JINSI YA
KUIMALIZA CORONA (COVID-19) ULIMWENGUNI POTE.
BWANA YESU ASIFIWE watu wa MUNGU nawasalimu kwa jina la
MUNGU aliye hai aliyeumba mbingu na vitu vyote vinavyoonekana na
visivyoonekana. Katika jambo hili linalotikisa dunia kwa sasa kupitia huu
ugonjwa wa Corona napenda mjue na kuelewa kwa wale ambao hawajui chanzo cha
ugonjwa kuwa ugonjwa huu haujaletwa na MUNG, bali umeletwa na shetani ili
aangamize watu wote na shetani amepata nafasi sababu watu wamefanya dhambi sana
mpaka shetani akawashtaki wanadamu na ndipo akapata kibali cha kuleta pigo
hili, MUNGU yeye ni wa haki na shetani anajua kabisa MUNGU anafuata haki, na
ndipo aliposhtaki na akapata nafasi ya kuipiga dunia.
Nimekuwa nikieleza kwenye YouTube sana na pia kwa njia ya
makala ni jinsi gani tufuate maelekezo ya MUNGU ili tuweze kuliondoa hili pepo
Corona. Hapa cha kufanya ni kuomba rehema na toba watu wote wa ulimwengu na
kumaanisha kuacha dhambi kabisa, tena iwe ni toba na rehema ya kudumu siku zote
za maisha yetu ili huyu adui asije akapata tena nafasi ya kuipiga dunia. Tumemwomba
MUNGU na ameturehemu na sasa Corona itaisha sababu MUNGU anasikia maombi ya
watakatifu wake anaopendezwa nao katika dunia hii. Ila bado litakuja pigo
lingine kwa wale wanaoabudu miungu, majini, mapepo, mizimu na vitu vyote
ambavyo siyo MUNGU wa mbinguni, hivyo nawasihi mataifa kwa wale wasiojua kuwa
ni dhambi kuabudu miungu waache maana kazi ya Nabii ni kutoa taarifa kwa ajili
ya yatakayokuja na ndiyo niliyoambiwa na MUNGU, hawatakuwa na amani kabisa
wamrejee MUNGU watubu sasa, hili jambo la miungu litakuwa ni pigo kubwa zaidi
ya Corona (Covid-19), ila litawahusu tuu hao wasiomuabudu MUNGU aliyewaumba,
muiache, haiongei, hajibu, haijakuumba.
Someni neno mkumbuke habari za Nabii Eliya na wale mabaali,
mabaali walipatwa na mabaya na kila
anayeabudu miungu anafananishwa na mabaali. MUNGU anasema miungu haina hata
fedha wala utajiri wala ardhi, miungu inakufaga. Kwa hiyo ikataeni nyie mataifa
msije mkatupwa katika shimo la moto, tazameni hata sasa wapo walioiomba miungu
ya sanamu iliyotengenezwa na wanadamu lakini haikuwaokoa na Corona, wamekufa
haijawajibu hata baadhi yao imebidi wakaibomoe na kuitupa baharini sababu
waliona haina maana yoyote imeshindwa kuwaondolea Corona mpaka sasa watu wanarudi
kwa YESU kuomba rehema na ndipo sasa ugonjwa unaanza kupungua na ndio njia ya
kuisha sasa na pia mkarudia uovu sababu mshtaki yupo macho ambaye ndiye
ibilisi. Shetani hafurahii kabisa mkiomba toba na rehema sababu anajua dunia
itasamehewa kwa ajili ya uovu wake na ikisamehewa ndipo uponyaji utashuka,
hivyo basi haifai kuwa waoga au kujifungia ndani tu, hiki ni kipindi cha kuomba
sana maana ni cha hatari, kuzuia watu wasife na Corona maana hata hao waliokufa
hao wote siyo MUNGU kasababisha, walitakiwa wawe hai, maana pia katika hao
waliokufa wapo ambao walikuwa wanasubiria kuokoka na wapo ambao bado walitakiwa
waishi. Hivi ndivyo mumjue shetani alivyo mbaya sana. Sasa mrejeeni YESU ambaye
ndiye mwokozi wa uliwengu huu bila yeye hakuna uzima.
ANGALIZO:
Corona ni pepo la shetani ambalo ni sumu yake aliyoitoa
kuzimu ili kuangamiza watu, sasa basi mpokee YESU ili mwili wako uwe na damu ya
YESU, hili pepo linaogopa damu ya YESU na jina la YESU, ila iwe ni YESU wa ukweli
kweli hasa siyo YESU wa uongo. BWANA YESU naomba toba na rehema unisamehe
dhambi zangu zote najikabidhi mkononi mwako unilinde milele, uniandike jina
langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.
PROPHET
HEBRON.