ROHO YA MAPOOZA AU NGUVU YA MAPOOZA
BABA MUNGU ninakushukuru, ninalibariki jina lako ninalitukuza, na kuliinua juu sana, najua yapo uliyoyaanda kwa ajili ya watoto wako, waliosogea mbele zako, wakisubiri kuinuliwa, kutolewa walipofungwa vifungo mbalimbali, kiroho na kimwili, BABA ninaomba Neema ya kufunguliwa na kuwekwa huru kwa kila mmoja katika jina la YESU Kristo wa Nazareti Mwana wa MUNGU aliye hai. Amen.
NENO: MARKO 2:1-12 - Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa kwamba yumo nyumbani. Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mangoni, akawa akisema nao neno lake, Wakaja watu wakimletea mtu wenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne, Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, walitoba dari pale walipokuwepo; na wakiisha kulivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye YESU, alipoiona Imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, mwanangu umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwemo huko, wameketi wakifikiri moyoni mwao, Mbona mtu huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndie MUNGU? Mara YESU akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua kuwa mwana wa adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (Hapo amwambia yule mwenye kupooza) Nakuambia, ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Mara akaondoka akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza MUNGU, wakisema, Namna hii hatujapata kuona kamwe.
Nawasalimu katika jina la Bwana wetu YESU Kristo;
Ø Bwana YESU asifiwe; Napenda kuwakumbusha kuwa mambo mengine hayawezekani pasipo kufunga na kuomba na mtazidi kumwona MUNGU katika kufunga na kuomba.
Ø Hongereni kwa wale ambao mmefunga siku ya leo BWANA amefanya; mtamwona MUNGU amefanya kaa katika mtazamo wa kuona jambo, tulifunga kwa ajili ya kumshukuru MUNGU kwa mambo mengi, kwa sababu mambo mengine hayawezekani pasipo kufunga na kuomba name, nimetangulia katika kiti chake cha enzi naye ameniambia amefanya.
Leo tunajifunza juu ya mapooza, nguvu ya mapooza, jinsi roho za mapooza zinavyofanya kazi na kuzing’oa roho za hizo ili uwe huru. Neno hili limekuwa likitufundisha mambo mengi na hata sasa linaendelea kufanya kazi kama vile apendavyo MUNGU. Mwanadamu ameumbwa na MUNGU kwa mapenzi yake MUNGU na sio ka mapooza
AINA ZA MAPOOZA – unaweza ukapoozwa kiroho au kimwili – na kama nilivyokwisha kuwafundisha ya kwamba jambo lolote katika maisha yako linaanza katika Roho na ndio maana Biblia inasema MUNGU hapendezwi na mtu baridi anataka mtu Moto, na MUNGU hakutuleta sisi ili tupoozwe kazi ya adui ni kuleta mapooza, kupooza watu yawezekana unapoozwa au umepoozwa na wachawi majini, mapepo, mizimu na mambo kama hayo ya ufalme wa shetani, (kupooza tunakoongelea si kupooza mikono au miguu tu, lakini nataka ujifunze jambo; huenda ikawa kuna mambo unataka kufanya, lakini hauwezi unaweza ukakaa mwaka mpaka mwaka mwingine pasipo mafanikio katika jambo hilo, hivyo uelewa bayana kuwa una mapooza, umevikwa roho ya mapooza na mapooza. Ukiwa na mapooza mambo hawawezi kwenda, na ikiwa hata jambo moja hulifanyi, wala hukuweza kulifanya basi uelewe fika kuwa hiyo ni dalili kuwa umepoozwa kabisa katika ulimwengu wa roho, unaweza ukawa unatembea lakini umepooza ila wewe kama wewe hujitambui. (Maana haya huanzia katika roho) YESU amekuja kuwatoa wale ambao walikuwa wamepooza ili wasimame na watembee. YESU anataka unyanyuke utembee, ufanikiwe, ubarikiwe na hatimaye ufike Mbinguni.
Kazi ya adui ni kuwapooza watoto wa MUNGU na adui huanza kuwapooza watoto wa MUNGU katika ulimwengu wa roho na adui huchukua nafasi yako , nyota yako, mafanikio yako , huduma yako na zile Baraka ambazo MUNGU alikuandalia katika ulimwengu waroho na kukuwekea mapooza na ukiwekewa mapooza hutanyanyuka utabakia kituo kimoja, na mafanikio yako yanageuzwa yanatolewa kwako na anawekewa au kujiwekea yeye au yule ambaye anahitaji kumpa. (Wanackukua nafasi yako yeye ndio atakayekuwa au aliyekuwa anaitumia kabla ya wewe kuondolewa mapooza na BWANA YESU.) Tazama hata huyu ambae alikuwa amepooza uhai na uzima wake ulikuwa na mapooza, akaja YESU akamrejeshea, akasimama, wakashaangaa na leo mapooza yatakapoondolewa nawe utasimama, utafanikiwa na watu watashangaa.
Yesu aliponinituma ili kuja kufanya kazi yake ya injili hapa duniani, maana mbinguni hakuna shida ya injili, na injili imetoka mbinguni, akaniambia “Mtumishi wangu Hebron nenda duniani kwa kila kiumbe, ukawasimamishe waliopooza” na usifikiri kuwa waliopooza ni wale tu ambao wako vitandani, wasiosikia nk. Unaweza ukawa umepoozwa kibaraka, fedha uchumi, maisha, Imani, huduma nk. Chochote unachofanya hakiinuliwi wana kufanikiwa na vyote havikukubal na hatima yake umebakia tu kulia na kulaumu; unahitaji msaada. (Maana siku zote mtu aliyepooza mfano kimwili, lipo jambo ambalo anahitaji kufanya, na hawezi yamkini ni kusimama, kunyanyua mkono au mguu au chochote haweza na kiroho ni hivyohivyo) ni mpaka aje BWANA YESU akuinue lakini usifikiri kuwa ni jambo jepesi maana hata YESU alipingwa, akaambiwa wanawezaje kuwasamehe hawa!! Mafarisayo wakachukia, Hata wewe unapofanikiwa wapo wanaochukia, hasa unaponyanyuliwa juu kiroho au kimwili wale wenye ROho za mapooza watakusema na kukusimanga ni wanafiki…tazama hata hapa kwenye biblia YESU aliijua mawazo ya mioyo yao n ahata sasa YESU anajua mawazo ya mioyo yetu.
ZIJUE TABIA ZA MWANADAMU:
Ø Tabia ya nje - Hapa utamwona mtu kwa nje ni mzuri mwenye heshima, mnyeyekevu matakatifu, mpole, mwenye hekima na busara,
Ø Tabia ya ndani – Tabia hii imefichika ndani, YESU ndio anayeijua na kama ndani yako ipo tabia mbaya ya ndani basi itoke na tabia njema iingie ili ukamwone Bwana YESU. Je! Hujawahi kukutana na mtu ambaye anaweza anakusalimia na baadae akamwambia mtu wa pembeni nimemsalimai lakini simpendi au anakuambia kabisa, Bwana YESU asifiwe, halafu anakuchukua!! Nadhani umeshaona; Je! Umeshawahi kujiuliza ni nani anaweza kusoma tabia ya ndani ya mtu? Ni YESU tu. YESU akasema¬ Mimi nazijua tabia zenu za ndaniajijua, Mnanipinga kwa sabau nimemtoa huyu mapooza, ni hata sasa kuna watu wanaokuchukia au wanachukua wenzao wakitamani hata wafe kwa sababu tu wametolewa mapooza; au wameponywa au umerudiana na mke/mme au wamefanikiwa kiroho au kimwili. Jambo hili linashangaza sana unapokuwa na mambo kama hayo au tabia za ndani zilizofichika, na hata kama umekaa kwenye wokovu unaimba, unamtumikia MUNGU, maisha yako hayatapata mabadiliko kiroho au hata kimwili unabakia palepale, upako, Neema haiongezeki. unakuwa kama msindikizaji ka sababu ya tabia ya ndani iliyojificha. Jichunguze Tabia ya ndani yako ikoje? kama ina Chuki jichunguze, na kama zipo roho zinginezo, ujue lipo Pepo ndani yako na hata kama MUNGU atakutumia anakutumia anaingia akimaliza kukutumia anatoka anakuacha hivyo.
Ø Ukiwa na mapooza au ukisimanga wenzako, unakuwa adui wa MUNGU unakuwa kama mafarisayo na masadukayo; maana kila jema ambalo MUNGU anamfanyia mwenzako kwako inakuwa kinyume unajenga chuki na uadui. (Roho za Mafarisayo hutavuka, hutafanikiwa, na utazidi kukauka kiroho na kimwili na Utabakia na manughuniko, na MUNGU hapendi wanughunikaji).
Ø Chuki huondoa upendo na matokeo yake Shetani atakutumia anakudunda na kukuvunja, unaweza ukawa huponywi, hukui kiuchumi, kiroho au kimwili kumbe unatabia ya ndani mbaya! Mwambie MUNGU akuchunguze, usipende kuchunguzwa na mwanadamu na uamue kubadilika.
Ø Unapofikia hatua ya kuona wenzako hawafai wewe ndio unafaa na kujiona ni mtakatifu wa watakatifu au kama vile wewe ndio Zaidi ya hao, napenda nikufundishe uelewe uelewe jinsi ambavyo tabia ya ndani ilivyo, Bwana YESU asifiwe, unakuwa mnafiki, unasema wenzako, huna upenndo, huna Amani, mchoyo, mbinafsi na ukiwa na mambo mengi kama hayo; unakuwa adui wa MUNGU na MUNGU atakuacha pembeni.
Ø Acha nikufundishe upate ufahamu maana hata nikikuombea nisipokufundisha Hutabadilika na hutamwona MUNGU kwa sababu umejaa mapooza ukiona una wivu kwa lolote hiyo ni roho ya mafarisayo na masadukayo huna shukrani kwa MUNGU, mazoea, dharau, kudharau watumishi, waumini, viongozi ukawaida uchoyo, uvivu nk.
Ukipoozwa hutaweza kufanya jambo loote au ukifanya sio kwa kiwango kile ambacho MUNGU alikuumba nacho hata ardhi, safari zako na vitu vyako vyote vinakataa unabakiwa na nuksi, balaa, mikosi na madeni.
Ø Ndoto mbaya ni mapooza.
Ø Ipo habari njema, amua ili imani yako imrejee BWANA YESU, Neno linasema aliyepooza alibebwa na watu wanne yamkini na wewe unabebwa na watu20 au 40 watu wanalia na kukuombea kwenye maombi baadhi mabaya na wengine mema na kwa kuwa BWANA anakwenda kukuinua na wao watashangaa jinsi ambavyo maisha yako yanakwenda kubadilika; lakini ujue kuwa wewe ndio sababu ya maisha yako kubadilika au kutokubadilika
Ø Shetani akaipooza dunia Bwana akaniambia Hebron wewe ni moja ya watumishi wangu nakutuma uende ukaondoe mapooza ambao maana watu wamepoozwa ili wasiende Mbinguni, Je! kuna Mwanadamu ambaye anakataaga kwao? Hasa pa;e ambapo alipokuwa ameumbiwa au alipotoka (achana na kwa wazazi wako ulipotoka) kwa aliye kuumba yaani MUNGU unapakataa? kumbuka utakufa na utatakiwa kurudi huko huko kwa MUNGU lakini mtu hataki kurudi kwa MUNGU kwa sababu amepoozwa, Imani amepoozwa asimpookee BWANA YESU na kama umepoozwa ujue kabisa unaelekea Jehanamu na sio Mbinguni lakini ukimpokea BWANA YESU unapokea nguvu mpya ya kwenda Mbinguni.
Ø Wanadamu watakucheka lakini usiogope, mtumaini BWANA YESU kwani yeye ni Moto na atakuinua uende Mbinguni achana na maneno ya wanadamu kuwa; waliookoka wamepitwa na wakati waambie wao ndio walioopoozwa na ndio wamepitwa na wakati; na Mbinguni hawatafika mpaka watakapoondolewa mapooza na endapo hayataondolewa watachomwa moto; mtu ambaye ameokoka na kumpokea na kumkiri YESU yeye ni moto n ahata shetani hawezi litaja jina lako na ndio maana ELIYA na HENOKO walipandishwa na Moto na wewe endapo hutakuwa na mapooza na umeokoka utakuwa mmoja wao. Wanadamu ambao hawataki kuokoka wamepumbazwa.
Ø Tuliletewa ubatizo wa mapooza kwa kikombe , kisima, bahari na kama huo ndio maana mtu anabatizwa ili kuwa mwanafunzi wa YESU lakini hawezi wala hataki kumpokea YESU kwa sababu ya mapooza ambayo aliyapata kwa njia ya ubatizo ambao ni tofauti na ule wa YOHANA
Ø Mapokeo ya wanadamu ni mapooza, kimwita mwanadamu MUNGU, mafundisho ya uongo, michango kubadili, Neno hayo yote ni mapooza, na hata kama yanatajwa kwa jina la YESU, lakini ni Mapooza endapo yataondolewa unakuwa MOTO hata jina lako linavyotajwa linakuwa la moto, hata shetani akilisikia anachanganyikiwa.
Ø Lakini kuna ujanja ambao jeshi la shetani hutumia ili waweze kupooza moto wa wana wa MUNGU (Nilipokuwa mdogo nilikuwa naangalia picha /video za vita wanatuma scadi na wengine wanatuma kulipooza ili bomu likishuka lisiwe na moto) sasa ujanja huo huo wanautumia kiroho ili wakupooza; lakini ukumbuke kuwa BWANA YESU kila alipokuwa wanataka kumpooza haikuwezekana kwa sababu hakuwa na roho ya mapooza na angelikuwa na roho ya mapooza alipokufa asingelifufuka, ndio maana alifufuka; alikuwa na ile Roho ya mbinguni ndio maana alipokufa na baada ya siku tatu alifufuka .. Na wewe mpokee BWANA YESU ili hata ukifa uende mbinguni lakini ukifa na mapooza hutafika mbinguni.
Ø Shetani anamipango mibaya na dunia, baadhi ya wakrisrto wamepoozwa kwa kusoma biblia katika mitandao, hiyo biblia sio salama “ Mimi Nabii Hebron nawaambia, kwa sababu kwa dakika moja yamkini biblia hiyo husomwa na watu 10,000,000 husomwa na wachawi, wapinga kristo free mason nk. Hapo hujui ni maneno yapi ambayo kila anauempinga YESU anayovuviwa ili wakristo wapooze na wamsiende Mbinguni, na hujui kuwa aliyeiweka alikuwa na lengo gani. Na hata ikiisoma hutapata mafunuo utakufa kiroho, utapoozwa na hutaenda Mbinguni, (Kumbuka kila Mkristo ana Biblia yake katika ulimwengu waroho na biblia yako kimwili ukiwa nayo, unaweza kuiombea kuikomboa , na je! hiyo ya mtandaoni je? Utaikomboaje?? Utapateje mafunuo?? Haya mfano tablet au simu ipotee, utafanyaje na je! Mfano. siku moja ukute biblia hiyo haipo mtandaoni utafanyaje??? Lengo ni kuuaa Roho za watu kiroho, watu wasimwelewe MUNGU, na ndio maana wakisoma baada ya mda vinafutika kwenye ufahamu na hata ukiulizwa umesoma kitabu gani hata hujui.
Ø Unaweza kusema kuwa umempokea YESU sawa yamkini ukaona una nguvu na utaweza lakini jua kabisa kusudi lao ni kuvuvia watu wasimwelewe MUNGU, hivyo hutapata mafunuo. Hebu Tafakari. Simu hiyohiyo unasengenyea wenzako, unasimanga, unaangalia picha za X na uchafu mwingine mwingi hapo hapo unasoma Biblia utaelewa kweli?? Hebu jiulize.
Ø Wengi wanaona aibu kubeba Biblia eti kuwa watu watamwonaje? Hii ni dalili ya kumtokumpenda MUNGU.
Ø Kama Huomb,i hufuungi, mwizi wa fungu la 10%, hukai katika utakatifu , hatima yake ni kufa kiroho, macho na masikio ya rohoni pia yanakufa unabakia na mapooza.
Ø Kataa kujitete kaa katika hali ya kujisahihisha.
Ø Mbona marafiki, watoto, wachumba unawapenda lakini MUNGU humpendi? Sio vibaya kuwapenda lakini Zaidi nafasi ya kwanza mpe MUNGU kwa sababu MUNGU anaishi milele, lakini mwanadamu anakufa, MUNGU habadiliki lakini mwanadamu anabadilika.
Ø Penda wenzako waombee, wainue, maana kama unamchukua mwenzako basi hata MUNGU pia utakuwa unamchukia. Mwisho wa mwaka shetani huandaa mapooza ili kila kitu kipooze ila angalia usiwe sababu ya kuwapooza wengine kila wakati Mshuhudieni MUNGU, tabia chafu si za Mbinguni hata kama mwenzako amedondoka, amerudi nyuma, mwinue, mwombee na umrejeshe kwa upendo.
Ø Ukiwa na Roho Mbaya ni mapooza kushindwa kuomba ni mapooza kuombea ndani ya blangeti ni mapooza
Ø Usiwe sababu; mfano MUNGU anamponya mtu wewe unachukia, wewe ni nani, hata umhukumu wenzako YESU alikuja kwa ajili ya wote, Wewe uliyeokoka hutaki hata kumshuhudia mwenzako kisa hutaki aende Mbinguni!!! Huo sio upendo, hutaki hata kumpeleka mwenzako mahali sahihi ili awe huru sababu ya wivu? MUNGU hapendi na hizo sio Tabia za mbinguni, MUNGU hufurahi mmoja akiponywa maana aliyemuumba ili siku moja aende mbinguni.
Ø Kila kitu ni cha MUNGU, mrejee MUNGU, MUNGU anatupenda sana ila shida ilianza kwa wanadamu kumbuka kuwa sio kila Mhubiri ni wa MUNGU wako wenye mapepo pia wapo walioitwa na MUNGU na wapo walioitwa na shetani ila nao humwita shetani mungu maana ndio mungu wao (hao wahubiri waliobadilisha neno la MUNGU)
Ø Kama unampenda MUNGU ondoa upendo wa kumpenda shetani na kama hujaokoka basi ujue kuwa wewe unampenda shetani hu ndio ukweli japo hujui au unajua na unafanya maksudi, lakini Wokovu up na mtu anaweza kuokoka akiwa duniani na baadae atafika Mbinguni ila asikuambie mtu kuwa hakuna wokovu.
Ø Mungu aliacha Huduma 5 na baadhi ya makanisa hawatambui manabii, eti wanadai Nabii awe chini ya mchangaji huko ni kubadikisha neno nabii ndio kiongozii wa kanisa na sio askofu.
Ø YESU alikuwa nabii, Musa alikuwa nabii, na biblia yenyewe imeandikwa kinabii kanisa ambalo haliongozwi na Nabii lipo kinyume na neno la MUNGU.
Ø Usiwe kama Yona, MUNGU alipoghairi alichukia sana na hatimaye alikufa, ukiwa na tabia mbaya wewe ni muuaji au pepo na unakuwa adui wa MUNGU. Je! Jiulize! Endapo mwenzako akifa kwenye dhambi utafaidi nini???
Ø Mambo yamebadilika kubali ubadilike uonyeke, ukikaza shingo, shingo itavunjika ; acha uzinzi, funga ndoa; madhara ya roho za mapooza Baraka zinaondoka na hatimaye MUNGU anakuacha. Na utakuwa unafungulia milango ya adui.
Ø Ukiwa hufungi, huombi, huna kiu ya kuongea na MUNGU adui anakupooza katika kitengo cha maombi na kukuwekea mapooza kiroho na kitengo cha njaa kiroho na kimwili.
Ø Dhambi ni mapooza, kuzoea vipindi vya kanisa ni mapooza
Ø Huduma yako, ufaya kazi wako, uinjilisti wako, uchungaji wako, nk umepoa kwa sababu ya tabia za ndani, watoto wako, familia yako ni mapooza kwa sababu ya tabia ya ndani, hatima yake ni mapooza.
Ø Amua sasa na useme mwenyewe mapooza sikutaki, mapooza yakuachie leo, na mwaka utavuka bila kupingwa, tunaenda na speed ya MUNGU, kila kitu kiende sasasawa na mapenzi ya MUNGU, maana ya kuokoka ni kuondolewa mapooza na mabaya, matatizo yaliyo ndani, masengenyo, chuki, fitina na uchafu, n ahata mambo mengineyo ambayo watoto wa MUNGU wanayoyapitia sio uchawi ni mtu /wewe mwenyewe.
Ø Nenda sawasawa na hali uliyonayo, nenda sawasawa na kipato chako, mwombe MUNGU akupe hekima ya maisha, hekima yako ikiwa imewekewa mapooza hali ya maisha inakuwa mbaya hekima ni kila kitu ni utajiri, hata kama mali zitaondoka lakini hekima ikiwepo mambo yataenda sawa.
SEMA:
Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina lagu katika kitabu chako cha uzima wa milele, ninaomba unisamehe pale ambapo nilikuwa na roho za mapooza na tabia za ndani ambayo hazikukupendeza naomba ukaiondoke hata mimi hazikunipendeza, nakuwa mwema machoni kwa watu hata nikimsalimia mtu BWANA Asifiwe namsalimia kwa kinywa lakini ndani ya moyo wangu ni mbwa mwitu kabisa, mimi sitaki hali hii najua ukija utaniacha, endapo nitakuwa nimeshikilia tabia hii, nimewachukia wengi, nimewakataa wengi nikajiona kuwa mimi ni bora kuliko wengine, BWANA YESU, ninaomba toba na Rehema nirejeshee Roho wako maana wewe ndio MUNGU, hakika roho yako ingelikuwa ndani yangu nisingelichukia mtu nisingelitamani mtu afe, nisingechukia mtu akinyanyuliwa, akifanikiwa kiroho na kimwili, nilikuwa mtumishi wa shetani na maroho yake yalinitumikisha, naomba toba BWANA YESU naomba nikawe furaha kwako BWANA YESU, nataka Kila ninapoomba BWANA YESU na mimi niweze kusogea chini ya miguu yako Bwana YESU, mda mrefu nilikuwa naomba nisigee chini ya miguu yako nikakuta gate na malaika walinizuia nimejua mimi ndio shida BWANA YESU naomba unisamehe ikiwemo na dhambi ya kulipinga neno lako niondolee na roho ngumu ambayo ilinitesa nikatakaa ubatizo wako miaka na miaka naomba Bwana YESU uniponye, Imani uliyonipa wewe ya kupata matunda, lakini Imani yangu akaharibiwa ikaanza kumwona mchungaji ndio MUNGU au YESU, BWANA YESU naomba unisamehe, nimeteseka mda mrefu sikuchuma matunda, nilichuma mabaya BWANA YESU, hata katika kukutolea nikakutolea Katika njia ya kimapooza, nikafundishwa kimapooza na mimi sikujua au nilijua wala sijitetei BWANA YESU niliambiwa toa hela upone nami nikatoa, nikapokea mapooza na biblia inasema sadaka ni siri yako mimi nikaambiwa niandika jina nikapewa na risiti na hayo MUNGU hupendezwi nayo na mimi siyataki wewe wanijua niangalie BWANA YESU, niweke katika njia upendayo nikakutane na wewe. Amen.
PROPHET HEBRON.