KUTAFUTA UFALME WA MUNGU
MATHAYO 6: 33-34 – Basi utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha siku kwa maovu yake.
Ufalme wa MUNGU umejengwa na MUNGU mwenyewe na ufalme huo ni wa dhamani sana katika maisha ya kila mwanadamu.
Neno la MUNGU linatufundisha na kutuelekeza kuwa tuutafute kwanza ufalme wa MUNGU na mengineyo yote tutazidishiwa. Unaweza jiuliza kuwa tutazidishiwaje? Au huo ufalme wa MUNGU unatafutwaje?
Jinsi ambavyo Ufalme wa Mungu au Ufalme wa Shetani unavyotafutwa.
· Okoka
· Fuata ubatizo wa ufalme wa MUNGU (kama YOHANA alivyokuwa anabatiza) sio ufalme wa ubatizo wa visima na vikombe nk. Kama umebatizwa kinyume cha hapo hata kama unasoma biblia huwezi kumwona au kumwelewa MUNGU, Kumbuka biblia hii hata wachawi wanaisoma; Swali ni ufalme upi uliopo ndani yako?
· Tafuta ufalme wa MUNGU ukiwa hai na fya na sio ukiwa umekufa maana MUNGU maana ukiwa umekufa ndio basi tena, huwezi fanya jambo lolote kiroho au kimwili, ila ukiutafuta ukiwa na nguvu utafika maana wenye nguvu wanaupata ufalme na wanakwenda mbele .
· Maisha ya taabu sio ufalme wa MUNGU maisha ya ufalme wa MUNGU maisha yananyanyua juu.
· Penda kubarikiwa na MUNGU na sio Wachungaji au uchungaji wa mshahara.
· Jifunze kumwangalia MUNGU mkumbuke Ayubu … alimpenda MUNGU
· Jifunze kujiongeza, kufunga, kusoma neon kufanya kazi ya MUNGU kwa moyo bila kushurutishwa.
· Ukimpenda MUNGU atakuinua.
· Jiulize, Je! unafahamu kiasi cha upendo wako na MUNGU au na wenzako?? Hapana ni MUNGU tu aliyesirini anajua ni kwa kiasi gani unampenda au unapenda wenzako na watu wake pia.
· Mpende MUNGU kwasabau ni BABA, ni MUUMBAJI ni MWOKOZI wako utaona akikubariki hadi ushangae na sio umpende kwa sababu tu anakujibu, Mpende MUNGU kwa Moyo wako wote hebu angalia maua na ndege – wanachanua wanaimba kwa sababu wanampenda MUNGU.
· Mpende MUNGU katika raha maana katika raha watu wengi humsahau MUNGU ila shida taabu na dhiki inapoingia ndipo humpenda MUNGU na kumtafuta MUNGU, hiyo sio sahihi, kipindi cha raha ndio kipindi cha kuomba sana na kusogea mbele za MUNGU.
· Usiangalie wanaokudharau angalia kile ambacho MUNGU amekiweka ndani yako na utukufu umrudishie MUNGU, hata Daudi alipoitwa walimdharau hata mimi walinidharau lakini nilimwangalia na kuzidi kumpenda MUNGU
· Mpende mtu au mtumishi wa MUNGU vile alivyo sio sababu ya upako au alikuombea ukapona la hasha!! Tunajifunza hata kipindi cha YESU kuna baadhi ya waliokuwa wameponywa wakataka amfuate YESU sio kwa sababu walimpenda ila ni kwasababu aliwaponya (YESU alifahamu hayo ndio maana alibakia na wale ambao walimpenda kiukweliukweli)
· Pia angalia na Jinsi unavyooomba, huwezi nenda mbele za MUNGU kwa kelele na kumlazimisha MUNGU haja za moyo wako, ,hata kibinadamu huwezi mwomba mtu kitu kwa kelele ila kuna namna ya kuomba na kumwomba MUNGU haaaaa kama ukiomba kwa kelele, kwa kiburi, kwa dhahau kwa lazima JE! unadhani kuwa MUNGU anaweza jibu maombi kama hayo? ukweli ni kwamba hata MUNGU hawezi kukujibu… hapana hatajibu.
· Turejee tumpende MUNGU atakavyo.
· Toa Sadaka kwa MUNGU kwa upendo sio kwa malalamiko - baadhi ya watu akimtolea MUNGU huwa wanalalamika sana mioyo inauma ikiwa hivyo ujue kuwa ufalme wa mungu mwingine ndio upo ndani yako.
· Usiibe fungu la kumi.
· Muombe MUNGU kwa unyenyekevu, upendo, subira naye atakujibu kwa upendo na kwa mapenzi yake ila ukipiga kelele mh. Hatakujibu.
· Utaishi miaka mingi endapo utampenda MUNGU na watoto wa MUNGU, pia penda kazi zake, angalia kanisa, ombea watu waende mbinguni ombea watoto wa MUNGU
· Usitishwe na vitisho vya wanadamu mwangalie MUNGU naye atakuinua wakati mwingine matisho ni mengi lakini atakayevumila mpaka mwisho atapata dhawabu.
· Katika kumpenda MUNGU lazima ujikane angalia mfano: watumishi waliotangulia, Ayubu, Musa, Petro Maria Magdalena na wengineo, walimpenda YESU
· Jifunze kuchukia mapepo, majini, mafundisho ya uongo, uovu, dhambi na mambo kama hayo na katika hayo na shetani atakukimbia na utazidi kumpenda MUNGU.
· Katika kumpenda MUNGU hata ukipita kwenye magumu MUNGU atakuvusha na atakukumbuka.
§ Neno la MUNGU linasema wenye nguvu ndio watakao uteka ufalme wa MUNGU, hawa ni wale ambao wameamua kuutafuta ufalme wa MUNGU kwa akili zao, fahamu zao na wamejikana nafsi zao kwa ajili ya kumtafuta MUNGU na ufalme wake.
§ Ufalme wa MUNGU hupatikana kwa kumkiri BWANA YESU, ila kuna baadhi ya watu ambao mpaka sasa hawataki kuukiri ufalme wa MUNGU kwenye mioyo yao, na kukiri kuwa YESU ni BWANA na Mwokozi wa Maisha yao, na unapokataa kumkiri BWANA, ina maana umemkataza Bwana YESU kuandika jina lako katika kitabu chake cha uzima wa milele. Ina maana kuwa, mtu huyo anaufalme mwingine na falme hizo zinapingana, hata sisi kabla hatujaokoka tulikuwa na ufalme mwingine mpaka pale ambapo ulipookoka na kumkiri BWANA YESU, ndipo tulipoanza safari ya kuokoka na kuutafuta ufalme wa MUNGU.
§ Ufalme wa MUNGU unautafutwa hatua kwa hatua, sio tu kwamba unapookoka ndio tayari umeupata kwa asilimia 100%, hapana! Mfano: sio watumishi wote ambao wamepakwa mafuta ya kumtumikia MUNGU ndio uone kuwa u Mtakatifu na ndio umeupata ufalme wa MUNGU, hapana, ufalme huo hutafutwa siku hadi siku na kwa kuomba, kusoma Neno, kufunga, utakatifu, unyenyekevu na mambo kama hayo, BWANA YESU asifiwe inastaajabisha sana, wale ambao wanautafuta ufalme wa giza au wachawi wao huutafuta ufalme wa giza siku hadi siku na kwa bidi zaidi wakiona nguvu zimewaishia au zimepungua wanaenda kwa wakubwa wao kuongezewa nguvu, ni kama ilivyo sasa mwisho wa mwaka watu wanaenda kwa mizimu, majini, miungu kutafuta uso wa shetani lakini wakiambiwa tafutani uso wa MUNGU huwataki; ila ki wepesi sana kukimbilia kwa wanajimu, miungu, mizingu, shetani na jeshi lake, kununua majini, kufanya matambiko na yote haya ni ili tu wafanikiwe kiroho na kimwili ila kupitia ufalme mwingine ambao sio ufalme wa MUNGU. (Uso wa ufalme wa Shetani hutafutwa kwa kuchanjachanjwa, ibada za mizimu, kwenda kwa waganga, uovu, uchafu maagano mabaya, kutoa kafara, na yote maovu ambayo wanadamu wanafanya ni kuutafuta uso wa MUNG)
§ Tanzama MUNGU BABA anavyotupenda, na hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila amwaminie awe na uzima kiroho na kimwili, na huyu ni YESU wa Nazareti Mkombozi wetu, MUNGU ametuandalia makao ambayo yapo, (baada ya maisha haya makao hayo yanatusubiri na makao hayo hayafananishwi na chochote na akatueleza bayana kuwa makao yapo). Ni upendo wa MUNGU kwetu ila baadha yetu hatutaki hayo ambayo tumeandaliwa kwa Neema ila tunataka yale ya Mpinga Kristo, ya Masharti, tunataka vitu vya haraka haraka, kuangalia ya shetani tunatautafuta kwa namna yeyote ili kumridhisha Shetani na sio kumridhisha MUNGU. Mfano wa wale ambao wanatafuta waume au wake wa kuoa, utajiri, ukimtafuta kwa mganga utapata wa kwa mganga, mwishowe ni mateso na vilio. Mwangalie Bwana Yesu tafuta ufalme wake. BWANA YESU asifiwe, Kwake kuna kila kitu na ametuwekea sisi.
§ Jiulize kwa nini unakaa kanisani lakini hufanikiwi? shida ni ipo wapi? Mbona unamwomba MUNGU hujibiwi? Shida ipo wapi? Mbona wapo wanaovushwa, kufanikiwa kuinuliwa mbona wewe hufiki shida ni nini? Jichunguza Zaidi madhabahu hutoa Baraka, mafanikio ya kiroho na kimwili, ukiona madhabahu ni ya MUNGU na uhufanikiwi shida ni wewe sio madhabahu, sasa basi amua kuachana na ufalme wa giza na upate ufalme wa MUNGU aliye umba Mbingu na dunia.
§ Ufalme wa MUNGU hutafutwa kwa upendo na furaha na Amani, hata kimwili unapompenda mtu kwa ajili ya kazi, umaarufu au jambo Fulani ambalo anakusaidiaga, kama huna mapenzi ya dhati kwake unampe kwa vile anakupaga msaada au unategemea jambo toka kwake huo sio upendo wa kweli maana siku akisitisha msaada au siku akisitisha kukupa pesa, na upendo huo unaisha, na hata sasa Kuna baadhi ya watu ambao wanakuja kwa YESU ili wapate kazi tu, waponywe tu, wasilogwe, wapate pesa lakini sio kwa ajili ya kuutafuta ufalme wa MUNGU, mtu huyo hautafuti ufalme wa MUNGU, Mtu huyo anatafuta vya mwilini, tumbo tu hautafuti ufalme wa MUNGU. Ukimpenda MUNGU hebu utafute ufalme wake na mengine utazidishiwa.
§ Katika ufalme wa MUNGU zipo Baraka za Rohoni na mwilini, wakati mwingine unatarajia kupata Baraka MUNGU akubariki mpaka ushangae, Lakini je kama huutafuti uso wake utapataje Baraka zake? Utainuliwaje kama wewe mwenyewe huutafuti uso wa MUNGU? Kwa kusoma Neno, kwa kuomba, kwa kunyenyekea kwa kukubali, maonyo, kutii amri, sheria na kuyafanya yale ambayo ni mapenzi ya MUNGU,
§ Katika baadhi ya madhabahu utakuta yamkini ni mchungaji / mhubiri anapenda kufanya miujiza ya upako wa YESU wakati hampendi YESU, na kama huna YESU wala humpendi YESU, hutapata miujiza au upako wa YESU au wa Madhabahu ya Mbinguni hatimaye mtu huyo atatumiwa na mizimu, waganga na wachawi, ataanza kwenda kutafuta nguvu kwa wachawi, kimwili waumini wataona wako kwa YESU kumbe ni nguvu nyingine inayo tenda kazi mahali hapo(Maana mtumishi alishamwacha YESU)
Kama ni mtumishi wa MUNGU tafuta uso wa MUNGU na MUNGU atakutunza zaidi ya ndege zaidi ya maua; ila watu wengi wa sasa wametafuta ufalme wa dini, mazingira na mapokeo ya wanadamu, mambo hayo hayafai yanaharibu maisha ya mwanadamu tafuta kwanza ufalme wa MUNGU.
Jiulize unaenda kanisani kutafuta ufalme wa MUNGU au kumtafuta MUNGU unamtafuta MUNGU au unataka Baraka za MUNGU tu .
§ Upendo wa kumpenda mtu kwa sababu anakitu ni mbaya kuna matajiri wengi duniani watu wanawapenda na wanaona watu wengi wanawapenda ila wengi hawawapendi kwa sababu walivyo wanawapenda kwa sababu ya alichonacho magari nk. tumbo misaada ndio inapendwa akiishiwa watu wote huondoka na hubaki na wachache wanaompenda kwelikweli. Wengi hupenda watu kwa sababu ya walichonacho, kikiondoka basi nao wanaondoka na upendo wao kwao unakuwa umeisha. Je! kwako wewe unakuwaje? Au unawaza nini juu ya MUNGU? Je! Unakuwa sawa na wanaompenda YESU kiukweliukweli au na wewe unayempenda YESU ili ukifa uende mbinguni, hapa umetanguliza kifo sio YESU. Upendo hauna mipaka au sababu amua sasa mgeukie MUNGU ukaone uwezo wake, neema yake, baraka zake.
§ Utasoma biblia lakini ndani yako ufalme gani upo? Hakuna kitu bora kama Bwana YESU, mioyo ya watu imejaa tamaa sio YESU huna tofauti na mtu ambaye anayempenda mtu kwa sababu unapata kitu fulani. Maana usipopewa ugali au chakula, utanuna na siku hana ataachana na huyo. Hata mimi nimeishi na watu wanaonipenda kiukweli na kwa sababu ya vitu ninavyowapa.
§ Tusipende kunyooshea vidole wengine jiangalie kwanza je, unampenda MUNGU huwezi mpenda MUNGU wakati humpendi jirani yako; unamsengenya, hupendi ainuliwe, unamsema vibaya, ukiwa hivyo wewe unapepo. Watu wengi husahau kile ambacho MUNGU amewafanyia, huona na kusema yale mabaya kumbuka MUNGU alichokufanyia amekuponya, amekuepusha na mengi amkulinda amekupa hewa kwa Neema yake, afya kiroho na kimwili, lakini baadhi ya watu huona mabaya tu haifai huo ni unafiki angalia isiwe kwako ukiawa na ufalme wa MUNGU yote utapata mpaka ushangae. Jiulize ni nani aliyetoa vyote? Jibu ni MUNGU hivyo mtafute kwanza.
§ Ufalme wa MUNGU hutoa huduma za MUNGU bure sio kwa Pesa na ufalme wa MUNGU hauchangamani na wa shetani japo shetani atajifanya kama vile ni wa MUNGU ndio maana hata YESU alipingwa ndio maana hata ukiokoka unapingwa usishangae ujue kuwa ni ufalme mwingine unakupinga .
§ Ukitaka vya dunia kwanza na kumwacha MUNGU hatima yake ni kufa kiroho na mali kupotea na zaidi ya yote utapata magonjwa kwa sababu sio ufalme wa MUNGU ambao unalinda vitu vyako bali ufalme wa shetani ambao hatima yake ni presha sukari, filisi na mambo kama hayo ila ukiutafuta ufalme wa MUNGU na haki yake mengine yote utazidishiwa utakuwa na vyote na ulinzi katika yote kiroho na kimwili.
§ Pia uaweza mpenda Mhubiri kwa sababu ya upako. Ukienda kwa waganga huo ni ufalme; katika Roho au Mwili hakuna ufalme unaoweza kushindana na MUNGU na kila wakati YESU alipotaka kutolewa katika ufalme wa MUNGU alisema BABA yangu BABA yangu…BABA yangu BABA yangu; hata wewe haijalishi ni jambo gani unalopitia ita BABA yangu, BABA yangu, mwangalie MUNGU, Petro alimpenda YESU sana lakini YESU alimwambia Petro JE! Unanipenda mara tatu? Petro alihuzunika, kwa sababu ndani ya Petro ulikuwepo upendo wa kumpenda YESU kweli kweli, ni kama leo ninavyokuuliza kuwa unampenda MUNGU? Unahuzunika yamkini kuna mahali au kwa madhaifu ya mwanadamu hatumpendi ndio maana tunaulizwa.
§ Unapoanmbiwa utafute kwanza ufalme wa MUNGU na mengine yote mtazidishiwa sio kwamba eti usiwe na vitu vyako maana baadhi ya watu wakiokoka hawataki kazi wao wanakuwa wavivu tu, hawafanyi kazi.. Tazama akina Daudi, Sulemani na wengineo walikuwa na MUNGU na mali zao na vitu vyao pia kufanya kazi ni lazima ili MUNGU akubariki.
§ Kuna baadhi ya watumishi ambao wengi wapo katika ufalme mwingine na hawafanyi kazi na huo ufalme haujibu hatima yake husumbua waumini kwa kutaka vya mwilini badala ya kumuuliza MUNGU na kufanya kazi ili MUNGU awabariki, hivyo hulibebesha kanisa yaani watoto wa MUNGU majukumu ya MChungaji au mhubiri huyo kwa sababu ya uvivu na ufalme unaotenda kazi ndani ya huyo mchungaji, hivyo humwaibisha MUNGU na mpaka wakati mwingine kama mchungaji huyo hajapewa haja ya moyo wake huanza kulaani na hatimaye mhh. Kanisa linachoka na watu wanaona kuwa YESU hajibu au hayuko ni kweli mahali kama hapo YESU hayuko maana YESU huwalisha waTumishi wake hivyo pia angalia madhabahu ipi unayoabudu??? Na ufalme gani utatenda kazi hapo.
§ Baadhi ya viongozi wa makanisa hulaumu waumini hasa pale ambapo haja zake binafsi hazijatimizwa mfano. Kapu la mama mchungaji nk. Mavazi, ada nk. Kumbuka laana isiyosababu haimpati mtu badilika sadaka yako ni siri yako na MUNGU, mtumishi wa MUNGU haruhusiwi kulaani yampasa kubariki … (usilaani usije ukalaaniwa Pesa ni ya Kwako ukitaka kumtolea MUNGU mtolee huo ni Upendo kati yako na MUNGU na sio kushurutishwa)
§ Wakati unaambiwa pokea chunguza na ufalme gani unatenda kazi ndani ya huyo mtumishi … Ukiwa na ufalme wa MUNGU unachanua
§ Hata wenye dhambi hupeana vitu vya dhambi kwa upendo na wakinyimana huona kuwa wana roho mbaya ni kweli kwa sababu wako katika ufalme wa shetani ila ukiwa katika ufalme wa MUNGu ukitenda vya dhambi vitaonekana kuwa ni vya dhambi kwa sababu katika ufalme wa MUNGU watakatifu tu ndio wanaotawala.
§ Tamaa ni mbaya ukiwa unaangalia vitu haaaaa utabakia kituo kimoja kwa sababu humpendi MUNGU unapeda vitu vya YESU.
§ Tunaishi wote kwa Neema na kwa Mapenzi ya MUNGU lakini yule ambaye huutafuta ufalme wa MUNGU kwa bidii hujazwa Zaidi na Zaidi, MUNGU humpenda kila mtu ila mwanadamu hampendi MUNGU
Tubu ili MUNGU arejeshe mambo mazuri, Mwokozi anakuja ukuambiwa tafuta ufalme wake hutaki, okoka hutaki, kabatizwe hutaki, vya ufalme wa MUNGU hutaki ila vya duniani mlango ni mpana watu huvifuata kwa wingi, ila kumbuka siku ile inakuja, wengi watalia na kusaga meno, wengi wataambiwa sikujui sikujui!!!! MUHESHIMU MUNGU MAANA NDIO BABA ASIYEBADILIKA – WANADAMU HUBADILIKA. Dunia na vyote vitapita MUNGU atabakia pale pale heshimu wazazi walakini usiheshimu yale ambayo ni kinyume na mapenzi ya MUNGU (usiheshimu yale ambayo wanakuongoza kinyume na mpango wa MUNGU)
KUMBUKA - UPENDO WA MUNGU HAUCHUJI ILA WA MWANADAMU UNACHUJA.
Asante MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo asante Bwana YESU, asante Roho Mtakatifu kwa neno lako na uwezo wako nakuomba BWANA YESU, uuvunje ufalme wa shetani ndani yangu na kuujenga ufalme wako, kwa sababu nilikuwa katika ufalme wa giza wa mapepo, mizimu, majini, matambiko, jeshi la shetani lilinitawala kwa namna tofautitofauti, lakini sasa ninafuta na kukataa magano na mazindiko, na mapatano niliyofaya na shetani na jeshi lake. Bwana YESU nimekuwa nikijichanganya kwasababu sikujua ni ufalme gani uliokuwa ndani yangu, ila sasa nimetambua nilikuwa nikishindana na wewe, MUNGU wewe ndio unijuaye nichunguze nifinyange BABA. Bwana YESU ninakuomba unisamehe kabisa kuanzia sasa niutafute ufalme wako wa Mbinguni, MUNGU uliyeumbwa mbingu na dunia nazikataa falme zote ambazo sio zako najitenga na hizo falme ambazo sio za kwako MUNGU kuanzia sasa na hata milele katika jina la YESU. Amen.
Baba katika jina la YESU, ninabomoa na kuteketeza walioshikana na miungu mapepo majini waliotafuta MIUNGU wanaadamu, miungu ya wachawi nina ibomoa kwa jina la YESU serikali zao kwa umoja wao katika ulimwengu wa Roho nazibomoa zianguke na zikukatae kuanzia sasa nyote yako iwe huru na ufalme wa MUNGU uwejengwe ndani yenu. Amen
MUNGU AWABARIKI,
IMEANDIKWA NA NABII HEBRON