Pages

Tuesday, January 26, 2021

SABABU ZA YESU KUJA ULIMWENGU AU KWANINI YESU ALIKUJA ULIMWENGUNI - YOHANA 1:1-15, 19

 

Baba ninakushukuru, asante kwa mda huu, asante kwa neno lako, asante kwa fadhili zako, ninaendeleka kuharibu kila mipango ya ibilisi kila mahali, MUNGU ukathibitike, Mungu ukawajenge, Mungu ukawatie nguvu kwa viwango vingine, nakushukuru kwa mwaka mpya wa 2021,  naomba  yakawe mapya katika maisha ya watoto wako. Bwana Yesu asifiwe. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Yesu ni Bwana na Mwokozi wa Mataifa yote, ana neema, ana uzima, ana utajiri, ana ukombozi anakupenda sana, mshangilie Bwana Yesu. Yesu ni rafiki yako, amekuja kwa ajili yako, mwambie asante Yesu, ameleta neema  na  nguvu, utakatifu, kuitwa mwana wa MUNGU ni neema ya ajabu mwambie Yesu nakushukuru, Mpigie  MUNGU makofi, Mpingie Bwana Yesu makofi, mpigie Roho Mtakatifu mwambie MUNGU asante kwa sababu Ninasimama kwasababu ya neema yako, nimekuja kuambudu kwa sababu ya neema yako, nimekuja kuambudu kwa sababu ya neema yako, sina cha kukupa mfalme, nasema asante nishike mkono Bwana, niwezeshe Bwana Hata kama kuna majaribu, najua majaribu ni mtaji, nilipata hasara sana, majaribu yaninishinda lakini sasa ninapokea upako wa kushinda majaribu. Haleluya, Haleluya, Nampenda Yesu sana, nampenda Yesu sana, kazi yangu ni kumtete YESU lakini wewe unamteteaga YESU? Yesu anatetewa kwa kusema kweli tu na kwa kutokuongeza au kupunguza yale yaliyoandikwa katika neno lake.  www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Kwanini Yesu alikuja ulimwenguni? Kwasababu kulikuwa na lengo, pasingekuwa na lengo asingelikuja, pasigelikuwa na lengo la baba yake, angelikaa Mbinguni tu mpaka leo, lakini nataka nikuulize na wewe? Yesu amekuja hapa dunia, Je! lengo lake unalitaka au unalipuuzia??  Au unaliona sawa tu, rafiki yangu angalia sana ili siku ile ya mwisho kusudi liwe limetimia kwako ila usipokuwa makini basi  utakuwa umelikataa kusudi lake na hutalipokea. Bwana Yesu asifiwe, www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Hapo mwanzo kulikuwa na Neno,

          Tumesoma Neno la MUNGU, akasema akatumwa mtu toka mbinguni, lakini huyu ambaye tunaongea habari zake, yeye alikuwepo tokea hata ulimwengu huu ulipoumbwa alikuwa na baba yake,  Bwana yesu asifiwe, ina maana ni mwana wa pekee wa Mungu, mzaliwa wa kwanza, inamaana YESU ndio mtoto wa kwanza wa MUNGU , mwana wa pekee, sasa Kwanini alikuja hapa uimwenguni kwa sababu hii dunia hapo mwanzoni ilikuwa nzuri sana na MUNGU aliiimba vizuri sana na alipotupwa shetani akaja  akaiharibu  dunia, na ndipo mwana wa MUNGU  akamwambia baba nitume mimi niende, awali kulikuwa kuna uzima kila mahali ila  alipokuja shetani kukawa kuna mauti, kwa hiyo vitu vyote na viumbe vikakosa uzima, na ili uzima urejeshwe na MUNGU ilikuwa ni kupitia kwa Bwana YESU tu, Bwana Yesu asifiwe,  Uzima ninaoongela ni uzima katika roho, kuna uzima wa aina mbili, kuna uzima wa kimwili ambao upo katika mpango wa MUNGU na kuna uzima wa milele ambao pia upo katika mpango wa MUNGU na kuna mauti ambayo inakaa na mwanadamu lakini anaishi na  kuna mauti ya kiroho ambayo intembea na mwanadamu kiroho lakini hafi, vyote hivyo vinategemea kukaa juu ya mtu, kwa hiyo kama huna uzima una mauti, kwa hiyo kila mwanadamu na kila kiumbe  ili kiwe na uzima lazima kimpokee  Bwana Yesu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Biblia inasema, akaja kwao na wakamkataa huo uzima, uzima ninaofundishha au kuzungumzika ni katika roho,  unapomkataa na hata kama unamtaja Bwana Yesu, hutakuwa na uzima na kama kungelikuwa kuna uzima, Yesu asingelikuja, lakini dunia imebadilika uzima hakuna, na watu wanazuiwa kumpokea Yesu. Kwanini Yesu anaitwa Mwokozi wa ulimwengu?kwa sababu yeye ni Mwokozi wa kila kitu, viumbe vyote  ni mali yake, ila vilishaingia katika mauti naye Yesu akaja kuviokoa, ni ajabu sana watu wamepataa corona na wanahangaika na chanjo,  ni sawa kuitafuta chanjo, lakini dunia ingelihangaika, kila mtu amtafute Bwana YESU, kutafuta uzima wa Yesu kuokoka, kwa sababu uzima kupitia Yesu unaondoa corona. Umezaliwa hapa duniani, na umezaliwa na mauti ndio maana Yesu akafa, ili utakapompokea yeye na atafufuka, ila ipo shida neno la Mungu limepindishwa pindishwa ili watu waendelee kuwa na mauti. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Yesu amekuja kuikombo dunia, ila dunia nayo inashaangaa, kwasababu dunia ilizoea mauti na sio uzima. Hata wewe ambaye umepokea Yesu unakuwa na uzima wa Mbinguni japo kimwili upo hapa, na kama hujaokoka unaweza kimwili uko hapa na unaishi lakini ukawa na mauti ya milele hata ukifa hutaenda mbinguni, hebu mpokee Yesu, hebu tunza huo uzima ni kitu cha thamani kuliko vyoteulivyonavyo, Bwana yesu asifiwe. Yesu ndio kila kitu katika vile vizuri njia mojawapo ya kwenda mbinguni ni kuupokea huo uzima, unataka kujua huo uzima unapokelewaje? Ni Kwa kukiri sala ya toba, hebu jiulize uumekaa na mauti kwa mda gani? Je ni Uharibifu gani umetokea kwako kwa kukaa katika mauti mda huo wote? na wengine mpaka sasa ambao hawajaokoka ni sawa na kusema  bora kuishi na kifo, kuliko kuokoka,  lakini nina habari njema ya kukufundisha, nataka shetani apate hasara,  kama hujaokoka mpaka sasa hivi ujue wewe una mauti kwa sababu ile siku ya mwisho Yesu atachukuwa wale wenye uzima wake, wale walioupokea na neno la MUNGU halitakiwa kugeuzwa linatakiwa litekelezwe na kufundishwa kama lilivyo, inastaajabisha sana kwani baadhi ya wahubiri waliopo katika dunia hii ni mwalimu lakini ni mwalimu wa uongo,  kazi ya mwalimu ni kufundisha, umefundishwa kusuka, kuendesha gari, kupalilia  na kazi nyinginezo aliyekufundisha huyo ni mwalimu, sio lazima awe na degree, mambo mengi watu hufundishwa kutokana na shughuli za kila siku na ni automatic hata kama hujaenda shule unaweza kuvifanya kwa sababu umefundishwa na  vitu hivi tumezaliwa navyo kwa neema ya Mungu, nikuulize, nani anamfundisha samaki mdogo kula? Au hata mtoto aliyezaliwa kunyonya, Hakuna, ila yeye mwenyewe hufungu mdomo. kuna vitu ambavyo mwenyezi Mungu ametuwekea ila shetani ameviua/amevifisha  ili  watu wasimjue Mungu, na ndivyo ambavyo amefanya ili watu apotee kupitia waalimu wa uongo, walimu wa uongo hataitwa wa uongo, inashangaza mwalimu wa masomo ya hesabu, chemistry , jographia anafundisha vizuri sana  kuliko mtu anayehubiri au kufundisha kupitia biblia, watu wametolewa kwenyye mwongozo thabiti wa Mungu na wamefundishwa uongo,  mfano: waalimu wakiwafundisha uongo wanafunzi wanaosoma siku ya mtihani wasahihishaji ndio watakao sahihisha na sio mwalimu ambaye aliwafundisha uongo,  hivyo wanafunzi hao hawatapata maksi kwa sababu walifundishwa uongo na lazima majibu yao yatakuwa ya uongo, hawatafaulu mtihani, mwanafunzi ataumia sana, moyoni mwake atasema  nilisoma na nikakesha lakini nimefeli sababu ya mafundisho ya uongo ambayo alifundishwa, ndivyo ilivyo hata sasa kwenye wokovu nyakati hizi, wengi wanafundisha uongo,  ndio maana Yesu alikuja ili kufundisha ukweli ili tuachane naya muovu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Ukitaka uzima wa Yesu, cha kwanza ni lazima kumpokee yeye, ukweli ni kwamba  unaweza mkuta mwalimu / mtumishi anawaambia watu hakuna wokovu, huyu lazima ni mwalimu wa uongo, Yesu alikuja hapa duniani kwa kusudi la kuuokoa ulimwengu,  ila wengi wamemkata na Yesu atakuja na atasema nilikuja kwenu mkanikataa, yawezekana ni mwalimu  alikufundisha au anafundisha kumkataa Yesu, na mwalimu huyo nae anaongeza wanafunzi wa kumkataa Yesu, kwa sababu yeye hayuko kwa ajili ya kumtetea Yesu bali anajenga ufalme mwingine. Sasa kama na wewe hutaki kuchomwa, acha kufuata Imani au waalimu, wahubiri wa uongo, mchungaji, mwinjilisti, nabii  wa uongo ili uweze kupona maana huyo nae anakuchunga katika kundi la uongo lakini wale wenye Roho Mtakatifu huwa wanashtuka na kutafuta mahali Yesu ambaye ni uzima anapopatikana. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Tunajua MUNGU wetu sio Mungu wa wafu, baadhi ya walimu au viongozi wa uongo watakuambia ukifa tutakuombea, maiti inaweza kumkiri Yesu?  Hebu tukatae kuchezewa maisha yetu, kwa Mungu kuna mazuri lakini tukikubali kuchezewa au kufundisha uongo kinachokuja mbele ni kibaya maana ni jehanamu, shetani aligundua njia ya kumteka mwanadamu  kumfundisha uongo tu maana shetani anajua wanadamu wanampenda Yesu, Bwana yesu asifiwe, Kwanini watu wengi wanajiita wakristo lakini hawataki uzima yaani Yesu, (Wokovu) ni kwasababu mwanadamu amejaa kiburi, anasema si ninaishi?  Rafiki yangu huo uzima ni wa mwili tu, unatakiwa kuwa na uzima wa Roho usipumbazwe kuitwa mkristo maana siku ya mwisho utatamani kupigana na yule ambaye amekufundisha uongo, lakini haitawezekana, uzima unaopokea sasa hivi ukiwa hai kwasababu mwana wa  Mungu aliyehai atapokea wale wenye uzima wake, hatakuchukua wewe ambaye hujaokoka kwenda nae mbinguni, usidanganywe na wahubiri wanaokuambia usiokoke, usidanganywe na wahubiri ambao wanakuambia usiokoke, wala wale ambao wakijua kuwa umeokoka tu wanakutenga, wakijua tu umempokea Yesu wanaanzisha vita,  au wanakuambia kaa kule nyuma,  hilo kanisa ujue ni la mauti ambalo limekataa Yesu, wakati ule mafarisayo wenyewe walikuwa na mauti  baadae walijuta, usipumbazwe na ukristo ambao una mauti kwasababu tu hutaki kumpokea Yesu, angalia kazi kubwa  ambayo MUNGU aliifanya juu yako wewe, rejea kwa MUNGU sasa , rejea umpokee yeye, uwe na uzima, uandikwe jina lako katika kitabu cha uzima wa milele, na siku moja ufike mbinguni. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

 Wengi wanataka mambo ya MUNGU  lakini wanampenda shetani, huwezi mpenda MUNGU kama humpendi Yesu, Sema huwezi kumpeenda MUNGU kama hujampokea Mwana wa Pekee, kama ulikuwa hujui acha nikwambie, hatua ya kwanza ni kuokoka, shetani amebadilisha badilisha mwongozo ambao Mungu alituachia, Mungu alimtuma Yohana kutengeneza njia na akafika na akakutana nae, na wewe leo hii  neno lake limekufikia mimi Hebron ni mmojawapo wa kukutengenezea njia ya Bwana Yesu, umpokee Yesu katika roho,  bado unasema  badobado,  na hata kipindi kile ilikuwa hivihivi kimwil,  hebu mrejee Bwana, pokea uzima, usipende kuambiwa pokea pokea  hujui unapokea nini? ujue siku hizi kuna mahubiri mengi ya uongo na wao husema pokea pokea  kwa jina la Yesu laini hutumia nguvu za giza, kichawi na ukiwaambia hao wahubiri habarri za wokovu wanakuambia hakuna wokovu,  amua sasa mpokee Yesu, pokea uzima, kila mahali shetani amepita na kuchezea injili ya kweli/ jina la Yesu,  lakini nabii Yesu alishasema kuwa watatumia jina lake , kwa hiyo usishangae nikisema kuwa wanatumia jina la Yesu lakini ni wa uongo, na haya mengine ninayokufundisha ni majaribu ambayo unatakiwa uyashinde na hao wanakucheka bado wana mauti, Mwokozi kama akija sasa hivi sijui kama watabakia wapi,   hebu angalia  dunia itakavyo haribiwa na watu watakavyochomwa moto maana wanasema mimi siokoki, ina maana wanasema mimi sitaki kwenda mbinguni,  mimi sitaki kuishi maisha ya milele, nataka nikachomwe milele, hiyo ndio maana yake, mpaka sasa hivi kamahujaokoka nuru haijashuka kwako na Nuru mkiipokea unaipokea lakini mwingine anaipokea na anaiacha ina maana anapokea uzima anauacha. Biblia inasema pepo limtokapo mtu hurudi kucheck nafasi na wakipata nafasi hali ya yule mtu inakuwa mbaya zaidi,  umetolewa kwenye kifo ina maana kila aliyeokoka ameshatolewa kifo,  ameshatolewa mauti,  Bwana Yesu asifiwe  maana anayeleta mauti ni ibilisi, kwanini watu hawafanikiwa? Kwanini watu wameharibikiwa? shetani ameweka mauti kwenye kazi,  kwenye fedha, kwenye wokovu,  kwenye maisha, wewe unashindwa kusimama imara  wakati shetani hawezi kugusa roho yako, tazama Ayubu vyote viliisha,  viliwekewa mauti,  vikaondoka laini roho yake ilisimama imara ikapona,  lakini wewe kitu kidogo tu umekufa / jaribu dogo unashindwa, watumishi wengi wamemwacha Yesu kwa sababu walishindwa majaribu mimi niliaambiaga kwamba wakitukana waongeze mara mia, wewe ukitukanwa tu umevunjika Moyo, Mbinguni wanakwenda wenye kushinda na fomula moja wapo lazima jaribu ulishinde,  angalia watumishi waliopita waishinda na hakuna jaribu ambalo litakuja kwako ambalo sio size yako,  linakuja kwasababu unapendwa ili upewe kitu kikubwa Zaidi mbele lakini wewe ndio sababu ya kuchelewesha  au jambo lisitokee, acha nikufuundishe kwasababu mengineyo siyo ya maombi,   natakiwa nikuelekeze na kukufundisha, wakikulaani waambie walaani sana wakikuwinda acha wakuwinde, maana wakati mwingine Mungu anakupima,  Mungu anaangalia kama uzima aliokupa utatikisika,  wengi waoga sana, waoga hawaendi Mbinguni, funga ndoa! Usipofunga ndoa, Baraka zako zinachelewa, sasa funga ndoa, ili Baraka zako uzipate kwa wakati sasa mmejua kama hujafunga ndoa na unaishi na mwanamume au mwanamke ni dhambi na shetani anakushitaki na unachelewesha Baraka zako za kiroho na kimwili. Neno linakupenda, neno linaakuhitaji, Neno linakupenda, linataka nafasi kwako lifanye kitu, wewe ndio kikwazo cha kuchelewesha, kuna ahadi za uzima tele, za kwenda mbinguni unafikiri wenye mauti ndio wameandaliwa Mbingu? Hapana! waliokoka ndio wameandaliwa Mbingu, Yesu anasema mpokee sasa, unavyompokea anasema anaandaa makao yako kule mbinguni, lakini wewe mpaka sasa hivi haujaokoka  makao yako hayatafanana na yule ambaye alisha mpokea Yesu ukimpokea Yesu makao yako yanazidi kuimarishwa zaidi,  unaposema bado bado nitaokoka unachelewa na unaweza ukawa mfungulia wenzako geti na hata kulifungua hili geti ni kwa Neema tu, maana usifikiri kuwa mbinguni hakuna kazi kunasehemu za kustarehe,  sehemu za kufurahi,  angalia waliotangualia kuokoka  wanaweza kuwa  waajiri zako, maana badala ya wewe kupigiwa saluti na Malaika kwa kuwa ungelikuwa umeshinda, wewe unaenda Mbinguni kama mtu ambaye ametoka ICU  kwa Neema. (Mfano wa mtu amliyetoka katika chumba cha wagonjwa mahututi – maana umefika mbinguni kwa neena neema tu kwa sababu ya ukaidi wako wa kumkataa Yesu kukataa uzima). Na maisha yako atakuwa mahutitimahututi tu,  amua sasa sio unaenda mbinguni mithili ya umahuhututi hututi tu, ni kama mfano wa abiria ambaye amechelewa Ndege,  kabla ya ndege kuanza kuondoka hutafutwa na kuitwa jina ila mlango wa ndege ya abiria ukifungwa ndio basi tena, hakuna ndege ambayo inaondoka halafu irudi kumchukua abiria ikiondoka imeondoka sasa angalia na wewe  usije ukaachwa,  amekuja uwe na uzima,  uwe na uzima,  Yesu nakupokea, unapompokea uzima unaingia na mauti inaondoka,  lakini mauti ikimshikilia mtu sana mtu huyo hatataka kuokoka atadai siwezi  acha dini ya baba na  mama siku ile  kila mtu atabeka mzigo wake mwenyewe, mke hatakaa nyuma yako,  wala mjomba,  wala baba, wala mama,  kule hakuna kuoona wala nini. Hapa duniani tulikuja kuijaza dunia na wengine wanajaza haswa lakini ole wako wewe unyejaza watoto halafu huwatunzi una dhambi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Pokea uzima mtu anakuambia anamjua Mungu na anashika bibllia, ni sawa ila hatua ya kwanza ni kumpokea yeye, Mbinguni watu hawaendei kwa kutaja jina la Yesu, kwa sababu hata wachawi wanataja jina la Yesu, waganga, wanataja jina la Yesu, tena watu wengi ambao ni wachawi ndio wanalitaja sana jina la Yesu na hao ndio wamejificha kwenye mlango wa dini, kama ulikuwa hujui jicho la Mungu linakuangalia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

 Jaribu kubwa limekuja katika dunia hii Yesu amekuja kwa ajili yako ni mfalme  mpokee, ila jaribu hilo umeshindwa kulivuka, unaona aibu watu watanionaje,  pombe nitaachaje, kwa hiyo umeona kuwa mauti na pombe ndio nzuri sana,  kila jaribu unatakiwa kuvuka  sio kurudi nyuma. (kuamua kumpokea Yesu hilo ni jaribu ndio maana kuna waliovuka na ambao bado hawajavuka)  mwingine unaweza ukawekewa jaribu kuangaliwa tu kama kweli unampenda Mungu, watu wengi wameachana na Mungu kwa sababu ya majaribu na ukiachana na Mungu shetani hukupenda sana, hata kama wachawi wanakutembelea kumbuka Neno moja nimekuambia kuwa Roho yako hawaiguswi, mtetezi wako yu hai, ujue hivyo, Ayubu alitambua kuwa anauzima na shetani alitaka kumuua lakini Ayubu alishinda jaribu, hata wewe kwani unajua ni wachawi wangapi ambao wanatamani ufe, na wanaosambaza mauti ni wachawi, ukinunua gari au chochote wao ndio waweka hiyo mauti ili vitu hivyo visifanye kazi, na ukiingia kwenye uzima wachawi wanachukia sana ukipokea ule uzima wa kweli watahangaika wakutoe katika ule uzima wa kweli hata kama watamtukana mchunhaji wako aliyekuongoza sala ya toba, waambie hamniwezi ninyi,  unampa chenga kama vile wacheza mpira  mtu anasubiri mpira yamkini kwa mbele wewe unachomoka kwa pasi ya nyuma au kando kwa sababu ndani yako upo uzima. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Mauti ni mbaya , mtu aliyeokoka akikaa na Yesu mweye uzima hawezi kuwa na roho mbaya, masengenyo, kuchukia kazi ya Mungu, wivu, Roho za kwanini, ukiwa na tabia hizo ujue una mauti na mauti ilishakunyemelea, mauti huwa inaingia kidogo kidogo baadae inakuvaa chap, unaona uko vizuri, unakuwa mzito hujielewi, hapo sasa funga milango ya mauti. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Kuwa makini hata kwenye Ndoto maana Baba yangu Marehemu Moses Kulola aliniambia, siku moja miaka ya nyuma, alikuwa Mkoani Mbeya Shetani akamtokea kama Yesu, akamwambia wewe ni fulani, akataka kumwekea mkono kama kumbariki, Moses Kulola akamwambia nimekugundua wewe sio Yesu aligundua kwa sababu  alikuwa na uzima ndani ya moyo wake, ule uzima ukamwambia huyu sio Yesu. Sasa kuna baadhi ya watu wanaweza kukuambia kuwa nimemwona Yesu kumbee la! Pima kwanza ndani. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Baadhi ya watu au watu wengi wanarudishwa nyuma kwa sababu ya mauti ya ibilisi, unaweza ukawa unatoka sadaka zako, mafungu ya kumi laini yakawa ni mauti, hutaki wokovu, umefundishwa kuwa hakuna wokovu hayo yote ni mauti sasa inafika wakatti unataka kubarikiwa unamwambia Yesu nikumbuke, Yesu atakukumbukaje kwa sababu sadaka zako zilipokelewa na shetani na siyo Yesu kwa hiyo Shetani atakufilisi kabisa na jina lako litaandikwa kwenye mauti. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

          Kuna namna tofauti tofauti za kumtumikia MUNGU, kutoa sadaka, kufunga kuomba, kufanya usafi, kumpenda MUNGU, kutenda wema, kutenda mema, ambao hawataki kumtumikia MUNGU ni kuwa jaribu limewashinda, mnataka mambo makubwa sana lakini shetani  anakuwekea jaribu, jaribu la kuiba fungu la kumi, yamkini ni sh.100 utasota sana, utabakia ukiangalia wenzako wamefanikiwa wewe utabakia,  Mungu huangalia neno lake, wahubiri  wengi  wameshindwa kwa sababu wao wamekuwa ombaomba, hufanya waumini vitega uchumi vyao hao wameshashindwa wamekuwa mauti, angekuwa na uzima angelitoa huduma ya MUNGU bure sio kwa Pesa injili unauzwa imekuwa nyanya  au bidhaa? Sadaka yako ni ibada yako na MUNGU, mchungaji hatakiwi kuijua, wana kuifanyia mnada, Wala sio ya mchungaji, nae aende akamtolee MUngu, Kama ulipokea uzima wa miungu basi nawe utapokea hizo roho;  dalili za kuwa na mauti unapenda kufanya matambiko, Unapenda ibada za giza, Mshirikina na mchawi, hauokoki, lazima una mauti, uwe tajiri au masikini jua una mauti, kwanini Yesu alisema Kanisa lilitekwa asilimia 98  ni kwasababu makanisa mengi yalikuwa na mauti, ni vizuri kuwa na makanisa mengi ila hebu ingia kwenye ibada hizo, jambo la kwanza sala ya toba  hakuna au wokovu hakuna dini kubwa ndogo au ya katikati kama hakuna wokovu wameshatekwa, sasa kwanini wanamtaja  Yesu lakini hawataki uzima? Waache kudanganya watu Yesu anarudi mimi siigizi ila ndivyo nilivyo, nataka uzima ujae kwako, sio unaishi kwenye dunia kama mkimbizi hauna amani, masikini, nk. Na mahubiri ninayokufundisha mimi sio ya mafanikio maana watu wengi hupenda mafanikio utapata gari, nyumba, ndio wanadamu wanataka hayo, acha nikufundishe habari za Yesu ili uwe na uzima hayo mengine utazidishiwa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Neno linasema palipo na mzoga ndipo tai wengi wanashuka, Neno hili lina maana sana maana mahali palipo na mafundisho ya uongo wanadamu wanapenda sana kuyasikiiza na kuyafuata, mfano, kanyaga mafuta, leta pesa uombewe, ubatizo wa kikombe, kutaka kujulikana kwa viongozi maana umetoa sadaka nyingi, wewe unakuwa tai, mahali watumishi wanajiita MUNGU, ukienda na wewe unakuwa tai unafuata mzoga, unataka tu miujiza hutaki neno, ila Palipo na ukweli watu hawataki penye uongo mzoga watu hukimbilia. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Watu hawamtaki Yesu kwa sababu hapa duniani kulikuwa kuna asili ya mauti, katika ardhi ipo mauti, ibilisi yuko huko chini, na wanadamu wanapokanyaga hapa mauti inaingia, hivyo kuna mauti inayomfuata na kumwongoza  kwenye mizoga. Kama mnakumbuka kuna kipindi ilitokea huduma ya uponyaji wa kikombe, kuna vikombe vinaponya, kinachopanya kwa jina la Yesu au unakuta mchungaji anatumia jina la Yesu kwa kuchangisha Pesa, Jiulize hivi Yesu alitoa huduma kwa Pesa? Kwa vikombe? Au kwa Neno la Mungu tu ambalo alikuwa akisema ponywa unaponywa, fufuka unafufuka, Neno la Mungu linasema toa bure. Sasa hapo kwenye mizoga wengi walienda, wafalme na watu mbalimbali walienda chap kama Tai kufuata mizoga na wachungaji walitangulia kuwalisha watoto wa Mungu mizoga. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

 Bwan Yesu asifiwe,  amenituma leo, mliambiwa  kipindi cha mwisho injili yake itakuwa ya tofauti, uwezo wake ni tofauti, nguvu yake ni tofauti,  kama ulizoega mzoga, hapa hakuna mzoga na kama ulikuwa Tai uvunwe ubakie na Yesu sasa unajua mzoga unavyonuka? Kwanini usikatae mafundisho ya uongo maana ni mizoga, kukatazwa kuokoka ni mizoga, halafu unampenda Yesu halafu unataka mzoga utakuwa tai, kataa mpokee Yesu, sasa hakuna wa kukutikisa, mpokee Yesu, hata ukifa unakufa katika MUNGU aliye hai na sio ufe katika mungu anayenuka kama kinyesi (Shetani) www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Njoo kwa Bwana Yeye ni Mwokozi, Nuru ya Ulimwengu huu, Kama unataka kumbariki mtumishi mbariki hujakatazwa, lakini kama mtumishi nakuambia nipe kiasi Fulani nikuombee au anaomba omba hela kwa waumini huyo hafai, hata katika madhabahu hii mwambie wewe ni mzoga na katika madhabahu hii hao hawakai. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Mkatae kula mizoga baadhi ya makanisa wameweka makaburi ya watakatifu wao mfano. Daudi, Yusuph nk. Mimi Hebron hata nikienda kwenye kaburi la Yesu hata goti langu sitapiga kwa sababu naenda kwenye utalii tu, kuwa Yesu alilalaga hapo, kinyume cha hapo ni ibada ya mizoga. Mbona chakula kikiharibika huli, kwa sababu utaharisha, tumbo litauma, utapata kipindupindu nk. Ila sasa watu wengi wana kipindupindi cha kiroho, Sasa mbona roho yako unailisha mizoga? Ndio maana Roho yako imedumaa, unakuwa umekufa lakini unatembea, na uliambiwa nenda na amani ya mungu na mtumishi wa uongo huo ni mzoga unakuwa umeenda na mzoga. Biblia imeongezwa vitabu hiyo ni mzoga. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Yesu ameleta uzima mzima, ila imani yako imekataa, inakula mzoga heee Jina la Yesu halishirikiani na mzoga, Ipo mizoga ya kiroho na  mda mwingi ulimkata Yesu, kumbuka haya mauti yalikaa kwako mda mrefu, ukapoteza uzima, sasa mrejee Yesu yeye ana uzima,  Yeye atiae uzima,  anakwenda kukurejesha, Nyota inakuwa na uzima, miaka yako aliyokupa Yesu itakuwa na uzima na heri, usiogope majaribu, maana ni mtaji, wengine wamekata kumtumikia Yesu kwa kuogopa kusemwa , ngoja nikupe mtaji sasa,  ukipewa mtaji ndio unaenda kufanya kazi, ukitukanwa mwambie Yesu asante, ukibenzwa mwangalie Yesu, maana ndie mtetezi wako, usiangalie kushoto wala kulia.  Hata mimi nilitukanwa matusi yote, maneno yote na mambo mengi  lakini sikutikisika nikawaambia waongeze zaidi, wakajua atakufa, hatakuwa na watoto, hataoa, tulifanywa vitu va ajabu sana, wakasema kanisa litakufa lakini hawakufanikiwa, Lakini ndio nadunda na Yesu. Nakutia moyo hata kama ni ujenzi, au mipango yako imekwama mwangalie Yesu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Baada ya kula cha uzima leo, undelea kula chakula hichi siku zote, ila ujue kuwa shetani anakunyemelea sasa usilee chakula ambacho sio cha uzima.

Tofauti ya sadaka na makusanyo ni hii Sadaka unaipeleka mwenyewe hiyo inaitwa sadaka ila ya kushawishiwa ni makusanyo kama ambavyo Zakayo mtoza ushuru.  Usishiriki ibada ya mauti au mafundisho ya mauti, adui kila wakati anashangaa anataka uangamie anashangaa sana unaishi hadi leo au umefanikiwa kiroho na kimwili, haya yote ni kwa sababu umepaata uzima. “Mwambie adui nina uzima kwa sababu nina baba wa uzima”. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

Sema Bwana Yesu  naomba unisamehe dhambi zangu ikiwamo dhambi  kutokukupokea wewe, kwa kujua na kutokujua, nikijua kwamba  nitafika mbinguni nikiitwa mkristo na nikitaja jina lako na kusoma biblia lakini nilikataa kuokoka, nikawa nimebakia na ibilisi, nakushukuru kwa Neema  yako hii Bwana, naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele lisitoke huko tena. Bwana Yesu naomba nisiwe kati ya wale ambao ulikuja kwagu nami nikakutakata, Bwana Yesu, Mimi ninakuhitaji, imeandikwa waliompokea walipokea uzima nakupokea Baba kwa jina la Baba, na la Mwana na Roho Mtakatifu. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org.

 

Mungu awabariki.

Nabii Hebron.