JE UMEOKOKA?
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KWA NINI MUNGU ANATAKA KILA MTU AOKOKE?
BWANA YESU ASIFIWE watu wa MUNGU, kwa mataifa yote. Popote ulipo wewe ni mtu wa MUNGU na amekuumba MUNGU mwenyewe na yeye ndiye anayetaka uokoke katika dunia hii. Neno KUOKOKA lilikuja hapa duniani lilitokea Mbinguni. MUNGUalimtuma mwanae wa pekee ambaye ndiye YESU aje hapa ulimwenguni na MUNGU akafanya njia ya kuwa YESU ndiye mwanae aliyemchagua aje afanyike WOKOVU kwa wale watakaompokea na kumwamini na kuacha maovu yaliyopo hapa ulimwenguni ambayo yanaletwa na adui ili ufuate yale ya Mbinguni.
a. NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA maana yake ni kukata VISA (kibali) ya kwenda Mbinguni alipo YESU, au kumkiri awe BWANA na mwokozi wako, pamoja na kuacha matendo maovu na kuishi katika utakatifu, au kukubali kumkiri YESU kwa kinywa chako na kufuata nyayo zake kama anavyotaka MUNGU Mbinguni ndipo aone umeikubali VISA yake. Hata hapa duniani ukitaka kwenda nchi fulani mfano unataka VISA ya kwenda UK ni lazima uitafute na ukiipata ndipo utaweza kuruhusiwa kwenda huko. Ukiwa na hiyo VISA ndipo hata wanaokata tiketi za ndege watakupa tiketi, wasipoiona hiyo VISA watakwambia nenda katafute mpaka uipate na ukikosa hata hiyo tiketi hawatakukatia kwa sababu wanajua hawaruhusiwi kumkatia mtu tiketi ambaye hajakubaliwa na nchi hiyo. Huu ni mfano wa wanaokwenda Mbinguni, Mbinguni ni nchi ambayo anaishi MUNGU na Malaika wake na ndipo mahali tunapotakiwa kila mtu kwenda kwa yule tu atakayependa kwenda Mbinguni.
b. NINI MAANA YA KUTO KUOKOKA (MATHAYO 23: 13-24)
Jambo hili si geni tena ni ajabu hata mtu mwingine anapozungumza kwa ujasiri bila kujua anajiangamiza nafsi yake kwa kujua au kutokujua, ikimaanisha yeye haendi Mbinguni. Hiyo ndiyo maana halisi kwa mtu pale anaposema mimi sitaki kuokoka au siokoki. Natumaini mataifa yote mmepata maana yake. Haijalishi unasema unaenda Mbinguni, utabakia kusema tu lakini hautakwenda kwa sababu bado hauna VISA ya Mbinguni, bali unayo VISA ya Jehanamu kwa kujua au kutokujua. Haijalishi unajiita ni mkristo na ni mfuasi wa YESU na dini yako. Kumbuka hata YESU aliposema hiki ni kipindi cha wokovu kuwadia alipokuwa madhabahuni YESU alifukuzwa na kutukanwa kwa sababu wale waliopo katika dini walikuwa na VISA za jehanamu katika ulimwengu wa roho japo kimwili waliona wapo salama soma Isaya 61.
Nimatumaini yangu watu wengi watafunguka na kukubali wokovu na wasiache tena bila kupokea wokovu, kwa sababu siku si nyingi BWANA YESU anarudi atawachukua wale wenye VISA tu za Mbinguni, VISA hizo za kiroho hazionekani katika mwili bali ni katika roho na YESU anazijua na anamjua aliyemkubali hapa ulimwenguni na humwandika jina lake Mbinguni. Hivyo nawasihi sana,upo moto ulioandaliwa wa kuwachoma watu wote ambao watakuwa hawajaokoka yaani hawajampokea YESU, iwe umekufa kabla ya kiama au utabahatika kuwepo mpaka ile siku ya mwisho, hautaenda,utabakia ukiteseka hapa na ndipo utalia machozi ya ajabu. Ni bora uokoke sasa. Nimesema siwezi kunyamaza huku nikijua ukweli na kitakachowapata wanadamu wakati wa mwisho. Na cha ajabu baadhi ya makanisa sehemu mbali mbali yanayoitwa kwa jina la YESU yamekuwa yakikataza watu wasiokoke na mtu aliye okoka humchukia au hata kumtenga na kumwona amepotea. Nakutia moyo, haujapotea, bali umepotea katika safari yao ya kwenda jehanamu, hakika haupo nao tena kiroho bali wewe unaelekea Mbinguni.
Na cha ajabu watu wengi wanapenda sana kuishi na VISA za jehanamu, yaani maisha bila wokovu. Huu ni wakati wa neema, itafika kipindi utajuta na kusaga meno wala hii VISA hutaipata tena ya kwenda Mbinguni, wakati ni sasa. Na endapo utazuiliwa kuokoka na mtumishi yeyote Yule, sasa umeshaelewa yeye ni wakala wa jehanamu na ndani yake ipo roho ya kuwakataza watu wasiende Mbinguni. Watumishi wa namna hiyo mtubu na kuacha tabia hiyo, moto unawasubiri, na zaidi mrejeeni YESU. Haiwezekani umtumikie YESU kuongoza kondoo, halafu unawakataza kuokoka, mnawazuia wasiende Mbinguni wakati nyie wenyewe hamwendi.
BWANA YESU ameniambia atapambana na nyie ajuavyo yeye, wewe ona ni maneno tu haya ninayokueleza. YESU anahasira sana juu ya watu wanaowazuia watu wasiende Mbinguni na kuwafanya kondoo wa jehanamu na siyo kondoo wa kwenda Mbinguni. Jiulize sasa upo tayari kupokea VISA ya kwenda Mbinguni na kuiacha VISA ya jehanamu. Okoka sasa, sema, BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu kwenyekitabu chako cha uzima wa milele naichoma VISA ya jehanamu, naipokea VISA ya Mbinguni. Naomba Roho wako aniongoze salama katika utakatifu na mengineyo, Amen.
ANGALIZO:
Zaidi fuatilia masomo katika blog hii ya Prophet Hebron na YouTube. MUNGU awalinde, awaokoe, nyakati hizi ni za mwisho yu njiani anakuja usiseme kesho kesho bado unafikiria kuendelea kushika VISAya jehanamu, kataa sasa.
Nawatakia baraka za ushindi wa kuokoka na siku moja twende Mbinguni. Je uko tayari kuchoma VISA ya kwenda jehanamu na usiseme tena kuwa mimi siokoki, na unaposema kwamba hauokoki ina maana kuwa unamwambia MUNGU huhitaji kwenda Mbinguni hiyo ndiyo maana yake. Kwa hiyo usije ukamcheka au kumdharau mtu ambaye tayari ameokoka, yeye anaakili, amepata neema ya kujua ukweli. Na zaidi mtu haendi Mbinguni kwa kusema naenda Mbinguni au kwa kuimba, MUNGU anaangalia tendo la kumpokea YESU. Lakini kumbukeni pia shetani ana mbingu yake na mbingu hiyo watu huenda bila kuokoka kwa kujua au kutokujua. YESU amekuwa akinisisitiza sana niwaeleze mumpokee, yeye anawapenda na msikate tamaa yupo njiani anarudi. Angalia usije ukawa mmoja wapo, ile mwisho ukaambiwa sikujui sikujui, hata kama ni mkristo hata kama una dini yako, yeye ni YESU wa watu wote, yeye hana dini, yeye hakuleta dini, alizikuta dini na pia dini zilimkataa na sasa zinaendelea kumkataa kwa sababu wamekataa WOKOVU. Kumkataa YESU ni pamoja na kutaja tu jina lake na kuzuia watu wasiokoke.
Ubarikiwe sana na uwe mmoja wa watakaokwenda Mbinguni sasa na siyo mmoja wa watakaochomwa moto.
PROPHET HEBRON
TANZANIA.