Pages

Tuesday, January 26, 2021

 

KESHA ILI MABAYA YASIKUPATE – MATHAYO 13: 24-27

Baba MUNGU ninakushukuru  nalibariki jina lako na kulitukuza na nakushukuru kwa vipindi vyote vilivyopita, naomba neno lako likaongee ndani ya  ya maisha yao, roho Mtakatifu akafanye yaliyo ya mapenzi yako na MUNGU mapenzi yako yakatimie kupitia neno lako, nakushukuru kwa ajili ya kila mmoja, kwa maana unawapenda na  unawawazia  mema na mazuri, MUNGU nakuomba masikio  ya viumbe vyako vyote yakasikie na macho yao yakafumbuke wapate kukuelewa MUNGU na ukapate kuwatendea  lile ulipendalo na yale mabaya ambayo adui ibilisi amepanga ili yawapate watoto wako  hayatawapata katika jina la Yesu naomba Mbingu zikawe wazi Malaika wako wakiendelea  kupanda na kushukuka  na uzidi kutimiza Neno lako. Amen

Mathayo 13:24-27 – Akawatolea mfano mwingine akisema, Ufalme wa Mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake.  Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye shamba wakaenda wakamwambia bwana hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia adui ndiye alieyetenda hivi.

Ni jambo jema kujua au kujifunza, mara nyingi watu wanapata au kupitia jambo Fulani gumu au shida Fulani na hawajui sababu au kwanini wanapitai au kupata shida hiyo na wengine wanajua sababu zinazowapelekea kupata shida au kupitia mambo hayo magumu na pia shetani hampendi mtu anayejua kuhusu mambo ya Mungu na Ufalme wa Mungu, kwa sababu mtu ukishaujua  ufalme wa Mungu na  akaushika na kumaanisha ni ushindi kwa mtu huyo na shetani hataweza  kumchezea mtu huyo kwa sababu ana ulinzi wa Mungu. Bwana Yesu asifiwe.

Ufalme wa MUNGU umefananishwa na konde ambalo limepandwa kwako, lakini ufalme huo wa Mungu umejengwa kwako na anayejenga ni MUNGU. Ila zipo falme mbili, Ufalme wa Mungu na wa shetani,  Ufalme wa Mungu umejengwa ndani yako,  lakini pia ufalme wa shetani ukipata nafasi  unaweza ukapandwa kwako pia. Mtu anaweza kuwa anajiona kuwa yuko vizuri kiroho, na baada ya muda anajiona yuko vibaya kiroho, ina maana kuwa alilala adui akapata nafasi ya kupanda mabaya, baadhi yao au wengine mpaka sasa adui hakupata nafasi mpaka sasa hivi ina maana kuwa hao hawakulala.

 Maana ya kukesha sio kuwa usilale siku zote, la hasha ni kuwa makini na kuwa macho na Mungu,  tumesoma na tumejifunza tusipende kulala, ukiangalia hata kipindi cha Yesu wanafunzi wake walikuwa wanapenda kulalalala mpaka Yesu aliwakemea, akawaambia, msilale, msije mkaingizwa majaribuni, maana ya kukesha ni kuomba, kuna baadhi ya watu wanaomba  jumapili kwa jumapili tu hilo ni kosa, unatakiwa kuomba majira yote, asubuhi, mchana, jioni na hata usiku kwa kufanya hivyo adui hatapata nafasi ya kupanda mabaya, umasikini, magonjwa, shida, vifungo nk. Unaweza kuwa umeokoka ila kila wakati ukawa unapata shida, magonjwa, huvuki, unashindwa kuomba, huna hofu ya Mungu, unashindwa kuacha dhambi na mambo kama hayo, ujue kuwa ulilala hukuwa unaomba, lakini ukijua siri hii au ukiwa unapenda kuomba basi adui hatakuchezea chezea na mabaya hayatakupata kwasababu una ulinzi wa Mungu, ukiwa mwombaji kweli utaishi kwa wepesi, maana unapoomba unakuwa unaongea na Mungu.

  Kula jambo lina utaratibu wake, (fomulas) utaratibu wa Mungu lazima kuomba, na hata waliopo upande wa shetani huomba japo sio kwa Mungu aliye juu,  hao ambao wapo upande  wa shetani huwazuia wana wa Mungu waziombe  hata usiku unajikuta unalala tu na pia wale ambao ni wa upande wa shetani ni waaminifu sana kwenye hiyo kazi ya shetani,  wakiambiwa chochote hufanya bila kujali mda, mahali, nyakati zote humfurahisha shetani, ndio maana hata walipewa maagano au masharti magumu na waganga , au wachawi huyafanya kwa sababu ya kumtii shetani na mawakala wake.

Watu wengi wanampenda Mungu lakini hawataki fomula ya MUNGU yakuomba na  kukesha, Kukesha ni kusoma neno la Mungu, kufunga, kuja kanisani, kuimba kwaya, kumsifu Mungu, kushuhudia, kutoa sadaka, kutenda mambo mema, utii, uaminifu na mambo kama hayo. Kuna watu ambao ni wazee wanasoma neno ila baadhi ya vijana na mabinti wapo ambao hata hawasomi neno, wanasubiri jumapili kwa jumapili, wala hawana habari na Neno la Mungu wametekwa na shetani katika mitandao ya kijamii, akilala cha mwisho kinachombembeleza ni simu akiamka tena cha kwanza ni simu hakumbuki hata kuomba, unayefanya hivyo ujue kuwa umelala, umelazwa na miungu na wachawi, majini, mizimu na roho za shetani, wanafanya hivyo ili tu roho yako isitanuke, isikue, na hatimaye usifike Mbinguni, hata mtoto  anaokula chakula anapata afya  na roho yako inaposoma neno inazidi  kung’aa na kuinuka na kukua  Bwana Yesu asifiwe.

Je! Unakesha? Unaomba? Kanisani unalala? hutaki kuomba? Shetani anakuzubaisha, anakuzuia, anakupumbaza, ili ulale nae aweze kukuteka. Kukesha sio kwamba usifanya kazi, fanya kazi ila ukiwa na nafasi nenda kanisani kasha. Unapoacha kuomba adui anapanda mabaya kwako, mabaya yakishapandwa utakuwa unataka kujenga huwezi, maendeleo yanakukataa, huvuki, ni taabu, shida na magonjwa ndiyo yatakayokuandama, hata kama ni mtumishi wa Mungu na Mungu amekuita halafu ukaacha sheria zake ukaacha kumwomba Mungu adui anapanda mabaya, wengi wakiokoka wanapoa kwa sababu ya kuacha kuomba, ujue kuwa  adui yako hajalala, wengi pia hupenda kwenda kwa wachawi, mizimu, waganga, ili wakupandie mabaya, amka sasa,  omba, kesha, ili uweze kushinda.

Baadhi ya watu au asilimia kubwa ya watu duniani huona vigumu sana kukesha kwa Mungu, ila kwenye dhambi anaweza kukesha, mtu anaweza kwenda mbali kukufanyia mabaya, hata nchi moja hadi nyingine ili tu afanikiwe kutenda mabaya na kumfurahisha shetani, uzinzi,uasherati, mabaya yote unayoyatenda, kwena kwa waganga, na mambo kama hayo, huo ndio mkesha wa upande wa adui. (Shetani) Unafikiri Yesu alipokuwa duniani alikuwa hafuatiliwi? Alikuwa analogwa, Yesu alikuwa anapigana vita kiroho, maana Yesu aliishi kama sisi tunavyoishi hapa duniani ila Yesu alijielewa na dhamani yake aliielewa, ndio maana kila wakati alikuwa akiomba, lakini kuna baadhi ya watu hawajielewi wako kiukawaidakawaida, usipende kuwa kawaidakawaida, kimazoeazoea, kumzoeazoea Mungu, kuacha kuyafanya mapenzi ya Mungu, unakuwa umelala, Ukawaida ukawaida hulaza kazi  zako, huzorotesha uchumi, maisha, umeacha kumtolea Mungu fungu la kumi  ujue umelala na shetani anapata nafasi ya kukukandamiza, Amkeni Amkeni na Kesheni!

  Duniani kuna msemo unaosema; ukimwamsha aliyelala; utalala wewe; sasa mimi nataka muamke, kiroho msije mkalala, baadhi ya watu hukesha kanisani, (Yaani hawataki kuomba wala kufuata mapenzi ya Mungu bali hukaa na kulala tu kanisani wakidhani hawawezi kulogeka) hao ambao wamefundishwa hivyowamefundishwa mafundisho mabovu, injili ya uongo, na wengi wametekwa kwa namna hiyo, amka! Omba! Mwombe Mungu, kukesha ni kumwomba MUNGU.  Mafundisho mapotofu yanakutenga na Mungu na huwarudisha watu nyuma hata ukiwa ndani ya nyumba umelala usingizi, nyumba ikiungua na kama wewe upo ndani, siunaungua pamoja na hiyo nyumba? Ila kama upo macho nyumba ikiungua utaamka nakujiokoa. Sasa amka.

Unaweza kuwa ulikuwa  na bidii  na mengi, ila unaona sasa yamelala, hata sasa vijana wamelala baadhi yao  hawaoi wala kuolewa kwa sababu  umelala, ukiwa umeala hata mwenzi wako utamwonaje? Amka! Kesha! Naweza kusema Kesha na baadhi ya watu wasilale usingizi hata kimwili wakabakia kusema nabii alisema kesha, nawaandikia hili kwa sababu baadhia ya watu hupokea ujumbe kwa namna tofauti tofauti, unaweza kukamfundisha mtu kuwa kesha, mwingine hatalala kabisa atakuwa anakesha tu, nimeshawaeleza kuwa kukesha ni kutenga mda kwa ajili ya Mungu.

 Kazi ya shetani ni kuleta injili ya uongo, ili watu walale kiroho, unajua unaweza kuwa ulikuwa na bidii ya kumtafuta Mungu lakini umelala, kabla ya kuolewa unakuwa msafi, unaomba, unafanya ya mapenzi ya Mungu na kazi zako zinaenda sawa ila baadaya kuolewa unaacha kukesha nyumba zinakuwa chafu, huna mda tena na Mungu, Amka! Nataka nikuone una mambo mazuri, hata shuleni  watu huamka kusoma hata usiku ili uweze kufaulu vema. Wachawi, majini, mapepo, mashetani, hawalali, adui halali, sasa simama imara, ukiwa unaomba hata mapepo hawatakuweza, shetani hatakuweza, utakuwa unag’aa Kama enzi zile za Yesu.

 Napenda nikufundishe  na ujue kuwa kuna wanaoomba kwa jina la Yesu  lakini sio kwa Yesu  Mwokozi wetu, ambaye alikufa na kufufuka kwa ajili yetu, wanaomba kwa yesu Mwingine, ukitaka kujua kuwa upo ukweli katika jambo hili rudisha fikra zako na ujipime wewe mwenyewe wakati unajiuliza maswali haya! Ulipokuwa hujaokoka; Kabla ya kumpokea Yesu wa kweli Je! si ulikuwa unalitaja jina la Yesu?  na ulikuwa unafanya maovu? Na kwa waganga ulikuwa unaenda, unaabudu sanamu, unafanya uasherati, na waliookoka uliwaona kuwa wao ni washamba na wameshanganyikiwa na hata sasa wachawi wanataja jina la  Yesu,  na kujifanya watakatifu kwa kujifisha katikati ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu.

Watu wamepigwa upofu badala ya kuombewa bure, kama neno la Mungu lilivyo agiza kuwa umepewa bure, toa bure ina maana huduma zote za  kiroho zitolewe bure kama Yesu alivyofanya ila wao wanalipishwa pesa kwa ajili ya uponyaji, hao wanakuwa wamelala, mapepo wanakula pesa zao, kwa sababu baadhui ya watu wamelazwa wakawa vipofu na hawawezi kuona,  kuna wanaokesha kilabuni, kwenye vitu vya ajabu, kwa mashetani, watu wengi hupenda palipo na usingizi, yaani penye mahubiri ya kupokea Baraka na pasipokemea dhambi ndio utaona watu wengi wanapapenda, anapoibiwa na kuhubiriwa uongo na mbingui hawaendi, wanapewa faraja za hapa duniani tu ndipo wanadamu wanapapenda au baadhi ya makanisa yanayofanya hayo ndio watu wengi huyakimbilia, Huo ni usingizi, mmelazwa kiroho na kimwili mnaibiwa na mbaya Zaidi Mbinguni hamtafika kwa sababu hiyo sio injili ya Yesu ni ya mapokeo.

Amkeni njooni kwa Yesu, Kwa Yesu upo uzima na Neema tele, zipo faraja na utajiri a kiroho na kimwili. Baadhi ya watumishi ambao wanatumia jina la Yesu vibaya wanasema Nabii Hebron Huwakataza watu kutoa sadaka, wengine wanasema nawazuia kutoka sadaka, ila mimi sijawahi wala sitawazuia kutoa sadaka, ila tu nawafundisha msijemkaibiwa na hao ambao wanasema kwa jina la Yesu lakini kumbe hawako na Yesu. Wako baadhi ya watumishi wanasoma biblia lakini hawaielewi, ndio maana wanafundisha uongo, kwa sababu anachokisoma hakielewi ila wapo baadhi yao ambao wanasoma na kuielewa lakini hufanya makusudi kwa sababu wanatafuta pesa, Yesu ameniambia waamshe! dunia nzima waamke!

Mda mfupi ujao na itafika kipindi dunia nzima itamwelewa Mungu na ole wenu ninyi wahudbiri ambao mnawatesa watoto wa Mungu, Maana waumini wote watamwelewa Mungu sasa baadhi ya nyumba za ibada zitakuwa wazi, namaanisha hivi hakuna mwana wa Mungu ambaye ameamka na kuujua ukweli ambaye ataingia katika hizo nyumba za Ibada, maana watu wote ni wa Mungu na watakuwa wanajua ukweli, unadhani watakubali tena kuingia mahali ambapo hakuna Mungu wa kweli? Hata kama ni wewe je! utakuwa unaenda tena huko? Yesu ni ukweli na sio uongo. Hivi unawezaje kumwita mwanadamu Mungu, maana katika baadhi ya nyumba za ibada mtumishi akiingia kwa akiji ya ibada waumini huambiwa Mungu anaingia pigeni makofi, huyo mwongoza ibada ni Mungu? Kwani huyo mwanadamu mwingiza ibada alikuumba wewe? sasa amka.  Nataka baraka zenu za kiroho na kimwili ziamke, Lakini haziamki kwa sababu wewe mwenyewe ndio kisababishi cha Baraka hizo kulala kwa sababu ulikuwa umelala, ukiulizwa mkesha wa kanisani umehudhuria siku gani hata hujui, umesoma lini biblia hukumbuki yamkini ni ibada kwa ibada,  ulipoanza kulala  kila kitu kilianza kulala. Zamani wamama walikuwa wanaamka mapema, kuikomboa siku na kuanza na Mungu, lakini sasa hivi watu wanalala tu! Amka mapema siku iangalie, amka mapema, komboa siku, Komboa uumbaji, siku moja utalipwa na Mungu. Komboa uumbaji kwa kuomba hata maji kwa sababu kuna vitu vinafanywa na wachawi na majini ili kudhoofisha watoto wa Mungu na waombaji pia, komboa siku, ondoa mabaya kwa maombi, ombea watu na kazi zao, omba wanadamu wamrejee Mungu, ombea kazi ya Mungu na siku moja utalipwa mbinguni.

Kama vile ambavyo mwizi huja mkiwa mmelala, na ukiwa macho anaogopa kuwa mtapiga kelele, au atakamatwa na kiroho hivyo hivyo  ukilala adui anaingia, wanakuwekea mbegu, huombi, kanisani unakata tamaa na hata huendi tena, huwi mwaminifu, unadhulumu wenzako, unakuwa umelala na mbegu mbaya inarushwa kwako.  Umekuja kwenye ufalme wa Mungu acha Mungu apande mbegu ya kwake, na ukikataa ya Mungu basi adui anapanda mbegu mbaya. Kukesha ni kutenda sheria za Mungu, wengi hupenda kufanya mapenzi ya shetani, jichunguze kama adui hajapandaga mbegu mbaya kwako, jichunguze, hata Yesu alikuwa anapandiwa mbegu mbaya lakini alikuwa naomba anaomba Mungu anavushwa na anasonga mbele, anabarikiwa, anainuliwa, akafa, akafufuka, alistahimili mapigo,  katika hayo yote Yesu alitulia na aliyavumilia, ili kutimiza mapenzi ya Mungu. Amua kwa sugu, kuwa moto, amua kufuata ya Mungu, amua kuomba na kukesha, ili  yakija ya adui yaungue,  Amka sasa, amua kuamka.

Kuna aina mbili za waombaji, wako waombaji wa Mungu na wa miungu. Siki zote kaa ukijua kuwa kila mtu anatafutwa na shetani, na kama u mwombaji wa MUngu shetani hawezi kukupata ila pale ambapo tu unaacha kuomba, hapo ndipo shetani atakupata kwa urahisi, hivyo sababu ya kupatwa au kutokupatwa na shetani ni wewe mwenyewe, baadhi ya watu husema mioyoni mwao siombi, nitaombewa, jiulize je kama hata ambaye ulitegemea anakuombea amelala? Amka, omba, songa mbele. Wengine husema Nabii Hebron ataniombea, nitaomba sawa, ilakumbuka kuwa Mimi nasimama kwenye nafasi yangu, wewe je? Wakati mwingine Roho Mtakatifu hukuamsha uombe lakini wewe hutaki, na baadhi ya watu huamka kuomba baada ya kuota mabaya, hicho sasa ni kiburi maana unaomba kwa sababu ya jambo fulani, acha maombi ya kiburi, shuka, nyenyekea kuwa na adabu mbele za Mungu, amka.

Usingizi utakufanya uachwe, Kuwa na kiasi, soma neno, omba, imba. Baadhi ya watu au watu wengi wanakuwa macho katika uongo, kusengenya, na umbea, uongo,  Hutumia mda mwingi katika hayo na hata kikisemwa kibaya juu ya mtumishi wa Mungu wa kweli au juu ya Yesu hawezi kumtetea Yesu, chuki, fitina, na unafiki ndio hutawala mioyo ya watu wengi na sio kukesha kayika Yesu. Angalia!  

   Mungu hukuinua ili uweze kupata Baraka Zaidi kwake, lakini wewe hata kama Mungu alikuinua mf. Kufagia kanisa, kazini, shambani, au popote ila pale ambapo utalala na kuwekewa usingizi hutakaa uvipate. Lakini pia tuangalie upande wa pili hebu waambie watu twendeni disco, wengi wataenda disco, usiku watajianda, kimwili, kifedha, na kiingilio watatoa, lakini kwa Yesu hawataki, mtu huyo huyo mwambie tukakeshe, twende ibadani jumapili hataki, wala hajigusi, jumapili ndio analala hata kimwili, anasema acha nipumzike, amesahau week nzima ni Yesu aliyemwezesha katika yote, amemsahau hata aliyemuumba, anajiandaa kwenda kwa shetani asilimia zote, kwa gharama zote! Amka mrejee Mungu.

 Ukiijua karama Mungu aliyokupa, hata familia inarelax, msipigane, usimseme mwenzako mwombee, Wanawake ni jeshi, kesha mwanamke akiomba  Mungu anamsikiliza  wanamke kwa sababu amewekewa kunyenyekea, na usipoelewana na mke wako hata maombi yako hayafiki kwa Mungu.  Usimwombe Mungu ukiwa na hasira, msikilize mwenzako, tanguliza unyeyekevu, na kusubiri sio ubabe. Kataa kulazwa kiroho na kimwili. Tumepewa Roho ya kuamini, kufika, sio kukata tamaa. Maana kama kukata tamaa, Yesu ndio angekata tamaa, maana jaribu Lake lilikuwa Lake, naye alishinda, jaribu la mtu ni la mtu kila mtu na lake na Yesu pia alikuwa na lake. Baadhi ya aahubiri hulaza watoto wa Mungu kwa mafundisho potofu, ukilala unakua na mawenge, mfano. Mchungaji anakunyang’anya gari anakuambia Yesu amesema umpe na gari unampa na unacha kanisani, hapo umeliwa bwana, Yesu si mnyang’anyi, ukitaka kutoa kitu kwenye nyumba za ibada toa kwa maamuzi yako sio mchungaji akuambie, ukibatizwa ubatizo tofauti na ule wa Yohana ambao alipewa maagizo na Mungu unakuwa umelazwa na umelala usingizi.

Tafakari! Miaka mingapi umealala?? Unatakiwa hatua nyingine Zaidi. Ukiwa macho kiroho mambo yako yanakuwa smart, active, huyumbishwi. Hata kimwili wakati wa kulala unakuwa umezubaa, na hata mavazi ya kulala yanatofautiana na mavazi ukiwa macho.

Angalizo:    ukiwekewa mkono mtumishi ambaye amelala au unaabudu katika nyumba za ibada ambazo zina sanamu na za mapokea ya wanadamu, ambazo zina ubaguzi, na ambazo zinamichango michango, zinazotanguliza Pesa, na kuangalia wenye pesa na wengine kama hawastahili kwa sababu haweana pesa hapo unakuwa umelazwa, utalala, utaendelea kulala na wanakulaza, moto wa Mungu ndani yako unazimika,   wanabeba vitu vyako kiroho, usisonge mbele, unaanza kuchoka katika wokovu hivi tafakari mtu ambaye  amelala anaweza kulima, kula, na kufanylakini akiamka ataweza kufanya vyote. Sasa amka kata usingizi.  

Baba ninakushukuru, Yeshova ninakushukuru, endelea kumwangalia Mungu, yeye anaenda kukukomboa.

 Bwana Mungu asante kwa mda huu na wakati huu ulisema tukeshe, Yesu naomba nguvu ya kukesha, amani, mafanikio, mioyo imelala Baba, pale nilipokuwa nimelala nikawekewa mabaya ndio maana yamekaa  katika maisha yangu, Bwana Yesu naomba kila pando la adui, wachawi, mabaya, magonjwa shida na dhiki zing’ooke, katika jina la Yesu.

 Neema ya Mungu ikuwezeshe kusimama upya,   Pale ulipolazwa na adui ili  usiwe katika njia ya Yesu urejeshwe, Mwaka huu usimame, malengo yako yakawe na nguvu na ufanikiwe, nakutenga na adui na mabaya natamka ufufuo, nawakomboa na kuwasafisjha kwa damu ya Yesu nawaombea na  imani zenu ziongezeke  kwa damu ya Yesu, nafungua fahamu, akili na mioyo yenu muweze kusoma Neno  na muweze kukumbuka, na Neema ya Mungu iwawezeshe kumnyenyekea Mungu na msiwe na ukawaida  wa kumzoea Mungu. Mkiri Bwana na Jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima wa Milele Mungu awe nanyi. Mkaone mema na mazuri. Amen.

Imeandikwa na Nabii Hebron.