ZAWADI YA KRISMAS – (UPENDO WA YESU USIOFANANISHWA NA CHOCHOTE)
Baba katika jina la YESU ninakushukuru, asante kwa siku njema hii, ambayo tunakumbuka kuzaliwa kwa BWANA wetu YESU Kristo ambapo kupitia yeye tumeokolewa, na Zaidi kuwa na Amani, kuona ushindi na kuwa na matumaini mapya, asante MUNGU, asante Roho Mtakatifu, utukufu ukurudie juu Mbinguni, Amen
Tumshangilie, Bwana YESU Heri ya Krismasi,
Bwana YESU asifiwe, Heri Ya Krismas kwa kila mmoja , heri ya Krismas na Mbinguni Maana wao pi wanashangilia, wanakumbuka siku hii pia, japo alikwisha kuzaliwa miaka 2020 iliyopita.
Bwana Yesu asifiwe, Mathayo 2:1-15
Haleluya, Bwana YESU asifiwe, haleluya, siku kama ya leo miaka 2020 iliyopita ndipo shetani alianza kilio, na leo tunakumbuka siku ambayo BWANA YESU alizaliwa kiongozi wa viumbee vyote, mfalme wa amani hakuna wa kufananishwa na YESU, wala hatakaa awepo, Bwana YESU asifiwe, ni zawadi aliyotupa MUNGU aliacha maisha yake ya kifalme akasema nitume mimi Baba, wote mmesoma historia ya YESU, kutoka katika ufalme tena wa Mbinguni usiofanana na chochote hapa duniani, kwa ajili yako na yangu ni upendo wa namna gani huu, sijawahi kuona wala sidhani kama utakaa uwepo, ndio maana anaitwa mwana wa pekee na mambo yake ni ya kipekee, upendo wa kipekee, maamuzi yake ya kipekee, utiifu wake wa kipekee, utakatifu wake wa kipekee, kumsikiliza kwake MUNGU ni kwa kipekee, kuamini kwake ni kwa kipekee, jina lake lina nguvu ya pekee, damu yake ina nguvu ya kipekee, sura yake ni ya pekee, kuzaliwa kwake ni kwa pekee, Je! umeshawahi kusikia mtu ameambiwa abebe mimba wakati hajakutana na mwaume? Ni wa pekee.
Tunaona nyota ilionekana, na mfalme H erode alikuwa akiogopa, akataka kumwangamiza YESU lakini malaika wa MUNGU alikuwepo pamoja nae YESU, kila mbinu alizokuwa akizifanya adui juu ya YESU, MUNGU alikuwa anazipangua ni kama wewe kila mbinu ambazo adui alikuwa anazipanga zinapanguka, Bwana YESU asifiwe, hapo ndipo shetani anatakaga kujing’ata meno, maana kila baya ambalo anapanga juu yako anaona unapita tu, unakwenda tu, Bwana YESU asifiwe, amezaliwa miaka 2020 iliyopita napenda nikuambie jambo moja, pale alipoamua kumpokea YESU, ndipo YESU anazaliwa ndani yako, alipokuja YESU wapo waliomkataa, wako waliomfurahia, wapo waliompa zawadi, na wewe ambaye YESU mezaliwa ndani yao leo katika ulimwengu wa Roho na wewe ambaye YESU alikwisha kuzaliwa ndani yako, haijalishi ni miaka 10, 5, 2 au leoleo, kwa muda huo ndio Happy birthday kwako pia, kwa maana ndipo YESU alipozaliwa ndani yako na kama ndio leo ndio unampokea Bwana ndio birthday yako, kumbuka hatazaliwa tena pale Yerusalemu bali anazaliwa pale unapomkiri na kumpokea, anazaliwa ndani yako na akisha zaliwa badala ya kupewa zawadi kimwili MUNGU na Malaika zake ndio wanaleta zawadi kiroho kwako na leo mtakwenda kuongezewa zawadi nyingi sana kutoka kwenye kiti chke cha enzi.
Alizaliwa Yerusalemu akapelekewa na zawadi, wakaenda wakamsujudia mfalme amezaliwa na wewe dani yako kitu chochote ambacho ni kinyume na mpango wa MUNGU kinaenda kuanguka kama Herode ila mwana wa mfalme (ambaye ni wewe uliyemkubali YESU) upite kwa wepesi, na kama kuna vizuizi walivyoviweka malaika watakwenda kukuonyesha uvitoe / vioke kwako. BWANA YESU asifiwe, mimi nashangaa mpaka sasa kuna watu amabao hawataki kumpokea YESU, napenda nikufundishe, kama unataka kwenda na ili uende Mbinguni ni lazima umpokee Bwana YESU, amezaliwa, amezaliwa, alipozaliwa nyota yake iling’aa na za kwenu zinaenda kung’aa na pia nyota zenu zitakwenda kung’aa sana leo, Bwana YESU asifiwe na kile ambacho kitaendelea kufuatailia maisha yako, wako malaika ambao wataendelea kukishughulikia, utaendelea kunyanyuliwa juu na utaendelea kutiwa nguvu sana Haleluya, siku ya leo inamaana kubwa sana , unatiwa nguvu, unainuliwa juu Zaidi, wengine nyota zimezimika zitakwenda kuwaka, nyingine zimeharibiwa zitarejea, Mwokozi amezaliwa, kama ni Baraka za kimwili na za kiroho zimekombolewa, ndoa afya yako pia imekombolewa, vitu vyako na safari yako ya kwenda Mbinguni imekombolewa pale tu ulipomkubali Bwana YESU, Haleluya! Lazima uelewa maana ya Krismasi.
Mbinguni leo ni sherehe, wanakumbuka jinsi ambavyo YESU alikuja kuteseka hapa, lakini nakutiaa moyo kama YESU alizaliwa Yerusalemu pale, kulikuwa na watu ambao walikuwa na ufalme wa shetani akiwemo Herode, ambao ufalme huo ulikuwa umejengwa ndani yao, Herode hakufurahi, hakutaka kwa sababu alijua kuwa ndio mwisho wake, na wewe pale ambapo umeamua kumpokea YESU kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako kuna ufalme ambao hautafurahi, iwe ni mizimu, mapepo, majini, shetani, wachawi, hawatafurahi lakini wewe unatakiwa usonge mbele.
Napenda nikufundishe jambo, pale amabapo unampokea YESU halafu ukarudi nyuma, tayari umerudi kwenye giza tena, unakuwa ni kama ufalme wa farao, naunakuwa na ufalme wa shetani, unakurudisha nyuma, unakuuwa, japo unatembea ili kile ambacho MUNGU alichokiweka ndani yako kife, kisitokee, hata YESU walitaka kumuua kimwili, sasa hivi ni kirohho na ilitabiriwa, “nalimwita kutoka misri”, na ikatokea YESU akaenda kufuchwa Misri, mpaka farao akafa, Bwana YESU asifiwe, na aliporudi tena alikuta mfalme mwingine, ndipo baba mlezi wa YESU Yusuph akaona hapo kuna mfalme mwingine ambaye ameachwa na Herode, akaamu kwenda Nazareti, kumlea YESU huko, lakini pia iliandikwa ataitwa Mnazareti, kwa sababu alilelewa pale na kuishi pale, kwa huyo unabii wa MUNGU ni lazima utimie, na kwako lazima utimie, MUNGU yeye ni nabii na YESU yeye ni nabii, Bwana YESU asifiwe, kwa kingereza anaitwa JESUS, kwa kifarasa ana jina lake, kwa Kiswahili ni YESU, ka kiarabu anaitwa Issa, ulimwengu wote una jina ambalo wanamwita, huyu ni YESU mfalme wa wafalme, Kwanini amekuja,? Na kwani hatakiwi? kwa sababu amekuja kutafuta kilichopotea, ili akufanye mwana wa mfalme, maana kuna ufalme ambao ulishatawala hapa duani, kuhakikissha kwamba utakumaliza, kwa hiyo kama ni kiuuwawa aliuwawa yeye kwa ajili yako na kama ni kutukanwa alitukanwa kwa ajili yako na akama alizaliwa alizaliwa kwa ajjili yako, maana kabla ya hapo wanadamu wengi walikataa kumgeukia MUNGU, kumrejea MUNGU unajua ni kwanini? kwa sasabu kulikuwa na ufalme mwingine ambao ulikuwa umezaliwa ndani yao, ndio maana iikuwa ni vigumu kumrejea MUNGU lakaini wote waliompokea YESU ufalme wa shetani uliondolewa, hata alipozaliwa YESU, Herode yeyey alikataa kumkiri YESU ndio maana alitaka amuue, ila haikuwezekana ni kama wewe iliyempokea YESU wengine wanakucheka, mara unajikuta umerudii nyuma umeacha wokovu unatakiwa usimame na YESU, sema YESU kwangu anaishi milele. Yusuph akamkimbiza mwanaye asiuawe, kwanini wewe unarudi nyuma? kwanini ukitukanwa tu kidogo kuhusu YESU unarudi nyuma? Nataka nikwambie, ukiacha wokovu ule ufalme ambao ulikuwa umezaliwa ndani yako ambao ni Bwana YESU unakuwa umeuondoa na sasa unakuwa umerehusu ufalme wa shetani uzaliwe ndani yyako kwa kumkataa YESU au kurudi nyuma kwenye wokovu, utabakia mkristo lakini mkristo wa ukristo wa shetani maana ufalme wake ndio umeuruhusu ndani yako, Kwa kujua na kwa kutokujua.
Kumbuka si rahisi ufalme wa MUNGU uwe umezaliwa ndani yako halafu shetani akutese, majini, mapepo, mizimu au wachawi, halafu zaidi uombe MUNGU na MUNGU asikusikie, ukiona unateseka shida ni wewe jitadhmini kuwa Je! Ni ufalme upi uko ndani yako? (Matendo yako). Lakini ulifungwa na kudanganywa na mafundisho ya uongo hayo ndio yakawa yamezaliwa ndani ya wanadamu hakiku zaliwa kile ambacho kilikuwa kinatakiwa kwahiyo kama bado hujaokoka okoka na wewe uliyeooka endelea kusimama na leo utaendelea kujazwa nguvu sana kamam ni mtoto ulikuwa unaenda tetete katika wokovu sasa utapata nguvu utatembea haleluya. Haleluya, Bwana YESU asifiwe, leo ni siku njema sana pasipo YESU pasingelikuwa na Amani, utunze sana Amani uliyonayo, tunza kwenye Nchi, tunza kwenye familia yako, YESU ndie aliyeileta hiyo Amani. Je! Leo umejiandaaje, najua wengi wamejiandaa kwa chakula, na mavazi mapya, ni vizuri sana lakini inakuwa aibu sana katika siku ya leo yamkini mtu anajiandaa kufanya vitu ambavyo si mpango wa MUNGU, inamwaibisha MUNGU. Wengine wana lewa eti ndio wanafurahi Krismasi, Rafiki yangu hapo unakuwa umemwabudu shetani, kwasababu matendo mabaya hayamtukuzi MUNGU na baadhi ya watu mda huu wamelewa sana wanasemaa wanasherekea Krismas, haisherekewi kwa uovu, wala kwa matendo ya aibu husherekewa kwa kumtukuza Bwana yale ambayo Bwana amesema tusiyafanye kweli tuyaache na kama ziko madhabahu ambazo zinasema kwa kunywa ndio wanamtukuza Bwana waache sio hivyo imeandikwa, Msiwape watu vilevi, Krismas Inaadhimishwa kwa upendo, mpe mwenzako mkono mwambie heri ya Krismasi, na iwe hivyo kweli, Bwana Yesu asifiwe, Hata Mbinguni wanafurahi, wengine wanaenda kuzini wameshajiandaa huko sio kusherekea, je wanaofanya maovu wanamwazimisha YESU au wanampindua YESU? Wengine mkesha wa Krismasi wanalewa akisikia nyimbo za krismasi anazifurahia wakati kalewa, lakini Je! hapo anamtukuza YESU wakati kalewa inawezekana kweli, YESU na pombe? haifai hayo ni ya shetani kwa sababu ya mafundisho ya uongo, laiti tungelifundishwa mambo mema ya YESU, YESU angekaa kwetu nasi tungelikuwa tunamfurahia YESU kweli na tungelimfanyia YESU vizuri na YESU angezidi kuonekana kwetu, ziko zawadi za rohoni ambazo YESU anaenda kutoa lakini shetani nae ana zawadi zake za rohoni ambazo anaenda kuwapa watu wake.
Tazama siku ya leo katika dunia nzima, hata kama watu wamesafiri maeneo mbalimbali, huwa wanaenda nyumbani kujumuika na ndugu jamaa na marafiki, kusherekea, hakuna sherehe kubwa kama hii ya mwokozi wa ulimwengu wengine watakaa nyumbani wanafurahi na wengine wanakaa na marafaiki wanazungumza ni furaha tu wanakutana, wengine wanaongea ni furaha basi hii furaha iwe katika utakatifu, iwe ni furaha njema, usije ukaiharibu krismasi yako unafikiri wale mama jusi waliokwenda kumwangalia YESU waliondoka kama walivyoenda la hasha waliondka na furaha, na Baraka na ili ujue walipoambiwa na Herode wakatoe taarifa kuwa walimwonaje, malaika wa Bwana akawapa maelekezo wasiende kwa Herode, maana pale tu walishapokea Baraka za kuwa wana wa MUNGU, akawaambia Nendeni hivi na hawakwenda kwa Herode, Tunasherekea Krismasi, tule kwa kiasi tusivimbiwe, mkumbuke vya bure vinaua muwe na kiasi, Haleluya, ukimtukuza MUNGU ukimwambia MUNGU asante Neema yake na ule upako wake ukitembea na wewe kila wakati ukitenda mambo mazuri ukidumisha amani, uache mambo mabaya, hapo utakuwa umemuenzi YESU na yeye atakuenzi, lakini mambo ya kwenda kusherekea kinyume na mpango wa MUNGU haifai, utakuwa bado hujasherekea na BWANA YESU endapo utatenda dhambi, yamkini Herode nae alikunywa kilevi cha hasira na mawazo kwanini bwana BWANA YESU amezaliwa, kwanini amezaliwa, nendeni mkamtafute, alitaka kumuua, lakini haikuwezekania, na kwako wewe ambaye umempokea YESU ukiokoka tu, familia, marafiki, ndugu, wanakasirika, nashangaa hata baadhi ya wachungaji ukiokoka wanachukia. Unapompokea BWANA YESU ndio kumuenzi YESU kama hujampokea YESU haina maana kwa wewe kusherekea krismasi. Bwana YESU asifiwe alizaliwa, akaonekana mtoto mdogo na wewe umezaliwa u mtoto mdogo katika maisha yako ya wokovu, MUNGU atakwenda kukupa mahitaji ambayo yatakwenda kukusaidia katika kuishi siku zote. Bwana YESU asifiwe, vilivyozaliwa vibovu vitakwenda kuondoka, kuna baadhi ya watu hawana hata furaha, hata kama hujui kuwa utakula nini, isikupe mawazo, YESU ni Zaidi ya chakula, YESU ni Zaidi ya majumba na chochote kilichopo dunia nzima, hebu Imani yako ibadilike, sijui nitakula nini? Imani yako inakuwa imeshuka, acha kuangalia mambo madogo, angalia makubwa, Yesu mwenyewe alipozaliwa haujaja na thermos ya maziwa, nguo, lakini vililetwa, hakuwa na Pesa mkononi lakini vililetwa na wewe uliyempokea Bwana ni Yesu amezaliwa kwako mwangalie yeye akutunze mwambie nimekupa nafasi kwenye moyo wangu, kuzaliwa kwake aYESU kulikosekana nafasi, walikuwa wamekwenda kwenye sensa, nyumba za wageni zilikuwa zimejaa, wakakosa mahali pa kulala na sasa YESU anatafuta mahali pa kulala kwako, Je nafasi ipo katika moyo wako? au akalale kwa jirani? au akalale kwingine? mbona unasema badobado je iko nafasi ya YESU ndani ya moyo wako au haipo? Au unasherekea kama msindikizaji au unashereke kama mpambe, Bwana YESU asifiwe, Je! Ni wangapi wanakuombia usiokoke? ina maana wanakuambia usikubali kumpa YESU nafasi, Utubu kwa hilo Kuna mambo ambayo ungeyapata miaka mingi lakini wewe ndio sababu kubwa ya kuyachelewesha, ilitabiriwa atazaliwa, ikatabiriwa, atakufa na kufufuka, na amefufuka na amepaa Mbinguni, ilitabiriwa anakuja kulinyakua kanisa lake, je amempata nafasi kwako? Je kuna nafasi au ndio unasema hapana! Au umekuwa kama Herode, unajua unatakiwa uende kimatendo.
Imetabiriwa nyakati za Mwisho yatakuja maafa mengi, lakini ameniambia, niwaambie nyie ambao mmekubali azaiwe na amezaliwa kwenu msiogope hata ingekuja nini, imeandikwa itafika mahali kama huna namba hutanunua kitu wala kufanya chochote sio kwama utakimbia hii dunia ila kaa hivyohivyo na YESU yeye atakushindia hivyo hivyo maana anakujua usikate tamaa Mwokozi anarudi wengine wasemaa toka nimezaliwa wanasema tumeambiwa atakuja hatujamwona, napenda nikwambie hata yeye kuzaliwa kwake ilitabiriwa, na wako ambao walisikia walikufa na hawakumwona na kwanini una kichwa kigumu? Wewe utaishigi milele au ipo siku utakufa, sasa kwanini unampinga MUNGU? Unasema harudi basi pinga sasa kuwa utaishi milelel hutakufa. Ni njema, ni nzuri ni furaha sijui asingekuja ingekuwaje Shetania alijua atakuja ndio maana hata alimtuma na Herode ili amuue, YESU lakini MUNGU ananjia nyingi, njia ambayo shetani au mchawi anaona kuwa atakuweza wewe ziko njia za MUNGU ambazo MUNGU atakupitisha wewe, Ni mahali walikuwekea mitego MUNGU atakupitisha, kama YESU alipowekewa mitego Yerusalemu MUNGU alimwandalia Nazareti na hata wewe MUNGU atakufanyia njia ambayo hata wewe huijui, tunakwenda katika Roho na wewe anakwenda kukufanyia lakini Je! umekubali azaliwe ndani yako au umemwambia kuwa hakuna nafasi? Tukapumbazwa kwamba hakuna wokovu sasa YESU alizaliwa ili nini?? Si angelikaa Mbinguni tu, kweli siku ile watu watahukumiwa bila huruma, bila huruma si bora sasa angelikaa zake mbinguni, kama ingelikuwa dunia haikuwa na shida? kulikuwa na shida ndio maana alikuja, na tusingeliitwa wakristo kama YESU asingelikuja na kama dunia isingalikuwa na shida YESU asingelikuja, lakini tulikuwa na shida ndio maana Mkombozi alizaliwa, tunaelewana jamani, lakini itakuwa gharama kulipa siku ile ya mwisho maana Neno la MUNGU haliji bure, Bwana YESU asifwe linda sana ulichonacho asije mwizi kukuibia, huyu Herode anayekufanyaga uache wokovu mwambie nimeshakutambua, maana anaweza akamtumi mtu ili akutatishe tamaa katika wokovu, Mfano. Unajifanya umeokoka, unajifanya unamjua MUNGU Unajifanya mtakatifu?? Mwambie ndio, mwambie ukweli, lazima uwe mbabe kwa YESU Mfalme amezaliwa Herode anakasirika mfalme amezaliwa. Mapepo, mizimu, majini yamekasirika waambie ndio nimeokoka, tazama Herode alikufa na anayekurudisha nyuma ili uache wokovu mkatae songa mbele yeye ndio akufuate, Bwana YESU asifiwe, Umempokea YESU kweli umeokoka mwaka gani? Haijalishi ni lini Mda uliotimiza katika wokovu ndio birthday yako. Kwa sababu umejitahidi kumshikilia YESU lakini endele jitahidi kumshikilia kabissa, YESU anasema atakaye vumilia mpaka mwisho ndiye atakayefika, utakayevumilia kukwazwa, kutukanwa, wakitaka kukurudisha nyuma usikubali vumilia mshike YESU, mpaka mwisho. Wewe uliyeamua kumpa YESU nafasi endelea kuvumilia atakapoingia ndani yako atakupa Neema ya kushinda.
Haleluya; Sema Bwana Yesu naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, Bwana YESU ninakubariki kwa sababu ulikubali kuzaliwa kwa sababu yangu na wengineo ili nipate kukombolewa, ninaomba toba na rehema Miaka mingi pia nilisema hakuna nafasi kwenye moyo wangu, nikakaa na ufalme mwingine ninaomba toba na rehema nakupenda YESU ninaomba unirehemu, Nakupenda YESU nafasi ipo ndani ya Moyo wangu, uzaliwe ndani ya moyo wangu uandike jina langu kwenye kitabu chaki cha uzima wa milele, nitie ngungu nikuze kiroho, niongoze, kama wewe uivyoshinda ukarudi mbinguni na mimi iwe ni sababu kwa wakati wako na kwa mapenzi yako na ile siku ya unyakuo ukaninyakue BWANA nitie nguvu, yaliyo tabiriwa kuhusu kununu vitu kama huna namba ile yametimia, umezaliwa ndani yangu nawe umesema tutakao kushika mpaka mwisho tumeshinda ninaomba nitie nguvu, BWANA shuka ndani yangu tembea nami, BWANA tembea nami, tembea nami nakuhitaji Bwana utukufu nakurudishia MUNGU kwenye kiti chako cha enzi, Amen.
“Baba Katika jina la YESU tazama yule ambaye amezikwa mfufue, anaumwa mponye, kuna vitu vibaya na maisha mabaya yaliyozaliwa yanatoka na mbegu zake magonjwa ya ajabu wanafunguliwa wengine nyota zao zinarejeshwa kutoka kwenye mavumbi, kuna jambo MUNGU alipanga uwe fulani halikutokea mizimu, wachawi majini wakaliua Mwokozi wako amekurejeshe na kukulipia madeni yote katika ulimwengu wa Roho. Naona mbingu zikifunguka naona hekalu la MUNGU limeng’aa sana najua kuna kitu kinashuka toka mbinguni kwa ajili yako sasa mahitaji ambayo ulikuwa huna na unauhitaji MUNGU amekujaza. Pokea uponyaji pale ambapo ulikuwa unaumwa, ninaona milango iliyokuwa imeshikilia Baraka zetu ikiwa inavunjwa na vitu vyenu vikirejeshwa, nyota zenu zirejeshwe, nyota ndio kila kitu ilipoonekana nyota ya YESU walijua mfalme anazaliwa, Malaika Mikaeli ninakusihi mtumishi wa MUNGU mwanajeshi mkuu wa jeshi la MUNGU, sasa anapita juu yenu kwa kila ya liyeshika nyota yako, Mikaeli kamanda mkuu rejesha, YESU, YESU, YESU, wako wanaoona wivu kwa ajili ya kile ambacho MUNGU amekupa, maisha yaliyofungwa yafunguiwe kwa jina la YESU, naona kuzimu ikiachia nyota za watu, mizimu na mapepo wachie vitu vya watu, naona mizimu viti vya enzi vya shetani wakiachia vitu vyako, kila mpaka na maagano waliyokuwako YESU ameyavunja, Mauti uondoke” Walioko magereza nawaombea wawe huru, “sema ufalme wa shetani uondoke, wanaotembea kwenye nyumba na kuniloga waondoke ”
Mwenyezi MUNGU awabariki, Heri ya Krismasi tuko pamoja wote katika jina a YESU, sisi ni ndugu wa YESU, YESU amezaliwa nasi ndani yake, Heri ya Krismasi na Mbinguni Pia, Naona mkono wa YESU ukikushika. Pokea nguvu na Muwe na sikukuu njema, vilivyopugukiwa vijazwe. Amen.
Imeandikwa na Nabii Hebron