Pages

Friday, August 16, 2019

MTUMISHI AKIFUNDISHA TOFAUTI NA
UKWELI ANAKUWA HAMPENDI YESU.

BWANA YESU ASIFIWE, soma katika kitabu cha Yohana 14:24. 

"Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno
mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka."


Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU Kristo wa nazareti aliye hai, najua watu wengi wanampenda YESU sana katika mioyo yao na hata katika fahamu zao na pia wapo ambao
wanamchukia YESU kabisa ambaye ndiye mwokozi wa ulimwengu
huu na ambao wakiwa na lengo la kuwapoteza watu wasijue ukweli
kuhusu YESU wakiwa wamevaa vazi la kondoo na bali ndani ya
mioyo yao ni mbwa mwitu.

YESU amesema mtu asiyempenda yeye hayashiki maneno yake, sasa napenda kufafanua hapa kwa sababu pamekuwapo na wanafiki
wengi katika ulimwengu huu wanaosema wanampenda YESU ndio
sababu wanahubiri habari za injili, bali pasipo watu kuwajua kumbe wanakutana na wahubiri ambao hawampendi YESU na ndio sababu YESU alisema mnampenda kwa midomo ila ndani ya mioyo ni wanafiki wakubwa kwake yeye YESU.

Soma Mathayo 15: 8-9
Maneno haya alikuwa anawaeleza wahubiri kipindi kile
alivyokuwepo hapa ulimwenguni kimwili na sasa yuko mbinguni.
Baadhi yao wameendelea kutompenda YESU kwa kujua au
kutokujua. Wanang'ang’ania jina lake ili kutafutia pesa na siyo kwa nia ya kuwaongoza watu katika kweli ili siku moja wafike mbinguni.

Kwa mafundisho yao ya uongo yanayowafanya wanadamu
kuyafuata na kuyashika wapelekwe jehanamu siku ya mwisho. YESU amesema mnayoyasikia ya uongo kwanza siyo neno lake na pili ambaye hampendi YESU ni lazima afundishe ya huyo anayempenda ambaye ndiye baba uongo (lusifa).

JINSI YA KUMJUA/KUJIJUA HAUMPENDI BWANA YESU

 Utawatoza watu pesa ili uwaombee;
 Utawabatiza ubatizo wa uongo;
 Utaifanya madhabahu kuwa ni soko;
 Harambee kanisani;
 Kuabudu wafu, mizimu, matambiko;
 Kuwa mchawi au freemason;
 Kuzuia watu wasiokoke;
 Kubariki uovu na pombe.

ANGALIZO: Yapo mambo mengi ambayo yamewafanya hata
wahubiri waliokuwa wanampenda YESU kiukweli wakaanza kuwa
wanafiki kwa YESU na sababu zilizowafanya kuwa wanafiki, zipo
nyingi, ikiwepo kulitumia jina la YESU na kulichanganya na uongo
na huko kusema kwao uongo, ndiko kunakomfanya mtumishi awe
MNAFIKI na zaidi ukiongozwa na mtumishi mnafiki kwa YESU na wewe muumini utavaliwa na hiyo roho ya unafiki kwa kuchukia
ukweli. 

 Kuhusu injili ya kweli jambo la kwanza jiulize je MUNGU
anabadilika? NENO lake linabadilika? Kwa nini alikataa na
akaonya NENO lisibadilishwe (Ufunuo 22:18-19). Je wewe ni
nani unayemchezea MUNGU na je haujui hautaishi milele hapa
duniani? Je haujui ipo siku ya kuhukumiwa kwa wanafiki?
Kama ulikuwa hauelewi, tubu na kuacha kwa sababu yeye ni
wa rehema ila kwa watakaoendelea na injili ya kinafiki, moto
wa jehanamu unawasubiri, huo ndio ukweli, japo wapo
waliojiingiza kabisa katika ufalme wa shetani ili kuwapoteza
wanadamu wakati wao wenyewe wanajijua kabisa hawaendi
mbinguni bali wale wanaotakiwa kwenda mbinguni
wanawazuia kwa kuwapa injili yenye uongo au kweli
iliyochanganywa na uongo na kuwafanya wanaohubiriwa
uongo kufanyika wanafiki pia bila wao kupenda wala kujua na
ikaja kusababisha watu wengi wakataliwe na YESU na siku ya
hukumu waelezwe siwajui siwajui tokeni hapa nyie mlio
waovu. Haijalishi walijitunza wasifanye dhambi ila kwa dhambi
hii ya unafiki ya kumchukia YESU kwa kulifuata neno la uongo
na yeye atakukataa kwa sababu YESU ni wa haki hivyo basi ni
bora ufuate NENO lake la kweli kuanzia sasa na utubu na
kumaanisha uache dhambi ikiwemo ya kumchukia YESU kwa
kuwatoza watu pesa. Napenda muelewe watu wote wa mataifa
yote, ujumbe huu ni yeye mwenyewe YESU anayewapenda
watu wote ndio aliyenieleza niwaeleze, atakaye tii atapona
atakayekataa ataangamia. Hao watumishi wote wanaowatoza
pesa watu, hawampendi YESU bali wanampenda shetani, kwa
sababu kuwatoza watu pesa siyo NENO lake YESU, bali
imeandikwa mmepewa bure, toa bure sasa anayempenda YESU
na yeye ataombea watu bure maana ndilo NENO lake.

 Anayejiita YESU yeye ni adui mkubwa wa YESU hapa duniani.

 Anayejiita MUNGU, hivyo hivyo na yeye amemchukia MUNGU
kabisa na hata hao anaowaongoza na wao wanaendelea na
hiyo roho ya Jehanamu pasipokujua na wengine kwa kujua.

 Anayebatiza tofauti na YESU anakuwa anamchukia YESU.

 Wapo wanaobatiza sasa hivi kwa ubatizo wa online, hawa watu
wanamchukia YESU kabisa kwa sababu hayo yote siyo maneno
ya YESU.

ANGALIZO: 
Nimeeleza kwa kifupi ili upate kuelewa jinsi dunia ilivyopotoshwa
na wanafiki wakitumia jina la YESU kwa midomo yao kwa nje bali
ndani ya mioyo yao ni wanafiki. Na jinsi ya kujitambua upo kwenye kundi gani, jichunguze kimatendo katika utumishi wako, je ni maneno ya YESU unachanganya na uongo? Basi ujielewe sasa, wapo waliofuata makundi ya kinafiki, na hata YESU kipindi kile alisema “enyi wanafiki wakubwa” na hata sasa bila kuficha injili ya wizi na unafiki imeota mizizi na ukisema ukweli wewe ambaye
unamtumikia YESU kwa kukataa mambo ya kinafiki utachukiwa,
utatengwa, mimi nawatia moyo, msiogope, songeni mbele, mbele ni pazuri ila wale wanaoendelea na unafiki na wao ile siku ya mwisho mbingu itawajibu majibu yao ya kweli.

PROPHET HEBRON.