KWANINI
YESU ALISEMA UTUPE LEO RIZIKI YETU
Mathayo
6:11, 4:1-4
Wagalatia
1:6-7
Haleluya!
Baba ninakushukuru
kwa majira haya na nyakati hizi, neno lako likatimie kwa watoto wako na kwa
mataifa maana lina kitu ulichokiweka wewe mwenyenzi Mungu. Naendelea kusafisha
anga kwa damu ya YESU, kila eneo nikirusha katika ulimwengu war oho na mwili,
naendelea kusafisha kila eneo kwa damu ya YESU, udhihirisho wa wachawi
nikiuharibu, miungu katika mji huu na kila taifa na kazi zake nikizirudisha
nyuma na kuziharibu kabisa katika jina la YESU. Nakushukuru BABA, kwa vipindi
vilivyopita watoto wako wamepata kitu wamejengwa, wamefunguliwa wamekusifu na
umewasikiliza na umetenda, nasema asante BABA. Hata sasa kipindi kingine
nakisogeza tena mbele zako, masikio ya watoto wako na mioyo yao ukiendelea
kuilisha kwa nguvu zako, uweza wako, kwa utukufu wako, upendavyo na kwa viwango
vyako, nasema asante. Amen.
Bwana YESU asifiwe!
Nakwenda kufundisha kwanini YESU alisema utupe leo riziki yetu, tuombe riziki.
Utapokea riziki yako! Nitasoma neno la Mungu kutoka
Mathayo 6:11 biblia
inasema hivi: “Utupe leo riziki yetu”.
Kwanini YESU alifundisha neno hili, mstari mmoja tu utupe leo riziki yetu, Je
hauhitaji riziki, lakini yawezekana haupati riziki au unayo riziki ya namna
nyingine. Lakini napenda nikufundishe wewe kama mkristo, shetani yupo pia
kukutafuta akupe riziki zake, na pasipokujua au kwa kujua unaweza ukawa na
riziki za shetani.
Tutaangalia katika kitabu cha Mathayo 4:1-4
utaona Bwana YESU alipokuwa anapewa riziki za shetani akakataa, kwa sababu
haikumpasa kupokea riziki za shetani biblia inasema hivi: “Kisha YESU alipandishwa na roho nyikani, ili ajaribiwe na ibilisi.
Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia
akamwambia, ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate. Naye
akajibu akasema, imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno
litokalo katika kinywa cha Mungu.”
Bwana YESU Asifiwe!
Hapa utaona shetani alimuona YESU katika hali ngumu sana katika mfungo, sio
kwamba YESU alishindwa kufanya jiwe kuwa mkate angeweza lakini YESU alikataa, Ina
maana kama angekubali angekuwa amepokea riziki kwa shetani. Bwana YESU asifiwe!
Nitasoma katika Wagalatia 1: 6-7 nataka tuingie zaidi katika riziki anasema: “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi
yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
Wala si nyingine: lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya
Kristo.”
Bwana YESU asifiwe!
Hili neno riziki lina mambo mengi sana, lakini naongea kiroho na kimwili. Bwana
YESU asifiwe! Umekuja hapa unahitaji riziki, mtu anapoenda kutafuta kibarua
anahitaji riziki, kuna maombi unaomba ili upate, na unapoyapata ndiyo riziki
yako. Lakini kuna mwingine unaweza ukawa unaomba hupati riziki yeyote wala
hujibiwi. Bwana YESU Asifiwe! Sasa kwa kujua na kutokujua maisha ya watoto wa
MUNGU wengi katika dunia hii yameharibika kwa sababu waliomba riziki kwa
mashetani. Unakuta mtu anaenda kwa mganga ili apate mke au mali, huyo amekwenda
kuomba riziki kwa shetani, au mababu wamekufa anakwenda kuomba riziki kwao.
Mwanadamu anatakiwa apate riziki kwa MUNGU, na riziki hii MUNGU aliyokupa ni
lazima uombe, ndio maana amesema omba utapewa, tafuta utaona. Lakini sasa hata
mashetani wanasema omba utapewa na tafuta utaona katika ufalme wao. Nilipokuwa
nikitafakari neno hili nimekuta ipo shida kuna watu wana riziki za shetani,
wengi mmekwenda kuomba wachawi mkategemea kupata kitu, Ina maana unakuwa na
riziki za shetani na mwenyenzi MUNGU anashindwa kuingiza baraka zake maana
riziki za MUNGU hazichangamani na za giza.
Bwana YESU Asifiwe! Unaonaga
vibao vile vya waganga vinasema utakubalika, utapata kibali huyo mtu ameenda
kutafuta riziki kwa shetani. Wote tunaelewa nini maana ya riziki mnajua Kiswahili.
Lakini ukisoma biblia YESU anasema yeye ndio chakula lakini huwezi kula huu
mwili, ni kwa ajili yako neno lake, jina lake. Bwana YESU Asifiwe! Ndio riziki
mwenyenzi MUNGU aliyoileta duniani kwamba kila mwanadamu anayetaka kwenda
mbinguni ampokee. Kuna wanadamu hawataki riziki ya mwenyenzi MUNGU, kuokoka
nikupokea riziki, kumkiri Bwana YESU ni riziki, lakini kuna wanadamu wanabaki
kusema wao ni wakristo lakini hawataki riziki ya Bwana YESU. Mimi mwenyewe sala
ya baba yetu, utupe leo riziki yetu nimesoma sana nikiwa mtoto mdogo, niliomba
riziki ya kufaulu nilifeli, niliomba kuwa na ndege nikiwa mtoto mdogo sikupata.
Mimi sijui imekuwa kama ni nyimbo, tena kuna wimbo ambao hata ukicheza kidogo
mwili unasisimuka, unaomba riziki MUNGU anahitaji uombe riziki kwake, kuna
riziki ulinzi katika mambo mengi, lakini sasa yawezekana ulivyoomba hii riziki
katika eneo ambalo MUNGU hayupo, riziki za majini, riziki za mpinga kristo sasa
umeokoka bado unazo hizo riziki, zinatakiwa zitoke maana hata shetani huwapa
watu wake vitu.
Bwana YESU Asifiwe! MUNGU
anatoa, miungu inatoa, majini yanatoa. Bwana YESU asifiwe! Sasa usije
ukaangalia biblia, shetani anaijua, wachawi wanaitumia na wanatumia jina la
YESU na wanakwambia utapata kitu na utafunguliwa. Sasa riziki za mwenyenzi MUNGU
ni tofauti, hainunuliwi. Riziki katika injili, alisema utupe leo riziki zetu
tunaomba MUNGU atupe leo hii riziki yake. Na riziki aliyoitoa ni neno hili la
leo, neno lake. Lakini ukisoma katika Wagalatia 1:6-7 anasema mnaigeukia injili
ya namna nyingine, MUNGU alishatupa injili ambayo ni riziki yake imenyooka ila
watu wanataka riziki za kona kona, riziki za uongo. Wewe unaabudu sanamu ambayo
sio riziki kutoka mbinguni, alafu unakuja na kiherehere mbele za YESU ukiomba
na sanamu yako atakwambia toka huko, wala hakusikilizi. Maana yeye hakutupa riziki
za kuweka magogo, riziki zakuita wanadamu MUNGU au kumuita YESU. Shida anasema
njooni kwangu ninyi nyote mnaolemewa na migizo, hapa kila mtu analo hitaji,
usifiche unataka riziki ya kuponywa, riziki ya amani, riziki ya kuishi, mambo
mengi yanatoka kwake na si kwa wanadamu. Ndio maana wanadamu wanakufaga,
wanaisha wote lakini neno liko pale pale.
Bwana YESU Asifiwe!
Una uhitaji ndio maana katika ile sala ya baba yetu inasema “utupe leo riziki
yetu”. Je wewe umeomba kwa nani? Umeomba kwa mpinga kristo, mwambie Bwana
naomba riziki ya ubatizo wako, wewe una wa kikombe, wewe una wa kisima, amekupa
Bwana hiyo, ndio maana maisha ya watu yanayumba. Watu ni wakristo lakini wengi
hawana riziki za mwenyenzi MUNGU wanabaki kusema wao ni wakristo lakini si
riziki kwa mwenyenzi MUNGU. Wengine watasema anajifanya sana anamjua YESU,
lakini haya yalikuwepo, yataendelea kuwepo wala yasikutishe sikiliza kweli
amua. Bwana YESU Asifiwe! YESU naye atakuja kuchukua riziki zake wale ambao
wamemkubali, unajua kama umeshaona katika kila kaisari kuna sharia zake, embu
vunja wanakuja polisi wanakupeleka mahakamani unahukumiwa. Lakini ajabu sana
watu wanaogopa kuvunja sheria ya kaisari kuliko kuvunja neno la MUNGU,
kwasababu hawajui siku ile ya mwisho hii itakuwa vilevile. Mtu anaogopa kumpiga
mtu kwasababu atapelekwa ndani, lakini muogopeni MUNGU zaidi utaona unafanya
vizuri na mtu mwema zaidi. Lakini watu wanaogopa kufungwa zaidi kuliko kuvunja
amri ya MUNGU. Sasa mabunge yanapotunga sheria kipengele hiki na hiki, vivyo
siku ya mwisho utafunguliwa kipengele kwa kipengele. Riziki ya MUNGU alileta
ubatizo wa maji mengi, wewe una riziki gani utafungwa vile vile. Kwa hiyo hapa
kwa kujua na kutokujua wewe ni mwalifu mbele za mwenyenzi MUNGU. Ukiambiwa uje
uwe mtu mzuri wengine wametekwa na shetani uendelee kuwa mtu mbaya kwa kujua na
kutokujua. Kwa hiyo wakristo wengi na wanadamu wengi bado ni wafungwa wa
shetani japo hawana kamba katika ulimwengu wa roho ni wafungwa. Imeandikwa
nikiri riziki kutoka kwa Mungu okoka, wengine wanasema hakuna kuokoka. Sasa
usicheke watu wenye kesi magerezani, wakati wewe ya kwako ni makontena ya
mafaili.
Bwana YESU Asifiwe!
Nikwambie ukweli hata wahubiri wengi wanaochukua pesa za watu, hawa ni wafungwa
wa shetani. Sema tu hukumu haijafika ile siku ya mwisho ambapo kila mmoja
atafika atoe hesabu yake. Watu waombewe bure wewe unachukua pesa, hawa ni waovu
na wafungwa wa shetani. Lakini anatembea na biblia akisema bwana! bwana! lakini
kumbe ni wafungwa, usiabudu sanamu lakini bado wewe ni mfungwa na kazi ya
mfungwa ni kuhukumiwa. Na ile siku ya mwisho ndivyo itakavyokuwa kama
unavyosikia mahakamani leo hukumu inatoka ndivyo itakavyokuwa. Sasa umekufa
bado hujatengeneza utakufa na ufungwa wako okoka. Usiambiwe kwamba tutakuombea,
kama unaombea waliokufa na wewe bado ni mfungwa kwasababu MUNGU ametoa riziki
yeye ni HAI watu wanahangaika na maiti kuiombea haisaidii. Watu wanaogopa
kaisari kuliko MUNGU angalia kina Daniel simama imara mimi nakwambia MUNGU atakutetea
na hata kaisari hautavunja sheria zake MUNGU atakutetea. Bwana YESU Asifiwe!
Amesema BWANA ametwaa jina la BWANA libarikiwe, wewe ni riziki yake akitaka anakuchukua,
akitaka unakaa hapa, amekuweka hapa ili aweke mapenzi yake haya muombe BABA naomba
unipe riziki zangu unazozijua. Ila wengine sasa wana riziki za watu nyota ya yule,
magari wameiba riziki ya nyumba. Sasa hata katika injili hapa umekuja kutafuta
riziki na MUNGU anakupa, sasa unaweza ukawa umefata riziki za mashetani, wanaosema
misukule inadondoka ione hiyo hao ni watoa riziki za shetani. Nimeenda kwa
mtumishi akaniombea bwana akatenda kumbe umepewa riziki za shetani, napenda
nikufundishe jambo hili likusaidie utakauka utachoka siunapokea kiroho riziki
za mashetani, za majini lakini huelewi. Injili yenyewe asilimia kubwa sio
riziki iliyotoka kwa MUNGU.
Bwana YESU Asifiwe!
Nasikia wengine wansema wanamtaka YESU tu hawaamini roho mtakatifu, utasema
wanapokea riziki ya mwenyenzi MUNGU? Vyote vilitoka mbinguni alichokileta YESU
ni chakula cha uzima ndio riziki yetu, lakini riziki iliyokuja mbona ni
tofauti, riziki ya ubatizo sio hii, mara kisima sio hii, mara vumbi sio hii.
Bwana YESU Asifiwe! Mara kubariki pombe sio hii riziki ya MUNGU lakini sasa
unapumbazwa kusema mimi ni mkristo. Ukristo bila kufata riziki zake MUNGU ni
kazi bure bado wewe ni mwalifu. Na ili ujue wakristo atakuwa anajivunia yeye
kuwa haendi mbinguni, biblia inasema usinywe pombe lakini yeye ndio anakunywa
pombe anajipiga na kifua kabisa. Ivi YESU angekuwa yupo kimwili hapa duniani
waalifu ni wangapi? ninaona bora waizi hata ni wachache lakini watu
wanaomchezea MUNGU kwa kuvunja sheria yake ni wahalifu wengi . Hupendi wenzako
mwalifu, unamuonea mwenzako wivu muhalifu, unapinga neno la Mungu muhalifu.
Sasa toa kwanza boriti kwako, unapoita mtu mwizi na kutaka akamatwe je wewe sio
mwalifu, au kwasababu huukumiwi kikaisari, yupo anayehukumu ambaye ni Bwana
YESU ile siku ya mwisho, mambo yote yatapita na ndivyo itakavyokuwa. Hili
hekalu la MUNGU lakini watu wamejaa machanjo, machale sio vaccines ila na
mapanga kabisa miili ina uhalifu. Imani zina uhalifu kulala makaburini, mapete
ya uhalifu kufunga ndoa na majini unajua kuna watu wanavaa mapete lakini
wamemaanisha amefunga ndoa na sharifu, ana jini la ulinzi, jini la akili, la
kuzungumza yaani ni mwalifu, lakini amevaa smart anaendesha Range kumbe ni mwalifu mkubwa au majambazi. Sasa
majambazi haya yatahukumiwa na Bwana YESU kwasababu ya kutesa watoto wa MUNGU,
Injili kupindisha watu hawataki ukweli, watu wanaomba msalaba ndio hujibu, mbao
itakusaidia nini. Ndivyo ilivyo maisha ya kiroho na ya kimwili, BABA yetu
naomba unipe riziki wakati ulienda kutafuta mtoto kwa mchawi, huyo mtoto hawezi
kuwa riziki ya MUNGU. Mume au Mke upate kwa mganga hawezi kuwa riziki kutoka
kwa MUNGU, na kama alikupa shetani au alikuteka huwezi kuwa riziki. Mwambie MUNGU
atengue huwi riziki, amekupa nyota yako wakaiba na wewe hapo ukataka nyota za
watu ni muovu. Sasa iko shida watu wengi hawana riziki, na riziki MUNGU
alizowapa wamenyang’anywa na ndugu na wachawi haya ni mambo ya kiroho. Wale
wanaosema wanataka wakipita tu wapendwe, wametafuta riziki za kupendwa kwa
majini au ning’are uso. Hata ukipaka mafuta unang’aa. Ila tatizo watu wana
makontena mizigo ya riziki za shetani na ukicheza wale adui zako wanaenda
kukuombea kwa shetani upate mabaya na usipokaa vizuri riziki za shetani
zitakuingilia kama hasra, chuma ulete lakini usiogope nataka nikufundishe jambo
linda sana riziki zako, mwambie MUNGU naomba unipe riziki zangu, niliomba
vibaya kwa kujua na kutokujua, niliomba masanamu na nikazidi kupokea, na
nilipokea toka umepokea ulishakataaga na
ndio maana riziki za MUNGU hazichangamani na vitu vya ajabu, vitu vinapanda na
vinaporomoka. Mwingine ameua ndio akapata baiskeli, siamemuua mtu, Kaini
alimuua Abeli ambaye aliomba dua zake na riziki kwa MUNGU lakini Kaini yeye
alikuwa na roho mbaya na wivu akaomba vibaya na alikuwa mchoyo hivyo hakupewa
riziki na MUNGU, hata wewe unaweza ukawa unaomba kwa MUNGU lakini anaona moyo
wako ni mchoyo riziki haziji. Utabaki kusema mbona MUNGU anampendelea huyu,
kwahiyo hata leo hii kuna wakristo wengi wanaona wengine wamefanikiwa wanasema
kwanini huyu hao hawana tofauti na Kaini. Ni vizuri ungejua ni wapi umekosea
ili riziki zako zije, kusamehewa ni riziki.
Bwana YESU Asifiwe!
Lakini hii sala ya baba yetu inatumiwa na mpinga kristo, inatumiwa kwenye
sanamu, inatumiwa kwenye kisima, kila mahali watu wanashika biblia na wanataja,
lakini MUNGU anaangalia ni wapi, Je ni mahali pake? Mahali panapoitwa pa Bwana
yeye MUNGU anapajua na Bwana anamjua mtumishi wake aliyeweka mafuta yake, wapo
waliojiita, wapo walioasi. Bwana YESU Asifiwe! Kama zamani mafarisayo na
masadukayo, kwahiyo hivyo hivyo neno la MUNGU litaendelea kung’ang’aniwa. Mimi
nakufundisha ili usimame imara nahitaji upate riziki kutoka kwa MUNGU, na kama
ulikuwa na riziki kutoka kwake shetani zikuachie, shetani anakupa mikosi sio
riziki yako hiyo. Anasema mtakuwa kichwa, kwanini hauwi kichwa, tabia zako sio
za riziki ya mwenyenzi MUNGU, hauponi ulishasema kule utupe leo riziki yetu
embu itengue ile riziki si ulitaka uponyaji unaweza ukapokea riziki mahali
sipo, hawa wanaokwenda kwa waganga asubuhi asubuhi ni watafuta riziki hao,
mwizi anapoiba usiku anatafuta riziki. Ulishaona mtu anakaa nyumbani riziki
ikamfata hapo ni lazima atembetembe, washetani wanatafuta riziki wakati wa giza
na shetani naye anawapa. MUNGU ndio ana riziki, mwanadamu angekuwa kila kitu
anacho hapo asingeomba MUNGU. Hapa ndipo MUNGU ametuweza na ndio hivi atapata
watu, na shetani naye akashika riziki ili watu wakitaka wakamwombe yeye ili
wawe watu wake sasa wewe sema mimi naomba riziki yangu kwa MUNGU. Bwana YESU
Asifiwe! umewekwa hapa ili upate lakini sasa ile kwa MUNGU ipo hivi sio saa
hiyo hiyo, ila kwa MUNGU utaisotea. Na wanadamu wanapenda vitu vya haraka ila
MUNGU hataki kukupa saa hiyo hiyo kwasababu hataki uporomoke. Utajiri wa MUNGU
anaokupa hauumizi, si unaona wanapewa riziki na shetani mara wanaendesha magari
bila viatu, mara analala chini, chooni tena anaambiwa hakuna kupiga chafya hata
kama choo kinanuka si umetaka riziki. Kuna wengine ni wake au waume za watu sio
riziki yako. Kutafuta limbwata ili upendwe kwa vidawa dawa, utakuwa riziki ya
majini na mapepo hapo iko shida. Injili imekuwa asilimia kubwa sio riziki ya
mwenyenzi MUNGU, maombi sio riziki ya mwenyenzi MUNGU. Mtapewa bure kwa wale
watakaoleta kiwango cha chini shilingi 5000 na watu wanajibu AMEN, hao wote ni
watoa riziki za shetani na utabarikiwa na shetani. Sasa mafanikio na watu
kupata vitu ndio watu wanakimbilia, na mafanikio pasipo riziki ni haramu. MUNGU
anaweza kuwapa kiongozi ambaye ni riziki yake mkiikataa mnabaki na haramu, mimi
nashangaa watu husema nguruwe haramu lakini mzoga hawasemi ni haramu wanakula
tu. Mkono wako umewekewa vitu vya kupata, wengine husema mkono umeibiwa wakati
bado upo unakula nao ugali, lakini kuna vitu vikishachukuliwa basi, akili yako,
ufahamu wako, na ndipo pale ulipo kazi unafanya sana lakini haunyanyuki, riziki
zako yupo anayetumia, acha tumyang’anye anayetumia riziki zako. Lakini na wewe
utubu pale ulipoomba riziki kwa waganga, hata shetani ni baba unapopata ubatizo
na kuomba riziki kwa ambaye humjui ana pembe, ana mkia katika ulimwengu wa roho
huyo ndiye baba yako, wakati nikipigana na shetani katika ulimwengu wa roho
anaposema acha watoto wangu kwanini? Ukifuatilia unakuwa ulimkiri shetani kwa
kujua na kutokujua, kwenye sanamu ulisema Baba yetu nisaidie, unamjua. Sasa
MUNGU anachoangalia unaposema Baba naomba riziki, anaangalia ubatizo,
anaangalia mtumishi aliyemuweka na kwenye ulimwengu wa roho ndio kunakuwa na
haki ya maombi yako kupenya mpaka kwake anakupa riziki. Usipokuwa makini kwa
vitu ambavyo vimepinda pinda havijanyooka tayari umepokea riziki nyingine,
umechukua mwana.
Watu wengi sana
shetani alikuwa ni baba yao. Husema “Baba yetu uliye mbinguni” sawa wewe
unampenda lakini msingi ulionao ubatizo sio wake, na hakuna kuokoka hapana.
Unajua MUNGU ana watoto wake na fomula zake anataka waweje, shetani naye
anataka hivyo hivyo. So usije ukashangaa hata mtu anacheza madhabahuni
anamtukuza MUNGU kumbe yeye ni riziki ya shetani katika sehemu za mashetani.
Wewe hujawahi kuona mtu ni jambazi anamshukuru MUNGU alikwenda kuiba akapigwa
risasi lakini hajafa, na anatoa sadaka ya shukurani amesimama kanisani. Sio
hivyo tu atakuja na mzee wa kanisa aliyeloga ili apate cheo anasema, namshukuru
MUNGU kwa kunipa nafasi yakuwa mzee wa kanisa kumbe yeye kila siku anashinda
kwenye vibuyu, hivyo mnakuwa na mzee wa kanisa sio riziki. Bwana YESU Asifiwe!
Unakuwa na nguvu ambazo sio riziki kutoka kwa MUNGU, maisha yanachakaa, maisha
yanaharibika hapana kijana simama imara, amua leo kwamba mimi ni riziki kutoka
kwa MUNGU. Na Kama riziki zinamsubiri mwanadamu anataka za giza, anataka za
MUNGU na MUNGU yeye anafanya. Ukiangalia riziki nyingi huku duniani ni za
shetani kuanzia wafalme mpaka mwenye sifuri, asilimia kubwa ni riziki za
shetani, unafikiri angempataje mwanadamu, mwanadamu anapenda vitu. Leo hii
kusingekuwa na riziki za shetani usingesikia watu wanauana, makafara,
usingesikia. Na MUNGU akaona dunia hii imechafuka shetani ndio amefanyika
riziki kwao akamtuma YESU. Haya YESU amekuja riziki anakusamehe, akupe amani,
ufate njia zake maana yeye ndiye njia lakini hautaki maana umejiita tu wewe ni
wa Bwana YESU, utaambiwa mnafiki pita kule siku ya mwisho. Pata picha hukumu
ingekuwa ni sasa hivi kama jaji anavyosema kipengele kwa kipengele watu wengi
dunia hii ni waovu, na bado wanajitia moyo sisi ni waovu badilika sasa, kila
siku wanakufa wanaondoka ukishakata roho hakuna anayekuombea itasaidia bali
unakufa na tiketi yako ya uovu, unakwenda kwenye jela kubwa huko kuzimu
unasubiri siku yako wewe mwalifu. Niwaambie shetani anawachekea hapa lakini saa
ukishakata roho!! Mimi nimeshaonaga mpaka wafalme wanavyokamatwa, wanapigishwa
deki vyoo, na vyoo vya kule vinyesi vya kule ni vitu vya ajabu, lakini huku
alikuwa ni mfalme akitembea saluti na mabodigadi sasa wanajuta watoke lakini
haiwezekani. Kwa sababu tayari muda wake umekwisha unadanganywa na sala za
wahubiri kwamba tutakuombea nchi nzima lakini hakuna kitu, ninachokwambia sasa
mpokee BWANA, hiyo ndio sheria ya MUNGU. Hapa duniani wanasheria wanaweza
kumchezea jaji au hakimu kwa kuhonga lakini siku ile hakuna mwanasheria wala jaji,
matendo yako yataonyeshwa na TV inaonyesha huyo ambaye hataki kuokoka, anavizia
riziki za ndugu yake anataka kumuua ili apate riziki zake wewe ni muovu, lakini
njooni kwake hata anayetafuta riziki zako MUNGU atafanya vita na yeye.
Bwana YESU Asifiwe! Neno
la MUNGU hili kila wakati linabadilishwa liwe riziki ya shetani, limeandikwa
hapa usiabudu miungu, nyie mnaendaga kikwenu, je hiyo ndio nini? Huo ni uhalifu
hiyo kwenda kikwenu kuingia ndani na fagio tano na kichura ni miendo ya kiungu
hiyo, achana na hayo mambo yalishafanya watu watumwa. Bwana YESU Asifiwe! Ndio
maana leo hii watu wakisikia ukija utafanikiwa utapata kazi, nenda utanyolewa
na nywele na kunyang’anywa na hizo riziki ulizokuwa nazo na maisha yako huzidi
kuharibika, unaibiwa wanapewa wengine na wewe unabaki na ujinga. Unakwenda kwa
mganga unachanjwa damu hapo mwanadamu huwa anashangaza, anakuwa kama mwehu.
Embu mtu aje na kiwembe akwambie akuchanje sehemu ya mwili wako kama utakubali,
lakini ukishakuwa mwehu utakaa na kwenye kichaka, unapoambiwa unatakiwa
uchanjwe nyuma ya kalio la kushoto unatulia na kukubali kuchanjwa kisa
anatafuta riziki. Nimeombea watu wengi yaani kuna vitu vya ajabu sana, riziki
ya macho yako ya leo, unajua MUNGU leo anajua unakula nini, na kesho, riziki ya
mavazi yako, riziki ya neno lake. Lakini sasa kuna watu wanafata kimwili zaidi
kuliko kiroho, sasa utegemee pia kiroho iwe ni kwa MUNGU zaidi. Maana hata wale
wa shetani wakishapata ile riziki ya kiroho zaidi ya giza ndivyo shetani
anazidi kuwafanikisha kigiza zaidi na kuwapa nguvu zaidi. Bwana YESU Asifiwe!
Mtu anayeshiba sana anakuwa na nguvu zaidi, achaneni na hizi riziki za shetani
pokea! pokea! pokea! Utapokea visivyopokeleka. Sasa ndio shida hapo umempokea
YESU, pokea riziki ambayo hata kama ukifa utafufuka na utapaa, lakini sasa watu
riziki ya kupaa hawataki. Wanasema kuhusu dhambi za asili lakini je huyo mtoto
amepata wapi, je huyo mwanaume na mwanamke walitoka wapi kwanini usimfuate YESU
unapindisha neno la MUNGU unapoweka baba au mama wa ubatizo, mimi mwenyewe
nilishakuwa nikawa muovu lakini MUNGU amenisamehe kwa kujua na kutokujua na bado
watu wanalelea uovu, kuchafua neno la MUNGU na kuvunja sheria ya MUNGU, shetani
anaendelea kuwadanganya anajua mnakwenda kufungwa maana ni waovu. Utasema yule
aliyetukana yule ni muovu, lakini uovu wa kwenye biblia msiwe wachawi ni
wachawi, kwenye cheti cah kuzaliwa mkristo lakini muovu, hata kama ni askari,
hata kama ni mwanajeshi, mfalme lakini ni muovu mbele za MUNGU wewe ni kiumbe
chake ndio maana uanakufa.Tumeona wafalme, malkia wakipita, tumeona kina Farao
wakipita, kina Musa wakipita watu wamekufa na uovu, wanakufa na kufungwa. Yaani
kama hujaokoka ukifa umefungwa, unakufa na ufungwa wako sema unasubiri ile siku
ya mwisho na ile riziki ya mwisho ambayo ibilisi amekupa ya kupigwa moto na
yeye, na riziki aliyotoa Bwana YESU ni kuuridhi uzima wa milele ambapo ni
furaha na kumshangilia baba yao mbinguni. Watu hawataki riziki, unaenda kwenye
maombi wanakuuliza ivi huna kazi wewe achana na yeye, watu wanaangalia kazi
sana huyo MUNGU siku akikunyang’anya hiyo kazi wataanza kusema naomba
mkaniombee kanisani kwenu, lakini hata ukiombewa haikusaidii maana wewe unataka
riziki za MUNGU lakini hautaki cha MUNGU. Huku duniani wakisema kitu ambacho si
riziki hakiliki sasa mbona mnakula vitu vya shetani, lakini roho inakula na
kinachotafutwa ni roho yako ile kitu ambacho sio riziki ndio maana usiku
unakula, unakunywa vile vitu unavyolishwa sio riziki ni vya kuharibu maisha
yako.
Bwana YESU Asifiwe! Kuna
watu wanapenda riziki za paka, nasema paka maana yake uchawi na hupenda kutumia
paka sana. Wakilia tu kwa namna fulani huwa ni watafuta riziki hao, amka omba
na kupiga hao ni wezi wa riziki. Hata mbwa anapolia mlio fulani lakini hauoni
mwizi wala kitu chochote hao ni waiba riziki, mbwa anamuona mchawi na mchawi
hampendi mbwa hivyo hulia kuashiria waiba riziki ambao ni wachawi, na wakikaa
muda mrefu ndio hubomoa haswa, hata kuja na magari kubeba riziki. Bwana YESU
Asifiwe! Riziki zako utazilindaje?
Utazilinda kwa maombi, funika kwa damu ya Yesu, hata katika kutoa fungu
la kumi MUNGU anasema atamkemea alaye, aibaye ni nani? Ni riziki. Kwa hiyo MUNGU
anakupa kitu na humtolei tena fungu la kumi hivyo zinakosa ulinzi, wakija
wanatafutaga mlango hata waizi wakiiba mahali wanaangalia ni wapi watapita,
wakikuta kote kumefungwa vizuri wanaisoma namba.
Ni muhimu kuangalia
unayeita Bwana kwasababu hata shetani ni aina ya bwana kama ilivyo bwana
mifugo, bwana shamba hivyo ni vizuri kujua kutofautisha hizi bwana kuanzia
Bwana YESU, maana zipo za kwake na zipo feki. Bwana YESU Asifiwe! Basi kitu
ambacho umenyang’anywa riziki yako nakwenda kuomba na usifikiri mtu akichukua
riziki yako kiroho itaonekana kile alichonacho ni cha kwake lakini sio chake.
Sasa unaomba nini MUNGU akupe riziki wakati alishakupa nyingi na zimechukuliwa
wacha zirudishwe. Bwana YESU Asifiwe! Lakini utunze sasa riziki zako na
kuzifunika kwa damu ya YESU, mtu anaweza kuwa anaishi maisha ya ajabu ya
kifalme kumbe ni riziki zako, tena akakuajiri na wewe na anakupa mshahara
anakukata. Na tabia nyingine za waiba riziki akaikupa hela lazima azifanyie
mambo, kabla watu hawajalipwa mishahara labda zinapelekwa kaburini, au mnalipwa
hela usiku tu. Mimi nilishafanya kazi mahali siku ya mshahara boss anatoa hela
kwenye mguu. Kama hujui huwezi kuelewa. Ukishika hela haikai, unakuja na riziki
lakini zina mambo. Ni ajabu sana kanisa kudharau kwamba hakuna uchawi, watu
wengi wanapigwa na wachawi kwasababu wanaamini ukishakaa kanisani na kuwa
mkristo na imani hawakuwezi, Ni lazima usimame kuna vita. Usitiwe moyo kwa
kuombewa na vitabu vya nyimbo vingi amekufa kwamba bwana atakupokea tuonane
bandarin, je hiyo bandari unaijua, sisi tutapanda boti au tutapaa. Tuende kwa
amani ya bwana je ni bwana yupi? Ametoka Kwa udongo atarudi kwa udongo
tutakutana naye je mtakutana wapi? Kila mtu ametoka Kwa Bwana Yesu.
Maombi: BABA MUNGU ninakushukuru tazama wewe
YESU uliwafundisha watoto wako waombe riziki kwako, najua una mpiango mingi ya
kuwapa na mimi nikisimama katika neno lako kutoka Mathayo ya kwamba ni wakati
wa kuwapa riziki, na wale waliopewa riziki ambazo sizo zikaondoke wako ambao
watoto wao wamepewa riziki za ajabu, riziki za utundu, uchokoraa, tabia za
ajabu, wako ambao wamepewa riziki mpaka watakavyokufa wawe sifuri, eeh! Yehova
ninakuomba uangalie neno lako Mathayo 6:11 riziki ya kwanza ;
SALA YA TOBA:
SEMA :Bwana YESU naomba unisamehe dhambi
zangu zote, uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele,
namkataa shetani na mambo yake yote na riziki zake, nikimaanisha mambo yake,
tabia za kwenda kwa wachawi, tabia za uovu, riziki za adui hizo, na vifungo
sivitaki maana vingine niliomba katika madhabahu nilizotokea ambapo sehemu
nyingine kulikuwa hakuna MUNGU nikaomba nipokee na kweli nikapokea,
nikabadilika, nikapokea kufeli tu, kurudi nyuma tu, YESU nimekukimbilia wewe, Asante Yehova. Amen.
Imeandikwa na Mtume
na Nabii,
HEBRON
WILSON KISAMO.