Pages

Monday, August 12, 2019

NJIA ZIPI ZIMEFANYA KANISA KUWA SOKO NA SIYO KANISA TENA?

(MARKO 12: 38-40)


BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote, natumaini watu wote
wakienda kanisani wanaenda kwa nia ya kumwabudu Mwenyezi MUNGU
na sio kitu kingine. Ila kumekuwa na malalamiko kwa watu wengi waaminifu
na wanaompenda YESU sana kwamba wanaposhiriki ibada kanisani wanajua
wanaenda kukutana na haja za mioyo yao kwa MUNGU kumbe si hivyo.

1. KANISA NI NINI?
Kanisa ni mahali ambapo watu hukutana kumwabudu MUNGU aliyeumba
mbingu na dunia. MUNGU alishaweka njia zake zifuatwe wakati akiabudiwa ili
watu wake wanaposhiriki mahali hapo aipokee ibada hiyo. Lakini napenda
mjue kuwa neno KANISA hata shetani hulitumia na kufanya ibada zake, na
kama unasoma Biblia utaona kwamba YESU alisema nitalivunja hekalu hili na
kulijenga baada ya siku tatu. Kanisa alilolivunja YESU ni la shetani au la
miungu (the gods) hii ni kwa sababu aliona jinsi watu wanavyopotoshwa na
kuzidi kuangamia, na ndio sababu alisema wengi watakuja kwa kutumia jina
lake na watawapoteza wengi kama ilivyo sasa.

YESU aliingia kanisani (soma Marko 11:15), alikuta kanisa limekuwa siyo
kanisa tena bali limekuwa soko na kama lilikuwa ni soko basi siyo nyumba
yake wala mahali pake na kama MUNGU akiondoka mahali, miungu, mapepo,
mizimu na mapokeo ya wanadamu huja kukaa hapo na kutawala. Hapa ndipo
watu wakiendelea kushiriki ibada sehemu kama hizo wanaharibikiwa kwa
sababu kazi ya adui ni kuharibu wanadamu.

2. AINA ZA MAKANISA
Zipo aina nyingi za makanisa ila nitaelezea kwa ufupi haya yafuatayo;
 Kanisa la YESU;
 Kanisa la Mpinga kristo;
 Kanisa la Dini;
 Kanisa la Freemason;
 Kanisa la Shetani;
 Kanisa la Mizimu;
 Kanisa la Familia na mengineyo.

Makanisa mengi yanatumia Biblia na jina la YESU ila yapo yanayofuata ukweli
wa Neno bila kuchanganya na uongo na yapo yanayolitumia jina la YESU lakini
yanaongozwa na freemason, mizimu, shetani, nk. Jinsi ya kuelewa usalama
wako ni kulifuatilia neno lilivyo na kujaribu roho inayotenda kazi mahali hapo
au kwa huyo kuhani kiongozi.

Neno freemason watu wengi hawajui undani wake wanadhani ni mpaka
uende ukajisajili kimwili, la hasha (si hivyo). Tambua kwamba kila roho
inayompinga YESU hiyo ni roho ya freemason. Roho za freemason zinafanya
kazi na zimejiingiza katika kanisa ila watu hawajui na wala hawazijaribu ni
roho gani hizo. Zijaribu kwa kulinganisha na NENO kwanza; kwa mfano
imeandikwa; "nimekupa bure, toa bure" sasa kwa nini utozwe pesa wakati
mwenye kanisa ambaye ni YESU amekataa? Mtumishi unapowatoza watu pesa
za maombezi, hapo tayari umeshajiunga na freemason katika ulimwengu wa
roho bila kujua, japo wapo wengi zaidi wanalijua hilo. Unapotoa pesa ili
uombewe, kwa kujua au bila kujua na wewe unakuwa umeunganishwa na
freemason katika ulimwengu wa roho.

YESU ameniambia niwaeleze watoto wake kwamba shetani anawatega watu
kwa mitego mingi na mtego mkubwa anaotumia ni kwa njia ya utoaji, kwa
sababu sadaka inanena. Sadaka inanena pia kwa miungu, pale unapoitolea,
unajengewa madhabahu ya aina ulipoitolea.

Pia ubatizo wowote wa uongo; unapokuwa unabatizwa tofauti na YESU
alivyobatizwa, uelewe mtu huyo afanyaye hivyo anakuwa anatawaliwa na
freemason, hata kama utakataa ukweli unabaki pale pale. Yapo mengi sana ila
nitaelezea kwa ufupi ili upone na mwisho wa siku MUNGU akatukuzwe. YESU
aliyakataa yote hayo ila kwa sasa yamejaa.

Kumwabudu mchungaji kama yeye ndiye MUNGU au anajiita YESU, hapo
mtumishi tayari unakuwa umeshakuwa freemason kiroho na ndiyo maana
hiyo roho ya kujifananisha na MUNGU humvaa juu yake na waumini wote
wanavaliwa na hiyo roho ya freemason, hivyo kazi ni wewe kujifanyia
tathmini na ujichunguze. Mimi naandika anavyonieleza YESU au kwa dini
nyingine wanamuita Nabii Issa.

ANGALIZO: Freemason inawapiga upofu watu wengi hasa wakristo na hiyo
roho imejiingiza ikaweka mizizi kabisa na ndio sababu imefika mahali sasa
manabii, wachungaji, mitume, wainjilisti, maaskofu hawana majibu ya nchi
zao wala majibu ya watu wanaowatumikia. Wamebaki watumishi wachache
sana wenye roho ya MUNGU wa kweli tena ni wakutafuta sana. Kumbuka
kipindi cha Eliya na mabaali, na sasa ndio hivyo hivyo. Viongozi wa kiroho
wakiwa vipofu wanawatumbukiza watu na taifa katika shimo. Na kama taifa
limeshauriwa na kuongozwa na viongozi wa kiroho vipofu hutumbukizwa
katika balaa au shimo la giza. Yapo makanisa mengi ila YESU alilijenga kanisa moja tu, haya mengine yametokea wapi na nani kayaleta?

3. KWA NINI BAADHI YA MAKANISA YAMEKUWA NI SOKO? NA KWA NINI
BAADHI YA WATUMISHI WA INJILI SIYO WATUMISHI BALI WAMEKUWA
MABWANA SOKO?

Maneno haya aliyasema YESU miaka 2000 iliyopita na sasa mnaona
udhihirisho, yanatimia. Ni vibaya sana mtu anaamini anaenda kanisani lakini
mahali anapoenda kumbe ni sokoni na Biblia inatumiwa mahali hapo.
Wanaimba, wanatoa sadaka na wanabatiza kwa kulitumia jina la YESU, Roho
Mtakatifu na hata kumtaja MUNGU kabisa.

Jambo la kwanza makanisa mengi hayaongozwi na wachungaji bali
yanaongozwa na mabwana soko japo wamevaa vazi la uchungaji kwa njia ile
ya kwamba ndani ya mioyo yao ni mbwa mwitu na Biblia inasema utawajua
kwa matendo yao ya kuwa ni mbwa mwitu kwa sababu ya kulibadilisha Neno
na kulichanganya na uongo. Kwa mfano, imeandikwa nyumba ya sala siyo
soko, ndio sababu YESU alikuja kanisani akayafukuza ili kanisa libakie kuwa
kanisa. Ila imekuwa ni kinyume kwa sasa katika baadhi ya sehemu duniani.
Kama nilivyoelezea mwanzoni, Kanisa ni mahali ambapo watu hukutana
kumwabudu MUNGU aliyeumba mbingu na dunia, basi angalia usije ukakaa
katika kanisa ambalo shetani anataka liwe kwa jinsi yake. Imefika mahali jina
la YESU linatukanwa kwa sababu ya mabwana soko wanaotumia Biblia
kunyang'anya watu kwa kutumia jina la YESU na kusema uongo. Kwa mfano:
Nabii, Mtume, Mchungaji, Askofu na wengine wote iwe kwenye facebook hata
kama anatabiri na kukwambia mambo yako ili mradi tu mwishoni utoe sadaka

umtumie ndio akuombee, napenda kuwajulisha kwamba hao ni maadui
wakubwa wa MUNGU, BWANA YESU NA MALAIKA. Hao ni marafiki wa shetani
na tena ndio hao mabwana soko na ili wafanikiwe huduma zao za kipepo
masharti ni lazima wafanye hivyo na unaposhiriki tu kutoa ili uombewe kwa
kupitia hiyo sadaka yako unaunganishwa katika ufalme wa freemason. Lakini
ili wakupate, wanapewa ujanja wa miujiza ya kishetani, kumbuka pia kipindi
cha Musa pale kwa Farao na yeye wachawi wake walifanya miujiza. Ila kwa
sasa miujiza inawafanya watu watekwe zaidi na shetani, miujiza ya YESU ipo
ila hainunuliwi, miujiza ya YESU anatoa bure ila ya miungu ni lazima ununue.
Unaweza ukadhani unamfanyia MUNGU kumbe unafanyia miungu na kwa njia
hiyo miungu hununua maisha yako.

Mtu akipenda kumtolea MUNGU hairuhusiwi mtumishi yeyote kukupangia
kiasi, sadaka ni ibada yako na MUNGU. Inapokuwa unapewa risiti au
unaandikwa jina au unasifiwa madhabahuni kwamba umetoa sana au bwana
soko asimame aanze kufanya mnada, kwa mfano siku hizi ibada nyingi naziita
ni Sunday Markets na siyo Sunday Church kwa sababu bwana soko ataanza
kusema kwa mfano mwenye $5000 usimame uje mbele na ukitoa
unaombewa, anashuka labda milioni, hivyo hivyo yule asiye na kitu anarudi
nyumbani kama alivyokuja (mtupu) na hizi ndizo Sunday Markets, hata
uliyetoa uelewe umetupa tu chini hakuna lolote na hata mambo yako
yanaharibika kabisa unabakia unajiuliza shida ni nini, sababu freemason
ameipeleka pesa yako kwenye ufalme wake au kwa mganga wa kienyeji
pasipo wewe kujua.

Sasa mataifa muelewe kwamba YESU anawapenda sana na ndio sababu
kanieleza niwaeleze mambo haya na yatawasaidia wengi na mtapona na kama
mtayakataa hayo na kuyapinga bila uoga wala aibu ili mponye nafsi zenu.
Usiende tena sokoni bali nenda kanisani na kama hujui kama hapo ulipo ni
sokoni omba MUNGU atakuongoza sababu yeye anakupenda na hapendi roho
yako iangamie, zaidi utubu na sema, BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa
milele na ulitoe jina langu kwenye kitabu cha uzima wa maroho ya jehanamu
Amen.

Ingia kwenye website www.prophethebron.or.tz , subscribe kwenye YouTube
utakuta masomo mengi zaidi.

PROPHET HEBRON.