Pages

Friday, September 13, 2019


HAYA NDIYO MAJIBU YA MASWALI YAKO, KWA NINI BAADHI YA WACHUNGAJI WANAWAOMBEA WATU KWA KUWA TOZA PESA?

BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote, ni muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia maswali mengi katika fahamu za watu wengi wakijiuliza na wengine kushangaa kwa nini watu wanaohitaji msaada wa maombi kwa kupitia watumishi wanaotumia jina la YESU kuwadai watu pesa kwanza tena wakisema bila aibu wala hofu ya kumwogopa MUNGU.

Kwanza kabisa napenda muelewe MUNGU siyo kigeugeu na yeye habadiliki na NENO lake hataki libadilishwe kabisa kwa sababu NENO lake linapobadilishwa tayari mnakuwa mnabadilishiwa Mungu bila kujua au kwa kujua na ndipo ile siku ya mwisho watu wengi wanajiona ni wafuasi wa YESU na kumbe ni wanyang’anyi na watakataliwa wote na hata sasa muelewe kila mchungaji anaye toza watu pesa kwa ajili ya maombi yeye ameshakataliwa na MUNGU kwa sababu akifanya hayo anakuwa anamdharau MUNGU na kumtukana matusi makubwa.

Ukisoma Biblia, YESU alisema atamtuma Roho Mtakatifu aje kulisimamia Neno na kuelekeza Neno lake kama lilivyo. Sasa cha kujiuliza je ni Roho Mtakatifu ndiye analivuruga Neno, jibu ni hapana, basi huyo ni roho mchafu na ndiyo sababu imeandikwa msiziamini kila roho bali zijaribuni kwanza kama ni za MUNGU wa mbinguni. YESU alishaona mbele nini kitakuja kutokea na sasa vimetokea na vitaendelea kutokea ila mwenye akili na afahamu na asikie aelewe ujumbe huu, bali atakayekaza shingo atakutana na hukumu ya milele.

Zijaribuni roho, sasa enyi mataifa jaribu, angalia Neno linavyosema. Soma Mathayo 10:7-8, imeandikwa toa bure, ombea bure, hiyo ndiyo Roho ya MUNGU, sasa kama siyo roho ya MUNGU basi napenda muelewe watu wa MUNGU kwamba mnapokubali kutoa pesa, mnakuwa mnawekewa roho ya shetani badala ya Roho wa MUNGU katika ulimwengu wa roho na imekushikilia mpaka kimwili, sasa badala ya kupata mpenyo au mafanikio (breakthrough) matokeo yake unafungwa zaidi na hali kuwa mbaya zaidi, labda neema ya MUNGU ikupitie ukapata ufahamu, kama sasa unapofunguka ufahamu wako unaposoma habari hii. Na zaidi mchungaji akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu hata siku moja hatawa toza watu pesa kwa sababu Roho huyo anao umoja na YESU na MUNGU na pia jambo lao ni moja tu.

Mchungaji akishaingiwa na pepo lazima atakuwa mnyang’anyi haijalishi atasema kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, na msishangae YESU alishasema watakuja wengi na watatumia jina lake kuwateka watu wengi. Mfano halisi tazama dunia hii wakristo na wasiowakristo baadhi yao kwa idadi kubwa wanavyodaiwa pesa ili waombewe na wanakubali hivyo ndivyo kutekwa na shetani kiroho kwa sababu unapotoa na ukakubali unakuwa umemtii shetani (roho wake) na umemdharau Roho wa MUNGU bila kujua au kwa kupenda.

Nilikuwa ofisini kwangu ghafla akanitokea YESU mbele yangu tarehe 13.09.2019, akaniambia peleka ujumbe huu kwa watu wote, wapo wanangu wananipenda ila wanazidi kutekwa na shetani. Sasa mmepata majibu kamili. Na huo ndio ukweli, tubu na uache. Ila wale wanaotumiwa na shetani watakaza roho wataendelea ila hukumu tayari ipo juu yao au juu yake kila anaye toza watu pesa akitumia jina la YESU, MUNGU hata Roho Mtakatifu.

ANGALIZO:
Utume na kwa wengine ujumbe huu na zaidi unaweza ukausoma kwa lugha yeyote kupitia Internet.

NABII HEBRON WILSON KISAMO.