Pages

Thursday, December 24, 2020

SALAMU ZA KRISMASI KUTOKA KWA YESU

Baba ninakushukuru kwa muda huu na wakati huu, Neno lako lifike kwa watoto wako, Mioyo yao ikalipokee, likawatie nguvu, likawainue na nguvu zako zikawainue, na upendo wako ukawainue, nakwenda kumwaibisha ibilisi na kumteketeza aachilie maisha ya watoto wako MUNGU. Kwa jina la YESU na kwa damu ya YESU, ninakushukuru kwa upendo wako, ninakushukuru Yehova, utabaki kuwa MUNGU, MUNGU, MUNGU usiyeshindwa, MUNGU usiyefananishwa, MUNGU wa Ibrahimu Isaka na Yakobo,  Amen.

Bwana Yesu asifiwe, Tunasoma neno la MUNGU kutoka katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 1:1-3   ‘Ufunuo huu ni salamu za Krismas Kutoka kwa Bwana YESU, Alinipatia siku 3 zilizopita nafikiri, akaniambia useme na dunia pia uwaeleze.’ (Yaani niwape ujumbe huu)

 Neno la MUNGU linasema hivi; Ufunuo wa YESU aliopewa awaonyeshe watumwa wake kwamba mambo ambayo kwamba  hayana budi kuwako upesi, naye akatuma kwa mkono wa Malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana aliyelishuhudia Neno la MUNGU na ushuhuda wa YESU Kristo wa mambo yote aliyoyaona, heri asomaye  na wao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyashika  yaliyoandikwa humu kwa maana wakati u karibu.

Bwana YESU asifiwe tunakumbuka hata kuzaliwa kwa YESU  kulitabiriwa. Hizi ni salamu za Krismas kwa watu walio mkimbilia yeye, na wale ambao watakao mkimbilia yeye, anawaambia wasiogope, Bwana YESU asifiwe, kama ilivyotabiriwa kuwa kuna mwisho wa dunia, mwisho wa dunia kweli upo na  napenda uelewe kuwa kulikuwa na mwanzo wa ulimwengu huu pia, kabla palikuwa hakuna ulimwengu huu, lakini MUNGU aliufanya ukaanza, Bwana YESU asifiwe, ikatabiriwa atakuja, atazaliwa, atakufa na atafufuka, akaja, akazaliwa wakati kama huu miaka 2020 iliyopita, Bwana YESU asifiwe, tunaelewana, MUNGU akisema, amesema, mimi namwogopa MUNGU sana, lakini miungu mimi siiogopi, kwa sababu hakuna walilolifanya au waliyoyafanya yakatokea na wewe  usiogope miungu kabisa, ahadi za MUNGU kwako zitamia, kwa sababu yeye ni MUNGU, wala si mwanadamu, MUNGU hasemi uongo, akaniambia imetabiriwa kwamba  nitarudi, akaniambia niwaeleze kwamba  anakaribia kurudi, atarudi au kwa lugha nyingine mwisho wa dunia umekaribia,  akaniambia waeleze, maana wako ambao wamepumbazwa wameambiwa kuwa hakuna mwisho wa dunia, kwa sababu wapo waliosikia kuwa upo mwisho wa dunia lakini walizaliwa wakakua na kufa hawakuuona, na hata vizazi vingi vimepita wameambiwa kwamba  mwisho wa dunia umefika bado hawasadiki, lakini mjue kuwa mwisho wa dunia unafika, YESU anarudi, Yesu anarudi, akaniambia “Hebron mwanangu wametokea watu wanawaambia watu kuwa hakuna mwisho wa dunia, akaniambia nenda uwakumbushe” MUNGU ni MUNGU neno lake ni lile lile jana, leo na hata milele, na mimi wala sipunguzi, akaniambia waeleze, yalitabiriwa yatakuja maafa ndio dalili za kuja kwangu ,YESU asema, “Yeye haijui siku ya kuja kwake ila BABA yake ndio amemwambia wakati wowote nitakutuma,  akaniambia waeleze dunia, watu wamepumbazwa wanaona  kama hakunaga mwisho wa dunia tena, maana miaka mingi imepita, watu walikuwa wakiambiwa mwisho wa dunia umefika, wengine wamezaliwa, mpaka wakafa na mpaka wakazaliwa, na wengine hawajauona na baadhi yao wanaona hakuna mwisho wa dunia, akaniambia, lakini wakumbushe, maana  hata dunia alikuwa na mwanzo wake, wakumbushe hata habari  za kuzaliwa kwangu, wengine hawakuniona na walikufa na wengine hawakuniona lakini nikazaliwa, wengine walitabiriwa kuwa nitakufa na kufufuka na hawakuniona lakini nilikufa na nikafufuka na wewe  wajua”.  Mbona kila mwanadamu / wewe unasiku zako za mwisho za kuishi na utakufa, sasa kwanini ukatae kuwa kuna mwisho wa dunia? Hayo ni maneno ya kuwalaghai wanadamu, ibilisi anajua wakati wake umekwisha na hapendi kujua kuwa mwisho wake umefika, maana hataki kuingia katika moto wa milele na ataingia na wale wote wanaomfuata, akasema, “waeleze imetabiriwa kutakuja maafa, matetemeko, njaa na taabu, magonjwa ya ajabu, kama hivi mnavyoona sasa  kuwa dunia inatikisika, ilitabiriwa itafika wakati kama huna chapa ya mnyama yule,  hutanunua kitu supermarket, hutatoa pesa benki, hutapanda hata ndege, lakini msiogope na sasa mmeyaona iliandikwa na sasa mmeyaona,” YESU mwenyewe alimfunulia mtumishi wake Yohana, akayaona miaka ni mingi sana, sasa mnayaona. Program / mipango ya MUNGU ni kwamba mwisho ufike na utafika hakuna anayeweza kupangua na kwanini hutaki ufike?  Kama hutaki ufike, wewe una mpango na ibilisi maana ibilisi nae hataki  mwisho ufike, ila sisi tunataka siku moja turudi Mbinguni kwa baba yetu, lakini kuna ambao hawataki mwisho wa dunia ufike na hao ambao hawataki  ni wa ibilisi, hawataki maana wanajua ni moto (watachomwa moto) ameniambia waeleze na mimi nakwambia kama unakejeli, unadharau, endelea kusema kuwa yanasemagwa tu,  mimi ni Nabii wake,  nazungumzaga na kila nikizungumza kitu kinatokea maana Nabii ni kinywa cha MUNGU, YESU anarudi sijui utakuwa wapi wewe,  kumetokea magonjwa ya ajabu, akasema, wasiogope, maana  wale walionishika, wale walionipokea, nitawapitisha katikati yao, hayatakudhuru, kuna njaa haitakudhuru, ni matetemeko hayatakudhuru, yeye ndio anaitwa Mwokozi, atakukomboa katika majanga yote yaliyoko sasa hivi, atakukomboa, hata na korona iliyopo sasa hivi,  lakini yatakuja magonjwa mengine zaidi ya korona, lazima niwaambie,  Unaweza kujiuliza au unajiuliza huyu mtumishi anasema nini? Unabii ulisema na mimi ninasema na sitaacha kusema  nikinyamaza mtazidi kupumbazwa na mtazidi kuteketezwa na mimi nakuambia kweli katika jina la YESU hii ndiyo salamu ya Krismas na ikae ndani yako sio mle pilau tu, mshangilie mwaka huu habari ndio hiyo inayotoka kwa YESU mwenyewe, habari  kutoka mbinguni, ilitabiriwa, atazaliwa, akazaliwa, atapaa ,akapaa,  Bwana YESU asifiwe,  watoto wa MUNGU, watoto wa MUNGU, watoto wa MUNGU, nauliza tena mnanielewa? “NDIO” Baba wasikia angalieni mimi nilizaliwa hapa Arusha, hata YESU alizaliwa kule Yerusalemu akaishi Nazareti akawa fundi kapenta kwa miaka 30 yote alikuwa akiiishi  maisha ya kawaida, MUNGU alipokuja kumbadilisha,  hata pale kwao hawakumsikiliza, walimwona ni capenta tu, walimuona ni mtu aliyekuwa anuza stuli, kabati  na wakati mwingine wakiwa wanataka punguzo la bei aliwapunguzia, “nipunguzie bei bwana” , Wakati wa MUNGU ulipofika  akamfanya kuwa mtumishi wake,  watu walimwona YESU na kumchukulia kama alivyokuwa fundi seremala, wakisema mioyoni mwao, huyu Seremala ataniambia  nini? Walimwona mtu wa shida tu, asiyeweza kuishi mpaka achonge kitanda ndipo apate pesa, “Mazoea”   ndivyo ilivyo hata sasa ukiwa Mtumishi  wa MUNGU  watu watakudharau, sasa na wewe uelewe. Unapokuwa mtumishi wa MUNGU usitegemee kuwa watu watakupenda sana, la hasha, ukiwa mtumishi wa MUNGU au ukiokoka, ndipo wanapata pakukutukana na kukuchafua kwasababu wanangalia historia ya maisha yako kabla ya kuokoka, ndipo inaletwa mbele na watu ndio wanayoikumbuka hiyo maana ndio yaliyomo katika mioyo yao (Historia mbaya)  hawayaoni wala hawatayasema yale ya Utukufu wa MUNGU. (Yaani maisha au mema au jinsi ambavyo MUNGU amekubadilisha na anavyokutumia kwa Utukufu wake),  lakini kwa yule ambaye hajaokoka yeye anaonekana  kawaida tu, mzuri tu na kwa wewe ambaye umeokoka watakuona unakasoro Fulani lakini ni kwa sababu umemkataa Ibilisi. Tazama hata wakati YESU anakufa, mpaka saa anakufa watu wanamwona mbaya tu, na wakati anakata roho wanasema hakika  alikuwa mwana wa MUNGU yule…  na hata katika dunia ya leo mtu akifa ndio utasikia ni mzuri, hata kama alikuwa  mchawi. YESU kwao hawakumsikiliza na hata mimi wapo ambao hawatanisikiliza sawa, lakini mimi sipendi ifikie wakati huo, ambapo mtanitafuta au utataka kunisikiliza hutanisikia wala hutaniona, sipendi ufike wakati huo ambao utatamani au utasema au utabakia kusema  alikuwa nabii wa MUNGU kweli, lakini utakuwa umechelewa sasa angalia usije ukalia sana, usije ukaangamia sana, mnanielewa watoto wa MUNGU, usijiangalie ulivyo achana na sauti za shetani mwangalie MUNGU, YESU anarudi, unasherekea  kuzaliwa kwake kweli ni sawa na kwa kimwili umenunua nguo, unapiga makofi unasherekea ni sawa ila kumbuka ilitabiriwa, sasa tunasubiri kurudi kwake, imetabiriwa anakuja kukuchukua. Wewe ambaye umemkubali  usiogope majanga yaliyopo, umempokea, wewe usiogope sio umetengwa usiishi katika dunia, maana duniani kuna wachawi lakini YESU yupo na wewe ,kuna wakukushusha, kukufunga, kukupeleka  mahakamani ili usiinuke, lakini yeye YESU yupo pamoja na wewe, nani kama MUNGU? Hakuna! Kwa MUNGU kuna neema mfano: kama huna kazi atakuvisha, atakulisha, hata kama wanadamu wamekukataa yeye atakukubali, Pesa imekataa MUNGU  anakupenda, jirani haongei na wewe  lakini MUNGU anaonge na wewe, songa mbele yamkini mtu haongei na wewe kwasababu humpi pesa huo sio upendo wa MUNGU huyo anakupenda kwa sababu ya pesa ila MUNGU anakupenda ulivyo.
          Mwanadamu anatabia mbili kimwili na kiroho; wanaopendaga kimwili, wakitenda dhambi  ukiwaonya hawakubali wanakimbia aibu, lakini yule  anaeonywa aliyekosea kiroho anatuliaga na kunyenyekea, sasa  na wewe  umemkosea au ukimkosea MUNGU nyenyekea na kutulia  utamwona MUNGU ila  kijapo kiburi kifo huja mbele sio mpaka ufe kimwili ila unaweza ukawa unatembea vitu vimekufa, amani imekufa,  vitu vikifa shetani anashangilia  Sasa mrejee MUNGU, mrejee MUNGU, Samehe, Mrejee MUNGU, mreje MUNGU.  MUNGU anawatu wengi sana lakini anakupenda wewe,  anakupenda sana,mnanielewa lakini?, lakini mnanielewa?  Muwe na Krismas njema, muwe na mwaka Mpya mwema na msiogope hata wakiwaloga waambie logeni sana mie niko na YESU napita tu, hata waliokulaani sana waambie laanini sana mie niko na YESU napita tu, wamekusema uongo waambie ongeza sana niko na Bwana YESU, waambie napita katikati yao niko na Bwana YESU, napita katikati yao, sio  kwa maneno ndivyo ilivyo naona mnapita,  mmepita, mnafika, umefika na wengine naona malaika  watakuja kuwanyanyua ile siku ya mwisho mpo hapa, mpo hapa maana wanakujua kwa jina lako, wewe ambaye umekubali kwamba ipo siku ya mwisho, nakuambia vile ulivyokubali tu ni kibali chako wewe kuondoka nawe ili usije ukaliwa  na wadudu na wanyama,  jina la BWANA libarikiwe

Baba  nakushukuru kwa maombi yangu kwako kwa ajili ya kundi hili ulihifadhi Baba, ninakuomba MUNGU na ninajua umeshajibu na naona umefanya, Chunga watoto hawa na asiwepo adui yeyote atakate gusa uwalinde MUNGU, linda nchi yetu Tanzania, Asante MUNGU, asante BABA ninakutukuza na kukuinua sana BWANA MUNGU juu ya nabii zako mwanzo wa dunia uliuanzisha wewe na mwisho wa dunia utaumaliza wewe ulimwandaa mwanao, akatabiriwa, akazaliwa  ninakubariki Bwana “Nyoosha mikono yako juu mbariki Mungu, mbariki Yehova, bariki Mbingu,  ni MUNGU anayefanya kitu na kitakuja kutokea. Mipango yote ya wanadamu na maadui waliyofanya juu yako MUNGU ataiondoa, MUNGU si mwanadamu hata aseme uongo,  unayelia na kufuta machozi Bwana anakupenda,  Kiburi na umaarufu wako si kitu Bwana anakupenda sana, Mbele kuna mazuri, mrejee Bwana, anakuhitaji akutumie kama chombo chake, kwa utukufu wake. Baba ninakuomba ile siku ya Krismas yakazaliwe mema zaidi na zaidi kwa kila mmoja wakati huu na yale  mabaya yakaangamie na vile ambavyo vilikuwa vinaua watoto wako na vitu vyao, vikaangamie haleluya. Asante MUNGU, amani ya MUNGU iwe nanyi Jina la Bwana litukuzwe siku zote. Nawatakia heri ya Krisma na Baraka tele, MUNGU awabariki sana. Amen.

 

Imeandikwa na Nabii Hebron