Pages

Thursday, January 7, 2021

 

HERI YA MWAKA MPYA!  HAPPY NEW YEAR 2021 - MWANZO 1:1-13 

                   Baba ninakushukuru kwa siku hii njema ya leo, mfalme uliyeumba mbingu na dunia, uliumba siku, miaka, masaa, uliumba sekunde, ulieumba miezi, ikiwa ndio mpango (plan) wako kwa sisi wanadamu na kwa viumbe vyote, ninakushukuru Bwana, Leo hii umetupa mwaka mwingine tena wa 2021 kutoka mbinguni, wala si mwaka wa shetani, naendelea kulifungua anga na kulitakasa naendelea kuvunja kila mipango mibaya ya miungu, MUNGU ninaomba ulichokikusudia kikatendeke na kusiwe na kitakachoweza kukunyamazisha. www.prophethebron.or.tz. Ninakumbuka MUNGU siku ya kwanza mpaka ya sita uliumba dunia  MUNGU na leo MUNGU ni mwaka mpya  kwetu sisi wanadamu uliotupa, mwaka mpya, mambo mapya,  baraka mpya, nguvu mpya, uwezo mpya, fahamu mpya, uwezo mpya, mamlaka mpya, furaha mpya, upako mpya, uweza mpya utajiri mpya, kiwango kipya, ndoa mpya, cheo kipya, siku mpya,  masaa mapya, sekunde mpya, dakika mpya, miezi mipya kila kitu kipya, ubarikiwe MUNGU, uzao mpya, kanisa jipya, matawi mapya, wokovu mpya,  ufufuo mpya,  zaidi ulinzi mpya, speed mpya, ufahamu mpya, kufaulu kupya, kusogea mbele ya MUNGU  zaidi upya,  Kazi za mikono kuzipata kupya, taifa jipya, uchumi mpya. www.prophethebron.or.tz

                   Happy New Year! Kwa Bwana YESU, Kwa MUNGU wetu na kwa Maserafi, Happy New Year kwa Malaika na serikali yote ya Mbinguni, Happy New Year kwa kanisa na Matawi yake yote na kwako ndugu msomaji, Asante Mungu Baba, Asante Bwana Yesu, asante Roho Mtakatifu. www.prophethebron.or.tz

                   Napenda nikuambie kuwa siku ya Leo ndio siku ya ushindi wa Mwaka Mzima kwako, Bwana YESU asifiwe. www.prophethebron.or.tz. Naona mmevuka mwaka  Umevuka eti,  lakini nataka tujifunze jambo moja  tumesoma kitabu cha Mwanzo 1:1-13 lakini endelea kusoma mpaka mwisho, tukaona mwanzilishi wa siku na Miaka ni MUNGU, ikawa asubuhi, ikawa mchana na sasa inakuwa asubuhi na inakuwa usiku anayofanya hayo ni MUNGU,  Bwana YESU asifiwe. MUNGU ametupa mwaka, umeshajiuliza na kwanini unaitwa mwaka mpya? Ni kwasababu bado hatujautumia ndio maana unaitwa mwaka mpya, siku mpya, mwezi mpy,a masaa mapya, siku mpya, sekunde mpya, dakika mpya, kwa sababu bado hujazitumia,  yale yaliyopita mwaka jana na tangu ulipozaliwa muda, masaa, miaka, ulishayatumia. (Used) Bwana Yesu Asifiwe, nilipokuwa nikiongea na MUNGU juu ya mambo Fulani, aliniambia mambo makubwa ambayo yanatisha, ila nitakueleza kwa kiwango chako www.prophethebron.otz  Unajua maana ya mwaka mpya? Maana yake kama umeanza na MUNGU unakwenda kuwa mpya, nguvu mpya, kama umechakaa unaendea kutengenezwa, kama umepwaya unaenda kuwekwa sawa (kufutishwa) Bwana Yesu asifiwe, Naomba nikuulize umepokea mwaka kutoka kwa MUNGU au Miungu, waganga au bado hujapokea mwaka, yamkini katika maisha yako ulishiriki mambo kama hayo, ambayo ni kinyuma na mambo ya MUNGU, napenda nikuambie kwamba ulipoteza miaka hiyo na ujue kuwa ulivuka au ulipita na miaka iliyokwisha kutumika ndio maana ulipwaya. www.prophethebron.otz

                    Hata majini nao hung’aania mwaka mpya, Naomba nikuulize hivi majini, wachawi, au mashetani Je! Watapewa Mwaka mpya na MUNGU? Jibu ni hapana. Majini, Miungu na mawakala wa shetani hawa hupewa mwaka na shetani, yamkini na wewe ulishaenda au ulishawahikwenda kwa mganga kutafuta ulinzi wa miaka yako, ulinzi wa mwaka mzima yamkini kwa mababu na mabibi, na baadhi ya watu wanasafari sehemu mbalimbali wakienda kutafuta  miaka kwa mizimu ili Mizimu iwalinde mwaka mzima na sio ulinzi wa MUNGU. Heri yako wewe uliyekutana na MUNGU na siyo miungu na ukapewa mwaka na MUNGU maana MUNGU ndiye atendaye, MUNGU ndie afanyae. Ila Mizimu, waganga, shetani mwenyewe ni takataka huwa wanawapumbaza wanadamu kwamba mtalindwa, kwamba mtasaidiwa, matokea yake unachoshwa na unakata tamaa Bwana YESU asifiwe. www.prophethebron.or.tz

                   Faida za mwaka mpya kama umeanza na MUNGU, mtu ataongezeka, mazao, mali, ufahamu utakua, na kila kitu kitakuwa kipya, lakini unaweza ukavuka na mwaka used au pia unaweza ukabadalishiwa mwaka, watu wengine wanasema mwaka huu mbaya, Tubu, hakuna mwaka mbaya, wewe tubu,  MUNGU hatoagi mwaka mbaya,  Vitu vyake amevikatatisha na ni vitakatifu kwa ajili yako wewe, Bwana YESU asifiwe, unaweza ukabadilishiwa  mwaka na shetani badala ya mafanikio,  unakuwa kituko, kuna mwaka wa wokovu wako, ukibadilishiwa wokovu wako unaondoka, kila mtu ambaye anakataa wokovu ni kwamba amebadilishiwa majira yake ya kuokoka. www.prophethebron.or.tz Usifikiri kuwa shetani anafurahi kuwa umebadilishiwa Mwaka shetani, umepewa mwaka mpya na MUNGU, shetani hafurahi, adui hafurahi kwa sababu umepita katikati yake, adui anajua kwamba umepita katikati yake na umeupokea mwaka kutoka kwa MUNGU tarehe 01.01.  Mpaka tarehe ya mwisho wa mwaka, na kuendelea, kila siku ina kitu chake, MUNGU ni wa mipango, siku ya kwanza alifanya nini?  Mapaka siku ya sita, na siku ya saba akapumzika na kama plan zako zilicheleweshwa au kuchezewa na wachawi na mimi nawachezea haswa leo. www.prophethebron.or.tz

 Kuna majira yatakupata na kuchuma,majira ya kuoa na kuolewa, majira yako  yakibadilishwa utakuwa unazunguka tu, ndio maana kuna majira ya kuzaliwa na kufa, MUNGU ni alfa na aomega,  mimi Hebron nilikuwa naomba katika siku hizi tatu  ili kuhakikia kwamba unavuka na vitu vyako vyote, kila  mtoto wangu  na likiwamo taifa  la Tanzania limevuka na vitu vyake vyote (full) www.prophethebron.or.tz na plan  aliyopanga MUNGU kwa sasa mwezi, siku, dakika, sekunde tarehe, yatatimia  na kwako yatatimia.

                   Kuna majira ya dhambi na majira ya kuokolewa usione wale ambao hawataki wokovu wanafanya dhambi kwa sababu majira yao wa wokovu yameibiwa, tuwaombee wamrejee MUNGU, hata wewe kabla ya kumjua MUNGU majira yako yali yalikuwa yameibiwa, ndio maana ulikuwa haumsikilizi MUNGU, unaweza ukawa umeibiwa siku zako zote zikawa za jehanam, nitapita kwenye maombi. Nataka kuona mwaka huu unakuwa Na mafanikio kweli kweli. Je ulishawahi kuvuka na mwaka uliotumika? Hii ina maana kuwa katika maisha yako mwaka hadi mwaka huwi na mafanikio kiroho wala kimwili watu wengi walishavuka na wengine wamevuka na mwaka used, kunawakati ulipokea mwaka ukiwa vilabuni kwa kelele za mambo ambayo hayamtukuzi MUNGU, kwa kelele unajisifika eti umevuka, umevuka nini? Bila MUNGU? Wengine wamevuka na uzinzi, amelewa, mpaka sasa hujaokoka je  umevuka na MUNGU? Huwezi kusema kuwa umevuka na MUNGU wakati hupendi vitu vya MUNGU, napenda nikwambie jambo Fulani kutaja jina la YESU na kulitumia sio kwenda mbinguni  hata YESU alisema kuwa wengi watatumia jina langu hata sasa watu si wanatumia jina la YESU na hawaendi Mbinguni? Na wananena na hawataenda Mbinguni Mpokee YESU na utavuka nae. Kuna watu wanasemaga yaani siku Fulani ndio nafanikiwaga?  Yamkini na pia mtu anaweza akawaamechukua siku zako, yeye anafanikiwa lakini wewe hufanikiwi ila yamkini kakuachia siku moja au mbili ndo unabakia nazo, na wewe unabakia kusema siku fulani tu ndio naafanikiwaga, zingine zilishaibiwa, umeshaibiwa wewe. www.prophethebron.or.tz lakini Neema ya MUNGU leo itarejesha na nitakuombea hata kama huwezi, mimi nitaomba kama vile MUNGU alivyonivusha nabii wake na wewe utavuka usivuke kimaneno nataka nikuvushe kimatendo. Nilipokuwanikiomba nilikuwa namsikia shetani amepanga mipango mibaya kwa watu wengi tu, sasa na wale  waliokuwaa wamepewa kazi ya kushughulikia wengine, shetani alikuwa anawapiga kwa sababu walipewa jukumu na shetani ili kuwashughulikia watu Fulani hawakuwaweza (wao wamefunikwa kwa Neema ya MUNGU) hivyo sasa shetani anawaadhibu aliowapa kazi kwa sababu wao walishindwa kazi. Na bado watendelea kuchapwa, kuna baadhi ya watu wanatamani wenzao wafukuzwe kazi mwezi wa pili sasa masaa yako na siku zako nitazirejesha na nitakuweka wakfu mpaka Dec, je ni nani atakayekusogelea? Hakuna.  Majini, mapepo na wale ambao wanakunyooshea mkono nao watabakia na maumivu sawa sawa. www.prophethebron.or.tz 

  Haleluya! MUNGU ni mzuri sana na siku ya leo ina maana kubwa sana Bwana YESU asifiwe, Cha kwanza mpokee YESU,   Tukisoma biblia MUNGU aliumba dunia kwa siku sita, lakini kila nilipokuwa nasoma biblia nilikuwa naelekezwa na kufundishwa kwa miaka mingi iliyopita, dunia hii iliumbwa miaka mingi sana iliyopita, hata kabla ya YESU hajazaliwa, lakini kidunia na dunia itasema sasa hivi ni miaka 2021, ni kweli kwa hesabu za kibinadamu, Sasa jiulize kwanini ilianza kuhesabawa baada ya YESU kuzaliwa? Jibu ni kuwa YESU alikuja kuanzisha miaka ya kwenda Mbinguni, ile ya zamani awali kabla ya YESU kuja iliwekwa pembeni, yaani kabla ya kuja YESU, ndio maana anaitwa mwana wa pekee, Bwana YESU asifiwe, Napenda nikufundisjhe jambo. www.prophethebron.or.tz Sio kwamba MUNGU aliumba siku kama hivi tunavyohesabu sisi hapana, Miaka 1000 ndio siku moja kwa MUNGU, kwako wewe mwanadamu, kwa siku moja ya MUNGU,  kwa majira  ya kibinadamu ni miaka 83, ila cha kustaajabisha baadhi wakifika miaka 83 tu hawezi fanya jambo lolote, hapo hawajamaliza hata siku moja ya MUNGU,  MUNGU akaumba dunia kwa siku 6, ambayo ni miaka 500, kwa hiyo sio kuwa aliamka jumatatu tu akaanza hapana alitumia masaa milioni 262,800,000 kuumba hii dunia, hayo  ndio baba yangu anavyonifundisha kaniambia “nilifanya hivi Hebron, nikafanya hivi” www.prophethebron.or.tz.  Ndio maana biblia inasema siku moja kwa MUNGU  ni miaka 1000 Bwana Yesu asifiwe, Mwana wa  MUNGU, ambaye ni Bwana YESU amezaliwa katika miaka ya kimungu ni siku 2 tu na siku chache tu, ila kwa majira ya kibinadamu ni  83+83=166.  Tunaelewana, nitawafundisha wakati mwingine na haya ndio baba yangu aliyonifundisha. Najua kuwa ni sekunde ngapi alizozitumia, hata Musa alielekezwa na MUNGU mbona sana mnashangaa? Bwana YESU asifiwe, Wanadamu wengi hawafikishi hata mwaka katika hesabu ya miaka ya MUNGU wengi hufa wakiwa na miaka 40 na kuendelea au hata chini ya hapo. MUNGU akaumba, akatamka haya zimekuja, kimungu ni siku mbili tu toka YESU azaliwe na hiki kizazi hakitapita Yesu atarudi, kinaitwa kizazi cha nyoka, amesema atazaliwa, atakufa, atafufuka, atapaa, na ikawa unaona MUNGU anakwenda kwa saa, kwa wakati na kwa majira na wewe  siku yako itatimia, kifo cha YESU walifikiri hatafufuka na walifikiri kuwa watamwibia ufufuko wake, hawakuweza kwa sababu ulikuwa ni mpango wa MUNGU,  alifufuka yamkini na wewe  umeibiwa vitu katika miaka yako ili visifufuke Au umebadilishiwa  miaka, nitakuombea jinsi vile atakavyoniongoa MUNGU, Nadhani umeshawahi kusikia kuwa wachawi wenye level ya juu wanaenda kurenew miaka,  nakwambia sasa watakufa, labda tu waje kwa YESU, hakutakuwa na hiyo nafasi ya kurenew uchawi,  watubu wamrejee MUNGU hiyo ndio salama yao vinginevyo, ndio itakuwa hivyo (watakufa) nimesema wala sio jambo la kuomba, maana huu ni mdomo wa MUNGU, Usishangae! Nabii ni kinywa cha MUNGU. Yesu mwenyewe katika hii miaka ambaye ni kizazi chake,  ambacho YESU  atakuja kulichukua kanisa, MUNGU mwenyewe anajua  kuwa ni mda gani YESU atakuja kuchukua kanisa, atakuja lini, na atamchukua nani,  kwa sababu MUNGU ni wa mipango,  nataka tukaharibu mipango ya shetani,  hakuna   kitu kibaya kama mtu kuishi kwa kupoteza wakati, “time is money” Wengi husema hivyo  kwa sababu watu wanapenda pesa, kwa sababu watu hupenda pesa sana,  ndio maana wanasema hivyo mbona hawasemi time is food au chochote?   Kizazi hiki kinapenda sana pesa ni vyema, ila penda Pesa, lakini isikutawale, www.prophethebron.or.tz

Umeshawahi kujiuliza kwanini mtu analipwa kwa siku, kwanini mtu analipwa kwa masaa, angalia mimba ya mtoto, inasiku ya kwanza mpaka mtoto anakuwa, alikuwa majimaji, anaanza kuwa na mifupa inafika kipindi mama akienda clinic mtoto anazungukazunguka kwenye tumbo ni kiumbe hai na siku moja anazaliwa, tunaelewana watoto wa MUNGU. JE! Niwangapi mnaona mabadiliko katika miaka yenu? ulikuwa huna mvi sasa unazo, ulikuwa huitwi babu au bibi sasa unaitwa hivyo, unastaafu kwa sababu miaka imeongezeka na hata mwanafunzi akisoma akirudishwa mwaka kila wakati hata kaa amalize shule,  yawezekana  miaka yako imerudishwa nyuma katika miaka Baraka, wokovu,  utakuwa unarudi nyuma tu ila mwanafunzi huyo anapofanikiwa  kurudia mwaka na akafaulu atapata cheti pia watu baadhi ya watu  wamezoea kununa na wapo ambao wamevuka na kinyongo na hasira, mie nakushangaa  umevuka mwaka na wivu na hila kuwa nitamkomesha huyu  jamaa  je! huo ndio mwaka  wako mpya? www.prophethebron.or.tz au ndio mwaka wako na majini shetani na mapepo? Bwana Yesu asifiwe, nakuambia mtapita katikati yao haswa wana wa Israel walipita katikati ya bahari, kibinadamu si jambo rahisi lakini kwa MUNGU kupitia YESU ni rahisi.

                    Nataka nikuambie habari moja   hivi viumbe vyote na vitu vyote havina nguvu aliyonayo YESU, YESU anaweza akaikunja  hii dunia kwenye kiganja, acha nikuambie upone maana watu wanamwona YESU kama Karanga. YESU anaweza akakunja sayari zote kwenye kidole chake, ukuu wake hamuuelewi,  acha niwaambie wanadamu mbadilike, hii dunia  anaweza akaikunja, hivi sasa anarudi, imeandikwa itafika wakati kutakuwa kuna mangonjwa yasioyotibika, si iliandikwa, si majira  yanatimia, MUNGU anajua,  si nyakati kwanini sasa yasitimie?  Lazima yatimie, lakini anasema tena, wewe unayemtegemea utapita katikati yao hata kama namba hiyo ipo. www.prophethebron.or.tz

Watu wengi wamekata tumaini kwa sababu wameambiwa lazima kuchomwa sindano kwa sababu neno la MUNGU limeandika siku za mwisho hutaweza kununua au kuuza bila kuwa na alama ya mnyama huyo ninachokuambia MUNGU akisema kitu amesema na mimi ninachokuambia nimekuambia hii dunia anaweza akaikunja ikawa kama sisimizi mnaelewa kwanini kuogopa haya ninayokuambia mimi, moyo wako na Imani yako ibadilike mtegemee MUNGU kama ninavyokuambia mimi kuwa na Imani kuwa utapita katikati yao.. www.prophethebron.or.tz

                   Dunia kwa kipindi hichi imefika mahali ambapo imekuwa kama wale wana wa Isreal walipookuwa wakitoka Misri, mbele yao wakaona Bahari, hawakujua cha kufanya na wawawezi kuvuka waliona ndio mwisho wao ila MUNGU alimtumia Musa mtumishi wake akamwambia inua mkono maji yakafunguka, wakapita katikati ya bahari, hata leo utakwenda kuvuka. Mkono wa Musa wa Leo ni mimi Nabii Hebron utakwenda kuvuka. www.prophethebron.or.tz. Nitavunja, nitapasua pasua, utasonga mbele kama kuna mawimbi yatanyamazishwa, Yesu ananguvu kuliko bahari anaweza akasema hii bahari ikauke ikakauka, anaweza akasema miti yote iungue na ikaungua www.prophethebron.or.tz naomba muelewe ukuu wa mwana wa pekee wa MUNGU lakini baadhi ya watu wanamwona YESU kama takataka,  Biblia inasema alikuja kwao wala hawakumkubali, lakini wewe mkubali MUNGU si wa kuchezea, ameumba hii dunia kwa miaka 500, kila saa, kila dakika, kila sekunde, bila kupumzika,  kwa hesabu za kibinadamu na kwa majira ya kibinadamu, sasa fikiri kama ufahamu wake unaweza kuangalia kwa miaka 83 ndio siku moja, na akakaa siku sita, nay a saba ndipo alipopumzika je wewe? www.prophethebron.or.tz Wewe ukifikiri kwa ufahamu wako mpaka saa 12 umelala huwezi hata kuamka, sasa Nikuulize swali mfano. Una miaka 30 umeshalala mara ngapi? Umefumba macho mara  ngapi?  Sasa kwanini wengine wanajifananisha na YESU na wanajifananisha na MUNGU? Wafungue macho basi miaka 83 bila kufunga kama wanaweza. www.prophethebron.or.tz MUNGU amempa mwanadamu kisehemu kidogo cha  akili, shetani naye anakitumia na anakutumia wewe kumchezea MUNGU, Tafakari, mrejee MUNGU.

                   Huu ni mwaka 2021 unamambo mapya siku mpya, sekunde mpya, dakika mpya, yote yanakwenda kutimia kwako na huu utakuwa ni mwaka wa mapenzi ya MUNGU kutimia kwako,  lakini sio tu utatimia hivyohivyo utatimia pale ambapo wewe utayafanya mapenzi ya MUNGU,  kuna baadhi ya watu wanatakaga mambo yao yatimie lakini hawataki sheria za MUNGU lakini acha nikufundishe itakusaidia wewe kuvuka watu wanasema dhambi ni tamu na utakatifu ni Mchungu, nakuambia utakatifu ni mzuri, majira yako ya utakatifu yako wapi? Majira yako ya kwenda mbinguni yako wapi? na majira yako ya kukaa na YESU yako wapi? www.prophethebron.or.tz Au umewekewa majira ya kukaa na shetani au unamajini au mapepo kwa shetani majira yake ni mabaya, majira ya shetani yana  mapigo na vilio lakini kwa YESU ni pepesi, ila napenda nikufundishe jambo moja, MUNGU anasema lazima mkafanye kazi ndipo mfanikiwe, baadhi ya watu waliookoka hawapendagi kufanya kazi,  wamekuwa na imani ya kuomba, kuomba omba tu, sio vibaya kuomba msaada ila sasa hufanyi kazi unasubiri kuomba omba unakuwa kama omba omba wa mtaani.  Lakini hebu fanya kazi na MUNGU atakunyanyua siku kwa siku na kama ni mwanafunzi soma atakunyanyua  www.prophethebron.or.tz sio mwaka wa kulia sio mwaka wa kukata tamaa ni mwaka wa kuyaweza yote katika yeye atutiaye nguvu.  Biblia inasema  Neno la MUNGU kila siku ni jipya kwa hiyo neno la MUNGU kila siku ni jipya  wewe umechoka kiimani umekuwa na mawazo machafu,  naona kuna baadhi ya watu wanakutakia mambo mabaya tu na wameshatoa pesa kwa waganga  na wengine wamekuombea mambo mabaya,  waambie hivi,  mimi nimeshika mwaka hayo yote  mtayavuna ninyi na kweli watayavuna kisawasawa,  Bwana YESU asifiwe, ninamshukuru MUNGU kwani hakuna mwanangu yaani muumini wa kanisa hili aliyeshikwa na korona dunia nzima hakuna aliyekufa na Corona, mimi Hebron namshukuru MUNGu kwa hilo sana na niliwaambia kuwa hakuna atakayekufa na Corona na hakuna. www.prophethebron.or.tz  Na sasa nawaambia mtafika, ila nataka pia Baraka zako kimwili uzipate na pia hata hizo chanjo zisikutishe wewe mwangalie MUNGU na mimi nikiendelea kukuelekeza kadiri ninavyopata maagizo kutoka kwa MUNGU na bado naendelea kumwomba MUNGU juu ya maelekezo kuhusu hizi chanjo maana baadhi ni balaa tupu ninyi mwajua ila Mungu atawapitisha MUNGU hawezi kuacha wanawe waangamie katika kipindi cha nyakati za mwisho. Shetani anataka eti mapenzi yake MUNGU ya kukunyakua yasitimie? Haiwezekani Mapenzi ya MUNGU lazima yatimie nakama ni hivyo basi ni lazima kuna maelekezo ambayo atanipa ndio maana anatumia Nabii kutoa maelekezo na usitishwe rafiki yangu haleluya!   Nikuulize swali Je! MUNGU si anaahadi ya kukupeleka wewe mbinguni Jibu ni Ndio.  Kwa hiyo shetani ndio anaahadi ya kukuvuna? Hapana! Hivyo sikiliza ninachokuambia. www.prophethebron.or.tz

                   Imefikia kipindi ambacho wanadamu wamefikia mwisho wa mawazo yao, vichwa vinauma, hawapati ufumbuzi, wanatumia akili nyingi, juu ya hali ya dunia inavyoenenda na juu ya hali halisi ya sasa, magonjwa hayana tiba na wao hawana majibu, na kweli hakuna majibu, hakuna tiba,  ila Jibu ni moja tu  waombe Toba na Rehema na MUNGU atawasamehe hata sasa mataifa mengi yanaomba miungu, wanaomba kwa ng’ombe, kwa miti, majini , na hata baadhi ya viongozi walipewa madaraka kishetani,  kwa hiyo maombi wakiomba wanaomba kwa mashetani, kwa hiyo nchi haziwezi kuwa na upenyo. Mimi Hebron Kabla hata ya Ndege za Nchi kununuliwa niliwaambia MUNGU amesema kutakuwa na Ndege za Nchi, kutakuwa na miundo mbinu kwa ajili ya maandalizi, nah ii ni Eden anaitengeneza ili mataifa waje, na waponee hapa, ni Neno la unabii. Neno la Unabii na siku MUNGU alivyoniambia niliwaambia Ndege zitakuja na niliwaeleza na zimekuja ilikuwa ni siku yake ambayo MUNGU aliniambia  na pia siku ya mataifa kuja na kumiminika hapa Tanzania mpaka mtashangaa inakuja  kwa hiyo miundo mbinu lazima  itengenezwe kwa ajili ya ujio wa YESU najua shetani nae yuko pembeni ananyemelea lakini  na sisi tutaendelea kumpa zake,  wewe ni kamanda wa mwaka wa YESU  ahaaa   Nitakapokuombea na kukuweka wakfu hakuna jini  litakalokusogelea www.prophethebron.or.tz

                   Tunapita katikati yao kwa nguvu na kwa ujasiri  sio kwa maneno ni kama vile mimi  ninavyopitaga, nadunda tu,  mdogomdogo,   kwa Kiswahili mdogomdogo ni kwa maringo na kwa kujiamini, katika hii dunai wanadamu wengi wamebadilika sana mambo yao ni mabaya na ilifika mahali walitaka kumsukuma YESU kwenye korongo  akapita katikati yao, wewe ni mara ngapi umepita  katikarti yao?  Waambie nadunda na YESU na wanaopaa usiku waambie utapita katikati yao ni mwaka wa kupata motto, harusi, lakini pi harusi ikiibiwa hakuna sherehe, mabinti wengi huwa wanajivalishaga pete kwa sababu hajapata wa kumvalisha hivyo anaogopa kuchekwa maana wenzake wamevalishwa, yeye anajivalisha, acha YESU atakupa mwenza / mchumba.  Inakuja siku ambayo Yesu atakuja kunyakua kanisa lake sio jingo, kanisa ni wewe uliyempokea na kufuata sharia zake,  lakini kanisa isiwe la shetani au miungu likiwa hivyo utabakia hapa hapa,   kuna majira ya kupaa  kama Elia na Henoko walipaa ni mpango wa MUNGU,  sio kwamba MUNGU hakujui au hana plan na wewe ni kwamba watu wengi maisha yao yako kwenye plan za shetani. www.prophethebron.or.tz

                   Unavuka mwaka bado unakumbuka jinsi ambavyo mtu alivyokutesaga mwaka jana, kama hujasamehe umevuka na mwaka uliopita, kwanza samehe,  Bwana YESU  asifiwe halafu songa mbele mbele ni pazuri. www.prophethebron.or.tz

                   Siku ya saba MUNGU akapumzika  mpaka leo anandelea kupumzika  anafurahia uumbaji wake, anafurahia alivyokuumba, anangalia kutoka kwenye kiti chake cha enzi  anafurahi, sasa wa watumishi wanahubiri, kama Hebron ninavyohubiri, MUNGU anafurahia  wewe unampigia makofu, unatoa shuhuda, anamfurahia sana na sasa zimebakia nyakati zake za yeye kukuchukua wewe  lakini nawaombea uchawi nitaumaliza, ikiwa u kilema wa kiroho utasimama, mwanamke  huwezi pika utapika,  baba uko ovyoovyo utakuwa fiti, mtumishi huwezi  kusonga mbele utasonga mbele, waliokuwa wanakucheka waambie mmebakia na mwaka used mimi nilishavuka.  Mimi nashangaa Sana aliyekosa ibada leo, hivyi ulizaliwa used au mpya?  Unajua wewe ni mpya kwa sababu hata kidole chako hakifanani na mtu mwingine, Baraka zako hazifanani na mtu mwingine lakini wengine hutamani vya wengine ukitamani vya wengine ujue umekuwa mchawi. Mwambie MUNGU naomba vyangu, unajua unaeza kunga’ang’ania vya mwingine kumbe vyako ni vizuri Zaidi ya vya kwake. Tunaelewana?www.prophethebron.or.tz Je! ni wangapi sasa wameelewa? Katika miaka yako, yaani kila mwaka mpya unavyokuja unavuka na used?  Maana MUNGU ndio nakuangalia hata kama upo online nyoosha mkono. Baadhi walitaka kujenga au kufanya jambo fulani walishindwa kwa sababu walivuka na miaka used. www.prophethebron.or.tz

                   Bwana YESU ninaomba unisaheme dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua Bwana YESU naomba jina langu litoke katika miaka  used ya ibilisi, ya umaskini, vifungo, magonjwa, used ya kutangishwa na shetani, miaka ya maroho yote mabaya, miaka ambayo wachawi walionishikilia, miaka iliyoshikilia  miguu yangu, miaka iliyoshikilia maeneo yote, ninakutaka Bwana wewe ni MUNGU wa mipango na mipango yako ikatimie kwangu kupitia maombi ya Nabii wako Hebron kama Musa  alivyowaombea wana wa Israel niko tayari kupokea Amen.  Endelea kumshukuru MUNGU. www.prophethebron.or.tz

 

Baba katika jina la YESU, Kuna watu ambao wanaishi na vitu vyako wewe ukabakia huna chochote, kuna watu ambao wanabakia kuota upo tu mahali Fulani mfano shule ya msingi, kijijini wakati huko ulishaondoka na uko sehemu nyingine  ina maana  kuna walioiba wakakupa used sema mimi kwa  jina langu ninataka ya kwangu na nimeamua sasa kwa jina la YESU virejeshwe,  Sema Bwana YESU gusa vitu vyangu unavyovijua, unajua aliyutumia, unamjua shetani,  unajua majini, na vihitaji YESU, maana ni haja ya moyo wangu na wewe Bwana ni haja ya moyo wangu mimi kutembea  nawe ndio maana ulinipa kwa utukufu wako, nimekuwa nikiishi kwenye vifungo kwa mda mrefu. Amen.          www.prophethebron.or.tz

                   Yako majira yaliyonunuliwa na wachawi na wako walioiba wakapata vyeo, ndoai, utumishi wa shetani, ufahari, Baraka, utajiri na mengineyo, Kuna nguvu ya kurejesha vinarejeshwa kwa jina la YESU. Majira yaliyoibwa yanarejeshwa. Nautamkia mwezi wa kwanza mpaka wa kumi na mbili utapita katikati yao mpaka wanaoabudu miungu watashangaa utapita katikati yao mpaka wao watamfuata MUNGU unayemwabudu. www.prophethebron.or.tz

                   Baba ibariki Tanzania, mbariki Raisi wa Tanzania, bariki uchumi wa Tanzania, ni nchi yako, ni Eden, kama ulivyoniambia nami nimetamka Baba na ndivyo ilivyo na kila mmoja ikawe utakavyo MUNGU. www.prophethebron.or.tz

                   Eee Mungu wa Mbinguni uliyeumba mbigu na dunia najiweka mikononi mwako kwa jina la baba na la Mwama na la Roho Mtakatifu, mimi ni kiumbe chako, uliniumba kiumbe kipya, na nikaokoka nikawa kipya  sasa najikabidhi kwako unifanye upendavyo katika jina la YESU. Amen. www.prophethebron.or.tz

                   Asante Bwana;   Mliopo kwenye nchi mbalimbali, nawaombea, amani na furaha, magonjwa, yawakimbie, wala yasiwapate, Baraka zishuke kwenu, milango ya Baraka naifungua mingi sana, yule alaye namwangamiza. Nayaombea matawi ya kanisa lako Baba,  ulilonituma kulianzisha na  kondoo na watumishi wangu  Baba, Baba, Baba, wajaze, watie nguvu, wafanikishe,  asante baba, asante baba, asante baba,  Baba endelea kuwalinda watu wasife na Corona,  tazama wazungu wanakufa sana, Bwana ni watoto wako,  na wengi hawakujui Bwana,  naomba rehema kwa ajili yao, Bwana zote ni rangi zako Bwana  ninajua kila mtu ana damu  nyekundu MUNGU ni rangi tu za ngozi tu ,zimekuwa tofauti  oh. Baba naomba uwaponye, naomba toba na rehema kwa ajili ya  maraisi  na wafalme na kwa ajili ya serikali mbalimbali baba,  naomba uondoe hili pepo,  ili mapenzi yako MUNGU yakatimie, sifurahi watu kufa,  ninahuzunishwa mfalme,  ninakuja mbele zako  mfalme, ninaomba Bwana,  nimefunga kwa  ajili yao na kwa ajili ya Taifa letu. Baba, Baba najua wako wengine waliofunga pia, najua Mimi nimeongea nawe kivyangu na kila mmoja umeongea nae kivyake, nakumbuka uliloniambia ukalitende Bwana, ukawainue.

                   Amani  ya MUNGU iwe nanyi na Amani ya Bwana  YESU iwe nanyi  Muendelee kuongezeka  kibaraka, kiamani, kwa faraja,  mliochoka miili muwe vijana, mliokuwa mkitembea kwa kuchechemea muwe na nguvu kama  vijana . Bwana YESU asifiwe, MUNGU awabariki sana MUNGU awe nanyi Muende na amani ya Bwana.

Prophet Hebron