MUNGU
AMESEMA WATU WOTE WA MATAIFA YOTE WAACHE KUABUDU miungu (HARAKA)!
BWANA YESU ASIFIWE!
Nawasalimu wanadamu wote popote mlipo mkiwa mmeumbwa na
MUNGU aliyeumba ulimwengu wote na ndiye MUNGU mwenye vitu vyote wakati miungu
hawana kitu chochote. Mnamo tarehe 4.4.2020 nimeamriwa na MUNGU niwaeleze
habari hizi japo siyo nzuri kwa watu watakaoendelea kuabudu miungu anasema kila
mwanadamu arejee kwake MUNGU na amwabudu yeye tu na endapo ataendelea basi hata
pata amani tena katika maisha yake au siku zake, hiyo amani aliyokuwa nayo
itaondolewa kuanzia leo. Watu wa MUNGU mimi ni chombo tu cha kukufikishia
ujumbe wake MUNGU kama apendavyo yeye sababu anakupenda, amenitumia nabii wake
niwape taarifa hii na onyo ila sauti yake MUNGU ikisisitiza sana kwa hasira sana
akisema iweje mimi niwaumbe wanadamu halafu waabudu vitu ambavyo havijawaumba?
Ina maana wamenikataa!
Sasa waeleze Hebron watakaoendelea ninaondoa amani kwao
ile amani itakaa tu kwa wale wanaoniabudu mimi MUNGU niliyeumba mbingu na
dunia. Waeleze hata mali walizonazo hao wanaosema ni matajiri huo utajiri ni wa
kwangu, kama ni pesa ni zangu, kama ni dhahabu ni zangu, miungu haina chochote
ilichokileta wala kutengeneza. Mimi nitaihukumu miungu pamoja ana wanaoiabudu,
ila hiki ni kipindi cha neema ukipata ujumbe huu utubu na uombe rehema uachane
kabisa na miungu kuiabudu au vitu vyote kuvifananisha au kuviita mungu yeye
MUNGU hatengenezwi na wanadamu wala kiumbe chochote yeye ni ALFA
NA OMEGA. Hana mwanzo wa mwisho. Kwa hiyo nawaombea mioyo yao hao wasiojua na wanaojua waache sababu
sasa inakuja kipindi cha mapigo kwa atakayemdharau yeye aliyewaumba wanadamu
naomba muelewe kuwa ibilisi aliwateka watu fahamu na akajifanya yeye ni mungu
akawapa baadhi wanadamu vitu na mali na umaarufu kwa njia za nguvu za giza hata
baadhi katika mataifa watu wakaona hamna MUNGU, na wengine wakatumia elimu zao
kuona hakuna MUNGU, wanasahau hata nguvu ya kusimama, hata uhai ni yeye MUNGU
kampa mtu huyo huyo ambaye ameona hakuna MUNGU bali kuna miungu, wakati hata
miungu inamwogopa MUNGU na inajua itauwawa kabisa. Sasa ni heri kurejea kwa
MUNGU, tazama hata wana wa Israeli walijitengenezea ndama wakaiita mungu Musa
akaivunja na sasa muikatae miungu kiroho na kimwili kuanzia sasa.
Kwa kifupi nitaeleza aina za miungu kwa mifano ili kwa
usiyeyajua upate kuelewa maana miungu ni mingi sana.
1.
Kitu chochote kilichoumbwa na MUNGU au
kutengenezwa na kazi za mikono ya wanadamu usikiabudu; mfano mnyama, madini,
miti, mashetani, sanamu ya namna yeyote ile. Ibada za matambiko, mambo ya wafu
na mila, kumwabudu mtu anayejiita yeye ni YESU au MUNGU vyote hivyo ni miungu,
hata kutumia uchawi, kubeba irizi, kutafuta umaarufu kwa uchawi, hata kutafuta
ufalme kwa nguvu za giza au kwa wachawi, hata kupiga ramli na mengineyo mengi.
MUNGU aliyeumba mbingu na dunia anasema waeleze wanirejee nawasihi kwa jina la
YESU rejeeni wacheni miungu hiyo haina faida itakuangamiza na hautaurithi
ufalme wa MUNGU mbinguni.
2.
Unapotegemea nguvu za giza zikusaidie katika maisha
yako au mizimu pia hapo unakuwa umeabudu miungu na kukufanya amani iondolewe na
MUNGU kwako. Ninaposema kuwa amani itaondolewa kwa atakayeendelea yapo mengi
mabaya yatampata ikiwemo na mapigo kwa mtu yeye kama yeye hayo ni ya MUNGU siri
yake.
3.
Mafundisho ya uongo yote ni ibada na ni maneno
ya miungu haijalishi zinatumia jina la YESU. Neno lake YESU halibadiliki.
4.
Kuabudu waliokufa. Ukisoma neno la MUNGU
aliyeumba mbingu na dunia na kila kitu anasema yeye siyo MUNGU wa wafu, basi
kama utaabudu wafu uelewe kuwa utakuwa tayari unaabudu moja ya aina ya miungu
ya wafu yani wasiishi tena na wanasubiri kuhukumiwa.
ANGALIZO:
MUNGU awaokoe mataifa yote mumrejee YESU kuwa ndiye BWANA NA
MWOKOZI na ndiye anayesubiriwa sasa kuwanyakua watu ambao wanamwamini yeye na
kuokoka na kumwamini MUNGU aliyeumba mbingu na dunia aliyeumba vitu vyote na
watu wote waseme na wakiri yeye ndiye MUNGU aliye hai anayestahili kuitwa ndiye
MUNGU aliyekuumba. Usiabudu hivyo vitu tena maana shetani anatumia njia hiyo
ili awateke wengi bila kujijua na kwa kujua pia.
SALA YA TOBA:
Sema MUNGU uliyeumba
mbingu na hata kuniumba mimi natubu naomba na rehema, nimekujua kuwa ni wewe
ndiye uliyeniumba na hata vitu vyote na utajiri wote katika ulimengu wote ni
mali yako. Nyie miungu nawakataa kwa jina la YESU siwataki kuanzia sasa. Uandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima mbinguni kwako wewe MUNGU aliye hai,
namkataa shetani na kazi zake zote na
miungu nawakana mbele za MUNGU mbinguni akiniona muda huu kwa jina la YESU,
mimi siyo mtu wenu kuanzia sasa. Amen.
Ubarikiwe! Ujumbe huu uwatumie na wengineo ili waepuke
mapigo yajayo!
Kwa mafundisho zaidi tembelea www.prophethebron.or.tz
NABII HEBRON.