Pages

Saturday, December 19, 2020

 

JINSI YA KUTEKA BARAKA

Baba katika jina la YESU Kristo wa Nazareti, Ubarikiwe uinuliwe milele na milele,  kwenye Neno, katika uumbaji, na kila mahali na mapenzi yako yazidi kutimia,  naharibu mapenzi yote ya Ibilisi,  Naliinua NENO lako juu sana mfalme,  wewe ni MUNGU utendaye, unayebariki, unayepiga maadui zetu, unayetuwazia watoto wako mazuri  na makubwa sana, naombea fahamu za watoto wako ulizoziandaa katika uumbaji wako zikapokee yale uliyowaandalia sawasawa na Mapenzi yako na kwa jinsi ulivyoziandaa na Mapenzi yako yazidi kutimia na hata fahamu ambazo hazipokei naziombea  zikapokee, Bwana na utukufu ukurudie MUNGU, Amen,

BWANA  YESU asifiwe, Nawasalimu katika jina la YESU Kristo wa Nazareti aliye hai.

Ndugu Msomaji, Mungu anampango mzuri kwa ajili ya kila Mwanadamu aliyemuumba na hata wale watakaozaliwa tena.

 KUMBUKUMBU LA TORATI – 28.1-20 – Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, MUNGU wako, kwa bidi, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia, na Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA MUNGU wako, Utabarikiwa mjini utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa na uzao wa tumbo lako na uzao wanchi yako na uzao wa wanyama wako na mifugo, maongeo ya ng’ombe wako  na wadogo wa koondoo zako, litabarikiwa kapu lako na chombo chako cha kukandia unga, Utabarikiwa uingiapo utabarikiwa utokapo, BWANA atawafanya adui zao wainukao juu yako kupigwa mbele zako; watakutokea kwa njia moja lakini watakimbia mbele zako kwa njia saba,  BWANA taiamuru Baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkononi mwako naye atakubarikia katika nchi akupayo na BWANA Mungu wako, BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia utakaposhika maagizo ya BWANA Mungu wako, na kutembea katika njia zake, Na mataifa yote duniani yatakuona umeitwa kwa jina la BWANA nao watakuwa na hofu kwako, BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri na  katika uzao watumbo lako na uzao wa wanyama wako wa mifugo na uzao wan chi yako, katika nchi ya , BWANA aliyowaapia baba zako  kwamba atakupa. Atakufunulia mali na hazina  yake nzuri ya  nayo ni mbingu kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake  na kubariki kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi nawe hutakopa wewe, Bwana atakufanya kuwa kichwa wala si mkia nawe utakuwa juu tu wala huwi chini utakapoyasikiliza maagizo ya Bwana MUNGU wako nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya,msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lolote kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

Lakini itakuwa usipotaka kuisikiliza sauti ya BWANA MUNGU wako, usiyaangalie na kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa  kapu lako na chombo chako cha kukandia, Utalaaniwa uzao watumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe wako na wadgo wa kondoo zako, utalaaniwa uingiapo na  utalaaniwa utokapo,BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa katika yote utakayo yatia mkononi mwako, kuyafanya, hata uangamie na kupotea upesi, kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.  

Malaki 3:10-12 – Leteni zaka kamili ghalani; ili kiwemo chakula katika nyumba yangu; mkanijaribu  kwa njia hiyo

 

¾    Kwa mtu ambaye ameokoka yakupasa uwe unamiliki Baraka za Kiroho na za kimwili pia, Haipendezi  pale ambapo mtu ameokoka halafu hana Baraka.  Baraka ya kwanza ni kumpata Bwana YESU, kwa kumkiri BWANA YESU, na pia  unaweza ukawa unamkimbilia YESU lakini hujampokea.

¾    Katika kuziteka Baraka kuna kuzipokea, kuzichota na kupewa. kila mwenye mahitaji akienda mahali anachota na anabeba.  Lakini umesha wahi kujiuliza Kwa nini mwingine anatoka hana kitu, Hata wewe hebu jiulize je una Baraka? Maana  Baraka ni kitu kizuri kutoka  kwa MUNGU.

¾    Angalia Mifano: Ya watumishi wa MUNGU waliotangulia, Abrahimu, Petro, Daudi, Yusuph na wengineo wengi MUNGU aliwabariki na walikuwa na Baraka za kiroho n ahata za kimwili, Walibarikiwa.

 

ZIPO BARAKA ZA KISHETANI NA ZA MUNGU

Nataka kuona Baraka za MUNGU kwako

    ¾            Zipo njia za kuteka Baraka za MUNGU, Kwanza okoka, uwe mwombaji safi, Usiwe na chuki, fitina, Mpende YESU, na sio umepende ili akupe Baraka mpende yeye YESU kama YESU, yeye atakupeleka mahali uzichote Baraka, huwezi mpenda YESU pasipo kuokoka na kumkiri na kwa kuwa Mwaminifu kwake.

    ¾             Wanadamu wengi hupenda MUNGU awe mwaminifu kwao lakini wanadamu sio waaminifu kwa MUNGU ila MUNGU ni mwaminifu kila wakati, jitahidi na uombe Neema ya kumpenda MUNGU na kuwa mwaminifu kwake, katika majira yote. (Ya Amani, furaha, huzuni mapito na mengineyo kama hayo.

 IPO MIFUMO YA KUFUATILIA BARAKA ZA MUNGU NA WA SHETANI.

    ¾            Adui  mtu upofu ili asione Baraka zake kiroho na kimwili, ni Dhahiri kuwa kipofu haoni hivyo unapigwa upofu na hatimaye unababaika na kuhangaika huni wala hutaona Baraka zako, utasikilizia kwa watu.

    ¾            Kuna namna nyingi za kuteka Baraka, kiimani na kimatendo. Hata kumchezea YESU, kupiga makofi, Kuinua Mikono juu, kusoma Neno la MUNGU, kumsujudia  kumpenda, Neno linatufundisha; Mpende Bwana MUNGU wako kwa akili zako  na vyote ulivyonavyo ila Shetani anawawekea ugumu  watoto wa MUNGU, huondoa moyo wa ukirimiaji wa moyo mweupe kwa upande wa MUNGU na huuweka Moyo huo kwa upande wa shetani, ndio maana ukiwa na fedha. Mfano.  1,000,000.00 kutoa 10% ambayo ni 100,000 inakuwa vigumu sana, unawaza mpaka basi tena hatimaye umnamkopa MUNGU sadaka ya  na hapo ndio huyohuyo shetani anakukamata na kukushitaki. (Ona huyu kaiba fungu la 10 na Malaki 3:10-11 inatufundisha vyema.

    ¾            Baraka za  upande wa MUNGU hazina masharti magumu, n ahata hayo mepesi baadhi ya watoto wa MUNGU wanashindwa kuyatimiza lakini kwa ambao wapo upande wa shetani, hupewa masharti magumu na wao walioko upande huo hutimiza( wakiambiwa ua, bomoa, haribu vunja nk. Anafanya hivyohivyo)

    ¾            Nikiwa kama baba wa kiroho napenda mfanikiwe – Kiroho na kimwili. Usiibe fungu la kumi, Ukiiba ni laana - Hivyo unakuwa unateka filisi njaa, balaa nk. Katika kuteka Baraka unatakiwa uwe mjanja na kuchukua hatua, Makanisa yanavyoongezeka ni Baraka maana nilipoitwa ilikuwa Baraka.

    ¾            Ukiokoka umebarikiwa.

    ¾            Kwenda kunyume na mpango wa MUNGU ni laana – Mtumishi akifuata mapenzi ya MUNGU ni baraka ila akikataa ni laana.Adam na Eva walibarikiwa  shetani akawadanganya tukapata mabaya lakini YESU alikuja akatuletea Baraka tele.

    ¾            Kanisani ni mahali pa kuchota Baraka nyenyekea, msikilize anayokufundisha, usijiinue, nyakati nyingine MUNGU huangalia na kukupa kidogo ili usipoteee, ila ukikaa vizuri ukikubali kutengenezwa na MUNGU na kutii utapata Baraka nyingi,

    ¾             Laana zinakuja makanisani kwasababu baadhi ya watu wanawatukana, wanawabeza, hawawaheshimu   watumishi  wa MUNGU,  ukimtukana mtumishi wa MUNGU Baraka na ulinzi unaondoka, hata waliomtukana MUSA walikufa usimdharau kuhani au mtumishi wa MUNGU ipende madhabahu ya MUNGU YA YESU ni BWANa na Mwokozi wa Mataifa yote. Madhabahu ndio uinayokupigania inakupa Baraka inakulinda na mabaya hayatakusogelea, jini wala mchawi hatakuweza

    ¾            Ukikaa vizuri madhabahu hukupeka Mbinguni unapomnyooshea kuhani kidole unaporomoka na vitu vyako vinaporomoka.

    ¾            Kuiombea madhabahu, ni namna ya kumpenda na kupata Baraka za MUNGU, iombee ile madhabahu inakubariki kiroho na kimwili na jinsi unavyojikonect unazidi umwagiwa Baraka.

    ¾             Moyo wa uchoyo hauna Baraka - MUNGU hana shida anataka kujua kuwa anampenda anakujaribu je unafunga, unaomba au umekaa kama tikiti maji au mzigo, maana hivi vitu mpaka vipate msaada ndipo visogee. Sasa  mpaka usogezwe? hufungi huombi upo tu.. Baraka za mtu hazifanani na mwingine, ukiambiwa Kuokoka hutaki,  kuomba hutaki, kabatizwe unatoa jibu kuwa una dini ya mama na Baba,hivyo unakataa  ubatizo.

    ¾            Ni laana kulitumia Neno la MUNGU vibaya,  huduma ya michango ni laana katika ufalme wa  MUNGU lakini kwa upande wa shetani  ni Baraka kwa watumishi wake, maana shetani hana kitu ni mwizimwizi tu anaiba Baraka kila kona,  hivyo watumishi wa Shetani kuwabebesha watoto wa MUNGU michango na mizigo mizito kwao ni sawa na shetani huwabariki.

    ¾            Ukuwa katika upande wa MUNGU,  Utaingia kwa Baraka utatoka na Baraka,  Kama unanjia mbili mara kwa wachawi,  Miungu NK.. utapata laana MUNGU hachangamani, Kama una laana hutavuka utachokea njiani hutafika.

    ¾            Penda kuwa Baraka na sio laana..  Ukiona mambo yako hayaendi wewe unalaani, unashutumu, unalaumu badala ya kushukuru MUNGU hapendezwi na hayo.

    ¾            Ukiwa mahali palipo na MUNGU; miungu, wachawi hawakuwezi.. Baraka Kubwa toka kwa MUNGU ni ulinzi kiroho na KIMWILI.

    ¾            Hata katika Kutoa sadaka au unataka kumfanyia MUNGU jambo fulanio, huo  ni upendo wako na MUNGU utatoa kile ambacho MUNGU amekujalia kwa upendo.

    ¾            Kuwa na Moyo wa upendo na kunyenyekea kwa MUNGU, Neno lake ukilisikia linakutetemesha. Endapo Madhabahu ina Harambe, michango nk. Ukilaaniwa unakuwa mshamba, unakuwa wa mwisho kila wakati, mchelewaji, hukeshi, huombi, hufungi, du  utapataje Baraka? Usiwanyooshee kidole mtumishi / watumishi wa MUNGU ni wa muhimu wanakuombea wanakesha kwa ajili yako madhabahu itakupiga ukimtukana au kumsema.

    ¾            Mtumishi akiwa wa MUNGU utaponywa na utapokea Baraka na endapo amemwacha MUNGU utalaaniwa maana hata sadaka zako zitapokelewa kwa miungu na laana wala si  Baraka.

    ¾            Baraka  za MUNGU huachiliwa kutokana na kiwango ambacho umebarikiwa nacho au ambacho hakitakutoa katika mpango wa MUNGU. Baraka huipata kutokana na level ya Imani yako wengi wanakosa Baraka kwa sababu wanakuwa na wivu na WIVU ni mbaya YESU atakuacha aisee. Acha Masimango .. acha !!!

    ¾            Usimlalamikie MUNGU – Mambo megine ni mwanadamu anachelewesha unaposhukuru unainuliwa na unaponung’unika hupewi.. Moyo wa uchoyo ni mbaya sana kata kuwa mchoyo maana kama mikono yako haitoi hata huwabariki wengine wewe utapokeaje??  Omba moyo wa Utajiri, shukrani, kutoa nk.  Jinsi mtu alivyo ndivyo hivyohivyo moyo wake ulivyo.

    ¾            Unawaza nini juu ya MUNGU kazi yake, neema yake, nguvu yake, injili yake nk. Ukiwa mchoyo hupewi, angalia mfano Dhahiri; Matajiri  walio na hela hupewa Zaidi na Zaidi maana anatoa, wanaajiri watu, wanalishsha watu na  MUNGU humwongezea ili aongeze wafanyakazi na Baraka zizidi kusambaa.

    ¾            Baadhi ya makanisa yana utajiri wa kishetani na baadhi yao wanakuwa na utajiri wa kimaskini.. Usipende kusema shida yangu, ugonjwa wangu, presha yangu, kawaida yangu, kataaa  kwa kinywa chako, maana kinywa huumba na pia Baraka p au uponyaji ukakukimbia kwa sababu ya ukiri wa kinywa chako,

    ¾            Moyo wa dhambi unaondoa Baraka, omba unyenyekevu, Omba MUNGU  akupe moyo wa upendo, kama humpendi unayekaa nae utampendaje huyu??? Penda kila mmoja, Chukia mabaya ya mtu lakini mpende mtu kama alivyo. YESU ndio chemichemi ya uzima, akasema  njooni kwangu,  mtachota Baraka lakini endapo mtaenda  makaburini au kwenye MIKUYU hizi ni baraka za wafu na shida, mtachoka, kumbuka madhabahu hizo za kinyume na MUNGU  ni za Mikosi au wafu  ndio utapata hayo,  ikiwa ni ya mabaya mabaya  yatakufuata. 

    ¾            Kazi ya kuhani ni kuzaa vipawa na karama na hatima yako,  Kuhani wa MUNGU huzaa vya MUNGU na wa shetani  hivyohivyo.  Kama umepata mume au mke kwa  laana hutabarikiwa,  hivyo omba mtegemee MUNGU ndio maana anasema “ Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa” kwa sababa kwake kuna kila kitu, ni mkao wa mtu kuamua ni njia ipi aiendee ya Baraka au laana, Penda kazi ya MUNGU Penda Neema yake  na upende Baraka zake.

    ¾            Funga masikio angalia MUNGU wala sio mwanadamu..  Mwandamu hawezi kukubariki ila MUNGU anakubariki, sasa amua uchume matunda ya Raha na sio ya taabu.. Usiibe vitu vya MUNGU, hata sadaka usiile maana utapata laana na Ukiiba 10% tegemea kupata mikosi, kitu kidogo kinakukosesha Baraka kubwa maana mshitaki wetu yupo, Wengi sana tumechota mikosi badala ya Baraka

    ¾            Afya pesa.. maisha marefu hata kifo chako kiwe Baraka ili malaika tu watakapokuja kukuchukua wakuchukue kwa Amani.

    ¾            Mungu ndie mtendaji,  Neno la MUNGU litasimama hivyo hivyo, kuna baadhi ya watu wanalaana wanatafuta vitu hawapati,  maana baadhi ya watumishi wamefanya watoto wa MUNGU kuwa laana, kuwadai hela za service/ huduma za maombezi sasa hapa anayetoa na anayepokea wote mnakuwa mmelaaniwa, na huenda ikawa akaja mtumishi kutoka mbali yamkini nchi za nje mkadhani ni Baraka kumbe ni laana amebebeshwa mizigo na laana aje kuambukiza hizo roho,

    ¾            Haiwezekani kama katika nchi kuna watumishi wa MUNGU wa kweli na CORONA naiondoki Nchini hapo jiulize!!!  Jibu ni kuwa Maombi ya baadhi ya watumishi ambao ndio asilimia kubwa hawaombi kwa MUNGU wa mbinguni bali huomba kwa baali na baali ndio anayewajibu na baali hana nguvu kumbuka kipindi cha Eliya.  Baadhi ya   wahubiri wanaoenda kinyume na MUNGU amelaniwa na MUNGU.  Waumini wengi hutaka mchungaji awaone, hufanya kazi kwa sifa au kutoa kwa sifa ili mchungaji awaone, la  hasha ! hii nayo ni laana...sasa penda na omba MUNGU akuone na sio mtumishi akuone..

    ¾            Mtumishi ambaye ni omba omba huyo amelaaniwa na MUNGU mtu asiyetunza wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko yule asiyeamini, amua sasa mwangalie MUNGU mtumaini MUNGU.

    ¾            Penda kulea watoo wako upate Baraka.

    ¾            Teka, chota, tunza na katika kuchota Baraka kuna hofu, uoga, angalia kila aliyejitoa kwa MUNGU alipata Baraka, Kwanini unampenda shetani na vitu vyako mwambie MUNGU naomba unisamehe maana nahitaji kukupenda Zaidi  na wewe ndio utakaye nipeleka Mbinguni.

    ¾            Sio kila mkutano, maombi au nyumba za ibada za kukimbilia, leo huku kesho kule, baadhi ya watu wamelaaniwa kupitia  kutumia mafuta ya  upako ya watumishi wenye laana,maana ikiwa mafuta ya upako ya mtumishi ambaye MUNGU hamtambui ukiweka nyumbani mwako hutapata Baraka haiwezi kuwa Baraka kwa sababu yeye amelaaniwa, hivyo utaishia Nuksi, balaa na Mikosi.

    ¾            Katika kutafuta Baraka viko vikwazo, ila mwamini MUNGU utavuka, Utaishi atakuilinda hiyo Baraka, anza uaminifu na MUNGu usiwe sababu badilika penda  kuelekezwa na MUNGU, mpende MUNGU, kiasi ambacho shetani akikuwaza tu apate kibano, ukipendwa Zaidi MUNGU atatunza yote yaitwayo kwa jina lako.

    ¾            Mwangalie MUNGU…. Ukimpenda MUNGU utafika kwa MUNGU, Mwanadamu sio YESU tubu, nyenyekea, utashawi sana,  Miti, majani au ua hunyeshewa, humea na kustawi,  Uwe na Imani ya matendo ili usiwe unalongwalongwa kila wakati.

SALA YA TOBA: BWANA YESU ninaomba unisamehe nilikuwa nimekataa kukukiri kwa kinywa na kukupokea uwe BWANA na MWOKOZI wangu, na Baraka zangu  zilinikataa, ninakupenda YESU ninaomba unifundishe, unioshe na ni ninaomba unisamehe, naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Amen

 Nianaamuru kila utajiri urejeshe mali zilizofichwa zirejeshwe shetani na watenda kazi na maajenti wake warejeshe vitu vyangu, nafuta maagano yote na  damu iliyotolewa ili kuharibu maisha yangu inyamazishwe kwa damu ya YESU sema mikosi, shida, madeni kuingia na kutoka na laana sizitaki.. popote nilipofungiwa na shetani aniachie kwa jina la YESU. Naomba rehema nilipoharibu agano la Baraka na MUNGU wa Mbinguni niolipokwenda kwa miungu  naomba unisamehe nafuta maagano na mikataba   niliyoingia ee Bwana YESU unisaidfie. Nafuta mabaya yote niliyonenewa kiroho na kimwili kwa jina la YESU ee MUNGU naomba niumbe upya nifinyange sawasawa na mapenzi yako. 

Bwana YESU ninaomba uniondollee moyo wa shida, filisi, magonjwa, mauti na moyo wowote ambao ni kinyume na MUNGU uondoke ndani yangu  ee Bwana YESU ninaomba moyo wa Wokovu, unyeyekevu, Imani, maombi, kufunga, kuomba BWANA YESU ninaomba unisaidie, ninaomba unirejeshe, kiroho na kimwili. Nakataa maombi ya laana niliyoyapokea. Bwana Watoto wako tunakupenda mioyo yetu inakupenda ee MUNGU usikae kimya, usinyamaze tunakuita BABA, tunakuiota YESU, tunakuita Yehova mapenzi yako, yatimie juu ya maisha yetu. Amen.

 

 

IMENDIKWA NA NABII HEBRON