Pages

Thursday, January 31, 2019



JE UNAJUA KUWA JINA LA YESU LINAWEZA KUTUMIWA NA WACHAWI NA MIUNGU KUFANYIA KAZI ZAO?

BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, najua watu wengi watashangaa inawezekanaje wachawi, miungu, mizimu walitumie jina la YESU kufanyia kazi zao za giza wakati hawana uhusiano wowote. Kwa watu mnaompenda YESU naye anawapenda sana, napenda kukufunulia haya yaliyofichika. Amenituma mimi Hebron, Nabii wake nikaeneze habari zake za ufalme wa BABA yake MUNGU wa Mbinguni ili kuubomoa ufalme wa shetani bila mipaka kama atakavyo MUNGU mwenyewe na si vinginevyo. Wakati wowote mwanae YESU anarudi kuwachukua wafuasi wake wa kweli. Soma kitabu cha Mathayo 7:20-23.

20Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 21Si kila mtu aniambiaye, BWANA, BWANA, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya BABA yangu aliye mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile, BWANA, BWANA, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Kwa msisitizo soma mstari wa 22. Ile siku ya mwisho, kwa nini wengi wataambiwa sikujui sikujui wakati walikuwa wanatumia jina la YESU? Na YESU anasema sikuwajua ninyi kamwe, yaani tokea waanze kufanya huduma hizo na miujiza. Nitaelezea kwa ufupi ila nimeelezea vizuri zaidi katika ibada, utaangalia YouTube hiyo. Ukirudi nyuma YESU alishasema kuwa watakuja waongo watawapoteza watu wengi zaidi hata wale waliokuwa wateule wangu kwa kupitia jina langu. Vile vile usishangae enzi zake wakati YESU akiwa hapa ulimwenguni akayasema na hata sasa ameniambia niwakumbushe tena watu wote hiki ni kipindi cha neema yake. Napenda ieleweke kwamba hakuna jina kama hili katika dunia hii na popote pale, hili jina ni la ajabu. Linatoa msamaha wa dhambi; hakuna popote pale jina linalosamehe dhambi wala la kukupeleka mbinguni kama jina la YESU; hata majina ya mitume na manabii waliopita na waliopo, wala wafalme bado hawataweza kulifikia, ni jina la pekee kwa utukufu wake mwenyezi MUNGU ili kuwaponya na kuwakomboa wanadamu kutoka katika dhambi. Wanadamu walijua hilo na shetani analijua hilo. Shetani alijua kuwa kila mwanadamu atampenda YESU, sasa akaona atafanyaje ili awateke wanadamu na awapoteze au kuwapiga upofu au kuwapumbaza haraka ili atakapokuja YESU baadhi ya watu wakachomwe moto naye. Ndipo neno linasema siku hiyo wengi watalia na kusaga meno YESU atakavyo waruka wanadamu akiwaambia siwajui kabisa, nyie ni waovu, iwe ni mchungaji, mwinjilisti, mwalimu, askofu, nabii, mwimbaji, muumini na wengineo.

Sasa napenda muelewe kipindi hiki wapo watumishi ambao ni wachawi, freemasons, wengine wanatumia hirizi, wanaofanya matambiko na kufanya maagano ya kishetani au ya mizimu, na utashangaa wanalitaja jina la YESU au kujiita watumishi wa YESU na hata kuongoza watu sala za toba ambazo sala hizo akikuongoza pasipo wewe kujua au kwa kujua kinyume chake inakuwa katika ulimwengu wa roho umeandikwa katika kitabu cha uzima cha mpinga kristo na kwa sala hiyo unakuwa umejifunga kwa maneno yako na kwa kinywa chako. Hivyo nawasihi muwe makini, siyo kila mtu akikuongoza sala ya toba utaandikwa jina lako mbinguni, ni mpaka ameitwa na ametumwa aifanye hiyo kazi na MUNGU wa mbinguni. Ila kwa sasa katika ulimwengu wote mambo yamebadilika, shetani na yeye amejiingiza katika kila kitengo akiwatumia wanadamu ambao baadhi yao wamekubaliana na shetani na wanajua kabisa wanafanya nini na hawa ndio YESU amewaita wamevaa ngozi za kondoo kwa nje ila kwa ndani mioyo yao ni MBWA MWITU.

Nitaelezea kwa ufupi hili jina la YESU, nafikiri mtakuwa mmeshasikia mtu anaenda kwa waganga ili awe mchungaji, nabii, mwalimu, mwimbaji na hata baadhi ya wazee wa kanisa na mengineyo. Sasa wengi mtakua mnajiuliza inakuwaje wanataja jina la YESU na mapepo yanatoka na watu wanapona, wanatabiriwa na mengine mengi na wanasoma biblia na mapepo yanakuwa yanatoka? Hapa sasa naomba unielewe, wanakuwa wanalitumia jina la YESU lisilo na kama siyo lake basi hilo jina linakuwa ni la mpinga kristo. Jina la YESU likitumika na mpinga kristo kwa kawaida halina utukufu wa mbinguni. Hapo anayeenda kwa wachawi anatengenezwa aonekane ni mtumishi wa YESU na kumbe siyo, anawekewa nguvu ya majini na utambuzi, anafanywa awe mganga, kama mganga wa kienyeji anavyoagua au kutibu ila katika ulimwengu wa roho, japo kimwili kwa wale wenye macho ya rohoni ambayo yanaona vizuri humtambua kabisa siyo mtumishi wa kweli bali anatumia nguvu nyingine. Hiyo nguvu nyingine ndiyo hiyo ya giza mfano majini au matambiko kupitia mizimu, na mizimu huwasaidia kuwaletea watu wale wenye mizimu katika ulimwengu wa roho. Ndio maana utaona watu wanaenda mahali kwa wingi hata kama wanajua huyo mtu ni mchawi au ameachwa na MUNGU. Wanachokifanya ile mizimu inapewa vitu vyao inawapeleka watu mahali hapo au majini yanawapumbaza ili wajue hapo walipo ni mahali pa YESU na ni salama na kumbe ni mahali pa kuuliwa kiroho au ni kaburini. Siri hii wanaijua watumishi.

Kwa kifupi, ndio maana utasikia kanisa linachinja wanyama madhabahuni au kufukia biblia, kuzika vitu vya waumini au dhahabu za watu na mengine mengi kinyume na biblia au neon la Mungu. Hayo yanakuwa ni maagano (ni masharti), lazima wafanye kama vile mchawi anavyoelekezwa sheria za kichawi ili afanikiwe na zaidi hawa watumishi huzaa watoto wa kiroho wakaendelea na hiyo roho ya kichawi na kuwa mchungaji, nabii na mengineyo. Na biblia inasema jinsi alivyo mchungaji ndivyo na waumini walivyo. Ndugu zangu, kwa kweli MUNGU awafungue macho mataifa yote, kwa sababu watu wengi ni wakristo lakini watachomwa moto siku ile ya mwisho kwa kutokujua au kujua, kwa sababu umefanana na baba yako wa kiroho ambaye ana nguvu za uovu (uchawi).

Nasema Ole wenu nyie wachawi mnaolitumia jina la YESU kwa uchawi na kufanya miujiza na mengineyo tena mkitumia biblia. Ole wenu mtapambana na YESU, na dunia sasa mtayaona na wala msishangae. YESU anahuzunika sana, amechezewa sana, amedharauliwa sana na baadhi ya wanadamu, na wapo walioitwa na YESU lakini walipoachwa na YESU wakaamua wajiunge na freemason na wachawi, badala ya kuendelea kutubu labda wangesamehewa. Wakaona kuliko tuaibike na wanadamu watatuonaje basi wakaenda kuzindikwa kwa waganga, na kila aliyeenda kwa waganga nataka muelewe yeye siyo mtumishi wa MUNGU tena bali yeye ni mganga wa giza, amevaa koti la kondoo ila ndani ya moyo anajua anachokifanya, soma Mathayo 3: 22-23 na 1Timotheo 6:3-5.

3Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya BWANA wetu YESU KRISTO, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, 4amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya; 5na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.”

Neno linaelezea vizuri tena jinsi ya kufananisha neno la kweli na nguvu za kweli. Kwa mfano, napenda muelewe, jina la YESU lina nguvu yake na jina lake huponya bure ila linapotajwa jina la YESU na kutozwa pesa ili uponywe sasa hapo uelewe jina hilo limechanganywa na nguvu za giza au uchawi, miungu, majini kama kivuli na ile nguvu itakayofanya kazi hapo ni nguvu ya shetani. Nataka pia uelewe, hakuna ushirikiano kati ya nguvu za nuru ya mbinguni na nguvu za giza. Mfano mwingine kwa mtumishi aliyeitwa na YESU, jina lake lipo juu yake na nguvu zake na atasema ukweli na zile nguvu zitatenda kabisa, kwa mfano kuombea watu bure. Na ikiwa unaombewa kwa kutozwa kiasi Fulani, haijalishi wanasimama na mistari ya biblia, uelewe hizo ni nguvu za giza, zinazotenda kazi kwa kuvaa vazi la kondoo kumbe ni mbwa mwitu, na sasa mbwa mwitu ni wengi sana katika dunia hii wakitumia jina la YESU ili kuwamaliza kiroho wengine. Utawajua kwa matendo yao.

Mfano mwingine ni katika ubatizo, kila mtu anajua YESU alibatizwa katika mto wa maji yanayotembea, MUNGU alimtuma Yohana kutoka mbinguni na YESU alijua hilo akaenda kubatizwa na udhihirisho wa MUNGU ukaonekana. Sasa ipo shida, ukisoma kitabu cha Ufunuo 22:18-19 imeandikwa usiongeze wala kupunguza neno la MUNGU hilo ni ONYO! Na kama ikiongezwa biblia inasema sehemu yake, ataenda jehanamu katika ziwa la moto yeye aliyeshiriki na anayefanya hivyo.
Mimi mwenyewe Hebron nilikuwa mmoja wa kwenda kwenye ziwa la moto ila kwa neema yake nikabatizwa upya kama YESU, kwa sababu nilidanganywa nikamwagiwa maji kichwani, tafuta katika biblia hakuna huo ubatizo, sasa kinachofanyika utabatizwa kwa jina la BABA, YESU, na ROHO MTAKATIFU, nakuambia ni nguvu nyingine ya giza itakaa juu yako pasipo wewe kujua au kwa kujua. Ukweli kabisa katika hili, siku ile ya hukumu, watu wengi watatupwa motoni. Ni bora sasa unajua, hiki ni kipindi cha neema. Injili ilibadilishwa na baadhi ya watumishi waliobatizwa na mizimu, shetani kwa mapokeo ya wanadamu yaliyotokana na fikra zao na siyo neno lilivyo.

Ubatizo: unabatizwa kwa jina la mchungaji halafu unaweka BABA, YESU, na ROHO MTAKATIFU, hapo mchungaji huyo anakuwa anaongozwa na mizimu au amejizindika na uchawi ili afanye hiyo kazi ya kuwapeleka watu jehanamu na wakati huo huo shetani akimpa umaarufu au utajiri hapa duniani, ila nakwambia ule mwisho atakuwa majivu kwa jinsi atakavyo chomwa.

Maombi ya kuombea wafu: ukisoma neno linasema kuwa MUNGU yeye siyo MUNGU wa wafu au mizoga, wanadamu wanapofanya ibada za wafu hapo huja miungu kutukuzwa na anayeshiriki na yeye huzidi kutambuliwa kuwa yeye ni wa mungu mfu siyo yule aliye hai hata kama jina la YESU hutajwa ni kazi bure.
Kuhusu sadaka: sadaka ni ibada kubwa sana kati ya mtu na MUNGU. Vile vile usipokuwa makini unaweza ukawa unawapa fungu la kumi au sadaka zako miungu na ukabaki kusimama na biblia na kulaumu mbona hakemei mabaya? Hakika hatakemea kwa sababu mungu mfu yeye haongei bali aliye hai atakemea. Kwa mfano, sadaka inapokuwa siyo siri yaani imeandikwa jina na kutolewa risiti, hata litajwe jina la YESU, nawaeleza haipokelewi, katika ulimwengu wa roho inakuwa inaenda sehemu ya giza. YESU hachangamani na uongo au tofauti na neno lake na ndio sababu watu wengi hawaoni majibu katika utoaji wao kwa sababu ya huu unyang’anyi wa mafarisayo.

Napenda kuwaeleza mataifa yote hakuna jambo linalofanyika sasa kinyume na biblia litakua na utukufu wa MUNGU, YESU hakujua kuwa litakuja kutokea hivyo basi sasa mfuateni YESU, acheni mapokeo ya wanadamu ili mpone. Hivyo natumaini mmelewa kwa jinsi gani jina la YESU linavyotumiwa na wachawi, jambo la kwanza pima matendo, maombezi ya pesa, batizo za uongo, kupinga ya YESU, ubatizo kwa jina la mchungaji, ubatizo wa kisima; yote hayo ni ya uovu na kulisingizia neno yaani biblia na mimi nauliza je hayo yote yametokea wapi? Ubatizo usiojulikana? Jibu ni kwamba, hayo yote yametoka kwa mungu asiyejulikana, aliyeenda kuzurura, yule mungu wa baali, siyo MUNGU wa Eliya.

Kuponywa kwa sabuni ni UCHAWI.
Kutozwa kiasi cha pesa ili kuonana na mtumishi ni nguvu ya giza na siyo YESU na nguvu zake.

Kuchagua ngamia tu yaani matajiri na kuwatenga mbu yaani wale wasio na utajiri, mahali hapo siyo nguvu ya YESU wa mbinguni inatumika. Ingekuwepo ingeunguza mambo hayo yote na kuyateketeza.
Wapo watumishi waliojiita na siyo MUNGU kawaita kufanya huduma, wao wanatumia nguvu ya mizimu, uchawi au akili zao, hao wote njia yao ni jehanamu pamoja na kundi wanaloliongoza, kwa sababu kiongozi akiwa kipofu na wote aongozao kiroho hutumbukia shimoni.

ANGALIZO:
Kazi ya MUNGU imeingiliwa na wachawi wengi zaidi katika ulimwengu wote, ni asilimia chache sana ambao siyo waganga, wengi wanatumia jina la YESU wakichanganya na uchawi na kufanya miujiza ya kichawi, kwa mfano kuwatoa watu misumari na mengineyo. Ile siku ya mwisho mtaona moto ukichoma watumishi wa kichawi kwa mabara yote, waliokuwa na watakaokuwa wanatumia bado nao watachomwa moto.
Rejeeni kwa YESU, OKOKENI. Sema; BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, shetani sikutaki kuanzia sasa na milele yote. Amen.

PROPHET HEBRON.