipo wewe kujua na wengine pia wanakuwa wameingia share au mkataba na mashetani kiroho pasipo wewe/wao kujua.  Watu wachache sana wana mali ambazo wanamiliki kihalali.

Unaweza kuwa ni  mchungaji au mwinjilisti au mtumishi wa MUNGU kwa namna ambavyo MUNGU amekuita, unakuwa umetolewa sadaka ambazo zinakufanya usikae na MUNGU, usiwe na utulivu usiweze kumtumikia MUNGU usiwe na kanisa na usiweze kufanya kusudi la MUNGU, unakuwa unyumba yumbayumba, hujielewi, nguvu ya sadaka ya mashetani inakuwa imekutangulia na inanena mabaya juu yako ili kukutenga na MUNGU, unajua sadaka inanena ndio maana hata kwa Mgerasi na YESU, YESU aliwaambia kuwa waondoke wakasema tuacheache , lakini walimtii YESU kwa sababu YESU mwenyewe alifanyika sadaka kwa watu,  ndio maana jeshi lile la mapepo lilimwachia.

Kuna sadaka ambayo hata wewe unatakiwa kuitoka kwa MUNGU, unamwambia MUNGU  kama mimi  wananitolea sadaka na mimi natoa sadaka yangu ya kunilinda, hata kama wakifuata vitu vyangu sadaka yangu ninayoitoa kwako MUNGU ikanene wasivione sadaka hii iwanyamazishe iwapige, Naona wachawi wanaanza  kupasuka mbavu hivyo tutawanyang’anya mpaka senti ya mwisho aiseee, Hiki kiburi  cha sadaka kiko kila mahali, mfano. Ofisini wanatoaga sadaka kunyang’anyana vyeo au kuchafuliana kazi au hata kufukuzana kazi, unakuta cheo ni chako lakini hupewi lakini utajikuta wanasema imekuaje? Unakuwa pale hupandishwi cheo sasa jibu ni kuwa wapo wanaotoa au waliokutolea sadaka kwa  mashetani wewe unakuwa pale tu sasa amua,  kutoa kwa MUNGU alioye hai ili ulindwe usikubali  wale ambao wanatoa kwa mashetani wakushinde, Unakuwa umeshindwa na hao wanaotoa kwa mashetani kwa sababu umeshindwa kutoa sadaka yako kwa MUNGU aliyekuumba. Kumbuka wakikuwahi wanakuibia Baraka zako halafu unarudi nyuma tena mpaka upate Neema ya MUNGU ya kukutoa katika mkono washetani.

Toa sadaka kwa ajili ya ulinzi wa vitu vyako, familia yako, Nchi na watu wa MUNGU pia,  shetani hatoagi  vitu vyake bure, yeye mwenyewe ni mwizi huiba hivyo basi lazima .akupe kwa gharama kubwa, lakini  MUNGU tu ndio hutupa vitu bure sasa yatupasa sisi tuviwekee ulinzi kwa njia sadaka ili visiibiwe kipepo kwenye ulimwengu wa Roho,  Ukiweza  kutoa sadaka zako kwa MUNGU kila mara kwa ajili ya ulinzi au maombi ya namna tofauti, tofauti vile ambavyo unahitaji MUNGU akutendee basi  changamoto katika maisha yako zile za kuona umeishiwa, huwezi, umekosa au kufukuzwa kazi, umeshuka kiroho, huwezi kuomba na mabaya mengineyo mengi yataisha, sadaka yako uliyoitoa kwa MUNGU itakuwa ulinzi,  hutarudi nyuma tena.

Wakati tulipoanza huduma hii, wapinzani wa MUNGu walikuwa  wakijitahidi sana kutoa sadaka na zingine zilikuwa zinaleta mpaka kwenye milango ya kanisa, sadaka za aina mbalimbali  tunazikuta mpaka za kuchinja na kutupa vitu vibudu hapo, lakini nilipata Neema ya kufundishwa  na nilikuwa natoa sadaka kwa MUNGU kwa huyo hizo za kipepo, za kumpinga MUNGU kwa maombi yao waliokuwa wakifanya ili jambo hili laMUNGU lisiendelee hazikufanikiwa ila zile ambazo nilitoa na kumwomba MUNGU ulinzi zilinene kwa MUNGU Mbinguni zilinena na ndio maana mpaka sasa kanisa  linaendelea na watoto wa MUNGU wanazidi kubarikiwa kiroho na kimwili.  Kumbuka kuwa pia kuna baadhi ya wahubiri ambao wanatumia jina la YESU lakini ni mawakala wa shetani ambao wanajificha kupitia jina la YESU, maana wahubiri haoau wale ambao wanategemea kufanya kazi ya MUNGU kwa uchawi au kwa namna ya kipepo hawapendi kazi ya MUNGU wa kweli hivyo lazima watoe sadaka kwa shetani kwa sababu MUNGU hawajui na majina yao hayako mbinguni wala sio watenda kazi wa MUNGu hivyo basi hujitahidi kuharibu kazi ya ufalme wa MUNGU na hutoa sadaka ili huduma za MUNGU wa kweli zife, wachungaji na watenda kazi wa MUNGU wasiweze kumtumikia MUNGU ila mimi nilikuwa nawarudishia  hayo maombi yawe kwao ili kazi ya MUNGU wa kweli isonge mbele naya wakala wa shetani na watumishi wa shetani ambao wanatumia jina la YESU  kwa kuwadanganya watu iharibike ili MUNGU na kazi ya MUNGU wa Mbinguni isonge mbele na watu wengi wafike Mbinguni.

Kuweni makini  baadhi ya sehemu ambazo watumia jina la YESU, sio kuwa kila mahali ambapo wanamtaja YESU ni kwa YESU wa mbinguni,  baadhi ni kwa mpango wa shetani – kwa sababu  Baadhi ya makanisa wanatumia nguvu za giza kuwateka watu, utakuta wana  wa wanawaumini wengi, na wengi wakisikia mhubiri Fulani amekuja wanakimbilia wakijua kwa MUNGU kumbe la!  Wanaenda kusombwa, na kuibiwa vitu vyao, maana mhubiri ambaye si wa MUNGU hutoa sadaka kwa Mashetani ili kupata wafuasi wa kumpelekea shetani, kwa vile mhubiri huyo ametoa sadaka kwa shetani basi na haop wanaomfuata wanakuwa wametolewa sadaka kwa shetani na kwa vile asilimia kubwa ya watu hawaombi wala kumuuliza MUNGU kuwa waende wapi au sehemu sahihi ya kwenda kuabudu ni wapi,  kwa kuabudi na  kwasababu kiroho hawajakaa vizuri husombwa na kupelewa kwa hao wa kipepo kwa kujua na kutokujua maana walitolewa sadaka  ya kuvutwa kiroho na kimwili watapelekwa huko, au watajikuta wamefika huko na  kuibiwa vitu kiroho na kimwili pia , matokeo yake  wana wa MUNGU wanakwenda kula na kumtolewa dhabihu shetani pasipo kujua, japo wao wanapenda kumtolea MUNGU matokeo yake ni mikosi na filisi, na mpaka uje kushtuka unakuwa umefilisika.

Ukimtolea MUNGU sadaka yako mwambie MUNGU sadaka hii ni ya ulinzi naitoa kwako anayefuatilia mali zangu kwenye ulimwengu waroho ikamwadhibu, ikamtandike, ikamporomoshe, ikamwangushe na wala wasisogelee, haleluya! utaona Baraka MUNGU alizokupa zanona zaongezeka lakini ukikaa tu bila kuomba ohoo.  Shetani na jeshi lake wanaingia wanabeba wanaondoka. BWANA YESU asifiwe.

Zipo sadaka za ulimwengu wa  Roho ndio maana  unaota upo machakani, kwa nini  unaota uko uchi, shule wakaati umemnaliza, umeshindwa, umechoka, unakata tamaa ni sadaka hizo zinanena, zimeshatolewa, na wakakutengenezea jambo la aibu limeshakuwa limeshaandaliwa na mashetani  na linakuja au limekuwa ila ukizibatilisha hizo za kishetani na ukatoa sadaka yako ukanenea kwa YESU, mwambie BWANA YESU walipoiba wafuatiliwa, warejeshe, ninabaatilisha sadaka na mipango ya shetani kwenye maisha na vitu vyangu, ninapindua sadaka zao na kuvunja na  ninateketeza maagano yao   kwa jina la YESU, utaona mambo yananyooka.  Napenda nikufundishe yamkini umeota ndoto mbaya mwezi mzima hata hukumbuki,  ukitafakari kuwa umeota ndoto mbaya ngapi hukumbuki, ndoto mbaya haziji hivi hivi wala adui haji kwako hivi hivi, wanajipanga na wameplan wanataka na wanakuja kuchukua kitu Fulani kwako, wengine wakishindwa hujaribu tena na tena, Nilikuwa nimeona katika maono jamaa fulani alikuwa anamtafuta moja ya muuni wa kanisa hili, sasa kwa vile walishatoa sadaka nyingi sana na hazikunena kwa shetani akawa anatoa ya damu panzi na damu ya nguruwe nami nikaona nikamrudishia iwe juu yake nika mwambia hupati kitu pale, sasa tafakari je ulishawahi kuwaza kama mwanadamu anaweza kutoa sadaka ya damu ya Nguruwe?

Baadhi ya watu wa kabila fulani  wao wakitaka kujenga lazima wachinje kwanza, hivyo kwa agano la sadaka hiyo wengine hawataweza kujenga na wakitaka kujenga lazima na wao wachinje kwanza hilo ndilo agano lao, na kwa agano hilo katika nyumba hizo MUNGU hataonekana na itakuewa ni sadaka ya dhuluma kwa sababu wengine hawataweza kujenga. Kwa sababu muasisi ameanza na umemwita shetani, Unaweza ukawa umetolewa sadaka hutakaa upate kazi, watoto, Amani, hutakaa ushike kitu, unakuwa umekaa kaa tu mpaka unajiuliza kuwa ni nini? Maneno makali ya mtu anayokuambia mfano, tuone utafika wapi, utakufa, Malaya, hutaweza, yanaendanaga na sadaka na ndani yake yana kiburi cha shetani, ndio maana mtu anakuwa na uwezo wa kukuambia maneno mabaya, na mara nyingine huwa yanakupata kwa sababu maneno hayo yameambatana na sadaka za kuyafanya  yafanye kazio kwa aliyenenewa na mapepo na majini huwa makini kufuatilia mpaka yatimie, hata mimi nilishatolewa sadaka sana za kishetani lakini hazikufanya kazi nami nakutia moyo kwa sababu wewe ni kamanda  utashinda, toa sadaka kwa MUNGU inene utashinda, yamkini unakampuni  unashule, una baishara unakuta imeshatolewa sadaka, inakufa imesinyaa, umetolewa sadaka utazaa na yule na yule unaoa au kuolewa na kuachika kila wakati,  wakati mwingine unaweza ukawa na mali, yamkini umeshawishiwa kwenda kwa mganga au hauna na mganga atakuambia  tamkia hiki kitu  jambo au neno Fulani kwa vile umetamkia hee unakuwa ndio mwisho wa jambo hili, si umetamka, si umenenea, inakuwa mwisho, unapotamka tu wanakuibia wanampa mwingine, wewe hutakaa upate.  Mtu akikutamkia kwa nia mbaya hutakaa upate, Lakini ukikaa meza moja na MUNGU hata kama wakitamka mabaya, mambo yanakuwa safi, ili afanikiwe kwa MUNGU anakuwa ameshatoa sadaka kwa MUNGU.

Ziko njia nyingi ambazo shetani huzitumia, mfano:  Shetani huwa anaweka akiba za kumbukumbu za yale ambayo ni yake yaliyopandwa na kutolewa sadaka kwa kusudi la kuimarisha ufalme wake, Mfano. Mtoto amezaliwa tu amewekewa kamba nyeusi mkononi au kiunoni,  kumbukumbu zipo kwa mashetani au pale ambapo ulikuwa unakaa au hata shule, ulipozaliwa, pia wachawi humulika watoto wapi wana akili  ili waziibe au kwenye kazi, lakini ukiwa na YESU wakikuita kwenye ramli hawakuoni  au wanapasuka na ramli haifanyi kazi, kwa vile kwenye ramli hawakuoni wala kwenye dhambi kwa vile umeokoka, wakawa wanawapata watu kwa njia ya sadaka zao na kumbukumbu za mashetani ila sasa na njia hiyo imeharibiwa kwa  jina la YESU, unajua hata mwanajeshi  lazima afundishwe mbinu na mbinu za kishetani hazina nguvu kama za MUNGU wao wanatoa sadaka na sisi  tunatoa sadaka kubatilisha,pia unaweza wakutolee sadaka  miaka yako iwe ya shida shida, watuma mapepo miaka yako iwe ya shida shida, kumbuka damu ya Abel ilinena, kwa nini damu yakeilioongea? kwasababu sadaka yanena,   BWANA YESU asifiwe, Mizimu pia wanatoa sadaka mbalimbali ili kuwa na wafuasi au watu wakawasujudie na kuwaomba ila ukiwa na YESU za mizimu hazitanena, Sitaki kusikia mtu anasema maisha magumu na wewe mtolee MUNGU sadaka mwambie sadaka  walionitolewa na mimi nasimama kwenye madhabahu ya MUNGU aliyehai natoa,  ninainenea ikawanyamazishe, ikabatilishe, ikarejeeshe vitu vyangu vyote  A to Z, utaona mabadiliko.

Sadaka zinatesa watu, unashindwa yale ambayo ilikupasa uyafanya unatakiwa uwe bosi, uweze kusoma, uweze kusonga mbele watu wengi hutoa sadaka kwa mashetani ili zikanene huko,  hata kama unafanya biashara yeyote au jambo Fulani hata kama ni ndogo wao wanaiba, Wanaiba hata upendo wa mume na mke au watoto wanaiba katika roho na matokeo yake hutapendwa tena, huwezi endesha gari, hofu mashaka, kuharibiwa sura, maisha, safari, mafanikio. Vitu vingi vimeibiwa hata Baraka zako hutolewa sadaka. Ziko sadaka za maneno hutafika, hutaolewa hutakaa na mwanangu, sadaka inaongea, sadaka ya mahari, na pia zipo mahari ambazo mtu hutolewa kama sadaka yaani unaolewa na mtu aliyekufa, kimwili huku duniani hutakuwa na mume unakuwa umekaa tu, ila waliotoa sadaka wanakuwa wamekutolea sadaka unakuwa mke wa mtu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita, mke wa mzimu Fulani kwa jina lake sababu tu yule aliyekufaga hakuoaga au alishatoaga sadaka kwa shetani hata kama atakuwa amekufa awe na mke duniani ambaye yupo hai.   Wengine hujiita matowashi wakati tamaa za mwili zipo pale pale kutamani wanaume au wanawake sasa ni bora ukaoe au kuolewa ili usiendelee kula meza moja na mashetani.

Zamani mababu na mabibi walikuwa wanatoa sadaka na sasa imekuja neema ya kumjua MUNGU, leo tupo ibadani tunatoa sadaka, sadaka pamoja na neno hili ninasimama katika ulimwengu waroho na wachawi pia wanaendaga kufanya ibada na ibada za wachawi ni za ajabi ajabu wengine hutoa sadaka ili wawe na macho kama ya kwako naya kwako yataanza kupofuka pofuka, ibada za wafu, unasoma huajiriwi, ili usioe au kuolewa, au uolewe au kuoa kupitia  mashetani na utajikuta umemkubali mtu pasipo kumpenda mtu, husikii wala huelewi ukiona msg huyo unamkimbilia mtu baadae sana ukipata neema ya MUNGU ndipo utaanza kujihoji, imekuwaje nimeolewa na huyu jamaa au nimemuoaje huyu binti, hapo ndipo endapo utapata neema ya MUNGU utachomoka la hasha utakuwa na ndoa ndoana yaani mateso matupu ila sasa kwenye kanisa hili  wengi wameshatoka katika mateso hayo.

Sadaka yako, hata ukiamka inene, ikatoe vitu watu wako, maisha yako, baraka zako, huko ambapo zilipokuwa zimeshikiliwa, ikazuie waizi na kuwateketeza kwenye ulimwengu wa Roho na  utaanza kuona mabadiliko na biashara za wachawi zitaanza kuporomoka na kuisha, lakini sio kwamba wataacha, wachawi nao watakazana kutoasadaka, wataendeleza na wewe unaendeleza kutoa sadaka na kubatilisha za wachawi ili  wasikunyang’anye tena, usiozubae ili wasikuweze,  Kuwa mwaminifu kwa MUNGU,  ziko sadaka mbalimbali, hata  na mimi kuhani lazima ziwatolee sadaka kwa MUNGU kwa namna ninavyojua mimi lakini yanipasa nikufundishe na wewe ili uweze kusimama  katika  nafasi yako, na ili ufanikiwe,  naona vibuyu vya wachawi vinaanza  kupasua nao kuchanganyikiwa  sasa vitu vya watu vikiwa vimerejeshwa  hapo ndipo shetani na jeshi lake na mawakala wake watakapochanganyikiwa zaidi na watu  wataona shetani hana kitu ni masikini,  ndipo wachawi, waganga na washirikina wataona hawana wateja na kazi imewashinda na wao wataokoka  na watarudi kwa MUNGU  na wengi wataokoka.

Wapo watu ambao wamejenga nyumba au amefanya jambo kwa kupitia wewe, kwa kutoa sadaka na kuiba vitu vyako kwa  kuiba  kipaji chako kwa sababu aliviona na akafanikiwa  lakini wewe huna hata nyumba na  mambo yako yamekwama sasa navunja hilo agano la sadaka sasa mimi nazipindua, nazipindua, maana unatakiwa  uwe na cheo Fulani au maisha Fulani huna kwa sababu walikutoleaga sadaka kwa mashetani na zinanena  hata Tanzania baadhi ya watu walikuwa wanapata vyeo kwa njia hiyo lakini sasa haitawezekana tena hapa ni MUNGU tu ndie anayetupa viongozi, mimi nabii niko hapa sitaongozwa na kiongozi wa Shetani,  hayo mambo yalishapita  na Tanzania inaendelea kupata viongozi toka kwa MUNGU. Endapo viongozi au mtu anayekuongoza amepata cheo hicho toka kwa mganga tutakuwa tunaongozwa na mganga  na niliwaambia wanaoenda kutafuta vyeo kwa waganga waache wataporomoka hawasikii sasa na wengine pia watakufa kama wao hawataki kuacha, maana ukipata kitu toka kwa mganga, unakula meza moja na shetani, na kama umeenda huko tena   ili upate cheo cha kuongoza watoto wa MUNGU,  hapana!  sisi sio watu wa kuongozwa na watu wa aina hiyo, sisi tunaongozwa na MUNGU tu, Je utapenda kuongozwa na mtu anayeongozwa na shetani anayetoa  makafara, Pia unaweza kwenda kwenye baadhi ya makanisa ukakuta upo kwenye meza ya shetani, unaishi na shetani na unakula na shetani na ukienda kanisani ambapo  MUNGU yupo unakula na MUNGU na unaishi na MUNGU kumbuka kipindi cha baali na Elia, ila katika madhabahu hii utafika na itaongea juu ya maisha yako, na wale ambao mmekwama  katika maisha ikifika mwezi wa Nane mtakuwa na taswira na mafanikio sana,  lakini  uwe umeamua kuachana na meza za shetani na mambo yake na uamue kusonga mbele na utaona mafanikio,  lakini wengine wamejizoesha kupenda ukilema wakati wewe si kilema, hata mimi nilivyoitwa na MUNGU ningekaa mahali na kusubiria  bila kuchukua hatua nisingelifika hapa, ila nilichukua hatua nikaanza hatua ya kuomba na MUNGU akafungua njia lakini sasa kwenye  kuchukua hatua watu wengi ni wabishi  wanatakaga mambo mazuri kwanza, hawatakagi kuanzia chini shida hiyo yamkini MUNGU anataka uwe tajiri lakini anataka uanze kwa kuchoma mahindi, lakini wewe hutaki yeye anakuacha,  si amekuambia anza hatua ya chini hata  matajiri wakubwa jinsi walivyoanza walianzia chini sana,  hutaamini, watu wengi hawapendi kujishughulisha, nimesema hivyo sio  uanze kujishughulisha na uovu  ili ufanikiwe subiri kuwa na subira anza kufanya yenye utukufu wa MUNGU.

Unaweza ukatolewa hata sadaka za kukosea mchumba, Umechwa na huoi wala huolewi, hutakaa na pesa na pesa hazikai, kumbuka umoja wa wachawi wanafanya kazi kisawasawa wana rada, antenna, na setelaiti wanajua unakwenda kufanya nini, na mda upi?,  na mambo kama hayo, sasa kwa bahati mbaya kwa kujua na kutokujua wewe katika ulimwengu waroho umeacha wazi, hakuna ulinzi wa sadaka, wanaona vitu vyako viko tu, sasa si wanakuwa na uwezo wa kuviiba?  Ila amua na wewe  fanya kazi kisawasawa katika ulimwengu wa Roho yenye utukufu wa MUNGU aliyekuumba na wewe toa sadaka katika ulimwengu waroho, kwasababu MUNGU anasubiri utamke jambo, umepewa akili na mimi nakupa maarifa,  toa sadaka yako mtolee MUNGU mwambie natoa sadaka hii ikanene katika ulimwengu waroho, waliozichukua, walioiba wakanyang’anywe huko huko, hata waliokufa na vitu vyako wakanyang’anywe huko huko, unaweza ukashangaa mtu amekufa na mtu amekufa navyo,  pesa  ni roho, roho ya uzima,nyumba ni roho  ya kuishi maisha mengi na heri na Baraka ni roho, roho ya wokovu sasa  wakikuibia wanakuachia roho ya mpinga Kristo, kila kitu kinaanza katika roho na ndio maana wanaiba katika ulimwengu war oho na ndipo hutimia kimwili.  Na hata  wewe kama iliwahi kwenda kwa mganga basi tubu maana kama hujatubu wewe bado ni jambazi tena jambazi la hatari sana Zaidi ya anayevunja nyumba, maana kitendo cha kupeleka sadaka kwa mganga hapo ulijenga na kujijengea  madhabahu, kwa mganga hivyo usimnyooshee jangili kidole wakati pia wewe pia ni jangili, maana  kwa kwenda kwa shetani, shetani hukuagiza  tupe kitu Fulani na wewe ulipeleka na pia baadhi ya makanisa wanatoa sadaka kwa shetani utaona yamejaa  lakini ni mambo ya kishetani yaani yale yanayopinga neno na kweli ya MUNGU ndio yanafundishwa na watu waona lakini wanakuwa  wameshatekwa wamefanywa wajinga wanaona sawasawa tu ila wenye ufahamu akili zao hufunguka na wanaondoka, sasa huduma hii itavunja kila mpango wa ibilisi na kila sadaka ambazo wamekutolea nakwenda kuzivunja, inamaana sadaka za shetani zitanyamaza lakini pia vitu vyako vikarejeshwe.

Unaweza  kutolewa sadaka ili usiende binguni lakini YESU alitolewa sadaka ili tuende Mbinguni, Mpokee YESU mkubali YESU, wachawi wakishakushindwa, wanang’ang’anaga na wewe mpaka wahakikishe kuwa wanakutoa pale ambapo panawamaliza yaani mahali sahihi pa MUNGU na wanaweza kukutoa lakini ufahamu ukirejea utatafuta palepale ambapo MUNGU yupo yaani madhabahu sahihi ya MUNGU,  Leo omba  hivi – Baba katika  jina la YESU vitu vyangu vikarejee vyote, natoa sadaka katika jina la YESU, BWANA YESU asifiwe,  Kuna kitu unakitamani lakini hakifiki sio kwamba kinafunguka hivyo hivyo lazima ukitafute pia uelewe au ukate kuwa mpinzani wa MUNGU, mfano mtu anamaisha mazuri na Baraka zake toka kwa MUNGU, halafu wewe ukamfitini au ukaingia wivu, kumbuka MUNGU akimbariki mtu unapochukia inamaana unapinga kazi ya MUNGU,

Zaidi chukua hatua katika kila jambo, mfano. Hata Unapotaka kupata mtoto lazima kuna hatua wazazi wanachukua ili kupata mtoto na sio kukaa tu, wakikaa tu mtoto hatapatika. Pia Usipende mtu ajifananishe nawe na usijifananishe na  nao,  wao ni wao ni mimi ni mimi,  ndio maana vidole, sauti maisha na kila kitu cha mtu hakifanani na cha mwingine, na cha mwingine hakifanani na cha kwako, hakuna mtu anafanana na mwingine

Sala ya Toba: -  Bwana YESU  naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizofanya  kwa kujua na kutokujua, naomba toba na rehema hata mimi ambaye nilitoa sadaka kwa mashetani nilikaa meza moja na mashetani nikala nao kwa kujua na kutokujua nataka nikakae nawe BWANA YESU, nikale mkate wako, ambalo ni Neno lako la kweli, nimekula mikate  mingi ya uongo,  kumbe wewe  YESU ni mmoja, tunajua wewe ni mmoja, lakini tunaokula ni wengi, wanaokula ni wengi na kupitia  wewe sisi ni wamoja tunakuwa mwili mmoja,  BWANA YESU  na katika maisha yangu ziko  sadaka mbalimbali zilizotolewa na majini, mapepo na madhabahu na ukoo mbalimbali wakaiba  vitu vyangu na kuvikwamisha, magari, miaka, hekima, maisha, ndoa,  Baraka, huduma, na mengineyo mengi, BWANA YESU, ninatoa  sadaka katika ulimwengu wa Roho kunyamazisha, kubatilisha, na  ninaomba nikarejeshewe kila kitu kilichoibiwa naipatanisha na sadaka hii niliyoitoka katika jina la YESU na kuanzia leo watakao nitolewa sabada mahali popote au kwa chochote nilichonacho ili wakiibe ninawazuia, ninabatilisha, ninawateketeza,  ninaweka ulinzi kupitia sadaka niliyoitoa  leo katika jina la YESU, BWANA YESU jina langu likae kwenye kitabu chako cha uzima wa milele kwa jina la YESU na kwa damu ya YESU.

 

Sema na mimi napinduapindua sadaka zote,  zilizotolewa kwa wachawi na waganga kwa yeyote, mizimu, majini mapepo, umasikini utoke kwa jina la YESU, antena zao, rada na mitambo yao, naibomoa, bomoa kwa jina la YESU, waliponimbia hufiki, nitafika, naamuru warejeshe vitu vyangu vyote walivyoiba kupitia sadaka mbalimbali. “Nami naziharibu katika ulimwengu wa Roho wanyang’anywe, ulipouzwa, kununuliwa, kuuzwa urejeshwe kwa jina la YESU” “Ninaomba toba na Rehema narejesha mali zao  na nasema kama aishivyo MUNGU sadaka walizokutolea kwa mashetani ili waibe vitu vyako na  wakaiba  sasa nasema fimbo ya Nabii Hebron ikawe kichapo sasa na hata milele. Namwombe Raisi wetu, sadaka zozote ambazo ni kinyume nawe MUNGU ambazo zilitolewa zisinene juu yake namfunika kwa damu ya YESU”

Baba katika jina la YESU naharibu kila anaina ya sadaka inayonena kwa kila mmoja nami narusha damu ya YESU kwenye ulimwengu waroho waliokuwa wakiona mali zao hamtaziona tena,  Mpofuke kwa jina la YESU, Waliokuwa wameshikwa na mpinga kristo na roho ya kusulubiwa juu yao damu ya YESU inaondoa mateso uliyonayo, uliposulibiwa, mahangaiko yameondoka, nami nakuombea moyo wa kupokea kuhifadhi na kumpenda MUNGU, moyo ya upendo, wa kumpenda MUNGU, uhifadhi, utakatifu, Imani nakuondolea moyo wa chuki, maneno maneno, wivu, utoke kwako katika jina la Baba, Mwana na la Roho Mtakatifu,  kila mgonjwa awe mzima sadaka iliyonena ili upate mateso inyamaze kimya, katika ulimwengu wa  roho twende pamoja kwa sababu hata anayetoa sadaka kwa mashetani kwenye ulimwengu waroho huyo mganga anamsindikiza,  lazima uelewe  na mimi kuhani na Nabii wako, haya twende.  Anayekata kudhubutu kuiba vitu vyako na aache, naombea vilivyoibiwa katika familia mbalimbali virejeshwe, nami narusha damu ya YESU nazinyamazisha vyote, walitumia kibali chako kwa kutolea sadaka nimerejesha vyotewote nimeyanyang’anya kwa jina la YESU.

 Hakuna silaha itakayosimama juu yako tena, zilikuweza kwa sababu zilitolewa sadaka, na mimi nimezifuta. Mnone mpendeze kwa jina la YESU mpaka wawashangae.

 

Imeandikwa na Mtume na Nabii Hebron.