Pages

Friday, October 14, 2022

 

KUNG’OLEWA ROHO YA KUKATALIWA.

 

Haleluya Mbinguni, Haleluya kwa Malaika wake! Haleluya kwa Madhabahu ya YESU ni BWANA  na Mwokozi wa Mataifa wote na kwa  Malaika wa Kanisa hili, Haleluya kwa kondoo wake. Baba MUNGU nakushukuru vyote nimeviondoa kupitia maombi niliyoomba kwako na sasa kutana na watoto wako, kutana na kila mmoja, vichaka vimekatwa mbele yao na mawe yameondolewa mbele yao, mageti yaliyo mbele yao yamevunjwa, na sasa wako huru,  asante Baba, asante Roho Mtakatifu.

Haleluya!  MUNGU anaendelea kuwafungua, na wakati nilipokuwa nawaombea, MUNGU amenielekeza mengi ya kuwafungua, mengine nimeshawaombea, mengine nimewafungua na mengine mtaendelea kufunguliwa sawasawa na mapenzi ya MUNGU.

 

SOMO: Kitabu cha Nabii Ezekiel 16:1-10; Yeremia 1:9-10

Kama kuna kukataliwa ujue kuna kukubalika, MUNGU alipokuumba hapa duniani alikukubali,  kila mwanadamu  wakati anazaliwa damu ilimwaagika chini, na hakuna ambaye damu yake haikumwagika chini katika ardhi, kila mmoja alitunzwa katika chupa au sehemu maalumu ambayo MUNGU ameiweka kwa mapenzi yake ndani ya tumbo la mwanamke/ wanawake, chupa ya uzazi huwa inapasuka ndipo mtu anazaliwa iwe  umezaliwa hospitalini au nyumbani.

 Tumezaliwa katika familia mbali mbali, za Waamori, za Wahiti vizazi na vizazi, damu haikuanza kutoka au kumwagika leo, na damu hiyo ilimwagika ardhini na inaendelea kumwagika ardhini na ndivyo ilivyo.

Kitovu hukatwa na kinapokatwa damu hutoka pia na kinakatwa kwa sababu ya kumtenga mtu na mtu (mama na mtoto) ndio maana kila mwanadamu ambaye alizaliwa damu yake ilimwagika, hata kama kitovu kumechomwa au kimeungua au kimechimbiwa mahali au kimetupwa baharini au kufanyiwa jambo lolote lakini damu yake ilimwagika chini. 

MUNGU akasema nikaona ukigaagaa chini katika damu yako ukachukiwa na mambo yaliyokuwepo hapa duniani, MUNGU alikuleta ukiwa u mbegu nzuri na ukiwa na baraka zako na ukiwa na tabia njema lakini ukarithi kukataliwa na kuchukiwa roho ambayo ndio inatenda kazi kwa sababu ukimpenda MUNGU utachukiwa na mambo ya dunia hii na ukiyapenda ya dunia hii utapendwa na dunia na ya dunia ila mambo mema ya MUNGU hutayaona. Hata YESU alivyozaliwa alichukiwa, na hatimaye alishinda, YESU ana neema yake ambayo tofauti na yetu, sasa basi ilinipasa nifanye maombi ya kukomboa kitovu chako, kikombolewe kuanzia siku umezaliwa, inawezekana kuna ni vifungo unakaa navyo hata ukiombewa havifunguliwi kwa sababu ulirithi kukataliwa lakini MUNGU anakupenda, Je! Wewe unampenda?

   Roho ya kukataliwa ni roho itendayo kazi ili kumkwamisha mwanadamu, inaweza ikawa ni roho ambayo imetangulia katika biashara, kazi, maisha, vibali, masomo na hata shughuli mbali mbali ambazo unazofanya zinakukataa, hazina mafanikio ni roho ambayo yamkini inaweza ikawa imetumwa na majini au ni laana, au ya kurithi, au inaweza ikawa imetumwa na mtu na ndipo inafika mahali vitu vinakataa, mipango ni ya kwako lakini inakukataa, inakuwa na nguvu ya kukukataa.

Ni kama ilivyo hata sasa baadhi ya watu wanamkataa BWANA YESU,  na ni kwa sababu shetani ametuma roho ya kumkata BWANA YESU, Roho ya kutataa  kweli, Roho ya kukataa Neno na hata katika familia yako unaweza ukawa unaomba  watu waokoke, waje kwa YESU lakini endapo wameirithi roho ya kukataliwa na roho ya kumkataa BWANA YESU basi watakuwa wanamkataa BWANA YESU na kumkubali shetani kwa kujua au kutokujua, na  katika dunia hii, asilimia kubwa ya watu wana roho ya kumkataa BWANA YESU na kumkubali shetani,  na Neno la MUNGU linasema Mkiri kwanza YESU  na baadhi ya  watu wanashika na hata kusoma biblia lakini wamemkataa MUNGU (Kumkataa MUNGU au kumkubali MUNGU na kufuata amri, sheria na Mapenzi ya MUNGU endapo hufuati amri, sheria na mapenzi ya MUNGU unakuwa umemkataa YESU na umemkubali shetani)

Yamkini unaweza ukawa na mipango yako mizuri tu ambayo ulivyoipanga ulijua kabisa kuwa unaweza kufanikiwa, kwa bahati mbaya mpango huo ukawekewa au ukiingia roho ya kukataliwa, roho hiyo ikiingia huwezi kufanikiwa, yamkini unaweza ukawa umerithi roho hiyo, hivyo mipango yako haiwezi kufanikiwa, hushiki pesa, unaweza na watu au mtu au hata au vitu vikakutakaa na pia wewe ukamkataa hata na YESU, ila YESU anakupenda, MUNGU anakupenda, lakini jichunguze je! Wewe unampenda MUNGU? Unampenda YESU?

 Mchawi akikufunga anakupazawadi  ya roho ya kukataliwa, ndio maana hufanikiwa, lakini MUNGU yeye ni MUNGU wa upendo, neno linathibitisha kuwa upendo wa MUNGU si sawa na ule wa mwanadamu, Upendo wa MUNGU ni wa tofauti sana, Je! Unampenda mwenzako? Upendo ni nguzo, ndio maana tulipewa amri hii ya upendo, upendo una mapana sana, Je! Unawapenda ndugu zako? Jamaa na marafiki? Je! Unawaombea mema? Je! Unawaeleza kweli ya MUNGU na MUNGU anataka waweje? Je! Unawaeleza na kuwafundisha kuhusu YESU, injili ya kweli na kuwaelekeza mahali YESU alipo? Je! Wakifanikiwa unafurahi au ndio unapata wivu? Jitathmini.

Tunazungumzia roho ya kukataliwa ndani ya roho hiyo kunakuwa na vipengele mbali mbali, roho hiyo inaweza ikakufuata ili ukataliwe na karama au elimu au ujuzi fulani ndio maana utafanya sana kazi lakini hakuna kitu unajikuta unakata tamaa sana na unapenda kujitenga mwenyewe, mwenyewe sana, au akawa anaishi mwenyewe  hutaki mtu au hata akitaka watu hawaji, utaona katika ndoa, kabla ya ndoa walikubaliana na kupendana ila  ikirushwa roho ya kukataliwa wanandoa wanaanza kukataliana, inafikia hatua ya kuwa wanandoa wanakaa pamoja ila hawapendani, chuki inaingia, matokeo yake ni faraka na hatimaye kuachana na watoto kupata taabu, kuhuzunisha familia za pande mbili  na kusababishia watu kupata dhambi, kumbe chanzo ni roho ya kukataliwa.

 Wanandoa – mnaweza mkaa kwa upendo ila mara roho ya kukataliwa ikiingia na mmoja wapo akianza kumwambia mwingine nenda kwenu, ujue kuwa roho ya kukataliwa imeshaingia, na akikuambia mwambie siendi tuishi pamoja hapa hapa, akikuambia nenda mwambie siendi tutabanana hapa hapa, ila wakati unamwambia hivyo kazana kumwomba MUNGU na kumtenga na kujitenga na roho, hiyo kwa sababuhata ukifanya vitu havikukubali kila siku hasara, hasara, na ndio maana niliwafundisha  muwe wasiri, miradi yako unayowaambia watu ndio unawekewa roho ya kukataliwa,  tunza siri, kutunza siri ni Utukufu wa MUNGU.

 

Roho ya kukataliwa huambatana na roho ya kukata tamaa, kukata tamaa ni dhambi na ukikata tamaa unaanza kumwazia MUNGU vibaya, unaona kama MUNGU amekuacha, dunia ni mbaya, maisha mabaya unatamani kufa tu, Je!Kweli MUNGU amekuacha? MUNGU hawezi kukuacha ila mwanadamu ndio anaweza kumwacha MUNGU, na unamwacha MUNGU kwa matendo yako mabaya na sio vinginenvyo, jitathmini Je! ni kweli MUNGU amekuacha ua ni hiyo roho ya kukata tamaa inakuponza? MUNGU anakupenda sana.

MUNGU ni wa haki akiwa upande wako hakuna kitu ambacho kitakusumbua, mtu ambaye ana roho ya kukataliwa huwa anachuki chuki tu, na yeye hujiona kuwa yu safi kuliko malaika,  hiyo roho ya kukataliwa inakuletea  vifungo, inakuwa vigumu sana kuwaza mambo ya MUNGU, inakuwa inapinga roho ya MUNGU, roho hiyo inakupumbaza, yawezekana umekataliwa na wazazi, yaani mzazi akikataa mtoto, mtoto anakuwa akiwa na roho ya kukataliwa ila kuna Neema ya kukubaliwa na MUNGU endapo wanadamu wanapokukataa,  MUNGU niwa upendo hata kama mwanadamu atakutakaa MUNGU anakupenda, unaweza ukawa na nyota lakini hufanikiwa,  ikiwa imewekewakukataliwa hautafanikiwa,  hata mwili unaweza kuwekewa roho ya kukataliwa, unaoga hautakati, haukubali mafuta, wala nguo, maji yanaweza kukukataa, na hali ya hewa inaweza ikakutakaa, hupati mtoto tumbo lina roho ya kukataa watoto, wazazi wengi wana roho ya kukataliwa kwa sababu wana roho ya kukataa watoto wao, na kwa sababu baadhi ya wazazi walikuwa wakoloni sana watoto wakakua katika uchungu  kwa sababu ya kukataliwa, wazazi waliwakataa watoto wao, ndio maana utakuta watoto hawawakumbuki wazazi wao kwa sababu wana roho ya kukataliwa, ila ipo neema ya MUNGU sasa, ni jambo  gani limekukataa   mwenye roho ya kukataliwa anakuwa na mambo mengi na ni mengi kweli na mipango mingi ila haikamiliki, na umeshawahi kujiuliza kwa nini haikamiliki? Kwanini hayatendeki? njoo kwa BWANA YESU yeye atakufanya ukubalike ufurahie na sio kwamba wale wa shetani hawakubaliki ila wanaiba vibali vya wana wa MUNGU na anakubalika akishakuibia basi  yeye na anakutazama tu na kusema acha niangalie atafika wapi, yamkini  kakufunga kwa sadaka au agano fulani lakini kwa vile MUNGU anakupenda na wewe ukimpenda MUNGU watatoa kila gharama au kafara ili wakuondoe kwenye neema ya MUNGU lakini  hawatakuweza, tulia MUNGU atakupigania,  unaweza ukawa unakataliwa, na wanaweza wakawa ni wale ambao wapo upande wa shetani ndio wanaokukataa au roho za shetani zinatenda kazi ndani yao  ili kusudi la MUNGU lisitimie kwako, mfano YESU walimkataa akasema asulibiwe, asulibiwe,  iliandikwa kuwa atapigwa atasulubiwa yale ambayo  yalikuwa yameandikwa yalitimia ila yale ambayo hayakuwa yamendikwa kuhusu YESU hayakutimia kwa sababu YESU alikuwa na MUNGU.

Katika safari ya maisha na safari ya wokovu  jua kabisa hutapendwa na watu wote kwasabau wengine watakuchukia tu bila sababu na wengine yamkini walitaka kukufanyia jambo baya ila kwa sababu ulikuwa na Neema ya MUNGU  ulipata ulinzi hivyo hawawezi kukupenda kwa sabau jambo lao halikutimia.  Sasa jitathmimi wewe kama wewe, ulianza vizuri na moto, vipindi vya ibada hukosi, utakatifu, upendo wa kupenda watu na MUNGU pia, ulikuwa unaifanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kujitolea kuomba, mikesha, sasa upo mahali ambapo unaweza kufika kanisani lakini unasema nitaangalia YouTube ila awali ulikuwa unahudhuria kanisani, sasa Je! Umekosa mazuri mangapi? Mheshimuni MUNGU naye atawatetea zaidi, atawavusha atawapigania mtakuwa salama.

Kama wewe si muombaji, roho ya kukataliwa na faraka itakupata pia mwili unaweza ukakataliana na wa mwingine na ndio maana watu wengi ambao walikuwa wamepanga kuoana wengi wao wamekataliwa sana na hatimaye wengi wao wamejikuta wameoa au kuolewa na mtu ambaye sio hata kama hujafanya nae ushirika wowote na baadae mmekuwa wazee inabakia story, zama za kale zimepita, ila huenda ikawa umeoa au kuolewa na mtu ambaye haikuwa chaguo lako.

Jikane! Ukijikana na ukaamua ndani yako kuwa umeamua kumfuata MUNGU na kufuata mapenzi ya MUNGU, MUNGU atakupigania na kukutetea katika kila jambo, vitu vingine sio usubiri kuombewa ng’ang’ana na MUNGU, baadhi ya watu hawawezi hata kuamka kuomba, kufunga hafungi, ukitaka kufunga unaona umaumwa, penda kujikana, funga kwa ajili ya roho itendayo kazi ndani yako ili uwe huru, shetani ndiye anayependa watu wakataliwe na MUNGU ili nae apate wafuasi.

MUNGU amesema watu wamsifu yeye ila watu wengi hupenda miziki ya upande mwingine ambayo sio ya kumtukuza MUNGU, inafika mahali hata mtu ukisikiliza kwaya watu wanakushangaa  ila ukiisikiliza miziki  ya upande mwingine  wanaona ndio sawa,  hiyo ni roho ya kuikataa injili,  unawekewa roho ambayo hata kazi ya MUNGU kuifanya inakuwa vigumu,  huwezi hata kufikiria kuwa nataka nimfanyie MUNGU jambo fulani  kanisani mwake,  wengi wetu tumezoea siasa, tukizisikia tunazifuatilia na kuzishangilia, ila kumshangilia YESU inakuwa ngumu, yatupasa kumshangilia YESU,  umekuja kwake anataka ufanikiwe uinuliwe, mambo hayaendi kwa sababu adui ametanguliza scadi, na lipo na wewe,  ukiwa na roho ya kukubaliwa hata kama umekaa ndani mema yakakufuata, vizuri vitakufuata na mema yatakufuata utakumbukwa. Ninakuombea na YESU atakufungua na kama ulikuwa hupendwi na haukubaliki utaenda kukubalika na kupendwa sana kama ni mizimu na majini yataenda kuteketea kabisa ila na wewe kama unataka upendwe jifunze kuwapenda watu jifunze kuwatakia watu mazuri, mwambie mwenzako wewe ni mzuri, mzuri sana, meno yako mazuri, mzuri wewe macho yako mazuri, mwambie wewe ni mzuri, mpe sifa njema mwenzako, mwambie mume wako au mke wako wewe ni mzuri. Tuache tabia ya asili jifunze kuwaambia watu wewe ni mzuri.  Anza zoezi la kumwambia mwenzako wewe ni mzuri, jirani yako mwambie nakupenda, unapomwambia mtu nakupenda mtu anakusikiliza maana upendo hauhesabu mabaya.

 Je! Unapenda Neno la MUNGU? Unapenda ubatizo wa MUNGU? ila ukimwambia mtu akabatizwe hataki atakuambia nilishabatizwa kwa kisima au  kikombe kwa sababu watu wengi hawapendi kweli, hata dini zitatoa mahesabu ya kumkataa MUNGU na kukataa kweli dini ya baba au ya mama haikupeleki mbinguni ila wokovu tu. Kumbuka roho ya kukataliwa inaamuriwa na shetani na inapewa na sadaka na agano mpaka walitimize sasa wewe umekuja umeokoka, YESU amekufanikisha nyota yako imerudi umefanikiwa sasa wanakutumia roho ya kulikataa kanisa hili, roho hiyo ikiingia, naukiisha ikataa, wanakupata wakikupata hali yako inakuwa mbaya hivyo ng’ang’ana na YESU. Ukiwa na roho ya kukataliwa unaweza ukawa unakunywa dawa lakini huponi, hata dawa zinakukataa, mshukuru MUNGU maana neno hili au somo hili ni zaidi ya chakula cha kimwili. Unaweza ukawa na mfanyakazi ila akiwa na roho ya kukataliwa hawezi pata kitu. Na pia binti au kijana unayetarajia kuoa au kuolewa kaa na BWANA YESU wakati wako ukifika utaoa au kuolewa, usikubali ndoa za dhambini (come we stay) jiamini kaa katika utakatifu.

Nataka MUNGU afanye marejesho na hakika MUNGU atafanya na MUNGU atarejesha maana MUNGU anakupenda na anasema  hakuwepo mtu yeyote  aliyekusafisha damu yako, (naongea katika roho) na usikubali tena adui akaja kukupenda kwa sababu umekuwa mzuri, rafiki wa kweli ni yule ambaye yupo nawe katika majira yote, rafiki mzuri anakutetea, hakuzunguki yupo nawe majira na nyakati zote huyo ndiye rafiki wa kweli,  rafiki ni zaidi ya ndugu na ukimpoteza kumpata ni kazi ndugu ni wengi, rafiki yuko nawe siku zote ana uchungu nawe,  una rafiki wangapi utasema wengi ila ukichuja ni watatu au mmoja tu kati ya hao wengi.

Ukimpokea YESU anakaa ndani yako; sasa kuna baadhi ya watu wameokoka ila YESU aliingia na alitoka ila nataka YESU akiingia, YESU aishi ndani yako, aishi ndani yako, Je! ndani yako  YESU anaishi au aliingia akatoka mtu wa michanganyo ujue kabisa YESU alishatoka, YESU hakai kwenye moyo au hekalu lenye uovu,  mchungaji anayechangisha YESU  haishi ndani yake, ukikuta mtu anaacha wokovu halafu anarudi nyuma  YESU alishaingia akatoka, Nataka YESU aishi ndani yako, YESU kwako ameondoka au anaishi au ametoka basi okoka upya.  Chunga sana wokovu wako, YESU atakuja kuuchukua ulimwengu na akakukuta haupo, na kwa wale ambao pia wamewadanganya watoto wa MUNGU kwa injili ya uongo nao watatoa hesabu siku ile ya mwisho hesabu ya maneno yao; pale unapomshawishi mtu amwache YESU au ukiwa sababu ya mwingine kurudi nyuma siku ile ya mwisho utatoa hesabu ya maneno yako na jinsi ambayvyo uliwazuia wengine kufika mbinguni kwa kujua au kutokujua siku ile ya mwisho utahukumiwa umehukumu wangaopi? Tubu na urejee.

SALA YA TOBA

BWANA YESU ninaomba unisamehe dhambi zangu zote  nilizozifanya kwa kujua na kutokujua hata pale nilipokukataa au pale ambapo nilipokupinga wewe, ninaomba  unisamehe, mimi ninaomba unisamehe najua unainipenda na mininakupenda naomba unisamehe,  Ninakupenda na unanipenda Roho Mtakatifu naomba unisaidie, unisaidie BWANA YESU  ujae ndani yangu naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele na mimi ninamkataa shetani na kazi zake zote na mambo yake yote, ee BWANA YESU ninaomba unishike mkono siku zangu zote. Amen

BABA katika jina la YESU ninaomba kwa ajili ya wale ambao hawapatagi uponyaji au hawaponi maisha yamewakataa, roho zilizotumwa  na wachawi zitoke kwenye maisha yako uliyofungwa na mizimu itoke kwenye maisha yako,  siku zako, ndoa yako maisha yako yarudishwe, upendo urejeshwe, shetani  uliyekataliwa na MUNGU huna mamlaka na watu hawa, Kila kitovu cha mwanadamu yeyote kisikie damu ambayo ilirithi laana na kukataliwa na damu ikadondoka  kwenye ardhi ikarithi tabia za waamori zikuachie,  damu za mababu na mabibi  ulizorithi kutoka ukoo wenu zikuachie, ni wakati wako wa kufanikiwa, kila kilichokukataa kikukubali, uliye mpweke unaishi kwa neema ya MUNGU, MUNGU akufungue,  Roho ya uasi ikutoke pokea roho ya unyenyekevu, roho ya kujiua, kutaka tamaa, kujiua ninaing’oa kwa jina la YESU malango ya kuzimu yakuachie, kwa jina la YESU,  kila roho iliyoishi na wewe ikuachie,  Roho ya kumkataa YESU itoke, roho ya kupenda sanamu ikataee, ondoa uchungu ndani ya roho yako, mabaya yatoke, samehe watu, jifunze kusamehe ili uwe huru Roho hiyo iliyokutangulia iondoke, na mimi nachosema kwa kinywa changu utakubalika tu, MUNGU akisema amesema tu, wewe jishushe usipande kiburi, sadaka zenu zikanene na zinaongea mbele za MUNGU,  kuna watu watakumbukwa kwa mazuri mpaka watashangaa kwa sababu  umefungua moyo wako kitu kinaweza kuwa cha kwako lakini unapokuwa na Roho ya kukataliwa kinakukataa ila ukisha kubaliwa na MUNGU mema yanakukubali.

MUNGU AWABARIKI SANA

Imeandikwa na Mtume na Nabii

HEBRON WILSON KISAMO.