BANGI
YA KIROHO
Shalom!
Katika makala hii ya leo nimeamua kufichua mipango ya
shetani aliyoipanga ili kuwaharibu wanadamu wamfuate yeye. Katika makala hii
itaelezea kuhusu kilevi kibaya
kinachoitwa bangi, siyo neno geni japo ina majina mengi ikiwemo marijuana.
Mmea huu asili yake ni kuzimu ila inapatikana kimwili pia hapa duniani, na pia
inapatikana kiroho, ninaposema kiroho ina maana kuwa haionekani kimwili na kama
haionekani kimwili basi inasambazwa kiroho na roho za giza. Bangi ni kilevi
ambacho mtu anapokivuta kinamwongoza kufanya jambo ambalo halijatoka katika
akili yake, mfano utakuta mtu akitaka kulima basi anavuta bangi kwa ajili ya
kulia na bangi inamtuma hivyo hivyo au kuiba na inamtuma hivyo hivyo na anakuwa
hana aibu kabisa sababu tayari anakuwa ametawaliwa na nguvu ya bangi katika
ufahamu na kumwendesha kama bangi itakavyo mpaka pale iishe kichwani mwake, ila
madhara yake inampumbaza huyo mtumiaji
au baadaye kufanya awe kichaa yaani akili zinamruka mfano anasahau ovyo au
anaropoka ropoka ovyo au ugomvi au hata kufanya mtu maisha yake yaharibike na
kuangamia hivyo, kilevi hiki ni hatari sana kimwili.
Mimi ni kiongozi wa kiroho, nimeongelea kimwili ila sasa
naongelea kiroho ndio sababu nasema bangi ya kiroho na kwa nini imeletwa bangi
ya kiroho na shetani. Imeletwa ili kuwavutisha watu wanaomfuata MUNGU kiroho
pasipokujua au kujua ili kumvuruga mtu ufahamu wake uende tofauti na mtu
anavyotakiwa ampende MUNGU au asome biblia aelewe kama ilivyo lakini inakuwa ni
shida kubwa katika ulimwengu wote kiasi kwamba mwanadamu hamuelewi aliyemwumba wala kumtii wala kuwa na hofu ya
MUNGU ikiwa kwenye makanisa baadhi mpaka waumini wake.
Nitaelezea kwa ufupi kuhusu hii bangi ya kiroho unawezaje
kuvutishwa , unapoona unaota unavuta sigara ya aina yeyote katika ndoto uelewe
hiyo ndiyo bangi ya kiroho na unaweza ukaona unavuta mwenyewe lakini katika
ulimwengu wa roho wamekupa kabisa na ukakubali kuvuta, unapovutishwa linakuwepo
lango la kukuharibu kiroho endapo wameshindwa kimwili, wachawi pia hutumia njia
hiyo kuvuruga watu ufahamu mfano wanakujua labda una mipango mizuri au una
akili au una hekima sasa ili wakuvuruge wanakutumia mapepo bangi au jini bangi
sawa sawa na level ya kukuvuruga. Na zaidi uelewe jinsi mtu hapa duniani na
maisha yake na tabia zake, hata umaskini au utajiri ndivyo alivyo katika
ulimwengu wa roho, inaanza kwanza kiroho
ndipo kuja kimwili, na ndiyo sababu YESU akasema mwenende katika roho na
kweli, hata kumwabudu MUNGU inatakiwa katika roho na siyo kimwili; kiroho na
utakatifu na kweli, siyo kiroho halafu neno linachanganywa na uongo, inapokuwa
hivyo tu uelewe bangi ya kiroho kavutishwa mtumishi na akishavutishwa basi neno litapelekwa na ufahamu wa bangi na
inapokuwa hivyo tu basi linakuwa siyo neno takatifu la kweli na wote
wanaolifuata neno hilo tayari na wao wanakuwa wanaendeshwa na pepo bangi,
sababu hata neno linasema jinsi alivyo kuhani ndivyo na picha ya kanisa
lilivyo.
Njia nyingine ambayo malango ya kuzimu hutumia kuwatumikisha
watu bangi ya kiroho hutuma moshi wake na kuchafua hali ya hewa unaweza
ukajikuta unapiga chafya bila sababu au unawashwa macho tena mara nyingine
utayasugua mpaka yawe mekundu japo mnielewe zipo sababu nyingine za kukufanya
upige chafya mfano vumbi na kadhalika. Bangi hii ina majina mengi wengine
wanaiita dope, shada, sigara ya bob marley, sigara kubwa, kila nchi ina jina
lake, ila tuendelee kiroho. Bangi hii wapo watumishi baadhi wanavuta kabisa
kimwili ili waweze kuhubiri sawa sawa na bangi inavyowatuma kulihubiri neno la
MUNGU bila uoga wala hofu na ndipo jina la YESU kutumika vibaya.
Bangi ya pili ya kiroho ni anavutishwa mtumishi kiroho pale
ambapo atajiunga na upande wa shetani au kawa freemason ni lazima avutishwe
kabisa ili akili yake ianze kuendeshwa na pepo bangi (hili ni pepo dogo aina ya
bangi au jini bangi hili ni jini lenye roho ya bangi ndilo lina uendesha
ufahamu wake yeye anayesaini mikataba ya shetani au kwa waganga au kujiita na
hajaitwa na MUNGU. Napenda mjiulize maswali watu wote ni kwa nini mtumihi
anasoma biblia kama kitabu cha
kuwaongoza yeye aongoze yale yalioandikwa
lakini yeye hayafuati? Mfano biblia inasema mtu aombewe bure lakini cha
ajabu asilimia kubwa ya watu wanadaiwa pesa za maombezi tena kwa viwango vikubwa na vidogo siri mmeijua
wanavutishwa bangi za kiroho, aibu inaondoka na anakuwa haoni aibu kwa wanadamu
na kwa kile anachokifanya na zaidi usiku kabla hajaenda kwenye hayo maombi au
ibada yake huwa wanatuma mapepo bangi au majini kwa watu kuwapeleka katika
kanisa hizo bila kupenda wala kujua sababu ufahamu unamtuma aende pale pale hata
umwambie ni pa shetani hawezi kukuelewa mpaka siku pepo bangi litoke katika
ufahamu na akili ndio mtu ajitambue na aanze kujuta sababu ufahamu umekuwa
huru.
Nimeelezea bangi mtu anapovuta hutawala akili na kumpeleka kama bangi
inavyotaka, sasa haya mapepo bangi ukishatumiwa yatakuongoza kutii kila ujinga
atakaosema mchungaji na utatii, hata wacha gari lako utaliacha, hata kakope
benki pesa zote unipe na utampa na matokeo yake unakuwa umeibiwa na wala
haujamtolea MUNGU bali ni ufalme wa shetani. Ukisoma biblia soma kuhusu ubatizo
aliouleta YESU wa maji mengi sasa inakuwaje waasisi baadhi wakabadilisha neno
la mwenyezi MUNGU, soma Ufunuo 22:18-19. Kweli hizi bangi za kiroho zitawafanya
wengi wachomwe moto siku ile ya mwisho kwa kujua na kutokujua. Imeandikwa usiabudu
sanamu mbona duniani watu wengi wanaabudu sanamu tena kwa ujasiri bila kumhofu
MUNGU? YESU yupo njiani kurudi watu
wengi wanavutishwa bangi ya kiroho inawaendesha wamkatae mwokozi. Jiulize iweje
umkatae aliyekuumba na ubakie na asiyekuumba yaani shetani ambaye anasubiria
kuchomwa moto jehenamu, kila mtu anayempenda YESU aokoke, ukristo bila wokovu
ni bure wala sikukuu ya krismasi wala pasaka haitakupeleka mbinguni, mbinguni
unakipangia sasa hivi na siyo ukifa, hata sala za makaburini hazisaidii, wewe
ndie unayejipangia pa kwenda na siyo mpaka uwe mzoga. MUNGU yeye siyo wa wafu
ila bangi ya kiroho inawatuma watu fahamu zao kuwa ukifa utaombewa na
utasamehewa, soma biblia hakuna toba ya maiti au mzoga. Umepewa uzima yaani
uhai na mwenyezi MUNGU umpende ukiwa na uhai, muda atakapoutoa uhai anakuwa
anajua kabisa huyu ni wangu au siyo. Sasa hizo ibada hazimsaidii lolote
aliyekufa, sasa hata kama angemezwa na mamba ni lazima ile siku ya mwisho
atafufuka ajibu kwa BWANA. Miaka mitatu
iliyopita YESU alikuwa akinieleza mambo fulani limoja lilikuwa anasema waeleze
watu ukweli kuhusu mimi sababu mimi ndiye njia ya kweli, kuanzia neno lake sasa
unakuwa mkristo kwa kuangamizwa bila kujua wala kupenda kwa ajili ya kuamrishwa
uongo, elimu ya uongo mfano hairihusiwi watu kubatizwa kwenye beseni, visima,
haijalishi ni maji mengi bado utakuwa ni feki huo ubatizo. Hivyo mataifa yote
ni wakati wa kujitenga na bangi ya kiroho ili isikupeleke pabaya, unayo akili
kabisa unajua kusoma lakini katika neno utaamrishwa kutoa pesa ili uoate huduma
ya kiroho, napenda muelewe haya mambo ya kiroho yapo ya aina mbili:
1.
Kiroho katika utakatifu na kweli, hapa ndipo pa
YESU kiimani na matendo.
2.
Kiroho katika utakatifu na uongo hapa ndipo pa
shetani na mpinga kristo- hapo roho ifanyayo kazi ni lazima ulipe tena
litatajwa jina la YESU kutumika kuwaibia watu mali zao au kanisa kufanyika
nyumba ya biashara na wanyanganyi, unapumbazwa tena unaweza ukavutwa kutoka
nchi yako ukavutishwa hiyo bangi ya kiroho ukasafiri maelfu ya kilomita kwenda
kuonana na mtumishi na utashangaa unarudi hauna mabadiliko wakati mwingine
nitaeleza zaidi kuhusu hii bangi ya kiroho mambo mengi kwa kipindi hiki katika
sehemu baadhi za ncho zote ni mbaya kwa jinsi jina la YESU linavyotumika siyo
kwa waliosomea theologia wala ambao hawajasomea, tena asilimia kubwa theologia inaficha ukweli ni laana, roho mtakatifu
yeye hana mipaka ya kusema ukweli, yeye ni mwalimu mzuri kuliko vyuo vyovyote
na ndio sababu YESU alimtuma roho aje asaidie na kutuongoza, sasa baadhi ya
theologia zimeleta mapokeo ya wanadamu.
Napenda uelewe muelewe kila imani ina theologia yake
wanaoabudu ngombe, majini, watu, mzimu na nyinginezo utaona na zote zimemsema
MUNGU lakini cha ajabu biblia inasema pitia YESU ndio utafika mbinguni,
theologia nyingine ni ya kuwapeleka watu jehanamu. Na kama ukimkuta mkristo amesomea theologia halafu
amefundisha uongo, ubatizo wa uongo, chaji watu pesa, unyanganyi, au ametumia
uchawi, hivi hamuoni zitakuwa ni theologia za mipango ya wanadamu ya kumpinga
MUNGU? Neno linasema siku ile ya mwisho wengi wataambiwa sikujui ni sababu moja
wapo, ni bangi za kiroho zinaendesha watu tofauti na mpango wa MUNGU. Imefika mahali
baadhi ya watu wanajiita YESU jamani jiulize amezaliwa na Maria? Yeye alikufa
na kufufuka? Amefanya nini hapa duniani wakati tunajua YESU akirudi kwa miguu
yake nyota zitaanguka, milima itashuka na mengineyo, huyo anayejiita YESU mtu
huyo bangi ya kiroho ndio imemtuma hivyo na hata wanaomwamini huwaga wanavutishwa
katika ndoto fahamu zao zimeanza kumwona ndiye YESU, shtukeni na mkatae uongo,
naamini watu wengi watakaposoma ujumbe huu hiyo bangi kama ulivutishwa ukuachie
kwa jina la YESU.
Alisema YESU watu wengi watalitumia jina langu kusema ni
mimi nimewaita kumbe hawajatumwa na YESU na cha kujiuliza ni mtumishi ametumwa na
YESU muombee watu mwachaji watu pesa za kuombewa? Ndio hao wavuta bangi za
kiroho je mmetumwa mkawabatize watu
kwenye visima, vikombe, madrum kwa majina yenu? Wacheni kumsingizia YESU. Jambo
lingine, theolojia baadhi ni roho mtakatifu au YESU kasema watu wasitubu
wasubiri wafe? Wataombewa waende mbinguni. Wengine kulipindua neno la MUNGU je
ndio theolojia ya mbinguni? Mtu akisoma theolojia anajifunza kuongoza watu
waende mbinguni kikweli lakini kwa kiwango kikubwa hata hizi theolojia nyingi
ni za kumpinga MUNGU na kulibadilisha neno lake. Zipo theolojia za kujisomea
ili upate kazi na mshahara kuishi. Napenda kusema ukweli, kusoma theolojia siyo
kuitwa na MUNGU au ukafikiria MUNGU anakutambua na cheti chako cha theolojia,
kazi ya MUNGU ni wito tena akupe yeye, maana unaweza ukapewa wito na freemason
au wachawi au dini na ndipo penye shida hata watumishi wa MUNGU wenye wito wa
kweli mnalijua hili tatizo baadhi mnanyamaza hamsemi ukweli madhara ni ile siku
ya mwisho mtaulizwa na BWANA.
Mnaona mtaonajwe na baadhi ya watu, au taifa lako BWANA na
yeye atakuonea haya (aibu mbele ya baba yake siku ile ya mwisho) ukweli
haisemwi sehemu nyingi sababu ya wito wa kuigiza giza, na ukweli ni nuru
inangaa katika giza, ni ajabu sana hata serikali baadhi duniani zinafanya kazi
kiuaminifu kwa kufuata sheria zake kuliko kanisa, ukitaka uovu upo kanisani,
uwizi, uchawi, kubadilisha neno la MUNGU kanisani, unyanganyi na mambo mengine
mengi tena bila hofu wala uoga katika
sehemu baadhi za makanisa na baadhi ya
watumishi. Nyie watumishi mlioamua kusema kweli endeleeni mnamfurahisha MUNGU
na anawapenda msikate tamaa sababu ya idadi kubwa imejiunga na shetani au
mpinga kristo. Ukifanya mtihani ya biblia uulize baadhi ya wanatheolojia
watafeli, swali la kwanza je YESU aliagiza tubatizwaje? Imeandikwa wapi watoto
wabatizwe? Imeandikwa wapi harambee zifanyike kanisani? Imeandikwa wapi mnada
ufanyike kanisani? Imeandikwa wapi ujiite YESU au MUNGU? Imeandikwa wapi uombee
watu kwa kuchaji pesa? Usiabudu vitu au sanamu na mengineyo mengi.
Na wapo hata watumishi ambao waliitwa au kutumwa na MUNGU,
waliacha kumsikiliza MUNGU, walivutishwa bangi ya kiroho na ndipo utaona
mhubiri amebadilika ameingia katika uongo japo ameendelea. Na pia kila mtu
duniani anayeenda kwa waganga kufanya uchawi ni lazima kabla ya kwenda awe
anajijua au hajijui atavutishwa katika ndoto au hewa chafu na fikira zake
zitabadilika ataacha kumtegemea MUNGU, afuate kulaaniwa na MUNGU, ukishiriki
ushirikina unalaaniwa na MUNGU na kila mchawi aelewe anayolaana ya MUNGU, tubu
na kuacha.
Wapo wanaofundisha watu kuchimbia biblia kuzika neno,
usishangae ni bangi ya kiroho ya upande unayomtumikisha ndiyo inayofanya kazi. Hata
sadaka kikapu cha mama mchungaji hayo yote ni lazima avutishwe na mapepo katika
roho halafu yanamtuma afanye hivyo ili aishi, na ikiwa ni hivyo hiyo huduma
haina mwelekeo wa kupeleka watu mbinguni ila utaijua kwa matendo yake.
Bangi ya kiroho imefanya watumishi wasiwe na aibu wala hofu
ya MUNGU wakifikiria waumini hawaelewi wanadanganywa. Naikemea hii bangi ya
kiroho na nguvu zake isifanye kazi kwako na kwa wengine kumchafua MUNGU. Zijaribuni
kila roho kiimani na kimatendo yapo makanisa yanamfuata MUNGU kweli, wapo
watumishi wanaomfuata MUNGU kweli, hivyo hivyo yapo makanisa yanayotumia jina
la YESU lakini ni kujifichia wanatumia nguvu za giza wapo na watumishi ambae walimwacha
MUNGU wakajiunga na hao waliojiingiza katika mkataba ya kuuwa watu kiroho bali
wamejionyesha linawajenga watu kiroho waende mbinguni lakini ni kinyume, mwenye
akili na aelewe.
Huu ni wakati wa mwisho ni heri kutubu na kuacha urejee kwa
YESU kabla siku zile mbaya hazijaja. Maneno haya yametoka mbinguni utakaye yapinga
ubarikiwe, utakayekubali ubarikiwe. Kilio kinakuja cha hukumu. Sema BWANA YESU
naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniondolee roho ya bangi katika fikra na
moyo katika ulimwengu wa roho na mwili ili nisiamini uongo na akili yangu kutumikishwa
na adui. Asante BWANA YESU najitenga na pepo bangi, jini, miungu na nguvu zake
za kiroho, sasa na hata milele, Amen.
PROPHET
HEBRON.