HAPPY
PASSOVER 2020!
HERI
YA PASAKA 2020!
Shalom watu wote wa mataifa yote. Nawasalimu kwa jina la
mwokozi YESU wa Nazareti ambaye ndiye anayesababisha kuwepo siku hii ya
ukombozi wa viumbe vyote. Nawatakia heri na baraka zake.
Na pia nakukumbushia kuhusu yale aliyoniambia MUNGU kuhusu
miungu ya kuwa kila mwanadamu asiabudu tena maana atakosa amani na itaondoka
kwake na kwa watu ambao wataendelea kuiabudu. Anasema miungu haina hata
utajiri, wala fedha, wala uhai, vitu vyote ni mali yake yeye aliye Alfa na
Omega kwa hiyo mrejeeni hiki ni kipindi cha neema kabla hali haijawa mbaya
labda uwe haujui au unajua sasa uelewe. Kumbukeni hata uhai ulionao wewe
mwanadamu upo katika mkono wa MUNGU, sasa kwa nini kuabudu vitu vya
kutengenezwa na wanadamu ukawaita mungu au kwa nini kuabudu hata viumbe vyake,
sasa swali je ni vyenyewe ndio imekuumba? Jibu siyo, na kama siyo basi uelewe
yapo aliyekuweka hapa ulimwenguni ndiye umwabudu tu. MUNGU anachukia na sasa
ataitoa amani kwa wanaoabudu miungu, ikiwemo na wachawi na freemason na umoja
wao. Ujumbe mkubwa ni kukataa miungu kabisa na muda siyo mrefu wapo watu
wameshaisikiliza sauti ya MUNGU na ujumbe huu wataitupa miungu au kuivunja
vunja kama vile Musa alivyoivunja vunja ile ndama kule jangwani.
ANGALIZO:
Cha kujiuliza mnajua kuna siku ya mwisho wa hukumu je ni
nani atakayekuhukumu? Je ni hivi vitu ambayo vimetengenezwa na wanadamu? Jibu
siyo maana hata watakaoviabudu hata kuvitengeneza na wao watahukumiwa na
MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Siku
ile ya mwisho siyo miungu itatoa hukumu bali na yenyewe itachomwa moto na hata
hao ambao watakaokuwa wameiona ndiyo
miungu wao. Kwa hiyo zipo madhehebu nyingi ambazo pia zinatumia jina la YESU
lakini YESU hayupo hapo bali ni miungu nazo pia hawatakuwa na amani.
Waliomsaliti Mwokozi YESU wakafuata miungu na wao pia waache
na wasipoacha hawatakuwa na amani na jambo hili litafanyika kwa ulimwengu wote,
sababu yupo yeye aliyeuumba ulimwengu huu na ni mali yake. Sasa amekasirika,
amenituma niwaeleze mumrejee yeye sababu ataondoa amani, sasa kama unafanya
hayo uache ili uwepo katika wale ambao MUNGU atakaa nao, sababu mwanaye YESU
wakati wowote atarudi na mjiandae kwa utakatifu na kudumu katika wokovu wa
kweli na atawachukua wale tu ambao pia linamwabudu BABA yake yaani MUNGU aliyeumba
mbingu na dunia.
Jambo lingine ambalo ni miungu na watu wengi hawalijui
sababu adui amewapiga upofu wanadamu japo wahubiri baadhi yao wanajua kabisa
wametumwa na miungu yao au kutekwa na miungu. Katika neno unapoona
linachanganywa na mapokeo ya wanadamu hapo inakuwa ni miungu binadamu; kwa
mfano katika ubatizo angalia aliobatizwa YESU ndio uliotoka kwa MUNGU aliyeumba
mbingu na nchi, sasa ukiwa unapata au kufuata batizo tofauti hapo uelewe
unafuata miungu binadamu.
Imeandikwa na MUNGU watu waombewe bure, ila watu wanachajiwa
pesa kitendo hicho mnakuwa mnachajiwa na miungu na kuiabudu miungu.
Usiingie katika nyumba za miungu, nyumba za ibada
inayoifanya kanisa kuwa soko, michango, minada, mapokeo ya wanadamu, kulipinga
neno au madhabahu zenye maagano ya kuhani.
Tubu sasa mrejee YESU, sema BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu zote unaindike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele
ulitoe jina langu kwa miungu kwa shetani naikataa, siitaki tena nyie siyo MUNGU
hamjaumba mbingu na dunia na vyote vilivyomo, nawakataa kiroho na kimwili, YESU
najikabidhi mikononi mwako. Asante kwa ajili ya kufa kwa ajili yangu na
ukafufuka. Amen.
PROPHET
HEBRON.
Happy Passover 2020